"Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamechagia fasihi simulizi kuwa na sura mpya",Jadili kauli hii kwa mifano halisi.
"Fasihi simulizi ina tanzu za watoto na watu wazima",Chagua tanzu mbili za watoto na tanzu tatu za watu wazima kisha eleza faida na hasara kwa jamii inayohusika.
Jadili aina mbalimbali za wahusika watumiwao katika fasihi simulizi.
Fasihi simulizi hutumia zaidi wahusika wasio binadamu kwa malengo, fafanua malengo hayo kwa hoja madhubuti.
Fasihi simulizi hubadilika badilika kama kinyonga, jadili kauli hii kwa hoja mbali mbali.