MCHANGO WA BONGO FLAVA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

5.1Muhtasari wa tasnifu.
Utafiti huu uliadhimia kuchunguza  nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya.Nilifanikiwa kuhojiana na wasanii,wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma  pamoja na wakazi wa manisipaa ya Dodoma  mjini.Kwenye utafiti huu niliongozwa na malengo matatu ambayo ni Hadhi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ,sababu zinazo pelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana zaidi pamoja na kuonyesha mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
Tasinifu hii imekamilishwa na sura tano,Sura ya kwanza inaelezea tatizo la utafiti likiwa ni Kuangalia nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya                         Imejumuisha usuli wa tatizo ,tamko la tatizo la utafiti,manufaa ya utafiti,nadhari ya utafiti na malengo ya utafiti,manufaa ya utafiti  na maswali ya utafiti.katika sura ya pili imefafanua maandiko mbalimbali yanayozungumzia muziki wa kizazi kipya .Mapengo yaliyotumika katika mada  yamebainishwa na maandiko hayo.
Sura ya tatu imebainisha mbinu na vifaa vilivyotumika katika mchakato mzima wa utafiti wangu,vitu hivyo ni mpango wa utafiti,walengwa wa utafiti,jamii ya watafitiwa,eneo la utafiti,uchambuzi na uunganishaji wa data,zana na njia za kukusanya data pamoja na vikwazo mbalimbali nilivyokumbana navyo wakati wa mchakato wa ukusanyaji na uchambuzi wa data.
Sura ya nne imetoa matokeo ya utafiti uliofanyika .Mjadala  huu  umegawanyika katika sehemu tatu kulingana na maswali yaliyoongoza utafiti huu. Sehemu ya kwanza  hadhi  ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya inajadili.Katika sehemu ya pili nimeelezea sababu zinazopelekea vijana wengi kupenda kusikiliza muziki wa kizazi kipya zaidi.Sehemu ya tatu nimejadili mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni wa lugha ya kiswahili.Mwisho nimetoa muhtasari kwa kuelezea yote yaliyojadiliwa katika sura hii.
 Katika sura ya tano nimehitimisha kwa kutoa muhtasari wa utafiti kwa ujumla yakiwemo matokeo ya utafiti huu. Pia nimetoa mapendekezo kwa tafiti zijazo kuhusu mambo yanayofaa kuzingatiwa katika muziki wa kizazi kipya wanapotumia lugha ya kiswahili.

5.2 Mchango Mpya wa Utafiti Huu.
Ni matumaini yangu kuwa  kutokana  na utafiti uliyo fanyika utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa kwa jamii na kwa wizara ya  sanaa utamaduni na michezo pia kwa baraza la sanaa na wasanii wenyewe ambao ni chipukizi na waliofanikiwa katika muziki huu wa kizazi kipya Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.Pia utaleta changamoto katika kuibua tafiti zingine.Kitokana na utafiti huu pia nimefanikiwa kuibua mambo ambayo ni chachu ya maendeleo ya muziki wa kizazi kipya kwa wapenzi wa muziki huu na hata wale wasio penda kusikikliza:
Katika utafiti huu nimefanikiwa kufafanua  kwa kina baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa vinawatatiza wapenzi wa muziki wa kizazi kipya jinsi lugha ya kiswahili inavyotumika katika muziki wakizazi kipya .Nimafafanua kwa kina mambo yafuatayo:
Nimejadili hadhi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya kwa kuonyesha kuwa wasanii pamoja na taasisi za kiswahili zina changamoto kubwa  katika kuikuza lugha hii ya kiswahili  hivyo basi  wana muziki wanapaswa kuitumia lugha hii vizuri na kuipa hadhi au heshima yake katika kuitumia hili linaambatana na taasisi za lugha ya kiswahili kuweza kufanikisha soko la  muziki huu ambalo ndilo lengo la wasanii kuweza kupata soko la kazi zao kwasababu wasanii wengi wanapenda kuimba kwa kuchanganya lugha,lugha za matusi wanazo tumia na kuifanya lugha ya kiswahili kuwa na hadhi ya chini na hivyo kinyume na utamduni wetu kwamba lugha inaonekana ina  matusi, pia mchango wa utafiti huu ni kuitaka serikali kwa kushilikiana na taasisi za kiswahili kutilia mkazo utumizi wa lugha iliyo sanifu katika nyimbo zao ili kuikuza vema lugha hii ya kiswahili.
Katika kufafanua sababu za vijana kupenda kusikiliza muziki wakizazi kipya kuliko kundi lingine katika jamii inayotuzunguka,nimeweza kufafanua sababu hizo ambapo wasanii wanaweza kujirekebisha  ili sanaa yao iwe ya watu wote nasi vijana endapo wata badilisha lugha wanazo zitumia na kutumia lugha inayoeleweka na jamii nzima,kuacha kutumia lugha ya matusi pia lugha ya kisheng ambayo wasanii wa Tanzania wanaaza kuitumia ktika nyimbo zao na kupelekea muziki huu kuwa amali  vijana peke yao.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiitumia lugha ya kiswahili vema kutokana  na utafiti nilioufanya itasaidia kuondoa utabaka uliopo baina ya wasikilizaji wa  muziki huu wa kizazi kipya kwasababu utatoa fursa kwa rika zote kuupata ujumbe uliokusudiwa na wasanii hawa wa muziki huu.
Vilevile kitendo cha wasanii kuchanganya lugha,kutumia misamiati wanayoiibuwa wenyewe inasaidia katika kuongeza maneno au misamiati katika lugha ya kiswahili kutokana na  wasanii hawa kutohoa maneno toka katika lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya kiingereza  na lugha za asili.
Mwisho utafiti huu utoa ufafanuzi kwa wasanii kutumia lugha inayoeleweka ilikulinda utamaduni wa lugha yetu ya kiswahili na jamii kwa ujumla kutokana na hili utafiti huu unawataka wasanii kuilenga jamii nzima ili ujumbe ufike kama ulivyo kusudiwa kufika na si kwa kundi moja ambalo ni vijana kwamba kuna wazee pia wanao penda kusikiliza muziki huu wa kizazi kipya lakini wanapopata fursa ya kusikiliza wanapata tabu kuelewa misamiati inayotumiwa na wasanii hao.Utafiti huu unatoa mchango kwa kuwakumbusha wasanii wa muziki huu kuwa sanaa yao ni mali kwa jamii nzima .
Wale wasanii wanao chipukia sanaa hii ili waweze kufanya vema zaidi ya waliotangulia na wanapo pata mwanya wa kuenda kufanya  shoo zao nj’e ili waweze kuutangaza utamaduni wa lugha hii vizuri na kuendelea kuitangaza lugha hii ya kiswahili ndani na n’je ya nchi yetu.Pia wasanii wanapaswa kutambua kuwa muziki wao unatazamwa na kusikilizwa na  jamiii kwa ujumla hivyo basi kulinda utamaduni wa lugha yetu ni muhimu zaidi kwasababu  wanamuziki wengi huiga wasanii wa n’je kimiondoko,mavazi na hata mambo wanayo imba katika nyimbo zao pia yanasadifu hadhi ya nj’e na vijana wengi mambo yao mengi wanayo ya fanya huwa  wameyasikia katika nyimbo hizi za muziki wa kizazi kipya hivyo basi wasanii hawana budi kufuata sheria na taaratibu za utamaduni wetu.
Hivyo ufafanuzi huu wa kina utakuwa chachu kwa jamii ambayo ni wapenzi wa muziki wa kizazi kipya na wanaoipenda lugha hii ya kiswahili nj’e na ndani ya nchi.  Hii ni pamoja na jamiii iliyo kuwa ikiuchukulia kuwa muziki wa kizazi kipya ni wakihuni ili waweze kubadilisha mtazamo wao wa mawazo na kuweza kuusikiliza muziki huu wa kizazi kipya hasa wazee ambao huona muziki huu ni wakihuni.
5.3 Maoni Kuhusu Utafiti Huu.
Muziki wa kizazi kipya ni aina ya muziki ambao umekuwa ukibadilika siku hadi siku sio kama hapo mwanzo ambapo muziki huu ulikuwa chombo cha vijana kuelezea matatizo yao,.kwa sasa  jamii inaona muziki huu ni wakihuni kutokana na muziki huu unavyo wasilishwa kwa jamii na kuonekana ni wa vijana zaidi.Utafiti huu utauwa fikra na mitazamo ya wazee wengi ambao hawapendi kuusikiliza muziki huu wa kizazi kipya kwa kuwa wanauona ni muziki wa kihuni na una walenga vijana zaidi.
Maoni yangu kutokana na utafti nilioufanya kuhusu nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ninaona vema taasisi za lugha ya kiswahili zikishilikiana na baraza la sanaa na lugha kuweza kukaa na wasanii na kuongea nao kuhusiana na sanaa pamoja na lugha wanazo zitumia katika utungaji wa nyimbo zao  ikiwa ni pamoja na kuangalia swala la utumizi mzuri wa lugha ya kiswahili katika nyimbo zao.
Pia maoni yangu mengine ni kwa jamii inayo sikiliza muziki wa kizazi kipya hasa wazazi wanao waachia vijana wao ambao wana umri mdogo kusikiliza nyimbo hizi ambazo zingine zinachochea mapenzi na kuwaafanya vijana kuanza mapenzi wakiwa katika umri mdogo pia kuvaa mavazi ya ajabu kutokana na kuwaangalia picha za wasanii ambao huuvaa mavazi ya ajabu katika shoo zao.vilevile kwa wasanii ambao wana vaa nguo za ajabu mtaani ambazo ni kwa ajili  ya kufanyia shoo na wakati mavazi mengine yanakuwa hayasadifu utamaduni wetu na hivyo wasanii hawa kujidharirisha na kuwafanya vijana wengine kuiga mavazi yao.Pia wasanii wanapaswa kutumia lugha inayoeleweka na jamii yote na hii itawasaidia katika soko la kazi zao ikienda sambamba na ujumbe wanao utoa kwa jamii kwamba wasiegemee kwenye mapenzi zaidi kwasababu wasanii wengi nyimbo zao zimejaa dhamira ya mapenzi sana na hii ndiyo inayopelekea vijana wengi kujiangiza katika swala la ngono wakiwa katika umri mdogo.Endapo watazingatia hayo muziki wa kizazi kipya utakuwa ni mali ya jamii nzima na itakuza na kueneza lugha ya kiswahili vema nj’e na dani ya nchi.
5.4 Mapendekezo Kuhusu Tafiti Zijazo.
Napenda kupendekeza mambo yafuatayo kwa tafiti zijazo ambayo yatachangia maendeleo ya lugha ya kiswahili na muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.
Kwa watafiti watakao jikita katika swala hili la lugha ya kiswahili pamoja muziki wa kizazi kipya ni vema wakaangalia  chanzo cha misamiati inayotumiwa na wasanii hawa katika muziki wa kizazi kipya kwasababu misamiati mingine inatoholewa katika lugha za asili na misamiati mingine ni maneno ya vijana ambayo yanafaahamika miongoni mwao tu na kupeleke muziki huu kuwa ni mali ya vijana peke yao.Hivyo itakuwa vema endapo watafiti wa kazi zijazo kutazama vema chanzo cha misamiati wanayoitumia katika nyimbo zao.
Pia natoa pendekezo kwa vyombo vinavyojihushisha na lugha ya kiswahili pamoja na sanaa kwa ujumla kutoa kipaombele kwa kazi za wasanii hawa kwasababu sanaa kwa upande mkubwa inatangaza taifa kuliko nyanja nyingine yeyote kwa njia ya shoo wanazo kwenda katika mataifa mengine.Hivyo basi watafiti watakao fanya utafiti wa kazi hii itawapasa kushirikiana na taasisi za lugha pamoja na wasanii kwa kushirikiana na serikali.
Pia naendelea kusisitiza kuwa msanii anapaswa kujitambua kuwa yeye ni kioo cha jamii na ni mtu muhimu sana kwa jamii.Hivyo basi wasanii hawana budi kuheshimu kazi zao,kujiheshimu wao wenyewe hii ina ambatana na mavazi ya wasanii wanyewe kuva katika shoo zao ,lugha inayotumiwa na wasanii katika nyimbo zao,mienendo ya wasanii katika maisha yao ya kila siku na mwisho kabisa msanii anapaswa kuzingatia ujumbe na kuwa mfano kwa jamii na vjina.
MAREJEO.                                                           
 Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981),TUKI,Dar-es-salam.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu  Toleo la pili(2005),TUKI,Dar-es-salam.
Mbaabu I. N. K( 2003).English-Kiswahili Dictionary of Sheng: Deciphering East Africa’sUnder-World Language. TUKI,Dar es Salaam:

Mkangi, K.( 1984).Sheng and the Kenyan Culture. The Standard, Nairobi, August 30
(17–18).
Mukhebi, L. (1986)..Is Language and Culture Inseparable? Kenya Times, Nairobi, May 28

Masamba D.P.B(2006),Jarida la Taasisi ya Uchunguzi  wa Kiswahili,Dar-es-salam.
Taji. L(2008),Chimbuko la Muziki wa kizazi kipya,Bongo celebrity,Dar-es-salam.
Wamitila K.W(2003),Kichocheo cha Fasihi simulizi na andishi,English press;Dar-es-salam.
Chachage ,C.S.L.(2002),Ndani ya Bongo utandawazi na migogoro ya utamaduni”Makala yaliwasilishwa katika mkutano wa kumi wa hali ya siasa Tanzania.Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Senkoro.F.E.M.K.(2003)Rethinking popular Arts and culture in the 21st century East Africa”Makala yaliyowasilishwa katika maadhimisho ya 30 ya codesria.
Majembe.A.K.(1998) “language use in Tanzania Hip Hop scene”,Un- published research paper, University of Dar es salaam.
Fenn,J na Perullo,A.(2000),language  choice and Hip Hop inTanzania katika popular music and society.University of Bowling Green City.
Fema,(2006),Bongo flava utambulisho au umaarufu,vol.16
www.google.com. Halhamisi,28/4,2010.
www.freemedia.co.tz/habar php? Halhamisi28/4/2010.
Powered by Blogger.