Fasihi Kwa Ujumla



Maana ya Sanaa
Sanaa ni ufundi au ustadi wa kuwasilisha mawazo mbalimbali yaliyo katika fikra za binadamu.
Tanzu za Sanaa
 
FASIHI                          MUZIKI                         UCHORAJI
UDARIZI                       SANAA                         UFINYANZI
UCHONGAJI                USUSI                           MAONYESHO
 
FASIHI
Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe kwa jamii husika. Sanaa katika fasihi ni ufundi wa kutumia lugha ili kuleta hisia Fulani na kufikisha ujumbe uliokusudiwa.
DHIMA ZA FASIHI
Kuelimisha jamii
Fasihi inapofikisha ujumbe wake kwa jamii juu ya kuepukana na vitendo vinavyoleta madhara katika jamii, kwa mfano kukataza jamii kutenda vitendo viovu kwa kupitia methali na misemo mbalimbali kwa mfano; asie sikia la mkuu huvunjika guu.

Kuburudisha jamii.                                                                        
Fasihi pia hutumika kama kiburudisho, huleta furaha kwenye huzuni
kwa mfano; nyimbo, mashairi na maigizo hivi vyote kwa ujumla huburudisha jamii katika maeneo tofauti tofauti.

Kuunganisha watu wanaotumia lugha husika
Fasihi huunganisha watu maana wale wanaotumia lugha moja huunganishwa na aina ya fasihi inayotumia lugha yao kwani fasihi ni sanaa inayotumia lugha kufikisha ujumbe wake. Kwa mfano nyimbo za Kiswahili huunganisha watu wanaozungumza Kiswahili.

Fasihi husisimua
Hii huonekana pale ambapo Fasihi inatumia misemo na tamathali za semi na picha kuelezea matukio mbalimbali aliotokea katika jamii husika, kwa mfano; “ndugu yetu amefariki”, “ametutupa mkono”, “ameaga dunia”.

Fasihi hukuza lugha ya jamii husika
Fasihi hukuza lugha kupitia namna tofauti tofauti ya jinsi inavyotumia lugha husika. Kwa mfano; kupitia muziki,mashairi, tenzi na ushauri lugha husika huongeza misamiati tofauti tofauti.
 
AINA ZA FASIHI
Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni;
  1. Fasihi similizi
  2. Fasihi andishi

 
Fasihi simulizi
Ni aina ya fasihi ambayo huifadhiwa kichwani na huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo.

Sifa za fasihi simulizi
Ni kongwe.
Ni mali ya jamii nzima.
Hukutanisha fanani na hadhira ana kwa ana.
Ina hali ya utendaji.
Hubadilika kutokana na mazingira.
Huwasilishwa kwa njia ya masimulizi.
Ina tanzu nyingi.
Ina wahusika wengi.                  

Fasihi andishi
Ni aina ya fasihi ambayo huhifadhiwa na kuwasilishwa kwa njia ya maandishi.                               
Kwa mfano; riwaya, tamthilia, na ushairi
 
Sifa za fasihi andishi
Si kongwe
Ni mali ya mwandishi au mtunzi
Haikutanishi fanani na hadhira
Haina hali ya utendaji hivyo si hai
Haibadiliki kutokana na mazingira
Ina tanzu chache
Ina wahusika wachache
Huwasilishwa na kuifadhiwa kwa njia ya maandishi 

TOFAUTI KATI YA FASIHI SIMULIZI NA FASIHI ANDISHI
                           Fasihi simulizi                                                                                                        Fasihi andishi#000000 solid;margin:15px;width:95%;">
Huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomoHuwasilishwa na kuifadhiwa kwa njia ya maandishi
Ina tanzu nyingi  Kwa mfano;   ngonjera, maigizo, na methaliIna tanzu chache mfano; tamthilia na riwaya
Ni hai kwani huonesha vitendoSi hai haina vitendo
Ina wahusika wengiIna wahusika wachache
Ni mali ya jamii nzimaNi mali ya mwandishi au mtunzi
Ni kongweSi kongwe
Hukutanisha fanani na hadhiraHaikutanishi fanani na hadhira
 
 
 
 
 
 
 
Powered by Blogger.