SIRI YA MUUAJI

JALADA: BENCHRYS. INC.
Aliishiwa pozi baada ya kushuhudia wingi wa walinzi waliokuwepo maeneo yale, alitegemea angekuta hata walinzi wawili au watatu. Lakini alikutana na walinzi wengi waliojikusanya sehemu moja wakipiga soga.
‘’Hapa panatakiwa mpango butu ufanyike laa sivyo, nikubali kuwagutusha na walioko ndani. Hapana itakuwa ngumu kwangu kufanya hivyo, mpango butu unahusika hapa.’’. Alijiwazia mwenyewe na kumuangalia nyoka aliyemshika.
Alitabasamu na kumgonga makonzi ya haja kwenye kichwa yule nyoka, hasira zilimpanda na kufanya kutoa sauti za maumivu kutokana na makonzi ya Masoud kumuingia vilivyo, Masoud alitabasamu na kumtupia yule nyoka upande walipo wale walinzi waliokuwa wameshughulishwa na upigaji wa soga... Nyoka aliteleza chini ya ardhi yenye majani makavu kwa kasi huku kichwani mwake akiwa na hasira zilizopitiliza.
‘’Mpango butu,hii ni pata potea.’’. Masoud aliongea mwenyewe na kutabasamu huku macho yake akiyaangaza mbele kwa wale walinzi, alitaka kuona kitakachotokea kwenye mpango wake butu usio na makali yoyote yale.
Yule nyoka aliteleza chini ya ardhi kwa kasi mpaka katikati yao, alimgonga mmoja mguuni na kumfanya aruke, wengind nao waliungana nae kwenye urukaji.
Walipoona ni nyoka ndie anaewafanya waruke ruke kama watoto, walichukua silaha zao na kummiminia risasi nyoka yule.
‘’Nasikia kama milio ya risasi huko nnje.?’’ . Waziri wa ulinzi nchini congo, alimuuliza kiongozi wa waasi baada ya kusikia milio ya risasi nnje.
‘’Itakuwa kuna uvamizi.’’. Kiongozi yule alijibu hivyo na kunyanyuka kutoka kwenye kiti alichokaa na kulisogelea dirisha... Aliangalia nnje kuliposikika sauti za risasi, aliduwaa baada ya kuwaona vijana wake wakishangilia huku mmoja akiwa kamshika nyoka aliyekufa.
‘’Ni wajinga sana hawa, walikuwa wanamshambulia nyoka kumbe.’’. Alizungumza hivyo na kukirudisha kichwa chake pamoja na kiwiliwili chake ndani, waziri wa ulinzi alihema kidogo. Muhemo ambao uliashiria kuna jambo lilimuogofya ndani ya moyo wake.
Huku nnje vijana walikuwa wanapiga makelele ya kushangilia baada ya kumuua nyoka yule aliyetaka kuwasumbua, wakati wao wakiendelea kushangilia juu ya ushindi wao wa kumuangamiza nyoka.... Kijana Masoud alitoka sehemu alipokuwa kajibanza na kuelekea kule kwa wale vijana waliokuwa wameshughulishwa na upigaji kelele, mkononi alikamata bastola ndogo zenye uwezo wa kuhifadhi risasi takribani ishirini na nne, mbele ya bastola zake mbili alizozishika, aliweka kiwambio cha sauti ili kuzuia kutosikika na mwengine.
Alifika na kujichanganya katikati yao, miruzi ililindima kwa vijana wale waliokuwa hawana taarifa kama katikati yao kuna mmoja sie mwanakikundi mwenzao, Masoud baada ya kujichanganya nao. Alitoa kidubwana fulani kilichoundwa kama kibiriti cha gesi na kukifungua kisha yeye akajiziba usoni na kitambaa maalumu, kitu kile kilianza kutoa moshi mwembamba uliokuwa unasambaa kwa hewa... Ghafla vijana wale kila mmoja akaanza kudondoka chini na kuwa kimya kama mtu aliyelala usingizi, dakika tatu baadae vijana wote walikuwa wamelala bila fahamu.... Masoud baada ya kufanya vile, aliwakusanya na kuwaweka kwenye sehemu zao kama walivyokuwa wamekaa mwanzo, baada ya kuweka vile. Alitoka pale na kuzunguka upande wa pili kulipokuwa na kibanda kilichokuwa na mlinzi mmoja pamoja na taa kubwa yenye kuangaza kambi ile.
Alipanda kwa kutumia ngazi zilizowekwa kwenye kibanda kile kwaajili ya kupandia juu, alifika juu na kumkuta mlinzi akiwa kaangalia upande ule walipokuwa wenzake waliolala bila kupenda... Alichukua kitambaa cheupe na kukishika mkononi... Mlinzi yule baada ya kuyagandisha macho yake mbele kwa dakika kadhaa, aligeuka nyuma kwaajili ya kukagua upande wa pili kama kuko salama au laa.... Wakati anageuka nyuma, akakumbana na kitu usoni huku hewa aliyokuwa anaivuta hapo awali, ikibadilika na kuwa nzito hali iliyopelekea mwili kupoteza nguvu..... Masoud baada ya kumzimisha mlinzi yule, alimuegesha uapnde wa pili wa kibanda kile ili walioko ndani wakitazama juu ya kibanda waone kama mlinzi huyo kaangalia nyuma.
Baada ya kufanya vile, kijana Masoud alianza kutelemka chini na kuzama kwenye moja ya hema lililokuwa kambini mle.... Kitendo cha kuingia ndani ya hema lile, alikumbana na lundo la wasichana wa kila rangi wakiwa wamefungwa mikono na miguu huku mdomoni wakiwa wamebandikwa blasta kubwa zilizowafanya kushindwa kupiga kelele, Masoud alishindwa kuzuia machozi yasichuruzike kwenye mashavu yake kutokana na kitendo alichokishuhudia mbele ya macho yake. Mikono ilimtetema kwa hasira, midomo ilipigizana na kufanya sauti ya meno yaliyokuwa yanagongana kwa ghadhabu kusikika vyema kwenye masikio ya wasichana wale wenye umri mdogo sana.
‘’Hii imezidi sasa, ifike wakati waone aibu kuwafedhehesha wasichana kama hawa... Majumbani kwao kuna watoto wa kike kwa waume, hawafikirii kama hawa ni sawa na watoto zao. Aaaah hii inabidi kukomeshwa ila ikiachwa hivi hivi, itaendelea kukithiri kwenye kila taifa.’’. Alizungumza hivyo huku akipiga hatua mbili mbele, wakati akiendelea kusogea mbele kwa lengo la kuwafungulia wasichana wale.
Alishangaa baada ya kuona wasichana wale wakitikisa vichwa vyao kulia na kushoto huku miguno ya sauti zao zilizoishia ndani ya plasta, zikizidi.... Hakuelewa mara moja ni nini wanamaanisha wasichana wale ila alielewa baada ya kuona kimvuli cha mtu nyuma yake, alitaka kugeuka lakini alishindwa na kujikuta akianguka chini baada ya kitu kizito kugota nyuma ya kichwa chake, fahamu zilipotea baada ya chuma kukita nyuma ya kisogo. Sehemu yenye kila kitu cha mwanadamu hususani ni kama ubongo na maburangata.
Alibebwa na mtu aliyemfanyia vile na kupelekwa ndani kwenye nyumba waliyopo wakubwa wa kambi ile.
‘’Nilijua tu. Kama kuna panya atakuja baada ya kuona paka hayupo, walinzi niliwatoa kimakusudi kabisa nikiwa namaana ya kukuvuta zaidi kwenye ngome yangu, mpelekeni kwenye chumba cha mateso... Ataeleza nani aliyemtuma.’’. Kiongozi wa waasi alizungumza hayo baada ya kuletewa mwili wa Masoud uliokuwa unakokotwa.
Walinzi walitii amri na kumpeleka Masoud kwenye chumba cha mateso ambako, walimfunga nyororo ngumu kwenye mikono yake na miguu huku akisimamishwa kama yesu, vyombo mbalimbali vya mateso vilisogezwa karibu yake huku jiko la moto lililotawaliwa na vyuma vilivyokwisha badilika rangi na kuwa vyekundu kutokana na muda mwingi kuwa ndani ya moto navyo vilisogezwa, dakika kumi baadae, kiongozi yule wa waasi akiwa na waziri wa ulinzi wa nchi ya congo.. Waliingia kwenye chumba kile alichopo kijana Masoud na kumkuta akiwa kavuliwa nguo zote na kubaki kama alivyo zaliwa, mwili wake uliojazia kimazoezi ulitawaliwa na majeraha ya mjeledi aliyotapata kwa dakika kadhaa toka aingizwe kwenye chumba kile na hapo vijana waliendelea kumcharaza.
‘’Inatosha, mmwagieni maji kwanza.. Nahitaji fahamu zake zirejee ili anieleze aliyemtuma.’’. Kiongozi yule wa waasi alitoa agizo kwa vijana wawili waliokuwa wanamuadhibu kwa mijeledi kijana Masoud.
Vijana wale waliacha na kusogea pembeni wakimpisha mmoja wao aliyebeba ndoo ya maji ya baridi aelekee mbele kwaajili ya kummwagia maji Masoud, kijana yule mwenye ndoo ya maji baada ya kufika karibu na Masoud.... Alinyanyua ndoo yakd yenye maji ya baridi na kumwaga kwenye mwili wa kijana Masoud aliyegutuka baada ya maji kutua kwenye mwili wake.
‘’Aaaaaaaaa.’’. Alitoa ukunga wa maumivu baada ya kuzinduka, alifikicha macho yake na kujaribu kutazama mbele alipohisi kuna watu wamemsimamia lakini alishindwa kutokana na maji kuongezwa kwenye mwili wake.
‘’Niambie kijana, aliyekutuma kuja kusumbua kambi yangu ni nani.?’’. Baada ya maji ya awamu ya pili kuisha kwenye mwili wake na kumfanya Masoud apate uwezo wa kutazama mbele. Alikutana na swali hilo kutoka kwa kiongozi wa kambi ile.
Alimtazama bila kumjibu kitu kisha akaigeuza shingo yake upande wa pili alipokuwa waziri wa ulinzi. Macho yake yalipotua kwenye mwili wa waziri yule, alijikuta akiangua kicheko cha haj. Kicheko kilichowaacha midomo wazi wote waliokuwepo ndani ya chumba kile.
‘’Najua unacheka kwa kujifariji lakini ningependa kukupa taarifa kwamba, kwenye kambi yangu usitegemee kama kuna sisimizi yeyote yule ataweza kuingia na kukufikia hapa ulipo, nahitaji tuzungumze mazungumzo ya amani baina yangu na wewe ila ukikaidi, nitakufanya uzungumze kwa uchungu uliopitiliza. Swali langu linajirudia kwa awamu ya pili sasa, niambie aliyekutuma kuja kuigasi kambi yangu na nini dhumuni la kutumwa.?’’. Kiongozi yule alipiga hatua tano mbele na kusimama karibu ya Masoud ambapo alimuuliza swali baada ya kijana huyo kunyamaza kucheka.
Masoud alimtazama kwa sekunde kadhaa kisha akaangua kicheko cha dakika moja na kutema kohozi zito lililochanganyikana na damu, kohozi lile lisilokuwa na adabu wa uoga. Lilitua kwenye uso wa yule kiongozi na kuchuruzika mpaka kwenye mdomo.
Vijana walitaka kumshambulia Masoud kwa kitendo chake cha kumtemea kohozi kiongozi wao, lakini walisita baada ya kiongozi wao kutoa bishara ya mkono akiwataka wasiingilie mazungumzo yao, kiongozi yule alitoa kitambaa chake cheupe na kupangusha kohozi lililoanza kuganda kwenye uso wake.
‘’Mimi ni mtu ninaependa san amani tena kwa mtu kama wewe, lakini nashangaa unataka kuiharibu amani niliyokupa kwanini lakini.?’’. Baada ya kufuta kohozi alilotemewa na Masoud, alitoa chuma kimoja kilichokuwepo kwenye jiko lenye moto uliokolea na kumuuliza kijana Masoud kwanini anakataa kuzungumza kwa amani.
Masoud hakujibu chochote wala kuonesha dalili za kuogopa chuma kilichotolewa jikoni kikiwa cha moto mpaka kubadilika rangi.
‘’Niambie tu rafiki yangu, nani kakutuma kuja kuifanya hii kazi? Na mimi nitakuacha uende salama bila kukugusa.’’.
‘’Unajisumbua tu. Ni bora ungeanza kukimbia kwenye hii kambi kabla mambo hayajaharibika na sio kushughulika kumpigia mbuzi gitaa ukitaraji atasimama na kucheza.’’. Masoud alitoa tambo na kumtazama yule bwana kwa macho ya dharau.
‘’Oooh!! Basi sawa, naona unataka tuzungumze mazungumzo ya kishari zaidi.’’ Bwana yule alizungumza hivyo na kuruhusu chuma alichokishika kugusa kwenye tumbo la Masoud aliyekunja uso kutokana na maumivu aliyoyapata, chuma kilizidi kuunguza eneo kilipogusa mpaka ule uwekundu ukaanza kupotea, ngozi ilishindwa kuvumilia hali ile ikaanza kutoa mvuke kuonesha imeiva vya kutosha... Masoud alivumilia mpaka chuma kilipotolewa na yeye papo hapo akalegea na kushindwa kusimama tena na kubaki akining’inia.
‘’Unaweza kuniambia kambi yeni inapatikana wapi na mkubwa wako wa kazi ni nani.?’’. Bwana yule baada ya kutoa chuma kilichotoka na vinyama nyama vya eneo kilipogusishwa, aliuliza tena swali na kukiinua kichwa cha Masoud kilichokuwa kimeinamia kwa chini.
‘’Sahau kupata unachokihitaji kutoka kwangu.’’ Masoud alijibu kwa kejeri huku mdomo wake ukichuruzika damu kuonesha kile chuma kilichochoma kwenye tumbo lake, kilimletea shida ndani ya tumbo.
‘’Basi sawa kama hutosema jambo.’’. Kiongozi yule wa waasi alizungumza hivyo na kurudi hatua kadhaa nyuma na kutoa ishara ya mashine ya umeme isogezwe karibu kwaajili ya kutoa adhabu kwa Masoud mpaka pale atakaposema nani aliyemtuma.
Mashine ilisogezwa na kijana Masoud akatolewa pale alipofungwa na kusogezwa kwenye sinyenge zilizounganishwa waya za umeme, alifungwa mikono juu na miguu ikatanuliwa kidogo huku mgongo wake ukilazwa kwenye sinyenge zilizochongwa zikachongeka, maumivu yalianza baada ya kulazwa kwenye sinyenge zilizoanza kumchoma mgongoni na sehemu nyingine za mwili wake... Kwakua hakuwa na nguo ambayo ingemsaidia kuzuia sinyenge zisimchome, sinyenge ziliingia kwenye mwili wake bila tabu yoyote ile kwa maana nguo kijana Masoud hakuwa nazo.
Kijana mmoja alienda karibu na Masoud na kummwagia maji ya baridi na kurudi nyuma, kiongozi yule wa waasi alitoa ishara kwa kijana mmoja aliyekuwa kasimama karibu na mashine ya umeme akimtaka aiwashe, bila hiyana kijana akatii amri na kuiwasha mashine ile huku akizungusha sehemu itumikayo kuongeza nguvu ya umeme au kupunguza, kijana Masoud alitapatapa kwenye sinyenge zile baada ya umeme kusambaa.... Umeme ulizidi kuongezwa mpaka taa zilizokuwepo mle ndani zikaanza kuzima na kuwaka.
‘’Inatosha.’’. Kiongozi yule alitoa agizo baada ya kuona adhabu ile inatosha.
Kijana aliyekuwa kasimama kwenye mtambo wa umeme, alizima na kusubiri agizo jingine... Walitoka vijana wale waliompeleka Masoud kwenye sinyenge zile na kumfungua kijana Masoud aliyepoteza fahamu baada ya umeme kumzidia, walimpeleka eneo alilokuwa kafungwa hapo awali na kumfunga nyororo.
‘’Mzindueni, hawezi kufa kirahisi kiasi hiki.’’. Amri ilitolewa na kijana anaehusika na umwagaji wa maji akatoka mbele akiwa na ndoo yake mkononi na kummwagia Masoud alizinduka kutoka kwenye usingizi wa nusu kifo.
‘’Unaweza kunieleza sasa.?’’. Kiongozi yule aliuliza baada ya kuona Masoud ameamka.
Kijana Masoud alitikisa kichwa chake kuonesha yupo tayari kuruhusu kinywa chake kuzungumza, yule kiongozi alitabasamu na kupiga hatua ndogo ndogo mpaka pale alipofungwa Masoud na kuinama kwaajili ya kuambiwa siri iliyofichwa ndani ya moyo wa Masoud.
‘’Hii ni siri ya muuaji, kamwe hawezi kuitoa mbele ya mtu yeyote yule... Kifo chako kinakaribia.’’.
*******************************************************************
Itaendeleaaaaaa.......!!!!!!!!
Kuna watu wamelalama kwa kuvunja ahadi, nilipanga kupost saa 4 asubuhi lakini mambo yakaingiliana.
Nishasema nafanya kazi saloon muda wa kushika simu ni mchache, nilisema nitapost saa nne kwasababu nilitarajia jana usiku nitaandika, lakini nikapitiwa na usingizi data yenyewe niliiacha ikiwa imewaka.
Alafu tutambue kitu kimoja, sisi ni binadamu na kama sisi ni binadamu.. Matatizo ni mengi sidhani kama kati yetu kuna mmoja mwenye uhakika kama kesho atafika salama bila tatizo lolote lile....
Nisameheni kama niliwakwaza ila inawapasa kumfikiria huyu mtu kaamkaje kabla ya kuanza kulalama.
Mimi ni binadamu sijakamilika kama maneno yangu yatakuwa yamewakwaza basi niwieni radhi ila kazi ya uandishi ni ngumu ukichukulia unaandikia simu/ simu yenye kupigwa kila wakati na kutumwa sms kila muda achilia mbali kuishiwa chaji.
Powered by Blogger.