MCHANGO WA BONGO FLAVA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI.
Kiswahili ni lugha ambayo inawekwa katika kundi la lugha za Kibantu. Neno “Swahili” linatokana na neno la Kiarabu “sahel” linalomaanisha “sawahil” na katika Kiswahili ni “mpaka” au“pwani”(linalotumika kama kivumishi kumaanisha “wakazi wa pwani”. Kuongeza kwa herufi mbili za “ki” [‘lugha’] kupata “Kiswahili” kumaanisha “lugha ya pwani”. Wakati mwingine, neno“sahel” linatumika kumaanisha “mpaka wa jangwa la Sahara”. Unganishaji wa herufi ‘i’ mwisho wa neno “Kiswahili” ni kutokana na umbo la  kivumishi katika lugha ya Arabu (‘sawahil’). Jambo la hakika ni kwamba Kiswahili ni lugha ambayo imeazima maneno kutoka Kiarabu, Kiuajemi, Kireno na hivi karibuni Kiingereza. Hali hiyo, imekifanya Kiswahili kufika kiwango cha lugha ya kisasaZamani, Waswahili walitumia utawala wa mfumo wa mamlaka moja. Karibu na karne ya 10, pwani nzima ya Zanzibar ilikuwa chini ya utawala wa mfalme mmoja ambaye aliishi katika mji mkuu wa Safala.

Karibia karne ya 14, jamii ya Waswahili ilibadilishwa kuwa nchi yenye miji ya kisasa. Miji mingi hiyo ilikuwa midogo yenye majengo ya jiwe, misikiti, familia ya Waislamu walio na tabaka la juu na wengine wengi ambao hawakuwa Waislamu. Majiji makubwa kama Mogadishu, Pate, Mombasa, Malindi, Zanzibar na Kilwa yalijengwa na marijani na matumbawe ambayo yalionesha dalili za utajiri kwani yalikuwa  na vifaa vya ujenzi  vya gharama sana. Idadi kubwa ya majiji hayo yalikuwa chini ya utawala wa Sultani ambaye alikuwa Mwislamu. Ilifika kipindi ambacho majiji makubwa hayo yalitawala mengine ambayo hayakuwa na uwezo wa kuchukua mamlaka. Kwa mfano, Sultani wa Kilwa alitawala sehemu kubwa ya pwani ikiwemo Sofala na Zanzibar. karne ya 14 (kipindi cha mwaka 1390) idadi kubwa ya miji iliyotawaliwa na Masultani wa Omani kama Sofala ilianza kupata uhuru. Kuanzia karne ya 8 mpaka 19, Kiswahili kilizumgumzwa na makabila kadhaa kwa umbali wa maili 1000 kwenye pwani ya Afrika Mashariki kati ya Mozambique na kusini kwa Somalia.

Kwa mamia ya miaka,sehemuambazo palikuwa na Waswahili palikuwa vituo vya biashara muhimu kati ya wenyeji na nchi kama Arabia, India na Asia Mashariki na raslimali za Afrika Mashariki. Ushirikiano huu wa kibiashara uliathiri jamii ya wenyeji (Waswahili), utamaduni, dini na lugha katika Afrika Mashariki. Katika enzi za karne ya 19, Kisiwa cha Zanzibar kilikuwa kituo kikuu na cha umuhimu kwa ajili ya biashara iliyokuwapo kwenye pwani ya Afrika Mashariki; sehemu ambapo safari ya watu na usafirishaji wa bidhaa kwenda katikati ya eneo hilo (Afrika Mashariki). Wakati huo, Kiswahili kilitumika kama lugha ya biashara na ya mawasiliano. Kutokana na hali hii, watu wengi ambao ni Waswahili walihamia kuishi kwingine hasa katikati ya Afrika Mashariki kwa lengo la kufanya biashara.

Naye Profesa Whiteley (1969), amefafanua hali hii akisema,“Wakati upanuzi wa biashara ulipobadili mbinu ya biashara kwa kutumia msafara kutoka pwani, haja ya kuhitaji lugha muafaka wa biashara ulikuwa muhimu sana na hapo ndipo Kiswahili kilipojizindua jukwaani”.(“When the expansion of trade shifted the initiative to caravan from the coast, the need for an effective lingua franca became acute and Swahili came into its own”).Baadaye, yaani katika karne ya 20, wakati wa ukoloni wa Uingereza, lahaja ya Unguja (aina ya Kiswahili iliyotumiwa na Wazanzibari ilienea sana Tanzania na aina nyingine ya Kiswahili ilienea mpaka Kenya, Uganda, Burundi, Congo, Mozambique na ilifika mbali sana hata mpaka Afrika Kusini. Aina hii ya Unguja ilikuwa imeathirika sana na Kiarabu.

Aina nyingine zilizojitenga kutoka Unguja zilipitia mabadiliko tofauti wakati wa usambazaji wa Kiswahili. Kwa sasa, tuna aina nyingi za Kiswahili zinazotofautiana angalau kidogo sana katika lugha hii ya Kiswahili. Ni muhimu kukumbuka kwamba kulikuwa na sababu moja ambayo ilisababisha usambaaji wa Kiswahili. Hii ilikuwa hali ya kuoana miongoni mwa wafanyabiashara (ambao walikuwa Waswahili) na wenyeji ambao wengi walikuwa watumwa. Inakubalika bila shaka kwamba watoto waliozaliwa na familia ya mchanganyiko huo walipata nafasi ya kujua na kuongea Kiswahili.

1.4USULI WA TATIZO LA UTAFITI
Wahakiki na watunzi wa nyimbo hizi wamejikita kwa kiasi  kikubwa kuangalia fani vilevile na maudhui, Lakini tahakiki zao zimejikita katika fani.katika maudhi watafiti na wahakiki wengi wamegusia baadhi ya vipengere na kukisahau kipengere cha utabaka kutokana na matumizi ya lugha ya kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya ambapo hutenganisha jamii kwasababu nyimbo zao huonekana ni za vijana tu.Chachage(2002)amezungumzia muziki wa kizazi kipya kuwa lugha inayotumika katika nyimbo hizi zina matumizi makubwa ya maneno  yanayoibuka kila siku ambayoyanaonekana kuwa lenga vijana  na ndiyo wanaoelewa maneno hayo.Jarida la TUKI(2006)wameelezea vipengere mbalimbali vya Fani hasa lugha katika muziki wa kizazi kipya kama uchanganyaji wa lugha,lugha isotafsida,matumizi ya lafudhi za lugha za asili,matumizi ya taswira na matumizi ya tashititi. na maudhui ya muziki huu kama umasikini,unyanyasaji,ukosefua wa ajira na uchumi.

Hii inadhihirisha kwamba suala la nafasi ya lugha ya Kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya kama kipengere cha fani na  pia katika maudhi hawajaangalia kwa undani jinsi matumizi ya misamiati ya lugha ya kiswahili yanavyotumika katika nyimbo hizo inaleta utabaka kwa jamii kwasababu misamiati hiyo inaeleweka na vijana pekee yao.kukwepwa kwa vipengere hivyo kwa wasikilizaji wa nyimbo za muziki wa kizazi kipya na watumiaji wa lugha ya Kiswahili kuna leta utabaka katika jamii.Hii ni kwasababu usikilizaji wa nyimbo hizi unahitaji misamiati inayoeleweka na inayozingatia utamaduni wa lugha husika kwa jamii ili iwe mali ya jamii nzima.Hivyo,utafiti huu unatarajia kuziba pengo lililobainishwa hapo juu kwa kuchunguza hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya,kuangalia sababu zinazopelekea muziki wakizazi kipya kusikilizwa na vijana zaidi na mchango wa muziki wa kizazi kipya katika lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
1.5 TAMKO LA UTAFITI .
Katika kipengele hiki nilishughulikia  mada ya utafiti ambayo ni  nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.Watafiti wengi waliotangulia  walichunguza lugha ya kiswahili ilinavyotumika katika muziki wa kizazi kipya ambapo waliegemea zaidi kwenye kipengele cha fani. Hivyo utafiti huu ulichunguza nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya kwa kuzingatia kipele cha maudhui .
1.6MALENGO YA UTAFITI  .
Malengo ya utafiti huu yamegawanywa katika sehemu kuu mbili,sehemu ya kwanza ni malengo ya jumla na sehemu ya pili ni malengo mahsusi.
1.6.1 Malengo ya jumla.
Utafiti huu unalenga kuchunguza nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.

1 .6.2 Malengo mahsusi.
Malengo mahususi ya utafiti huu ni kama yafuatayo:
         i.            Kuchunguza hadhi ya Kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya.
       ii.            Kuchunguza sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana zaidi.
      iii.            Kuchunguza mchango wa muziki wakizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujmla.
1.7Maswali ya utafiti.
Maswali yatakayo tuongoza katika kufikia malengo hayo ni:
         i.            Lugha ya Kiswahili ina hadhi gani katika  muziki wa kizazi kipya.
Swali hili liliandaliwa ili liniongoze katika ukusanyaji na uwasilishaji wa data za utafiti wangu.Hili ni swali kuu la msingi katika tasnifu hii kwa kulijibu swali hili nilitaraji kubaini hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ,kwa kuwa wasanii wengi wa nyimbo hizi utumia lugha ya Kiswahili katika kufikisha maudhui ya nyimbo zao.
       ii.            Kwanini muziki wa kizazi kipya unasikilizwa na vijana tu?.
Swali hili liliandaliwa ilikukamilisha jambo mahususi lililoulizwa na swali kuu.Kwa kutumia swali hili mambo yaliyopelekea muziki huu kuwa mali ya vijana kwa asilimia kubwa na sio wazee.Swali hili lililenga zaidi katika kuibuka  na taarifa  kuhusu mada ya utafiti na kuweza kujua nini kianacho pelekea muziki huu kusikilizwa na vijana zaidi.
      iii.            Kuna machango gani wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.Swali hili liliandaliwa ilikujua mchango unaopatikana katika muziki wa kizazi kipya kwa jamii yetu,hii imetokana na sababu za mwanzo ambazo zilionyesha muziki huu ni wakihuni.hivyo swali hili litasaidia kufafanua mchango wa muziki huu katika utamaduni wa lugha yetu ya Kiswahili.
1.6 Manufaa ya Utafiti.
Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuleta manufaa yafuatayo:
         i.            Kwanza kabisa, utafiti huu utapendekeza maoni mbalimbali ambayo yanaweza kutumika kuharakisha utekelezaji wa wasanii kutunga nyimbo zao kwa kutumia misamiati iliyo sanifu ambayo itasikilizwa na jamii nzima.
       ii.            Vilevile, matokeo ya utafiti huu yatawasaidia viongozi  na Taasisi mbalimbali zinazohusika katika  kukuza lugha ya Kiswahili na sanaa, kuhakikisha wasanii wanaitumia vema lugha ya Kiswahili na kuuzingatia utamaduni wake wanapotunga nyimbo zao.
      iii.            Kuonyesha umuhimu wa muziki wa kizazi kipya kwa jamii nzima na kuisaidia jamii kuelewa mchango wa muziki wa kizazi kipya kwa vijana.
     iv.            Kuonyesha nafasi  ya lugha ya Kiswahili katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya.
1.9 Nadharia ya uchambuzi.
Utafiti huu utaongozwa na nadharia ya uhalisia  hivyo,ukusanyaji wa data,uchambuzi na uwasilishaji wake utafanywa kwa kuzingatia nadharia hii.
NADHARI YA UHALISIA.
Uhalisia ni hali ya ukweli kuhusu kitu au jambo na utayari wa kuupokea ukweli huo au kutendea kwa njia inayowezekana ,sifa ya kufanana kabisa na mtu,kitu,au mahali ambapo pamewakilishwa kwa njia ya michoro,muziki,mchezo wa kuigiza ,kitabu na filamu.Mtindo wa sanaa na fasihi ambao hujaribu kuwasilisha jambo ambalo linafahamika au liko wazi katika maisha halisi. Uhalisia kama nadharia ya kiuhakiki ni mkondo unaosisitiza usanii wa matukio       katika  fasihi ufanye matukio hayo yajitokeze kama maisha ya kila siku.
Neno uhalisia lilitumiwa kwa mara ya kwanza huko Ufaransa katika miaka ya 1850’s kwa lengo la kuelezea  kazi za sanaa zilizojaribu kusawiri ulimwengu kama ulivyo na si unavyodhaniwa   au kufikiriwa. Kama nadharia ya uhakiki,uhalisia huzingatia  namna ya ukweli unavyosawiriwa katika nyakati mbalimbali.Jinsi  ya kuusawiri au kuuelewa uhalisia hutofautiana  kutoka jamii hadi jamii na kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine,
            -Zamani za akina Galileo Galilei dunia ilidhaniwa kuwa kama meza,kumbe ni ya mviringo.
 -Zamani sayari  zilidhaniwa ni maumbo yasiyofikika,kiumbe kikitua huko,zitatunguka,kumbe ni mada zenye kudhibitiwa na mivutano  kama dunia.
            -Zamani kulidhaniwa kuwako ulimwenguni mmoja tu wenye mifumo ya jua ,kumbe yasemekana kuna ulimwengu zingine.
            -Zamani hakukuwa na vifaa anuwai  vya kisasa vya kizazi  na burudani ambavyo vimerahisisha sana maisha. Yote  hayo  na mengineyo mengi,kadiri ambavyo yamekuwa yakitokea,ndivyo  ambavyo yamebadili fikra za watu.
Kwa hiyo kila kizazi kina uhalisia  wake ambao huweza kusawiriwa na fasihi,lakini fasihi inaweza kusawiri uhalisia wa wakati ujao kwa kutumia huu uliopo.Hali kadhalika,fasihi inaweza kusawiri uhasilia kwa kutumia ubunifu unaongozwa  na msingi  ya kisayansi  na misingi ya kihistoria .
Nadharia ya uhalisia iliwekewa misingi na mwana-falsafa na Hegel katika kitabu chake cha Aesthetik(UJUMI),Hegel alipendekeza matumizi ya dhana ya uhalisia ielezee kazi ya fasihi inayowasilisha ulimwengu  wa maisha ya  kijamii  yenye wahusika wanaotenda mambo yanayodhibitiwa na hali ambayo wahusika hao wamo.Nadharia ya uhalisia husisitiza usawiri wa uhalisi katika ukamilifu wake,kwa maana kwamba yanayoshughulikiwa hayana budi kudhibitika.Hivyo mchango mkubwa wa nadharia hii ni kuchora maisha kama  yalivyo.
Mtaalam Larkin(1972),anasema  kuwa madhumuni ya mwandishi kwa anaowaandikia ni kuwaakisia ulimwengu wao wa kawaida,Kwa hiyo ulimwenguni huo sharti uwe halisi au wa ukweli.
Lukacs(1972),anasema  kuwa  nadharia  ya  uhalisia  ilianza  kuhusishwa  katika  fasihi kwa sababu waasisi wa nadharia  hii waliona kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya kazi za kisanaa na mtazamo wa msanii kuhusu  mazingira  aliyomo.
Hivyo,ninapotumia nadharia hii katika  fasihi tunataka kuona ni kwa kiasi gani mwandishi anatuleta karibu na maisha ya kawaida  ya kila siku.
Mhimili wa uhalisia ni  msanii kujitahidi kuchora maisha jinsi yalivyo  bila kuathiriwa;na hufanya hivyo kupitia vipengele muhimu vya maisha  kama  vile siasa,uchumi,utamaduni,jamii.lugha huwa ya kawaida inayoeleweka katika jamii  husika,mandhari na matukio yawe yanaonekana,kujulikana na yaendane  na jamii husika.,Msanii huangalia matatizo ya jamii na kuchunguza chanzo chake na kuzingatia mabadiliko ya  kihistoria ambayo husababisha hali mbalimbali ya maisha  ikiwa pamoja na kuathiri mfumo wa kifikra.
Hata hivyo  mchango wa  muziki wa kizazi kipya hususani katika kutumia lugha ya kiswahili  nitachunguza kwa kuangalia  vipengele vya  historia ya jamii lengwa,masuluhisho ya muziki  katika katika kutumia lugha ya Kiswahili kwa jamii na matatizo ya muziki hii katika  kulenga jamii.
>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>
Powered by Blogger.