Mtu mmoja auawa katika mgogoro wa madaraka ya kijiji Simanjiro.
ITV ilifika katika kijiji cha kambi ya chokaa katika maziko ya
mjumbe huyo wa serikali ya kijiji ambaye anatajwa kumunga mkono mgombea
mmoja kati ya wanaogombania nafasi hiyo anayedaiwa kuuawa na mashabiki
wa upande wapili katika vurugu zilizofanyika kijjijini hapo na
kushuhudia watu wenye uzuni na machozi baada ya mwili wa marehemu Yohana
Rometi kuwasiri ukitokea hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na ITV kaka wa marehemu Yohana Rometi Bwana John Rometi
amesema tukio ilo limewatisha na anashindwa kuamini kuwa watanzania
sasa wamefikia hatua ya kutoana uhai kwa ajili ya ushabiki wa kisiasa
tena kwa chama kimoja huku akiiomba serikali itende haki na mmoja wa
viongozi wa serikali ya kijiji hicho Kiberesa Kunei akiwataka familia ya
marehemu kuto lipiza kisasi kwani wameshaikabidhi serikali kuchukua
hatua.