MITAZAMO (NADHARIA) MBALIMBALI JUU YA SANAA ZA MAONYESHO
Tukizingatia
nadharia hii huenda tukaamini kuwa sanaa za maonyesho ni tamthilia tu. Kitu
ambacho kinaleta mashaka kidogo. Inafahamika kuwa tamthilia ni
utanzu ulioletwa na wakoloni hapa Afrika Mashariki. Kwa hiyo, kuamini nadharia
hii ni sawa na kusema kuwa hakuna sanaa za maonyesho zenye asili ya hapa Tanzania
ama Afrika Mashariki. Au kwa upande mwingine ni sawa na kusema kuwa kabla ya
mkoloni kutuletea tamthilia sisi tulikuwa hatuna sanaa za maonyesho zetu
wenyewe. Wazo hili si kweli na ni wazo potofu. (Taz. Mhando
&Balisidya 1976).
Kimsingi
mtazamo huu unatokana na fasili ya sanaa za maonyesho inayodai kuwa sanaa za
maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa za mchezo, mchezaji, uwanja wa
kuchezea na watazamaji. Ingawaje ufafanuzi huu ni sawa lakini hata hivyo
mtazamo huu ni dhaifu kwani ulitokana na watu waliokuwa wakifafanua sanaa za
maonyesho wakiegemea zaidi kwa zile za utamaduni wa kizungu. Ufafanuzi huu
haukuzifikiria sanaa za maonyesho zenye ya utamaduni wa Kitanzania.
Dosari
kubwa katika ufafanuzi huu imo katika neno mchezo (play). Neno
hili lina maana duni likilinganishwa na hali na umuhimu wa sanaa za maonyesho
zenye asili ya Kitanzania/Kiafrika. Tukichukua kwa mfano unyago, jando, kusalia
mizimu, au masimulizi ya hadithi, ambayo ni mifano ya sanaa za maonyesho zenye
asili ya Kitanzania, tunakuta zile sifa zote nne zipo. Isipokuwa tunajua kuwa
shughuli zote hizi siyo mchezo na umuhimu wao hauruhusu hata kidogo kuingiza
neno mchezo. Shughuli hizi zina maana muhimu ambayo inahusu maisha ya binadamu
katika jamii yake. Ni shughuli zinazobeba wazo maalum lenye lengo la kujenga
utu wa mwanajamii. Basi vipi tuseme shughuli hizi zina sifa ya
mchezo? Wenzetu wazungu wanaridhika na neno hili
kwa sababu sanaa za maonyesho za utamaduni wao mara nyingi
zinafanywa kwa masihara tu. Sanaa za maonyesho zao zaidi ni kwa madhumuni ya
kujiburudisha au pengine kutafuta kipato. Lakini kila aina ya sanaa za
maonyesho ya Kitanzania ina dhana fulani ndani yake, kwa mfano dhana kuhusu
maana ya maisha, kuhusu utekelezaji wa madaraka ya kiutu
uzima, kuhusu ushujaa, mafunzo ya historia ya jamii n.k.
>>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>