Dar es Salaam jiji ghali kuishi
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam
hutumia gharama kubwa zaidi, kulipia mahitaji yao ya muhimu kuliko
wenzao wengine wa Afrika mashariki, jijini Nairobi na Kampala,utafiti
uliofanywa na Shirika linalotathimini gharama za maisha,Numbeo umeeleza.
Utafiti
huu ulifanywa ukihusisha miji mikubwa 22 ukiangalia uwezo wa kununua
bidhaa,biashara za migahawani, hali kadhalika utafiti huu ulijikita
kwenye gharama za juu na urahisi wa maisha ya mijiniKwa mujibu wa Ripoti ya Numbeo , takwimu za gharama za watumiaji kwa wakazi wa Dar es Salaam kwenye bidhaa na huduma mbalimbali ni asilimia 62.83 ambayo imezidi Kampala na Nairobi zenye asilimia 54.34.
Kwa sasa Kenya ni nchi inayoongoza kwa kuwa na uchumi mkubwa Afrika Mashariki na iko nafasi ya sita barani Afrika, hata hivyo kwa mujibu wa matazamio ya Benki ya Standard Charterd , Tanzania inaelekea kuipiku Kenya na kuwa nchi yenye uchumi mkubwa ifikapo mwaka 2030 iwapo pato la taifa halitabadilika.