ISIMU

Pia wanamofofonemiki walichunguza ubadilishanaji huu wa sauti kwani walishindwa kujua ipi ni alofoni ya fonimu ipi. Ndipo wakagundua kuwa katika mazingira fulani /t/ hubadilika kuwa /s/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i” pia sauti /d/ hubadilika na kuwa /z/ baada ya kufuatwa na mofimu ya unominishaji “i”.
Baada ya kupendekeza umbo kiini maneno haya yakaandikwa kama ifuatavyo: kwa mfano neno {fuaTa} umbo {T} likawa umbo kiini ambalo linawakilisha sauti zote mbili yaani /t/ na /s/, pia neno {piKa} umbo kiini lake ni {K} ambalo linawakilisha sauti /k/ na /ʃ/
Kuchunguza mabadiliko ya sauti yanayotokea mofimu zinapoungana. Kwa mfano; katika lugha ya Kiswahili,
            U + ima         –        wima
            I + etu            –       yetu
            Mu + alimu    –      Mwalimu
            U + imbo      –       wimbo
            Vi + ake        –      vyake
Wanamofofonemiki wakagundua kuwa sauti fulani huweza kuungana na kuunda sauti moja na kubadili umbo la neno.
Chunguza muundo wa kifonolojia wa mofimu katika lugha. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili;
            Mu + huni – Mhuni
            Mu + gonjwa – Mgonjwa
            Mu + guu – Mguu
            Mu + uguzi – Muuguzi
            Mu + tu – Mtu
Wanamofofonemiki wakagundua kwamba mofimu fulani huweza kuungana na mofimu nyingine na kuunda umbo la neno.
Kuchunguza ubadilishanaji wa sauti ambao una una uamilifu wa kimofolojia lakini husababisha mabadiliko fulani ya kifonetiki. Kwa mfano katika lugha ya kiingereza;
            Play + s – [pleiz]
            Dog + s – [dogz]
Since – [sins]
            Else – [els]
            Place – [pleis]
Wanamofofonemiki wakachunguza kinachosababisha kuwepo na maumbo tofauti tofauti ya mofimu ya wingi. Kwa mfano; /s/, /iz/, /z/ Wakagundua kuwa kuna mchakato zaidi ya ule wa kifonolojia ambao ni wa kimofolojia unaosababisha umbo ‘s’ kutamkwa /z/ au /iz/ au /s/ 
MAREJEO:
The New Oxford American Dictionary. (2005), (2ndEdit), Oxford University Press. New York. 

Swali:Kwa kutumia data ifuatayo bainisha mabadiliko ya sauti yaliyosababishwa na mazingira ya kifonolojia pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia. Onesha kwa mifano kutoka katika data jinsi wanamofofonolojia walivyofanikisha kutatua matatizo ya kimofofonolojiaData.


Iba
Wizi
Cheka
Mcheshi
Mguu
Miguu
Nkindiza
Nkindiza
Mkuki
Mkuki
Mvuvi
Mvuvi

Katika kujibu swali hili tumeligawanya katika sehemu tatu. Katika sehemu ya kwanza tumetolea maana ya istilahi mbalimbali kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali. Istilahi hizo ni pamoja na maana ya fonolojia, mofolojia na mofofonolojia, sehemu ya pili tumejadili kiini cha swali ambapo tumeonesha mazingira mbalimbali ya utokeaji wa data tulizopewa na suluhisho la wanamofofonolojia katika kutatua matatizo ya kimofofonolojia na sehemu ya tumehitimisha kazi na kutoa marejeo. 

Kwa kuanza na maana ya istilahi hizo watalaamu wanatueleza kama ifuatavyo;
Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia kama tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binadamu. Hii ina maana kwamba fonolojia kama tawi la isimu hujishughulisha hasa na zile sauti ambazo sauti ambazo hutumika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahususi. 

John Habwe na Peter Karanja (2004) wanaeleza kuwa; fonolojia ni utanzu wa isimu unaochunguza jinsi sauti za lugha zinavyofanya kazi katika lugha mbalimbali. Fonolojia huchunguza jinsi sauti hizo zinavyotumika, zinavyounganishwa na kupangwa katika lugha yoyote mahususi ili kuunda tungo zenye maana. 

Hivyo kutokana na maana za wataalamu hawa tuanaweza kueleza kuwa; fonolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na ufafanuzi wa sauti katika lugha mahususi. Mfano Kiswahili, Kiingereza Kichina, Kijerumani na Kihaya. 

Baada ya kueleza maana ya fonolojia tuangalie maana ya mofolojia kulingana na wanataalamu mbalimbali.
Massamba na wenzake (2004) wanaeleza kuwa; mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa maneno katika lugha. 

John Habwe na Peter Karanja (2004) wanatueleza kuwa; mofolojia ni neno linalotumiwa kumaanisha utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa maneno. Fasili hii inamapungufu kwani katika mofolojia hatushughulikii miundo ya maneno katika lugha bali kinachoshughulikiwa ni maumbo ya maneno. Miundo ya maneno katika taaluma ya isimu inashughulikiwa na tawi na sintaksia.
 

Massamba (2010) akimnukuu Martinet (1965) ambapo Martinet alinukuu kutoka kwa Trubetzkoy (1929) anatueleza kuwa; mofofonolojia kama ilivyotumiwa na Trubetzkoy ilimanisha sehemu ya isimu ambayo ingeweza kutumia mofolojia kuelezea tofauti fulani za kifonolojia ambazo zisingeweza kuelezwa kwa kutumia data za kifonolojia peke yake. 

Baada ya kuangalia maana za istilahi mbalimbali zilizotumika katika swali hili, kifuatacho ni kiini cha swali kinachoonesha mabadiliko ya sauti yaliyotokea katika data tuliyopewa ambayo ni mabadiliko kifonolojia  pekee, kimofolojia pekee na kimofofonolojia. 

Tukianza na mabadiliko ya kifonolojia pekee, haya hutokea kwa namna tofauti au katika mazingira tofauti. Kwa mfano mazingira hayo ni; udondoshaji, uyeyushaji, muungano wa sauti, nazali kuathiri konsonanti na konsonanti kuathiri nazali. 

Hivyo kutokana na data yetu katika kubainisha mazingira ya mabadiliko ya sauti  kifonolojia pekee ni kama ifuatavyo;
                                        Mvuvi     [ ɱ  vuvi ] 

Badiliko lililotokea hapa ni la kifonolojia katika mchakato wa usilimishaji wa nazali yaani konsonanti kuathiri nazali. Hapa tunaona kuwa sauti ya midomo /m/ imesilimishwa na kubadili sehemu yake ya kutamkia na kuchukua sifa ya midomomeno / ɱ / baada ya  kukabiliana na sauti ya midomomeno /v/. Hivyo sauti /m/ imebadilika na kuwa / ɱ  /. 

Katika mabadiliko ya sauti ya sauti ya kitambaza /l/ kubadilika na kuwa kipasuo /d/ pia ni mabadiliko ya kifonolojia hii ni katika neno;

n-limi                            [ ndimi ] 

Utokeaji wake  ni kutokana na kanuni ya nazali kuathiri konsonanti. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti / / inapokabiliana na nazali / / yenye sifa ya kutamkiwa sehemu moja yaani kwenye ufizi hubadilika na kuwa / /.
 

Pia mabadiliko nazali /n/              kipasuo cha kaa laini  [ ŋ ] ni ya kifonolojia ambayo utokeaji wake ni wakiusilimishaji au kanuni ya konsonanti kuathiri nazali. Mazingira ya utokeaji wake ni sauti ya nazali kuathiriwa na konsonanti inayoiandamia hivyo kuifanya nazali kuifuata konsonanti mahali pa kutamkia. Mabadiliko hayo yameathiri sauti ya nazali /n/ na kutamkwa kama nazali ya  kaa laini [ ŋ ]. 

Hivyo katika uwakilishi litakuwa;
Umbo la ndani [ ŋkindiza ]
Umbo la nje  nkindiza.
Baada ya kueleza mabadiliko ya kifonolojia, tutazame mabadiliko ya kimofolojia. Kutokana na data hii tunapata maumbo kama; 
 

Haya ni mabadiliko ya kimofolajia. Mazingira ya utokeaji wake ni mabadiliko ya uongezaji au upachikaji wa  mofimu ya umoja na wingi ambapo; mofimu m- ya umoja imebadilika na kuwa mofimu mi- katika wingi.

 M-guu        umbo la umoja
Mi-guu     umbo la wingi.
 

Pia katika neno mkuki          mkuki, mabadiliko yaliyotokea ni ya kimofolojia tu kwani hakuna mabadiko ya umbo na kinachoonekana ni uwepo wa mofimu m- ya umoja katika umbo hili pamoja na mzizi -kuki. hivyo kilichofanyika ni kuongeza -kuki katika mofimu hiyo ya umoja na kupata neno m-kuki. Hivyo umbo hili linabakia na umbo lake ambalo hubakia kuwa vilevile.

M-kuki                          m-kuki, maumbo yote haya yako katika umoja   

               

Vilevile katika neno M-dalasini                    m-dalasini,  hakuna mabadiliko ya kimofolojia bali umbo limeendelea kuwa vilevile la umoja.
Baada ya kuangalia mabadiliko ya kifonolojia na kimofolojia katika data tulitopewa, kipengele kinachofuatia ni kubainisha mabadiliko ya sauti yaliyotokea kwa mabadiliko ya kimofofonolojia.
Kutokana na data yetu maneno;
Iba                                mwizi
                        Cheka                            mcheshi
 

Hivyo katika mabadiliko iba                  wizi, sauti ya kipasuo cha midomo /b/ kubadilika kuwa sauti ya kikwamizi cha ufizi /z/ imesababishwa na kuwepo kwa irabu /i/ ya unominishaji mwishoni mwa sauti /b/. Kutokana na kitendo cha “kuiba” tungetarajia kupata nomino “mwibi” kutokana na mofimu {mu-ib-i}. Lakini tunapata neno [w-iz-i]. Hapa konsonanti ya kipasuo cha midomo /b/ hudhoofika na kuwa konsonanti ya kikwamizi cha ufizi [ z ] katika mazingira ya kutanguliwa na irabu ya unominishaji /i/.
                     iba    [ w-iz-i ] 

Pia katika neno cheka     mcheshi, mabadiliko yaliyotokea hapa ni ya kimofofonolojia ambapo sauti ya kipasuo cha kaakaa laini /k/ inabadilika na kuwa sauti ya kikwamizi cha kaakaa gumu [ ∫ ] baada ya kufuatiwa na irabu ya unominishaji /i/.
                           Cheka            [ mče∫i ]
Uwepo wa mabadiliko sauti na umbo ambayo hayawezi kuelezwa, kwa mchakato wa fonolojia na  mchakato wa kimofolojia ndipo palipoibuka mchakato wa kimofofonolojia.
Katika utatuzi wao wanamofofonolojia walikuja na dhana ya umbo kiini. Umbo kiini hili liliwakilisha fonimu mbili. Waliteua umbo kiini kwenye neno la msingi. Na liliwekewa mabano mchirizi {  }.
 

Neno la msingi ni “cheka” ambapo waliteua sauti {K} kuwa umbo kiini. Fonimu {K} iliteuliwa kuwakilisha /k/ yenyewe katika neno cheka ambalo ni kitenzi na inawakilisha sauti  [ ∫ ]  kwenye “mcheshi” ambayo ni nomino.                                                                                             [k]
                     {K}
                                                                                              [ ∫ ]
Umbokiini   {K}   linawakilisha sauti  /k/ na [   ∫ ]
Pia katika neno iba na wizi umbokiini ambalo liliteuliwa ni {B} ambayo kuwakilisha sauti /b/ na sauti sauti /z/.
                                                                                              [ b ]
                                                                        {B}
                                                                                             [ z ]
Baada ya utatuzi huu baadhi ya wataalamu  walitoa maoni yao juu ya umbokiini. Baadhi yao ni Linhtner (1970) akinukuliwa na Massamba (2010) anaeleza kuwa umbo kiini sio halisi ni la kidhahania na kinasibu kwani halioneshi mchakato na namna ambavyo sauti na umbo hubadilika na kuwa katika sauti nyingine na kitu gani hasa husababisha mabadiliko hayo ya sauti. Umbokiini huishia tu katika kuteua sauti moja kuwakilisha sauti nyingine. Basi huo ukawa udhaifu wa dhana ya umbokiini.
Hitimisho, kutokana na wanamofofonolojia kushindwa kutatua matatizo ya kifonolojia wakaibuka wanafonolojia zalishi ambao waliokuja na mitazamo mipya katika utatuzi wa matatizo ambayo yalishindwa kutatuliwa na wanamofofonolojia ambapo walikuja na dhana ya misingi na mihimili ya kufuata ili kubainisha mabadiliko yaliyokuwa yanatokea yaliyoshindwa kuelezeka. 
Marejeo.
Habwe, J. na P, Karanja (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers

                                              Ltd.
Massamba, D.P.B. na wenzake (2004) Fonolojia ya Kiswahili Sanifu (FOKISA): Sekondari
                                              na Vyuo. Dar es Salaam. TUKI.
Massamba, D.P.B. (2010) Phonological Theory: History and Development. Dar es Salaam:
                                             TUKI.

Michakato ya kiusilimisho katika fonolojia.

Katika kujadili mada hii tutalenga kuangalia michakato ya kiusilimisho namna inavyotumika katika kuyakokotoa maumbo ya ndani kwenda maumbo ya nje katika lugha ya Kiswahili. Lakini kabla ya kuonesha ukokotozi huo ni vyema kwanza tuangalie maana ya mchakato, maana ya usilimisho, umbo la ndani na nje, kisha tutaelekea kwenye hitimisho pamoja na marejeo.

Tuki (2004) inaeleza kuwa mchakato ni mfululizo wa shughuli unaosababisha kitu fulani kufikiwa.
Hivyo katika uwanja huu wa fonolojia  tunaweza kusema kuwa mchakato utakuwa unafanyika pale ambapo mofimu mbili zinapokutanishwa huweza kutokeza mabadiliko fulani katika mofimu mojawapo au kutotokea badiliko lolote. Mfano viungu hubadilikia kuwa vyungu,kietu hubadilika kuwa chetu hapa tunaona kuwa mabadiliko yametokea lakini miti hubakia kuwa miti, kiti hubakia kuwa kiti na hapa tunaona kuwa hakuna mabadiliko yoyote yaliyotokea.
Massamba (2011) anaeleza kuwa kuna aina mbili za michakato asilia yaani mchakato usilimisho na mchakato sio-usilimisho. Lakini katika mjadala huu tutajikita kwa kuangalia mchakato mmoja tu yaani ule wa kiusilimisho, ambao Massamba anasema muwa usilimisho ni pale ambapo kitamkwa kimoja hufanywa kifananefanane na kitamkwa kilicho jirani yake kwa maana kwamba hupata baadhi ya sifa za kipande sauti chenziye kilicho jirani. Kwa mfano, konsonanti inaweza kupata baadhi ya sifa za irabu au irabu ikapata baadhi ya sifa za konsonanti, na konsonanti moja huweza kuathiri konsonanti nyenziye au irabu moja huweza kuathiri irabu nyenziye. Pia anaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha michakato kadhaa kama vile,unazalishaji wa irabu, utamkiaji pamwe wa nazali, ukaakaishaji, ughunishaji kati irabu, uhafifishaji kati irabu, tangamano la irabu, ughunishaji konsonanti shadda, muungano.
Habwe na Karanja (2004), wanaeleza kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kikamilifu kutokana na kuathiriana. Hapa sauti jirani katika neno huathiriana kiasi kwamba fonimu hupokea ama kupoteza sifa za kifonetiki kwa fonimu jirani, na matokeo yakiwa kuwa fonimu hizi hukabiliana sana katika kufanana. Pia wanaendelea kusema kuwa usilimisho unaweza kuhusisha kuimarika, kodhoofika, kuingizwa, kudondoshwa, au kuungana kwa fonimu katika neno.

Hivyo tunaweza kusema kuwa usilimisho ni kule kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kiukamilifu kutokana na kuathiriana kwake kunakosababishwa na fonimu iliyo jirani.
Baada ya kuangalia utangulizi huo sasa ni wakati wa kukokotoa michakato hiyo ya kiusilimisho kutoka umbo la ndani kwenda la nje.
Lakini kabla ya kukokotoa kwanza tuangalie umbo la ndani kuwa ni namna umbo lenyewe linavyoumbwa na mofimu zake au tunaweza kusema kuwa ni umbo la neno ambalo halijafanyiwa michakato yoyote ya mabadiliko. Na umbo la nje ni lile lililofanyiwa mabadiliko au michakato na mara nyingi huakisi umbo la ndani. Michakato itakayooneshwa ni ile ambayo imeorodheshwa na wataalamu lakini ambayo inahusiana na lugha ya Kiswahili tu kwani mingine inahusiana na lugha zingine kwa mfano michakato ya Massamba ameingiza michakato miwili inayohusiana na lugha za kigeni ambayo ni ughunishaji kati irabu na uhafifishaji kati irabu, hivyo hiyo hatajadiliwa.
Unazalishaji wa irabu
 Massamba (2011) anadai kuwa unazalishaji wa irabu ni aina ya usilimisho ambao irabu hupata sifa ya unazali kutokana na irabu yenyewe kutangamana na konsonanti ambayo ni nazali. Hivyo irabu nyingi hupewa sifa za unazali kutokana na ama kufuatiwa kwa nazali ama kutanguliwa na nazali. Na alama inayowakilisha unazalishaji ni alama ya kiwimbi [ ̴ ] ,zaidi tuangalie mifano ifuatayo.
Mifano

umbo la ndani
umbo la nje
/nondo/
[nondo]
/penya/
[penya]
/mama/
[mama]
/ngambo/
[   ambo]
/nyumba/
[  umba]
/muwa/
[muwa]

   Hivyo sauti zote zilizowekewa alama ya kiwimbi ( ̴ ) zina unazali kwa sababu zimefuatana na nazali na hivyo zimefanywa kuwa unazali.
Kanuni katika Kiswahili
Powered by Blogger.