SCIENCE PRACTICALSECONDARYNEWSENTERTAINMENTSHAHADA/UNIVERSITYSCHOLARSHIPSPRIMARY MCHANGO WA BONGO FLAVA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
SURA YA NNE.
4.0 MJADALA WA UTAFITI.
4.1Utangulizi
Sehemu hii ni ya muhimu sana kwasababu inaelezea namna utafiti ulivyofanywa uwandani .Hii ni sehemu yenye uchambuzi wa data pamoja na matokeo ya utafiti huu .hivyo katika sehemu hii mjadala wa utafiti umegawanyika katika sehemu kuu nne zinazo akisi maswali yaliyoongoza utafiti huu .Sehemu ya kwanza inaelezea hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
Sehemu ya pili inaelezea sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana kwa asilimia kubwa.Sehemu ya mwisho itaelezea mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
4.2 Hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu (2005)inasema kwamba “hadhi ni cheo daraja, uluwa,taadhima,utukufu,2.Heshima,staha,turuhani.Hivyo katika sehemu hii tutaangalia hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.Kutokana na utafiti ambao umefanyika na mtafiti anathibitisha hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya kwa kuangalia hadhi ya juu na hadhi ya chini.
4.2.1Hadhi ya juu ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.
Katika kuitazama hoja hii mtafiti anathibitisha hoja hiyo kwasababu zifuatazo: kutokana na utafiti na utafiti uliofanyika imeonyesha kuwa lugha ya kiswahili lugha ina hadhi ya juu katika muziki wa kizazi kipya kuliko lugha zingine wanazo zitumia wasanii wengi wa Afrika Mashariki kwa ujumla kwa mfano wasaniii wa Tanzania ambao wengi wanatumia lugha ya Kiswahili katika kutunga mashairi ya nyimbo zao nyingi.Lugha ya Kiswahili inapewa kipao mbele katika nyimbo/mashairi yao kutokana sababu zifuatazo:
Lugha ya Kiswahili ni lugha ya Taifa kwa nchi za Afrika mashariki.Lugha ya Kiswahili ni lugha ya taifa ambayo imepitishwa na sera ya lugha na mpango wa lugha ,ni lugha ambayo inaeleweka zaidi kwa jamii inayosikiliza mashairi ya wasanii wa muziki huu, wasanii wengi hutumia lugha ya Kiswahili kwasababu ndiyo lugha wanayo ifahamu vema na hii ndiyo sababu ya wasanii wengi kujiingiza katika muziki pasipo kuwa na elimu ya kutosha hivyo wengi wao uimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili kwasababu ndiyo lugha wanayoifahamu vema ingawa lugha hii pia ni lugha ya mawasiliano kwa nchi za afrika mashariki.
Urahisi wa lugha ya Kiswahili.Lugha ya Kiswahili ni lugha ambayo ni rahisi na inaeleweka vema kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya hivyo inakuwa rahisi kwao kuzungumza kutunga mashairi yao kwa kutumia Kiswahili na si lugha zingine ambazo hawazifahamu vizuri.
Katika utafiti uliofanyika nilimhoji kijana mmoja anayesomea shahada ya isimu ya Kiswahili, mwaka wapili katika chuo kikuu cha Dodoma kuhusiana na hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya, anayefahamika kwa jina la Rehema mhapa na kusema hivi:
“Lugha ya Kiswahili kwa mimi binafsi ni lugha ambayo naipenda sana kwasababu
Ni lugha yangu ya taifa pia ni lugha ninayoielewa na nina uwezo wa kuizungumza
Kwa urahisi bila kusitasita kama lugha zingine za kigeni mfano kingereza.Mimi ni
Mpenzi mzuri wa muziki wa kizazi kipya kwasababu mashairi yao wanatunga kwa
Kutumia lugha ya kingereza,hivyo hata ninapo sikiliza na furahia vionjo
vilivyopo kwasababu lugha inayotumika nina ielewa vema na kilichopo ndani ya
nyimbo yaani ujumbe naelewa zaidi kuliko nikimsikiliza 50cent.”
Kwa kuzingatia maelezo ya muhojiwa hapo juu tunapata dhana kuwa wasanii pamoja na wasikilizaji wanaipa hadhi ya juu lugha ya Kiswahili kwa sababu ndiyo lugha yao ya taifa na wanaielewa vema kutokana na lugha hiyo kuitumia katika mawasiliano yao ya kila siku.
Kijana mwingine ambaye naye ni mwanafunzi anayechukua shahada ya kwanza ya isimu ya Kiswahili pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye alijifahamisha kwa jina la James Christopher a.k.a JC aliseama hivi:
“Mimi katika utungaji wa nyimbo zangu napenda kutumia lugha ya Kiswahili
Kwasababu Ndiyo lugha ambayo ninamisamiati ya kutosha hata katika
utungaji wa mashairi yanguSiwezi kukwama kama ambvyo nikitumia lugha ya Kiswahili kwahiyo hapo na kuwa naSwaga za kutosha katika kuimba na utungaji wa nyimbo zangu,na isitoshe ndiyo lughayangu ninayo itumia katika mishemishe zangu za kitaa”
Wasanii wengi wanaifahamu lugha ya Kiswahili zaidi.Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya elimu yao ipo chini kwasababu wasanii wengi wameishia darasa la saba wengine elimu ya sekondari waliojitahidi sana kidato cha sita ingawa asilimia kubwa wengi wameishia kidato cha nne,hivyo kutokana na utafiti uliofanyika inaonyesha kuwa wasanii hawa hawatumii lugha ngeni zaidi kutokana na kigezo cha kutokuwa na elimu ya kutosha na wengi wao wanajiendeleza kwa kujifunza lugha ya Kingereza na lugha zingine wanapokuwa wamefanikiwa katika soko la muziki, ili waweze kuwa na mawasiliano mazuri wanapo pata fursa ya kwenda kufanya shoo za nyimbo zao n’je ya nchi.Hili tatizo ni kubwa na utafiti unaonyesha kuwa vizazi vya sasa wengi wao wana kimbilia kuimba wanapo shindwa kufaulu vema katika masomo yao pia wanapokuwa wamefanikiwa katika ajira hii ya muziki wanaikwepa elimu na kuendelea na muziki.Hali hii ndiyo inayopelekea lugha ya Kiswahili kupewa fursa ya kwanza katika utunzi wa nyimbo nyingi za wasanii wa muziki huu wa kizazi kipya.
4.2.2 Hadhi ya chini ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kpya.
Katika kuitazama hoja hii mtafiti anathibitisha hili baada ya kuchunguza na kupata majibu tofauti kutoka kwa watafitiwa namna ambavyo lugha hii inavyochukuliwa na jamii wanaposikiliza muziki huu wa kizazi kipya.Yafuatayo ni maelezo ya baadhi ya watafitiwa kuhusiana na lugha ya Kiswahili kuonekana ina hadhi ya chini kutokana na namna inavyotumika katika nyimbo hizi za kizazi kipya.Yafuatayo ni maelezo ya watafitiwa kuhusiana na hoja hii ya Kiswahili kuonekana ina hadhi ya chini katika muziki wa kizazi kipya.Mkazi mmoja wa Dodoma aliyejitambulisha kwa jina la mary john ambaye ana umri wa miaka 23,ni mfanyakazi wa saluni alisema hivi:
“Wasanii wetu wanatumia lugha ya Kiswahili vibaya,misamiati wanayoitumia katikaNyimbo zao inashusha hadhi ya lugha ya Kiswahili kwasababu wao wanatumia lugha isiyotafsida katika nyimbo zao katika baadhi ya nyimbo zao na kuharibu utamaduni wa Misemo wanayoitumia ni ya mtaani sana kiasi kwamba baadhi ya maneno hatuyaelewi Vema na ujumbe haufiki ulivyokusudiwa kwa jamii,zaidi wanao faidi muziki wa kizazi Kipya huwa ni vijana tu.”
Hivyo basi lugha ya Kiswahili inashushwa hadhi kutokana na matumizi mabovu ya lugha wanayoitumia na kupelekea muziki huo kuonekana ni wa kihuni miongoni mwa wapenzi wa muziki huu na wasikilizaji wa muziki wa kizazi kipya,kwa asilimia kubwa muziki wa kizazi kipya hapo mwanzo ulionekana ni wa kihuni na unawahusu vijana kutokana na muziki huu mwanzoni uliimbwa na vijana kwa lengo la kufikisha matatizo ya vijana kwa njia ya nyimbo mfano katika swala la ajira kwa vijana,manyanyaso,umasikni na elimu vyote hivi viliimbwa na wasanii hawa lakini hivi sasa nyimbo hizi zimekuwa na changamoto kubwa katika mapenzi zaidi na kusahau mambo mengine ya kijamii ambayo wakiyaimba yataigusa jamii kwa undani zaidi.mfano misamiati aliyo itumia masanii huyuAboubakar Chende mwenye umri wa miaka 16 anayejulikana kwa jina la Dogo janja yupo kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Makongo katika wimbo wake wa najua kuna misamiati aliyoitumia ambayo kwa mtu mzee hawezi kuelewa nini anachomaanisha mfano katika ubeti huu:
“Nakimbiza kinyama mapaka maboya wanahema,hakuna kuhanya,tunawameza
Tunawatema,mtakipatapata fresh ya mwaka paka wanatetemeka kuona wabena
Meka tuko full mzukaaaaa,Wagoro tulianza tu Ngarenaro Masoro wameishiwa
Idea wanatubero yelooooooooooo!”
Misamiati kama “kinyama” akimaanisha yeye ni zaidi katika kuimba,”kuhanya” ni neon la kibantu likiwa na maana ya kuhangaika au kuwa na hofu,”full mzuka” likiwa na maana ya kuwa kamili yaani kujikamilisha hivyo basi mtu mzee hawezi kuelewa nini anacho maanisha msanii huyu.Hali hii ndiyo inayopelekea hata jamii nyingine kuona lugha ya Kiswahili ni lugha ya kihuni hivyo hali hii inashusha hadhi ya lugha ya Kiswahili kutokana na utumizi mbovu wa maneno yasiyo sanifu.
Uchanganyaji wa msimbo.Kitendo cha kutumia lugha mbili katika sentensi moja au msamiati mmoja mfano katika wimbo huu wa msanii Nick aliomshirikisha Joe Makini katika mojawapo ya mistari iliyopo katika wimbo wake huo kachanganya lugha ya Kiswahili na kingereza kama ifuatavyo:
“Yaani four plus four mtaani sio eight na bado utajiri aupo
Nyuma skirt,hey babies squeeze everybody tuwanasomebody
High,high me take you higher,nakupeleka higher higher
Nakuhitaji kwa higher higher”
Msanii kaingiza maneno ya kingereza katika mistari ya nyimbo zake na hivyo kufanya lugha ya Kiswahili kuonekana kuwa haijitoshelezi kimsamiati,hali hii ipo katika nyimbo nyimgi za wasanii wa muziki wa kizazi kipya.Utafiti umeonyesha kuwa wasanii wengi huchanganya lugha lugha kwa lengo la kupata soko la kazi zao kwa jamii,wasanii wanapo tumia lugha mbili mfano kingereza na Kiswahili,Kiswahili na lugha za asili au kuchanganya na lugha zingine aidha kwa kuwashirikisha wasanii wa n’je katika kuimba nyimbo zao mfano wimbo leo wa msanii Ay aliomshirikisha msanii mwanadada Avril:
“Excuse me baby boy yasikie yanayotoka moyoni mwangu
Inabidi ungoje boy nishalizwa, nishaumizwa sana
Sina imani sina imani tena nishalizwa nishalizwa sana
No no no aaaah aaaah I like the way your lakini
Sidhani utanifaa kunipa raha hahahaha! My heart is ready
And let it be.”
Nilipata uthibitisho huu baada ya kupata maelezo kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye niliweza kuzungumza naye kwa njia ya simu wakati akiwa katika tamasha la burudani nyumbani mjini Mbeya katika uwanja wa Nzomwe ambalo huwakusanya vijana pamoja na wasanii tofauti kwa lengo la kutoa burudani ya kutosha kwa wapenzi wa muziki wa kizazi kipya.Msanii Danny msimamu yeye alisema kuwa:
“Mimi kwa upande wangu naweza kusema kuwa tunatumia lugha ya kingereza
Ilikuweka swaga tofauti katika nyimbo pia mpango mzima ni kupata mashabiki
Wakutosha na kupata soko kutoka n’je na ndani ya nchi,kitu kingine ni kuongeza vionjo na kuonekana tofauti na wasanii wengine ndiyo sababu wengine wanapenda kutumia lugha zao za asili,pia hata waandaaji(producer)wakati mwingine wao ndiyo wanapenda kutumia lugha ya kingereza,mfano mimi katika wimbo wangu I just wanna peace mwanzoni producer(muandaaji)alipenda nianze kwa kuimba kingereza”
hii ni baadhi ya mistari ya mwanzo ambayo msanii huyu aliimba kwa kunipa vionjo vya mwanzo vya wimbo huu ambao lengo kuu ni kuwaasa wezi wa kazi za wasanii kuacha na kuwaonea huruma wasanii hawa:
“It is the shame some nigger gonna slow the rolemen,slow down
Your roll player,you know what I mean cause some nigger
Have been acting right you know when you act like this is like
You don’t know what time is,so listen up here goes you nigger talking shit.Nimechoka nyimbo zangu kupigwa redioni halafu silipwi hata kumi
Huu ni uhuni ,redio zinaingiza kwa matangazo ya biashara,inamaana
Wimbo wangu unaopigwa ni hasara kwanini haulipwi huu ni uchawi
Sheria haizingatiwi au nazo wameziloga,nazielezea hisia zangu bila uwoga”
Hivyo hali hii ndiyo inayoonyesha hali kubwa iliyopo sasa kwa wasanii wengi ambao wameimba kwa kuchanganya lugha tofauti katika lugha zao huku lengo lao kubwa likiwa ni kufikisha ujumbe kwa jamii,kwa watu wengine ambao wanafahamu lugha ya Kiswahili na wasio fahamu lugha ya Kiswahili.Huku wasanii wengine wakitumia lugha zao za asili katika kuimba ili kuitangaza lugha zao na utamaduni wao mfano Mr.Ebbo katika wimbo wake wa mimi mmasai bwana.
“mimi mmasai bwana nasema mimi mmasai nadumisha mila ile nyingine ishashindwa Mi mmasai bwana nasema mi mmasai”
4.3 Sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana kwa asilimia kubwa.Swali hili ni mojawapo ya maswali katika maswali ya utafiti huu,linajadili mambo ambayo yanachangia vijana wengi kusikiliza muziki wa kizazi kipya kuliko kundi lingine katika jamii.Utafiti huu umepata data ambazo zinapelekea vijana wengi kusikiliza muziki wa kizazi kipya zaidi kuliko nyimbo zingine kama nyimbo zingine ,mfano dansi,r&b na ragge,sababu zilizopatikana kutokana na utafiti huu ni lugha inayotumika kwenye nyimbo hizo ni ya mtaaani,nyimbo nyingi zinalenga maisha ya vijana,ni sehemu ya ajira ya vijana ambayo wanaitegemea,vijana wengi wanapenda utamaduni wa nje kuliko utamaduni wao pia muziki wa kizazi kipya ndiyo muziki ambao kwa sasa una wafaa vijana kutokana na kipindi kilichopo.
Lugha inayotumika katika muziki wa kizazi kipya ni ya mtaaani.Kutokana na utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa kwa asilimia kubwa misamiati wanayo itumia katika mashairi yao sio sanifu utumizi wa maisamiati ya mtaani ndiyo chanzo cha vijana kusikiliza muziki wa kizazi kipya kwa sababu kinachoongelewa katika nyimbo hizo huwa wanaelewa vema ,tofauti na mzee ambaye akika kaa na kusikiliza nyimbo hizo hawezi kuelewa kabisa nini kinachozungumzwa katika nyimbo hizo.mtafiti alipata uthibitisho wa data hii baada ya kufanikiwa kumuhoji mzee Abdallah Yusufu mwenye umri wa miaka 55 mfanyabiashara wa Dodoma katika soko la Sabasaba wakati akijibu swali hili kuwa kwanini muziki wa kizazi kipya uansikilizwa na vijana kwa asilimia kubwa:
“Mwanangu mimi mzee na mda wote nipo hapa sokoni,kwanza wanachokiiamba
Vijana hawa wa siku hizi mimi naona uhuni maana huwa hata sipendi kusikiliza
Nyimbo zao,mwananagu hata nikisikia sitelewa maneno wanayoyatumia”
Kijana mmoja ambaye ni mwanafunzi wa sekondari ya Jamhuri mjini hapa Dodoma yeye alisema
“Sisi vijana tunapendelea muziki wa kizazi kipya kwasababu ndiyo muziki wa vijana
Hatuwezi mkusikiliza dansi wala zilipendwa kwa kuwa hizo nyimbo zilikuwa za wazee
Wetu,pili ukizingatia muziki huu wa unatugusa vilivyo yaani zile swaga zake mimi
mwenyewe nazikubali sana hasa msanii Chidi benz,Mr.temba kiujumla kundi
zima la wanaume family kwamba wanacho kiimba kinatugusa vilivyo”
Hivyo basi kutokana na data hii tunaona kuwa muziki wa kizazi kipya ni wa vijana wakileo mfano katika wimbo wa msanii Chidi benzi katika wimbo wa Dar es salaam stand up tunaona maudhui yanayo imbwa na misamiati iliyopo ndani ya wimbo huu zinavyo akisi vijana zaidi na kufanya wazee kushindwa kuelewa baadhi ya maneno yana maanisha nii katika nyimbo zao.
“ Sijali bado chenga nawakomba ,mi beat na talwaza kama mumii na komba
Kama shilingi na konda,kicheche na ng’onda mlio wa vuumu na Honda
Spiriti na kidonda ,sipigani nikang’ata basi bora nikimbie ,si ng’ang’ani kung’ata
Bali uwezo ndiye , napanda siku baada ya siku sipandi mchana nishuke usiku
Naamini kitu kuliko kukosa kitu ,love kwa wasanii,love kwa wana jamii
Love mpaka kwa kina na niii hihiiiiiiiii hiii msitenge mwenzenu jamani chonde
Nawawakilisha mtatoka msikonde,hey my African people tukaze tusonge mbele
Nawa wakilisha tusisahau hii miiko tusonge mbele tugange basi hayo tusonge mbele
Tuachekupiga miayo tufikiri kwa urefu”
Hivyo basi katika wimbo huu ambao msanii anawataka watu kuwa amka katika swala la maendeleo na na pia wale wenye nia ya kuimba wasichoke bali wakaze mwendo ndiyo maana anasema sing’ang’ati kung’ata bora akimbie bali uwezo wake ndiye.hivyo basi kama mtu mwenye lengo na nia kweli inakubidi kupambana.
pia wasanii wa Tanzania wameanza kuimba nyimbo zao kwa kuingiza lugha ya kisheng katika nyimbo zao ambapo kishengi ni lugha ya mseto inayojumuisha Kiswahili na Kiingereza na hata msamiati kutoka lugha zingine za Kenya Sheng ni kifupisho cha “Swahili-English ,Sheng ni namna ya msimbo au kilahaja cha kundi fulani miongoni mwa vijana. Mfumo huu wa mawasiliano umesanifiwa na vijana hasa wale wanaoishi katika sehemu za mjini .Mfumo huu wenyewe hufuata muundo wa kisarufi wa Kiswahili na lugha nyinginezo za Kibantu ila hutumia maneno mengi mapya ya kubuniwa na ya mkopo kutokana na lugha mbalimbali kikiwemo kiingereza na lugha nyinginezo za Kiafrika kama vile Kikamba,Kiluo, Kikuyu, Kiluyia na Ekegusii. Maelezo haya ya kijumla kuhusu maana ya Sheng yametolewa na wasomi kadha kama vile:
Mkangi (1984: 17), ambaye ameueleza msimbo huu kama lugha mseto au lugha “kiunzi” ya kizazi kipya cha vijana wa mijini. Pia Ogechi (2002: 3) and Shitemi (2001) wanakubaliana na maoni hayo kwamba Sheng ni msimbo wa kijamii unaotumiwa hasa na vijana wa mjini na
mashambani nchini Kenya. Maelezo haya yanatoa baadhi ya sifa za kimsingi zinazoutambulisha msimbo huu. Kwa mfano, hutumiwa sana na vijana ilikuji tambulisha kama kama kundi la kijamii. Maoni haya pia yameungwa mkono na shitemi.Wachunguzi wengi wanakubaliana kuwa Sheng ilizuka katika miaka ya katikati ya sitini na sabini katika sehemu za makazi za Mashariki mwa jiji la Nairobi kama vile mitaa ya: Kaloleni, Mbotela, Kimathi, Pumwani, Majengo,Bahati, Buruburu, Barma, Umoja, Dandora, Huruma, Mathare, Eastleigh na viunga vyake(Mbaabu na Nzunga, 2003). Kufikia miaka ya awali ya 1970,Sheng ilikuwa imepamba moto sio tu Nairobi bali pia katika miji mingine kotenchini Kenya. Kufikia sasa, Sheng imekuwa kitambulisho cha takriban vijana wote nchini, mijini na mashambani wawe wa shule au la.
Kwa mujibu wa Mukhebi (1986: 11), Sheng ni tukio la kitamaduni ambalo linafungamana sana na mawazo au fikira, hisia na matakwa ya watumiaji wake.Anaeleza kuwa wazungumzaji asilia wa Sheng waligundua kuwa kutokana na hali na mazingira yao ya kifukara katika mitaa ya jamii yenye mapato ya chini,wasingeweza kupata elimu yao na kuwasiliana kupitia Kiingereza bali
walihitaji mfumo wao wenyewe. Anaongezea kuwa kutokana na ufahamu wao duni wa kingereza Kiingereza, iliwawia vigumu vijana hao kuweza kujifunza masomo mseto kwa kingereza kama vile Historia, Jiografia, Fasihi na maisha ya kijamii ya waingereza,masomo yaliyokuwa ya kimsingi katika mitala ya shule za msingi wakati huo.
Kuna nadhariambalimbali zinazojaribu kueleza asili na chimbuko la Sheng. Hata hivyo,
nadharia kuu ni mbili; nadharia ya uhuni na nadharia ya msimbo wa vijana. Kwa mujibu wa nadharia ya uhuni, msimbo wa Sheng ulibuniwa na kuibuka kutokanana wahuni au wakora jijini Nairobi (Kobia, 2006). Waliunda baadhi ya manenokutoka nyuma kuelekea mbele badala ya muundo wa kawaida wa neno. Kwa mfano, neno kama ‘nyama’ lilibuniwa na kuwa ‘manya’. Nadharia inahusishakubuniwa kwa Sheng na haja ya wahuni kuwasiliana kwa ‘lugha’ ambayo watu wengine hawangeweza kuifahamu.
.
Kufuatia kupatikana kwa uhuru hapo mwaka wa 1963, idadi ya wakazi wa jiji la Nairobi ilipanda kwa haraka sana kutokana nakumiminika kwa watu kutoka mashambani wakitafuta nafasi za kazi katika mitaa ya viwanda humo jijini. Wananchi hao maskini waliishia kuishi katika
mitaa ya makazi duni ya viwandani mashariki mwa Nairobi ambapo ndio kitovu cha maendeleo ya viwanda. Ijapokuwa wafanyikazi hawa pamoja na jamii zao walilazimika kutumia Kiswahili kwa mawasiliano baina yao, wengi walikichukia Kiswahili kwa vile kilikuwa kimedunishwa sana na sera ya ukolonikama lugha ya mashambani, lugha ya vibarua au “maboi” wa kuwatumikiaWazungu.Hata hivyo, watoto wa wafanyakazi hao hawakupendelea kuendelea
kukitumia Kiswahili kama wazazi wao kwa sababu kadha. Kwanza kabisa,
kinyume na wazazi wao, watoto wale walilazimika kuishi katika hali ya jamii yautatu-lugha: lugha za kinyumbani, Kiswahili na Kiingereza. Pia, walitambua kuwa ingawa walibidika kutumia lugha nyingi, ni Kiingereza pekee ambachokilipewa hadhi ya juu kama lugha ya utawala, mamlaka, heshima na uwezo wa kiuchumi.Ili kuepuka matatizo ya kimawasiliano na kama njia ya kusuluhisha utata wa hali hiyo iliyowakabili, vijana hao waligundua msimbo wa mawasiliano kati yao ambao, ingawa ulifuata sarufi ya Kiswahili, uliazima msamiati kutokana na
lugha za kiasili na kuunda baadhi ya maneno yake. Msimbo huo ndio uliotokea
kuwa Sheng hapo baadaye.
Lugha hii ya kishengi imeanza kujitokeza katika nyimbo za wasanii Tanzani na hii inatokana kitendo cha kuingiliana kwa jamii,pia wasanii kushilikishana katika nyimbo zao na kupelekea baaadhi ya misamiati ambao ipo katika lugha hii ya kishengi ambayo ni lugha ya vijana kupelekea kusambaa kwa jamii yetu ya Tanzania ingawa lugha hii bado haitumiki sana na vijana wa kitanzania ambapo baadhi yao wamekuwa wa kiiga na baadhi ya wasanii wa Tanzania wanatumia lugha hii katika nyimbo zao.Data za utafiti huu zinaonyesha kuwa wasanii wengi wa nchini Kenya ndiyo wanatumia sana lugha hii ya kishengi mfano Jua kali,Nonini,Nameless na wasanii wengine mfano wa baadhi ya maneno ya kishengi yanayo tumika na vijana na jinsi yalivyo katika lugha ambazo wana kopa maneno hayo au kutohoa kama yalivyo na kubadili mtindo wa msamiati hiyo mfano:Mifano ya matumizi kama hayo ya Kiingereza yametolewa na Nnamonu(1995), ambaye amedai kuwa mengi ya matumizi kama hayo huwa ni makosa yasiyokusudiwa na yanayotokana na athari za lugha za kiasili za Kiafrika. Bila shaka, Sheng imekuwa ikilaumiwa na waalimu kuwa ndicho chanzo kikuu chakuzorota kwa Kiingereza na Kiswahili sanifu nchini Kenya. Katika mifano hii,watumiaji hutamka dhana za Kiingereza kwa wingi ambazo kwa hakika hazina wingi: Mifano
Kiingereza Kiswahili
accommodation(s) malazi
ammunition(s) risasi
behaviour(s) tabia / desturi
cutler(y|ies) vyombo vya kulia
equipment(s) vifaa
elite(s) wasomi
Sheng Kiswahili san ifu
hitaji mahitaji
oni maoni
sumbuko masumbuko
jaribu majaribu
lezi malezi
Uundaji wa Nomino
Kama anavyosisitiza Ogechi (2005), uundaji wa maneno katika Sheng ni utaratibu changamano unaohusisha mbinu tofauti na kufuata hatua kadha.Akitumia mifano ya uundaji wa majina au nomino, vitenzi na vivumishi, Ogechianaonyesha kuwa leksia za Sheng hutokana na vianzo maalum katika Kiswahili,Kiingereza na lugha zingine za Kenya.Uundaji wa maneno katika msimbo wa Sheng hutumia njia mbalimbali.
Kuna matumizi ya ukopaji wa maneno kutoka lugha ya Kiswahili, Kiingereza nalugha nyingine za Kiafrika. Kuna pia kubuni kinasibu kwa maneno ya Sheng.Zifuatazo ni baadhi ya nomino zinazopatikana katika msimbo wa Sheng:
gichagi sehemu za mashambani
moti gari
chapaa pesa
manyakee wasichana
budaa, mbuyu baba
kingoso Kiingereza
dem msichana
Uundaji wa Vitenzi
Baadhi ya vitenzi huundwa kwa kuunganisha mwanzo kiambishi ku- na mzizi kwa kitenzi mkopo kutokana na lugha nyingine za Kenya au vitenzi vipya vyakubuniwa vilivyopewa kiambishi cha mwisho cha Kiswahili. Mifano:
ku-bonga kuzungumza
ku-ush kuondoka
ku-no kukasirika
(Kiingereza: “knock
Ufupishaji wa maneno
Katika msimbo wa Sheng, baadhi ya maneno ya Kiingereza yanayokopwa hufupishwa ili kuunda maneno mafupi. Maneno haya hujitokeza kama dokezo laneno kamili. Baadhi ya mifano ni kama vile:
tao mji (Kiingereza: “town”)
mat matatu
hao nyumba (Kiingereza: “house”)
Swa Kiswahili, Swahili
Cole chuo (Kiingereza: “college”)
pero mzazi (Kiingereza: “parent”)
hasii bwana wa
(Kiingereza:
>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>