Riwaya mpya ya Kiswahili
riwaya yenyewe na pia
ugeni na wizi wa utandawazi wenyewe. Katika Nagona kwa mfano, tunapata maneno
kama ‘Ego’, ‘Id’, ‘Superego’, ‘Sphinx’, ‘Cogito’, ‘Causa’ ‘Ultima’, ‘Disciplina
Voluntatis’, ‘De Anima’, ‘Politica’, ‘Metaphysica’, ‘De Poetica’, ‘Totem’,
‘Oedipus Complex’, ‘Neurosis’, ‘ashab’, ‘tabilin’ na ‘tafsir’. Katika Babu
Alipofufuka tunaona maneno kama ‘Gangar Wa’azu’, ‘Doggy’, ‘Neo- Casino’, ‘Proteus’,
‘Limonsin’, ‘shoyu’, ‘sake’, ‘beetles’, ‘spring chicken’, ‘semaa wa twaa’,
‘FKK’, ‘CD-ROM’, ‘Mona Lisa’, ‘zerha’, ‘manekineko’. Katika Dunia Yao tunapata
maneno kama ‘Muse’, ‘CD’, ‘video’, ‘TV’, ‘taj’widi’, ‘maulidi’, ‘kasida’, ‘C
Licence’, ‘TX’, ‘chip’, ‘Hillman’, ‘Vauxhall’, ‘mamluki’, ‘The Aritos’, ‘New
World Order’, ‘WTO’, ‘Globalisation’, ‘sanctions’, ‘RAP’, ‘Paradise’, ‘I Need
to Know’, ‘fantastic’, ‘Skyscrapers’, ‘cloning’, ‘dialectics’, ‘Zeus’,
‘Mnemosyne’, 14 Neno lenyewe kama jina la mhusika mkuu ‘Ndi-‘ limemeguka,
limevunjika. ‘Calliope’, ‘Clio’, ‘Erat’o’, ‘Euterpe Melpomene’, ‘Polyhymnia’,
‘Terpsichore’, ‘Thalia’, ‘Urania’ n.k. Katika kipengele hiki pia tunaingiza
uvunjaji wa kanuni za kisarufi, kiutanzu na kiujumi katika matini ya baadhi ya
riwaya za mwelekeo huu. Uvunjaji huu unalinganishwa na uvunjaji wa kanuni kadha
katika jamii ambazo zilidhaniwa zimeshakita na zisingeweza kuvunjwa kamwe. Ni
wazi kwamba katika Babu Alipofufuka na Dunia Yao kanuni za sarufi zinavunjwa
makusudi kama tunavyoona katika Babu
Alipofufuka...[u]wanja-wa-ndege-wa-kimataifa alisimama kujitayarisha kwa
ufunguzi wa milango (uk.29) ... komputa alimwambia kwamba mkewe Bi. Kiluba
alikuwa akimsubiri kumbi la chini (uk.67). Au katika Bina-Adamu tunagundua
kauli kama ...[I]nasemwa kuwa ... (uk.35) ambayo imechukuliwa moja kwa moja
kutokana na Kiingereza balada ya Kiswahili Inasemekana kuwa ... [W]anaamini
kwamba ukoo wao ni tukufu (uk.38) badala ya Ukoo wao ni mtukufu ... [H]apana,
labda ni kimo changu cha mtoto (uk.45) badala ya Hapana, labda kimo changu cha
utoto ... Matumizi wa sanaahati15 – yaani namna ya kucheza na mwandiko wa
maneno ili kutoa hisia fulani ya kimaana au ujumi ni njia nyingine ya matumizi
ya lugha kuelezea hali na taathira za utandawizi katika baadhi ya riwaya hizi,
hasa katika Babu Alipofufuka, Dunia Yao na Bina-Adamu. Katika Babu Alipofufuka
ukosefu wa uaminifu na kigeugeu cha utandawazi wenyewe na viongozi wakuu wa
nchi wanaoutekeleza kwa shauku, unaelezewa katika mabadiliko ya uherufi katika
sura mbalimbali kama vile tunavyoona katika neno Proteus linavyochorwa
kiwimawima, kimlalo (kiyombo), kimkolezo, kimfifio, kiudogo na kiukubwa. Kwenye
Dunia Yao tunapata nambari 36 ya miaka ya uhuru wa Zanzibar inakolezwa makusudi
ili msomaji atafakari mafanikio na mashindikano ya wakati wa baada ya uhuru wa
miaka hiyo 36. Maneno Wewe na mimi (uk.20) yanatofautishwa kwa mkozesho na
udogowesho kusisitiza ubinafsi na ule ukilamtu- na-lake wa siku hizi.
Usichochote nao unasisitizwa katika mpromoko wa maneno cider na nonentity. Neno
Superboyswawili linalosisitiza Umarekani na Urusi wakati wa vita baridi
linatiliwa mkazo na mkolezo wa wino. Neno ilhamu linalosisitiza kuzuka kwa
riwaya mpya katika wakati wa utandawazi na kuwepo mtindo wa riwaya ndani ya
riwaya (metafiction) au uzungumziaji wa riwaya ndani ya riwaya hasa kujibu hoja
ya baadhi ya wahakiki kwamba riwaya sharti ichukue mkondo wa uhalisia –
limekozeshwa wino pia. Bina-Adamu inatumia mkolezo wa wino au/na yombo na
herufi kubwa katika msisitizo wa baadhi ya maneno yake kama Njia ya UHALISIA,
UMERO-JAPA, Gastarbeiter, Nurenibaga, daktari wa kifo, Osagyefo n.k. Muhimu
sana katika mbinu hii ni jinsi inavyotofautisha sauti za wasimulizi na wahusika
mbalimbali katika riwaya ambamo herufi wima, herufi mlalo au yombo na herufi
yombo zilizokolezwa, zinatafautisha wasimulizi na wahusika mbalimbali katika
riwaya hii. Pia mbinu ya kuingiza mtindo wa utanzu mwingine katika utanzu wa
riwaya kama vile tunavyoona Kezilahabi anapojenga matini yenye mtiririko wa
kitamthilia (wa mazungumzo na majibu) katika sura 8 (uk. 47-52) yote
inayojadili ufisadi, ngono na ukandamizaji wa kisiasa ulivyotawala duniani. Pia
mwandishi huyu anavyotumia ufupisho wa sura yenyewe kama vile sura ya 10 (uk.
62) ambayo ina aya nne ndogondogo tu. Kwa kweli, riwaya za Kezilahabi ni fupi
mno, kwa kiasi cha Nagona kuwa na kurasa 62 na Mzingile 70. 15 Tafsiri ya
graphicart Mbinu ya mkarara wa kauli na maneno teuzi ni muhimu pia katika
matumizi ya lugha –mbinu inayorejelea utandawazi/utandawizi na kusisitiza baadhi
ya matokeo yake ambayo msomaji anatakiwa ayape uzito katika kuyafikiri. Katika
Nagona maneno ‘ukweli’, ‘mshumaa’, ‘vichaa’, ‘vicheko’, ‘ungamo kuu’, ‘ukimya’,
‘njia’, ‘barabara’, ‘mto’, ‘paa’, ‘ndege’, ‘mti’, ‘msitu’, ‘milima’, ‘mabonde’,
‘duara’, ‘vitabu’, ‘ukosefu wa watu’, ‘paka’, ‘mkombozi’, ‘ajali’, ‘ndoto’,
‘maluweluwe’, ‘uta’ na ‘mshale’ ni maneno yanayorudiwarudiwa kila wakati.
Katika Mzingile ‘mwanga’, ‘karne’, ‘kichaa’, ‘mkombozi’, ‘safari’, ‘ndoto’,
‘mto’, ‘giza’, ‘mzee’ na ‘ukungu’ ni baadhi ya maneno yanayorejewa kila baada
ya muda. Katika Babu Alipofufuka maneno ‘Proteus’, ‘Limonsin’, ‘Doggy’,
‘mzuka’, ‘Neocasino’, ‘kimya’ na ‘kompyuta’ ni maneno yanayotajwa sana. Katika
Bina-Adamu maneno ‘Bina-Adamu’, ‘P.P’, ‘huntha’, ‘Wotan’, ‘mto’, ‘safari’,
‘njia’, ‘Fyura’, ‘Yanguis’, ‘utandawazi’, ‘global village’ na ‘wizi’ ndiyo
yanayojitokeza sana. Lakini mbali na neno moja moja, baadhi ya kauli au picha
zinazojengwa kwa maneno mengi ambazo hurudiwa tena na tena kama tunavyoona
katika Babu Alipofufuka (uk.92, 96) kauli ya La, hatutaki, hata ikiwaje
hatulali tena... na katika Bina-Adamu (uk.140, 148) picha ya kuwa Ulimwengu
umekuwa kijiji kidogo siku hizi, mipaka haipo tena ... inarudiwa tena na tena
ingawa kwa maneno mengine. Kauli ya Hii ndiyo bustani yao ya Eden inarejewa
mara kadha (uk.64, 110). Pia katika kitabu hikihiki tunakuta kauli Sio sisi tu
akina Churchill, ukoo wa Kaiser, ukoo wa Gaulle, kina Franco na muhimu zaidi
P.P. anafanya hivyo! Huu ni ulimwengu wa uwongo... (uk.50, 51). Picha nyingine zinazorudiwarudiwa
katika riwaya hii ni ile ya hofu, ujinga, wizi, ufisadi, unanganyi na
unyang’anywaji. 4.0 Hitimisho Mjadala tuliouendeleza katika makala haya
unarejelea na kuthibitisha tasnifu maarufu katika somo la fasihi; ile tasnifu
inayosisitiza kwamba, kama maisha ya mwanadamu mwenyewe, fasihi nayo lazima
ibadilike hasa wakati wa matukio makuu ya kutisha au kufurahisha kama
utandawazi/utandawizi ambayo yanabadilisha kwa kiasi kikubwa, maisha ya watu wa
jamii fulani. Kwa sababu lugha ni nyenzo ya msingi ya kubunia na kuwasilishia
kazi ya fasihi, basi lugha haina budi kukidhi kimaumbo, kimiundo na kikazi,
mahitaji ya kazi ya fasihi na mahitaji ya jamii yenyewe inayobadilika. Marejeo
Bertoncini, Elena. (2002): When Grandfather Came to Life Again – S. A.
Mohamed’s New Novel Beyond Realism – makala iliyotolewa kwenye Kongamano la
Kiswahili, Bayreuth. Dittemer, Clarissa. (2002/2003): Said Ahmed Mohameds “Babu
Alipofufuka” ein magischrealistischer Roman – Kazi Maalum kwa Somo la Riwaya
Mpya ya Kiswahili, Sehemu ya Fasihi za Kiafrika kwa Lugha za Kiafrika,
Chuokikuu cha Bayreuth. Gromov, M. D. (1998). Nagona and Mzingile – Novel, tale
or Parabole? Katika Jarida la ‘Afrikanische Arbeitspapiere 55: Kiswahili Forum
V’, uk.73-78. ____________. (2004). Post-modernistic Elements in Recent
Kiswahili Novels. Katika ‘The Nairobi Journal of Literature: The Journal of the
Department of Literature, University of Nairobi’, 2, uk.28-36. International
Labour Force and Information Group. 1998. An Alternative View of Globalisation,
ILRIG, Cape Town. Jauch, Herbert (ed.). (2001). Playing the Globalisation Game:
The Implications of Economic Liberalisation for Namibia, Labour Resource and
Research Institute (LaRRI) Windhoek. Kezilahabi, E. (1990). Nagona.
Dar-es-salaam University Press. ___________. (1990). Mzingile. Dar-es-salaam
University Press. Khamis, Said A.M. 1999. Defamiliarisation and Experimentation
in the Kiswahili Novel: A Case Study of Kezilahabi’s Novel: Nagona. Hotuba
isiyochapishwa ya kupokea uprofesa Chuo Kikuu cha Bayreuth (Inaugural lecture).
________________. (2001). Fabulation and Politics of the 90s in Kezilahabi’s
Nagona. Katika Toleo la ‘African Languages Literature in the Political Context
of the 1990s’. Bayreuth African Studies 56 (2001): 119-133. ________________.
(2003). Fragmentation, Orality and Magic Realism in Kezilahabi’s Novel: Nagona.
Katika ‘Nordic Journal of African Studies’ 12(1), uk.78-91. King’ei, Kitula.
(2002). Fantasy and Realism in the Modern Kiswahili Novel: A Critical Look at
Babu Alipofufuka by Said A. Mohamed – an unpublished literary review. Mkangi,
Katama. (1995). Walenisi. East African Educational Publishers: Nairobi. Mkufya,
W.E. (1999). Ziraili na Zirani. Hekima Publishers: Dar-es-salaam. Mohamed, Said
A. (2001). Babu Alipofufuka. Jomo Kenyatta Foundation: Nairobi. ______________.
(2005). Dunia Y ao (kitatolewa na Oxford University Press: Nairobi).
_____________. (2005/2006). Mkamandume (kitatolewa na Longhorn (K) Ltd:
Nairobi). Murray, A. 2000. Public Sector Restructuring in Namibia –
Commercialisation, Privatisation and Outsourcing: Implication for Organised
Labour, LaRRI, Windhoek. Nicol Bran (ed.) (2002). Postmodernism and the
Contemporary Novel: A Reader, Edinburgh University Press. Offiong, Daniel A.
(2001). Globalisation: Post-Neodependency and Poverty in Africa, Fourth
Dimension Publishing Co.: Enugu Nigeria. Rettová Alena. 2004. Afrophone
Philosophies: Possibilities and Practice – The Reflexion of Philosophical
Influences in Euphrase Kezilahabi’s Nagona and Mzingile. Katika Jarida la
‘Kiswahili Forum’ 11, uk. 45-68.
Robert, Shaaban. (1951). Kusadikika. Nelson:
London.
_____________. (1967). Kufikirika. East African Literature Bureau:
Nairobi. Ruigrok W & R van Tulder. 1995. The Logic of International
Restructuring, Routledge: London/New York. Topan,
Farouk, (2002). Babu
Alipofufuka by Said A. Mohamed – an unpublished literary review. Wamitila, K.W.
(1991). Nagona and Mzingile: Kezilahabi’s Metaphysics. Katika Jarida la
Kiswahili 54 la (TUKI), Chuokikuu cha Dar-es-salaam, uk. 62-67.
____________.
(1997). Contemptus Mundi and Carpe Diem Motifs in Kezilahabi’s Works. Katika
Jarida la Kiswahili 60 la (TUKI), Chuokikuu cha Dar-es-salaam, uk. 15-24.
____________. (2002). Bina-Adamu. Phoenix Publishers, Nairobi.