SCIENCE PRACTICALSECONDARYNEWSENTERTAINMENTSHAHADA/UNIVERSITYSCHOLARSHIPSPRIMARY MCHANGO WA BONGO FLAVA KATIKA LUGHA YA KISWAHILI


SURA YA TATU:
3.0 MBINU YA UTAFITI.
Sura hii itaelezea  mpango  mzima wa utafiti kama vile,eneo la utafiti,jamii ya watafiti, zana na mbinu za kukusanya data pamoja na uchambuzi wa data.
3.1Mpango wa utafiti.
Utafiti huu ulikuwa wa uwandani na maktabani .Data zilikusanywa  kutoka kwenye  nyimbo za muziki wa kizazi kipya.Mbinu ya ufafanuzi ndiyo iliyochukua nafasi katika utoaji wa matokeo  ya utafiti huu.Data zote  zimekusanywa zimehakikiwa,kuchambuliwa na hatimaye kutolewa maelezo ya kina ili ziwafikie wasomaji .Nililikwenda uwandani kuwahoji wadau mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya ,watumiaji wa lugha Kiswahili  ili kujua  ni kwa namna gani? Muziki wa kizazi kipyamuziki wa kizazi kipya una mchango gani  katika utamaduni wa lugha ya Kiswahili pamoja na jamii.

3.2. Walengwa wa utafiti.
Walengwa wa utafiti huu ni  jamii ya watafitiwa kwa ujumla wake.
3.2.1 Jamii ya watafitiwa.
Jamii iliyo lengwa kutoa taarifa za utafiti huu ilijumuisha makundi yafuatayo:
         i.            Nyimbo mbalimbali za muziki wa kizazi kipya zimesaidia kuonyesha jinsi lugha Kiswahili ilivyo na nafasi katika muziki huo.

       ii.            Wapenzi ,wasanii na wasikilizaji wa nyimbo za muziki wa kizazi kipya au bongo fleva.

3.2.3Eneo la utafiti.
Utafiti ulifanyika Dodoma Tanzania.Eneo hili lilitosha katika ukusanyaji wa data.Dodoma ni eneo ambalo mtafiti anasoma ilikuwa rahisi kupata maoni kutoka kwa watu ambao ni wapenzi wa muziki na watumiaji wa lugha ya Kiswahili.

3.3 ukusanyaji wa data .
Sehemu hii inafafanua  njia na zana tofautitofauti zilizo tumika katika ukusanyaji data.


3.3.1Zana na  njia za ukusanyaji data.
Zana zilizo tumika ni uhojaji ,daftari na kalamu , mahijiano,na majadiliano ya vikundi pia nilisoma vitabu mbalimbali ambavyo ni vyanzo vya upatikanaji  wa data.Nilitumia zana hizi kutokana na elimu ya walengwa wangu  wa eneo lenyewe la utafiti.
3.3.2Uhojaji.
Nili uulizaji maswali ana kwa ana au kwa njia ya simu na njia ya mtandao(facebook na  barua pepe) ambayo niliwauliza watafitiwa kwa ajili ya kupata na kukusanya data .Nilitumia zana hii katika kukusanya data kutoka kwa watu  wazima na vijana,wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wapenzi wa muziki huu. Uhojaji ulirahisisha upatikanaji wa data mbalimbali zinazohusu muziki huu wa kizazi kipya.

3.3.3 Daftari na kalamu.
Zana hizi zilitumika katika mahojiano na kupitia maandiko mbalimbali,nilitumia zana hizi wakati wa kunukuu data zilizo patikana kutokana na maandiko mbalimbali na mahojiano nilyo fanya kwa ajili ya kutumika  wakati wa uchambuzi na uunganishaji.

3.3.4Mchakato wa ukusanyaji data.
Data za maktabani zilikusanywa kwa kutumia mwongozo wa usomaji ulioandaliwa.Mwongozo huo uliniongoza wakati wa kusoma tasnifu,vitabu,majarida na vielelezo mbalimbali ili kupata data  za utafiti huu.Data za uwandani zilikusanywa kwa kutumia uhojaji.

3.3.5Uchambuzi na uunganishaji wa data.
Uchambuzi wa data za utafiti huu ulitumia mbinu ya ufafanuzi wa maudhui yaliyojitokeza kwenye ukusanyaji wa data za utafiti huu.Mbinu ya ufafanuzi ilitumika zaidi katika utafiti huu kwasababu ilikuwa ya maelezo zaidi na sio takwimu. 
3.3.6Vikwazo vya utafiti.
Mambo yafuatayo yalikuwa kikwazo katika kuyafikia malengo.
         i.            Uhaba wa fedha za kugharamia shughuli mbalimbali kama vile nauli kwenda kwenye maeneo ya kutafuta data ,ukusanyaji wa data pamoja na uunganishaji na uandishi wa ripoti.
       ii.            Muda katika kutafuta data kwasababu ilikuwa ni kipindi cha masomo na sio likizo.kwahiyo ilikuwa vigumu kupata muda wa kutosha katika kukusanya data kwa kina zaidi kutokana na kutumia muda mwingi kwenye masomo  ya darasani.
>>>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>
Powered by Blogger.