Wanawake wafugaji waandamana kupinga watendaji kuuza ardhi.
Zaidi
ya wanawake elfu moja kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya oljoro
namba tano wilayani Simanjiro wamefanya maandamano makubwa ya
kuishinikiza serikali iwachukulie hatau watendaji wa kata na kijiji cha
namba tano wanaodaiwa kuuza kinyemera zaidi ya hekari elfu thelasini na
tano za ardhi ya kijiji na kusababisha mgogoro wa ardhi kati ya wakulima
na wafugaji.
Wanawake hao ambao wameandamana hadi katika eneo linalodaiwa kuuzwa
na kuwa kiwakilisha kilio chao kwa serikali kupitia mbunge wa jimbo ilo
aliyefika katika eneo ilo na kuona maandamano hayo kisha na yeye
kuuungana na wanawake hao wakisindikizwa na wenzi wao wamesema
wamechoshwa na migogoro na kuitaka serikali kuharakisha kuchukua hatua
za kisheria kwa watendaji hao huku diwani wa kata hiyo akiahidi
kupambana kufa na kupona katika kutetea ardhi hiyo.
Baada ya kilio cha wananchi hao mbunge wa Simanjiro Christopher Ole
Sendeka aliwasimamisha mwenyekiti wa kijiji na mtendaji wake watoe
maelezo kuhusu ardhi waliyoiuza zoezi liloonekana kuwa gumu baada ya
wote kushindwa kutoa maelezo ya kina huku kila mmoja akijaribu kujitetea
binafsi bila mafakinio.
Baadae mbunge huyo akatoa tamko la kuchukuliwa hatua watendaji wote
waliyo husika kuhujumu zaidi ya hekari elfu thelasini za ardhi ya
kijiji na kudai kamwe kitendo hicho hakivumiki.