SURA YA PILI : 2.0 MAPITIO YA MAANDIKO. Sura hii inabainisha machapisho mbalimbali yanayohusiana na mada hii,machapisho hayo yatahusu maandiko mbalimbali ya muziki wa kizazi kipya na lugha .Baadhi ya waandishi wameelezea muziki wa kizazi kipya kwa kuelezea maudhui na fani.Kwa ujumla kupitia kazi hizo muziki wa kizazi kipya umeonekana kuwa lenga zaidi vijana kutokana na lugha inayotumika katika nyimbo hizo.Muziki wa kizazi kipya umeonwa kama chombo kinacho wasaidia vijana kuelezea matatizo yao kwa kutumia lugha wanayoielewa wenyewe. 2.1 MAANDIKO KUHUSU MUZIKI WA KIZAZI KIPYA. Waandishi mbalimbali pamoja na wasanii wameuelezea muziki wa kizazi kipya jinsi ulivyoanza na mtazamo wao kuhusu uelekeo wa muziki huu hapo baadaye. Machapisho kuhusu wataalamu wanasema nini juu ya muziki wa kizazi kipya. Hapa tutawaangalia(Chachage,2002;Mgembe,1998;Fenn&Perulla,2000;Senkoro2003;) Majembe(1998),anasema “uchanganyaji wa lugha ndiyo sifa kubwa inayojitokeza katika nyimbo hizi kwasababu wasanii wengi huchanganya lugha tofauti ilikuonyesha ubunifu tofauti na wasanii wengine na kupelekea watu wazima kuona nyimbo hizo ni uhuni”. Senkoro(2003),katika maandishi yake ya sanaa anasema : “wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatumia lugha kama bidhaa ambayo wameizalisha baada ya kujiajiri wenyewe.Ingawa nyimbo hizi zina mchanganyiko wa kiingereza, Kiswahili na lugha za kienyeji nyimbo hizi zinatumia sana misimu sababu ndiyo inayoeleweka kwa vijana”. Chachage(2002) anasema : “Watanzania wengi wanadhani muziki wa kizazi kipya unapotosha utamaduni wa mtanzania hawa ni wapotofu wa mawazo.kwani utamaduni katika jamii ni mwingiliano wa mambo mengi toka ndani na n’je ya nchi” Chachage yupo sahihi lakini hata kama tunaiga utamaduni kutoka n’je haipaswi tuvuke mipaka ya utamaduni wa nchi yetu na lugha yetu.. Fenn na perulla(2000) “matumizi haya ya uchanganyaji lugha yanatokana na itikadi ambayo imejengeka miongoni mwa wasanii hao na pia kwa lengo la kupata mashabiki wengi.Wanatumia kingereza sababu ni lugha ya kimataifa, wanatumia Kiswahili kwasababu ni inayoeleweka kwa watumiaji wengi.” Senkoro,Majembe na fenn Perulla wameangalia nyimbo za muziki wa kizazi kipya kwa kigezo cha lugha hasa lugha ya kingereza. 2.2Pengo linalopaswa kuzibwa. Ukiyatalii maandiko hayo utaona kuwa hakuna aliyezungumzia suala la nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ,wachache wamejaribu kuelezea kidogo suala hili kwa kuchunguza vipengele vya fani vinavyopatikana katika nyimbo hizo hata hivyo waliotupia jicho suala hili halikuwa lengo lao bali limejitokeza katika mchakato wa kutiririsha mawazo yao.kwa kufanya hivyo tunakosa muwala mawazo.Aidha imebainika kuwa kipengele hiki kina epwa na wahakiki na watafiti wengi wa kazi za fasihi,watafiti wa lugha ya Kiswahili ambao uamua kufanya utafiti wa jumla wa fani na maudhui kutokana na upungufu huo niamua kufanya utafiti ili kubaini mambo yanayojitokeza katika katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya, katika lugha ya Kiswahili kwa kuangalia nafasi yake katika muziki wa kizazi kipya.Hatimaye kutathimini kufaa na kutofaa kwa muziki wa kizazi kipya kwa wakati uliopita/uliopo na ujao.


SURA YA PILI :
2.0 MAPITIO YA MAANDIKO.
Sura hii inabainisha machapisho mbalimbali yanayohusiana  na mada hii,machapisho hayo yatahusu maandiko mbalimbali ya muziki wa kizazi kipya na lugha .Baadhi ya waandishi wameelezea muziki wa kizazi kipya kwa kuelezea maudhui na fani.Kwa ujumla kupitia kazi hizo muziki wa kizazi kipya umeonekana kuwa lenga zaidi vijana kutokana na lugha inayotumika katika nyimbo hizo.Muziki wa kizazi kipya umeonwa kama chombo kinacho wasaidia vijana kuelezea matatizo yao kwa kutumia lugha wanayoielewa wenyewe.

2.1 MAANDIKO KUHUSU MUZIKI WA KIZAZI KIPYA.
Waandishi mbalimbali pamoja na wasanii wameuelezea muziki wa kizazi kipya jinsi ulivyoanza na mtazamo wao kuhusu uelekeo wa muziki huu hapo baadaye. Machapisho kuhusu wataalamu wanasema nini juu ya muziki wa kizazi kipya.
Hapa tutawaangalia(Chachage,2002;Mgembe,1998;Fenn&Perulla,2000;Senkoro2003;)

Majembe(1998),anasema
uchanganyaji wa lugha ndiyo sifa kubwa inayojitokeza katika nyimbo hizi
 kwasababu wasanii wengi huchanganya lugha tofauti ilikuonyesha ubunifu
 tofauti na wasanii wengine na kupelekea watu wazima kuona nyimbo hizo ni
uhuni”.

Senkoro(2003),katika maandishi yake ya sanaa anasema :
wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatumia lugha kama bidhaa
ambayo wameizalisha baada ya kujiajiri wenyewe.Ingawa nyimbo
hizi zina mchanganyiko wa kiingereza, Kiswahili na lugha za kienyeji
nyimbo hizi zinatumia sana misimu sababu ndiyo inayoeleweka kwa vijana”.

Chachage(2002) anasema :
Watanzania wengi wanadhani muziki wa kizazi kipya unapotosha
utamaduni wa mtanzania hawa ni wapotofu wa mawazo.kwani utamaduni
katika jamii ni mwingiliano wa mambo mengi toka ndani na n’je ya nchi
Chachage yupo sahihi lakini hata kama tunaiga utamaduni kutoka n’je haipaswi tuvuke mipaka ya utamaduni wa nchi yetu na lugha yetu..

Fenn na perulla(2000)
“matumizi haya ya uchanganyaji lugha yanatokana na itikadi ambayo
 imejengeka miongoni mwa wasanii hao na pia kwa lengo la kupata
 mashabiki wengi.Wanatumia kingereza sababu ni lugha ya kimataifa,
wanatumia Kiswahili kwasababu ni inayoeleweka kwa watumiaji wengi.”

 Senkoro,Majembe na fenn Perulla wameangalia nyimbo za muziki wa kizazi kipya kwa kigezo cha lugha hasa lugha ya kingereza.

2.2Pengo linalopaswa kuzibwa.
Ukiyatalii  maandiko  hayo utaona kuwa hakuna aliyezungumzia  suala la nafasi ya lugha ya Kiswahili katika muziki wa kizazi kipya ,wachache wamejaribu kuelezea kidogo suala hili kwa kuchunguza vipengele vya fani vinavyopatikana katika nyimbo hizo hata hivyo waliotupia jicho suala  hili halikuwa lengo lao bali limejitokeza katika mchakato wa kutiririsha  mawazo yao.kwa kufanya hivyo tunakosa muwala mawazo.Aidha imebainika kuwa kipengele hiki kina epwa na wahakiki na watafiti wengi wa kazi za fasihi,watafiti wa lugha ya Kiswahili ambao uamua kufanya utafiti wa jumla  wa fani na maudhui kutokana na upungufu huo niamua kufanya utafiti ili kubaini mambo yanayojitokeza katika katika nyimbo za muziki wa kizazi kipya, katika lugha ya Kiswahili kwa kuangalia nafasi yake katika muziki wa kizazi kipya.Hatimaye kutathimini kufaa na kutofaa kwa muziki wa kizazi kipya kwa wakati uliopita/uliopo na ujao.
>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>
Powered by Blogger.