Udhibiti Wa Kazi Za Fasihi Kwa Ufupi


E.Kezilahabi ni mmoja wa watu waliokumbana na kinachoitwa udhibiti wa kazi za fasihi. Udhibiti huu ulianzia Amerika ya Kusini na mtu wa kwanza kudhibitiwa huko alikuwa mtunzi mashuhuri wa mashairi Pablo Neruda ambaye alianza kupingwa baada ya kubadili utunzi wake na kusema maovu ya tabaka tawala. Rosa Mistika cha E. Kezilahabikilipigwa marufuku kwa kuwasema wakubwa akiwemo Deogratias aliyekuwa bwana maendeleo kwa kutembea na wanafunzi akiwemo Rosa, ili kudhiti siri za wakubwa kuwekwa wazi serikali ilitafuta visingizio vya kukipiga marufuku kitabu hicho na ikawa kama ifuatavyo:
1. Ilidaiwa na serikali kuwa kitabu hicho kinaharibu maadili kwa kuanika hadharani mambo machafu yasiyoendana na maadili ya mtanzania.

2. Wanawake nao wakaja juu kwa madai kuwa wamedhalilishwa kupitia matendo ya Rosa yaliyoandikwa kitabuni, inadaiwa kuwa mama mmoja aliwahi kuzimia baada ya kumkuta binti yake akisoma kitabu hicho.

3. Kundi la tatu ni kanisa Katoliki ambalo lilikuja juu kwa madai kuwa Mistika ni moja wapo wa sifa za Bikira Maria mtakatifu, hivyo ni udhalilishaji kumpa Rosa jina hilo hali ni mchafu wa matendo kiasi kile.

Kimsingi pamoja na udhibiti huo E. Kezilahabi alizidisha utunzi wake kwa kutumia lugha ngumu sana isiyoeleweka kirahisi hasa kwa msomaji wa kawaida. 

Watunzi wengine walokumbana na udhibiti kama huo kwa Afrika ni Peter Abrahams(Makhumazhan), David G. Mailu (My Dear Bottle), Ngugi wa Thiong'o ( I will Marry When I want - ambacho alikiandika upya kwa lugha yao kikaitwa Ngaaika Ndeenda), kwa ujumla hofu ya tabaka tawala ndio msingi wa udhibiti wa kazi za fasihi.

Mtunzi wa kazi ya fasihi huweza kuwa huru iwapo tu atakuwa na vitu vifuatavyo:

1. Utashi
2. Falsafa inayoeleweka
3. Msimamo
4. Kuitawala sanaa
5. Kuimudu lugha
Powered by Blogger.