HISTORIA YA MUZIKI WA HIP HOP NA BONGO FLEVA NA JINSI UNAVYOONEKANA KUATHIRIWA ZAIDI NA WASHAIRI WA KIMAPOKEO KULIKO WANAUSASA
Ama kwa hakika,
wasanii wasanii wa Hip Hop na Bongo Fleva si kwamba wanajigamba tu kuwa wao ni
wataalamu wa kutumia vina, lakini pia vina hiyo vinajidhihirisha katika tungo
zao. Hebu tuangalie baadhi ya tungo kuona jinsi wasanii wanavyozingatia
matumizi ya vina katika tungo zao. Tukianza na msanii Profesa Jay katika wimbo
wake wa Kubwa Kuliko:
Ubeti wa 1
Yo fani ni fani muulize,
Bishanga Bashaija,
Sanaa ya Bongo kwa wasanii
haina faida,
Ona wenzetu Mantoni mambo
safi kuku kwa mrija,
Na mimi nataka niishi kama
Kadija Kadija,
Wasanii wa Bongo bado
tunakufa maskini,
Nasubiri kiama changu na
sijui kitafika lini,
Wazee wa serikalini semeni
tatizo ni nini?
Mnataka mle jasho langu
nikienda futi sita ardhini,
Hapa jasho la mtu haliliwi
wala mtu haibiwi,
Jay najivinjali kama
kutumia kizizi,
Machozi yananilenga
nikimkumbuka mzee Nyanyusa,
Pamoja na umuhimu wake
wabongo walimsusa,
Baadhi ya mafao yake
wabongo wamefanya asusa,
Kwa mtu mwenye akili
lazima hii itakugusa,
Tunaposema Watanzania
tudumishe sanaa yetu,
Lazima mtuwekee mazingira
safi ya sanaa yetu,
Marijani Rajabu tulimuita
jabali la muziki,
Alifanya
maajabu,alivumilia mikimikiki,
Kinachonipa ghadhabu,
bwana sanaa ya Bongo hailipi,
Tofauti na chati yake,
ndugu yetu amekufa na dhiki,
Sasa kipi ni kipi maana
ufanisi haufanyiki,
Sababu viongozi wetu
mnatamaa hauridhiki,
Wakati ni huu wa kujifunza
watanzania,
Umoja wa wasanii wa bongo
hiyo ndiyo njia.
Kiitikio
Ninaposema Jay kubwa
kuliko,
Siko niliko ndiko liko
zindiko (Yataka moyo)
Ninaposema Jay kubwa kuliko,
Siko niliko ndiko liko
zindiko (Yataka moyo)
Sanaa yataka wito (yataka
moyo)
Sanaa ya Bongo nzito
(yataka moyo)
Sanaa ujiko mwiko (yataka
moyo)
Sanaa yataka wito (yataka
moyo)
Ubeti wa 2
Salamu Nicko zingilada
popote roho ilipo,
Wasanii wenzako wa Bongo
bado tunafanya zindiko,
Wasalimie sana kuzimu
walio hai na waliolala,
Waambie tunasuasua tu na
akina Mzee Jangala,
Hardblasterz, Sikinde na
Remmy Ongala,
Underground Soul na
Gangwe na Baby Stara,
Uncle Kabaino, IK pale
Kimara,
OTTU Jazz na Agley Face
kule Ilala,
Tunasubiri kudra za imani
kwa Mungu kwa waja wake,
Tunaotafuta labda tutapata
faraja zake,
Mambo si mambo
yameongezeka tu matukio,
Na ajali, rushwa na UKIMWI
tu ndiyo kivutio,
Sanaa imedumaa najua hiyo
huwezi shangaa,
Lakini hali ya sasa ni
mbaya na inatukatisha tamaa,
Soko limekuwa bovu wasanii
hatuungwi mkono,
Wananchi hawana kitu kila
siku wanafanya mgomo,
Kiasi wanachokipata
kinaishia kwenye bia na ngono,
Na kuhusu masoko ya nje
serikali imefungwa mdomo,
Mapromota wengi matapeli,
ukilemaa wanakuacha feli,
Unaangua kilio,
ulichotegemea kinakuwa siyo,
Wepesi kutimua mbio, wewe
linakupitia fagio,
Na sasa wametuacha na
kuleta wasanii wan je,
Hatimiliki ndiyo kwanza
inasua sua ndani ya Bunge.
Kiitikio
Ninaposema Jay kubwa
kuliko,
Siko niliko ndiko liko
zindiko (Yataka moyo)
Ninaposema Jay kubwa
kuliko,
Siko niliko ndiko liko
zindiko (Yataka moyo)
Sanaa yataka wito (yataka
moyo)
Sanaa ya Bongo nzito
(yataka moyo)
Sanaa ujiko mwiko (yataka
moyo)
Sanaa yataka wito (yataka
moyo)