MCHANGO WA BONGO FLAVA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI


Matumizi ya Jazanda na Tasifida
Msimbo wa Sheng huunda baadhi ya maneno yake kwa kuzingatia mbinu ya
jazanda na tasifida. Kwa mfano:
boli                                                                                          mjammzito
mahewa                                                                                   muziki
kuro                                                                                         kahaba
pupuu                                                                                      kwenda haja kubwa
susuu                                                                                       kwenda haja
Hivyo kutokana na hii hali ya wasanii kutumia lugha hii katika muziki wa kizazi kipya unaonyesha kuwa vijana wengi wanatumia lugha hii katika utungaji wa mashairi yao ambayo ni lugha inayotumika na vijana wengi Kenya na hapa Tanzania miongoni mwa vijana  wengi.Utafiti unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya  una soko kubwa sana na ni ajira kwa vijana wengi wa Afrika mashariki na hii inaonyesha kuwa baadaye lugha hii itazagaa kwa vijana wengi kwasababu kazi za wasanii wa Kenya pia zina sikilizwa na vijana wengi na wengi wao wanapenda ladha ya nyimbo za wasanii wa Kenya kutoka na misamiati wanayo itumia katika nyimbo zao,mfano katika nyimbo hizi mbili za wasanii wa Kenya,masanii Marya aliyemshilikisha mwanadada  mwenzie Avrill katika wimbo wa Tumekuja chokoza.
           
“Ai wewe mbona machali wanabehave hivi? tumeenda club lakini kunawanaume
Jamaa ajui kama napenda machali au mademu mimi nikiingia club nataka mabeste
Tujuane kwanza ,mimi na beste yangu tumekuja club kazi yetu sisi kuchokoza chali
Unipati after hii party ,tumekuja chokoza haaahaaa,usidhani kama utapata nafasi
Hahaaaaaa”
Wimbo mwingine ni wa msanii Bugz katika wimbo wake wa kamoja tu.
            Nina ubaya na mademu eeh,ah wamechili endelea kuchili ahopu
            Na hizo nywele  utatoa ukienda home kudai anang’owa ati
            Mambo ati mambo ni baada ya ndoa mimi mdogo sana siwezi oa
            Kausha weka mkono kwa koponi siunajua kutoa ni ngoi nikikuumiza basi sori
            Shiiiiii acha mastori mbona ucheki  mimi sisleki inaiva ila lakini haichomeki
            Njaasho kutoka kwa lips,chicks kwa hips”
Misamiati iliyotumika katika nyimbo hizi mbili zinaonyesha namna lugha hii ya vijana inavyotumika katika nyimbo zao na kuzidi kushika kasi katika matumizi ya lugha ya vijana nakupelekea wazee kushindwa kuelewa ujumbe unaotolewa na vijana na hivyo muziki huu kubaki kuwa mali ya vijana peke yao mfano msamiati mademu likiwa na maana ya wasichana,machali likimaanisha vijana,beste likiwa na maana ya rafiki,beshi pia likiwa na maana ya rafiki.
Hali inatokana na kitendo cha uigaji wa utamaduni miongoni mwa vijana wengi ambapo suala la kuiga utamaduni wa jamii nyingine ni pamoja na uwigo wa lugha,mavazi kwani hata mavazi ya vijana wengi kwa asilimia huwaiga wasanii jinsi wanavyo vaa mfano mashati yanayoitwa bushoke jina hilo lili tokana na sababu ya msanii huyo kuvaa shati hilo katika mojawapo ya video ya wimbo wake mmoja hivyo basi kuanzia hapo wakaanza kuyaita mashati hayo Bushoke,nj’e ya vijana kuiga mavazi pia hata matendo yanayoimbwa katika nyimbo hizo vijana hutilia mkazo kwa kuyatenda yale yanayoimbwa na wasanii hao.Mtafiti alimhoji kijana mmoja kwa jina alijitambulisha kwa jina la Derick yeye alisema:
            “muziki wa kizazi kipya ni muziki ambao umeshika vijana wengi katika
            Kuusikiliza na hata ukienda club(kumbi za starehe/sehemu ya muziki)kwa
            Asilimia  kubwa utakutana na vijana wengi.misamiati wanayo itumia naielewa
             Vema kwa upande  wangu”
Kutokana na nyimbo hizi kugusa maisha ya vijana ndiyo sababu kubwa inayopelekea vijana wengi kuupenda muziki wa kizazi kipya .Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa muziki huu unaoimbwa na vijana wengi unagusa maisha yao waliyonayo mtaani.Nyimbo za muziki wa kizazi kipya zinagusa maisha ya vijana katika swala la maendeleo ya kijamii,siasa na uchumi.
Maendeleo ya kiuchumi,muziki wa kizazi kipya unawagusa vijana wengi katika upande wa uchumi,utafiti uliofanyika umegundua kuwa vijana wengi hawana ajira na ajira kubwa wanayo itegemea ni hiyo ajira binasfi ambayo kwa upande mkumbwa ndiyo vijana wengi wanaipenda ,kwa asilimia kubwa utafiti unaonyesha kuwa vijana wengi hata waliopo mashuleni wanajishughulisha na utungaji wa mashairi ya muziki huu wa kizazi kipya na kuimba katika matamasha mbalimbali na mashuleni wakijulikana kama wasanii wachanga(Underground)kwa wale ambao bado hawajavuma/hawajajulikana  katika soko la muziki huu wa kizazi kipya.
Nyimbo za muziki wa kizazi kipya zingine zinawataka vijana kupamba na maisha na si kuwa nyuma katika kupambana na maendeleo katika maisha yao mfano katika wimbo wa  fungeni mikanda ulioimbwa na wasanii wa Tanzania Chege na Temba wanasema:
            “Vujana fungeni mikanda,fungeni mikanda tukokilimani twapanda
fungeni mikanda”
katika wimbo huu wasanii hawa wanawataka vijana kuwa wastahimilifu na kujikaza ilikupambana na maisha yanayo wakabiri katika misuko suko iliyopo,kwa upande mwingine wasanii wanawahasa vijana na jamii kumshilikisha mungu katika swala la kutafuta maisha  kuwa ni muhimu kumshilikisha mungu ilikuweza kupambana na maisha yanayo wakabiri vijana wengi.
Kwa upande wa siasa ,vijana wengi sasa hivi wamejingiza na siasa,pia utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa vijana wengi wa sasa huwa wanapenda kuimba nyimbo za siasa ilikuweza kupata soko kipindi cha uchaguzi kwasababu wanasiasa wengi kipindi cha uchaguzi huwa wanachukua vijana kwa ajili ya kuwaimbia wanapo kuwa wanajinadi kwa wananchi ilikuweza kuchaguliwa na kwa asilimia kubwa vijana wengi hujitokeza katika viwanja vya mikutano na kushawishika kumsikiliza mgombeaji  na baadaye kuweza kuwa na moyo wa kupiga kula mfano mzuri ni pale Rais wetu wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete alipomtumia msanii Marow katika kutumbuiza kwenye kampeni yake na kupelekea vijana pamoja wananchi kwa ujumla kujitokeza kumpa heshima ya kumsikiliza na baadaye kumchagua,pia Mgombe mwingine aliyekuwa anagombea kwa Uraisi kwa tiketi ya Chadema dakt.Wilbroad Silaa aliwatumia wasanii kama Danny msimamo,Mkoloni,G, Mapacha wa tatu.
Katika maendeleo ya jamii,muziki wa kizazi kipya unawagusa vijana,utafiti unaonyesha kwa sasa jamii imeanza kuona muziki huu sio wa kihuni kama hapo mwanzo ulivyokuwa unachukuliwa ,wazazi wa vijana wengi wanaona kuwa endapo  kijana ana uwezo wa kuimba basi haruhusiwe kuimba kwasababu ni mojawapo ya ajira ambayo kijana anaweza kujikwamua na kuondokana na makundi mabaya ya mtaani hivyo basi wazazi wengi sasa hivi hawa uchukuliii mziki huu kuwa ni wakihuni kama zamani,mzazi mmoja ambaye nilimuhoji kuhusiana na hilikuwa muziki wa kizazi kipya unagusaje? maisha ya kijana alijibu kama ifuatavyo:
            “Mimi kwa upande wangu kama mwanangu anaweza kuimba  sitoweza kumkataza
Zaidi nitajitahidi kumsaidia kimawazo na kumskiliza anchohitaji maana sasa hivi ukiangalia vijana wengi waliofanikiwa kutokana na vipaji vyao ni wengi na wana maisha
Mazuri wao na familia zao ,kwahiyo mimi nitafurahi sana kama mwanangu akiwa na kipaji cha kuimba,mimi naona sio uhuni kwakweli”
Maelezo ya mama huyu ambaye ni mfanyabiashara akijulikana kama mama vipodozi,yanadhihirisha kuwa muziki wa kizazi kipya unawagusa vijana kwa kiwango kikubwa zaidi na walio wengi wamefanikiwa wakiwa na umri mdogo mfano msanii Alikiba,Marow,Dogo Janja na wengieneo.Sababu hizi zilizopatikana katika utafiti ndizo zionyeshazo kwanii vijana wanapenda muziki wa kizazi kipya zaidi kuliko nyimbo zingine.
4.4Mchango wa muziki wa kizazi kipya katika  utamaduni wa  lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.Data za utafiti huu zinaonyesha kuwa kuna mchango chanya na hasi wa muziki wa kizazi kipya  katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
Mchango chanya wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni  wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla,utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya unasaidia kutangaza utamaduni wetu kwa kupitia shoo wanazo zifanya nj’e ya nchi,wasanii hawa wanapo kwenda kufanya shoo n’je huko wanakutana na watanzania wenzao  na watu wa jamii ya nchi hiyo ambayo wanafanya shoo.Hivyo basi kupitia muziki wa kizazi kipya lugha ya Kiswahili inatangazwa na kupelekea kukua na kufahamika,Kutokana na utafiti uliofanyika kwa njia ya kuwahoji baadhi ya vijana katika mtandao wa kwa njia ya facebook walijibu hili swali baada ya kuwaulizwa swali kuwa muziki wa kizazi kipya unamchango gani katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla kama ifuatavyo:Msichana Subilaga Chalres alisema:
“Kwanza unaongeza maneno au misamiati,2 unafanya lugha ya kiswahili
itambulike kwa urahisi hata katika nchi nyingine thus pia mi naona kwamba mziki
 wa kisasa una batilisha utamaduni huo maana hata lugha wanaiichanganya, Pili
una saidia kwa kuendeleza lugha ya kiswahili kwa misamiati mipya na kutangaza utamaduni huo kwa nchi kadha maana mziki huo unasikizwa hadi uropa.pia pale wanapoenda kushiliki mashindano ya nje wanakuza lugha yetu inaweza kuwa
 point moja.

Pia kijana mwingine anayeitwa Daniel simon alisema kuwa:
“ muziki unamchango katika kueneza maneno na misemo mipya ya kiswahili.
..mfano neno sharobaro!cjui ndo mnaiita misimu me naona una faida hapo
 kwa sababu wasanii wa kizazi kipya wana tumia misamiati ambayo inatubidi
kutafuta maana yake”
kijana mwingine anayeitwa Asulikwe Mjaba yeye anasema kuwa:
“me naic unakuza utamadun we2,zen unaelmisha,unaburudsha”
Hivyo basi kutokana na utafiti huu muziki wa kizazi kipya unamchango mkubwa katika lugha ya Kiswahili kutokana na misamiati wanayo itumia  pia  kutokana  na misimu inayotumika kwa vijana sana na hata baadhi ya wazee mfano neno sharobaro kwa sasa ni neno lililosambaa sana miongoni mwa watumiaji wa lugha ya Kiswahili,maana ya neno sharobaro linavyoeleweka na vijana wengi ni mtu msafi  na anaye jipenda.
Muziki wa kizazi kipya unachangia kukua kwa lugha ya Kiswahili na kuifanya lugha hii itambulike,kupitia muziki wa kizazi kipya na kujiongezea msamiati kwasababu kwa asilimia kubwa misamiati inayotumiwa na wasanii hawa katika nyimbo zao inatumiwa na jamii na maneno hayo yanapokuwa yamezoeleka katika jamii yanasanifishwa kisha kutumiwa  kama misamiati iliyosanifu.viilevile muziki wa kizazi kipya unadumisha mahusiano au kujenga ushirikiano kwa vijana  muziki huu unawakutanisha vijana pamoja pia kwa kutumia lugha ya Kiswahili katika kuwasiliana kunasaidia kukuza utamaduni wa lugha ya Kiswahili.Utafiti unaonyesha kuwa wasanii wanao kuja kufanya shoo wakati mwingine huondoka na maneno ya Kiswahili na kuyaingiza katika nyimbo zao mfano  msanii  micheal Jackson ambaye ni marehemu alishawahi kuingiza maneno ya Kiswahili  katika wimbo wake ambazo:
                         “nakupenda pia nakutaka pia mpenzi wee”

Mtafiti alipata maelezo haya kutoka kwa kijana  Hassan Juma ambaye alisema:
                     muziki wa kizazi kipya unadumisha mahusiano kwa vijana kwa
                      Kupitia matamasha yanayofanywa na vijana katika shoo zao
                     Kupitia hapo tunakutana vijana tofauti tofauti na kufamiana zaidi”
Mchango hasi wa muziki wa kizazi kipya katika lugha ya Kiswahili kutokana na utafiti ulio fanyika niliweza kupata majibu ya fuatayo baada ya kuwahoji vijana kwa njia ya  mtandao wa facebook, na haya ni baadhi ya majibu waliyotoa :
       “ hauna mchango wowote kwa upande wangu, 7bu zimejaa swangilish kuliko
        kiswahili fasahaawell me nadhani una mchango kiburudani na sio kimaadili
      wala katika fasihi ya kiswahili,maana lugha wanazotumia saizingine hazina maadili
       yoyote katika jamii”hauna mchango wowote kwa upande wangu, sababu zimejaa   
      swangilish  kuliko kiswahili fasaha”
kutokana na utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa vijana wengi wanabadilika au kuwa kinyume na utamaduni wetu kimavazi,lugha wanayotumia,chakula na maadili kwa ujumla, kwamba wasanii wengi maudhui ya nyimbo zao kwa sasa umeegamia katika mapenzi zaidi hivyo kutokana na hili vijana wengi hujihusisha na mapenzi wakiwanaumri mdogo kutoka na nyimbo wanzo zisikiliza na kuona picha za nyimbo hizo ambazo nyingi ni za mapenzi na kwa upande wa  mavazi kwamba wasanii wengi wa kike mavazi yao hayasadifu kabisa utamaduni wetu kwani wengi wao huvaa nguo za ovyo ambazo zina valiwa na wasanii wa nj’e na kupelekea wao kuiga mavazi yao.
Utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa vijana wengi huona ufahari kuvaa mavazi ambayo wasanii wana ya vaa bila na kusahau  kuwa huo si utamdauni wetu kwani mavazi wanayo vaa wasanii wengi  nj’e na utamduni wetu hafadhari wanaume wanapokuwa jukwaani wanavaa nguo za heshima ingawa wengine kuvaa ovyo mfano kuregeza suruali wanapokuwa wanafanya shoo zao.

Pia utafiti uliofanyika unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya unarudisha nyuma lugha ya Kiswahili kutokana na matumizi mabovu ya lugha inayotumika katika nyimbo hizo na kuu fanya lugha ya Kiswahili kuonekana ni ya wahuni kutokana na matumizi mabovu ya misamiati inayo tumiwa na wasanii hawa katika nyimbo zao kama kuchanganya lugha  na utumiaji wa  lugha ya matusi.mfano katika wimbo ufuatao:
SURA YA TANO
5.0HITIMISHO NA MAPENDEKEZO.
Sura hii ndiyo ya mwisho katika utafiti huu ,kipengele hiki kinaelezea hitimisho la utafiti huu na mapendekezo kwa tafiti zijazo sura hii inabainisha mhutasari wa tasinifu hii .Sehemu ya pili sehemu ya inazungumzia mambo yaliuibuliwa na utafiti wangu na sehemu ya tatu  inapendekeza maoni kuhusiana na mambo mbalimbali niliyoyabaini kutokana na utafti wangu na sehemu ya mwisho inatoa mapendekezo kwa ajili ya tafiti zijazo kutokana na maeneo mbalimbali yaliyoguswa na utafiti huu.
>>>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>
Powered by Blogger.