Matembele ni mboga maarufu sana, pia ni mboga yenye virutubisho sana, mara nyingi watu hula mboga hii kwa msimu, kama inapotokea uchumi umeshuka nyumbani.. Lakini matembele yana faida nyingi katika miili yetu.
1: Matembele yana madini ya chuma. Madini haya ndiyo muhimu katika utengenezaji wa damu, kwa hiyo mtu anapotumia matembele anakuwa anaongeza kiwango cha damu mwilini. Watu wenye upungufu wa damu na kina mama wajawazito wanashauriwa kula matembele kwa wingi.
2: Matembele yana vitamini A ambayo husaidia kuimarisha macho na hivyo kumsaidia mtu kuona vizuri hasa hasa nyakati za usiku.
3: Matembele yana vitamini C Ambayo humlinda mtu asipate kiseyenye (scurvy). Vitamini C huimarisha ngozi na fizi, unapotumia matembele fizi zako na ngozi huimarika na huzuia kuvuja damu kutoka kwenye fizi.
4: Matembele yana protini ambayo husaidia katika kuimarisha misuli na kusaidia katika ukuaji wa mwili. Wape watoto matembele ili wakue vizuri.
Unajua jinsi ya kupika matembele kwa usahihi ili usiharibu virutubisho? Fuatilia chapisho litakalo fuata.