MCHANGO WA BONGO FLAVA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI



IKISIRI.

Tasnifu Hii Inayoitwa “NAFASI YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI”Ina Malengo Mahususi Manne,Ambayo Ni Kubainisha Hadhi Ya Kiswahili Katika Nyimbo Za Muziki Wa Kizazi Kipya,Kubainisha Sababiu Zinazo Pelekea Muziki Huu Kusikilizwa Na Vijana,Kuelezea Mchango Wa Muziki Wa Kizazi Kipya Katika Utamaduni Wa Lugha Ya Kiswahili Na Jamii Kwa Jumla.Taarifa Zilikusanywa Kwa Njia Ya Mahojiano,Majadiliano Katika Vikundi,Mapitio Ya Maandiko Na Sampuli Niliigawa Katika Makundi Yafuatayo:Wasomi Wanao Sikiliza Muziki Wa Kizazi Kipya Na Wanafunzi Wanaosoma Isimu Ya Kiswahili.Sampuli Ilipatikana Kwa Nbinu Ya Sampuli Lengwa.Uchambuzi Ulifanyika Kwa Mbinu Ya Ufafanuzi(Uhalisia)

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya ni muziki ambao unabadilika kadri miaka inavyozidi kwenda na hivyo kutokana na hili inaonyesha kuwa endapo jitihada za taasisi ya utamduni na lugha isipo angalia swala la utumizi wa lugha katika muziki wa kizazi kipya hapo baadaye muziki huu utapelekea vijana kuwa na lugha yao na hivyo kusababisha utabaka katika jamii kwasababu utafiti unaonyesha kuwa muziki wa kizazi kipya ni muziki wa vijana na lugha inayotumka wanailewa wenyewe kwa asilimia kubwa hivyo basi  kutokana na mwingiliano wa wasanii katika shoo,nyimbo zinazosikilizwa na jamii kuna uwezekano wa kuibuka kwa lugha ya kisheng inayotumiwa na vijana wengi  nchini Kenya na sasa inasikika katika muziki huu wa kizazi kipya na kuididimiza  lugha ya Kiswahili.Kwasababu lugha  ya kisheng  ni mchanganyiko wa lugha ya  Kiswahili ,kingereza na lugha za kibantu na utafiti unaonyesha kuwa wasanii wa muziki huu wana mtindo wa kuchanganya lugha tofauti katika mashairi yao.



YALIYOMO.
HAKIMILIKI
SHUKRANI
IKISIRI
YALIYOMO
SURA YA KWANZA…………… ………..…………………1-11
1.1Ufafanuzi wa dhana  maalumu zilizotumika katika Tasnifu hii
1.2Usuli wa Tatizo. 
1.3 Tamko la Tatizo la utafiti.
1.4 Malengo ya utafiti.
1.5 Malengo la jumla.
1.6 Malengo mahususi.
1.7.Maswali ya utafiti.
1.8 Manufaa ya utafiti.
SURA YA PILI. ………………………………………………12-13
2.0.Mapitio ya maandiko.
2.1 Maandiko yanayohusu  muziki wa kizazi kipya kwa ujumla.
2.2 Pengo linalo paswa kuzibwa.
SURA YA TATU………………………………………………14-16
3.0 Mbinu ya utafiti.
3.1 Mpango wa utafiti.
3.2 Eneo la  utafiti.
3.3 Mbinu za kupata Data.
3.4 Mbinu za kukusanya data
3.4.1Mahojiano.
3.4.2 Majadiliano katika vikundi.
3.4.3 Mapitio ya maandiko.
3.4.4 Vifaa vya utafiti.
3.4.5 Mbinu za uchanganuzi data.
3.4.6 Mawanda ya Utafiti.
3.4.7 Mpango wa Tasnifu.

SURA YA NNE………………………………………….17-36
4.0 Mjadala wa utafiti.
4.1Utangulizi.
4.2Hadhi ya muziki wa kizazi kipya katika lugha ya Kiswahili.
4.3Sababu zinazopelekea muziki wa kizazi kipya kusikilizwa na vijana.
4.4Mchango wa muziki wa kizazi kipya katika utamaduni  wa lugha ya Kiswahili na jamii kwa ujumla.
SURA YA TANO…………………………………………37-41
5.0 Hitimisho la utafiti.
5.1 Muhtasari wa utafiti huu.
5.2Mchango mpya wa utafiti huu
5.3 Maoni ya ujumla kuhusu utafiti.
5.4 Mapendekezo kuhusu tafiti zijazo.

MAREJELEO……………………………………………….42-46
Nyongeza mbalimbali.
A,Picha za wasanii wa  muziki wa kizazi kipya wakiwa katika matamasha pamoja na picha za vijana wakifuatilia tamasha.
B.Maswali ya dodoso
SURA YA KWANZA.
1.1 Ufafanuzi wa istilahi maalumu zilizotumika  katika Tasnifu hii:
1.1.1 LUGHA.
kwa mujibu wa Kiswahili sanifu TUKI(2005,Lugha (1)ni mpangilio wa sauti  na maneno unaoleta maana  ambayo hutumiwa na watu wa taifa au kundi Fulani kwa ajili ya kuwasiliana.(2) ni maneno na mtumizi yake(3) ni mtindo anao utumia mtu kujieleza.

Kwa mujibu J.Habwe na P.Karanja,misingi ya sarufi ya Kiswahili(2004),lugha ni mfumo wa sauti zinazotumiwa na watu wajamii wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana.

 Hivyo basi lugha ni mfumo wa sauti nasibu na ishara za kisarufi ambazo kwazo watu wa jamii Fulani ya lugha huwasiliana na kupokezana  utamaduni wao.Hii ina maana kwamba  lugha ni chombo muhimu cha utamaduni ,lugha ni sehemu ya utamaduni na ni chombo kinachosheheni sifa za utamaduni wa jamii husika katika misamiati,miundo na matumizi ya lugha zinazo husika.Lugha utumika  kukuza utamaduni kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

1.1.2 MUZIKI.
Kwa mujibu kamusi ya English-Kiswahili toleo la 3(2005),muziki ni sanaa iliyokusudiwa na kuweza kukubaliwa na jamii, msanii hana budi kubuni mitindo ya lugha mbalimbali katika utungaji wake.
 Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu  Toleo la 3(2006),Muziki ni kitendo cha kutunga  na kutia sauti.
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu  toleo la pili (2004),Muziki ni mpangilio wa sauti za ala,uumbaji au vyote viwili.
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981), Muziki ni mpangilio  wa  sauti za ala na uimbaji unaoleta athari  fulani  kwa kiumbe.


1.2 Suala la muziki wa kizazi kipya.
Sehemu hii ina lengo la kuchunguza suala hili kihistoria,kwa kufanya hivyo tunaweza kupata  au kujua nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya  katika kukuza lugha ya Kiswahili ,katika kushughulikia suala hili ,nilichunguza hali halisi ya kuwepo kwa muziki wa kizazi kipya nchini baada ya vijana kuanza kuimba nyimbo hizi zenye mahadhi  ya kihiphop kutoka Marekani  na kutaka kujua  muziki huu una mchango gani katika lugha yetu  ya Kiswahili  kutoka mwaka 1970 ulipoanza kusikilizwa na jamii.Hii ni kwasababu jamii ndiyo  inayosikiliza ujumbe uliopo katika nyimbo hizo .Ambapo muziki huu hapo mwanzo ulikuwa ukionekana ni wakihuni  na ni wavijana pekee yao na sio wazee ,hii imekwenda sambamba na matumizi ya msamiati wa lugha ya Kiswahili inayotumika katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya .
Hivyo nimeona kuwa uchunguzi wangu uzingatie jamii inayosikiliza muziki huu wa kizazi kipya ,katika sehemu hii nimegawa makundi maalumu ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya ambao naamini kuwa suala la nafasi ya lugha ya kiswahili katika muziki wa kizazi kipya linaweza kudhirirka kwa uwazi zaidi.Pamoja na kudhihirika huko  katika makundi haya nyimbo nyingi za muziki wa kizazi kipya(bongo flava) zilikuwa zikisikilizwa tangu mwaka 1970 hadi sasa.
1.3Historia fupi ya muziki wa kizazi kipya
  ulianzishwa na Wamerekani weusi huko the Bronx, New York Marekani mnamo mwaka 1970.Wamerekani wenye asili ya Afrika ,ambao babu zao walichukuliwa kwenda Marekani kama watumwa.Elementi hizi za utamaduni wa hiphop zilikuwa zikijitokeza kwa awamu moja  na inapofifia inaibuka nyingine ,ilivyo ni kwamba ilianza grafiti ikafuatwa na udijei,mabreka,halafu rap(yasin,2001;rose1994;toop2000;mitchel2001;southern1983).
Mizizi hasa ya rap Afrika, mbali ya kuanzishwa na wamarekani weusi una sifa mbalimbali za kimuziki na kifasihi simulizi za kiafrika ikiwa ni pamoja na matumizi ya midundo au ridhimu usimulizi,kiitikio na majigambo.Hiphop au muziki wa kizazi kipya ulikuwa kama jukwaa la mshikamano miongoni mwa vijana wa kimarekani  wa mjini na baadaye kuwa kama mtindo  wa maisha na sauti ya vijana .Ni utamaduni ambao uliwakutanisha wale walionyimwa haki ,walionyanyaswa  na kugandamizwa katika historia  na ukawa utambulisho  miongoni mwa Wamerekani weusi na ukawa kipaza sauti chao.

Muziki wa kizazi kipya au rap nikipengele kimoja wapo  cha utamaduni wa hiphop.Ni aina ya ushairi ,usimuliaji,au usemaji unaopangwa vina kwa kufuata mdundo wa ala  za muziki (ambao tayari ulisharekodiwa ).Muziki huu ulianza kama sehemu ya burudani  ya vijana weusi na baadaye ukakuwa na kuenea  na kuwa maarufu  katika nchi nyingi  duniani .Hapa Tanzania  muziki wa kizazi kipya ulianza mwaka 1980.Vijana walianza  kuimba wakiwa ufukweni na baadaye katika sherehe mbalimbali ulianza kisikika redioni  mwaka 1995.
Kama ilivyokuwa kwa Wamerekani weusi vijana wengi  wa Kitanzania pia hutumia muziki wa kizazi kipya  kuelezea matatizo yao  ya kila siku kama vile ukosefu wa ajira  na athari zake ,Dola na nguvu zake  na umasikini.Hapo mwanzoni  nyimbo hizi ziliimbwa kwa kuwaiga wasanii wa  kimarekani kama vile Vanillah Ice,Kriss Kross na Naughty by Nature, halikadhalika walitumia  baadhi ya maneno au sentensi kutoka nyimbo hizo .Hivyo kila mwimbaji  alijaribu kuwa mbunifu na kutunga nyimbo zake mwenyewe ilikuwapata mashabiki na kujiongezea umaarufu.Muziki wa kizazi kipya unaojulikana sana kwa jina la Bongo flava ulishika kasi sana mwaka2000.muziki huu umewapatia vijana wengi  fusra baada ya kusikia nyimbo kutoka n’je ya nchi.

Tanzania  hususani marekani ambapo vijana waliiga na kutoka na staili yao wakitumia lugha ya Kiswahili na wengine walichanganya nyimbo hizo na lugha kama Kingereza na lugha za asili.
Walichoweza kufanya vijana wengi ni kuiga (ala) za Wamerekani lakini waliamua kutumia lugha ya Kiswahili ili kuweza kufikisha ujumbe  kwa Watanzani na kama inavyojulikana kuwa kazi yoyote ya sanaa ina malengo  ya kufundisha ,kukosoa na kuburudisha.Wakati muziki huu unaanza Tanzania hakuweza kuzaniwa kama unge fika karne za mbele lakini hivi sasa una waimbaji wengi pamoja na mashabiki wengi wa rika tofauti hasa vijana, watu wazima si wote wanao upenda muziki huu.
Baadhi ya vijana waliokuwa waanzilishi wa muziki huu kwa Tanzania,vijana wa mwanzo kabisa ambao kuanzia mavazi yao na kufokafoka kwao kulikuwa ni burudani tosha kwa watu kuanza kudadisi kuhusu utamaduni wa mavazi hayo ambayo yalionekana  kama uhuni tena wa kupita kiasi kutokana na uvaaji wa mavazi hayo kihip hop.Hawa ni baadhi ya wasanii wachache ambao walivaa kihip hop Samora Avenue,John simple,DJ Rusual,The BIG ONE,Babu manju,Davidi,Nhigula,Abdulhakim Magomelo,Kessy,Ibony Moalim,Tom
 London,Opp(now JayP)  NA DJ Ngomeley.Hao walikuwa chachu katika uvaaji wa kihiphop na katika kughani Muziki huu wa kizazi kipya.
Pia kuna wasanii wa mwanzo kabisa katika kuimba muziki huu wa kizazimkipya akiwepo mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (BBG lianza na MR.11)FreshXE Mtui,Adili Kumbuka,KBC(Mbeya Tech)Saleh Jabir,Samia X,The Big,Rhymson,2Proud,Kwanza Unit,GWM,Hard Blasters na Bantu pound ambao walianza kuimba katika sherehe za mashuleni,kwenye matamasha mtaani kabla hata ya kurekodi nyimbo zao studio. Kulikuwa na wale wenye kuimba kama wanamuziki wengi wa Marekani kwa kupitia matamasha mbali mbali katika Jumba la utamaduni la Urusi,Korea na mengineyo yaliyokuwa yakiandaliwa hasa na wanafunzi wa shule mbali mbali za sekondari jijini kama Forodhani pia matamasha yaliyokuwa yakifanyika kando kando ya ufukwe ambako wengi wenye kutaka kuimba walijitokeza.

Kulikuwa na  kundi kama la Mawingu na mwana dada Pamela,mwanadada Stara Thomas na Judith Wambura ambao uwezo wa kughani na kuimba kama Mc Lyte ulimuinua hasa alipofanya hivyo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha DJ show ya Radio One,shukrani kwa Ipyana Malecela Mkwavi (RIP) kwa zawadi ya LP yenye mdundo,ala ya single “Keep,Keeping on” ndiyo iliyomtambulisha Jay Dee wa leo Radioni kwa mara ya kwanza japokuwa kabla ya hapo alikuwa mwimbaji wa kwaya kanisani lakini mweye kusita kuingia kwenye muziki wa kidunia.
Pia Kundi la R&B lililojulikana kama Four Krewz Flava pia Herbert Makange ambaye pia alikuwa akiimba. Kwa kufanya haya na mengineyo mengi muziki huu sio tu utakuwa ni wenye kujijengea heshima bali kuweka kumbukumbu kubwa ya mapinduzi kwenye ulimwengu wa muziki Tanzania na hadhi yake kuwa ni ile isiyofutika kwa urahisi machoni na akilini mwa kizazi cha sasa na hata kile kijacho kwa muda mrefu.
>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>
Powered by Blogger.