Riwaya mpya ya Kiswahili

furaha? Nini maendeleo? Haya ni baadhi ya masuala machache yanayoulizwa katika riwaya hii ambayo inaweza ikaitwa riwaya ya kisomi au kifalsafa. Kazi zote kwenye mkusanyiko wa riwaya hii, kwa namna fulani, zina kipengele hiki muhimu cha usomi ambamo falsafa ya aina fulani inajadiliwa na kuendelezwa au kuchokozwa. Nagona inajishughulisha mno na suala la kutafuta ukweli. Safari yote ya mhusika mkuu ‘mimi’ ni safari ya kuutafuta ukweli ambao unaonyeshwa katika riwaya hii una nyuso nyingi. Mzingile inakita katika mzugiko wa akili wa mwanadamu katika kuumba hofu kwa dhana (kwa mujibu wa mwandishi) yake mwenyewe – dhana ya Uungu – kwa hivyo suala la nini dini? Nani Mungu? Ni dhana gani ya Uungu? Ina dhima gani dini katika maendeleo ya mwanadamu? Ziraili na Zirani inasaili haki ya dini moja kujiona bora kuliko nyingine iwapo lengo hatimaye ni kumwabudu Mungu mmoja yuleyule. Kwa nini watu wanagombana na kupigana katika vita vikali vya jihadi ikiwa ukweli wa Uungu ni mmoja na dini hatimaye zinafanana sana? Aidha inalaumu uwezo wa Kiungu unaosababisha tofauti za kimaisha hapa duniani. Kwa nini wengine wamepewa nafasi ya kuishi bora zaidi kuliko wengine na Mungu wao ni yuleyule mmoja? Jambo hili limeleta kani ya kufanyika mapinduzi mbinguni yakiongozwa na waasi akina Zirani, mhusika mkuu na wenzake wengine wenye msimamo wa kimaendeleo. Katika Babu Alipofufuka, Dunia Yao na hata Bina-Adamu, suala zima linaloshughulikiwa kifalsafa ni siasa. Nini maana ya uongozi au uongozi bora? Nini uhuru? Nini maendeleo? Nini maana ya kuishi? Nini uraia wa mtu? Nini uzalendo? Kwa nini pesa ina nguvu zaidi kuliko kitu chochote –hata zaidi ya heshima ya mtu? Zaidi ya mke na mtoto wake mtu? Zaidi ya hata nafsi yake mtu? Kwa nini kikundi kidogo cha watu kipange maisha ya watu wengi katika jamii fulani na nje ya jamii hiyo? Kuna dunia ngapi katika dunia moja ya jamii fulani? Mipaka ya dunia hizo ni miembamba au mipana kiasi gani? Nini maana ya kifo? Nini maana ya kuishi? Inawezakana mtu ambaye anaishi kuwa ameshakufa? Nguvu zipi zinaongoza ulimwengu wetu? Zinaongoza kwa masilahi ya nani na kwa taathira gani? Katika Bina-Adamu (uk. 53) na riwaya nyingine nguvu hizi zinaelezewa kwa ungamo la nguvu zenyewe zinazojieleza hivi: [I]takuwa vigumu kupambana nami ... Nimewaingia akilini kabisa. Ninahisika kwingi hata nisikokuwako. Kutokuwako kwangu ndiko hasa kuwako kwangu! ... Mwandishi wa Bina-Adamu (uk.154-155) anafikia hata kupendekeza kwa maneno ya wazi wazi namna gani ya kupambana na nguvu hii: [J]amii inahitaji kuelimishwa upya kuanzia chini hadi juu, mtoto hadi mzee, wote ... e.e. Huu ndio ukombozi ufaao; matakwa ya jamii yawekwe mbele. Kumbuka siku za ukombozi kuletwa na mtu mmoja zimepita! ... Unganeni kiuchumi, kisiasa na kijamii. Umoja ni nguvu! Mtaishia kumfunga yeyote, awe mkubwa! Nilikumbuka kile kisa cha Gulliver; jitu kubwa lililoishia kufungwa na wale mbilikimo waliokuwa wakiitwa Lilliputians ... Kwa njia hii mtaacha kuishi pembezoni pembezoni mwa kijiji! Itabidi tuwe nguli kupambana na hasidi wa kijiji – Global villain. 3.6 Lugha na Mvunjiko wa Utambulisho Uharibifu mmoja mkubwa sana wa utandawazi au bora tuseme utandawizi ni ule wa nguvu zake za kuvunja na kuharibu utambulisho wa watu katika viwango mbalimbali: kibinafsi, kinchi au taifa, kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kidini. Tunaambiwa katika Bina-Adamu (148) ... [U]limwengu umekuwa kijiji kidogo siku hizi, mipaka haipo tena ... Mtu binafsi amevunjikavunjika kwa sababu hana pahala pa kusimama katika kudai haki zake za msingi kama vile kuweza kupata kazi ya kumwendeshea maisha yake kwa sababu utandawazi/utandawizi umevuka mipaka na kuvunja kuta kuchukua vyombo vya taifa na kuvitia katika mitaji na utajiri au masilahi yao: viwanda vimenunuliwa, benki zimechukuliwa, machimbo ya madini na rasilimali nyingine yamehodhiwa, vyombo vya huduma vya wananchi kama mashirika ya usambazaji umeme vimebinafisishwa, huduma za maji na mafuta na sehemu ya shule na hospitali hazimo tena mikononi mwa serikali za wananchi. Uko wapi usalama wa taifa ukizingatia haya? Kinchi au kitaifa utandawazi/utandawizi umevunja nguvu na uwezo wa maamuzi ya nchi kiuchumi na kijamii. Nchi na taifa lazima zifuate masharti ya vyombo vinavyotetea utandawazi kama vile WTO. Kwa maneno mengine nchi changa ambazo haziwezi kujitegemea, sio tu hazina tena sauti katika mambo ya kiuchumi bali pia katika yale ya kisiasa na ya kidunia. Ni ajabu, kwa mfano, kuona kwamba nchi za Kiafrika au Dunia ya Tatu hazina msimamo wa dhahiri wa suala la ujangili na vita vinavyoendeshwa Iraki na Afghanistan –kimya kimetawala katika nchi hizi ambazo miaka iliyopita zilikuwa mstari wa mbele kukemea matendo ya mataifa makubwa. Ni muhimu kuwa na msimamo wa mambo haya kwa sababu Waswahili husema ukimwona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji. Sikwambii tena kiutamaduni, nchi changa zimekuwa nchi pokezi za tamaduni za wenzetu na hasa zile mbaya, hata maana ya utandawazi inageuka kuwa utanda-upande-mmoja. Katika riwaya hii mpya, lugha inayotumika mara nyingi ni ile ya kutokuwa na hakika tena ya jambo lolote. Hakuna hakika ya chakula, makazi, elimu, matibabu, heshima ya mtu, heshima ya nchi, uraia wake mtu, heshima ya Uafrika ambayo tokea mwanzo ilikuwa imekandamizwa sana wakati wa ukoloni. Mambo haya yote ndiyo yaliyokuwa msingi uliofanya nchi za Kiafrika na Dunia ya Tatu kupigania uhuru. Jambo hili limemfanya Wamitila kulalamika na kuhitimisha udhalimu wa utandawazi katika Bina-Adamu (uk.137) kwa kusema: [H]izi SAPS13 zinatusapa uhai ... Kijiji cha wizi hiki ... Dola inatukaba ... Yen ni kamba ya kitanzi! Ushahidi wa malalamiko haya umo pia katika Babu Alipofufuka (uk. 154) pale tunaposoma kwenye mabango ya maandamano ya kupinga utandawizi: ... M’mezifisidi nafsi zetu ... M’meivunja heshima yetu ... Vijana wetu wanapotea ... Vifo vya njaa na maradhi sababu si sisi ... Hatuna nafasi panapostahiki nafasi zetu ... Ardhi inachukuliwa hivihivi tunaona ... Kesho yetu imo katika giza ... Tunaangamia ... Tumeshakwenda kapa ... 13 Kwa urefu ni ‘Structural Adjustment Programmes’ Na hivi ndivyo tunavyomsikia mhusika mkuu Ndi-14 katika Dunia Yao (1) akilalama jinsi alivyovunjika kibinafsi... [L]abda nipo. Pengine sipo! Tofauti gani? Ndiyo, moyo bado unatuta. Hii labda ndiyo ishara pekee iliyobaki. Pangaboi linapepea pasi na nguvu za umeme. Kishumaa kidunya kinadiditia na kujitahidi kunilaza salama. Sijui lini lakini. Mwaka gani? Mwezi gani? Siku gani? Saa? ... Wakati hauwaziki tena –mashiko hauna, mantiki umeachana – umepoteza maana! Saa inatik’tika mezani. Inasonga mbele. Aaaa, saa! Chombo tu; na nambari zake, ishara ya jinsi wakati unavyokupuka –kasi, kasi; kasi isiyo kizuwizi. Lakini mbele nd’o wapi? Na nyuma ndiko kupi? N’navyojua mimi, wakati umeketi kichwani. Si juu ya uso wa saa ... 3.7 Mbinu Lugha zenye Mnasaba na Utandawazi/Utandawizi Kuna baadhi ya mbinu lugha ambazo waandishi wa riwaya hii wanazitumia kwa makusudi kuonyesha tabia na taathira ya utandawazi kwa nchi zetu. Mbinu ya kwanza ni ile ya maneno ambayo wameyaunda kuelezea hali hiyo. Kwa mfano, katika Babu Alipofufuka tunakuta meneno ‘uleo-wa-mawazo’, ‘ndoto-macho’, ‘kurongofywa’, ‘ukofiwatu’, ‘mkonowazi’, ‘mwambangoma’, ‘asijeurike’, ‘nakuona-wewe-mimihunioni’, ‘umaitikwenenda’, ‘mfuhai’, ‘watengeza-utamaduni-mpya’, ‘zizikinyesi’, ‘wenyesingazao’, ‘kizamoto’, ‘n’kupande-n’kushuke-kasheshe’, ‘tumejitoa-tumejitiawasasa’, ‘wapenda furaha’, ‘wapendakachiri’, ‘mmezakaseti’, ‘bwana-mwenye-nyumbakubwa’ n.k. Katika Dunia Yao tunasoma maneno kama vile: ‘pangaboi’, ‘mkaushausingizi’, ‘nyama- na- mifupa’, ‘kandamoyo’, ‘mtu- nyama– na- mifupa’, ‘baruapepe’, ‘wavumeme’, ‘umwamba- wa- kiume’, ‘kisichofaa- kinachofaa’, ‘babkubwa’, ‘elimujamii’, ‘wanaelimujamii’, ‘mkokota rikwama’, ‘dongo- la- zamani’, ‘mtapionuru’, ‘ki-TshombeTshombe’, ‘kimulatomulato’, ‘ki-hybridhybrid’, ‘ndoto-kweli’, ‘wauzatarabizuna- na- uzuri’, ‘Superboyswawili’ n.k. Katika Bina-Adamu, tunakutana na maneno kama ‘Bina-Adamu’, ‘wasichanawavulana’, ‘UMERO-JAPA’, ‘Zakongwe’, ‘Fyura’, ‘Fyuraha’, ‘rubo’, ‘Mefu’, ‘Yanguis’, ‘FUJO ASILIA’, ‘UMOJA WA FUJO’, ‘Jengo la Pembetano’, ‘zinatusapa’, ‘taifa-dola’, ‘Abubepar’, ‘Binberu’, ‘Mwajihawaa’, ‘Mwanakabila’, ‘Binrangi’, ‘Mkengeushi’ n.k. Pia riwaya hii inaingiza kwa makusudi maneno mengi ya kigeni kusisitiza usomi wa.......
>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>> 
Powered by Blogger.