HISTORIA YA MUZIKI WA HIP HOP NA BONGO FLEVA NA JINSI UNAVYOONEKANA KUATHIRIWA ZAIDI NA WASHAIRI WA KIMAPOKEO KULIKO WANAUSASA
Historia ya muziki wa
kizazi kipya (Hip Hop na Bongo Fleva)
Muziki wa Hip Hop tunaarifiwa kuwa
uliasisiwa na Wamarekani wenye asili ya Kiafrika katika mji wa Bronx huko New York
katika miaka ya 1970 (Omari, keshatajwa:1). Nchini Tanzania unakadiliwa kuwa
uliingia miaka ya 1980 Omari (keshatajwa), Mwanjoka (2011), Mbilinyi
(keshatajwa), Reuster-Jahn (2014). Katika kipindi hiki vijana wengi hususani
wale waliotoka katika familia zenye uwezo walianza kuimba mashairi (muziki) ya
rap kwa kuiga nyimbo zilizokuwa zikiimbwa na wanamuziki wa Marekani wakati huo.
Chachage aliwahi kuandika kuwa, katika mazingira hayo ndipo baadhi ya vijana
waliokuwa wakijitambulisha kwa kusikiliza muziki wa Reggae wa Bob
Marley na kucheza ‘Break Dance’ katika miaka ya 1980, ili
kujinusuru na kuyasahau matatizo yao, walipoanza kujipambanua na muziki
wa Hip Hop (Bongo Fleva). Mwanzoni ulikuwa ni muziki ulioambatana na
kuiga kisisisi muziki huo. Kuiga kisisisi maana yake kuiga kitu kama kilivyo.
Madai haya ya kuiga muzuki wa Marekani
yanaungwa mkono na Mwanjoka (keshatajwa, 8) anaposema,“Mbali na kuiga
nyimbo, vijana hao wa Tanzania waliingiwa na mapenzi ya ndani zaidi na
muziki huo hata kujikuta wakiiga mavazi, mitindo ya nywele, mienendo hadi
kuongea toka kwa wanamuziki hao wa Marekani na Ulaya.”
Hivyo tunaona kuwa wasanii wa Hip Hop na
Bongo Fleva mwanzoni walianza kuimba kwa kunakiri na kukariri mashairi ya
wasanii hao wa nje na hata midundo waliyokuwa wanaitumia ilikuwa ni midundo
hiyo hiyo ya wasanii wa nje. Mbilinyi (keshatajwa, 32) anaongezea kwa kusema
kuwa, “Kama kulitokea na aliyerap kwa kutumia lugha ya Kiswahili basi
alitumia flow (kutiririka) ya nyimbo za mamtoni zilizokuwa
maarufu kama ambavyo alikuwa anafanya mkongwe Saleh Jabir katika nyimbo kama
Ice Ice Baby ya Vanilla Ice na OPP ya Naught by Nature ilikuwa ndiyo staili ya
kipindi hicho.” Ufafanuzi katika mabano ni wetu.
Lakini baadaye wasanii wakaachana na
uigaji wa muziki wa kimagharibi na kuanza kutunga nyimbo zao binafsi kwa lugha
ya Kiswahili na Kiingereza jambo linaloendelea mpaka sasa ingawa tungo za
Kiswahili ndiyo hupewa nafasi kubwa. Na msanii wa kwanza kabisa kuanza kuandika
na kuimba kwa Kiswahili alikuwa ni Salehe Jabir ambaye kwanza tunaelezwa kuwa
alianza kubadilisha nyimbo za Kiingereza kwa kutumia Kiswahili zilizotamba
kipindi hicho na baadaye akaanza kutunga nyimbo zake mwenyewe. Hapo ndipo
ikachochea wasanii wengi kuona kumbe inawezekana kurap kwa Kiswahili ndiyo nao
wakaanza kujitokeza kutunga na kuimba kwa lugha ya Kiswahili, Mbilinyi
(keshatajwa) na Mwanjoka (Keshatajwa).
Baadhi ya wasanii na
makundi ya Hip Hop wanaotajwa kuwa ni waasisi wa muziki huu walikuwa ni, Fresh
XE, BBG, Adili Kumbuka, Salehe Jabir, KBC, Samia X, The BIG, Rymson, 2 proud
(Sugu), makundi ni kama vile, Kwanza Unit, Deplowmatz>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>>