UNOMINISHAJI NOMINO ZALIKA/UNOMINISHAJI
UNOMINISHAJI NOMINO ZALIKA/UNOMINISHAJI
Unominishaji kwa mujibu wa Habwe na Karanja
(2007) wanasema ni hali ya kuunda nomino kutoka katika kategoria nyingine ya
neno. Kategoria hizi zaweza kuwa kitenzi, kivumishi au hata nomino yenyewe. Ø
Kwa hiyo vinominishi (o, i) vinaweza kunominisha vitenzi vya Kiswahili katika
mazingira yafuatayo: Tukianza na kinominishi (o); kinominishi “o” huweza
kunominisha vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati “a”.
Kwa mfano:
tenda→ tend-o
Andika → andik-o
Piga → pig-o
Pata → pat-o
Jenga → jeng-o
Fundisha → fundish-o
Ona → on-o
Pamba → pamb-o
Hata
hivyo kuna baadhi ya vitenzi vya kibantu vinavyoishia na kiambishi tamati
“a”ambavyo havinominishwi na kinominishi “o” mfano wa vitenzi hivyo ni kama
lowa, tembea nk. Ø Pia kinominishi “o” huweza kunominisha vitenzi kwa
kuambatana na vinyambulishi (-i-) au (-li-) katika baadhi ya vitenzi.
Kwa mfano:
kaanga→ kaang-i-o
Chuja→ chuj-i-o
Pamba → pamb-i-o
Fua → fu-li-o
Kaa → ka-li-o
Mazingira mengine ambamo kinyambulishi
nominishi “o” huweza kunominisha kitenzi ni pale ambapo huambatana na mofimu
(-e-) Mfano:
Chekecha → chekech-e-o
Fyeka →
fyek-e-o Zoa
→ zol-e-o Ø Vilevile kinominishi “o” huweza kunominisha kitenzi kwa
kushirikiana na viambishi awali vinominishi.
Mfano: Lima → ki-lim-o
Soma →
ki-som-o
Kula → m-l-o
Lia → ki-li-o, m-li-o
Penda →
u-pend-o
Cheza → m-chez-o Ø Pia baadhi ya vitenzi huweza kuondolewa irabu ya mwisho na
kubakiwa na kinyambulishi “o” kama kinominishi.
Mfano:
toboa→ tobo Ø Vilevile unominishaji huweza kufanyika katika vitenzi vya
utendewa na utendeshwa kwa kuondoa mofimu (-w-a).
Mfano: somwa → som-o
Pigwa →pig-o
Lishwa →
lish-o
Tendwa →tend-o Ø Kwa upande wa kinominishi “i” pia huweza kunominisha kitenzi
katika mazingira tofautitofauti kama ilivyoonyeshwa hapa chini. Kinominishi “i”
huweza kunominisha kitenzi kwa kusaidiana na viambishi awali vinominishi.
Mfano: soma
→ m-som-i
Soma → u-som-i
Chunguza →
u-chunguz-i
Chokoza → u-chokoz-i Ø Kinominishi “i” huweza kuchukua nafasi ya kiambishi
tamati “a” katika kitenzi na kunominisha kitenzi hicho.
Mfano: Sema →
sem-i Ø Vilevile kinominishi “i” huweza kuambatana na vinyambulishi vingine ili
kunominisha kitenzi.
Mfano: Chuja →
chuj-i-o
Pita →
pit-i-o
Habwe na Karanja (2007:45) wanasema
kinominishi “i” kinapotumika kunominisha mizizi inayoishia na konsonanti,
mfano; (pik) na (jeng). Mofimu “i” inapopachikwa kwenye mizizi hubadili na
kuifanya kuwa nomino.
Mfano:
Kitenzi Unominishaji Nomino Pika mu+pik+i
mpishi Jenga mu+jeng+i mjenzi Iba mu+ib+i mwizi Ø Vilevile kinominishi “i”
huweza kunominisha shina la kitenzi cha mnyambuliko.
Mfano:
tembeza→ m-tembez-i
Kimbiza → m-kimbiz-i
Tapisha → ma-tapish-i ·
Kivumishi cha sifa kikiongezwa irabu “u” mwanzoni mwa kivumishi husika huunda
nomino zalika: mfano:
baya ubaya,
zuri uzuri,
vivu uvivu ·
Nomino zinazotokana na kuongeza kiambishi “ki” mwazoni na “o” mwishoni mwa
kitenzi. Mfano: soma – kisomo, apa – kiapo, piga – kipigo, ziba – kizibo, lia –
kilio. · Nomino zinazotokana na kuongezwa kwa kiambishi
“m” mwanzoni mwa silabi na “ji” mwishoni mwa kitenzi. Mfano: chora – mchoraji,
cheza – mchezaji, baka – mbakaji, kamua – mkamuaji, fagia – mfagiaji.
· Nomino zinazotokana kwa kuongeza viambishi awali “m” na “u” mwanzoni
mwa kitenzi au kiambishi tamati “vu” au “zi” mfano: legeza – ulegevu (hali),
mlegevu (mtu), teleza – utelezi (hali), mtetezi (mtu), kakamaa – ukakamavu
(hali), mkakamavu (mtu). · Kwa kuambatanisha maneno mawili.
Mfano: uambatanishaji wa jina kwa jina: askarikanzu, batamzinga, afisakilimo,
· Jina na kivumishi: mjamzito.
· Kitenzi na jina: chemshabongo, changamoto. Jina
tegemezi na jina huru: jinategemezi hutokana na kitenzi na linahitaji jina huru
ili maana ikamilike. Mfano: mpigambizi, kitindamimba, kifunguakinywa,
kifunguamimba, nk.