MITAZAMO (NADHARIA) MBALIMBALI JUU YA SANAA ZA MAONYESHO
Kabla hatujaanza
kujadili mitazamo hii ni vema tukajua kwanza dhana ya sanaa, kwamba tunaposema
sanaa tunamaanisha nini.
Sanaa ni uzuri unaojitokeza katika umbo lililosanifiwa, umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisi zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalum. Kuna aina kuu tatu za sanaa. Kwanza ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. Hizi ni sanaa za uonyesho. Nazo ni kama vile uchoraji, uchongaji, ufinyanzi, kutarizi n.k. sanaa amabazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo zilizotariziwa, vyungu n.k.
Aina ya pili ya sanaa ni sanaa za ghibu. Hizi ni sanaa ambazo uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali katika umbo linalogusa hisia. Mifano ni kama vile usahiri, uimbaji, upigaji muziki n.k. uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.
Aina ya
tatu ya sanaa ni sanaa za vitendo. Uzuri wa sanaa za aina hii
umo katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama
vitendo vikifanyika. Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa mwanasanaa na mtazamaji
wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja ama sivyo sanaa haikamiliki. Hali hii
ndiyo iliyosababisha sanaa hizi za vitendo kuitwa sanaa za maonyesho, kwa
sababu lazima wakati zinapotendeka awepo mtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake
umo katika vitendo vyenyewe.
Kwa hiyo
sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni:
i. Dhana
inayotendeka
ii. Mtendaji
iii. Uwanja
wa kutendea
iv. Watazamaji
Sasa baada
ya kuagalia dhana ya sanaa za maonyesho, sasa tuangalie nadharia zinazojaribu
kuelezea sanaa za maonyesho. Nadharia hizi zipo tatu ambazo ni:
1. Sanaa za maonyesho ni michezo ya kuigiza, ama ni michezo inayoonyeshwa
kwenye jukwaa lenye pazia na mataa mengi ya jadi au ni michezo ya Shakespeare. Huu ni mtazamo mmoja wapo ambapo baadhi ya wataalamu
wanaamini hiyo, kwamba sanaa za maonesho lazima zichezwe jukwaani, kuwepo na
pazia na mataa mengi.