DHANA YA ISIMU NA LUGHA
DHANA YA ISIMU NA LUGHA
Dhanna ya Isimu na Lugha Maana ya Lugha • Lugha ni mfumo wa sauti nasibu zinazotumiwa na watu wa jamii wenye utamaduni unaofanana ili kuwasiliana. • Lugha ni mfumo wa sauti nasibu zenye kubeba maana na zilizokubaliwa na jamii ya watu zitumike katika kuwasiliana. Sifa za Lugha • Lugha ni lazima imuhusu Mwanadamu Kimsingi hakuna kiumbe asiyekuwa mwanadamu (mtu) anaweza kuzungumza Lugha. Lugha ni chombo maalumu wanachokitumia binaadamu kwa lengo la mawasiliano.
• Sauti: Lugha huambatana na sauti za binadamu kutoka kinywani mwake. Binaadamu lazima atamke jambo kwa kutoa sauti zinazotamkwa kwa utaratibu maalumu kutoka kwenye maungo maalumu yaliyomo ndani ya mwili wa mwanadamu, ambayo kiisimu huitwa ala za sauti. • Lugha huzingatia utaratibu maalum; Sauti za lugha yoyote huwa zimepangwa kwa kufuata utaratibu fulani unaokubaliwa na jamii ya watu wanaotumia lugha inayohusika. Kwa maneno mengine, si kila sauti itokayo kinywani mwa mwanadamu kuwa ni lugha. Sauti za vilio vya watoto, hoi hoi na vigelegele vya waliofurahi, vikohozi vya wagonjwa wa pumu na vifua, vicheko, sauti za kupenga kamasi, mbinja na kelele nyenginezo haziwezi kuitwa lugha. Utaratibu huo maalumu unaofuatwa na lugha za wanadamu huitwa sarufi. • Lugha hufuata misingi ya fonimu, Wanaisimu wanakubaliana kwa ujumla kwamba fonimu ni sauti yenye uwezo wa kuleta tofauti katika maana ikipachikwa katika neno la lugha husika. Dhanna ya fonimu inatarajiwa kuzungumziwa kwa kirefu sana katika muhadhara wa saba. Kwa mfano baadhi ya fonimu za Kiswahili ni. /a/, /e/, /i/, /o/, /u/, kama zinavyoweza kubadilisha maana katika maneno yafuatayo:- /tata/~ /teta/~/tita/~/tota/~ /tuta/. /p/, /b/, /t/, /d/, /c/, /k/, /g/, /s/, /z/. kama zinavyoweza kubadili maana katika maneno yafuatayo:- pawa~ bawa~ tawa~ dawa~ chawa~ jawa~ kawa~ sawa~ zawa, n.k • Lugha hufuata mpangilio wa vipashio unaoleta maana; Muundo wa Lugha huwa unafuata mpangilio wa vipashio vyake maalumu na lazima vipashio hivyo vifahamike. Mpangilio wa vipashio huvyo huanza na fonimu, neno (ambalo huundwa kwa mkusanyiko wa silabi au muunganiko wa mofimu mbalimbali), kirai, kishazi na sentensi. • Lugha inajizalisha; Vipashio vinavyoiunda lugha husika huwa na sifa ya kuweza kunyumbulishwa ili kupata maneno mapya. Kwa mfano vitenzi hunyambulishwa kwa kuongezwa viambishi na kwa hivyo, lugha hujiongezea maneno mapya. Kwa mfano tuangalie mifano ifuatayo. i) Chez-a-------ku-chez-a-------ku-m-chez-a-------tu-li-m-chez-a. ii) chez-e-a-------chez-ek-a----------chez-ean-a-------chez-esh-a -----chez-w-a iii) chez-esh-a- chez-esh-an-a- chez-esh-ean-a
• Lugha husharabu; kwa maana ya kwamba huchukua maneno kutoka lugha nyngine ili kujiongezea msamiati wake.Tabia hii inazisaidia sana Lugha zinazokua. Tabia za Lugha
Lugha ina tabia ya kukua; Lugha hukua kadiri inavyoendelea kutumiwa na jamii. Kukua kwa Lugha kuna vigezo kadhaa vinavyozingatiwa. Miongoni mwa vigezo hivyo ni kubadilika na kuongezeka kwa msamiati wa Lugha hiyo. Maneno ya zamani yanabadilika na maneno mapya yanaingia katika Lugha mbalimbali. Hii ni kutokana na mahitaji ya umma au jamii katika harakati mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya ulimwengu kwenye nyanja tofauti tofauti zikiwemo za kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia.Tukichukua mfano wa Lugha ya Kiswahili, tunagundua maneno mengi yameingia kwenye Lugha hii kwa sababu kadhaa. Baadhi ya maneno ambayo sasa hivi yanatumika katika Kiswahili na ambayo miaka kama kumi nyuma hayakuwemo katika Lugha ya Kiswahili ni pamoja na kasheshe, dingi, miundombinu, mikakati, mdau, ngangari na mengine mengi. Kuongezeka kwa watumiaji wa lugha pia ni kigezo kingine kinachoashiria kukua kwa Lugha ambacho kinaenda sambamba na kigezo cha kutanuka na kuongezeka maeneo ambapo lugha hiyo inatumiwa.
Lugha ina tabia ya kuathiri na kukubali kuathiriwa. Lugha inaweza kuathiri na kuathiriwa na Lugha nyingine. Mfano lugha ya Kiswahili imeathiriwa sana na Lugha za Kiarabu, Kiingereza na hata Lugha za Kibantu. Yawezekana pia kwa kiasi fulani ikawa Kiswahili kimeziathiri Lugha hizo. Mfano wa maneno yenye asili ya Kiarabu ambayo yameingia katika Lugha ya Kiswahili ni: kalamu, kitabu, daftari, adhadu, thawabu, dhambi, dhahabu, sababu, aibu, laana, zinaa, dhima, wajibu, mahaba, sakafu, karibu, tafadhali, nafsi, roho, safari, salamu, amali, tabia, sifa, n.k. Mfano wa maneno yenye asili ya Kiingereza yaliyoingia katika Kiswahili ni buku, peni, begi, kabati, rula, buti, bia, springi, stoo, skrubu ,n.k. Mfano wa maneno yenye asili ya Lugha za Kibantu ni pamoja na; ikulu kutoka lugha za Kigogo, Kisukuma na Kinyamwezi, bunge kutoka katika lugha za Kigogo, Kisambaa, Kiha na Kiganda, ugiligili kutoka katika lugha ya Kinyakyusa, Kitivo kutoka katika lugha ya Kipare na Kisambaa, kivunge kutoka katika lugha ya Kipare, unga kutoka katika lugha ya kizigua na misamiati mingine mingi kutoka lugha tofautitofauti za kibantu.
Ubora wa lugha; Lugha zote ni bora. Hakuna lugha iliyo bora zaidi kuliko lugha nyingine. Ubora wa lugha upo kwa wale wanaoitumia.
Kujitosheleza; Kila lugha inajitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii ambayo inatumia lugha yenyewe katika kipindi husika cha maisha yake.
Dhima ya Lugha Ujumi: ujumi ni hali ya kutumia maneno ya lugha fulani kwa ufundi na ustadi wa hali ya juu kwa lengo la kuburudisha na kuwavutia watu wengine. Baadhi ya watu hutumia lugha kwa dhima hiyo, ili wasomaji au wasikilizaji wao wavutike na kuburudishwa na Lugha hiyo. Maeneo yatumikamo lugha yenye ujumi wa kiwango cha juu ni kwenye matangazo na kwenye fani ya utunzi wa mashairi.
Utambuzi: Ni hali ya kufikiria kwa makini, kukokotoa na kutoa majibu ya maswali tofauti ndani ya ubongo. Chombo kikuu kitumikacho kutoa majibu hayo ni lugha. Kutokana na muktadha huo tunaweza kusema kwamba lugha hutumika kama chombo cha utambuzi.
Hisiya: ni fikra za ndani alizonazo mwanadamu. Tunapotaka kuonesha hisiya zetu na vilevile kuwavuta wengine kwa maneno mazito yanayoweza kumtoa msikilizaji machozi ya huzuni au ya furaha tunachagua maneno makali/matamu yenye hisiya.
Kujielezea: Hali ya mtu kudhihirisha mambo mbalimbali aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake. Kwa mfano mtu anaposema nina furaha sana. Hapa mtu anatowa msisitizo wa kuonesha kiwango cha furaha alichonacho, hili linafanyika kwa kutumia lugha. kwa ufupi tunachoweza kusema hapa ni kwamba lugha hutumika kwa ajili ya kujielezea.
Kuamuru: Ni kutoa maelekezo kwa njia ya kuamrisha. Kwa mfano jaji anamuhukumu mshitakiwa kwa kumuamuru ‘Ninakufunga miaka mitatu jela’. Hapa lugha inatenda kazi ya kuamuru.
Kushirikiana: ni hali ya kutenda kitu kwa pamoja au hali ya kuwa na ubiya kwenye jambo. Lugha huwezesha watu kujenga mahusiano ya siri baina ya watu wawili au zaidi na kuweza kujitengenezea njia zao za kuwasiliana pasina wengine kuelewa.
Kuonesha: kumuelekeza mtu kitu kwa njia ya kuashiria. Unapotaka kuonesha jambo ni lazima utumiye lugha kwa njia moja au nyingine.
Matumizi na umuhimu wa Lugha
Kuwasiliana:- Lugha hutumika kupashana habari. Kuunganisha- Lugha hupatanisha na kuleta uelewano miongoni mwa wanajamii. Pia lugha huweza kutofautisha jamii moja na nyingine. Kujenga jamii- lugha huleta/huhimiza shughuli za maendeleo ya jamii, huleta amani na mshikamano katika jamii. Kufundishia- Lugha hutumika katika kufundishia elimu. Kutambulisha- Lugha hutumika kutambulisha jamii ya watu fulani. Kuhifadhi- Lugha ndicho chombo cha kuhifadhi na kueneza utamaduni wa jamii.
Ujuzi wa lugha: umilisi na utendaji.
Je, tunamaanisha nini tunaposema fulani anajua Lugha fulani? Jibu ni kwamba, tunakusudia kusema kwamba mtu huyu: Ana ujuzi wa aina na mpangilio wa sauti za lugha hiyo Ana ujuzi wa maana ya maneno na sentensi za lugha hiyo Ana ujuzi wa sentensi na zisizo sentensi katika lugha hiyo. Ujuzi wa mambo hayo unajulikana kama umilisi wa kisarufi ambao unatofautishwa na hali halisi ya matumizi ya lugha hiyo tuiitayo utendaji wa kisarufi. Ikumbukwe kwamba ujuzi huu hunaswa katika mpango uliokwisha kutayarishwa katika ubongo wetu kuanzia utoto wetu pale tunapoanza kujifunza lugha kutoka kwa mama zetu. Hakuna darasa la wazazi linalotufunza aina za sauti, maana ya sauti hizo na hata namna ya kuzitumia sauti hizo katika muktadha husika. Haya huzuka pengine bila sisi wenyewe kujua tumejifunza lini. Swali hili la ujuzi wa lugha katika ubongo, hushughulikiwa na tawi maalumu la isimu liitwalo isimu- neva ambalo katika kiwango chetu hiki halitashughulikiwa. Lugha asilia na lugha unde. Lugha asilia ni lugha inayotokana na jamii mahsusi ambamo imeibuka na kufungamana kiutendaji na katika utamaduni na maendeleo ya jamii husika. Kwa mfano Kiingereza, Kiswahili, Kichina n.k. Hizi ni lugha asilia zilizoibukia katika jamii hizo. Lugha unde ni lugha ya kubuni isiyotokana na jamii yoyote, ni lugha iliyobuniwa na watu wachache na kuundwa kufuatana na misingi ya lugha asilia na kisha kuenezwa ili itumike kwa mawasiliano baina ya jamii au mataifa tofauti. Kwa mfano: Kiesperanto, Kivolapuk n.k. ni lugha unde ambazo hazitokani na jamii yoyote mahususi. Lugha kompyuta pia ni miongoni mwa lugha unde. Maana ya Isimu Isimu ni uchunguzi wa lugha kisayansi. Ipo taaluma kama falsafa ambayo nayo inaweza kujishughulisha na uchunguzi wa maswala ya lugha lakini si kwa kutumia vigezo vya kisayansi. Wanaisimu huhakikisha kwamba wakati wa kutafiti na hatimaye kuwasilisha matokeo ya utafiti wao wanatumia vigezo vya kisayansi hatua kwa hatua. Kwanza huchunguza na kukusanya data. Halafu wanafanya mlinganisho kabla ya kuunda nadhariya na kuzipima nadhariya na matokeo yake. Baadae hujiundia nadhariya na kutoa kanuni ambazo zinapimika. Uainishaji wa makundi ya Isimu Isimu fafanuzi: ni taaluma ya utambuzi wa vipengele vya lugha au namna gani lugha imepangika. Kozi hii itajishughulisha na kujadili baadhi ya matawi ya Isimu fafanuzi pekee. Ndani ya taaluma hiyo kuna vitawi vidogovidogo ambavyo baadhi yake vitashughulikiwa katika kozi hii nzima. Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya vitawi vya isimu, fasili na tofauti zake. Fonetiki Ni tawi la isimu linaloshughulikia sauti za vitamkwa ikiwa ni pamoja na kuchunguza ala za matamshi, namna ya kutamka, uelewa wa sauti, aina za vitamkwa, kusafiri kwa sauti na jinsi zinavyofasiliwa katika ubongo. fonolojia Ni tawi la isimu linaloshughulikia Uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumiwa katika lugha fulani. Mofolojia Ni tawi la isimu linaloshughulikia uchunguzi wa maneno na aina za maneno. Sintaksia Ni tawi linaloshughulikia uchanganuzi wa mpangilio na uhusiano wa vipashio katika sentensi. Isimu historia Tawi la isimu linalofuatilia mabadiliko katika Lugha kama vile mabadiliko ya sauti,leksika,maumbo ya maneno na hata mabadiliko ya maana Isimu jamii Tawi linaloshughulikia uhusiano uliopo baina ya Lugha na jamii. Isimu Amali Tawi linaloshughulikia uchanganuzi wa Lugha kwa kutegemea maoni ya mtumiaji, hasa uchaguzi wa miundo ya maneno anaoufanya, vikwazo vya kijamii anavyokabiliana navyo katika kutumia lugha na athari za kijamii katika matumizi ya lugha yake. Isimu Neva Tawi linashughulikia ujuzi wa lugha katika ubongo. Isimu Nafsi Tawi la isimu linalochunguza jinsi mtu anavyojifunza lugha kwa kutumia misingi ya kisaikolojia. Isimu Anthoropolojia Tawi linaloshughulikia mahusiano baina ya lugha na utamaduni. Isimu kokotozi Tawi la isimu linaloshughulikia uchanganuzi wa vipengele vya kiisimu kwa kutumia mbinu za ukokotozi.
Chanzo: Kipacha Ahmed (2007).
Isimu matumizi: inajishughulisha na kutumia nadharia, mbinu na maarifa ya kiisimu katika kuelezea matumizi ya lugha, kwa mfano katika kufundisha lugha, kutunga kamusi, kuunda sera za lugha, leksikografia, tafsiri, lugha za matangazo, kimahakama n.k MUHADHARA WA PILI: UHUSIANO WA LUGHA NA JAMII PAMOJA NA TAMADUNI ZA JAMII Lugha na jamii Maana ya lugha: Lugha ni sauti za nasibu zinazotumiwa na watu katika kuwasiliana miongoni mwao. Maana ya jamii: Jamimi ni kundi la watu wanaoishi pamoja na wenye kuhusiana kijamii, kikazi au kiuchumi na wenye kutumia lugha moja kwa ajili ya mawsiliano yao.
Mahusiano ya lugha na jamii:
Lugha imefungamana na jamii kiasi kwamba haiwezi kutenganishwa na jamii na maisha ya mwanaadamu. Lugha ni sehemu ya jamii, kwani jamii haiwezi kuitumia lugha na kisha kuiacha na kuchukuwa lugha nyingine. Lugha ni kielelezo cha mahusiano ya jamii, yaani hueleza jinsi jamii inavyohusiana na mazingira yake halisi na namna wanajamii wanavyohusiana wenyewe kwa wenyewe. Lugha hubadilika kulingana na mabadiliko yanayoikumba jamii. Kutokuwepo uhusiano wa moja kwa moja wa lugha na jamii. Mbali na uhusiano uliopo baina ya jamii na lugha, hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya lugha na jamii kwa sababu Lugha sio lazima iwe ya watu wa jamii ile ile. Mathalani Kiswahili sio lugha ya waswahili peke yao. Watu wanaoishi katika nchi sio lazima wawe wa asili ya nchi hiyo, kwa hivyo jina la jamii haliwezi kuwiana na lugha wanayoongea. Lugha moja huweza kuwa na vilugha kadhaa ndani mwake, mfano lugha kiingereza ina viingereza kadhaa ndani yake, yaani lahaja nyingi mno. Kuna jamii yenye jina tofauti na lugha wanayozungumza, mathalani wamarekani, hawazungumzi kimarekani bali kiingereza.
Lugha na utamaduni- Nadharia ya Sapir – Whorf.
Lugha hutawala namna ya wazungumzaji wake waionavyo dunia. Ukichunguza baadhi ya misamiati ya wana lugha fulani utakuta kuwa yapo maneno pekee yanayowakilisha yale wayaonayo mbele ya macho yao au mazingira yao tu na kutokuwepo kwa neno kuna maanisha kwamba jambo hilo halipo ‘machoni’ pao. Sawa na kusema kuwa ‘lisilokuwepo machoni na moyoni halipo’. Lugha ya mtu hutawala mawazo yake. Dhana tulizonazo huunda kile tukionacho, kutuzunguka na kinachotuhusu. Mfumo wa dhanna ndiyo muhimili wa jinsi tuionavyo dunia yetu ya kila siku. Nida (1986) anasema kuwa, lugha ni kielelezo cha utamaduni wa wazungumzaji wake na sio muhimili wa uoni wao. Lugha hufuata jamii na wala si kuoingoza jamii hiyo. MUHADHARA WA TATU:
VIJILUGHA MBALIMBALI KATIKA LUGHA MOJA PAMOJA NA UMAHIRI KATKA LUGHA.
Vitarafa: ni vilugha ambavyo huzungumzwa na watu wa eneo dogo katika eneo kubwa la watu wanaozungumza lugha moja. Vibinafsi: ni kilugha cha mtu binafsi ambacho humbainisha yeye kwa namna anavyotamka au kuendeleza maneno. Lahaja: Lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi huhesabiwa kuwa lugha moja ispokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani, kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha hiyo inakozungumzwa. Rejista: Rejista ni mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli fulani au inayotumiwa na kundi maalum la kijamii ambayo ni tofauti na lugha ya kawaida. Kitabaka: Hiki ni kilugha cha wazungumzaji wa lugha ambao ni wa tabaka fulani katika jamii ambao hujibagua kulingana na nafasi yao kiuchumi, kisiasa au kielimu, n.k Lugha rasmi: Lugha iliyochaguliwa katika jamii kwa matumizi ya shughuli za kijamii za kila siku. Misimu: Misimu ni maneno yasiyosanifu yazushwayo na kikundi cha watu wachache wenye utamaduni mmoja ili kueleza mahusiano yao kama kikundi au kuhusu jamii kubwa ambamo vikundi hivyo vinaishi katika kipindi fulani cha wakati; na hatimaye maneno hayo hupotea na yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha inayohusika. Umahiri katika Lugha: Ni ujuzi wa hali ya juu alionao mtu katika lugha moja au zaidi katika stadi zote za lugha kama kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika. Mambo yanayomwezesha mtu kuwa mahiri wa lugha. • Kusomea lugha hiyo kwa kiwango cha juu • Kutumia lugha hiyo kwa matumizi ya kila siku. • Kuepuka athari za lugha nyingine katika lugha hiyo. • Kuwakosoa na kuwasahihisha waharibifu wa lugha. • Kuwa karibu na wazungumzaji wa lugha kwa muda mrefu Athari za umahiri:- Umahiri wa lugha wa mzungumzaji huathirika kwenye vipengele vifuatavyo:- • Matamshi • Msamiati • Sarufi/muundo • Maana
Mambo yanayopoteza umahiri wa Lugha • Kutotumia lugha hiyo kwa matumizi ya kila siku. • Kutosomea lugha hiyo kwa kiwango cha juu • Hamahama ya watu • Mfumo wa elimu • Kutokuwa karibu na wajuzi wa lugha. • Kasumba
Vigezo vinavyotumika kupima umahiri wa Lugha
• Kutambua ni sauti zipi zinazotumika kuunda maneno ya lugha yake na mfuatano upi unakubalika na upi haukubaliki. • Kutambua mfuatano sahihi wa vipashio katika maneno au sentensi za lugha yake. • Kutambua tungo ambazo zinavunja/hazivunji kanuni za sarufi ya (upatanisho wa kisarufi). • Kutambua kwa urahisi sentensi ambazo ni tata na pia kutambua jinsi ya kuondoa utata huo. • Kutambua kwa urahisi kusudio la sentensi. MUHADHARA WA NNE:
UCHAMBUZI WA DHANNA YA LAHAJA NA MISIMU
Maana ya Lahaja Maana ya lahaja kwa mtazamo pungufu: Katika mtazamo huu lahaja inafafanuliwa kuwa ni ki-lugha ambacho hakijaandikwa, kisicho na maandishi, na kwa ufupi huchukuliwa kuwa ni lugha pungufu. Huu ni mtazamo wa kimapokeo wenye misingi ya Kigiriki ambao unadunisha lahaja na kuikweza lugha. Maana ya lahaja kwa mtazamo wa kimaelewano: Mtazamo huu unafasiri lahaja kuwa ni lugha yoyote ile iwe imeandikwa au haikuandikwa, unaifafanua lahaja kama sehemu ya kundi- lahaja ambalo linatambulika kama lugha fulani. Sababu za kuzuka kwa Lahaja • Sababu za kijografia • Sababu za kijamii • Sababu za kiuchumi
Aina za lahaja
Lahaja za kijiografia; Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa na tofauti ndogondogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa sababu wanatoka katika maeneo yanayotenganishwa na milima, bahari au mito. Lahaja za kijamii; Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa na tofauti ndogondogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa vile wanatoka katika matabaka, rika, ujuvi, jinsia au itikadi tofauti.
Mgawanyiko wa lahaja za Kiswahili
• Lahaja za kaskazini Kwa mujibu wa Nurse (1982) lahaja za kaskazini ni lahaja za kutoka Somalia hadi kusini mwa Mombasa. Lahaja hizo ni Chimwiini, Kiamu, Kipate, Kisiu, Kivumba, Kimvita na Chifundi. • Lahaja za kusini; Lahaja hizi ni zile zinazoanzia Vumba ya kusini hadi Msumbiji, nazo ni : Kimtang’ata, Kimrima, Kipemba, Kihadimu (Kimakunduchi), kitumbatu, Kiunguja, Kimafia (Kingome), Kimwani na Kiekoti. Maana ya Vizingasifa: Hii ni mistari inayochorwa kuonesha tofauti za matamshi baina ya lahaja moja na nyingine Aina za vizingasifa:
Zipo aina nne za vizinga sifa:
• vizinga sifa msamiati, mfano nyanya Tanzania bara, huitwa tungule kule Tanzania visiwani. • Vizinga sifa mofu, mfano nitakuja kama itamkwavyo kwenye Kiswhili sanifu, hutamkwa kama takuja kama litamkwavyo Pemba au sakuja kama litamkwavyo huko utumbatuni. • Vizingasifa sauti: njia katika Kiswahili sanifu, hutamkwa ndia katika Kimvita. • Vizingasifa maana, mf. Mfereji- bomba.
Uelewano katika lahaja: Uelewano ni hali ya vikundi lugha tofauti vilivyotengana kimasafa hufahamiana baina yao. Kwa mfano wapemba hufahamiana na watumbatu hata kama ni watu wa makundi Lugha tofauti.
Atlasi Lahaja : Atlasi lahaja ni uwekaji wa vielelezo vinavyoonesha matamshi mbalimbali, vipengele mbalimbali vya kisarufi na msamiati wa lugha fulani. Kwa maneno mengine, atlasi lahaja ni mkusanyiko wa ramani na vielelezo vinavyoonesha maneno ya lugha (au lahaja) mbalimbali katika nchi au eneo lahaja jiografia. Vigezo vya kiisimu vinavyotofautisha lahaja. • Kigezo cha kifonolojia • Kigezo cha kimofolojia • Kigezo cha kisemantiki/maana • Kigezo cha kisintaksia Dhima za lahaja • Kusanifisha lugha • Kukuza lugha • Kupamba lugha • Kuongeza msamiati katika lugha rasmi. • Kurahisisha mawasiliano. Dhanna ya misimu Maana ya misimu: Misimu ni maneno yasiyosanifu yazushwayo na kikundi cha watu wachache wenye utamaduni mmoja ili kueleza mahusiano yao kama kikundi au kuhusu jamii kubwa ambamo vikundi hivyo vinaishi katika kipindi fulani cha wakati; na hatimaye maneno hayo hupotea na yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha inayohusika.
Chanzo cha misimu/Sababu za kuzuka kwa misimu::
• Misimu huzuka kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii katika nyakati mbalimbali. • Misimu mingine huzuka kutokana na hali ya utani miongoni mwa watu mbalimbali. • Mara nyingi misimu ya aina hii hubeba kebehi, dhihaka, kejeli, mabezo, dharau au kusifu kusiko kwa kawaida. • Utani miongoni mwa wanajamii • Kutaka mazungumzo yawe siri. • Kudhania matumizi ya misimu ndio ujuzi wa lugha. • Kufanya mambo mazito na ya maana kuwa mepesi na ya kawaida.
Njia zitumikazo kuundia misimu:
• Njia ya kufupisha maneno • Njia ya kutohoa kutoka lugha za kigeni. • Njia ya kutumia sitiari • Njia ya kutumia tanakali • Njia ya kubadili maana ya msingi
Sifa za misimu:
Misimu huzuka na kutoweka. Misimu ni lugha isiyo rasmi. Misimu ni lugha ya mafumbo. Misimu ina chuku nyingi. Misimu ina maana nyingi. Misimu ina mvuto na kwa sababu hii hupendwa na watu wengi. Misimu huhifadhi historia ya jamii. Aina mbalimbali za misimu Kwa kutumia kigezo cha mada. Misimu inayohusiana na pesa Misimu inayohusiana na majina ya vyakula. Misimu ya ulevini Misimu ya nguo Misimu inayohusiana na usafiri Misimu inayohusiana na wana wake
Kwa kutumia kigezo cha kufuatana na makundi ya watu wanaozitumia. Misimu ya wanafunzi Misimu ya wafanyabiashara Misimu ya majangili Misimu ya majambazi Misimu ya wanamichezo Misimu ya walanguzi n.k
Kwa kutumia kigezo cha jumla/kawaida i) Misimu yenye maneno ya kawaida lakini usemi wake unajitokeza yanapotumika katika mazingira maalum. ii) Misimu ya maneno ya kujitokeza tu. a) Misimu ya pekee b) Misimu ya kitarafa c) Misimu zagao
Matumizi ya misimu
Kukuza Lugha kupamba lugha Kufanya mawasiliano yawe mafupi na yanayoeleweka kwa haraka Kuficha lugha ya matusi Kuwaunganisha watu wa makundi (matabaka) mbalimbali Kuhifadhi historia ya jamii. Kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji Kufurahisha na kuchekesha Kukosoa na kuiasa jamii Misimu huleta msamiati wenye matusi Misimu hupunguza hadhira
Matatizo ya kutumia misimu
• Misimu huharibu lugha kwa sababu siyo lugha sanifu • Misimu baadhi ya wakati huleta msamiati weye matusi • Misimu ni lugha ya mafumbo na hufahamika na kikundi kidogo kinachotumia misimu hiyo. • Misimu imetiwa chumvi nyingi kwa hivyo haiaminiki katika jamii • Misimu huzuka na kutoweka • Misimu ina maana nyingi MUHADHARA WA TANO: UCHAMBUZI WA DHANNA YA REJISTA Maana ya rejista; rejista ni mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli fulani au inayotumiwa na kundi maalum la kijamii ambayo ni tofauti na lugha ya kawaida.
Aina ya rejista
Rejista za mitaani:- Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni ambayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kutokana na kikundi cha watu ambacho ni kidogo. Lugha hii hudumu kwa muda mfupi tu, halafu hufifia. Wakati mwingine hukubaliwa na jamii na kuweza kuingizwa katika msamiati wa lugha hiyo. Mazungumzo ya kwenye shughuli maalum (Rejista za mahali): Mazungumzo ya kwenye shughuli maalum hayafanywi kiholela, bali yanafuata taratibu na kanuni maalum zinazojitokeza katika mazingira ya sehemu hiyo. Kutokana na kutumiwa kwake kwa muda mrefu kwenye mazingira ya aina hiyo hiyo. Rejesta zinazohusu watu: Ni yale mawasiliano yasiyo rasmi, ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku yanayoendelea baina ya watu. Lugha ya Kitarafa: Hiki ni Kiswahili cha tarafa fulani, ambacho pindi kikisemwa katika tarafa nyingine huwa ni vigumu kwa watu wa sehemu hiyo kufahamu kisemwacho. Kiswahili Rasmi/Sanifu: Haya ni masawazisho kutokana na vilugha mbalimbali vya Lugha ya Kiswahili. Ni Kiswahili kikubaliwacho na wengi katika nchi na ndicho kitumikacho katika shughuli rasmi za taifa.
Umuhimu wa Rejista:
• Rejista hutumika kama kitambulisho: - Rejista hutofautisha mtindo wa lugha miongoni mwa wazungumzaji. Rejista inawatambulisha wazungumzaji kuwa wao ni wahusika wa kundi fulani. • Rejista hupunguza ukali wa maneno. Rejista inapotumiwa na kundi la watu, huficha jambo fulani linalozungumziwa lisieleweke kwa wengi. Hivyo hadhira inapuuzwa kwa sababu siyo watu wengi wanaoelewa. • Rejista inatumika ili kurahisisha mawasiliano. Rejista inatumika ili kurahisisha mawasiliano au kupunguza muda wa kuwashughulikia watu au wateja wengi. • Rejista hupamba lugha miongoni mwa wazungumzaji. Lugha ya rejesta, kutokana na mtindo wake mara nyingi huonekana kama pambo la Lugha miongoni mwa wazungumzaji wa kundi fulani la jamii inayotumia rejista hiyo. • Rejista huweza kuwa kiungo cha ukuzaji wa Lugha. Kutokana na matumizi ya rejista mbalimbali, lugha inayohusika inaweza kuchukuwa baadhi ya maneno ya rejesta na kujiongezea msamiati wake. Baadhi ya maneno yanayokuwa yakitumika kwenye rejista ya aina fulani yanaweza kuingia na kudumu katika lugha ya kawaida.
Sababu za kuzuka kwa rejista
• Ubinafsi; ni tabia aliyonayo mtu, iwe ya muda au ya kudumu hasa inayohusu namna ya uwasilishaji wa mazungumzo yake. • Maingiliano; Makundi ya watu mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao. • Kupita kwa wakati; Kila mahali katika jamii hujitokeza mtindo wa uzungumzaji katika kipindi maalum kinachoelezea mambo mbalimbali ya wakati huo. • Shughuli iliyopo, hapa hutegemea ni mazingira gani ambapo shughuli hiyo inafanyika. • Tofauti za hadhi za wahusika (uhusiano wa wahusika): Mfano msomi/wasiosoma, mwajiri/mwajiriwa, tajiri/maskini. • Matumizi ya uficho/Tafsida; hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejista kwani husababisha mitindo mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji. MUHADHARA WA SITA : DHANNA YA FONETIKI DHANNA YA FONETIKI Maana ya fonetiki: Ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu zote zinazohusiana na utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa jumla.
Matawi ya fonetik:-
Fonetiki matamshi au fonetiki utamkaji: Tawi hili hujishughulisha na uchunguzi wa sauti namna zinavyotamkwa na mahali ambapo sauti hizo zinatamkiwa, yaani mahali pa matamshi. Fonetiki mawimbi sauti au fonetiki akustika: Hili ni tawi la fonetiki ambalo hujishughulisha na jinsi mawimbi ya sauti ya Lugha yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha msemaji hadi katika sikio la msikilizaji. Fonetiki masikizi au fonetiki sikivu: Kimsingi tawi hili la fonetiki hujishughulisha na jinsi utambuzi wa sauti mbalimbali za Lugha unavyofanywa, na uhusiano uliopo baina ya sikio, neva masikizi (yaani neva zinazohusika na usikiaji wa sauti) na ubongo. Fonetiki-tiba matamshi: Tawi hili hujishughulisha na matatizo yanayoambatana na usemaji au utamkaji wa sauti na jinsi ya kuyatatua Fonetiki kokotozi: Hii ni taaluma ambayo inachambua mawimbi sauti na kuweza kutumia mchoro wa spektogramu kuonesha picha ya sauti katika vipengele vyake vya kasimawimbi. Fonetiki ushawishi: Ni taaluma inayohusiana na kurikodi sauti kwa kutumia kinasa sauti na baadae kuchambua kwa kusikiliza tu. Fonetiki majaribio: Inahusika na uchukuaji wa sauti iliyorikodiwa na kuingizwa katika kompyuta kwa ajili ya kutafuta matokeo ya uchambuzi. Alasauti: Sehemu mbalimbali za maungo ya mwanadamu yatumikayo katika utoaji wa sauti za Lugha huitwa alasauti. Aina za Alasauti Alatuli- ni sehemu au maungo mbalimbali ya binadamu ambayo hayawezi kujongea au kusogea wakati wa utamkaji wa sauti za lugha, mf. ufizi, kaakaa gumu, nyuzi za sauti n.k Alasogezi- Ni zile sehemu au maungo mbalimbali ya binadamu ambayo yana uwezo wa kujongea au kusogeasogea wakati wa utamkaji wa sauti za lugha, kama vile ulimi na midomo. Nyuzi sauti: ni nyama laini mfano wa nyuzi za gita zilizoko katika koromeo ambazo zina uwazi katikati unaoruhusu mkondo wa hewa kutoka nje na ndani ya kifua.
Vitamkwa na uainishaji wake
Maana ya vitamkwa: Vitamkwa ni sauti dhahiri inayosikika wakati wa utamkaji wa maneno, na ambayo huweza kubainishwa kama kitu kimoja ambacho huweza kuwakilishwa kimaandishi kwa kutumia alama zijulikanazo kama herufi za alfabeti.
Aina za vitamkwa ni:
Konsonanti- ni aina ya sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa kutoka mapafuni, ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje. Viyeyusho- ni aina ya vitamkwa ambavyo si konsonanti na wala si irabu; yaani ni vitamkwa ambavyo huchukuliwa kuwa katikati kati ya irabu na konsonanti. Irabu- ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasina kuwepo kizuizi chochote katika mkondo wa hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywa na chemba ya pua.
Sifa bainifu za kifonetiki.
Hizi ni sifa za zinazoweza kuitofautisha sauti moja kutokana na sauti nyingine kwa kutumia vigezo vya kifonetiki. Vigezo vitumikavyo kubainisha konsonanti mbalimbali namna ya kutamka mahali pa kutamkia mkondo wa hewa hali ya glota Namna ya kutamka Kwa kuzingatia kigezo hiki konsonanti zimegawanyika katika makundi kama vile: • Vipasuo: Sauti za vipasuo hutamkwa wakati mkondo wa hewa unapofungiwa kabisa katika sehemu yoyote ya bomba la sauti na kisha kuruhusiwa upite ghafla. • Vikwamizi: Kwa jina lingine vipasuo huitwa vikwaruzo: hizi ni sauti ambazo hutamkwa wakati alasauti zinapokaribiana na kupunguza upenyo wa bomba la sauti kiasi cha kufanya hewa ipite kwa shida na hivyo kusababisha mkwaruzo. • vipasuo kwamizi: hizi ni sauti ambazo hutolewa kwa kuchanganya mzuio wa muda mfupi (kama katika kipasuo) na mzuio nusu unaosababisha ukwamizi. Hizi ni konsonanti ambazo utamkaji wake unahusu mkondohewa kuzuiwa na kuachiwa taratibu kwa kukwamizwakwamizwa. • Nazali:- ni konsonanti ambazo hutamkwa kwa kuruhusu mkondo hewa kupitia puani. • Likwidi/Vilainisho:- Hizi ni sauti ambazo hutamkwa wakati ala za sauti zinapokaribiana na kutatiza hewa kwa namna maalum. Hutamkwa huku hewa ikiendelea kupita. Wanaisimu wamebainisha aina mbili za likwidi, ambazo ni vitambaza na vimadende. Vitambaza hutamkwa wakati ncha ya ulimi ikiwa imekita katika ufizi huku hewa ikiruhusiwa kupita kandokando mwa ulimi. Vimadende hutamkwa wakati ncha ya ulimi ikigotagota kwenye ufizi huku hewa ikiendelea kupita. Mahali pa kutamkia Kwa kuzingatia kigezo hiki konsonanti zimegawanyika katika makundi: • Sifa ya kwanza ni midomo: Mkondo hewa unapozuiwa kwa kubana mdomo wa chini na mdomo wa juu kisha ikaachia au ikabanwa kwa kuviringwa huku ikiwa imeacha upenyo kidogo huwezesha sauti kadhaa hutolewa. • Sifa ya pili ni midomo-meno: Sifa hii inahusu utamkaji wa sauti ambao kwao meno ya juu, ambayo ni alatuli,hugusana na mdomo wa chini, ambao ni alasogezi, na wakati huohuo hewa inaruhusiwa kupita kwa kukwamizwakwamizwa katikati ya meno. • Sifa ya tatu ni ya meno: Sauti hizi hutamkwa kwa ncha ya ulimi ikiwekwa katikati ya meno ya juu na ya chini. • Sifa ya nne ni ya ufizi: Sauti hizi zinapotolewa, ncha ya ulimi hugusana na ufizi. • Sifa ya tano ni ya kaakaa gumu: Sifa hii inahusu utamkaji wa sauti ambapo ulimi hufanya kazi ya ala sogezi. Ulimi hugusana na kaakaa gumu ambalo ndiyo alatuli. • Sifa ya sita ni ya kaakaa laini: Sifa hii huhusu utamkaji wa sauti ambao huandamana na sehemu ya nyuma ya ulimi, ambayo ni alasogezi, kugusa kaakaa laini, ambalo ni alatuli. Mkondo wa hewa; Mkondo hewa kutoka mapafuni waweza kupititia katika chemba ya kinywani au ya puani. Kinachosababisha hali hii ni kilimi. Kilimi chaweza ama kuteremka chini kuelekea shina la ulimi na kuruhusu hewa kupita puani au kuinuliwa juu kuelekea upande wa juu wa ukuta wa koo na kuruhusu hewa kupita kinywani. Sauti inayotamkwa huku mkondo wa hewa ukipita puani huitwa sauti ya nazali. Mfumo huu wa upokeaji wa sauti wakati mkondo wa hewa unapita puani huitwa kuwa ni Ung’ong’o.
Hali ya glota au koromeo; Katika koromeo au glota kuna kitu kinaitwa nyuzi sauti. Nyuzi sauti ni nyama laini zilizoko katika koromeo ambazo zinauwazi katikati unaoruhusu mkondo wa hewa kutoka nje na ndani ya kifua. Nyuzi hizo huwa katika nafasi za aina mbili wakati hewa inapopita. Kuna wakati nyuzi hizo zinakaribiana au kuwa pamoja na wakati mwingine zinakuwa zimeachana. Hewa inapotoka ndani ya mapafu kuja nje kupitia kwenye pango la kinywa au la pua nyuzi hizo zikiwa zimekaribiana au kuwa pamoja, nyuzi hizo husukumwa na kutetemeka.Sauti zinazotolewa wakati huo huwa na mghuno na huitwa sauti ghuna. Zikiwa nyuzi hizi zimeachana, hewa hupita kwa urahisi bila kuzuiliwa, na hivyo hazikwami na kusababisha sauti zinazotolewa kutokuwa na mghuno. Vigezo vitumikavyo kubainisha irabu mbalimbali, irabu hupangwa kutokana na vigezo vitatu: Ulimi uko juu kiasi gani kinywani (ujuu), ni sehemu gani ya ulimi inainuliwa au kushushwa (Umbele), na midomo iko wakati huo katika hali ya (Uviringo). • Ujuu Wakati wa kutamka irabu juu, ulimi unakuwa umeinuliwa juu katika kinywa, ambapo irabu chini hutolewa wakati ulimi umeteremshwa chini. • Umbele • Uviringo; Wakati unainuliwa kinywani, unaweza kupelekwa mbele katika kinywa, na hivyo kutolewa irabu mbele. Ikiwa ulimi utarudishwa nyuma, basi irabu zitolewazo zitakuwa irabu nyuma. Irabu [a] kama ya Kiswahili hutolewa ambapo ulimi hauko mbele au nyuma, bali uko katikati.
Sifa za AKIKI/Msingi wa AKIKI.
• Kuwekwa vigezo vya kuainisha vitamkwa ambavyo ni:- -Jinsi (namna) vitamkwa vinavyotolewa [manner of articulation] na Mahali vitamkwa vinapotolewa [place of articulation] • Kutenganisha vitamkwa katika makundi ya Irabu na konsonanti; kama ndio aina kuu za vitamkwa kwa kutumia vigezo vya jinsi na mahali vinapotamkiwa. • Hudai kuwa kila herufi huwakilisha kipashio kidogo kabisa cha sauti chenye ubainifu, yaani FONI. • Foni huwakilisha jinsi sauti zinavyotamkwa na si jinsi zinvyoandikwa. Foni hizi huorodheshwa katika jedwali la alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa (AKIKI) kwa kuzingatia mahali zinapotamkiwa, na jinsi/namna zinavyotamkwa. MUHADHARA WA SABA : DHANNA YA FONOLOJIA Dhanna ya fonolojia Maana ya fonolojia • Fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binaadamu. • Fonolojia hujishughulisha hasa na zile sauti ambazo hutumika katika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahsusi. • Fonolojia hujihusisha na sheria au kanuni zinazoandamana na utowaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi. Uhusiano na Tofauti kati ya fonetiki na fonolojia Fonetiki na fonolojia zinalingana kwa kuwa, malighafi ya mwanafonolojia huwa ni sauti za lugha ambazo huwa zimeelezwa na kuainishwa na mwanafonetiki. Katika kutumikizwa sauti za Lugha huweza kubadili sifa zake bainifu kutokana na kuathiriana kwa sauti jirani katika neno. Ingawa kuyachunguza haya ni kazi ya mwanafonolojia, lakini sifa bainifu hizi zinazochunguzwa na mwanafonolojia huwa tayari zimeshaelezwa na mwanafonetiki. Kwa ujumla tanzu hizi mbili zinauhusiano wa moja kwa moja kwa vile zote hushughulikia sauti za lugha, lakini katika viwango tofauti. Zote ni taalimu za kiisimu. • Fonetiki ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu na mambo yote yanayohusu utoaji, usikiaji, usafirishaji, na ufasili wa sauti za lugha ya mwanadamu, wakati fonolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi, uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binaadamu. • Kazi kubwa ya fonetiki na mwanafonetiki ni pamoja na kuchunguza jinsi sauti za Lugha zinavyotamkwa, zinavyosafirishwa kati ya kinywa cha mnenaji na sikio la msikilizaji na jinsi zinavyotafsiriwa katika ubongo wa msikilizaji ili kutowa ujumbe wenye maana. Mwana fonetiki pia huchunguza muundo wa mawimbi ya sauti na jinsi yanavyoathiri hewa kwa kuangalia hali ya hewa wakati wa kutoa sauti. Katika harakati hizi mwanafonetiki hutoa sifa mbalimbali za sauti na kuzitambulisha, wakati kazi kubwa ya fonolojia na mwanafonolojia ni kujishughulisha hasa na zile sauti ambazo hutumika katika kutofautisha maana za maneno katika lugha mahsusi. Fonolojia hujihusisha na sheria au kanuni zinazoandamana na utowaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi.
• Matawi ya fonetiki ni:
Fonetiki matamshi au fonetiki utamkaji; Tawi hili hujishughulisha na uchunguzi wa sauti namna zinavyotamkwa na mahali ambapo sauti hizo zinatamkiwa, yaani mahali pa matamshi. Fonetiki mawimbi sauti au fonetiki akustika; Hili ni tawi la fonetiki ambalo hujishughulisha na jinsi mawimbi ya sauti ya Lugha yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha msemaji hadi katika sikio la msikilizaji. Fonetiki masikizi au fonetiki sikivu; Kimsingi tawi hili la fonetiki hujishughulisha na jinsi utambuzi wa sauti mbalimbali za Lugha unavyofanywa, na uhusiano uliopo baina ya sikio, neva masikizi (yaani neva zinazohusika na usikiaji wa sauti) na ubongo. Fonetiki- tiba matamshi; Tawi hili hujishughulisha na matatizo yanayoambatana na usemaji au utamkaji wa sauti na jinsi ya kuyatatua. Fonetiki kokotozi; Hii ni taaluma ambayo inachambua mawimbi sauti na kuweza kutumia mchoro wa spektogramu kuonesha picha ya sauti katika vipengele vyake vya kasimawimbi. Fonetiki ushawishi; Ni taaluma inayohusiana na kurikodi sauti kwa kutumia kinasa sauti na baadae kuchambua kwa kusikiliza tu. Fonetiki majaribio; Inahusika na uchukuwaji wa sauti iliyorikodiwa na kuingizwa katika kompyuta kwa ajili ya kutafuta matokeo ya uchambuzi. Fonolojia kwa upande wake haina matawi maalumu lakini hujishughulisha na vipengele kadhaa vya kifonolojia kama matamshi, kiimbo, mkazo, lafudhi, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti katika kuunda mofimu, mfuatano wa mofimu katika kuunda maneno na otografia.
Kipashio cha msingi kinachotumika katika uchunguzi wa kifonetiki ni foni, na kinafasliwa kuwa ni kiungo kidogo kabisa cha sauti kisichohusishwa na lugha mahsusi, wakati kipashio cha msingi cha kifonolojia kinachotumika katika uchunguzi ni fonimu, na kinafasiliwa kuwa ni kipashio kidogo kabisa cha sauti katika lugha kinachobadili maana ya neno. • Fonetiki ni sayansi huru, kwa sababu tawi hili hutoa nadharia za sayansi halisi kama vile bayojia na nyinginezo na hufaidi matokeo ya kiutafiti ya taaluma hizi, kwa mfano ili kuelewa jinsi ala za sauti zinavyofanya kazi, mwanafonetiki atafaidika na maelezo ya kibayolojia huhusu jinsi mwili wa mwanadamu unavyofanya kazi. • Fonolojia kwa upande wake ni taaluma ya kiisimu ambayo huongozwa na misingi na taratibu za kinadharia za kiisimu. mwanafonetiki si lazima awe mwana isimu. • Mwanafonetiki si lazima awe mwana isimu, wakati mwanafonolojia ni lazima awe mwana isimu. • Fonetiki ni taaluma ya jumla wakati fonolojia zipo nyingi jinsi lugha zilivyo. Kwa mfano tuna fonolojia ya Kiswahili, Kidholuo, Kihehe n.k. • Machine hutumika katika uchunguzi wa kifonetiki, wakati kanuni za kifonolojia hutumika katika uchunguzi wa vipashio vya kifonolojia. Kipashio cha msingi cha kifonolojia (Fonimu) Maana ya fonimu: Fonimu ni kitamkwa cha msingi cha lugha kitumiwacho kujenga maneno yenye maana tofauti au vinavyoweza kubadili maana za maneno. Uainishaji wa fonimu: Fonimu za lugha huainishwa kwa kile kiitwacho na wana isimu kuwa ni jozi mlingano finyu, ambao unafasiliwa kuwa ni utaratibu wa kulinganisha maneno mawili yenye idadi sawa ya sauti lakini yenye tofauti ya sauti moja kwa mtazamo wa neno moja katika jozi inayohusika.
Mitazamo tofauti juu ya dhanna ya fonimu: • Fonimu kama tukio la kisaikolojia • Fonimu kama kipashio cha kifonetiki • Fonimu kama dhanna ya kidhahania yenye utendaji kazi.
MUHADHARA WA NANE : FONOLOJIA ARUDHI Fonolojia Arudhi Maana ya fonolojia arudhi Hizi ni sifa za kimatamshi zinazoambatanishwa kwenye sauti za lugha ya mwanadamu, sifa hizi huitambulisha sauti kimatamshi zaidi na husaidia kubainisha taarifa za msingi kama hali ya msemaji, hisiya za msemaji, umbali, n.k Matamshi: • Kifonolojia matamshi ni utaratibu maalum utumikao katika utoaji wa sauti za maneno ya lugha ya binadamu. Matamshi huhusu lugha za wanadamu peke yake. • Utaratibu wa matamshi ya sauti za lugha huzingatia mambo mawili: Mahali pa matamshi, yaani sehemu katika mkondo wa utamkaji wa sauti mbalimbali ambapo sauti fulani hutamkwa. Jambo la pili ni jinsi ya matamshi yaani namna ambavyo sauti fulani hutolewa. Lafudhi • Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za kimazingira. • Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, au kiwango chake cha elimu
Shadda/mkazo
• Ni utaratibu wa utamkaji wa maneno ambapo silabi fulani hutamkwa kwa nguvu nyingi zaidi kuliko ilivyo katika silabi nyingine za neno hilohilo. • Mkazo unaweza kuchukuliwa kama kilele cha kupanda na kushuka kwa sauti katika utamkaji wa neno. • Silabi yenye mkazo inakuwa na msikiko mzito zaidi kuliko silabi nyingine za neno hilohilo. • Lugha nyingi hasa za kibantu hazitumii mkazo, Lugha nyingi hutumia toni. Kiswahili sanifu hakitumii toni na zaidi hutumia mkazo.
Kidatu: • Kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.: Kiimbo • Ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza katika utamkaji wa lugha fulani. • Katika utaratibu wa utamkaji dhanna ya Kiimbo huandamana pia na dhanna ya kidatu (yaani, kiwango cha juu, cha kati au cha chini cha sauti katika usemaji), Kwa hivyo ni muhimu hapa kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu. Wakati kiimbo kina maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya lugha, kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.
Aina za kiimbo Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida msemaji wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka. Kiimbo cha kuuliza: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa . Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiani sana na kiimbo cha maulizo.Uchunguzi wa kifonetiki, unaonesha kuwa katika kutoa amri, mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko ilivyo katika kiimbo cha maelezo.
Otografia :- Neno otografia lina asili ya kigiriki na maana yake ni utaratibu wa kutumia alama au michoro ya maandishi kuwakilisha sauti zisikikazo katika lugha. • Kila lugha ina mfumo tofauti wa usemaji na hutumia mfumo tofauti wa sauti. • Kila lugha haina budi kubuni mfumo wake wa kuziwakilisha sauti zake katika maandishi. • Mfumo huo wa maandishi ndio ujulikanao kama othografia. • Mfumo huu huwa unawasilisha herufi maalumu zinazobuniwa ili kuwakilisha sauti za lugha inayohusika kimaandishi. Silabi: Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti. Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi funge na silabi huru. Silabi huru ni zile ambazo huishia na irabu na silabi funge ni zile zinazoishia na konsonanti. Silabi za Kiswahili sanifu mara nyingi huangukia katika kundi la silabi huru.
Miundo asilia ya silabi za Kiswahili
• Miundo ya silabi ya irabu peke yake (I). Mf. A katika Anasoma • Miundo ya silabi ya konsonanti na irabu (KI). Mf. Ka, ba, ma • Miundo ya silabi ya nazali pekee (N) Mf. N katika Nta,
M katika Mtoto
• Muundo wa silabi wa konsonanti, konsonanti na irabu (KKI) Mf. Cha, sha, • Muundo wenye konsonanti,konsonanti,kiyeyusho,irabu (KKkI) Mf. Shwa, • Muundo wa konsonanti,kiyeyusho,irabu (KkI) Mf. Kwa, mwa
Muundo wa silabi za Kiswahili sanifu zenye asili ya lugha za kigeni
• Muundo wa silabi wa Konsonanti, konsonanti na irabu (KKI) Mf. Labda, leksika, teknolojia
• Muundo wa silabi wa kosonanti, consonanti, konsonanti na Irabu (KKKI) Mf. Asprini, skrini MUHADHARA WA TISA : DHANNA YA MOFOLOJIA KWA UJUMLA Maana ya mofolojia: Mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na maneno jinsi yanavyoundwa, vipashio vinavyounda maneno hayo na jinsi vipashio hivyo vinavyoainishwa.
Dhanna ya mofu, mofimu na alomofu Mofu: ni kipashio kidogo kabisa ambacho kina uwezo wa kusitiri maana ya neno ambalo kwalo limeundwa. Mofu ni umbo linalowakilsha mofimu katika maandishi. Mofu ni Kipashio cha kiumbo kinachowakilisha mofimu. “Mofu ni umbo lenye kubeba mofimu.”
Aina za mofu kwa kuzingatia kigezo cha maana.
- Mofu huru - Mofu funge na - Mofu tata Aina za mofu kwa kuzingatia kigezo cha mofololojia au maumbo ya mofu. - Mofu changamani/changamano - Mofu kapa Aina za mofu kwa ujumla ni: - Mofu huru - Mofu funge - Mofu tata - Mofu changamani/changamano. - Mofu kapa Mofimu: Kietimolojia ni maana ambayo imesitiriwa/imehifadhiwa /imefichwa nadani ya umbo la mofu Alomofu: ni maumbo mbalimbali ambayo yanasitiri mofimu (maana) ya aina moja. Maumbo tofauti yanayowakilisha mofimu ya aina moja ndiyo yanayoitwa alo-mofu. Kuna aina mbalimbali za alomofu kama vile. • Alomofu zinazowakilisha mofimu ya nafsi • Alomofu zinazowakilisha mofimu ya njeo/wakati • Alomofu zinazowakilisha mofimu ya kutendea • Alomofu zinazowakilisha mofimu ya kutendeka • Alomofu zinazowakilisha mofimu ya usababishi Neno na leksinu Neno: Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa na ambazo huwa na maana (maana yaweza kuwa ni ya kileksika au kisarufi.) Leksinu: Ni kipashio kidogo cha msamiati ambacho kinaweza kusimama peke yake kama kidahizo katika kamusi. Ni neno lenye maana ya kileksika Mzizi na shina Mzizi: ni sehemu ya neno ambayo haibadiliki wakati neno hilo linaponyambuliwa katika hali tofauti. Shina: ni mzizi wa neno uliofungiliwa kiambishi tamati maana. Shina la neno huweza huweza kuwa neno kamili lenye mzizi asilia na kiambishi tamati maana. Mofimu na leksimu Mofimu: ni maana ambayo imesitiriwa/imehifadhiwa /imefichwa nadani ya umbo la mofu Leksimu: Ni kipashio kidogo cha msamiati ambacho kinaweza kusimama peke yake kama kidahizo katika kamusi. Ni neno lenye maana ya kileksika Njia za kuunda Maneno - Uambishaji na Unyambuaji - Uambatishaji - Urudufishaji - Akronimu - Uhulutishaji
MUHADHARA WA KUMI : AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE 1. Nomino Maana ya Nonimo : Nomino ni istilahi inayopewa maneno yanayotaja vitu, hali, mahali au viumbe ili kuviainisha na kuvitofautisha. Aina za nomino: • Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si kingine chochote. Hizi ni nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima, maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomino za pekee huwa kubwa hata kama nomino hiyo inapatikana katikati ya sentensi. • Nomino za kawaida: Hizi kwa jina lingine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi hazibainishi waziwazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni mtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Kelvin, Aisha ama Zawadi. Ikiwa ni ziwa halitambuliwi kama ni Tanganyika, Viktoria au Nyasa, yaani hutaja vitu bila kutaja umahususi wake kama ilivyo katika nomino za pekee. Nomino Hizi zinapoandikwa si lazima zianze kwa herufi kubwa isipokuwa zimetumiwa mwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida, lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee. • Nomino za jamii: Hizi ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja, yaani nimino zinazotaja umla wa vitu vingi. • Nomiono dhahania: Kundi hili hubeba nomino ambazo zipo kwa kudhani tu. Nomino hizi hutaja vitu, viumbe au hali ambazo hazishikiki wala kuonekana. Mf. Mungu, shetani, malaika, upendo, uchoyo, hasira, peponi, n.k • Nomino za kitenzi jina: Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi. Huundwa kwa kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino. • Nomino za wingi: Hizi hutaja vitu katika wingi japo vitajwa havina umoja wala wingi. Mf. Maji, manukato, mapenzi, mawasiliano, n.k
2. Vivumishi Maana ya kivumishi: Vivumishi ni maneno yanayofanya maneno mengine yavume. Vivumishi huvumisha kuhusu sifa, idadi, mahali, n.k kuhusu nomino.
Aina za vivumishi.
• Vivumishi vya sifa: hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi huweza kuwa nzuri, mbaya au yoyote ile. • Vivumishi vya idadi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.
Vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chake kimetajwa. Vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino hizo kiujumlajumla bila kudhihirisha idadi halisi. Vivumishi vya idadi ambavyo huonesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika orodha.
• Vivumishi vya kumiliki:- Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kinamilikiwa na mtu au kitu kingine. • Vivumishi Vioneshi:- vivumishi vya aina hii huonesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii hujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali. • Vivumishi vya kuuliza Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu maswali kama “gani? ipi? ngapi?” • Vivumishi vya pekee: Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu. Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya nomino ambayo kinaivumisha. Mizizi ya vivumishi hivi ni ote, o-ote, -enye, -enyewe, - ingine, -ingineo. –ote. Huonesha ujumla wa kitu au vitu -o-ote Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua” – enye Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino fulani. - enyewe Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani. – ingine Kivumishi cha aina hii huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu fulani – ingineo Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonesha ziadi. • Vivumishi vya A- unganifu Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwa awali. Vivumishi vya aina hii hutumika kuleta dhanna zifuatazo:- -Umilikaji -Nafasi katika orodha • Vivumishi vya jina kwa jina huwa ni nomino zinazotumika kama vivumishi ambazo hutumika kufafanua nomino ingine.
3. Vielezi Maana ya vielezi: Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au vielezi vingine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi, namna gani na hata mara ngapi? Aina za vielezi • Vielezi vya namna au jinsi. Vielezi vya namna hivi huonesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya namna vipo vya aina kadhaa.
Vielezi vya namna halisi. Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa moja katika uainishaji wa aina za maneno. Vielezi vya namna. Hivi ni vielezi ambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-). Viambishi hivi hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano. Ulifanya vizuri kumsaidia mwanangu. -Vielezi vya namna vikariri, hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili. - Vielezi vya namna hali, Hivi ni vieelezi ambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika hali gani. - Vielezi vya namna ala/kitumizi Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo. - Vielezi vya namna viigizi. Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea. Vielezi vya idadi: hivi huonesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasi fulani. Vielezi vya mahali. Vielezi vya namna hii huonesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwa kwa viambishi au kwa maneno kamili. Vielezi vya wakati: Vielezi vya namna hii huonesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea kama maneno kamili au kudokezwa kwa kiambishi {po.}
4. Vitenzi Maana ya vitenzi: Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka. Kitenzi huarifu tendo lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza kutenda jambo.
Muundo wa kitenzi cha Kiswahili
Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye uamilifu wa aina tofauti. Aina za vitenzi Vitenzi halisi: Hivi ni vitenzi ambavyo huonesha kutendeka kwa kitendo.Wakati mwingine vitenzi hivi huitwa vitenzi vya kutenda.
vitenzi elekezi: Hivi ni vitnzi vya ambavyo vinaweza kuchukuwa kitendwa/kitendewa (Yambwa/Yambiwa). Muundo wake unadokeza kuwa, kuna kitendwa au kitu kinachoelezea tendo hilo. vitenzi sielekezi: Hivi ni vitenzi ambavyo havichukuwi kitendwa/kitendewa (Yambwa/Yambiwa). Muundo wake haudokezi uwezekano wa kuwepo kwa yambwa/yambiwa. Tendo halielekezwi kwa yeyote. Aina za vitenzi halisi
Vitenzi vikuu: Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe muhimu wa kiarifu cha sentensi. Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu. Hutoa taarifa kama vile uwezekano, wakati, hali n.k. Vitenzi visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba viambishi vya wakati. Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi vishirikishi ambavyo vilevile sielekezi. Vitenzi hivi hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi.
Aina za vitenzi vishirikishi Vitenzi vishirikishi vipungufu: Hivi ni vitenzi vishirikishi ambavyo havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali. Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni kitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi “si” cha ukanushi. Vitenzi vishirikishi vikamilifu: Hivi huchukuwa viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na hata hali. Kazi za kitenzi kikuu: kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa. kuonesha wakati tendo linapotendeka kuonesha hali ya tendo Kuonesha nafsi kuonesha kauli mbalimbali za tendo Kuonesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea Kazi za kitenzi kishirikishi kushirikisha vipashio vingine katika sentensi Kuonesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu fulani au kitu fullani. Kuonesha cheo au kazi anayofanya mtu. kuonesha sifa za mtu. kuonesha umoja wa vitu au watu kuonesha mahali kuonesha msisitizo kuonesha umilikishi wa kitu chochote. Aina za wakati katika kitenzi. wakati uliopita wakati uliopo wakati ujao
Hali mbalimbali za kitenzi - Hali ya masharti - Hali ya kuendelea kwa tendo - kuamuru na kuhimiza n.k
5. Viwakilishi Maana ya kiwakilishi: kiwakilishi neno linaloweza kutumika badala ya jina. Hutokea nafasi ya nomino pindi nomino inapokosekana.
Aina za viwakilishi Viwakilishi vioneshi/mahali
Mf. Zile,yule,kule,
Viwakilishi vya nafsi ambavyo vipo vya aina tatu; ambavyo ni: viwaakilishi nafsi huru mf. Mimi,sisi,wewe,yeye, viwakilishi nafsi viambata mf. Ni,Tu,U,M,A na Wa viwakilishi nafsi rejeshi mf. Ambaye,ambalo,ambavyo, n.k Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa na mofu/kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina husika. Viwakilishi vya urejeshi ambavyo vinajengwa na shina -amba- pamoja na vipande vidogovidogo kama –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo vinachaguliwa kulingana na ngeli ya majina inayorejeshwa navyo. Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino, idadi hiyo huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla. Viwakilishi vya pekee: Hivi ni aina ya vivumishi ambavyo huwakilisha nomino kwa umaalumu wake. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa. Viwakilishi vya A-unganifu: Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi cha A-unganifu kusimamia nomino inayomilikiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani. kihisishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama mahali pa nomino. Viwakilishi vya sifa; Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika setensi.
6. Viunganishi Maana ya viunganishi. Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi. Dhima ya kiunganishi ni kuunga vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi. Aina za viunganishi: viunganishi huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo, katikati ya vipashio vinavyoungwa. Aina za viunganishi huru
Viunganishi nyongeza/vya kuongeza mf. Tena, Na, Zaidi ya n.k. Viunganishi vya sababu/visababishi Mfano; Kwa kuwa, kwa sababu, kwa vile, kutokana na, n.k. Viunganishi vya uteuzi/chaguo Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k. Viunganishi linganishi/vya kinyume Mfano; Ingawa, Japokuwa, Lakini n.k. Viunganishi vya wakati Mfano; kisha, baadaye, Halafu, Baada ya n.k. Viunganishi vya masharti Mfano; Kama, Ikiwa, Iwapo n.k Viunganishi vihusishi Mfano; Cha, La, Wa, Za n.k.
Viunganishi tegemezi: ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja huunda sentensi changamano au shurtia. Mfano; -ye-, -po-, -ki-, -cho- na -nge-.
7. Vihusishi: Ni maneno ambayo huonesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na lingine. Vihusishi aghalabu huonesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno mengine.
Mambo mbalimbali yanayoweza kuoneshwa na vihusishi huonesha uhusiano wa kiwakati huonesha uhusiano wa mahali huonesha uhusiano wa kulinganisha huonesha uhusiano wa umilikaji huonesha uhusiano wa sababu/kiini Aina za vihusishi vihusishi vya wakati Mfano; kabla ya, baada ya n.k vihusishi vya mahali Mfano; chini ya, juu ya, ndani ya, mbele ya n.k. vihusishi vya ulinganishi/ vya kulinganisha Mfano; kuliko, zaidi ya n.k. vihusishi vya sababu/ kusudi/nia Mfano; kwa sababu ya, kwa ajili ya n.k. vihusishi vya ala (kifaa) Mfano; kwa vihusishi vimilikishi Mfano; cha, za n.k vihusishi vya namna/jinsi/hali Mfano; moto wa kuotea mbali, macho yamviringo vihusishi ‘na’ cha mtenda Matumizi ya ziada ya kihusishi “kwa” kihusishi hiki huonesha mahali au upande kihusishi hiki huonesha sababu au kisababishi cha jambo kihusishi hiki huonesha wakati kihusishi hiki huonesha sehemu fulani ya kitu kikubwa kihusishi hiki hutumika kuonesha ‘nia ya pamoja na’ Kihusishi hiki huonesha jinsi kitendo kilivyotendeka
8. Viingizi/Vihisishi: Ni maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani. Maneno haya huwa na alama ya mguso yatokeapo katika maandishi.
Aina za viingizi: Viingizi vinaweza kugawanywa kwa kutumia vigezo vya kisemantiki. Mkabala huu unatumika kuvigawa viingizi kulingana na maana zinazowakilishwa na viingizi husika. Maana hizo ni hisia zinazobebwa na viingizi hivyo. Viingizi vinavyoonesha mhemko au hisiya kali
viingizi vya furaha viingizi vya huzuni viingizi vya mshituko viingizi vya mshangao
Viingizi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio. viingizi vya maadili
viingizi vya mwitiko viingizi vya ombi viingizi vya bezo viingizi vya kutakia heri viingizi vya kukiri afya/jambo viingizi vya kiapo viingizi vya salamu
MUHADHARA WA KUMI NA MOJA : UAMBISHAJI NA UNYAMBULISHAJI Uambishaji na Unyambulishaji. Maana ya uambishaji: Uambishaji ni ule utaratibu wa kuongeza viambishi katika mzizi wa neno, ili kulipa neno maana ya ziada. Viambishi: Kiambishi ni sehemu (mofu) ambayo huambikwa kwenye mzizi wa neno ili kulipa neno maana ya ziada. Aina ya viambishi: Kwa kuzingatia nafasi kiambishi katika neno
viambishi awali viambishi kati (havipo katika Kiswahili kwa sababu mizizi ya maneno ya Kiswahili huwa haiguswi) viambishi tamati Aina za viambishi kiuamilifu
• Viambishi vya nafsi ya kiima • Viambishi nyambulishi - Vya vitenzi - Vya nomino: • Viambishi vya njeo - viyakinishi - vikanushi • Viambishi vya hali - hali ya masharti - hali timilifu - hali ya kuendelea • Viambishai vya upatanishi wa kisarufi.
Aina za uambishaji Unyambuaji au unyambulishaji: Huu ni aina ya uambishaji unaosababisha neno kubadilika kutoka katagoria moja hadi nyingine. Neno jipya linalotokana na unyambuaji huitwa kinyambuo. Mf. Cheza: mchezo, uchezaji, mchezaji, mchezeshaji, n.k Uambatishi: Ni aina ya uambishaji ambao huhusisha kurefusha neno na kuliweka katika hali tofauti za katagoria ilelie. Viambishi ambatishi ni viambishi vinavyoambishwa kwenye mzizi au viambishi vingine vya neno. Uambishaji huu kwa kawaida haubadili kategoria ya neno wala maana yake.
mf. M-toto - wa-toto m-chezo - mi-chezo ki-roboto – vi-roboto
Viambishi ambatishi m-,mi-,wa-,ki-,vi- havibadili kategoria ya maneno hayo bali huleta dhanna ya umoja na wingi. MUHADHARA WA KUMI NA MBILI: TUNGO ZA KISWAHILI NA UCHAMBUZI WAKE Maana ya tungo: Tungo: Ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake. Ni matokeo ya kuweka pamoja vipashio vidogo sahili vya lugha ili kuunda kipashio kikubwa zaidi.
Aina za tungo:
Tungo neno: Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa na kuandikwa na kuleta maana katika lugha husika. Neno huundwa na mofimu moja au zaidi. Ikiwa ni mofimu huru neno huwa neno huru lakini neno likiundwa na mofimu tegemezi neno huwa changamano (Rejelea aina za maneno hapo juu). Tungo Kirai: ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu. Aina ya kirai hutegemea uhusiano baina ya neno kuu na maneno mengine.
Sifa za Kirai: Hapa tunakusudia kuainisha sifa kuu za viai. Kirai huwa ni kipashio cha kimuundo kisichokamilika; yaani ni kipashio kisichokuwa na muundo wa kiima – kiarifu kama zilivyo sentensi ambazo zinahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa. Kirai huainishwa kimuundo kulingana na neno kuu la kirai husika. Kirai ni tungo, yaani ni aina mojawapo ya tungo, aina nyingine za tungo ni neno, kishazi na sentensi. Kirai hudokeza maana, lakini maana hiyo si kamili. Maneno katika kirai lazima yapangwe kimantiki kwa mpangilio unaokubalika katika sarufi ya lugha husika. Japo virai huainishwa kimuundo, huweza kutumika kutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi. Kirai huweza kutokea upande wowote, wa kiima au kiarifu katika sentensi. Kirai huweza kuwa neno moja au zaidi
Aina za virai Kama tulivyobainisha hapo juu aina za virai hukitwa katika aina za maneno ambazo ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivyo.
Kirai nomino (KN) Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno. Kirai kitenzi (KT) Kirai-kitenzi ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika mahusiano ya Kitenzi na neno au mafungu mengine ya maneno. Hii ina maana kuwa neno kuu katika aina hii ya virai huwa ni kitenzi. Kirai kivumishi (KV) Kirai-kivumishi ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika kivumishi. Kwa kawaida muundo huu huwa ni wa kivumishi na neno au fungu la maneno linaloandamana nacho. Virai vivumishi hutokea ndani ya virai nomino pale ambapo kivumishi kinatokea kumiliki na kutawala kivumishi kingine.
Mf. Mzee mwenye mali nyingi, Watu Wenye watoto wengi
Kirai Kielezi (KE) Tofauti na aina nyingine za virai miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi ) na neno au fungu la maneno linaloandamana nalo. Badala yake miundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo. Kirai kihusishi (KH) Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya kihusishi na maneno mengine hasa nomino. Virai vihusishi japokuwa muundo wake hufanana ila hutofautiana kimaana, zipo maana tatu ambazo ni:-
a) Pahala – kwa baba, katika kabati, kwenye lindo b) Utumizi – Kwa kisu, Kwa mkono c) Uhusika – Na Mjomba, Na Bibi. Tungo kishazi: Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kujitegemea chenyewe.
Sifa za kishazi: Kishazi hupatikana katika/ndani ya sentensi. Lazima kishazi kiwe na kitenzi, sehemu yoyote ya sentensi isiyo na kitenzi, haiwezi kuwa kishazi. Kishazi huru hutawaliwa na kishazi kikuu na kishazi tegemezi hutawaliwa na kishazi tegemezi. Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi hata vikiondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu. Kishazi kinachoweza kujisimamia kama sentensi huitwa kishazi huru kikiwa ndani ya sentensi kuu na huitwa “sentensi sahili” kikiwa sentensi inayojitegemea. Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi ikiwa vitaondoshwa katika muktadha wa sentensi kuu. Vishazi vingi, hata vishazi huru huwa na kiima dhahiri. Kishazi kwa kawaida, hasa kishazi huru huwa na kitenzi kimoja kikuu. Kitenzi hicho huweza kuandamana na kitenzi kisaidizi. Pia, kitenzi katika kishazi huweza kuwa kitenzi kishirikishi. Kishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi. Tofauti ya kishazi na sentensi ni kwamba kishazi hupatikana ndani ya sentensi lakini sentensi hujisimamia kimuundo na kimaana. Aina za vishazi
Vishazi huru: Kishazi huru kinachotawaliwa na kitenzi kikuu ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili usiohitaji maelezo zaidi ya kukamilisha maana. Ni kishazi ambacho hata kikiondolewa katika muktadha wa sentensi ambamo kimejikita huweza kujitegemea kama sentensi. Vishazi tegemezi: Ni kishazi kinachotawaliwa ka kitenzi ambacho muundo wake hukifanya kutegemea kitenzi cha kishazi huru ili kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa. Kishazi tegemezi peke yake hakitowi ujumbe unaojitosheleza. Sifa za Kishazi tegemezi:
Kishazi tegemezi hakitoi maana kamili ila tu kinapoandamana na kishazi huru. Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana ya sentensi nzima. Kishazi tegemezi hutambulishwa na viambishi rejeshi Vinavyoambatanishwa kwenye kitenzi. Kishazi tegemezi vilevile kinaweza kutambuliwa kwa kuwepo vishazi kama vile ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, mzizi wa amba, mofu ya masharti n.k Kishazi tegemezi huweza kutokea kabla au baada ya kishazi huru. Aina za vishazi tegemezi
• Vishazi tegemezi vivumishi - Vishazi tegemezi vinavyotokea pamoja na nomino inayovumishwa. - Vishazi tegemezi visivyoambatana na nomino inayovumishwa • Vishazi tegemezi vielezi - vishazi tegemezi vya mahali - vishazi tegemezi vya wakati - vishazi tegemezi vya namna au jinsi - vishazi tegemezi vya masharti - vishazi tegemezi vya hali, hitilafu au kasoro iliyoko katika tendo. - vishazi tegemezi vya sababu/chanzo Dhima na hadhi ya vishazi Kishazi chaweza kuwa huru kikajitegemea chenyewe kikiwa na maana kamili na inayojitosheleza. Lakini kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi vyenyewe, bali hutegemea vishazi vingine. Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili). Kishazi tegemezi hakina hadhi hii, vishazi tegemezi ambavyo hutegemea vishazi vingine hushuka daraja na kuchukuwa dhima ya kikundi. Baadhi ya vishazi tegemezi huchukuwa dhima (hufanya kazi) ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno. Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo. Sentensi: sentensi ni kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea chenye kiima na kiarifu na inaleta maana kamili. Sifa za sentensi - Sentensi lazima iwe na mpangilio wa maneno ambao unakubaliwa na wazungumzaji wa lugha husika. - Sentensi lazima ikamilike kimaana, kimuundo na kisarufi. - Sentensi huwa na muundo wa kiima na kiarifu/huwa na kirai nomino na kirai kitenzi. - Sentensi huweza kuwa na zaidi ya kiima kimoja na kiarifu zaidi ya kimoja. - -Sentensi inaweza kuundwa na kitenzi kikuu kimoja au zaidi. - -Sentensi inaweza kuundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. - Sentensi huonesha hali mbalimbali, kama vile amri, ombi, mshangao, swali n.k Muundo wa sentensi kimapokeo/kikazi/kidhima/kiuamilifu Kiima: Ni sehemu katika sentensi ambayo hujaza sehemu ya mtenda au mtendwa wa jambo linaloelezwa. Katika tungo kiima hutokea kushoto mwa kitenzi. Kiarifu: Ni sehemu katika sentensi inayojazwa na maneno yanayoarifu tendo lilofanywa, linapofanywa au litakalofanywa na mtenda. Kiarifu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika sentensi ambayo wakati mwingine huweza kusimama pekee, kwani wakati mwingine huchukuwa viwakilishi vya kiima.
Vipashio vya kiima Nomino peke yake Nomino, kiunganishi na nomino Nomino na kivumishi Kivumishi na nomino Kiwakilishi peke yake Kiwakilishi na kivumishi Nomino na kishazi tegemezi vumishi Kitenzi jina Nomino na vivumishi zaidi ya kimoja Kitenzi jina na nomino Umbo kapa
Taarifa zitolewazo na kiarifu kuhusu kiima ni:
kiima ni nani kiima kina nini kiima hufanya nini kiima kinahisi nini Sifa za kiarifu: Huwa na kitenzi na pengine na maneno mengine. Kiarifu kwa kawaida huja baada ya kiima
Vipashio vya kiarifu
Kitenzi kikuu peke yake. Kitenzi kisaidizi au vitenzi visaidizi vilivyosambamba na kitenzi kikuu. Kitenzi kishirikishi na kijalizo yambwa (shamirisho) kijalizo chagizo
Sifa za chagizo Chagizo kwa kawaida huwa ni kielezi au kirai husishi ambacho kinafanya kazi kama kielezi. - Kwa kawaida ni vipashio vya ziada. Si lazima viwepo katika sentensi ili ijisimamie. - Huwa cha lazima ikiwa kinafuata kitenzi kishiriki. Hali ikiwa hivyo, kinatumika kama kijalizo. - Hutumika kufafanua kitenzi/kivumishi /kielezi. - Hutumika kujaliza kiima/kama kijalizo. Kuainisha sentensi Kuainisha sentensi kulingana na uamilifu kimawsiliano/kimapokeo tunapata: - sentensi za taarifa - sentensi ulizi - sentensi agizi - sentensi hisishi - sentensi ya masharti - sentensi za kukanusha - sentensi tatanishi Aina za sentensi kimuundo Sentensi sahili Miundo ya sentensi sahili - muundo wa kitenzi kikuu peke yake. - muundo wa kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi - muundo wa kirai-nomino na kira-tenzi - muundo wa virai-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’ - miundo ambamo virai-nomino vimeandamana na vijalizo
Sifa za sentensi sahili - Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa kwa kuwa kinaeleweka. - Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi au kitenzi kishirikishi na kijalizo na chagizo. - Haifungamani na sentensi nyingine na inajitosheleza kimuundo na kimaana.
Sentensi changamano: Hii ni sentensi yenye kishazi huru kimoja na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Sifa moja kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho hutegemea kishazi kingine huru ndani ya sentensi hiyo. Msingi muhimu wa uhusiano ndani ya sentensi hizo ni ule wa kishazi kimoja kutegemea kingine.
Miundo ya sentensi changamano - miundo yenye vishazi virejeshi. - miundo yenye vishazi vielezi
Sentensi ambatano: Hii ni sentensi inayojengwa na sentensi mbili au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia viunganishi kama vile lakini, wala,na,ingawa, au nakadhalika.
Miundo ya sentensi ambatano
- miundo yenye sentensi sahili tu. - miundo yenye sentensi sahili na changamano - miundo yenye sentensi changamano tu - miundo yenye vishazi visivyounganishwa kwa viunganishi.
Uchanganuzi wa sentensi • Hatua za uchanganuzi wa sentensi - kutaja aina ya sentensi, yaani kama ni sahili, changamano au ambatano. - Kutaja sehemu zake kuu, yaani kiima na kiarifu au kirai nomino na kirai kitenzi. - Kutaja sehemu kuu za kiima na kiarifu au sehemu kuu za kirai nomino na kirai kitenzi. - Kutaja aina zote za maneno yaliyomo katika sentensi hiyo. - Kuandika sentensi yenyewe upya.
• Mikabala ya uchanganuzi
i) Mkabala wa kikazi/kimapokeo - njia ya mishale/mistari - njia ya matawi - njia ya visanduku/jedwali. - njia ya maneno/maelezo ii) Mkabala wa kimuundo/kimambo leo - njia ya mishale/mistari - njia ya matawi - njia ya visanduku/jedwali. - njia ya maneno/maelezo
MUHADHARA WA KUMI NA TATU : NGELI ZA NOMINO NA UAINISHAJI WAKE PAMOJA NA DHANNA YA O-REJESHI. Mitazamo mbalimbali inayohusiana na uainishaji wa ngeli za nomino.
A. Kigezo cha kimofolojia/maumbo ya umoja na wingi:
1-mu- 2-wa i) Majina ya viumbe vyenye uhai isipokuwa mimea ii) Majina yanayotokana na vitenzi vinavyotaja watu 3-m- 4-mi i) Majina ya mimea ii) majina ya vitu yanayoanza na m- 5-ji- 6-ma i) Majina yanayoanza na ji- umoja na ma- uwingi. ii) Majina ya kigeni yenye ma- (wingi) iii) Majina yenye kueleza dhanna ya wingi japokuwa hayahesabiki 7-ki- 8-vi- i) Majina ya vitu yanayoanza na ki- (umoja) na (wingi). ii) Majina ya viumbe yanayoambishwa ch- umoja na vy-uwingi
9-N-
10-N i) Majina ambayo huanza na N inayofuatwa na konsonanti, ch-, d-, g-, j-, z-, na y- katika umoja na wingi. ii) Majina yanayoanza na mb-, mv. iii) Majina ya kigeni. 11- U- 12- N Majina yote yanayoanza na u umoja na N-, na mb (wingi) 13- U- 14- Ma Majina yote yanayoanza na u-umoja na ma- wingi. 15-Ku- Majina yanayotokana na vitenzi yanayoanza na ku- (vitenzi-jina) 16- PA- Huonesha mahali hasa 17- Mu- Huonesha mahali pa ndani. 18- Ku- Huonesha mahali pa mbali na mahali pakubwa zaidi au hata mahali popote.
Faida ya kigezo cha kimofolojia: • Kigezo hiki kinasaidia kuonesha uhusiano kati ya lugha za kikoa kimoja; na ni mojawapo ya uthibitisho kuwa lugha ya Kiswahili inaingia katika kundi la lugha za kibantu. • Asilimia kubwa ya nomino za Kiswahili zinaonesha maumbo dhahiri ya viambishi ngeli, na tukichukulia kuwa angalau ngeli (10) za kwanza zinajigawa katika jozi za umoja na wingi, inawezekana kabisa kuzigawa nomino katika makundi yake kwa kutumia kigezo hiki cha maumbo. • Husaidia kutambulisha ngeli na pia kuonesha idadi (umoja na wingi) katika nomino za Kiswahili.
Matatizo ya kigezo cha kimofolojia
Kuna nomino ambazo zina kigezo maalum, lakini zinatawanyika katika ngeli tofauti. Baadhi ya nomino huwa na viambishi vya umoja na wingi ambavyo ni tofauti na viambishi vinavyoitambulisha ngeli hiyo Baadhi ya nomino hazina viambishi vyovyote. Ngeli ya PA-MU-KU- inatambulishwa kwa kuzingatia upatanisho wa kisarufi kwa kuwa kuna nomino moja pekee inayopatikana hapa ambayo ni “mahali” na haina viambishi. Ufundishaji wa ngeli kwa kutumia umbo la nomino hauzingatii upatanisho wa kisarufi. Kuna viambishi ambavyo vinafanana/kujirudiarudia. Kutokidhi mahitaji ya sulubu ya sentensi.
B. Kigezo cha kisintaksia /upatanisho wa kisarufi: Huu ni mtazamo wa kisasa wa uainishaji wa ngeli ambao umeyagawa majina katika makundi kulingana na upatanisho wa kisarufi kati ya jina na viambishi awali vilivyo katika vitenzi yaani, vipatanishi. Kwa kigezo hiki wataalamu wameainisha ngeli tisa tu ambazo ni:
1. Ngeli ya:YU/A-WA 2. Ngeli ya :U-I 3. Ngeli ya: LI-YA 4. Ngeli ya KI-VI 5. Ngeli ya I-ZI 6. Ngeli ya U-ZI 7. Ngeli ya U-YA 8. Ngeli ya KU- 9. Ngeli ya PA/MU/KU- Faida za Kigezo cha kisintaksia • Kigezo hiki kilionekana ni bora kwa sababu majina mengi yanahusiana na mengine, na kila jina lina kipatanishi katika kitenzi. • Mwishoni mwa upatanisho wa kisarufi hautatanishi kwa vile kiambishi awali katika kitenzi huwa bayana sana • Majina yasiyo na viambishi mwanzoni, ngeli zake hujulikana kwa urahisi zaidi kwa kutumia upatanisho wa kisarufi kuliko kwa viambishi vya mashina ya majina. • Majina yote huainishwa kwa kuzingatia sifa na hadhi ya kila jina mf. Viumbe hai peke yake.
Udhaifu wa kigezo cha kisintaksia
• Kuna vipatanishi vinavyofanana katika ngeli hizi/kujirudiarudia. • Katika ngeli ya kwanza, kuna vipatanishi viwili vya umoja, YU/A lakini ukweli ni kwamba, matumizi ya kiambishi YU- ni ya kilahaja zaidi Kuliko ya Kiswahili sanifu. • Huyaweka majina ya maumbo tofauti katika ngeli moja. • Yapo baadhi ya maneno ambayo yana utata katika upatanisho mf. Makala,Jambazi
Matumizi ya ngeli
Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana na kufungamana kutokana na kigezo muhimu. Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majina na vivumishi. Hutumika kuleta upatanisho wa kisarufi katika sentensi. Hutumika katika kuonesha uhusiano uliopo baina ya lugha za Kiswahili na lugha zingine.
Dhanna ya O-rejeshi: Ni kiambishi kinachotumiwa kurejelea kwenye nomono ambayo huwa imetajwa kabla ya kitenzi chenyewe kutajwa. Viambishi hivyo ndivyo vinavyosababisha utegemezi katika sentensi. Dhima ya muundo wa O-rejeshi
- Hutumika Kama kirejeshi - hudokeza mahali - hudokeza wakati - Hutumika kama kiunganishi - Hudokeza namna
MUHADHARA WA KUMI NA NNE : DHANNA YA MOFOFONOLOJIA Maana ya mofofonolojia Mofofonolojia ni muunganiko wa taaluma za aina mbili za kiisimu: taaluma ya mofolojia (mofo) na taaluma ya fonolojia (fono) = Mofofonolojia. Tunaweza kusema kwamba Mofofonolojia ni taaluma inayojishughulisha na uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri maumbo ya mofu katika mfuatano wake. Hii ni taaluma inayojishughulisha na uchanganuzi wa vipengele vya kifonolojia ndani ya maumbo ya kimofolojia.
Utawala wa kifonolojia:
Ni mazingira ya kifonolojia yanayotawala utokeaji au utofauti wa maumbo ya maneno. Yaani, kuwepo kwa umbo fulani ni matokeo ya kuwepo au mfuatano wa fonimu fulani. Utawala wa Kimofofonolojia: Ni mazingira ya kifonolojia yanayoshindwa kutawala utokeaji au utofauti wa maumbo ya maneno. Yaani, kuwepo kwa umbo fulani hakutegemei kuwepo au mfuatano wa fonimu fulani. Mara nyingi hujitokeza kama vighairi.
Vighairi:
Ni mifano ya maumbo au miundo inayopingana na kanuni ya jumla ya utokeaji wa vipashio vya kimofolojia. Kanuni mbalimbali za kimofofonolojia: 1. Kanuni ya udondoshaji.Kanuni ya udondoshaji inasema kwamba, “irabu u inapokabiliana na konsonanti halisi, katika mpaka wa mofimu, hudondoshwa, lakini inapokabiliana na irabu inayofanana nayo hubakia kama ilivyo. mfano Umbo ndani Umbo nje /mu+ezi/ [mwezi] /mu+alimu/ [mwalimu] /mu+izi/ [mwizi] /mi+aka/ [myaka] /Vi+angu/ [vyangu]
/u/ [w]/-I; I # u /i/ [y]/-I; I # i
2. Kanuni ya uyeyushaji.Kanuni ya uyeyushaji inasema kwamba iwapo irabu inayokabiliana na u au i inafanana kabisa na irabu hizo basi irabu u au i itabaki jinsi ilivyo; lakini inapokuwa irabu inayokabiliana nazo haifanani nazo basi ama irabu hizo hubakia kama zilivyo au huyeyuka (yaani hupoteza nguvu zake za usilabi) na kuwa kiyeyusho. Mfano: Umbo ndani Umbo nje
mu+ezi mwezi mu+alimu mwalimu mu+izi mwizi mi+aka myaka Vi+angu vyangu u w/-I; I # u i y/-I; I # i
3. Kanuni ya muungano wa sauti. Kanuni ya muungano wa sauti inasema kwamba kuna uwezekano wa irabu ya mofimu moja kukabiliana na irabu ya mofimu nyingine katika mipaka ya mofimu mbili kisha irabu hizo mbili zikaungana na kuzaa irabu moja tu na aghalabu irabu inayozaliwa hailingani na yoyote kati ya irabu hizo mbili. Mfano:
Umbo ndani umbo nje Wa + enye wenye Wa + ingi wengi Ma + ino meno Wa + izi wezi
/a,i/ e/k-k
4. Kanuni ya nazali kuathiri konsonanti Kanuni ya nazali kuathiri konsonanti inasema kwamba kuna baadhi ya sauti ambazo huathiriwa na nazali /n/ inapokuwa sauti hizo zinaandamana. Hii ina maana kwamba sauti hizo zikikabiliana moja kwa moja na nazali /n/ huathiriwa nayo. Mfano:-
Umbo ndani Umbo nje n+limi [ndimi] n+refu [ndefu]
Hapa tunaona kwamba sauti [ l ] na [ r ] zinapokaribiana na irabu haziathiriki lakini zinapokaribiana na nazali “n” hubadilika na kuwa “d”
l d/N- r d/N-
5. Kanuni ya konsonanti kuathiri nazali Kanuni ya konsonanti kuathiri nazali inadai kwamba katika maneno umbo la nazali linategemea mahali ambapo konsonanti halisi, ambayo inakabiliana moja kwa moja na nazali hiyo , hutamkiwa. Mfano umbo ndani umbo nje n+buzi [mbuzi] n+bwa [mbwa] n+papai [mpapai]
n m/-N
6. Usilimisho
Ni kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kabisakabisa kutokana na kuathiriana. Hali hii husababishwa na sauti jirani katika neno kuathiriana hivi kwamba fonimu hupokea au kupoteza sifa za kifonetiki kwa fonimu jirani. Kwa mfano kitamkwa chenye sifa ya kikwamizi kinaweza kuathiriwa na kufanywa kuwa kitamkwa chenye sifa ya kipasuo.
Usilimisho huweza kuhusisha. - Kuimarika na kodhoofika kwa fonimu - Kuungana kwa sauti/fonimu - Kuingizwa na kudondoshwa kwa fonimu.
Kuimarika na kudhoofika kwa fonimu Mfano : sauti za vipasuo zinazotamkwa, wakati zimeshikana kabisa huhitaji nguvu zaidi katika kuzitamka kuliko wakati wa utamkaji wa sauti za vikwamizi.
Hapa vipasuo hudhohofishwa na kuwa vikwamizi. Kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba kudhohofika kwa sauti kunaweza kutokea pale ambapo nguvu chache za misuli katika ala za sauti na msukumo kidogo wa mkondo hewa hutumika katika alofoni kuliko kutamka fonimu yake. Mengi ya mabadiliko ya aina hii huwa ni ya kimazingira. Kudhohofika kwa konsonanti za Kiswahili aghalabu huhusisha kubadilika kwa konsonanti za mpasuo na kuwa za mkwaruzo. Hii inaweza kuwasilishwa kama ifuatavyo kwa kutumia sifa bainifu: [+kipasuo] [-kipasuo] [-vokali]
Tuangaliye mifano ifuatayo.
sheria hii inamaanisha kuwa Kuungana kwa sauti zinapoathiriana kiasi kwamba sauti moja hupoteza sifa bainifu zote kwa sauti jirani, au pengine sauti zote mbili huungana na kuzua alofoni mpya ya fonimu inayohusika. Kwa mfano:[ pa+iηgine ] huwa [pєηgine] yaani [a+i]-------->[є].
7. Kuingizwa na kudondoshwa kwa fonimu
Uingizaji hapa unarejelea uchopekaji wa sauti moja au zaidi katika neno. Kwa upande mwingine udondoshaji hurejelea utoaji wa sauti moja au zaidi katika neno. Uingizaji na udondoshaji waweza kuwa wa kimakusudi au kutokea kibahati katika historia ya fonolojia ya lugha. Hali hii aghalabu hutokea ili kuleta muundo wa silabi wa neno unaokubalika katika lugha husika, hasa kwa maneno yenye asili ya kigeni. Kwa mfano, sauti ya likwidi /l/ imedondoshwa katika baadhi ya maneno ya Kiswahili sanifu kihistoria. Kwa mfano neno ‘oa’ zamani lilitamkwa, ‘lola’.
Kuna aina tatu za udondoshaji. Udondoshaji sauti awali Udondoshaji sauti kati na Udondoshaji sauti tamati. mfano: Umbo ndani umbo nje
mutu mtu mwalimu mwalim muzito mzito
/u/ [θ]/M-
8. Tangamano la irabu: Ni hali ya irabu kuathiriana. Irabu iliyo katika mzizi wa kitenzi hasa kwenye silabi moja kabla ya ile ya mwisho huathiri irabu ya mnyambuliko. Mfano: ikiwa katika mzizi wa neno utakuwa na irabu a, i, au u basi irabu ya mnyambuliko itakuwa i katika kauli zote za unyambulishi; kauli ya kutendea, kutendeka, kutendesha/ kusababisha. Mfano.
Imba --------------imbia Andika-------------andikia Funga ------------ fungia Daka --------------dakia a
//Utendea// i/-mz+ i
u
• Ikiwa irabu ya mzizi iliyo kwenye silabi moja kabla ya ile ya mwisho ni e au o basi irabu ya mnyambuliko itakuwa e katika kauli zote za unyambulishi; kauli ya kutendea, kutendeka, kutendesha. Mfano:
Oga----------------ogea Sema --------------semea e
//utendea// e/-mz+
o
MUHADHARA WA KUMI NA TANO: DHANNA YA SEMANTIKIA Maana ya semantiki Semantiki ni stadi inayojishughulisha na maana katika muktadha wa lugha ya mwanadamu.
• Semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo. • Maana hushughulikiwa katika viwango vyote vya lugha, kama vile sauti, maneno na sentensi.
Maana ya maana Hakuna jibu la mkato au jibu rahisi linaloelezea juu ya dhanna ya maana.Tuangalie maana mbalimbali za maana zilizopo hapo chini. • Maana ni maelezo yanayotumiwa kukitambulisha au kukifafanua kitu • Maana ni kusudio au dhamira ya mtu. • Maana ni ishara au dalili ya jambo. • Maana ni thamani, umuhimu au nafasi ya kitu au jambo fulani kwa
mtu.
• Maana ni sababu. Aina za maana Leech,G (1974) amedhihirisha aina saba za maana kama ifuatavyo:- Maana msingi/tambuzi (conceptual/denotative). Hii ni ile maana ya msingi ya neno. Pia hujulikana kama maana ya kikamusi au maana tambuzi. Neno hupewa maana hii pale tu dhanna mpya inapoanza kutumiwa katika jamii na kupewa neno la kuitambulishia. Maana ya ziada/Maana ya kimatlaba/ashirifu (connotative meaning) Hii ni maana ya ziada ambayo neno hupata yaani maana ya kimatlaba. Maana hii hutokana na maana ya msingi ya neno. Maana hii huhusishwa na kitajwa cha msingi. Maana hizi hutokana na mabadiliko ya matumizi ya maneno kimaana katika jamii. Maana ya kimtindo/stylistic meaning. Hii ni maana ya kimuktadha; hii ni maana inayotokana na matumizi ya Luhga kulingana na mazingira halisi ya wakati wa mazungumzo. Maana akisi/ Reflective meaning. Hii ni maana inayopewa kitu kwa kufananisha na kitu kingine. Kwa mfano mtu anapommwita mpenzi wake mtoto au malaika anamaanisha mzuri, asiye na makosa. Maana dhamirifu (thematic meaning) Maana hii inapatikana kutokana na namna mtumiaji wa Lugha anavyopanga maneno yake katika sentensi. Aghalabu, ile taarifa ambayo muhusika anaiona kuwa ndiyo muhimu huiweka mwanzoni. Maana shawishi (affective meaning) Hii ni maana inayotokana na hisia na mtazamo wa mzungumzaji au mwandishi juu ya kitu. Je, ana mtazamo hasi au mtazamo chanya? Maana endefu/Tangamano /collocative meaning. Kuna baadhi ya maneno ambayo maana zake hupatikana kwa kuwa karibu au pamoja na maneno mengine maalum; kinyume chake haiwezi kukubalika katika hali ya kawaida.
Nadharia tano za maana ni:-
• Nadharia za urejeleo za maana: Hii ni maana inayoelezea kitu halisi. • Nadharia za kidhanna za maana: Haya ni mawazo yanayohusishwa na neno. • Nadharia za kitabia za maana: maana hutolewa kutokana na tabia ya kitu. • Nadharia za masharti ya ukweli za maana:- maana ni ukweli. • Nadharia za tendo - usemi wa maana.
MUHADHARA WA KUMI NA SITA: UHUSIANO WA KIMSAMIATI Dhanna ya uhusiano wa kimsamiati: Huu ni uhusiano wa maneno unaozungumzia maingiliano yaliyopo baina ya maneno. Uhusiano utakaoongelewa hapa ni wa sinonimia, antonimia, homonimia, polisemia na haiponimia. Sinonimia Maana ya sinonimia: ni uhusiano wa kileksika au kimsamiati ambapo huwa kuna maumbo tofauti katika lugha ambayo maana zake ni sawa. Maneno yanayotofautiana kimaumbo lakini yakafanana au kulingana kimaana huitwa sinonimu. Mambo yanayosababisha kuzuka kwa sinonimia: • Uchukuaji wa msamiati: Maneno yakiwa na asili tofauti huleta hali ya usinonimia. • Jinsia: Sinonimu nyingine hutokana na visawe vinavyorejelea wanawake na wanaume. Kuna maneno yenye maana moja kimsingi lakini huwa na umbo tofauti kutegemea jinsia.Kwa mfano hali ya kuwa na sura nzuri hurejelewa kwa kisawe cha “urembo” kwa wanawake na “ujamali” au “umaridadi” kwa wanaume. • Dini: Dini tofauti huwa na maneno tofauti kuelezea dhanna zinazolingana. Kwa mfano dhanna inayorejelea mahala pa kuabudia kwa waisilamu msikitini, kwa wakiristo kanisani na sinagogi kwa mayahudi. • Tofauti za kimaeneo: Wazungumzaji wa Lugha wanapogura au kuhama Kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, Lugha yao hubadilika kimuundo na kimsamiati ili kukidhi mahitaji ya mazingira mapya. • Tofauti za kilahaja: Dhana moja huweza kutajwa kwa maneno yenye matamshi tofauti. Kwa mfano neno nchi katika Lahaja sanifu ya Kiswahili huwa ni nti kimvita au chi Kitumbatu. • Taaluma: Visawe vya Kitaaluma huitwa istilahi. Mfano wa sinonimu za aina hii ni aya katika riwaya na ubeti katika ushairi vinavyorejelea kitengo katika mfululizo wa maandishi. • Wakati: Baadhi ya sinonimu za Lugha huzuka kutokana na mabadiliko ya kihistoria. Antonimia Maana ya antonimia: Antonimia ni uhusiano ambapo kuna maneno katika Lugha ambayo maana zake ni vinyume”. Kinachokusudiwa kusemwa hapa ni kwamba maana za maneno hayo huwa zinapingana. Maneno yenye maana zinazopingana huitwa antonimu. Aina za antonimia:
Antonimia za kiukinzani: ambapo zipo tofauti kabisa kimaumbile au kimaana. Antonimia za kipimo: Kinachozingatiwa hapa ni tofauti ya wingi wa kinachopimwa Antonimia za uhusiano: Kinachozingatiwa hapa ni uhusiano uliopo baina ya vinyume
Homonimia Maana ya homonimia: Huu ni uhusiano wa kimsamiati unaohusu maneno tofauti yaliyosadifu kuwa na maumbo sawa lakini yaliyotofautiana kimaana. Kufanana kwa maumbo hayo ni kwa kusadifu tu. • Maneno hayo huwa hayana usuli mmoja wala kihistoria. • Maneno mawili au zaidi yanayofanana kwa maumbo na kutofautiana kwa maana huitwa homonimu. Aina za homonimia: • Homofoni: Ni kuwepo kwa maneno yenye matamshi sawa, lakini maana zinatofautiana kabisa. • Homografia: Ni hali ya maneno mawili au zaidi kuwa na tahajia sawa lakini maana zake tofauti. Polisemia: Polisemia ni hali ambapo maneno huwa na maana zaidi ya moja. Katika polisemia maneno huwa na uhusiano wa kihistoria.Huu ni uhusiano unaohusu umbo moja la neno lenye maana mbalimbali. Haiponimia: Huu ni uhusiano wa kimsamiati ambapo maana fulani ya neno ni sehemu ya maana kubwa ya neno. Neno lenye maana kubwa huitwa maana jumuishi ilihali maneno yenye maana ndogo huitwa haiponimu
MUHADHARA WA KUMI NA SABA: UTATA KATIKA LUGHA NA DHIMA ZA KISEMANTIKI PAMOJA NA UPANA WA DHANNA. Dhanna Ya Utata Katika Lugha Utata: Ni hali ya kipashio cha kisarufi kama neno, kirai, kishazi na hata Sentensi kuwa na maana zaidi ya moja. Aina za Utata: • Utata wa kimuundo • Utata wa kimsamiati
Sababu za kuwepo utata katika Lugha Neno kuwa na maana zaidi ya moja, kama ilivyo neno endesha, mbuzi, kaa, buibui na mengi mengineyo. Kutumia neno bila kuzingatia mazingira au muktadha unaohusika na matumizi ya maneno hayo. Utumiaji wa maneno yenye maana ya picha au maana iliyofichika yaani, viashiria husababisha utata. Kuwepo kwa mofimu ya kauli ya kutendea /li/, /le/, /i/, na /e/. Kuwepo kwa kiambishi nafsi kiambata ‘a’ na ‘wa Matumizi ya vimilikishi –ake na –ao Matumizi ya mzizi ‘ingine’ Matumizi ya baadhi ya viunganishi. Matumizi ya baadhi ya vihusishi Makosa ya kisarufi na kimantiki
Dhanna na dhima za Kisemantiki • Maana ya dhima za Kisemantikia:
Ni dhima inayosimamia kazi na majukumu ya nomino mbalimbali zilizomo ndani ya sentensi. Kwa ufupi hizi ni dhima za kitajwa katika sentensi. Kinachoshughulikiwa hapa ni “nani amefanya nini kwa nani kwa njia gani na kwa kutumia kifaaa kipi” Kila nomino katika tungo kishazi au sentesi kamili ina dhima au jukumu maalumu. Dhima za kisemantiki zijulikanazo ni: Mtenda :mtenda ni jukumu linalohusu nomino inayorejelea mtu au kitu chenye uhai kinachosababisha kitendo fulani kutendeka. Kitendo kinachotendeka kinaakisiwa na mtenda. Mtendwa: Ni jukumu la mtu, watu, au vitu vinavyopata athari. Mara nyingi athari hizi huwa zinapatikana au kusababishwa na mtenda. Kifaa: Hili ni jukumu linalohusu nomino inayorejelea kifaa cha utendakazi. Kifaa hiki hutumiwa mara nyingi na mtenda. Mwathiriwa:- Mwathiriwa ni dhima/jukumu linalotekelezwa wakati ambapo nomino inarejelea mtu au kitu kinachopata athari fulani. Athari hizi mara nyingi huwa hazitokani na mtenda. Nguvu:-Jukumu la nguvu hutekelezwa na kirejelewa au kitu kisichoonekana kwa uwazi. Mara nyingi nguvu huwa ni vitu vya kidhahania. Chanzo :- Jukumu la chanzo hutekelezwa na nomino zinazorejelea mahali, wakati au mwanzo wa kitu fulani. Lengo: Lengo tofauti na chanzo , ni mahali au wakati wa kuishia kitendo fulani. Wakati: Jukumu hili hutekelezwa na nomino zinazorejelea wakati. Mahali: Jukumu la mahali ni lile linalotekelezwa na nomino zinazorejelea mahali fulani. Nomino za mahali hurejelea mahali maalum bila kuhusisha nomino ya chanzo au lengo. Malighafi: Mali ghafi ni jukumu linaloakisiwa na nomino inayorejelea vitu vinavyotumika katika utendaji wa kazi. Katika hali hii vitu hivyo havitumiki kama vifaa, bali kama mali ghafi ya kazi. Matokeo: Haya ni matokeo ya kutumika mali ghafi. Katika sehemu ya malighafi hapo juu uzi na kitambaa ni mali ghafi ya suti na suti ni matokeo. Mfumo wa udhahania Dhana ficho/Kengeushi: Dhanna zilizo katika sentensi za mazungumzo, zisizo wazi. Umenyu (Typicality): Hali ya kuwa mashuhuri zaidi kuliko vingine vyenye umashuhuri katika fani au kada fulani. Upana wa dhanna: Ni hali ya kuiwasilisha dhanna moja kwa maneno tofautitofauti kutokana na tofauti ndogondogo zinazojitokeza ndani yake
MUHADHARA WA KUMI NA NANE: ISIMU JAMII Maana ya isimu jamii: Isimu jamii ni taaluma inayochunguza matumizi ya lugha katika jamii. Malengo ya Isimu jamii:
Kuchunguza na kufafanua tofauti zilizo katika lugha na uhusiano ulio katika lugha hizo, na tofauti zilizo katika jamii. Kuchunguza uhusiano uliopo kati ya lugha na wazungumzaji.Lugha inamtambulisha mzungumzaji na kundi analoliwakilisha. Kutafiti na kufafanua nafasi ya lugha katika jamii ili kufahamu idadi ya lugha zilizomo katika jamii, kubaini uamilifu na uwezo wa kila lugha. Kutafiti na kufafanua tofauti zilizomo ndani ya lugha na namna zinavyohusiana na tofauti zilizomo ndani ya jamii.
Uamilifu wa Lugha:
• kutolea elimu k.v. kufundishia masomo shuleni • kuendeshea shughuli za serikali, siasa, mahakama • kufanya mawasiliano ya kawaida miongoni mwa jamii husika ambayo ni pamoja na shughuli za kila siku za jamii k.v. matambiko, misiba, harusi, ngoma na sherehe mbalimbali. • kutumika katika mawasiliano mapana hususan kati ya jamii zenye kuongea lugha tofauti hasa katika biashara.
Dhima ya Lugha
• Dhima kuu ya lugha ni kufanya mawasiliano kati ya mtu na mtu • Lugha huwawezesha watu wa jamii moja au jamii tofauti kuwasiliana na kuwawezesha waelewane.
Binaadamu na Lugha • Binadamu huwasiliana miongoni mwao kwa lugha itumiayo maneno ambayo ni sauti zilizokubaliwa na kuwekwa pamoja ili kuleta maana mahsusi. • Lugha itumiayo maneno ni sauti za nasibu zilizoteuliwa na kukubaliwa na binadamu ili wazitumie kuwasiliana. • Lugha itumiayo maneno ni mahsusi kwa binadamu pekee. • Katika kuwasiliana kwa kutumia maneno, binadamu huweza kuunda mitindo ya aina mbalimbali k.v. rejesta, lahaja, simo, vitarafa n.k. na kuzalisha maneno na tungo zisizo na kikomo kwa lengo la kufanikisha mawasiliano. • Binadamu hutumia pia ishara kuwasiliana miongoni mwao. Mfumo wa ishara ni mfumo unaotumia viungo vya mwili k.v. mikono, vidole, kope za macho, kichwa n.k. ambavyo huchezeshwa kwa namna fulani na kutoa ujumbe unaoeleweka kwa wazungumzaji na wasikilizaji. • Ishara hizi zimeteuliwa kinasibu pia kwa maana kuwa hakukuwa na utaratibu wa kuziunda na kuzipa maana, ila ziliibuliwa na wanajamii, zikazoeleka na kukubalika. • Kwa kutumia viungo vya mwili binadamu huunda mfumo wa ishara fulani zenye kuwasilisha ujumbe kwa msikilizaji. • Aidha binadamu hutumia sauti za mkururo k.v. kuguna, kufyonza, kukoroma, kucheka n.k. kueleza hisia zake ambazo ni ujumbe kwa msikilizaji ama kwa kudhamiria k.v. kufyonza kama ishara ya dharau, au kukoroma kukiashiria kulala pasi na mhusika kusema ‘nimelala’.
Lugha na viumbe wasio wanaadamu: • Wanyama hutumia ishara kuwasiliana. Mara nyingi wanyama hutoa milio maalum kuwasilisha ujumbe kwa wenzao, kama vile mlio wa kuwaarifu wenzao kuwa na hadhari kwani kuna adui au kiumbe asiye mwenzao jirani nao. • Wanyama wengine hutumia milio maalum kutafutana na wengine hutoa mlio wa kufurahia mlo uliopatikana, kwa mfano fisi, bila shaka ikiwa ni kuwaita wengine waje. • Mfumo wa ishara ndio njia ya mawasiliano pekee itumiwayo na wanyama. Wanyama pia hutumia harufu kuwasiliana. Nadharia za chimbuko/asili ya Lugha: Krioli na Pijini Maama ya krioli na pijini: • Lugha yenye mfumo uliorahisishwa sana ambao hutumiwa na wazungumzaji wenye lugha tofauti katika mazingira maalum na kwamba pijini sio lugha mama kwa mzungumzaji yeyote. • Lugha mama inayotumiwa na wazungumzaji wazawa ambao kihistoria wametokana na jamii lugha ya pijini. Launi za Lugha (A.kipacha) Kila mtu huzungumza kwa namna tofautitofauti hata kama hutumia lugha au lahaja ya aina moja tu. Tofauti hizi hutokana na sababu kama vile: umri (vijana au wazee), mahali (mjini au kisiwani), kazi,urasimi au matabaka. Mazingira ya kijamii yana mawanda mbalimbali kama vile nyumbani, shambani, sokoni, ofisini, n.k
Aina za launi za lugha Ziko aina nne za launi za lugha ambazo ni: Lugha rasmi, Lahaja jamii, Lahaja jiografia na rejista. Lugha rasmi: Ni aluni iliyopitishwa na kusanifishwa kuwa rasmi kwa shughuli rasmi za kiserikali na umma kwa ujumla. Lahaja jamii: Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa na tofauti ndogondogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa vile wanatoka katika matabaka, rika, ujuvi, jinsia au itikadi tofauti. Lahaja Jiografia: Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa na tofauti ndogondogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa sababu wanatoka katika maeneo yanayotenganishwa na milima, bahari au mito. Rejista: Rejista ni mtindo wa lugha inayotumika mahali penye shughuli fulani au inayotumiwa na kundi maalum la kijamii ambayo ni tofauti na lugha ya kawaida.
Launi za lugha
Lugha rasmi lahaja-jamii lahaja-jiografia Rejista
Uwezo jinsia umri kazi urasimi siorasmi ufundi Vigezo vitumikavyo kuteua lahaja rasmi:
• Uteuzi: Kwa njia moja au nyingine lahaja rasmi huteuliwa miongoni mwa lahaja zilizopo. • Uandishi: baadhi ya taasisi kama vile TUKI, huwa wanatunga kamusi na vitabu vya sarufi ambavyo watu huvifuata. • Dhima: Lugha rasmi haina budi itumike katika shughuli za serikali na elimu ya juu. • Ukubalifu: launi lazima ikubalike na wazungumzaji au jamii kwa ujumla. Ikisha kubalika hubeba dhanna ya kuunganisha jamii na huwa ni ishara ya uhuru wa jamii hiyo. Dhanna ya vizingasifa na aina zake Vizingasifa ni mistari inayogawanya tofauti za matamshi baina ya lahaja moja na nyingine. Unaporuka mpaka huo wa kizingasifa unakuwa umeruka kutoka eneo lahaja moja kwenda kwenye eneo lahaja lingine. Aina za vizingasifa 1. Vizingasifa msamiati (Isolex) Hutenganisha msamiati lahaja tofauti mf. - Tungule (KS): nyanya (Nzn) - nswi:samaki 2. vizingasifa mofu (Isomorph) Hutofautisha lahaja moja na nyingine kufuatana na tofauti za kimuundo (mofu) mf. - Ninakuja (KS): ni-θ-ja (kingome,kivumba) - Anakuja (KS) : yu-a- θ-ja (kipwani) 3. Vizingasifa sauti (Isophone) Hutenganisha tofauti za kifonolojia Mf. - ndoo (kiMvita) : ndoo (KS) 4. vizingasifa maana (Isoseme) Hii ni michoro au mistari katika atlas lahaja inayotenganisha maana tofauti.
Mf.
- Mfereji (Ki-Unguja): bomba la maji (KS) Mambo mengine yanayohusu jamii na Lugha Nadharia ya Pijini na krioli
>>>>>>>INAENDELEA>>>>>>>>>>