Misamiati 20 ya Kiswahili Unayoitumia Kimakosa

Uongozi ni dhamana; tena ni nafasi ya kipekee inayopaswa kutumiwa vyema. Tuna viongozi wengi katika jamii yetu lakini siyo wote ni viongozi bora.
Baadhi hutumia uongozi kama silaha, chanzo cha kipato au hata kichaka cha kuficha maovu. Kwa hakika kila kiongozi anatakiwa kujitambua na kupata maarifa stahiki ya uongozi. Ikiwa unapenda kuongeza maarifa yako au unataka kufahamu zaidi kuhusu uongozi; basi karibu nikufahamishe nukuu 30 za uongozi.
  1. “Kiongozi ni yule anayefahamu njia, anakwenda kwenye njia hiyo, na anaonyesha njia.”
    John C. Maxwell
  2. “Pasipo na maono, hakuna tumaini.”
    George Washington Carver
  3. “Ubora wa kiongozi unadhihirishwa na viwango alivyojiwekea yeye mwenyewe.”
    Ray Kroc
  4. “Siogopi jeshi la simba linaloongozwa na kondoo; Ninaogopa jeshi la kondoo linaloongozwa na simba.”
    Alexander the Great
  5. “Usitafute kosa, bali tafuta suluhisho.”
    Henry Ford
  6. “Ubunifu unatofautisha kati ya kiongozi na mfuasi.”
    Steve Jobs
  7. “Kujimudu wewe mwenyewe, tumia kichwa chako, kumudu wengine, tumia moyo wako.”
    Eleanor Roosevelt
  8. “Kiongozi mashuhuri siyo yule anayefanya vitu vikubwa sana. Bali ni yule anayewawezesha watu kufanya vitu vikubwa sana.”
    Ronald Reagan
  9. “Usiwaambie watu jinsi ya kufanya vitu, bali waambie ni nini cha kufanya na waache wakushangaze kwa matokeo yake.”
    George Patton
  10. “Uongozi ni sanaa ya kumfanya mtu mwingine afanye unachohitaji kifanyike kwa sababu mtu huyo anahitaji kukifanya.”
    Dwight D. Eisenhower
  11. “Usimamizi ni kufanya kwa usahihi; uongozi ni kufanya vitu sahihi.”
    Peter F. Drucker
  12. “Kuwa mfano siyo kitu kikuu cha kuwahamasisha wengine; bali ni kitu pekee.”
    Albert Schweitzer
  13. “Siwezi kumwamini mtu asiyeweza kujitawala yeye mwenyewe atawale wengine.”
    Robert E. Lee
  14. “Sanaa ya uongozi ni kusema hapana, sio ndiyo. Ni rahisi sana kusema ndiyo.”
    Tony Blair
  15. “Uongozi ni tendo na siyo nafasi.”
    Donald McGannon
  16. “Kiongozi huwafikisha watu pale ambapo wasingefika wao wenyewe.”
    Hans Finzel
  17. “Kuwa aina ya kiongozi ambaye watu watamfuata kwa hiari, hatakama huna cheo au nafasi.”
    Brian Tracy
  18. “Mtu mashuhuri huvutia watu mashuhuri na anafahamu jinsi ya kuwashikamanisha pamoja.”
    Johann Wolfgang von Goethe
  19. “Yeye ambaye hajawahi kujifunza kutii hawezi kuwa muamrishaji mzuri.”
    Aristotle
  20. “Uongozi ni ushawishi.”
    John C. Maxwell
  21. “Ufunguo wa uongozi wenye mafanikio leo ni ushawishi, siyo mamlaka.”
    Kenneth Blanchard
  22. “Viongozi hufikiri na kuzungumzia suluhisho. Wafuasi hufikiri na kuzungumzia matatizo.”
    Brian Tracy
  23. “Tunapotazama karne mpya, viongozi watakuwa wale wanaowawezesha wengine.”
    Bill Gates
  24. “Elimu ni mama wa uongozi.”
    Wendell Willkie
  25. “Viongozi bora hawatambuliki kwa kukosa madhaifu, bali kwa kuwa na nguvu dhahiri.”
    John Zenger
  26. “Uongozi na kujifunza ni muhimu kwa kila kimoja.”
    John F. Kennedy
  27. “Unachofanya kina matokeo makubwa kuliko unachosema.”
    Stephen Covey
  28. “Uongozi ni kuufanya uwezo wa watu kuwa bora.”
    Bill Bradley
  29. “Uongozi ni ufunguo wa asilimia 99 ya jitihada zote za mafanikio.”
    Erskine Bowles
  30. “Mtu anayetaka kuongoza bendi ya mziki ni lazima awageuzie mgongo watazamaji.”
    Max Lucado
Powered by Blogger.