NGELI ZA NOMINO NA UAINISHAJI WAKE PAMOJA NA DHANNA YA O-REJESHI.
NGELI ZA NOMINO NA UAINISHAJI WAKE PAMOJA NA DHANA YA O-REJESHI.
NGELI ZA NOMINO NA UAINISHAJI WAKE PAMOJA NA DHANNA YA O-REJESHI. Mitazamo mbalimbali inayohusiana na uainishaji wa ngeli za nomino.
A. Kigezo cha kimofolojia/maumbo ya umoja na wingi:
1-mu- 2-wa i) Majina ya viumbe vyenye uhai isipokuwa mimea ii) Majina yanayotokana na vitenzi vinavyotaja watu 3-m- 4-mi i) Majina ya mimea ii) majina ya vitu yanayoanza na m- 5-ji- 6-ma i) Majina yanayoanza na ji- umoja na ma- uwingi. ii) Majina ya kigeni yenye ma- (wingi) iii) Majina yenye kueleza dhanna ya wingi japokuwa hayahesabiki 7-ki- 8-vi- i) Majina ya vitu yanayoanza na ki- (umoja) na (wingi). ii) Majina ya viumbe yanayoambishwa ch- umoja na vy-uwingi
9-N-
10-N i) Majina ambayo huanza na N inayofuatwa na konsonanti, ch-, d-, g-, j-, z-, na y- katika umoja na wingi. ii) Majina yanayoanza na mb-, mv. iii) Majina ya kigeni. 11- U- 12- N Majina yote yanayoanza na u umoja na N-, na mb (wingi) 13- U- 14- Ma Majina yote yanayoanza na u-umoja na ma- wingi. 15-Ku- Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina) 16- PA- Huonesha mahali hasa 17- Mu- Huonesha mahali pa ndani. 18- Ku- Huonesha mahali pa mbali na mahali pakubwa zaidi au hata mahali popote.
Faida ya kigezo cha kimofolojia: • Kigezo hiki kinasaidia kuonesha uhusiano kati ya lugha za kikoa kimoja; na ni mojawapo ya uthibitisho kuwa lugha ya Kiswahili inaingia katika kundi la lugha za kibantu. • Asilimia kubwa ya nomino za Kiswahili zinaonesha maumbo dhahiri ya viambishi ngeli, na tukichukulia kuwa angalau ngeli (10) za kwanza zinajigawa katika jozi za umoja na wingi, inawezekana kabisa kuzigawa nomino katika makundi yake kwa kutumia kigezo hiki cha maumbo. • Husaidia kutambulisha ngeli na pia kuonesha idadi (umoja na wingi) katika nomino za Kiswahili.
Matatizo ya kigezo cha kimofolojia
Kuna nomino ambazo zina kigezo maalum, lakini zinatawanyika katika ngeli tofauti. Baadhi ya nomino huwa na viambishi vya umoja na wingi ambavyo ni tofauti na viambishi vinavyoitambulisha ngeli hiyo Baadhi ya nomino hazina viambishi vyovyote. Ngeli ya PA-MU-KU- inatambulishwa kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi kwa kuwa kuna nomino moja pekee inayopatikana hapa ambayo ni “mahali” na haina viambishi. Ufundishaji wa ngeli kwa kutumia umbo la nomino hauzingatii upatanisho wa kisarufi. Kuna viambishi ambavyo vinafanana/kujirudiarudia. Kutokidhi mahitaji ya sulubu ya sentensi.
B. Kigezo cha kisintaksia /upatanisho wa kisarufi: Huu ni mtazamo wa kisasa wa uainishaji wa ngeli ambao umeyagawa majina katika makundi kulingana na upatanisho wa kisarufi kati ya jina na viambishi awali vilivyo katika vitenzi yaani, vipatanishi. Kwa kigezo hiki wataalamu wameainisha ngeli tisa tu ambazo ni:
1. Ngeli ya:YU/A-WA 2. Ngeli ya :U-I 3. Ngeli ya: LI-YA 4. Ngeli ya KI-VI 5. Ngeli ya I-ZI 6. Ngeli ya U-ZI 7. Ngeli ya U-YA 8. Ngeli ya KU- 9. Ngeli ya PA/MU/KU- Faida za Kigezo cha kisintaksia • Kigezo hiki kilionekana ni bora kwa sababu majina mengi yanahusiana na mengine, na kila jina lina kipatanishi katika kitenzi. • Mwishoni mwa upatanisho wa kisarufi hautatanishi kwa vile kiambishi awali katika kitenzi huwa bayana sana • Majina yasiyo na viambishi mwanzoni, ngeli zake hujulikana kwa urahisi zaidi kwa kutumia upatanisho wa kisarufi kuliko kwa viambishi vya mashina ya majina. • Majina yote huainishwa kwa kuzingatia sifa na hadhi ya kila jina mf. Viumbe hai peke yake.
Udhaifu wa kigezo cha kisintaksia
• Kuna vipatanishi vinavyofanana katika ngeli hizi/kujirudiarudia. • Katika ngeli ya kwanza, kuna vipatanishi viwili vya umoja, YU/A lakini ukweli ni kwamba, matumizi ya kiambishi YU- ni ya kilahaja zaidi Kuliko ya Kiswahili sanifu. • Huyaweka majina ya maumbo tofauti katika ngeli moja. • Yapo baadhi ya maneno ambayo yana utata katika upatanisho mf. Makala,Jambazi
Matumizi ya ngeli
Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kufungamana kutokana na kigezo muhimu. Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi. Hutumika kuleta upatanisho wa kisarufi katika sentensi. Hutumika katika kuonesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
Dhanna ya O-rejeshi: Ni kiambishi kinachotumiwa kurejelea kwenye nomono ambayo huwa imetajwa kabla ya kitenzi chenyewe kutajwa. Viambishi hivyo ndivyo vinavyosababisha utegemezi katika sentensi. Dhima ya muundo wa O-rejeshi
- Hutumika Kama kirejeshi - hudokeza mahali - hudokeza wakati - Hutumika kama kiunganishi - Hudokeza namna
UTANGULIZI WA LUGHA NA ISIMU
Utangulizi wa Lugha na Isimu Malengo ya Jumla ya Somo Madhumuni ya jumla ya somo hili ni kumwelewesha mwanafunzi anayetaka kujifunza masomo ya isimu/Lugha aweze kuielewa vizuri dhanna ya lugha na isimu kwa ujumla. Maarifa ya somo hili ni msingi mkubwa kwa masomo mengine ya isimu katika ngazi hii ya shahada ya mwanzo na ngazi nyengine zilizo juu yake. Kwa kujifunza na kuhitimu kozi ya Utangulizi wa Lugha na isimu mwanafunzi atakuwa tayari amepata maarifa ya awali yanayohusu kozi kadhaa za Kiswahili zilizo chini ya Tawi la Isimu. Kozi hii inaonekana kuwa ndio chanzo na kitangulizi cha kozi za - Historia ya Kiswahili na Lahaja zake, - Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia, -Fonetiki na fonolojia, - Mofolojia ya Kiswahili, -Isimu jamii, -Kunga za Tafsiri na Semantikia na hata Elimu mtindo na Leksikografia ya Kiswahili. Karibu sana ujipatie maarifa haya kwa mustakabali wako katika taalimu ya somo la Kiswahili.