Riwaya mpya ya Kiswahili

Msomaji anaposoma lugha hii, anaona moja kwa moja kwamba huu ni mfano mmoja wa waandishi wa riwaya hii ambao wanapinga kwamba utandwazi una neema yoyote ile kwa nchi za Dunia ya Tatu. Na kusema kweli, hawaishii hapo tu. Wanaonyesha hasira zao kwa kile ambacho wao wanaona ni ujinga wa viongozi au serikali zetu kukubali kiholela kuihonga nchi kwa mataifa makubwa. Itakuwaje mataifa G7 ambayo yalitukandamiza kwa kila hali wakati wa ukoloni ndio leo yawe yanayotutakia mema? Itakuwaje vyombo kama Benki ya Dunia, IMF na WTO ambavyo vimekuwa vikitoa mikopo kwa masharti magumu mpaka kutunyang’anya uhuru wa kila kitu, viwe ni vyombo vya kutufikisha pahala pema? Itakuwaje itikadi ya uliberali-mpya iwe ndiyo itikadi ya kusafiria kwa nchi za kimasikini? Itakuwaje nchi zetu ziweze kuingia katika mashindano ya kibiashara na USA, Ulaya ya Magharibi, Japani, Australia na Korea ya Kusini? Vipi suala la ndizi za Jamaika? Je, huu haukuwa mfano wa kutosha wa kutufumbua macho? Wakulima wetu wanawezaje kushindana katika uzalishaji na uuzaji wa bidhaa na wakulima wa mataifa makubwa yanayopata fidia kubwa kutoka serikali zao? Hivi historia nzima ya udhalimu wa ukoloni na ukoloni mamboleo, haijawa funzo la kutufanya tushituke na kuuangalia uhusiano wetu na dunia upya na kwa makini zaidi? Kwa mujibu wa waandishi wa riwaya hizi, kukubali kudanganyika kirahisi na mambo haya, kumesababisha kuporomoka vibaya sana kwa nchi zetu katika sekta zake zote, ingawa takwimu za ukuaji wa uchumi zinazotolewa na wakubwa, zinawekwa juu. Hii ndiyo sababu mwandishi mmoja kati yao, Wamitila (keshatajwa: 85, 87, 155), ametumia neno utandawizi, badala ya utandawazi – kijiji cha Global Villain, global pillage. 3.0 Matumizi ya Lugha katika Riwaya Mpya Kwa ujumla, lugha ya aina hii ya riwaya mpya ya Kiswahili ina tabia tofauti na lugha ya aina nyingine za riwaya ya Kiswahili tangulizi ambazo zimekita kwenye uhalisia mkavu. Sifa ya mwanzo na ambayo ni ya msingi, ni ile ya usasabaadaye, ambao, kama mtindo fulani wa fasihi na sanaa kwa ujumla, unakwenda sambamba na utandawazi au ubepari mpevu, kuonyesha mkinzano mkubwa uliomo ndani ya mfumo wake. Usasabaadaye ni mfumo ambao huvunja kanuni zote za kijadi, kaida na namna ya kutumia lugha kisanaa. Sifa ya pili ni ya utouzowefu5 neno lililoanzishwa na shule ya urasimukanuni lenye kubeba maana na kazi maalumu katika fasihi –kazi ya kuichangamsha na kuitia lugha uvuguvugu ili inonekane mpya au ngeni kuliko ilivyokuwa, lengo kubwa likiwa kubadilisha mtazamo wa msomaji kwa kumwonesha ujumi wa lugha ambao utachukua makini ya msomaji, kumvuta kisanaa na kumfanya afikiri zaidi. Kwa mfano Mohamed katika Babu Alipofufuka (2001:13) anacheza na lugha kwa namna ifuatayo: [I]nasemakana Delpiero karibuni amemeza eneo zima la ardhi la pahala fulani tumboni mwake. Wavuvi waliposimama kidete kupuliza cheche zao za uchungu, K alikuja juu kuwaambia wastarehee neema zao ... Sifa ya tatu ambayo pia inashikana na sifa ya mwanzo na ya pili ni ile ya mvutogubi6. Neno hili linasimamia mjazo wa jazanda zenye fumbo, nguvu na mapigo ya kimuziki ambayo mara kadha huonekana ni muhimu zaidi kuliko maana – ingawa katika riwaya hii maana bado inabaki kuimarishwa. Hapa kwa mfano, tuna mchezo wa mvutogubi kutokana na riwaya ya Wamitila, Bina-Adamu (2002: 40): [S]ikujua kama nilikuwa nikitembea kuelekea jana au kwenda kesho au labda nilikuwa leo. Labda nilikuwa kote wakati mmoja ... Sifa ya nne, ni ile ya mchanganyo ndimi, hasa kwa sababu riwaya hii mara nyingi husomba na kujaza kila kitu katika matini yake: historia (‘Vita vya Fyura’ – Bina-Adamu uk. 34), uchumi (‘Nchi nyingi katika ulimwengu wa tatu zilipata pigo kubwa la njaa na mamilioni ya watu walikufa. Migogoro mingi ya kiuchumi iliendelea kuisakama dunia’ – Nagona uk. 18), siasa (‘Dunia yao ndivyo ilivyo; si hii yetu: Kwao taka husafishwa kwa taka; uungwana husafishwa na utumwa –madhali tu K anaramba kamasi tamu za pua...’ – Babu Alipofufuka uk. 10), utamaduni (‘Tupige darubini hivi vitu tunavyovikimbilia kutoka nje. Hizi video na filamu ni propaganda isiyokuwa ya moja kwa moja. Zinatumiwa kusambaza na kutangaza taswira maalumu za utamaduni mmoja tu...’ Bina- Adamu uk. 40), muziki (‘Nilipoingia ndani nilitia CD ya wimbo wa taarab wa Mohamed Ilyas: La Hasha!’ –Dunia Yao uk.87). Kisaikolojia, riwaya zote zinaonyeshwa akili za wananchi kufunikwa na utandu. Kwa matatizo ya utandawazi na mengine yanayoibua matatizo ya kisaikolojia na kisosholojia, mkondo mzima unaomchukua mwanadamu kubadilika na kuwa mnyama, unachunguzwa katika riwaya hizi kupitia kile ambacho tungeliweza kukiita sosiolojia ya riwaya. Aidha mna mchanganyiko wa visaasili, migani na harafa. 5 Tasiri ya Defamiliarisation ambayo ni tafsiri ya ’ostranenie’, neno la Kirusi lililoanzishwa na Viktor Shklovsky 6 Tafsiri ya Hermetic 3.1 Lugha na Usasabaadaye Kwa vyovyote vile, chochote kile kinachohusiana na kilichomo ndani ya fasihi na jinsi kinavyowasilishwa katika kazi hiyo, lazima kihusishwe na matumizi mbalimbali ya lugha. Makala haya yanatambua ukweli kwamba kile ambacho, kwa mfano, kinaitenga lugha ya sayansi na fasihi ni jinsi lugha inavyojitokeza tofauti kimaumbo, kimsamiati na kimuundo katika nyanja hizi mbili. Ukweli huu umo pia katika namna lugha za ushairi na nathari, uhalisia na fantasia, usasa ulioanza baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia; na usasabaadaye, ulioanza baada ya Vita vya Pili ya Dunia na kwenda mbele zaidi kuigeuza riwaya ya uhalisia jinsi ilivyokuwa kabla ya kuzuka kwa usasa huko Ulaya. Usasabaadaye, kama njia moja ya kubuni kazi za fasihi, ulianza mapema tokea miaka 1950, baada ya kuporomoka kwa uhalisia na usasa. Lakini ni katika miaka ya 1980 ndipo usasabaadaye ulipopata upana wa matumizi katika nyanja za falsafa na utamaduni na pia katika fasihi na uhakiki wa kifasihi (Gromov 2004:1). Lengo kuu la usasabaadaye, kinyume na uhalisia na usasa, ni kuonyesha kutoweza kwa mwanadamu kuufahamu ulimwengu, kwa sababu urazini wa mwanadamu hauwezi tena, katika hatua hii, kuutambua utata wa ulimwengu. Kile kinachowezekana labda ni kuchunguza picha au alama za vitu. Hii ni kusema kwamba mwanadamu haufahamu ulimwengu wake kwa sababu tu umekuwa ni ‘uwanja wa fujo’, bali pia kwa sababu ni kama matini tu; yaani mlimbikizo usiokuwa na mwisho wa alama zinazobuniwa kutokana na urazini wa mwanadamu. Kwa hivyo, uzoefu wa mwanadamu, historia yake, utamaduni wake –kila kitu ni mkondo wa alama, ambamo zile zilizo tata hutokana na zile sahili zilizokuwepo hapo awali. Hapa tutaitazama lugha ya riwaya mpya katika ugo huo. Lakini kabla hatujafanya hivyo, yafaa tukawazindua wasomaji wetu juu ya jambo moja ambalo Gromov (keshatajwa) analieleza na ambalo ni la kipekee katika riwaya hii mpya ukilinganisha na usasabaadaye katika fasihi za lugha na tamaduni nyingine. Jambo hili linahusiana na namna waandishi wa riwaya hii mpya wanavyobaki kung’ang’ania tamaa na kutukuza utu na ubinadamu. Katika hitimisho lake Gromov (keshatajwa: 12-13) anatwambia ... [l]azima tugundue kwamba kuna tofauti kubwa baina ya umahiri wa usasabaadaye wa nchi za ki-Magharaibi na ule wa jamaa zao wa Afrika Mashariki, Kiswahili kinakozungumzwa. Waandishi wa Kiswahili katika kuvutika na usasabaadaye wana mtazamo na msimamo wa pekee kuhusu maana na umuhimu wa ujumi ukilinganisha na ule wa wanausasabaadaye wa ki-Magharibi –wanausasabaadaye wa Kiswahili wana mtazamo mkali juu ya kuvunjiwa thamani dunia. Katika mtazamo wao mkali, waandishi wa riwaya mpya ya Kiswahili, utu na mapenzi vinatetewa kama tunavyosoma katika Bina-Adamu, pale mhusika mkuu Binadamu Msafiri anapoonywa kuutunza mkoba aliopewa na babu na kuambiwa ... [U]tunze huu, ndani mna utu, mapenzi na kiini cha kuwako kwako. Mkoba huu utakufaa sana siku zijazo: Usiudharau kwa sura yake; mwacha asili ni mtumwa ... Makala haya yanakubaliana sana na Gromov kuhusiana na ugunduzi huu muhimu wa suala la utu na mapenzi katika riwaya mpya ya Kiswahili na waandishi wake. Lengo mojawapo la makala haya ni kudhihirisha hivyo. 3.2 Lugha ya Uhakiki na Mkemeo wa Utandawazi Waandishi wa riwaya mpya ya Kiswahili katika uhakiki wao wa siasa na mwenendo wa jamii, wanataja wazi kwamba umefika wakati sasa Mwafrika ajilaumu mwenyewe juu ya balaa lote linalomkuta; na la kulaumiwa zaidi, hasa, ni taratibu za uongozi zitumikazo katika Afrika
>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>>>>>
Powered by Blogger.