NADHARIA KATIKA SEMANTIKI

Matatizo ya nadharia
v  Unaweza kueleza maana chache za kisemo cha lugha kwa kuwa hali nyingi za matumizi zimechanganyikana, semo nyingi za lugha hazithibitiwi na kichocheo katika muktadha zitokanamo. Kwa mfano mtu akiulizwa swali si lazima atoe jibu.
v  Maneno mengi hayataji vitu vionekanavyo au nduni zionekanazo , mfano njaa.
v  Wanalugha hawapokei maneno kwa vitu vinavyowakilisha maneno hayo.
v  Maneno dhahania hayaelezeki katika nadharia hii. Mfano njaa.


VIJENZI SEMANTIKI
Hudai kuwa leksimu zote zaweza kuchanganuliwa kwa kuzingatia seti si ukomo ya vijenzi semantiki ambavyo ni jumla. (Crystal, 1969) uchanganuzi wa vijenzi semantiki ni mkabala uanochunguza leksimu tu. Mfano mwanamke, fahiwa ya leksimu hii ina vijenzi vitatu ambavyo kwa hakika ni;
                                            i.            Mtu
                                          ii.            Mtu mzima
                                        iii.            me
                    Ufafanuzi
        i.            MWANAMKE = [+MTU], [+MTU MZIMA], [-ME]
      ii.            MSICHANA = [+MTU], [-MTU MZIMA], [-ME]
    iii.            MWANAMUME = [+MTU], [+MTU MZIMA], [+ME]
Kadhalika vijenzi semantiki huwa na jozi kinzani, jozi hizo huoneshwa kwa alama ya toa na jumlisha. Kijenzi mtu ni cha jimla kinahusisha leksimu hiyo na leksimu kinzani. Leksimu kinzani, mti, majani, vijenzi semantiki vya kijumla kama [MTU], [KITU], [OEVU] n.k. hutumika kupambanua leksimu zilizo katika makundi tofautitofauti ya maana. Dhima kuu ya vijenzi semantiki ni kupambanua leksimu zilizo katika kikoa kimoja cha maana. Kijenzi semantiki [ME] na [MTU MZIMA] tunaweza kufafanua maana za mwanamke, mwanamume, mvulana pamoja na msichana maneno haya ni vikoa vya maneno sawa.
Kwa mfano;

MWANAMKE
a.       MWANAMKE  [- ME], [+MTU MZIMA]
b.      MWANAUME [+ME], [+MTU MZIMA]
c.       MVULANA [+ME], [-MTU MZIMA]
d.      MSICHANA [-ME], [-MTU MZIMA]
     Upambanuzi huu unaonesha kuwa leksimu mwanamke inatofautiana na leksimu mwanamume kwa kutoa [-ME], leksimu msichana inatofautiana na leksimu mvulana kwa kutoa alama [-ME], pia leksimu mvulana inatofautiana na leksimu msichana kwa kujumlisha [+ME]
Mfano undugu wa damu.
Baba
Mama

Shangazi
Mjomba

Kaka
Dada

Mwana
Binti

Mpwa
Binamu

Maneno haya ya udugu wa damu ni tofauti na maneno mengine kwa kuwa yenyewe yanarejelewa kiwakilishi cha msemaji. Maneno hayo yanaweza kuwakilishwa kwa kijenzi kimoja ndugu na ili kukitofautisha ni lazima kiwe na kijenzi kingine.

Kwa mfano
                 [+me], [+mzazi], [mlalo],   [mfuatano]
Baba         [+me], [+mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Mama       [-me], [+mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Shangazi   [-me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Mjomba    [+me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Kaka         [+me], [-mzazi], [+mlalo], [+mfuatano]
Dada         [-me], [-mzazi], [+mlalo], [+mfuatano]
Binti         [-me], [-mzazi], [-mlamlo], [-mfuatano]
Mwana     [+me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Mpwa       [-/+me], [-mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]
Binamu     [-/+me], [mzazi], [-mlalo], [-mfuatano]



ULALO ngazi ya uhusiano wa usawa.
MFUATANO uhusiano wa wima.

Swali muhimu
Jadili ugumu unaojitokeza katika kufasili maana ya maana kwa kuzingatia nadharia za maana.


MAPUNGUFU YA KIJENZI SEMANTIKI
                                i.            Kutokuwepo kwa vijenzi vya uteuzi wa vijenzi, kwa hawajaeleza wazi ni kwanini wanatumia me na ke, kijenzi mlalo, na wima na si vinginevyo. Mzazi na mafuatano. Hivyo ni muhimu kueleza kwanini vigezo hivyo vimetumika.
                              ii.            Mkabala huu unatumia mbinu ya uwili ukinzani ambao unawakilishwa na alama za kujumlisha na kutoa. Unaweza kufaa kwa leksimu ambazo vijenzi vyake vinaweza kubainika kwa urahisi. Lakini pia unweza kufaa Zaidi katika leksimu nyingine kama vile viwakilishi.
                            iii.            Hakuna kikoa cha vijenzi semantiki hivyo hakuna kigezo maalumu kinachoweza kueleza idadi ya vijenzi semantiki.
>>>>>>>MWISHO>>>>>>
Powered by Blogger.