MICHAKATO YA KIMOFOLOJIA INAVYOTUMIKA KUUNDA MANENO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI






Fonimu za kaakaa gumu ni mbili yaani vizuiwa kwamizwa ambavyo ni ?t? na ?ts? kwa hiyo katika lugha ya kiswahili ukaaishaji wa fonimu hutokea wakati ambapo fonimu zisizo vizuiwa kwamizwa hubadilika na kuwa vizuiwa kwamizwa. Ukaakaishaji katika lugha ya Kiswahili hutokea zaidi katika vivumishi, nomino na vitenzi .
ukaakaishaji katika  vivumishi hutokea  katika mipaka ya mofu  za vivumishi, vivumishi vinavyohusika ni vile ambavyo mizizi huanzia na irabu. Kiambishi awali pekee ambacho husababisha ukaaishaji katika lugha ya kiswahili ni kiambishi/ ki/. Kiambishi / ki/ kinapowekwa pamoja na vivumishi ambavyo mizizi yao inaanzia na irabu ‘u’ ukaakaishaji hutokea
mfano
vivumishi vimilikishi
-angu- ki+angu- kyangu- chyangu- changu
-etu- ki+etu- kyetu- chyetu- chetu
Katika kanuni hii kizuiwa hafifu/k/ ambacho hutamkiwa kwenye kaakaa laini hubadilika kuwa kuzuiwa kwamizwa / ts/ ambacho hutamkwa kwenye kaakaa gumu.
Ukaakaishaji katika nomino, hutokea katika nomino chache za Kiswahili
Mfano
-ki+akula- kyakula- chyakula- chakula
-ki+ombi- kyombo- chyombo- chombo
Ukakaishaji katika vitenzi, hutokea pale ambapo mofu {ki} inapowekwa pamoja na mofu {o} ya urejeshi.
Mfano
{A} + {li} + {ki} + {o} + {ki} +{let} +{a}
1                  2         3       4         5         6           7
{A}+{li} + {cho}_ {ki}+ {let} + {a}   ambapo {ki} + o  cha
1       2                   3      4        5      6
Mofu ya tatu {ki} na ya nne {o} zinaungana na wakati  huohuo panatokea ukaakaishaji ambapo /k/ ina kaakaishwa na kuwa /ts/
Usilimisho pamwe wa nazali kanuni hii inahusu maathiriano ya mofimu zinazofuatana. Maathiriano haya huzifanya mofimu zifanane zaidi kuliko zikiwapelekee katika lugha ya Kiswahili ngeli ya 9, 10 na 11. Ngeli ya 9 umoja naya 10 uwingi  hujulikana kama ngeli ya nazali au kingo’n go. Ngeli ya 11 umoja uwingi wake ni ngeli ya 10

Mfano, N+ goma- {ngoma}
             N+ dizi- {ndizi}
             N+ buzi – {mbuzi}
           N+ geli- {ngeli}
           N + bingu – {mbingu}
Mifano hii inaonesha kuwa mofimu ng’ongo ambayo ni /n/ na /m/ hutokea kutegemea na sauti inayoanza katika mzizi Rubanza (1999) .
Vilevile Mgullu(1999) anajadili usilimisho pamwe wa nazali kutegemea usilimisho ambao fonimu jumuishi huupata. Usilimisho huu, hueleza kuwa hutegemea mahali ambapo konsanti inayofuata fonimu jumuishi hutamkiwa. mfano hutokea kama /n/ - /d/ katika maneno, ndizi, ndama, yaani fonimu jumuishi /n/ hutokea kama  /n/ katika maziongira kabla ya /d/
Pia hutokea kama /m/ - /b/ katika maneno mbuzi mbali yaani fonimu jumuishi /n/ hutokea kama /m/ katika mazingira kabla ya /b/. Lakini mtazamo huu una utata haungwi mkono moja kwa moja kuwa /n/, /m/ ni sauti tofauti za mofimu jumuishi moja.  Huenda ikaja kutokea,
>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>> 
Powered by Blogger.