MICHAKATO YA KIMOFOLOJIA INAVYOTUMIKA KUUNDA MANENO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
MICHAKATO YA KIMOFOLOJIA
INAVYOTUMIKA KUUNDA MANENO KATIKA LUGHA YA KISWAHILI.
Mofolojia
ni taaluma inayoshughulikia vipashio vya lugha na mpangilio wake katika uundaji
wa maneno. Vipashio hivyo vya lugha huitwa mofimu (Rubanza, 1996).
Mofolojia
ni tawi la taaluma ya isimu ambalo huchunguza maumbo ya maneno na hususani:
maumbo ya mofimu. (Mathews, 1974)
Hartman
(1972) anasema kuwa mofolojia ni tawi la sarufi ambalo hushughuliia na
uchunguzi na uchambuzi wa maumbo, fani na aina zao maneno yalivyo sasa pamoja
na histori zao.
Mofolojia
huchunguza mofimu na alomofu zake fulani na jinsi ambavyo hukaa pamoja kuunda
maneno mbalimbali katika lugha zinamotumika (Richard na wenzake 1985).
Kwa
ujumla, mofolojia ni tawi la isimu ambalo huchunguza maneno ya lugha fulani na
aina zake za maneno hasa upande wa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa
ajili ya kuunda maneno. Pia wana taalamu mbalimbali wamefasili maana ya maneno
kwa mitazamo mabalimbali kama ifuatavyo.
Tuki,
(1970) Neno ni mkusanyiko wa sauti ambazo huweza kutamukika na kuandikwa kwa
pamoja na kuleta maana.
Massamba
na wenzake (2003) wanafasi neno kwa kutafasili maelezo ya Lynos (1968:194- 208)
kuwa neno linawez kufafanuliwa katika misingi ya kiumbo sauti yaani kwa
kuchunguza sauti zinazounda umbo zima, kiontografia kwa kuchunguza herufi
zinazotumika katika kuliandaka umbo lake, kisarufi kwa kuchunguza kile
kinachowakilishwa na umbo husika katika lugha.
Katika
lugha ya Kiswahili, maumbo ya kimatamshi na ya kimaandishi huweza kuwakilisha
umbo moja au maumbo kadhaa ya kisarufi. Mfano, katika lugha ya
Kiswahili kuna umbo la Kimaandishi kaa. Kisarufi umbo hili linawakilisha maumbo
matatu yenye maana tofauti kama ifuatavyo.
Kaa-
tendo la kuketi kitako
Kaa-
aina ya samaki
Kaa-
kipande cha ukuni chenye moto au kilichochomwa.
Kwa
ujumla, neno ni sehemu ya lugha yenye kituo kidogo mbele na nyuma yake, au kwa
maandishi ni jumla ya herufi zenye maana zilizotengwa kwa nafsi nyuma na mbele.
Maneno
katika lugha ya Kiswahili huweza kuundwa kupitia michakato mbalimbali kama vile
kimofolojia, na kifonolojia, kwa kutumia mchakato wa kimofolojia, neno huweza
kuundwa kupita kanuni mbalimbali kama vile, udondoshaji, uyeyushaji, Muungano
wa sauti, nazali kuathiri konsonanti, konsonanti kuathiri nazali, Ukaakaishaji,
usilimishaji au usilimisho na mchato wa msinyao.
Katika
mchakato wa udondoshaji, kiambishi awali m- ambacho huonekana katika umbo la
nje la maneno kama mu- tu, mu- gonjwa, mu – kanda. Katika kanuni au mchakato
huu wa undoshaji. Irabu “u” hudondoshwa pale inapofuatiwa na konsonanti halisi
katika mpaka wa mofimu. Mfano.
Mu+
tu= mtu
Mu+
gonjwa= mgonjwa
Mu+
kanda= mkanda
Mu
+ guu = mguu
>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>>>