Faida 8 za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka
Kwanini ni muhimu kunywa maji?
Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo.
Ninawezaje kutumia maji kama tiba?
Unaweza kutumia maji kama tiba ya matatizo mbalimbali kwa kufanya haya yafuatayo:
- Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka.
- Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni.
- Kama huwezi kunywa angalau bilauri 4 za maji basi anza na moja kisha ongeza taratibu kadri mwili wako unavyomudu.
Karibu ufahamu faida 8 za msingi za kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka.
