FONETIKI AU UTAMKWAJI WA SAUTI-FONIMU ZA KISWAHILI SANIFU



Utamkwaji wa Sauti-Fonimu-Konsoni za Kiswahili Sanifu
Utamkaji wa fonimu-konsonanti za Kiswahili utafafanuliwa kwa mujibu wa vigezo vinne: utamkaji ki-alapahala, utamkaji ki-sampuli,     utamkaji ki-ughuna, na utamkaji ki-ung’ong’o.             

(i)     Utamkwaji wa Sauti-Fonimu-Konsoni za Kiswahili Ki-Alasogezi-Pahala
Fonimu-konsoni zote ishirini na tisa (29) za Kiswahili sanifu hudhihirishwa kimatamshi kwa kutumia alapahala saba (7) ambazo nazo huhusishwa moja kwa moja na alasogezi husika zilizomo katika bomba la sauti (Nchimbi, 1979), kama ifuatavyo:
           
Utamkwaji wa Vimidomo [p, b]: Wakati wa matamshi ya sauti za midomoni [p, b], alasogezi ya mdomo-chini hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya mdomo-juu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.
Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka, kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o. (Tazama Kielelezo 3.8).

Utamkwaji wa Vimdomochini-Menojuu [f  v]: Wakati wa matamshi ya vimdomochini-menojuu [f] na [v], alasogezi husika ambayo ni mdomo-chini, hujikweza na, ama kujibandika kwenye alapahala ya meno-juu, au hujisogeza na kuacha nafasi finyu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni hujipenyeza kwa taabu kadiri unavyopitishwa katikati ya nafasi finyu inayofanyizwa kwa mdomo-chini na meno-juu, au kati ya jino na jino wakati mkondo huo unapoelekezwa n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomoni.

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o.



Utamkwaji wa Viulimincha-Menojuu [θ  Ã°]: Wakati wa matamshi ya viulimincha-menojuu [θ] na [ð], alasogezi ya ulimi-ncha  hujisogeza kwenye alapahala ya meno-juu na kuacha nafasi finyu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni hujipenyeza kwa taabu kadiri unavyopitishwa katikati ya nafasi finyu inayofanyizwa kwa ulimi-ncha na meno-juu wakati mkondo huo unapoelekezwa nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomoni.

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o.   

                       


Utamkwaji wa viulimincha-ufizijuu [t d s  z ]: Alasogezi ya ulimi-ncha  na alapahala ya ufizi-juu ndizo zinazotumika wakati wa matamshi ya viulimincha-ufizijuu. [t d s  z  r l].

Utamkwaji wa [t d]: Alasogezi ya ulimi-ncha inajikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ufizi-juu; mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika ndii... kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o. Kwa mantiki hii, viulimincha-ufizijuu vinavyotamkwa ni [t  d ].



Utamkwaji wa [s z]: Wakati alasogezi ya ulimi-ncha inapojisogeza kiasi cha kuacha nafasi finyu kati yake na alapahala ya ufizi-juu, mkondo wa hewa utokao mapafuni hupata nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [s z ].


Utamkwaji wa Viulimikati-Burutiogumu [c ÉŸ Êƒ  j]: Utamkwaji wa [c ÉŸ]

Wakati wa matamshi ya viulimikati-burutiogumu [c ÉŸ], alasogezi ya ulimi-kati, hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya burutio-gumu kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya Bomba la Sauti kwa kupitia chemba ya midomo.

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [ÉŸ].
    
                  
Utamkwaji wa [ʃ  j]: Wakati wa matamshi ya viulimikati-burutiogumu [ʃ  j ]; alasogezi ya ulimi-kati hujisogeza kiasi cha kuacha nafasi finyu kati yake na alapahala ya burutiogumu.

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [ʃ  j].

Utamkwaji wa Viuliminyuma-Burutiolaini [k g  Æ”]: Wakati wa matamshi ya viulimikati-burutiogumu [k  g], alasogezi ya ulimi-nyuma, hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya burutio-gumu-nyuma kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.


Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [k  g], Tazama Kielelezo 3.15.

Unapojitokeza wakati wa matamshi ya [Æ”], alasogezi ya ulimi-nyuma hujisogeza kiasi cha kuacha nafasi finyu kati yake na alapahala ya ukuta wa marakaraka au ncha ya kidaka-tonge. Nafasi hii itaruhusu mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo. Midomo hubakia tandazi itamkwapo sauti [Æ”]

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o [Æ”]


Utamkwaji wa Kiglota [h]: Wakati wa matamshi ya kiglota [h], alasogezi ya ulimi hubakia chini kiasi cha kuacha nafasi kubwa kati yake na alapahala ya burutio. Mkondo wa hewa kutoka mapafuni unapopita katika chemba ya koromeo, nyuzi sauti zilizomo katika chemba hiyo ama hurindima na ikapatikana sauti [ h ], au hazirindimi na kupatikana sauti [h]. Aidha , mkondo huu wa hewa kutoka mapafuni hupitishwa moja kwa moja katika chemba ya kinywa bila kizuizi mpaka n’nje ya kinywa. Kwa mantiki hii, nyuzi sauti zinaweza kueleweka kama alasogezi ya matamshi ya sauti [h] ya fonimu /h/.

Midomo hubakia tandazi itamkwapo sauti [h]. Na alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o[h]

(ii)    Utamkaji wa Sauti za Fonimu za Kiswahili  Ki-Sampuli
Utamkwaji wa sauti ki-sampuli unabainisha kati ya sauti-endelezi na sauti-sendelezi.Utamkaji wa sauti ki-sampuli ni ule unaosababishwa na alasogezi ya ulimi na mdomo-chini inaponyanyuka kuelekea kwenye alapahala husika. Ulimi au mdomo-chini unaponyanyuka kuelekea kwenye alapahala husika, husababisha matamshi ya sampuli za sauti zifuatazo:
           
Sauti-sendelezi-konsoni ambayo wakati wa utamkwaji wake, alasogezi husika hujikweza na kujibandika kwenye alapahala husika; ambayo kwa [p b ] ni mdomo-juu, kwa [t d] ni ufizi-juu, kwa [ÉŸ ] ni burutio-gumu-mbele na kwa [k g N] ni burutio-gumu- nyuma kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti. Kuzuiliwa kwa mkondo huu wa hewa ni kwa muda mfupi sana. Kwa mantiki hii utamkaji wa sauti-konsonanti-katizi hauendelezeki. Mifano ya sauti-konsonanti-katizi katika Kiswahili ni [p b  t d  ÉŸ k g ].

Sauti-endelezi-konsoni-madende ambayo wakati wa utamkaji wake, alasogezi ya ulimi-ncha hujikweza na kujibandika kwenye alapahala ya ufizi-juu, kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo haupati nafasi ya kupenya kuelekea n’nje ya bomba la sauti. Kuzuiliwa kwa mkondo huu wa hewa ni kwa muda mfupi sana. Kwa mantiki hii, alasogezi ya ulimi-ncha huonekana ikiyumbishwa kana kwamba inajigongagonga kwenye matuta ya alapahala ya ufizi-juu. Aidha, utamkaji wa sauti hii huwa katizi unaoendelezeka kwa vigongo, yaani, kimadende.

Alasogezi ya kidaka-tonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakaraka kitendo ambacho hakiruhusu hewa kupenya hadi kwenye chemba ya pua. Hisia ya sauti inayosikika ni sauti-sing’ong’o. Mfano wa sauti-konsonanti-madende-endelezi ni [r].

Sauti-Endelezi-Konsoni-Kwama Kwamizi ambayo wakati wa utamkwaji wake, alasogezi husika hujikweza na kuunda mpenyo mwembamba sana kwenye alapahala husika, kiasi kwamba mkondo wa hewa utokao kwenye           chemba ya koromeo hupita, lakini kwa hukwamizwa kwamizwa, unapoelekea n’nje ya Bomba la Sauti. Matokeo yake ni matamshi ya sauti-konsonanti-endelezi kwama kwamizi, kama vile: [f  Î¸ Ã° s Êƒ [Æ”] h] 
>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>
Powered by Blogger.