SWALI 1: Unadhani katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia rejista bado zina umuhimu wowote? JIBU:

SWALI 1: Unadhani katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia rejista bado zina umuhimu wowote? JIBU:

Rejista (pia rejesta au sajili) ni matumizi ya lugha kulingana na muktadha maalum. Miktadha tofauti husababisha aina mbalimbali za lugha. Baadhi ya vipengele vya miktadha hiyo ni mada, eneo la matumizi ya lugha, mahusiano baina ya wahusika, umri, jinsia, wakati, na kadhalika. KIINI Rejesta zina umuhimu mkubwa sana katika lugha hasa kulingana na maendeleo yanayoikumba lugha kimatumizi. Umuhimu wa rejesta ni kama ufuatao Rejesta hutumika Kama Kitambulisho Rejesta hutofautisha mtindo wa lugha miongoni mwa wazungumzaji. Rejestainawatambulisha wazungumzaji kuwa wao ni kundi fulani. Mfano: Rejesta yawahunzi inawatambulisha kuwa wao ni tofauti na wavuvi ambao nao pia wanarejesta yao. Rejesta ya kanisani au msikitini ni tofauti na rejesta ya jeshini, n.k. (ii) Rejesta hupunguza Ukali wa Maneno Rejesta inapotumiwa na kundi la watu, huficha jambo hilo linalozungumziwalisieleweke kwa wengi. Hivyo hadhira inapuuzwa kwa sababu siyo watu wengiwanaoelewa. (iii) Rejesta Inatumika Ili Kurahisisha Mawasiliano Rejesta inatumika ili kurahisisha mawasiliano au kupunguza muda wakuwashughulikia watu au wateja wengi. Kwa mfano mganga anayegawa dawahospitalini anaposema “mbili asubuhi, mchana na jioni” akiwa na maana kuwamgonjwa anywe vidonge viwili asubuhi, viwili mchana na viwili jioni. Hapaamefupisha ili aweze kuwahudumia kwa wakati mfupi wagonjwa wengiwanaosubiri kupata dawa. (iv) Rejesta hupamba Lugha Miongoni mwa Wazungumzaji Kwa mfano, Rejesta ya Hotelini. Mhudumu: Nani wali kuku?Mteja: Mimi hapa!Mhudumu: Nani ugali-ng’ombe?Mteja: Mimi hapa!
Mazungumzo haya kati ya mhudumu na mteja licha ya kurahisishamawasiliano, vilevile yanapamba mazungumzo hayo. (v) Rejesta huweza Kuwa Kiungo cha Ukuzaji wa Lugha Kutokana na matumizi ya rejesta mbalimbali, lugha inayohusika inawezakuunda msamiati wake. Kuna baadhi ya maneno ya lugha yanayotokana narejesta mbalimbali.
HITIMISHO Ukuaji wa lugha ya Kiswahili hutegemea sana usanifishaji wa maneno yanayotumika katika jamii na kupata mashiko.
Powered by Blogger.