Faida Za Machungwa


Machungwa ni matunda maarufu sana sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania. Ni jamii ya matunda aina ya citrus, na yanapatikana kwa wingi na urahisi sehemu mbalimbali hapa nchini. Jamii hii ya matunda inajumuisha machungwa, machenza, tangarine, klementine  n.k.
Virutubisho Vinavyopatikana Kwenye Machungwa.
Machungwa yana mkusanyiko wa virutubisho vingi; Wanga, Protini kwa kiasi kidogo, Vitamini (A, B1,B2,B3,B5,B6,B9, C, E) madini (Kalsiam,Chuma, Zinki,Potasiam) na kambakamba (roughage/fibers).
Machungwa ni chanzo kikubwa na kizuri cha Vitamini C katika mlo. Chungwa la ukubwa wa wastani lina miligramu 50 za Vitamini C, na kwa kawaida mahitaji kwa siku ya Vitamini C ni miligramu 90 kwa mwanaume na miligramu 75 kwa mwanamke. Hivyo chungwa moja au mawili kwa siku yanaweza kutosheleza mahitaji hayo.

machungwa na juisi ya chungwa
Machungwa yanaweza kuliwa kama tunda zima au kwa kunywa juisi ya machungwa. Juisi ya machungwa huwa na virutubisho vyote vya machungwa isipokuwa kambakamba (roughage/fibers), ambazo zipo kwa wingi zaidi  mtu napokula chungwa zima.
Nile machungwa mangapi kwa siku?
Inashauriwa kula chungwa moja au mawili kwa siku, kwani hii hutosheleza mahitaji ya Vitamin C na madini mengine mwilini. Ulaji wa machungwa mengi sana(zaidi ya 50) kwa siku unaweza kusababisha kujaa Vitamini C (hypervitaminosis) ambako ni hatari kwa afya.
Faida za Machungwa:

  • Huimarisha Kinga ya Mwili.
Vitamini C pamoja na madini mengine ikiwemo Zinki, yanatumika kwenye ufanyaji kazi wa mfumo wa kinga ya mwili.
  • Hupunguza Hatari ya Magonjwa ya Moyo na Saratani.
Machungwa yana kampaundi ziitwazo phytochemicals kama hesperedin, ambazo hulinda mishipa ya damu na kupunguza lehemu (cholesterol) kwenye damu.Vitamini C pia iliyopo kwenye machungwa huondoa sumu za mwili (free radicals), ambazo huchangia kutokea kwa saratani na magonjwa ya moyo zinapokuwa zimelundikana mwilini.
  • Huimarisha afya ya fizi na mdomo.
Vitamini C husaidia kujenga protini za kolajeni za fizi za mdomoni, hii huimarisha afya ya fizi. Ukosefu wa Vitamini C mara nyingi huambatana na fizi kuvuja damu kutokana na kukosa protini za kolajeni za kutosha.
  • Hupunguza lehemu(cholesterol) mwilini.
Machungwa yana kambakamba laini (soluble fibers) ambazo huyeyuka kwenye chakula. Hizi husaidia kunyonya mafuta ya lehemu(cholesterol) yaliyo kwenye chakula na kutolewa nje ya mwili kama choo. Hii hupunguza mafuta ya lehemu(cholesterol) kwenye mwili wa mtu.
  • Kuona vizuri.
Machungwa yana Vitamini A ambayao inasaidia kuhakikisha macho yanaona vizuri, pamoja na kamapundi nyingine ambazo hulinda tishu za macho zisiharibiwe na mwanga.
  • Hupunguza hatari ya kukosa choo/kupata choo kigumu (constipation).
Machungwa hasa pale mtu anapokula chungwa zima, humpatia kambakamba ambazo husaidia kulainisha chakula kwenye utumbo na kukifanya choo kuwa laini.
  • Huimarisha afya ya ngozi.
Madini yaliyopo kwenye machungwa pamoja na Vitamini A na C husaidia kujenga na kuondoa seli za ngozi zilizokufa.
Fanya machungwa kuwa sehemu ya mlo wako kila siku ufaidike na kazi zake

USHAURI WETU KWAKO.

Changamoto nyingi za magonjwa zinatokana na ukosefu wa lishe bora, ni changamoto kubwa sana katika jamii zetu ndiyo maana magonjwa mengi ambayo yalikua ya watu wachache miaka 20 iliyopita sasa yamekua ni kwa mpaka watoto wadogo. Mfano: Ugonjwa wa kisukari au kansa ilikua ni kwa watu wazima lakini leo tumeona mpaka watoto wadogo wa miaka miwili au mitatu wanapata ugonjwaa huu!
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilifanya utafiti nakutambua kwamba tunahitaji jumla ya virutubisho tisini (90) kila siku, ilikuwa na afya bora na kuepukana na maradhi mbali mbali. Kutokana na sababu hii ya ukosefu wa virutubisho ndio maanamagonjwa mengi ambayo huanzia kwenye ngazi ya seli (damu) ambayo husababisha magonjwa kama kansa, kiharusi, Kisukari, Osteoporosis, Fibroid (vimbe) na kadhalika.
MAISHA TUNAYOISHI SASA YANAVYOCHANGIA UHITAJI KUTUMIA LISHE STAHIKI.


Watu wengi bado wanahoji umuhimu wa kutumia virutubisho wakati wote. Hapa kuna sababu chache za kuzingatia Kuongeza mlo wako na virutubisho:
1. Mbinu za kilimo za kilimo za kisasa zinaondosha udongo madini muhimu katika udongo na kusababisha chakula kukua Katika udongo huu bila kuwa na madini muhimu ambayo hutengeneza virutubishi katika mimea na kutumia mbolea kuvikuza
2. Vyakula vingi vinatumwa umbali mrefu na kuhifadhiwa kwa muda mrefu, wote ambao husababisha Kupungua kwa vitamini katika vyakula hivi, ikiwa ni pamoja na kama Vitamin B complex na vitamin C

3. Usindikaji wa chakula, kupikia, na kuhifadhi kunaongoza Kupungua kwa virutubisho katika usambazaji wetu wa chakula ambao hufanya vigumu kupata lishe ya kutosha kutoka vyakula peke yake

4. Matunda na mboga nyingi huzalishwa Kuboresha muonekano wake wan je na sio lishe inayopatikana katika tunda au mboga hiyo, ambayo husababisha kukosa ladha/ubora kuliko matunda au mboga zilizopatikana zamani enzi za baba zetu.

5. Kuna muda maalumu katika maisha na hali ya afya inaweza kusababisha kuwa hitaji la juu la kirutubisho fulani. Kwa mfano, folic acid huwa hitaji la juu wakati wa ujauzito, wakati Wanawake wa menopausal wanaweza kuwa katika hatari ya kalsiamu Upungufu.

6. Kuongezeka kwa viwango vya uchafuzi wa mazingira katika hewa yetu, Maji na chakula vinaweza kusababisha miili yetu kutumia Zaidi Virutubisho kuliko kawaida ya kuzuia na kuondokana na hatari Vitu. Hii ni kweli hasa kwa antioxidant Vitamini, ambazo zinajumuisha: "Vitamini vya ACE:" Vitamini A, C, na E.

7. Sisi sote tuna udhaifu wa maumbile (genetically), ambalo hupelekea hitaji la juu Mahitaji ya virutubisho vingine au viwango vya juu vya kupungua kwa Virutubisho fulani, na uwezekano mkubwa wa maumbile huleta baadhi ya magonjwa kama upungufu wa vitamini au madini.

LISHE YA TREVO SAHIHI KWA AFYA YAKO.
Trevo ni lishe yenye viungo 174 vya asilia vinavyopatikana katoka pembe zote nne za dunia, ambavyo ndani yake kuna matunda, mboga mboga, mimea na madini asilia vyote vimechanganya katika bidhaa moja kukupa lishe kamili. Trevo imetengenezwa fomula ambayo hufanya rahisi mwili kufyonza kwa urahisi kwenda Moja kwa moja kwenye damu na kuanza kutumika.
Trevo inamjumuisho wa vitu virutubisho vifuatavyo: • 13 vitamins muhimu • 14 madini mbali mbali • 24 matunda mbali mbali • 18 mboga mboga za majini na nchi kavu • 25 mitishamba • 5 green superfoods • Essential fatty acids • 20 amino acids • Marine grade coral calcium complex (1,000 mg)
Utakapotumia Trevo itakusaidia:
• afya ya utoaji sumu mwilini ( Ini na Figo)
• Afya ya mifupa na maungio
• shinikizo la damu afya
• afya ya mfumo wa kinga
• usimamizi wa uzito
• afya za seli za damu
• afya ya macho
• afya ya moyo
• mtazamo wa akili & utambuzi
• afya ya mfumo wa tumbo
• afya ya mfumo wa neva
Powered by Blogger.