MITAZAMO (NADHARIA) MBALIMBALI JUU YA SANAA ZA MAONYESHO

Kwa hiyo basi sanaa za maonyesho za Kiafrika ni dhana zilizo kwenye umbo linalotendeka na siyo mchezo. Kutokana na utamaduni wa Kiafrika tunaweza kusema kuwa: sanaa za maonyesho ni dhana inayotendeka. Na ili dhana hii itendeke anahitajika mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huyu huhutaji uwanja wa kutendea hiyo dhana na wakati akiitenda wanakuwapo watazamaji.   
         2. Sanaa za maonyesho ni vichekeso au ni maigizo yanayochekesha.
Wazo hili linatokana na historia ya sanaa za Maonyesho hapa Tanzania. Wakati mkoloni alipotuletea sanaa ya Maonyesho ya kikwao sisi tulishiriki katika tamthilia za Shakespeare kama washiriki au watazamaji tu. Kwani tamthilia hizi hazikuwa na maana yoyote kwetu kutokana na kuwa zilibeba na ziliongelea utamaduni wa kizungu. Tulifurahishwa na vile vitendo vilivyofanywa kwenye jukwaa katika tamthilia hizi na hivyo vitendo hivi vilituchekesha tu. Basi jambo kubwa kwa Mwafrika ikawa ni vile vichekesho na hivyo kudhani kuwa jambo muhimu katika tamthilia ni kule kuchekesha kwake.

        3.      Sanaa za maonyesho ni maigizo.
Wazo hili limetokana na tafsiri mbovu ya neno play ambalo limetafsiriwa kuwa mchezo wa kuigiza. Inawezekana aliyetafsiri neno hili alifuata nadharia za zamani sana za drama, ambapo ilidhaniwa kuwa uigizaji (imitation) ndio kiini cha drama. Hata hivyo nadharia hii ilitupiliwa mbali kwa vile haikudhihirisha kiini hasa cha drama. Tafsiri hii ndiyo imeleta matatizo hapa Tanzania katika kufahamu sanaa za maonyesho. Wengi wamepotoshwa na wazo kuwa uigizaji ndio kiini cha sanaa za maonyesho kama vile neno michezo ya kuigiza linavyoonyesha. Hivyo, hata katika kutazama sanaa za maonyesho za asili wengi wamekuwa wakitazama iwapo kuna uigizaji. Na hapa wengi wanakwama kwani katika unyago, jando, kusalia miungu n.k hakuna uigizaji bali wanaoshiriki wanashika nafasi fulanifulani. Hivyo ni bora kutumia neno tamthilia pale tunaporejelea neno plays.   

Kwa ujumla kuwepo kwa mitazamo hii huweza kuwa kumesababishwa na mambo yafuatayo: 
Wakoloni kutokutambua ama kwa makusudi ama kwa kutokuelewa kuwa tulikuwa na sanaa za maonyesho za kwetu, hivyo akatuletea drama  
Powered by Blogger.