NADHARIA KATIKA SEMANTIKI
NADHARIA KATIKA SEMANTIKI
Kutokana na ugumu wa kufasili maana ya maana katika taaluma ya semantiki ambayo ni tawi la isimu ambalo hujihusisha na uchunguzi wa lugha katika maana hususani maana ya msingi, taaluma hii hushughulikia maana za maneno na sentensi katika lugha mahususi na maana hizo hushughulikiwa kisayansi.
Maana katika semantiki ilianzakushughulikiwa tangu enzi za Plato, Aristotle, wataalamu mbalimbali walishughulikia falsafa, mantiki, saikolojia, isimu na Athropolojia. Kila taaluma ilitofautiana, kulikuwa na tofauti ya isimu na taaluma nyingine. Tofauti ya isimu na taaluma nyingine ni kwamba isimu iliangalia maana kisayansi na usayansi huo ulikuwa wa kiupangilifu, kiuakinifu kwa kutumia kanuni mbalimbali, ingawa walitumia kanuni bado kulikuwa na matatizo mbalimbali.
Swali
Kwa nini bado kulikuwa na matatizo ya kufasili maana ya maana?
Jibu: maana ilichukuliwa kama kitu ambacho akijatengamaa na kilikuwa tepetepe ama telezi kwani huwezi kukishika, kinateleza. Mfano maji huchukuliwa katika kikombe na maana hasa hutegemea sana uwezo na ufafanuzi wa msemaji kwa mantiki hiyo maana hufananishwa na kinyonga, maana hutegemea muktadha wa mzungumzaji. Wanahisimu wanaona kuwa maana ni kitu muhimu katika mawasiliano na maana inapokuwa tege mawasiliano huwa si kamili na hakika mawasiliano bila maana si kitu. Kwa maana hiyo maana ni muhimu sana katika mawasiliano kwani kuna kuwa na kitu ambacho mzungumzaji amekusudia kukisema.
Maana ya maana
Habwe na Karanja (2007), wanasema neno maana lina fahiwa nyingi watu wa kawaida wamelitumia kumaanisha vitu mbalimbali.
Mfano i/ una maana gani kufika umechelewa?,
ii/ yale mawingu meusi yana maana mvua itanyesha sasa,
iii/ mtu huyu hana maana yoyote,
iv/ manyunyu ina maana, mvua inayonyesha kidogokidogo,
v/ kuna joto,
vi/ kicheko katika mashetani kina maana gani?,
vii/ Aota maana yake ni mshipa mkubwa utokao moyoni na kupeleka damu sehemu za mwili,
viii/ msaada wako una maana sana kwetu. Sentensi hizi zina maana mbalimbali kama vile sababu, dalili, ishara, hafai, ufafanuzi, hali, kejeli, umuhimu. Swali katika tungo hizo ni maana ipi inayohusu maana ya msingi katika muktadha wa semantiki. Matumizi mapana na hivyo ni tata ili kuweka mipaka ya semantiki ni muhimu kubainisha maana ya maana ya semantiki.
Kutokana na utata wa maana kuliibua nadharia mbalimbali ambazo kwa kiasi fulani zimejikita katika kupunguza utata huo wa kuelezea maana ya maana. Katika mjadala huu nadharia bainishi kama vile urejeleo, nadharia tumizi, taswira/dhana, vichocheo mwitikio, vijenzi semantiki.
UREJELEO
Nadharia hii iliasisiwa na Ogden, C.K na Richards, I. A. Nadharia hii inahusu uhusiano baina ya kiambo cha lugha na kitu au vitu katika ulimwengu wa masilugha. Kwa mtazamo huu maana ya neno ni kitu halisi kinachorejerewa na neno. Maneno ni majina ambayo dhima yake ni kutaja vitu. Maana ya neno ni uhusiano baina ya neno hilo na kitu au vitu ambavyo neno hilo hurejelewa. Kwa mfano, kitabu, simu n.k.
UPUNGUFU
i/ si kilia kiambo au leksimu yenye maana ina kirejerewa chake. Mfano, katika lugha
kuna vinyambo ambavyo havina kirejeleo. Kama vile Mungu, upepo, shetani, (dhana).
ii/ haifanyi kazi kwa maneno yenye uhusiano wa kipolisemia. Kwa mfano Kichwa ni
leksimu yenye kuchanuza maana nyingi.
iii/ Haifanyi kazi kwa maneno yenye uhusiano wa kihomonomia. Kama vile kaa, chunga,
chungu, n.k.
iv/ pia haiwezi kufanya kazi katika maneno yenye uhusiano wa kisinonimia, vinyambo
zaidi ya kimoja (kisawe).
NADHARIA YA DHANA / TASWIRA
Nadharia hii inafafanua kuwa maneno ya kiambo ni dhana au taswira inayoibiliwa na kiambo hicho akilini mwa mwanalugha pindi kiambo hicho kinapotumika.
Neno – kisemo- sentensi, kisemo ni dhana ijengekayo akilini mara tu msemaji au msikilizaji anapozungumza ama kusikiliza, pia nadharia hii uhusisha maana na wazo, uhusisha maana na kitu moja kwa moja hivyo inasaidia kutoa majibu ya vinyambo visivyoweza kurejelewa.
MAPUNGUFU
· Si bainifu na haiwezi kuchunguzika, kutabili chochote, mwanaisimu hawezi kufanya utafiti wa aina moja.
· Picha za akilini ni dhahania ya kutosha kuweza kuwakilisha maana za nomino au vitenzi vya kawaida.
· Hakuna picha za jumla ya mguso.
· Si kila kiambo kinahusiana na taswira.
· Haiwezi kuelezea viambo viwili kuwa ni kisawe. Kinyambo huwa na taswira moja haina visawe.
· Haiwezi kuelezea maana ya sentensi au nahau.
NADHARIA TUMIZI
Nadharia hii iliasisiwa na mwanafalsafa mashuhuri aliyejulikana kwa jina la Ludwing Wittgenstein mwaka 1930, alitamka kwa mifano mingi ya maneno kuwa maana ya
neno ni matumizi yake katika lugha, msisitizo wake upo katika maana ya neno au kisemo kilichotumika katika muktadha maalumu. Mtaalamu huyu anaona kuwa maana ya neno ni matokeo au athari inayotokana na matumizi. Hata hivyo si muhimu kuuliza maana ya neno bali matumizi yake katika muktadha husika.
Nadharia hii imepunguza matatizo katika nadharia tangulizi kwani watoto wanapojifunza lugha hujifunza maana ya viambo vya lugha kutokana na jinsi vinyambo hivyo vinavyotumika na wanalugha wa jamii.
NADHARIA NA MATATIZO
Ø Si kweli kuwa maana ya matumizi ya neno hupatikana katika matumizi ya neno,
Ø Inahalalisha tabia ya mabadiliko ya maana kutokana na muktadha.
Ø Huifanya maana iwe mali ya kundi fulani.
NADHARIA YA VICHOCHEO MWITIKO
Nadharia hii iliasisiwa na mtaalamu ajulikanaye kwa jina la Bloomfield 1933, nadharia hii imejikita hasa katika kuchunguza maana ya umbo la kiisimu na hali ambamo msemaji hutamka umbo hilo na mwitiko huibuliwa na msikilizaji. Maana ni kichocheo cha msemaji na mwitiko wa msikilizaji. Mtaalamu huyu anadai kuwa maana ya kisemo huwa katika muundo wa tendo uneni.
CHOCHEO →MWITIKO………CHOCHEO → MWITIKO
Kasekwa anaumwa njaa, anaona tofaa mtini(hali ya msemaji) anatamka kuwa anataka tofaa (mwitiko wa msemaji)
NJAA ANATAKA
↓ ↓
CHOCHEO MWITIKO
Kapele anachochewa kuitika kwa kuruka ua, anaruka ua anapanda mti anachuma embe na kuliweka mikononi mwa kasekwa.
CHOCHEO → MWITIKO
NJAA → NATAKA
CHAKULA → KUPOKEA
>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>