DHANA YA ISIMU NA LUGHA
Maana ya pijini na krioli Pijini ni lugha yenye mfumo uliorahisishwa sana ambao hutumiwa na wazungumzaji wenye lugha tofauti katika mazingira maalumu na kwamba pijini sio lugha mama kwa mzungumzaji yeyote. Krioli ni lugha mama inayotumiwa na wazungumzaji wazawa ambao kihistoria wametokana na jamiilugha ya pijini. Sifa za pijini na krioli Kwa asili ni lugha chotara Zina mfumo wa lugha sahili Hutumika zaidi katika mawasiliano yasiyo rasmi
Umuhimu wa kujifunza lugha za pijini na krioli
Sababu za kihistoria na kijamii Chanzo muhimu cha Data za Isimujamii Changamoto kwa watunga sera za lugha.
Usanifishaji wa lugha ya pijini na krioli. Matatizo ya lugha za pijini na krioli • Lugha duni • Wazungumzaji hawako tayari kusahihishwa. ULUMBI
Ulumbi ni hali ya matumizi ya Lugha mbili au zaidi katika miktadha maalum. Ni hali ya mzungumzaji binafsi kuwa na umilisi wa lugha mbili au zaidi ambazo anaweza kuzitumia katika mazingira tofauti. Hali hii pia hujulikana kuwa ni uwililugha.
Aina za ulumbi
Ulumbi Taifa: Unatokana na kugawa lugha mbalimbali katika majukukumu tofautitofauti kama vile; lugha ya kisheria, lugha ya shule, lugha ya ibada. Ulumbi taasisi: Hapo tunaona kuwa kunakuwa na lugha mbili au zaidi zenye hadhi ya lugha rasmi. Kwa mfano ulkiangali hapa petu Tanzania utakuta kuwa ofisi nyingi zinatumia Lugha ya Kiingereza na Kiswahili kama Lugha mbili rasmi. Ulumbi binafsi: Hii ni hali ya mtu mmoja kutumia Lugha mbalimbali katika mazingira tofauti. Mfano huu unaelezea hali ya Watanzania waliowengi, hasa wasomi huwa wanajuwa kwanza Lugha za kikabila, pili Kiswahili na tatu Lugha ya kigeni yaani Kiingerza au hata Kifaransa.
Lugha zote hizo anazitumia katika mazingira tofauti. Kazini anaweza kutumia Kiingereza na Kiswahili. Mtu huyohuyo yawezekana akawa anatumia Lugha yake ya asili kama vile Kisukuma na Kinyakyusa. Ulumbi Binafsi pia unahusika na kipengele cha kubadili msimbo. Hii ni hali ya kubadili Lugha zaidi ya moja katika mazungumzo kwa mzungumzaji yuleyule. Kubadili msimbo ni mbinu ya mazungumzo inayovunja mipaka ya mawasiliano ili kujenga njia bora ya mawasiliano. Moja ya sababu za kubadili msimbo ni hali ya mzungumzaji kuwa na umilisi mdogo wa Lugha mojawapo hivyo huibia ile Lugha nyingine ili kukamilisha mawasiliano. Pengine huweza kutokea kuwa na mapengo ya kiisimu ambayo hayana budi kuzibwa kwa kubadili msimbo.
MUHADHARA WA KUMI NA TISA:
ISIMU - NAFSI: UCHAMBUZI WA MICHAKATO YA LUGHA
Dhanna ya isimu nafsi Maana ya isimu nafsi: • Taaluma inayoshughulikia uchambuzi wa michakato ya lugha. • Taaluma hii inachunguza ni kiasi gani maana ya maneno, sentensi na mazungumzo yanavyokokotolewa katika ubongo.
Matawi ya isimu nafsi.
• Elimu tambuzi (cognitivism)-Hii hujishughulisha na saikolojia ya kujifunza lugha. • Isimu matumizi (Applied Psycholinguistics)- Hujishughulisha na maendeleo ya lugha hasa upande wa neva.
Kuteleza kwa ulimi – Uspuna
• Dhanna ya uspuna: ni tendo la kuchanganya herufi za mwanzo za maneno bila kukusudia. Historia fupi ya uspuna: Dhanna ya uspuna imetokana na mchungaji Willium A. Spunner wa New College, Oxford, kwa jinsi alivyokuwa akitunga misemo au mashairi yenye kuchekesha kwa makusudi ili kupotosha namna ya usemaji. Mpangilio wa maneno katika ubongo • Kila mtu ana hazina ya msamiati ambayo ndiyo msingi wa mawasiliano kwa kutumia lugha. • Tunaitumia misamiati hiyo kama tutumiavyo kamusi. • Huwa tunanukuu hazina hiyo, tunapotaka kujua maana ya maneno, yanavyoandikwa na jinsi yanavyotamkwa.
Michakato ya Lugha na isimu
Mchakato wa fonetiki na fonolojia:- • Uchambuzi wa fonetiki na fonolojia unaonesha muundo wa lugha umejengwa katika ngazi mbalimbali za uwakilishi. • Vipashio vinagawika kimahali na namna ya utamkaji. • Vipashio vinagawika katika mfuatano wa silabi na alofoni. • Je, ni kwa kiasi gani mgawanyiko huu unachangia katika kuchanganua lugha?
Mchakato wa kimofolojia
• Uchambuzi wa mofolojia hujishughulisha na muundo wa neno. • Ni mfumo wa uchunguzi wa kategoria na kanuni za uundaji wa maneno. • Uchambuzi wa isimu-nafsi na michakato ya kimofolojia hujishughulisha na namna huo uundaji wa maneno unavyosaidia kuikuza lugha. Mchakato wa kisintaksi. • Tumeona kuwa katika nadharia ya uzalishaji sentensi ya Chomsky, ili kufikia maumbo ya nje ya sentensi, kwanza huwepo kwa maumbo ya ndani. • Maumbo hayo ya ndani yanapitia mchakato wa uzalishaji hadi kufikia hayo maumbo ya nje. • Wana isimu nafsi wamejaribu kuchunguza iwapo sentensi yenye mfumo uzalishi mwingi huchukua mchakato mrefu zaidi kuliko sentensi yenye mfumo uzalishi mchache.
SWALI 1: Unadhani katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia rejista bado zina umuhimu wowote? JIBU:[hariri chanzo]
Rejista (pia rejesta au sajili) ni matumizi ya lugha kulingana na muktadha maalum. Miktadha tofauti husababisha aina mbalimbali za lugha. Baadhi ya vipengele vya miktadha hiyo ni mada, eneo la matumizi ya lugha, mahusiano baina ya wahusika, umri, jinsia, wakati, na kadhalika.
KIINI Rejesta zina umuhimu mkubwa sana katika lugha hasa kulingana na maendeleo yanayoikumba lugha kimatumizi. Umuhimu wa rejesta ni kama ufuatao Rejesta hutumika Kama Kitambulisho Rejesta hutofautisha mtindo wa lugha miongoni mwa wazungumzaji. Rejestainawatambulisha wazungumzaji kuwa wao ni kundi fulani. Mfano: Rejesta yawahunzi inawatambulisha kuwa wao ni tofauti na wavuvi ambao nao pia wanarejesta yao. Rejesta ya kanisani au msikitini ni tofauti na rejesta ya jeshini, n.k. (ii) Rejesta hupunguza Ukali wa Maneno Rejesta inapotumiwa na kundi la watu, huficha jambo hilo linalozungumziwalisieleweke kwa wengi. Hivyo hadhira inapuuzwa kwa sababu siyo watu wengiwanaoelewa. (iii) Rejesta Inatumika Ili Kurahisisha Mawasiliano Rejesta inatumika ili kurahisisha mawasiliano au kupunguza muda wakuwashughulikia watu au wateja wengi. Kwa mfano mganga anayegawa dawahospitalini anaposema “mbili asubuhi, mchana na jioni” akiwa na maana kuwamgonjwa anywe vidonge viwili asubuhi, viwili mchana na viwili jioni. Hapaamefupisha ili aweze kuwahudumia kwa wakati mfupi wagonjwa wengiwanaosubiri kupata dawa. (iv) Rejesta hupamba Lugha Miongoni mwa Wazungumzaji Kwa mfano, Rejesta ya Hotelini. Mhudumu: Nani wali kuku?Mteja: Mimi hapa!Mhudumu: Nani ugali-ng’ombe?Mteja: Mimi hapa!
Mazungumzo haya kati ya mhudumu na mteja licha ya kurahisishamawasiliano, vilevile yanapamba mazungumzo hayo. (v) Rejesta huweza Kuwa Kiungo cha Ukuzaji wa Lugha Kutokana na matumizi ya rejesta mbalimbali, lugha inayohusika inawezakuunda msamiati wake. Kuna baadhi ya maneno ya lugha yanayotokana narejesta mbalimbali.
HITIMISHO Ukuaji wa lugha ya Kiswahili hutegemea sana usanifishaji wa maneno yanayotumika katika jamii na kupata mashiko.