Sifa 10 Zitakazokufanya Kuwa Kiongozi Bora

Je kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wengi au miaka mingi katika uongozi? La hasha, kiongozi bora hujengwa kwa sifa anuwai.
Ni rahisi kufikiri kuwa kiongozi bora hutokea kwa bahati tu au hakuna haja ya kujifunza jinsi ya kuwa kiongozi bora. Wewe kama mtu anayehitaji kusimamia na kuratibu shughuli mbalimbali ni lazima ufahamu sifa zinazomfanya mtu kuwa kiongozi bora ili uwe na mafaniko.
“Kama matendo yako yanawahamasisha wengine kupata ndoto zaidi, kujifunza zaidi, kufanya na kuwa zaidi, wewe ni kiongozi.”
John Quincy Adams
Katika makala hii utaweza kufahamu sifa 10 zitakazokufanya kuwa kiongozi bora.

1. Uwazi

Uwazi ni sifa muhimu inayomfanya mtu kuwa kiongozi bora. Kiongozi bora ni lazima awe wazi katika utendaji kazi wake.
Uwapo kiongozi kuna siri za kazi lakini namna ya utendaji kazi hautakiwi uwe siri au usioeleweka kwa wale unaowaongoza. Kiongozi bora anatakiwa kuwa na mpangilio mzuri na unaoeleweka wa utendaji kazi wake.

2. Maono

“Kiongozi ni yule anayejua njia, anakwenda njia hiyo na anaonyesha njia.”
John C. Maxwell
Maono ni picha inayojengeka katika fikira ya matokeo ya jambo ambalo linapangwa kutekelezwa.
Kama wewe ni kiongozi asiyeweza kuona picha ya baadaye ya kampuni au taasisi hutawea kuiongoza kampuni kufikia mafaniko na malengo yake. Jitahidi kujifunza kuwa na maono katika jambo lolote unalolifanya ili lifanikiwe.

3. Uadilifu

Ili uwe kiongozi bora huna budi kuwa mwadilifu. Heshimu kazi, tunza muda, tunza fedha pia tumia nafasi yako kwa njia amabyo si ya kibadhirifu.
Ni rahisi mtu kushawishika kutumia ofisi au nafasi ya kiuongozi kwa maslahi binafsi jambo ambalo linamfanya kupoteza sifa yake ya kiongozo bora.

4. Ujasiri

Huwezi kuwa kiongozi bora kama hutakuwa na ujasiri katika maswala mbalimbali. Unahitaji ujasiri kufanya maamuzi mbalimbali katika eneo au taasisi unayoiongoza kama vile kufanya uwekezaji mpya, kubadili mfumo wa utendaji kampuni au taasisi n.k.
Lazima kiongozi aoneshe ujasiri kwa watawaliwa au wafanyakazi wengine katika maamuzi yake anayoyafanya kila siku.

5. Subira

Kuna mambo yanayohitaji subira katika maisha. Kiongozi asiye bora hutaka kila kitu kitimie kwa siku moja. Kuwa kiongozi mkomavu ni kuwa subira na uvumilivu.
Wakati mweingine kampuni au taasisi yako inaweza kuwa inapita kwenye kipindi kigumu; usipokuwa kiongozi mwenye subira unaweza kufanya maamuzi ambayo yataathiri kampuni daima.

6. Mbunifu

“Ubunifu unatofautisha kati ya kiongozi na mfuasi.”
Steve Jobs
Kufankiwa kwa kampuni au taasisi kunahitaji ubunifu wa hali ya juu kila mara. Hivyo basi ili uweze kuwa kiongozi bora jitahidi kuwa mbunifu.
Buni mbinu, mawazo na miradi mbalimbali ambayo itawezesha kampuni au taasisi kukua na kufikia malengo yake.
Epuka kutegemea mawazo ya zamani hata kama bado yanailetea kampuni faida kwani mambo yanaweza kubadilika wakati wowote
Powered by Blogger.