HISTORIA YA MUZIKI WA HIP HOP NA BONGO FLEVA NA JINSI UNAVYOONEKANA KUATHIRIWA ZAIDI NA WASHAIRI WA KIMAPOKEO KULIKO WANAUSASA
Na siyo
bandia ka kontena lile la BOT,
Situkuzi
kilicho feki kama TOT,
Mi ndio
Roma ntasimama kaka KKT,
Ahsante
Bongo, macho juu, Nyamongo, TBC,
Mistari
yangu mitamu kama miwa ya TPC,
Na kwa
hizo fomu MC utalazwa KCMC,
Kodi ya
walalahoi pombe TRA,
Miili yao
ndio biashara ndani ya BBA,
Fataki
anatoa mikopo ndani ya TIA,
Licha ya
mimba haina uhakika mpaka DNA.
Katika
ubeti huu tunamuona msanii akiamua kutumia vifupisho katika kila mstari na
vifupisho hivyo alivyoviteua kuvitumia vinakamilisha vina katika ubeti mzima.
Vilevile, mtindo wa
wasanii kutunga na kuimba mashairi yao papo kwa papo kwa mtindo ambao wao
huuita mitindo huru huku wakizangatia suala la mizani, ni ushaidi mwingine
unaoonesha kuwa muziki huu unaonekana kuathiriwa na wanajadi zaidi kuliko
wanausasa. Samwel na wenzake (washatajwa, uk. 63-64) wanaeleza kuwa, msanii wa
Hip Hop au Bongo fleva anapotunga papo kwa papo huongozwa na fomula na hasa ile
ya urari wa vina na mizani. Wanaendelea kusisitiza kuwa, fomula hii humfanya
(msanii) kila mara kuhakikisha anapachika maneno ambayo yana vina. Wakimtolea
mfano msanii Roma, wanatueleza kuwa katika tamasha la Epiq Nation jijini Mwanza
alitoa ghani za papo kwa papo ambazo zinaonekana kuzingatia urari wa vina, kama
inavyoonekana hapa chini katika ghani hizo ambap msanii ametumia vina vya ao na
to ili hali mashairi hayo ameyatoa kichwani papo kwa papo;
Mwanza, msishindane na
mwanamke pedeshee atamuhonga noah,
Wanaume mjitahidi ipo siku
mtatoboa,
Mimi ni Rais wa ghetto,
Sina kabisa mchecheto,
Na wala sipigi punyeto,
Namiliki mademu kwa
kipato,
Mwanza sema oyee kwa Epiq
Nation.
Chanzo: Samwel na wenzanke
(washatajwa, uk.64)
Ama kwa hakika,
tukiangalia tungo za wasanii wa muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva tutakubaliana
kuwa mashairi yao kwa upande wa kuzingatia vina katika tungo zao inaelekea
kuonesha kuwa wasanii wa muziki huu wanaonekana kuathiriwa sana na wanajadi.
Aidha kipengele kingine
ni mizani, Abedi (keshatajwa) anafasili kuwa, mizani ni vipimo vinavyopima
urefu wa kila mstari, kila silabi moja ni mizani moja. Yeye anaona shairi zuri
ni lile lenye mizani16, lakini anatambua pia kuna mashairi yasiyotimiza mizani
hii, hivyo anatoa maelekezo ya namna ya kuweka kina cha kati katika mashairi
yenye mizani pungufu ya 16. Kupitia maelekezo haya tunaona hata wasanii wa
Bongo Fleva na Hiphop wanazingatia idadi ya mizani na katika utunzi wao japo
hawafuati mizani 16. Mara nyingi wamekuwa wakitumia mizani pungufu au zaidi ya
16. Mfano katika wimbo wa profesa J ametumia mizani 12. Katika wimbo wake
wa kubwa kuliko hasa katika kiitikio kama inavyojionesha
katika ubeti ufuatao;
‘ninaposema jay kubwa kuliko,
Siko
niliko ndiko liko zinduko,
Ninaposema jay kubwa kuliko
Tukichunguza mashairi
ya Hip Hop na Bongo Fleva tutaona kuwa hawazingatii ya nane nane kila kipande
cha mstari ili kupata mizani 16, mara nyingi mashairi yao mizani huweza
kutofautiana kati ya mstari mmoja na mstari mwingine katika ubeti mmoja lakini
suala la urari wa vina huzingatiwa kama inavyojionesha katika mfano tulioutoa
hapo juu, ambapo kila mstari unaishia na kina cha ko.
Tukiangalia pia mfano ufuatao kutoka kwa msanii Ali Kiba katika wimbo wake
wa Mwana:
Ubeti wa kwanza
Mali ni nyingi nyumbani,
kipi kilichokukimbiza,
Ona babiyo mamiyo, wote
wanakulilia,
Mtoto peke yako nyumbani,
kipi kimekukimbiza,
Ona babiyo mamiyo, wote
wanakulilia,
Ndani ya Dar Es Salaama,
ulikuja bure,
Tena kimwana kimwana,
hujui kuchuna,
Na zile lawama, za
wallokuzoeza,
Ulikuja jana na leo
tofauti sana,
Tena bora yule wa jana wa
leo tofauti sana,
Dakikia mbili mbele nyuma,
kichwa kinauma,
Mbona unawatesa sana,
Mbona unajitesa sana,
Ndani ya Dar Es Salaam
mambo matamu hakukuhisha hamu,
We bado mtoto kwa mama
hujayajua mengi,
Mwenda tezi na omo marejeo
ngamani,
Amesema sana mama, dunia
tambara bovu,
Kuna asali na shubiri,
ujana giza na nuru,
We mwana wewe mwana, mwana
jeuri sana,
Ulichokifuata hukupaa,
umekosa ulivyoacha,
Kwa baba yako mwana, na
mama yako mwana,
Kwa vicheche ulivyotaka,
na vingi ulivyoacha,
Tukiangalia wimbo huu,
tutaona kuwa mizani haijazingatiwa sana, kwani kila mstari unaweza kuwa na
mizani tofauti na mstari mwingine ndani ya ubeti huo huo. Kwa mfano mstari wa
kwanza una mizani 17 kipande cha kwanza cha mstari kina mizani 8 na kipande cha
pili kina mizani 9, wakati mstari wa pili una mizani 16, kipande cha kwanza una
mizani 8 na kipande cha pili una mizani 8. Lakini pamoja na tofauti hiyo, ya
mizani, urari wa vina unazingatiwa kama inavyoonekana katika kila beti, vina
vya za, a, na, cha vimetawala.