HADITHI Dhihaka ya Mke Mchawi



MAISHA ya ucnangudoa aliyoyaendesha Mwanahamisi na mwenzake Hilda hayakuwa na mtafaruku mkubwa kama maisha ya mke wa Isidori ambaye aliparamia uchawi kwa jinsi alivyoelekezwa na jamaa zake na kuishia kufukuzwa kwa mume wake.
Pamoja na kufanya kila hila ya kichawi ili kurudiana na mume wake, ndugu zake walikuwa wameshafanya  taratibu za kumkinga ndugu yao na akashindwa vibaya.
Mwishoni aliamua kutulia na hasa pale mume mwenyewe alipompasualia wazi kuwa alikuwa mchawi na wala hafai kwa chakula wala chai ya asubuhi.
"Wewe mchawi"
‘Wacha masikhara baba fatuma"
"Nakuambia kweli kwamba wewe ni mchawi na huwezi kunila nyama mimi wala kuniinamisha unachoweza kufanya ni kula nyama damu yako mwenyewe na kama usipofanya sasa hivi ujue huwezi kufanya tena mwanaharamu wewe'
"Kweli baba Fatuma unanifanyia hila hivi."
"Mimi wala sijakufanyia hila, hila umejifanyia mwenyewe. Mara ngapi umeondoka usiku ukaniachia fisi au gogo? Mara ngapi? yaani unajifanya kusikitika wewe mwanamke mbaya sana sijapata kuona"
Maneno hayakuishia hapo walizozana sana,hakika waliendelea kuzozana kwa muda mwingi, muda ambao ulitosha kuita majirani. Lakini hapakuwepo na mtu muda huo wa majibizano.Ilikuwa usiku na alimnasa wakati akirudi.
"Wewe unasema eti ulitoka chooni. Mbona uko uchi na midomo yako inameta. Hiyo lip shaini umeitia saa ngapi?Ona unavyoonyesha macho ya baridi halafu mimi si mchawi"
"Sasa unasemaje manake umesema sana leo?"
"Ondoka ndani mwangu"
"Wacha masikhara wewe ba Fatu, mimi najua kuolewa kuachika hapa unaweza kufanya kila kitu kuachika hapana"
"Siwezi kukuachisha katika urithi mliopeana . Unalisha uchafu naumwa kila siku unataka nini hasa?roho yangu? Roho ni ya mungu wewe huwezi kuichukua. Ni mali yake mwenyewe aliyeitengeneza wewe kazi yako ni kunilisha uchafu."
"Kama uchafu umekula sasa unachotaka kupiga kelele hapa nini?"
"Mwanamke huna haya wewe unaweza kusema mbele ya baba yako uchafu uliokuwa ukinilisha au tuseme ukaseme kwa mama yako?Huo uchawi wako unakuletea shida. Nitakufa siku moja lakini walahi wewe utasota duniani na akhera."
"Nakusikiliza umemaliza?"
"Ili unifumbe macho na masikio nisione?Najuta kukujua wewe"
"Umechelewa majuto mjukuu , umechelewa" akaondoka pale huku anamwaga kicheko kama fisi anayeshangilia kuona mkono wa binadamu. Hakuwa wa kawiada na isidori alitambua sawia kitu kile.

Alichomoa udi ambao alikuwa amepewa na kuuchoma kwa haraka na mara uliposhika  moto aliita :
"Mama Fatuma … Mama Fatuma… Mama Fatuma… " kisha akaendelea kwa utaratibu sana baada ya kutamka jina la mke wake mara tatu tena.
"Ni lazima uondoke ndani yanyumba hii unataka au hutaki.mmezoea sana kunichezea kama mpira sasa mtachezea jiwe lenye makali na wala hamtasamehewa mpaka mseme wazi mlichofanya duniani hapa katika siri na kuwa hadharani.Mama Fatuma na wenzako."
Kisha akauzima  udi ule kama alivyouwasha kwa kasi ya pumzi na mara sawia mke wake akafika toka chumbani/
"Baba Fatuma. Umesimama hapo muda mwingi twende tukalale"
"Sema niende nikalale ili uweze kunichawia, mwanamke nuksi wewe"
"Nitakapotaka kukuchawia  wala hutajua isidori, usiniletee hasira nikakuonyesha ninachokufanya kila siku"
"Wala usiseme kwa mighadhabu kwa sababu najua"
"Unajua nini wewe?"
"Kwamba mimi ni kitenisi"
"Hiyo haitoshi.Na kwa kuw aunadhani kusema kwako kutakuokoa leo umeingia pabaya"
"Wewe huwezi kunifanya kitu tena"
Akamtazama Isdori kwa dharau kubwa.akamwanzia utosini kisha kayapeleka macho yake yale ya baridi huku akionekana kuingiwa na hamu Fulani katika koo lake huku akiwa anaona uchu, akafika mpaka katika unyayo wake kisha akarejesha macho mpaka katikati ya maungo yake akajongea na kuyashika.
"Hapa nitaoka na kula mwenyewe. Si ndipo panapokufanya wewe uitwe isidori? Umeingia katika mtego na wewe huna nguvu ya kujinasua . Umenasa isidori. Unasemaje Baba Fatuma wangu au unadhani unaweza kujinasua"
"Nisiwe kujinasua kwa kisa gani hasa"
 akamwachia kisha akatabsamu.
"Kwa sababu si hiari yako isidori , si hiari yako nimeshakutia katika sihiri na u usingizini haya yote unayofanya sasa huwezi kuyakumbuka.U mtamu wewe na viungo hivi lazima viwe vitamu na kila siku nilikuwa nasubiri na nitaendelea kusubiri mpaka wakati ufike."
"Hutakaa uione hiyo siku, hakika hutakaa uione hiyo siku"
"unajindanganya mpenzi wangu la azizi, umeshakula vitu visivyolika na ulikuwa kwa raha zako ukaonyesha kila kitu unakipneda na mimi nitakapokuwa nakula wewe utatambua kwamba kila kitu chako nakipenda na  hiki na kipenda zaidi."
"Mmeshagawana mimi?"
"Sana mpenzi, kila mtu ameshachukua kitu chake. Mimi ni moyo wako , figo na hiki" akamshika tena.
"huwezi kuwahi hata siku moja."
"kwani unadhani ulinioa kwa hiari? Tulikuwa kila siku tukicheka wakati wazazi wako wanasema wanakuombea.Wanakuombea nini mdhambi wewe unayefurahishwa na kila dhambi tunayokupa"
"hakuna dhambi niliyofurahikia hapa"
"Hujala hiki" akamuonyesha kasha akacheka ulikuwa unafurajhi kama nini namimi nikakukoleza ili uingie jumla umeingia  wewe ni chakula tunachokinenepesha kwa sikuku yetu."
"Hicho cheo kukiimarisha itakuwa kazi kwelikweli, labda uitumie damu yako Fatuma si mimi wala hunijui"
"Tulikuchua zamani wakati umeanza kubalehe.mama akakuchezea na mimi nikakuchezea. Waka wangine wakakuchezea na kila siku wanakuchezea. Si ndio maana kila asubuhi ukiamka na kulalamika kwamba umechoka  mini huwa natabasamu tu manake najua jinsi unavyokamuliwa huku unachapwa mijeledi."
"Ilikuwa zamani"
"Mpaka sasa kama hivi ninavyosema" akaenda ukutani akazungumza maneno kadhaa kwa lugha ambayo Isidori hakuwa anajua na mara ukuta ukapotea akawaona wanawake 15 akiwemo mama mkwe wake wakiwa wanatabasamu na tena wapo uchi wa mnyama wamesimama mbele yake. 
Hawakumsikiliza wala kumwangalia kwa namna ambayo inastahili bali walianza kuimba nyimbo zao na kisha wakamfuata yeye na kumchukua kama mzigo na mara mkewe akageuka joka kubwa wale wote wakampanda na mama mkwe wake akawa yu mkiani mwa mtoto wake akiwa amemkumbatia mkwewe.Kisha bila kujua pakatokea mto wenye maji na mara joka lile likaanza kuchapia katika maji yake, kama mshale unavyotoka katika upinde, kajua mwnaamke wake ni nyoka na ndiyo gari ya safari. Nchi kavu pale maji yametoka wapi hakutaka hata kufikiri kwani hakuwa na majibu.

Hakujua wamefikaje pale lakini alichofahamu ni kuwa alikuwa amezungukwa na wanawake wenye furaha kubwa.
Safari hii alipolishwa, alikataa kula.
" Unajua hapa ndipo ninapopatwa na hasira" alisema na wanawake wengine walifadhaika pamoja naye kasha wakamfuata kwa pamoja.
Kwa namna ya ajabu kabisa alijiona katika msongamano ule amewatoka na yu nyuma yao lakini pale ambapo alistahili kuwa yeye lilikuwepo  jabali jeusi lenye makali sana, waliposhgika wote wakaruka na akajishtukia yupo kitandani mwake na mkewe anagumia.
"yaani baba Fatuma unanifanyia hivi kweli, unanipiga? Starehe zote nilizokupa"
"Nimekupigaje mke wangu"
"Nihurumie baba Fatu we, mbona hivi.Unaninyima raha. Nimetoka nyumbani nimekufuata wewe na halafu wewe unanifanyia hivi au .."
"Ungeniua wakatyi ule ule unile nyama sasa ni zamu yako kutesa kwa zamau."
"Nani amekuamsha usingizini mume wangu. Huyu ninaye"
"huna sababu ya kumjua na kwamba njia zenu chafu zilishajulikana na kama msipoomba msamaha mtaumbuka"
hakumsemesha tena, aliondoka akijua sasa anatakiwa kufanya nini.
Alichukua maji ya kwenye kichupa akamwagia.Akaenda kujipumzisha katika kochi. Bila kujua mkewe alianza kuugua hedhi tena yenye fujo kubwa. Dawa ilikuw ainafanyakazi kama ilivyokusudiwa. Asubuhi kabla hata mwale wa mapapambazuka haujakamilka mkwe wake na wamama wengine wawili aliwaona usiku uliofuata walifika nyumbani kwake, walikuwa wanamtaka Mama Fatuma woandoke naye.
Mama Fatuma hakuwa mbishi, alikuwa amepigwa vibaya, hakuwa anazungumza akawa anamtazama mume wake kwa jicho la huruma.
Mama Mkwe naye  alitoa mfyonzo mkali wakati anatoka na mtu anayeitwa isidori akabaki anatabasamu.
Powered by Blogger.