HISTORIA YA RIWAYA NA MAWAZO YA WATAALAMU


Ijapokuwa muundo wa masimulizi ulichangia kwa kiasi fulani katika riwarya nyingi za mwanzo, ni vyema kufahamu kwamba uhusiano kati ya historia ya riwaya ya Kiswahili na kipera cha fasihi andishi ya Kiswahili si wa kimuundo bali uhusiano huu zaidi uliotokana na uandishi wa hadithi za Kiswahili.
Kwa mujibu wa Mlacha na Madumulla,(1991:11), mwanzo wa historia ya riwaya ya Kiswahili yamkini unaweza kuangaziwa kuanzia wakati Edward Steere alipokusanya na kuhariri hadithi alizozipata kutoka kwa wakazi wa Zanzibar.
Kulingana na wataalam hawa, historia ya utanzu wa riwaya ulimwenguni haina muda mrefu sana hasa inapolinganishwa na historia ya tanzu nyinginezo za fasihi kama vile ushairi, tamthiliya ya fasihi simulizi.
Hata hivyo, kulingana na Mlacha na Madumulla, (1997:11), historia ya riwaya ya Kiswahili haikupishana sana na hali hiyo ya kutanguliwa na tanzu nyinginezo za fasihi.).
Historia ya riwaya ya Kiswahili imeangaziwa katika sura tofauti na wataalamu na watafiti mbalimbali.
TUKI, (2004:48), jinsi tulivyoeleza hapo awali, maana ya chimbuko ni mwanzo au asili, ambapo tanzu za asili yamkini ndizo zilizochangia kwa kiasi kikubwa sana katika kuibua riwaya za Kiswahili.
Mitazamo ya wataalamu
Wataalam na watafiti mbalimbali wa Kiswahili wameeleza mawazo yao anuai kuhusu historia ya riwaya ya Kiswahili.
Tunaweza kuainisha mawazo ya wataalam hawa kwa njia mbili jinsi ifuatavyo;
1. Wataalamu walioangazia historia ya riwaya ya Kiswahili pamoja na historia ya fasihi ya Kiswahili
Kwa mujibu wa Mlacha na Madumulla(1991:8) hawa wanajumuisha wataalam kama vile Rollins, 1993
2. Wataalamu ambao wameangazia au wamegusia kuhusu uandishi wa hadithi au ukipenda riwaya za Kiswahili
Kulingana na Mlacha (1991:8), wataalam hawa ni kama vile Balisidya (1976), Senkora (1977), 1989), Ohly (1981), na wengineo.
3. Wataalam wanaoangazia historia ya riwaya ya Kiswahili kuanzia mwishoni mwa karne ya kumi na tisa (19)
Mlacha na Madumulla (1991:1) wanawataja wataalam hawa kama vile Rajmund Ohly (1981), na wenzake katika kipindi cha mwaka 1870 ambapo Edward Steere alikusanya simulizi kutoka kwa wenyeji wa Zanzibar na kisha kuzihariri. Hadithi hizi zilikusanywa kupitia lugha ya kiasili na kutafsiriwa kisha kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Wataalamu hawa wanaiangalia historia ya riwaya kuanzia kwenye chanzo chake na vilevile kuanzia kwenye hatua za mwanzo katika maendeleo yake (Mlacha na Madumulla, 1991:8)
4. Wataalamu wengine wanaoangazia historia ya riwaya ya Kiswahili kuanzia kipindi cha robo ya kwanza ya Karne ya 20
Huu ni wakati ambapo vitabu kama vile, Mwaka katika Minyororo (Mary Sehoza, 1921), viliandikwa. Hoja hii vilevile inapigiwa debe na mtaalam Senkroro (1976).
Kwa mujibu wa Mlacha na Madumulla 1991:8, wataalam hawa walichangia hoja hiyo wakiwa wametanguliza kitabu cha James Mbotela (1934), cha Uhuru wa watumwa kuwa ndicho kilichoweza kuchukuliwa kama mwanzo wa historia ya riwaya ya Kiswahili.
Senkoro, (1976:75), anasema kuwa riwaya ya Kiswahili ilianza hasa katika kipindi hiki wakati James Mbotela alipoandika uhuru wa watumwa.
Hii ndiyo iliyokuwa riwaya ya kwanza ya Kiswahili na ambayo ilihusisha mandhari ya hukuhuku Afrika Mashariki.Wahusika vilevile walikuwa waswahili, na mandhari yake yaliwahusu waswahili kwa jumla ambapo mwandishi pia alikuwa mswahili.
5. Wataalamu wanaodai kuwa historia ya riwaya ya Kiswahili ilianzishwa na Shaaban Robert.
Hawa wanajumuisha wataalam kama vile Elena Bertoricini (1983:85), Shegov (1976), na Rollins (1983).
Hawa Rollins, (1983), Shegov, (1976) na Elena Bertoncini (1983:85), wanaichukulia historia ya riwaya ya Kiswahili katika hatua yake ya juu kimaendeleo na kuacha pengo kubwa ambalo ndilo hasa lililoweka msingi wa kukua kwa riwaya ya Kiswahili (Mlacha na Madumulla, 1991:9).
Baadhi ya wachanganuzi hata hivyo wana mtazamo kwamba historia ya riwaya ilianza kuanzia karne ya kumi na nane kipindi ambacho Edward Steer alipokuwa anakusanya hadithi fupifupi kwa wenyeji wa Zanzibar kwani hapa ndio ilikuwa hatua ya awali ya kuijua na kuiandika riwaya ya Kiswahili.
Powered by Blogger.