ULAJI SAHIHI WA MATUNDA
Wengi wetu tunajua kununua, kuandaa na kisha kula matunda, lakini ni wachache sana tunaojua wakati gani tunda lililewe au kati ya mlo wa kawaida na matunda kipi kitangulie. Wanaopata faida ya matunda mwilini ni wale tu wanaojua wakati sahihi wa kula matunda hayo.
NJIA SAHIHI YA KULA TUNDA
Unapaswa kula matunda kabla hujatia chakula kingine tumboni, siyo kula baada ya mlo kama inavyofanywa na watu wengi. Kwa kula matunda kabla ya mlo kunawezesha matunda hayo kuingia mwilini na kufanyakazi yake ipasavyo kama vile kusafisha mfumo wa damu (detoxification) na kuupa mwili nguvu.
Mfano; kula vipande viwili vya mkate kisha kula na vipande viwili vya matunda. Vipande viwili vya matunda vitasagika mapema kuliko vile vya mkate, kwa kuwa vipande vya matunda vinasagika haraka vitakosa mahali pa kupitia wakati vitakapokuwa tayari kwenda kwenye utumbo, hivyo matunda nayo yatakwama hapo.
Kwa mujibu wa watafiti wetu katika masuala ya lishe, chakula kinapoingia tumboni huumuka na kuwa na asidi, matunda yaliyokwama na kukutana na vipande hivyo vya mkate pamoja na yale majimaji ya kulainishia na kusaga chakula yaliyomo tumboni (digestive juice), matokeo yake huwa ni kuharibika kwa chakula chote na kuanza kuumwa tumbo. Kwa sababu hiyo inashauriwa tunda liliwe kabla kula kitu chocote au kabla ya kula chakula.
Baadhi ya watu wanapokula tunda ama kunywa juisi hupiga mbwewe au tumbo kuunguruma na hata kuuma na kujisikia kwenda chooni, hasa wanapokula ndizi mbivu, hiyo yote inatokana na kuchanganya chakula na matunda, hali hii ingeweza kuepukwa kama tunda likiliwa kwanza kabla ya kitu kingine au chakula.
Weusi unaotokea chini ya macho, kuota mvi, upara na kuwa na wasiwasi kila mara, kunaweza kuepushwa kwa kula matunda kabla ya kula kitu kingine. Kuna dhana potofu kuwa unapokula matunda kama machungwa na ndimu, husababisha gesi tumboni, lakini utafiti wa kisayansi unaonesha kuwa matunda yote yenye asidi yanapoingia tumboni huondoka asidi na kuwa ‘alikali’.
Kula tunda na nyama zake, kama vile chungwa, ni bora zaidi kuliko kunywa juisi yake, kwani nyama za matunda hayo zina ‘faiba’ muhimu yenye faida nyingi mwilini. Unywapo juisi, kunywa taratibu kwa kujaza mdomoni ili juisi ipate nafasi ya kuchanganyika na mate yako kabla ya kumeza.
Funga ya siku tatu kwa kutumia matunda, ni njia bora sana ya kusafisha mfumo wa damu na kuondoa sumu mwilini. Ili kufanikisha hilo, kula matunda na kunywa juisi za matunda tu katika kipindi chote cha siku 3 na utashangaa marafiki zako watakavyoona ulivyonawiri.
Katika kipindi hicho cha kufunga, utakuwa ukila matunda mchanganyiko na kwa muda tofauti na usile chakula kingine zaidi ya maji tu. Unaweza pia ukaandaa ‘salad’ ya matunda au mboga, ambayo yaweza kuwa nzuri zaidi.
Ukifanikiwa kutumia njia sahihi ya kula matunda, bila shaka utakuwa umegundua siri ya urembo, maisha marefu, afya njema, nguvu ya mwili, furaha na kuishi maisha ya kuwa na uzito wa kawaida siku zote