VYAKULA VYENYE KUONGEZA NGUVU NA HAMU YA TENDO LA NDOA










Tatizo la uwezo wa kufanya tendo
la ndoa linazidi kukua miongoni
wa wanandoa na wapenzi wengi.
Takwimu za kitafiti zinaonyesha
kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10
zenye umri wa miaka 3 na
kuendelea zinakabiliana na tatizo
hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10
wanatajwa kulalamikia upungufu
wa nguvu za kiume na kuacha
idadi ya wanawake
wanaokabiliwa na tatizo hilo kwa
mujibu wa uchunguzi kubaki na
asilimia 13.
Pamoja na matatizo mengine
kutajwa kuchangia upungufu wa
nguvu za kiume na kushuka kwa
msisimko wa tendo miongoni
mwa wanandoa, uchunguzi
umeonesha kuwa utumiaji holela
wa vyakula hasa vyenye mafuta ni
moja kati ya sababu
zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa
masuala ya uhusiano wa
kimapenzi wamebaini aina kumi
ya vyakula ambavyo vina uwezo
wa kumuongezea mtu nguvu ya
kufanya tendo la ndoa.Vyakula
hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa zimetajwa
kuwa na uwezo wa kusaidia
msukumo wa usambazaji damu
mwilini, ambao kwa kiasi
kikubwa ndiyo unaoweza
kumfanya mtu akawa na hisia kali
za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni
vema kwa wale wanaokabiliwa
tatizo la uwezo wa kufanya
mapenzi wakatumia pilipili si kwa
wingi bali kwa kiwango stahili, ili
waamshe hisia zao.Unaweza pia
ukaweka kwenye chai hasa kwa
pilipili mtama , ambayo
hutwangwa na kuwekwa kwenye
chai kirahisi.
PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula
ambacho husaidia kuongeza
uwezo wa mtu kufanya tendo la
ndoa ni Parachichi. Tunda hili
linauwezo mkubwa wa kuzalisha
vitamini E ambayo husaidia katika
uzalishaji wa homoni. Inatajwa
kuwa watu wanaotumia tunda
hili kwa wingi huwana msisimko
mkali wa kimapenzi na kwa
upande wa wanawake husaidia
kuongezamajimaj i yenye
utelezisehemu za siri na hivyo
kuzuia uwezekano wa kuchubuka
wakati wa kujamiiana.
NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa
kufanya vema tendo la ndoa
unatakiwa kuwaza juu ya uimara
wa misuli ya mwili ambayo
inatajwa kuwa ni sehemu kuu na
yenye muhimu katika kujamiiana.
Kwa msingi huo ulaji wa ndizi
mbivu unatajwa kusaidia kujenga
misuli mwilini na kumfanya mtu
aweze kuwa hodari katika tendo
la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza
uchangamfu mwilini na, hivyo
kumuwezesha mtu anayeshiriki
tendo la ndoa kuwa na mguso
sahihi kwenye fikra zake, jambo
litakalomuwezes ha kupokea
hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi
ya mtu ambaye anakwenda
kwenye uwanja wa sita kwa sita
akiwa mchovu wa mawazo.
CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa
baharini huwa na madini ya zink
na chumvi ambayo yanatajwa
kusaidia uzalisha wa vichocheo
vinavyohamasish a msisimko wa
mwili wakati wa tendo la ndoa.
Kwa upande wa pweza ukipata
mchuzi wake (supu ya pweza)
itakuwa ni bora zaidi.
POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda
mekundu yanayofananana na
apple. Haya yatajwa kusaidia
kuamsha mishipa ya fahamu na
kuweka mawasiliano sahihi ya
mwili na hivyo kumuongezea mtu
uwezo kwa kufanya tendo la
ndoa kwa hamasa kubwa.
TANGAWIZI
Ulaji wa tangawizi mbichi nusu
saa kabla ya tendo la ndoa
husaidia katika kuongeza hamu
na nguvu ya tendo la ndoa.
Unaweza ukanywa chai ya
tangawizi tu nusu saa kabla ya
kuanza tendo au unaweza
ukatafuna kipande cha tangawizi
mbichi kwa ukubwa wa dole
gumba la mtu mzima nusu saa
kabla ya tendo .
MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu
mbalimbali za matunda, mfano
Tikiti na Maboga husaidia
kuondoa ACID mwilini na
kumfanya mtu awe ni mwenye
afya njema na kuongeza ufanisi
katika tendo.
VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa
mwili.Mwisho wa aina hizi za
vyakula ni TIKITI MAJI
Ambalo linatajwa kuwa na
virutubisho vingi vyenye uwezo
wa kuusaidia mwili kuwa na
nguvu za kutosha kufanya tendo
la ndoa.
MBOGA ZA MAJANI
Hususani matembele na viungo
vya chai ikiwemo Mchaichai
husaidia sana katika kuimarisha
nguvu za viungo vya uzazi vya
mwanaume na kumpa hamasa na
kumudu katika kufanya tendo la
ndoa .
Powered by Blogger.