KISWAHILI -2 KIDATO CHA 5 & 6

 

MADA 1 :  FASIHI KWA UJUMLA

NADHARIA YA FASIHI

Nadharia ni mtazamo,mawazo,maelezo au mwongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza,kutatua au kutekeleza jambo Fulani mahususi.

Nadharia za fasihi ni mtazamo,mawazo au maelezo ya wataalamu mbalimbali kuhusu fasili au maana ya fasihi.

Wataalamu mbalimbali wametoa mitazamo tofautitofauti kuhusu fasili/Maana ya fasihi  kamaifuatavyo:-

1.     Fasihi ni jumla ya maandishi yote katika lugha Fulani.Mtazamo huu umeelezwa na Wellek na Warren (1986) wakisema kuwa ni njia mojawapo ya kuielezea fasihi ni kuichukulia kuwa ni jumla ya machapisho yote.

Ø Mtazamo huu unaudhaifu kwani hupanua mno uwanja wa fasihi na kujumuisha dhana ambazo si za kifasihi.Kwa matzo huu,maandishi yoyote,yakiwemo matangazo ya biashara,mafunzo ya historia,jiografia ama sayansi,yanaweza kujumuishwa humo.

Ø Mtazamo huu unabagua fasihi simulizi ambayo kimsingi haipo katika maandishi

2.     Fasihi ni maandiko bora ya kisanaa yenye  manufaa ya kudumu.Mtazamo umeelezwa na Hollis Summers (1989) ambapo anasema kuwa fasihi ni sanaa inayojumuisha zaidi maneno yaliyoandikwa.

Udhaifu wa mtazamo huu unaupa uzito ufundi wa kubuni lakini inafinya mawanda ya fasihi kwani inahusisha mawazo yaliyo bora tu.

3.     Fasihi ni tokeo la matumizi ya lugha kwa njia isiyokuwa ya kawaida ili kuleta athari maalumu.Waasisi wa mtazamo huu ni Roman Jakobson,Boris Tomashevsky na Viktor shklovisky.Wataalamu hawa wanasema Fasihi hukiuka taratibu za kawaida za matumizi ya lugha katika sarufi,maana na sauti ili kumvutia na kumuathiri msikilizaji au msomaji.

Ø Udhaifu wa mtazamo huu ni kuwa humfanya msomaji aitafakari lugha yenyewe badala ya kuutafakari ujumbe unaowasilishwa na ujumbe huo

Ø Vilevile fasihi inaonekana kuelemea zaidi upande wa fani na kupuuza maudhui,maana na muktadha wa kazi za fasihi.

4.     Fasihi ni sanaa ya lugha yenye ubunifu bila ya kujali kama imeandikwa au la.Mtazamo huu unaafikiwa na Peter Kirumbi (1975) ,Aldin Mutembei (2006) na F.E.M.K Senkoro (2011) ambapo wao wanaona hata nyimbo na masimulizi ya kisanaa ni fasihi ijapokuwa hayakuandikwa.Mfano Kirumbi anasema kuwa Fasihi ni taaluma ya sanaa inayowasilishwa kwa njia ya lugha katika muundo wa maandishi au matamshi.

Mtazamo huu ndio unaotawala katika taaluma ya fasihi.Inadaiwa kuwa neno fasihi limetokana na neno ‘Fasuh’’ la kiarabu lenye maana ya ufasaha au uzuri wa lugha.Hivyo istilahi ‘fasihi’ katika taaluma ya Kiswahili inatofautiana na istilahi ‘Literature’’ inayotumika katika kiingereza. Hivyo neno fasihi halihusiani na maandishi wala vitabu,bali linahusiana na ufasaha wa kauli.Kwa ujumla dhana hii katika Kiswahili inazingatiaaina zote za fasihi,yaani fasihi simulizi na andishi.Mtazamo huu umehusisha fasihi na sanaa itumiayo lugha ya maandishi au mazungumzo.

Ø Hata hivyo tatizo lake ni kutokuonesha uhusiano wa fasihi na jamii.

5.     Fasihi ni kioo cha jamii (maisha),Muasisi wa nadharia hii ni F.Nkwera (1978).Nkwera anafananisha fasihi na kioo.Anasema fasihi ni kioo na mwonzi wa maisha ya mtu na jamii.Kwa maana kwamba mtu anaweza akajitazama akaona taswira yake na akajirekebisha.Taswira hiyo inaweza kuwa nzuri au mbaya.Taswia nzuri ni matendo mazuri yanayofanywa na jamii na taswira mbaya ni matendo mabaya au maovu yanayofanywa na jamii.

Udhaifu/Dosari /kasoro ya nadharia hii:

Ø Kuona tu makosa au udhaifu Fulani katika jamii bila kurekebisha hakuwezi kuisaidia jamii kujitoa kutoka katika hali mbaya na kuingia katika hali nzuri/bora kimaisha.

Ø Kioo hakiwezi kuonesha sehemu zote za mwili

Ø Kioo hakiwezi kumweleza  mtu jambo lakufanya ili hali yake iwe bora zaidi

Ø   Si sehemu zote takazojiona kwenye kioo

6.     Fasihi ni hisi,Waasisi wa nadharia au matzo huu ni “John Radhani (1973),M.Balisidya (1973) na Tigiti Sengo na Saifu Kiango ’’ katika kitabu chao  kilichoitwa ‘Hisi Zetu’,Fasili hii ina maana kuwa lazima pawe na mguso fulani wa mwandishi ndipo mtu aweze kuandika na kueleza jambo Fulani.Wanasema “hisi ni kama kuona njaa, baridi, joto, uchovu pengine kuumwa. Hapa swali la kujiuliza ni kwamba, je fasihi ina maana moja kati ya hiyo? Uamuzi wa kutenda jambo huja wakati umeguswa?. Je hizo hisia ziko wapi? Je mtu ambaye haguswi  sana moyoni hawezi kuwa mwanafasihi  mashuhuri? Je mwanamuziki ambaye huusifu uzuri wa mwanamke anaguswa moyoni? Je mwandishi kama Shaban Robert,  E. Kazilahabi wameguswamara ngapi? Vile vile kivipi waguswe Zaidi ya wengine?  (Sengo na Kiango)

 

Udhaifu/Dosari/Kasoro za nadharia hii

Ø Ikiwa ili mtu aandike kazi ya fasihi lazima awe ameguswa,waandishi wenye kazi nyingi wameguswa mara ngapi,na kwanini waguswe wao zaidi ya wengine?

Ø Fasihi inaweza kuelezea hisi,kupitia mtindo wa fasihi,lakini fasihi yenyewe si hisi aidha fasihi huweza kuelezea mapenzi lakini yenyewe si mapenzi.

7.     Fasihi ni mwamvuli wa mtu na jamii na utu na maisha ya hadhi na taadhima.Muasisi wa nadharia hii ni Sengo T na Kiango S.D (1973).Fasihi  hii ina maana kwamba mwamvuli humkinga mtu katika mvua na jua na fasihi huhifadhi na kukinga amali za jamii zisiharibike maana hii ni nzuri kwani inasisitiza utunzaji wa kile kizuri kwa maana kuwa jamii inachambua kuwa makini na kuona amali za jamii zinazohifadhiwa. Lakini swali la kujiuliza ni kwamba jamii itasaidiwa?

Jamii haitulii kama maji katika mtungi  bali hubadilika mara kwa mara kutokana na nguvu za migongano, hivyo kitu kipya huzaliwa na cha zamani hufa kwasababu jamii haitulii, hivyo hakuna haja ya kuhifadhi amali za jamii chini ya mwamvuli. Zipo mila na desturi zilizohifadhiwa na makabila mengi ambazo hazina nafasi leo. Hali ya mabadiliko ya jamii kutokana na siasa, utawala, uchumi, elimu, sayansi na teknolojia vyote hivi katika maendeleo vitatoboa mwamvuli na kuziharibu amali zilizohifadhiwa.

Udhaifu/Dosari/Kasoro za nadharia hii

Ø Nadharia hii haijazingatia mabadiliko mbalimbali yanayoikumba jamii kisiasa,kijamii na kiuchumi kwani baadhi ya mila na desturi zilizohifadhiwa hazifai na zimepitwa na wakati,mfano ukeketaji ,ndoa za utotoni,ukabila n.k

 

8.     Fasihi ni sanaa ya uchambuzi wa lugha yoyote kadri inavyosemwa,inavyoandikwa na kusomwa,Hii ni kweli kuwa fasihi lazima itumie lugha kwani lugha ndicho chombo muhimu kitumiwacho na fasihi na si fasihi  tu bali taaluma zote hutumia lugha.Udhaifu wa fasili hii ni kwamba maana hii imejikita katika uchambuzi wa Lugha kana kwamba hakuna vipengele vingine vinavyochambuliwa katika fasihi zaidi ya lugha na hii ni sawa na kusema umeme ni waya wa shaba kwa vile umeme umepita kwenye waya huo.Na hii ni si kweli kwani Hisabati,fizikia au historia si fasihi ingawa hutumia lugha.

Udhaifu/Dosari/Kasoro za mtazamo huu

Ø Nadharia hii imejikita katika kuchambua kipengele  kimoja tu cha lugha na kusahau vipengele vingine vya fani namaudhui vinavyokamilisha kazi ya fasihi,vikiwemo mtindo,muundo,wahusika,mandhari,dhamira,ujumbe,n.k

Ø Kuna taaluma nyingi zinazotumia lugha kama vile fizikia,baiolojia,geografia,kemia n.k ingawa si kazi za fasihi.

9.     Fasihi ni kielelezo cha hisia za mwandishi juu ya mambo yanayomwathiri yeye,kikundi au jamii nzima anamoishi na kwamba lengo lake ni kustarehesha au kufunza wasomaji.Fasili(maana) hii ni nzuri kwa ujumla lakini mapungufu yake ni kwamba imemuwekea mwandishi kama chanzo pekee cha uumbaji wa Sanaa na hasa akili yake pia maana hii imetokana  na falsafa ya kidhaanifu kwa kuhusisha uchambuzi wa mambo katika fikra bila  kutazama hali halisi ya maisha ya watu na vitu.

Udhaifu/Dosari/Kasoro za mtazamo huu

Ø Nadharia hii imepuuza baadhi ya sababu zinazowafanya watunzi wa kazi za fasihi kutunga kazi zao kwaajili ya kujipatia fedha (fasihi pendwa) ambazo maudhui yake kwa kiasi kikubwa yamejikita kwenye kuburudisha zaidi na hayana uhalisi.

Ø Fasili au maana hii haijazingatia hali halisi ya maisha ya watu bali imejiegemeza katika mtazamo au falsafa ya kdhanifu kwa kuangalia fikra za mtu binafsi na sio uhalisia wa maisha ya jamii.

   10.    Fasihi ni chombo cha utetezi wa maslahi ya tabaka moja au jingine na kwamba mwandishi ni mtumishi wake anayejijua au asiyejijua atake asitake mwandishi huyu analengo au dhamira fulani anayotaka kuionesha.Wasomaji wanaweza kuyakubali au kuyakataa maudhui ya kazi yake na pengine jamii kufuatana na msimamo juu ya itikadi ya siasa (napengine amali za jamii)inayotawala kwa kipindi hicho  na jinsi mwandishi anavyooanisha maandishi yake na itikadi hiyo.

Fasili au maana hii ni nzuri sana kwani kwa kifupi ni kwamba fasihi ni mojawapo ya silaha nyingi zinazotumiwa na tabaka moja kutetea maslahi yake katika mapambano ya kudumu dhidi ya matabaka mengine.

Hitimisho kwa ufupi fasihi ni taaluma inayotumia Sanaa maalumu ya lugha ili kufikisha ujumbe kwa jamii inayohusika.Fasihi hutueleza uzuri wa maandishi au mazungumzo ambayo huonekana katika mashairi ,historia za maisha ya watu ,tenzi,hadithi za kusisimua na insha mbali mbali.

 

DHIMA YA MWANAFASIHI KATIKA JAMII

Maana ya mwanafasihi/mtunzi wa kazi ya fasihi

Ni mtu yeyote anayejishughulisha na uandishi au utungaji wa kazi za fasihi yaani fasihi andishi na fasihi simulizi.

 

SIFA  ZA MTUNZI WA KAZI ZA FASIHI/ MWANAFASIHI

Mwanafasihi au mtunzi wa kazi za fasihi anatakiwa awe na sifa muhimu zifuatazo;

Ø Aitambue kwa kina hadhira yake.Hii ni pamoja na kuelewa kiwango cha elimu cha watu wanaowaandalia kazi husika.

Ø Atambue kwa kina matatizo yanayoikabili jamii yake na atafute mbinu sahihi za kuyatatua.

Ø Ajue migogoro inayoikabili jamii yake na atafute suluhisho la migogoro hiyo.

Ø Afahamu  kwa kina utamaduni wa jamii yake.Hii ni pamoja na kutambua lugha,mila,desturi na mienendo ya maisha ya jamii husika.

Ø Afahamu vizuri itikadi na mifumo mbalimbali inayotawala jamii yake.Hii inajumuisha itikadi za kisiasa ,kiuchumi,kijamii na kiutamaduni

Ø Awe na uwezo mkubwa wa kuoanisha fani na maudhui ya kazi ya fasihi na uhalisia wa maisha ya jamii husika.

Ø Aitambue vyema historia ya jamii yake.

Ø Awe mbunifu wa hali ya juu katika kutumia vipengele vya fani vitakavyorahisisha ufikishaji wa maudhui kwa jamii iliyokusudiwa

 

 

DHIMA ZA MWANAFASIHI

1..Kuelimisha jamii,Mtunzi wa kazi za fasihi au mwanafasihi huwafumbua macho watu kwa kuweka wazi maovu yanayofanyika katika jamii kama vile uonevu,rushwa ,wizi,ukeketaji ,umalaya,udikteta,usaliti ,unafiki n.k. Wanaotenda maovu hayo hukosolewa na wanafasihi ili kuacha tabia hiyo hivyo kupitia watunzi wa kazi za fasihi jamii huanza kupambana ili kudai haki  na usawa kwa wote.Mfano Wasakatonge ( 2003) na mashairi ya chekacheka waandishi wameikosoa jamii ya Tanzania kwa kupiga vita dhuluma,unyonyaji,matabaka,uongozi mbaya,usaliti ,uonevu n.k maovu wanayofanyiwa  watu wa hali ya chini kimaisha.Pia Tamthiliya ya Ngoswe –Penzi kitovu cha Uzembe ( 1988) mwandishi anaikosoa jamii kwa kupiga vita suala la uzembe ,mapenzi kazini,uvivu,ndoa za mitala,imani potofu na ulevi.

2.Kuburudisha,zipo kazi mbalimbali za fasihi zinazoburudisha.Msomaji au msikilizaji wa fasihi huburudisha yaani husisimsha mwili na akili na huvutiwa kihisia na kazi ya fasihi anayoisoma au kusikiliza.Tabia ya msomaji au msikilizaji huweza kujengwa kutokana na mafunzo na mifano bora ya matendo ya kuigwa anayoyapata katika fasihi.

3.Kuhifadhi na kurithisha amali za jamii,Amali za jamii ni pamoja na mila na desturimtindo wa maisha,Imani, historia jiografia,visasili na visakale ni urithi wa maarifa ya kijadi kwa mfano tiba, sayansi ya kilimo,mbinu za uwindaji,ufundi wa aina zote n.k.Amali hizo huweza kuhifadhiwa na kuendelezwa na mwanafasihi na hivyo kurithishwa kwa vizazi vijavyo.

Kwa mfano tamthiliya ya Kinjikitile inahifadhi mengi kuhusu hali ya maisha wakati wa ukoloni wa kidachi,Kurwa na Doto (1969) ni riwaya yenye kuhifadhi japo kwa kejeli,mila,desturi na itikadi za jadi za waunguja,Riwaya ya BwanaMnyombokero na Bibi Bugonoka;Ntuhanalwo na Buliwaliiliyoandikwa na Anicet Kitereza imehifadhi mila,Imani,mtindo wa maisha,ufundi na taaluma mbalimbali za jadi za wakerewe mengi yaliyoeleza humo siku hizi hayapatikani popote isipokuwa katika riwaya hiyo, vile vile Mzishi wa Baba ana Radhi(1967) kinaeleza mila na desturi za wapangwa.Watunzi hasa nyimbo na visasili hukoleza pia shughuli za kijadi za kiutamaduni kwa mfano Ibada,matambiko,sherehe,katika shughuli za aina hiyo nyimbo licha ya kuwa kiburudisho hubeba ujumbe wenye kuhusiana na tukio hilo.

4.Kudumisha na kuendeleza lugha,Kwa kadri lugha inavyotumiwa na kufinyangwa na watunzi ndivyo inavyokuwa na kupevuka.Maneno mengi yatumiwayo leo katika lugha mbalimbali yalibuniwa na kuenezwa na watunzi wa mashairi,riwaya,nyimbo na tamthiliya katika Kiswahili.Mifano mizuri ni maneno mengi yahusuyo Sanaa ya ushairi(vina, mizani, beti, mishororo, miwala, tathlitha, takhimisa, tarbia n.k)

Katika jadi ya ushairi wa kiswahili inadaiwa kuwa ushairi ulikua ni ghala ya maneno.Washairi walitumia maneno magumu au yasiyokuwa ya kawaida makusudi ili kuyahifadhi ysipote.katika tamaduni nyingine kazi hiyo hufanywa na kamusi pamoja na vitabu viitwavyo Hazina ya maneno kwa kuwa waswahili hawakuwa na kamusi kazi ya kuhifadhi maneno ilifanywa na ushairi.

DHIMA ZA MHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI

Uhakiki ni kazi au kitendo cha kuchambua au kufafanua kazi ya fasihi, kuweza kupata maadili na ujumbe uliomo katika maandishi  ya mwandishi asilia.

AU  ni sayansi maalumu ya kuchambua na kuona ubora wa kazi hizo kwa kutumia vipengele mbalimbali vya fani na maudhui na kuangalia uwiano na uhusiano ama kuathiriana kwake. Uhakiki ni elimu na ujuzi wa kuipembua kazi ya sanaa inayohusika kimaudhui na kifani.

Uhakiki ni daraja ya juu ya maelezo ya kisanii yenye kuwalenga watu wa aina tatu:- wasomaji wa kawaida walio nyumbani na shuleni, waandishi asilia wa kazi za sanaa na wahakiki.Msomaji hupata mwongozo wa namna bora zaidi ya kumwezesha kuifahamu kazi ya sanaa kutokana na viwango tofauti vya uhakiki juu ya kazi za sanaa.

 

Mhakiki ni nani?

Mhakiki ni mchambuzi na mfafanuzi wa maandishi ya kisanaa hasa yale ya kifasihi. Ni jicho la jamii kwa vile anagundua mazuri yaliyomo katika kazi ya fasihi na pia ndiye anayeona hatari ya maandishi hayo kwa jamii. Mhakiki ni bingwa wa kusoma na kuchambua maudhui, maadili na ujumbe uliomo katika maandishi ya fasihi.

Ni mtu mhakiki anajihusisha na maandishi  ya waandishi asilia na hungalia kwa jinsi gani mwandishi anawakilisha hali halisi ya jumuiya ya watu. Kwa upande mwingine, mhakiki anashughulikia uwanja wa fasihi andishi pamoja na ule wa fasihi simulizi.

 

Sifa za mhakiki

Ø Ajue historia na mazingira yaliyomkuza mwandishi.Mhakiki ili aweze  kuifanya kazi yake vizuri anapaswa aelewe vema historia ya mwandishi na jamii yake inayohusika. Aelewe asili ya mwandishi, historia yake na utamadumi wake kwa ujumla. Kutokana na hali hii, mhakiki anaweza kuelewa kama mwandishi amefanikiwa kueleza ukweli wa maisha ya watu, yaani jamii inayohusika.

Ø Aelewe historia na siasa ya jamii inayohusika.Hii itamwezesha kuyaelewa matatizo ya jamii hiyo. Mhakiki lazima aifahamu barabara jamii ambayo mwandishi aliandikia juu yake ili aweze kuandika uhakiki imara, ama sivyo atakwama na kuandika uhakiki dhaifu. Mhakiki anapaswa kuelewa historia ya watu ambao maandishi hayo yanawahusu, bila kuifahamu historia yao, itakuwa vigumu kwake kueleza bayana baadhi ya mambo ambayo mwandishi aliandika na kwa nini aliandika hivyo. Uhakiki wake ukisomwa na watu wanaoishi katika jamii hiyo si ajabu kusema yeye si mhakiki. Mhakiki huangalia jinsi gani mwandishi alivyoiwakilisha hali halisi ya jumuiya na historia ya watu hao.

Ø Awe amesoma kazi mbali mbali za fasihi na siyo ile tu anayoifanyia uhakiki. Hii itamsaidia kuwa na ujuzi zaidi katika uwanja wa uhakiki.

Ø Asome tahakiki za wahakiki wengine katika uwanja wa fasihi na hata nje ya jamii yake ili kupata upanuzi zaidi katika kazi ya uhakiki. Hii itamsaidia kutoa uhakiki bora zaidi, kwani atakuwa amejifunza yale yaliyo mazuri na kuepuka makosa waliofanya wengine.

Ø Lazima awe na akili pevu sana ili aweze kung’amua mambo na akishayang’amua ayaandike kwa lugha rahisi ili mawazo yake yasomeke na kila mtu kwa urahisi, yaani atumie lugha ambayo itawatumikia wasomaji wake.

Ø Lazima ajiendeleze katika taaluma mbali mbali ili aweze kuwa na mawazo mengi ambayo yatamsaidia kuhakiki maandishi mbali mbali. Mhakiki hodari huichonga jamii yake kimawazo. Huiimarisha isitetereshwe au kupofushwa na waandishi wapotoshaji.

Ø Awe na uwezo wa kuchambua mambo kisayansi bila kuonyesha hisia za wasomaji. Asiwe na  majivuno na awaheshimu  anaowahakiki  na anaotaka wasome uhakiki wake. Asichukie au kusifia tu kazi za waandishi kwa sababu zake binafsi bila kueleza ukweli wa kazi hiyo. Mhakiki ni rafiki wa mwandishi na wasomaji . Kwa hiyo, mhakiki ni lazima awe fundi katika kutoa hoja zake na lazima ziwe zinagonga, zenye kuibua udadisi na kuathiri.

Ø Asiwe mtu wa kuyumbishwa na maandishi au maneno ya wahakiki au watu wengine. Tunatarajia aseme kweli kuhusu kazi hiyo.Uhusiano baina ya mhakiki na mwandishi usiathiri uhakiki wake.

 

TAHAKIKI NI NINI?

Ni kitabu kinachotolewa na mhakiki kinachambua vitabu mbali mbali vya maandishi asilia. Tahakiki hutoa uchambuzi na uhakiki wa vitabu vya hadithi/tamthiliya/ushairi kwa kuzingatia vipengele vya fani na maudhui. Mfano wa tahakiki ni kama vile:- Senkoro(1988). Ushairi: Nadharia na Tahakiki. DSM: DUP,Kiango, Msokile na Sengo (1987), Uhakiki wa vitabu vya Fasihi Sekondari na vyuo. NPA, n.k.

 

Dhima ya mhakiki

·        Kuchambua na kuweka wazi mafunzo yanayotolewa na kazi za fasihi:Hapa mhakiki anatoa ufafanuzi wa kimaudhui wa kazi ya fasihi. Mhakiki husoma kwa uangalifu kazi ya fasihi.Baada ya kusoma kwa makini, hutafakari na kuchunguza maudhui, maadili na ujumbe ambao mwandishi amekusudia kuwafikishia wasomaji wake na jamii inayohusika.

·        Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi:Mhakiki huwasaidia wasomaji ili wasishindwe kuyaelewa maudhui barabar kutokana na kukanyagwa na usanii. Matumizi, mathalani ya ishara ni baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kumkanyaga msomaji ambaye hajapata utaalamu mkubwa wa kuchambua.

Mhakiki wa kufichua ishara fulani ina maana kuwa amemsaidia msomaji kupata ujumbe kikamilifu.

Kuhusu matumizi ya picha, kwa kawaida, lugha ya picha ina mguso sana na huibua hisia Fulani  na hata kuchekesha au kuwafanya watu walie machozi. Mhakiki sharti awaambie kwamba, matumizi ya picha ni mbinu mojawapo inayosaidia maudhui kuwaganda wasomaji. Picha inayochekesha, kufurahisha, kukejeli, n.k. Haikomei pale tu, kwani baada ya kucheka, n.k. msomaji huathiriwa sana kinafsi na aghalabu huachiwa mafunzo fulani. Hivyo mhakiki lazima achambue na kuyaweka wazi mafunzo yanayotolewa na picha hiyo.

·         Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora zaidi, Mhakiki anamfundisha mwandishi juu ya yale anayoyasema yanavyoweza kupokelewa na jamii. Humwonyesha msanii uzuri na udhaifu wa kazi aliyoisaini. Kitendo hiki humfanya msanii ajifunze mambo yapi ni mazuri na yapi ni mabaya kama anavyoelekezwa na mhakiki, na hivyo humfanya awe na nafasi nzuri ya kuirekebisha kazi hiyo atakapoishughulikia kazi nyingine. Kwa msingi huo, mhakiki anaweza kulaumu au kusifu/kumpongeza mwandishi wa kazi yoyote ya kisanaa.

·         Kumwelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko ile ambayo angeweza kuipata bila dira ya mhakiki:Mhakiki huifunza jamii namna ya kupokea na kuifurahia kazi ya sanaa. Vilevile mhakiki huwasaidia wasomaji kuyabaini maandishi yaliyo sumu kwa jamii. Mhakiki lazima ayafichue maandishi hayo ili yasieneze sumu kwa jamii. Mhakiki lazima ayafichue maandishi hayo ili yasieneze sumu kwa jamii inayohusika.

·         Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi ya fasihi:Kutokana na ushauri anaopata mwandishi kutoka kwa mhakiki, humfanya awe makini zaidi wakati wa kushughulikia kazi nyingine.Vilevile wasomaji wanakuza kiwango chao cha usomaji kwa kufuata mawaidha ya mhakiki.

·         Kusema wazi kuhusu kiwango cha maandishi anayohakikiwa:Akisema wazi kwamba, maandishi hayo yako katika kiwango cha chini, mara mwandishi huyo asilia atakapoamua kutunga tena, atashawishika kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu zaidi. Na waandishi wengine watapatiwa msukumo wa kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu zaidi. Na waandishi wengine watapatiwa msukumo wa kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu pia. Na hivi ndivyo mhakiki anavyosaidia kukuza na kuendeleza maandishi ya taifa lake.

·        Kuheshimu na kuthamini kazi za waandishi na kuzifanyia haki:Jambo la msingi (lazima) kuzingatia na kuwa, mhakiki afanyapo kazi yake huwa vitani. Mhakiki anapaswa kujua namna ya kuwanasa wasomaji bila wao kujitambua na kuwa na uwezo au kuchambua kisayansi mambo bila kutoonyesha hisia za wasomaji. Anatakiwa asiwe na majivuno na aheshimu anaowahakiki na anaowataka wasome uhakiki wake. Awachukue hatua kwa hatua kifalsafa hata waone vigumu, na kwamba haiwezekani kupigana naye.

 

 

 

MISINGI YA UHAKIKI WA KAZI ZA KIFASIHI

Uhakiki wa kazi za kifasihi hufanywa kwa kuzingatia vipengele vya fani na maudhui. Fani na maudhui ni kama masanduku makubwa ambayo mhakiki huyafungua na kuanza kuchunguza vilivyomo ndani yake. Kila moja lina vipengele vidogovidogo ndani yake.

(a)Fani

Fani ni mbinu au ufundi anaobuni na kutumia mtunzi wa kazi ya kifasihi ili kufikisha ujumbe  kwa hadhira yake iliyokusudia. Fani ina vipengele mbalimbali. Vipengele hivyo ni pamoja na wahusika, mandhari, lugha, muundo na mtindo.

1.      Muundo

Ni mpangilio na mtiririko wa kazi hiyo kwa upande wa visa na matukio. Hapa tunachunguza jinsi msanii wa kazi ya fasihi alivyofuma, alivyounda na alivyounganisha tukio moja na jingine, kitendo kimoja na kingine, wazo na wazo, sura moja na nyingine, ubeti na ubeti, hata mstari wa ubeti na mwingine.

          AINA ZA MIUNDO

(a) Muundo wa msago, ni muundo wa moja kwa moja ambao tunafatilia matukio mbalimbali tangu la kwanza hadi la mwisho kwa mbinu ya utelezi. Kwa mfano, mhusika huzaliwa, hukua, huchumbia au kuchumbiwa, huoa au kuolewa, huzaa watoto, huzeeka, hufa. Riwaya ya kuli (1978) imetumia muundo huu. Katika riwaya hii tunamwona Rashidi akizaliwa, akikua, anaanza kazi, anaoa, anaanza harakati za kudai haki za makuli na mwisho anafungwa.

(b) Muundo wa kioo, ni muundo wa kimchangamano utumiayo mbinu ambayo huweza ama kumrudisha nyuma msomaji wa kazi aya fasihi katika mpangilio wa matukio yake au kuipeleka mbele hadhira ya kazi hiyo. Riwaya ya Zaka la Damu (1976)  imetumia muundo huu.

(c)  Muundo wa rukia, ni muundo ambao visa hupandana. Katika muundo huu kunakuwa na visa viwili ambavyo hupandana katika kusimuliwa kwake, na mwisho visa hivi huungana na kujenga kisa kimoja. Mfano ni riwaya ya Njama (1981).

Katika ushairi muundo tunaangalia idadi ya mistari katika kila ubeti wa shairi. Kuna miundo ya aina mbalimbali:

 

(i)                Muundo wa Tathnia – kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari miwili.

(ii)             Muundo wa Tathlitha – kila ubeti unakuwa na mistari mitatu.

(iii)           Muundo wa Tarbia – kila ubeti unakuwa mistari minne.

(iv)            Muundo wa Takhimisa – kila ubeti unakuwa na mistari mitano.

(v)             Muundo wa Sabilia – kila ubeti unakuwa na mistari sita na kuendelea.

2.     Mtindo,ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi hiyo na kuipa sura ambayo kifani na maudhui huainisha kanuni au kaida zilizofuatwa kama ni zilizopo au ni za kipekee.Mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hatimaye hutokeza au huonyesha nafsi na labda upekee wa mtungaji wa kazi hiyo.

 

VIPENGELE VYA MTINDO

Mtindo wa kazi za fasihi hujidhihirisha katika vipengele mbalimbali vya kazi hizo.Baadhi ya vipengele hivyo ni;

( i) Utomelezi;Humaanisha matumizi ya tanzu au vipengele vingine ndani ya utanzu mmoja.Mathalani,utomelezi huweza kufanywa kwa kupachika barua,nyimbo,shairi au hotuba katika kazi inayoshughulikiwa.Mfano wa utomelezi ni matumizi ya ushairi ndani ya hadithi au barua ndani ya hadithi kama ilivyo katika  Njozi Iliyopotea (C .Mung’ong’o 1978) na Mtendwa Hutendwa (Rose  Mbijima,2019)

( ii ) Dialojia (Majibizano): Hapa wahusika wanajibizana wao kwa wao.Ni mtindo wa kitamthiliya wenye kutofautisha tamthiliya na tanzu nyingine.Mtindo huu utaitwa mtindo mmojawapo kati ya mitindo iliyotumika katika kazi ya fasihi iwapo msanii atautumia katika utanzu mwingine tofauti na tamthiliya.

( iii ) Matumizi ya masimulizi na maelezo; Huu ni mtindo maarufu unaopambanua utanzu wa riwaya kutoka katika tanzu nyingine.Wakati mwingine,mtindo huu hujitokeza katika tanzu nyingine tofauti na riwaya.Hali hii inapotokea huchukuliwa kama mtindo wa mwandishi.

( iv ) Matumizi ya Nafsi: Nafsi ni kitu muhimu sana katika kazi za fasihi.Nafsi hutupatia  nafsi ya mwandishi na wahusika katika kazi Fulani.Kuna nafsi tatu ambazo ni; nafsi ya kwanza,ya pili nay a tatu.Msanii anaweza kutumia nafsi ya kwanza hasa katika kazi zenye uhusiano wa karibu na historia yake lakini si kila kazi ya fasihi yenye  mtindo wa aina hii huchukuliwa kama historia ya maisha ya mwandishi kwani kuna kazi zenye mtindo huu ambazo zinaelezea vitu ambavyo havihusiani na maisha ya mwandishi.

Ø Nafsi ya kwanza hutumiwa na msanii kwa lengo la kuifanya hadhira ijihisi  kuwa ni mshiriki katika yale yanayoongelewa na mwandishi.

Ø Nafsi ya pili huonesha kutohusika moja kwa moja kwa mwandishi juu ya mambo yanayozungumziwa ndani ya kazi husika.Wakati mwingine nafsi ya pili hutumiwa kama njia mojawapo

Ø Nafsi ya tatu hutumika katika kazi ili kuelezea matendo au tabia ya mtu mwingine

( v ) Mbinu ya kuhoji:Hii ni mbinu inayotumiwa na msanii katika kuelezea mawazo yake kwa hadhira.Kunakuwa na hali ya kuhoji hata kama masuala yanayoongelewa yanaeleweka.Pamoja na malengo mengine,mbinu hii hutumiwa kumfikirisha msomajia ua msikilizaji.Mbinu hii imetumika mwishoni mwa riwaya  Rosa Mistika ( Euphrase Kezilahabi 1971)

( vii ) Matumizi ya barua: Msanii anaweza kutumia mtindo wa barua katika kuandika kazi yake kama ilivyo katika ‘’Barua Ndefu Kama Hii’ (Mariam Ba 2009)

Kwa upande wa ushairi kuna aina mbalimbali za mitindo kama ifuatavyo;

(  i ) Mtindo wa kidato:Ni mtindo ambao baadhi ya mistari hufupishwa maneno yake au silabi zake tofauti na mistari mingine ambayo huwa na silabi au maneno mengi.Ufupishaji huu wa maneno au silabi  katika baadhi ya mistari hufanywa kwa lengo maalumu.Kwa mfano,katika shairi la Fumbua

(ii )  Mtindo wa pindu ; Hujidhihirisha pale ambapo neno au sehemu ya neno  la mwisho katika kipande au mstari  hurudiwa  mwanzoni mwa kipande au mshororo unaofuata. tazama mfano wa ubeti ufuatao.

 

Zuko.

Tika kitupu hutika, tika upya unafuka,

Uka huko ukaleni, leni mapya kulafuka,

Fukara we mzamani, ma’ni mapya hutataka,

Takataka mawazoni,zoni huna hukushika,

Shika-mimi sishikani, kanizo zapukutika.

 

Kulikoyela kahigi, katika mugyabuso mulokozi na kulikoyela kahigi,kunga za ushairi na diwani yetu (1982:79)

 

(iv)Mtindo wa kiitiko (kituo): Ni mtindo ambao mstari wa mwisho hujirudiarudia kwa kila ubeti.Mfano mzuri ni shairi la kwetu ni kwao kwa Nini? Mwandishi anasema:

Mtu huuliza nini,kitu hiki ni cha nini?

Kitu hiki cha nani,na hiki kitu cha nini?

Nacho kinaitwa nini,na cha nani na kwa nini?

Kwetu ni kwao kwa nini,na kwao kwetu kwa nini?

 

Na kwa nini cha nani,na chake kwa njia gani?

Jawabu liwe yakini,lisiwe purukushani?

Kwa nini sababu gani?kwao ni kwetu kwa nini?

Kwetu ni kwao kwa nini?na kwao kwetu kwa nini?

 

 

Kwa nini kwao kwa nini,kuwe kwetu ni kwa nini?

Na kwetu pia kwa nini?kuitwa kwao kwa nini?

Kwa nini ina yakini,kwetu ni kwao kwa nini?

 Kwetu ni kwao kwa nini,na kwao kwetu kwa nini

 

Mtu kwao huthamini,ijapokuwa jiweni,

Pia alale mtini,na baraza liwe chini,

Nile matunda porini,kuitwa kwenu kwa nini?

Kwetu ni kwao kwa nini,na kwao kwetu kwa nini?

Saadani kandoro,Mashairi ya saadani(1972:138-139)

 

 

3.     Wahusika

Wahusika wa kazi ya kifasihi ni viumbehai au wasio hai; halisi au wa kubuni, ambao wanatenda matendo mbalimbali ndani ya kazi ya kifasihi. Wahusika wanaweza kuwa ni binadamu, mawe, miti, malaika, miungu na mizimwi. Kwa kawaida, wahusika katika kazi ya kifasihi hutumika kuwakilisha au kubainisha maisha halisi ya wanadamu.

Aina za wahusika

Wanafasihi mbalimbali wamewagawa wahusika katika makundi tofauti. Hata hivyo, sisi tutawagawa katika makundi makuu mawili, yaani wahusika wakuu na wahusika wadogo.

·        Wahusika wakuu

Mhusika mkuu ni mhimili wa kazi ya kifasihi na huonekana kuanzia mwanzo hadi mwisho wa kazi ya kifasihi. Mhusika mkuu ndiye wa muhimu kabisa kuliko wote. Huyu ndiye anayehusiana zaidi na dhamira kuu ya kazi inayohusika.

·        Wahusika wadogo

Hawa ni wahusika wanaomsaidia mhusika mkuu kufikisha ujumbe wa mtunzi kwa hadhira. Kwa kawaida, wahusika wadogo huchomoza hapa na pale kwenye kazi ya kifasihi, kisha huweza kutoweka kwa muda au kutoweka kabisa. Kwa mfano, mhusika mdogo masikini anaweza kupambanishwa na mhusika mkuu ili kubainisha ukarimu au uchoyo wa mhusika mkuu, kisha huyo mhusika mdogo hatumwoni tena. Wahusika, wawe wakubwa au wadogo, wanaweza kuwa duara, bapa au shinda:

§  Wahusika duara

Wahusika duara (au mviringo) ni wahusika wenye sifa halisi za ubinadamu, yaani wanaonekana ni binadamu halisi. Hii ni kwa sababu wanabainisha katika maisha yao uzuri na ubaya – wema na uovu, ujasiri na woga, ushindi na kushindwa. Pia, wanabadilika kiakili, kimtazamo na kimaadili kadiri wanavyokutana na changamoto za kimaisha kama ilivyo kwa binadamu halisi.

§  Wahusika bapa

Hawa ni wahusika ambao hutokea wakiwa na tabia ya aina moja kuanzia mwanzo hadi mwisho.Wao hawakui au kubadilika,bali hubakia na msimamo au mtazamo ule ule walioanza nao. Kama ni mchoyo, anakuwa ni mchoyo kuanzia mwanzo hadi mwisho.

§  Wahusika shinda

Hawa ni wahusika ambao wako katikati ya wahusika duara na bapa. Wahusika hawa wanaweza kubadilika, lakini si kutokana na misimamo yao, bali ni kwa sababu ya kuyumbiswa na wahusika wengine. Ni wahusika ambao hawajitegemei kimawazo.

Tunaweza kuonyesha aina za wahusika kwenye mchoro kama ifuatavyo:

 

Wahusika

Wadogo

Wakuu

Duara

Bapa

Shinda

Duara

Bapa

Shinda

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


4.     Mandhari

Mandhari ni mahali ambako matukio ya kwenye kazi ya kifasihi yanatokea.Mandhari yanaweza kuwa halisi au ya kubuni tu. Kwa mfano, mtunzi anaweza akawaweka wahusika wake kwenye Jiji la Dar es Salaam. Haya ni mandhari halisi.

Vilevile, anaweza kuwaweka wahusika kwenye nchi iliyoko chini ya bahari au kwenye jua. Hayo yanakuwa si mandhari halisi bali ni ya kufikirika  au ya kubuni tu.Kwa hiyo, mandhari yanaweza yakawa mjini au kijijini, msituni au baharini, chini ya ardhi au angani.

 

5 .Matumizi yaLugha

Lugha ndiyo malighafi kuu inayotumiwa na mtunzi kuzalisha kazi ya kifasihi. Lugha ya kifasihi ni lugha yenye mvuto kwa vile husheheni maneno ambayo yameshibishwa taswira au picha, yaani ni lugha ya picha.Lugha ya kifasihi ni ya picha kwa kuwa ina mambo yafuatayo:

 

(a) Nahau

       Haya ni maneno, aghalabu mawili au zaidi, ambayo maana yake ya jumla ni tofauti na maana ya neno mojamoja ndani ya nahau hiyo. Kwa mfano, kuvunjika kwa moyo si kitendo cha moyo ulio ndani ya mwili kukatika vipande, bali ni kukata tama.Nahau hunogesha na kunakshi lugha, hivyo huongeza mvuto na kuupa uzito ujumbe uliokusudiwa.

             (b)Methali

Huu ni usemi mfupi wa hekima ambao kwa kawaida huwa umerithiwa kutoka vizazi vya nyuma, na ambao umebeba maana pana iliyojificha. Kwa mfano, kidole kimoja hakivunji chawa.

                (c)Tamathali za semi

Hii ni misemo ambayo hutumiwa kutoa maana tofauti na maana ya maneno yake. Zipo aina mbalimbali za tamathali za semi. Zifuatazo ni baadhi yake:

Ø Tashibiha

Huu ni ulinganishaji wa vitu au hali mbili tofauti kwa kutumia maneno: kama, mithili ya, sawa na, utadhani na, mfano wa.Kwa mfano:

·        Ametulia kama gogo la mnazi.

·        Tumbo limetangulia mithili ya ngoma ya gwaride.

·        Ana macho makali utadhani matone ya gongo.

Ø Sitiari

Huu ni ulinganishaji wa vitu au hali mbili moja kwa moja bila kutumia maneno: kama, mithili ya, utadhani na mfano wa.

                   Kwa mfano:

·        Kichwa chake ni benki ya majina ya shule nzima.

·        Maji ya kifuu ni bahari ya chungu.

·        Huyu mtoto atakuwa kiboko ya wote.

Ø Mubalagha

Huu ni uelezaji wa jambo kwa kutia  chumvi kuliko hali halisi ilivyo.

                   Kwa mfano:

·        Yaani Yule ana tumbo kama gunia.

·        Huyu dada anaweza kuongea hadi simu ikaishiwa chaji.

·        Kwa njaa niliyo nayo, naweza kumaliza hata mbuzi wawili.

Ø Tashihisi

Hii ni njia ya kuvipa vitu visivyo binadamu sifa za ubinadamu, kwa mfano sifa za kuongea, kufikiri, kucheka na kutoa hoja.

                   Kwa mfano:

·        Jua lilitudokolea jicho lake kali na kututemea moto wake hadi tukaenda kujificha chini ya dari.

·        Homa ile ilimng’ang’ania kwa makucha yake huku ikimvutia gizani,lakini alipambana nayo hadi ikatimua mbio.

·        Mlango ule ulitukaribisha kwenye tumbo la nyumba ile huku madirisha yakitukodolea macho kwa smshangao.

Ø Taashira

Hii ni njia ya kutaja kitu fulani  kwa lengo la kuwakilisha kitu au jambo jingine.

Kwa mfano:

·        Mwanafunzi Yule si kama wengine. Yeye ameweka kitabu mbele.(Kitabu kinawakilisha masomo.)

·        Ni vema kwa kuwa ameamua kuishi maisha ya jembe.

(Jembe linamaanisha kilimo.)

Ø Taniaba

Hii ni njia ya kutumia jina fulani kwa namna ya ulinganisho ili kumaanisha kitu kingine. Hivyo viwili vinakuwa na tabia fulani linganifu.

Kwa mfano:

·        Kiongozi Yule amekuwa ni Iddi Amini wanchi ile.

·        Sisi tunafuga mbuzi tu. Hawa ndio ng’ombe wetu.

Ø Majazi

Hii ni aina ya tamathali ambayo hutaja sehemu tu ya kitu kwa lengo la kumaanisha kitu kizima.

Kwa mfano:

·        Masomo haya yanahitaji vichwa kwelikweli. (kichwa = mtu mwenye akili)

·        Ajali ile imepoteza roho saba. (roho = mtu kamili)

Ø Dhihaka

Haya ni maneno yenye maana kinyume na vile yanavyosema, ambayo hutolewa kwa lengo la kudunisha au kushusha hadhi.

 

                   Kwa mfano:

·        Kijana huyu asione chakula; macho humtoka na miguu humwasha. Domo hujaa mate tele kama fisi aliyeona nyama.

·        Bosi wetu alikaa kwenye kiti chake, utadhani kakumbatia tungi la pombe ya kienyeji. Ama kwa hakika bosi kajaliwa tumbo. Tumbo hilo ni shimo refu ambamo zinaishia fedha za kampuni na jasho letu.

Ø Tasfida

Haya ni maneno ya heshima yanayotumika ili kupunguza ukali wa jambo linalosemwa, ambalo aghalabu, huwa aibu kulitamka mbele ya watu.

 

 

Kwa mfano:

·        Sehemu za siri                                  

·        Amechafua hewa

·        Yuko uani

Ø Shtihizai/Kejeli

Hii pia huitwa kejeli. Haya ni maneno ambayo yamekusudiwa kuleta maana kinyume na maana ya kawaida ya maneno hayo. Kwa mfano, kumwita mtu mweusi tii mzungu au cheupe; au mtu mwembamba sana kumwita bonge ni shtihizai au kejeli.

Ø Ritifaa

Katika tamathali hii, mtu huzungumza na mtu au kitu ambacho hakipo pamoja naye kama kwamba yuko nacho.

Kwa mfano:

·        “Nyerere na Karume, mlitupenda wanenu; mkatuwekea misingi ya upendo na amani. Ona sasa wameingia mbweha na fisi ulingoni. Ninajua kabisa hamngekuwa radhi nao hata kwa dakika moja!”

Mbinu nyingine

Kuna mbinu nyingine za kifasihi ambazo msanii anaweza kuzitumia, ambazo si tamathali za semi. Mbinu hizo ni pamoja na:

v Takiriri

Hii ni mbinu ya kurudiarudia manenokwa lengo la kusisitiza jambo.

Kwa mfano:

·        Wewe utafungwa, utafungwa utafungwa tu!

·        Ukifika pale ni kula, dansi; kula, dansi!

·        Rudi mwanangu; mwanangu rudi; rudi tu mwanangu; nitakupokea.

Takriri, pia inaweza kuwa ni kurudia sauti ileile katika neno zaidi ya moja ambayo yanafuatana karibu karibu.

Kwa mfano:

·        Matata alitamka maneno matano matamu. (sauti ma)

·        Sili wali ilhali ukali wa pilipili uko mbali. (sauti li)

·        Alipanda kwenye kitanda akajitanda shuka lake. (sauti nda)

 

v Tanakali sauti

Hii ni mbinu ya kuiga sauti fulani. Pia, hujulikana kama onomatopea.

Kwa mfano:

·        Kakachakakacha za kutembea kwao ziliniamsha usingizini.

·        Mara tulisikia ngo, ngo, ngo, mlangoni.

·        Kabla hatujakaa sawa, gari lile lilipita kama mshale, fyaaaa!

v Tashtiti

Katika mbinu hii, msanii huuliza swali ambalo jibu lake liko wazi.

                   Kwa mfano:

·        Kaka alipofika pale, alimwona rafiki yake akiondoka. “Unaenda kweli?” aliuliza kwa kutoamini.

·        “Ya nini kujisumbua? Ah! Acha nikalale zangu,” alijisemea Mawazo.

·        “Mara hii umesharudi?” Nilimuuliza kwa mshangao.

v Mdokezo

Hii ni mbinu ya kuanzisha mazungumzo au wazo,kisha unaishia njiani bila kulimalizia. Hii ni kwa sababu,kwa namna fulani, sehemu ambayo haikumaliziwa inaeleweka kutokana na muktadha wa mazungumzo au maelezo yenyewe.

                   Kwa mfano:

                             Mama:         Yaani Doto, umevunja tena kikombe?

                                                Njoo hapa! Leo nitaku……..!

                             Doto:                    Mama nisamehe. Bahati mbaya.

v Mjalizo

Hii ni mbinu ya kupanga maneno katika mlolongo bila kuweka viunganishi kati yake.

Kwa mfano:

·        Wewe lia, cheka, imba, lakini hutoki hapa!

·        Yule bwana alikaa chini, alisisimama, alijilaza chini, lakini maumivu yalibaki palepale.

·        Sisi tulifanya kila njia. Tuliita, wapi! Tukatafuta, wapi! Tukapiga simu, wapi! Mwishowe tukasema, liwalo na liwe!

v Taswira

Utengenezaji wa taswira katika kazi za kifasihi ni mbinu inayojitegemea,bali huambatana na mbinu nyingine, kwa mfano, tamadhali za semi. Taswira ni picha zinazoumbika akilini ambazo tunazipokea kana kwamba ni kupitia kwenye milango ya fahamu.

Kwa mfano:

·        UKIMWI unabugia watu katika domo lake na kuwatafuna bila huruma.

                          Ifuatayo ni mifano ya taswira mbalimbali:

Taswira za kuona

Kwa mfano:

·        Ana tumbo kubwa kama mtungi.

·        Uso wake umetokeza mbele utadhani wa tumbiri.

·        Nyumba ile ilikuwa kama kilima kikubwa chenye mapango ndani yake.

 

Taswira za kusikia

Kwa mfano:

·        Kicheko chake ni kama radi

·        Kelele za watu ukumbini zilikuwa kama maporomoko ya maji mengi.

·        Njaa husababisha tumbo langu kunguruma kama pikipiki.

Taswira za mguso

Kwa mfano:

·        Mikono ilikuwa inaparua kama msasa.

·        Alikuwa na ngozi nyororo  kama kikombe cha udongo.

·        Maneno yake yanachoma kama misumari ya moto.

Taswira za kunusa

Kwa mfano:

·        Ungemhurumia kwa vile ambavyo mguu ule ulitoa harufu kama mzoga wa paka.

·        Huyo bwana usimkaribie aongeapo ni kama unachungulia kwenye debe la pombe ya mnazi.

Taswira ya kuonja

Kwa mfano:

·        Mwonekano wake ulileta uchachu ndani ya akili yangu.

·        Ana maneno makali kama pilipili.

 

(B) MAUDHUI

Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma msanii hadi akatunga na kusaka kazi fulani ya fasihi.

Vipengele vya maudhui

·        Dhamira,Hii ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira hutokana na jamii. Kwa kawaida dhamira huweza kuwa za kisiasa, kiutamaduni au kiuchumi. Katika dhamira, kuna dhamira na dhamira ndogondogo.

·        Mtazamo,ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe. Wasanii wana mitazamo ya aina mbili:

-         Mtazamo kiyakinifu – Huutazama ulimwengu au mazingira yanayomzunguka binadamu na mfumo wa kihistoria. Mtazamo huu humfanya msanii kuutazama ulimwengu kama kitu dhahiri katika uhalisi wake.

-         Mtazamo wa kidhanifu – Huu huchukulia ulimwengu kama kitu kinachobadilika kulingana na matakwa ya Mungu. Msanii mwenye mtazamo huu, atawasilisha hivyo katika kazi yake.

·        Msimamo,hii ni hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani.Jambo hili linaweza kuwa halikubaliki na wengi,lakini yeye atalishikilia tu. Msimamo wa msanii ndiyo unaosababisha kazi ya sanaa iwe na mwelekeo maalumu na hata kutofautiana na kazi za wasanii wengine.

·        Falsafa,huu ni mwelekeo wa imani ya msanii. Msanii anaweza kuamini, kuwa mfano, mwanamke si chombo duni kama wengine wanavyoamini. Au, kwa wale wapinga usawa, wanaweza kuwa na falsafa ya kumwona mwanamke kuwa kiumbe duni.

Kwa hiyo, falsafa ya kazi ya fasihi inatakiwa ichambuliwe kwa kuzingatia jinsi kazi hiyo ilivyoutazama ulimwengu na kuueleza ukweli juu ya mambo mbalimbali. Ukweli huo lazima uhusishwe na binadamu.

·        Ujumbe na maadili

Ujumbe katika kazi ya fasihi ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi ya fasihi.

·        Migogoro

Migogoro ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi ya fasihi. Katika migogoro kuna migogoro kati ya wahusika ama vikundi vya wahusika, familia zao, matabaka yao, n.k. Na migogoro hii mara nyingi hujikita katika uhusiano wa kijamii. Migogoro yaweza kuwa ya:Kuichumi,Kiutamaduni,Kisiasa,Kinafsia.

 

UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI

Uhusiano wa fani na maudhui umekuwa ukiangaliwa na wanazuoni wanafasihi katika mitazamo tofauti.Mitazamo mikuu inayoangaliwa na wanazuoni katika uhusianowa fani na maudhui umo katika makundi makubwa mawili.Makundi hayo ni ya mtazamo wa kiyakinifu  na mtazamo wa kidhanifu.

 

A:MTAZAMO WA KIDHANIFU.

Wanazuoni wanaoegemea katika mtazamo huu hudai kuwa fani na maudhhui havina uhusiano wowote.Wanazuoni hawa wanaangalia uhusiano wa vijenzi hivi katika utengano ambapo wanaona  fani inaweza kujikamilisha bila ya kutegemea maudhui na maudhui pia kuweza kujikamilisha bila ya kutegemea fani.

Wanaeleza uhusiano wa fani na maudhui kuwa ni sawa na ule wa kikombe na maji au chaiiliyopo ndani ya kikombe hicho.Baadhi ya wanadharia hao wanahusisha mahusiano haya na yale ya sehemu ya ganda la chungwa lililo nje ya nyama ya chungwa .Wanazuoni wanaunga mkono mtazamo huo ni hawa wafuatao:

 

(i) Fr.F.M.V. Nkwera (1998) anadai kuwa fani ni maudhui havina uhusiano wowote  na amefananisha fani na maudhui kuwa ni sawa na  maziwa na kikombe.Kikombe anakiona na kukichukulia kama chombo kinachotumika kuhifadhi maziwa.Hivyo kikombe anakifananisha na fani kuwa ni umbo la nje la kazi ya fasihi.Maziwa anayafananisha na maudhui kuwa ni umbo la ndani la fasihi,kwa madai yake anadai kuwa maziwa yanaweza kutenganishwa na kikombe na kila kimoja hubaki upekeena maziwa hayo yanafananshwa na msomaji wa kazi ya fasihi.

 (ii) S.A Kiango na  T.S.Y Sengo (1993), wanafananisha fani na maudhui kuwa ni sawa na Chungwa na ganda lake.Maganda ya nje ya chungwa yanayomenywa ili kupatanyama ya ndani ya chungwa  sawa na fani ambalo ni umbo la nje ya kazi ya fasihi na nyama ya ndani ni sawa na maudhui.

Madai hayo ni kwamba kwa kuwa maganda ya chungwa yanaweza kutenganishwa na nyama ya ndani ya chungwa basi hata fani na maudhui katika kazi ya fasihi vinaweza kutenganishwa na kila kimoja kusimama katika upekee wake hivyo wanadai fani na maudhui havina uhusiano.

(iii)     Penina Mhando  na Balisidya ( 1976 )

Wanazuoni hawa nao wamo kwenye kundi hili la wenyemtanzamo wa kidhanifu madai yao makubwa kuhusu mahusiano ya fani na maudhui ni kwamba fani katika  kazi ya fasihi ni umbo la nje  basi kwa hali hiyo fani na maudhui vinaweza kutenganishwa kwa hiyo basi fani na maudhui havina uhusiano kwa vile kila kimoja kinaweza kusimama peke yake

 

UDHAIFU WA MTAZAMO HUO

Mawazo ya wataalamu hawa yanaonesha udhaifu mkubwa na yanaweza kuwadanganya wasomaji.Mawazo hayo hayaoneshi ama kuwakilisha ukweli wa mambo ulivyo juu ya uhusiano uliopo kati ya fani na maudhui katika kazi ya fasihi,kwani yanaonesha kuwa fani na maudhui ni vitu  viwili vinavyoweza kutazamwa katika utengano,jambo ambalo si kweli.

 

       B. MTAZAMO WA KIYAKINIFU

Wanazuoni wa fasihi wanaoegemea katika mtazamo huu wanadai kwamba fani na maudhui hutegemeana,huathiriana na kukamilishana.Wanazuoni wanaunga mkono mtazamo huu ni kama vile;

(i)  M.M. Mulokozi  na  Kahigi ( 1982 )

Wanazuoni hawa wanadai kuwa fani na maudhui haviwezi kutenganishwa bali huathiriana na kutegemeana pale unaposoma kazi ya fasihi kwa kupata miundo,matendo,mandhari,wahusika na matumizi ya lugha hivi ni vipengelele vilivyomo ndani ya fani ndipo msomaji anaweza kupata maudhuni ya kazi ya mwandishi kama vile dhamira,ujumbe,fundisho,falsafa ya mwandishi,msimamo na mtazamo wake kwa hivyo basi utaona kwamba fani hutegemea maudhui na maudhui ya fasihi hutegemea fani hivyo basi fani  na maudhui haviwezi kutenganishwa kwani hutegemeana na kuathiriana.Maudhui ni mawazo yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo.Fani ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia msanii kuwasilisha mawazo hayo kwa jamii husika.

 

(ii)F .E.Senkoro ( 1984 )

Mwanazuoni huyo pia anaungana na wanazuoni wa mtazamo wa kiyakinifu wanaodai kwamba fani na maudhui haviwezi kutenganishwa,senkoro katika madai  yake anafananisha uhusiano wa fani na maudhui kama sarafu moja yenye sura mbili,mfano sarafu ya shilling 200 yatanzania ili iweze kukamilika na kuwa yenye matumizi halali katika serikali halali ya tanzani inalazimika kuwa na picha ya karume na kuwa upande wa pili kuwa na picha ya simba na mtoto wake,kutokuwepo au kukamilika sura moja ya sarafu hiyo basi sarafu hiyo haziwezi kutumika kama sarafu halali.Kwa hali hiyo inamaanisha kwamba upande mmoja wa sarafu huwa ni sawa  na maudhui na mwingine ni sawa na fani  katika kazi ya fasihi

Hivyo basi ili sarafu ikamilike nilazima pande mbili zikamilike na hiyo ndiyo hali iliyopo katika fasihi kwamba ni lazima fani na maudhui zikamilishwe ndipo kazi ya fasihi hukamilika kwa hiyo huwezi kutenganisha fani na maudhui.

  Kwa maana hiyo kama kazi ya fasihi itakuwa na fani duni,lakini maudhui yake ni mazuri,basi hata maudhui yaliyokusudiwa hayatatoa ujumbe unaokusudiwa ipasavyo.Kwa mfano,riwaya za kikasuku zilizoandikwa baada ya azimio la Arusha zinazojadili dhamira ya ujenzi wa jamii mpya kama vile Shida (1975),Mtu ni Utu (1971),Ufunguo wenye Hazina (1969),Njozi za usiku (1973),Ndoto ya Ndaria (1978) n.k zilisisitiza zaidi maudhui na kusahau au kupuuza kipengele cha fani.

 Vile vile kama maudhui duni na fani ni bora ,pia jamii itapata hasara ya kufikiwa na maudhui yasiyo na mana katika jamii hiyo kwa kupitia fani iliyobora.Mfano riwaya ya pendwa zote zimeweka msisitizo kwenye fani na kusahau kipengele cha maudhui .Katika riwaya pendwa kama vile riwaya za upelezi,mapenzi, na uhalifu zina wahusika ambao hawaaminiki ,kwani wamepewa sifa ambazo si rahisi kuziona kwa binadamu wa kawaida.

 

NAMNA VIPENGELE VYA FANI VINAVYOIBUA VIPENGELE VYA MAUDHUI

·        Mandhari huibua ujumbe na dhamira

·        Lugha huibua migogoro, dhamira na ujumbe

·        Wahusika huibua migogoro,dhamira na ujumbe

·        Mtindo huibua Falsafa

·        Muundo huibua ujumbe  na dhamira

 

MADA NDOGO; 2- MAENDELEO YA FASIHI

CHIMBUKO LA FASIHI NA SANAA.

Kuna mitizamo mikuu minne  ya kiulimwengu inavyotokeza katika suala la chimbuko la fasihi .Mitazamo hiyo ni  kama ifuatayo;

 

1.     Mtazamo wa kidhanifu.

Mtazamo wa kidhanifu wa misingi yake katika kudhani tuyasiyotokana na uhalisi,kwa hiyo kufuatana na mtazamo huu inaaminika kuwa fasihi na Sanaa kwa ujumla kutoka kwa Mungu kwa hiyo mwanasanaa huipokea ikiwa imekwishapikwa na kuivishwa na Mungu huyo.

Mtazamo wa namna hii ulijitokeza tangu zamani sana wakati wanafalsafa wa mwanzo wa kigiriki na kinenzi kama vile Socrafes Plato na Anstotle,walipoanza kuingia katika ulimwengu wa nadharia ya Sanaa. katika uwanja wa nadharia ya fasihi/Sanaa ya Kiswahili kuna mifano mingi ya wahakiki wa mwanzo waliokuwa na mitazamo sawa naya wanafalsafa hao mfano F.Nkwera (1970),  insha yake ya fasihi inadhihirisha uaminifu wake wa mawazo ya kidhanifu kwa kudai “fasihi ni Sanaa ambayo huanzia kwa muumba humfikia mtu katika vipengele mbalimbali -ni hekima ambayo mtu ameshirikishwa apate kumtambua muumba  wake”.

Nkwera ameungwa mkono na wahakiki wengine ambao wanasisitiza mtazamo huu kwa kusema

“Matengenezo ya Sanaa huonekana kuwa ni shughuli ya kiungu yenyekumwiga Mungu ambaye ndiye msanii wa kwanza”

John Ramadhani pia katika makala yake ya fasihi ya Kiswahili anasisitiza kuwa.

Zaidi ya kwamba fasihi ni hisia vile vile kitengo cha mtu cha kubuni kazi ya Sanaa ni uigaji wa Mungu ambaye ndiye mfalme wa Sanaa zote”.

Mawazo haya ya akina Nkwera,John Ramadhani na wengine yamejaa   mwangwi tu wa mawazo yaliyochakaa ambayo yalikwisha kutajwa na kushughulikiwa  na wahakiki wa zamani tuliowataja kwa msimamo huu wa kidhanifu,Sanaa au fasihi havijifinyangwi kwa jitihada za akili za mikono ya mtu  bali hupokelewa kutoka katika mikono mbayo mtu hana uwezo wa kuiona.

Udhaifu, mtazamo  huu  umepotosha maana halisi kwa kuchanganya Imani na taaluma,pia unajaribu kumtenganisha msanii na jamii yake kwani unatoa nadharia inayomwinua msanii na kufanya aonekane kuwa  mtu wa ajabu aliyekaribu na Mungu kuliko watu wengine wa kawaida.

2.     Mtazamo wa kiyakinifu

Kulingana na mtazamo huu Chanzo cha fasihi  ni sawa na chanzo cha binadamu wenyewe yaani Binadamu na mazingira yake ndio Alfa na Omega ya fasihi.Iwe kwa kuumbwa au mabadiliko kuanzia chembe hai ambayo imepitia maendeleo kadha ya makuzi hata kufikia mtu binadamu alioanishwa na kazi ili kuyabadili mazingira yake.Katika harakati zake za kujiendeleza kiuchumi kila mara alijaribu hiki na kile alichokiona kinafaa alikiendeleza Zaidi na kukidumisha katika hali hii hadithi(ngano),methali,vitendawili,nyimbo,tenzi(mashairi) n.k vyote hivyo vilitungwa na kusimuliwa kwa madhumuni  ya kufunza,kukosoa,kuadhibu,kuchokoza fikra na kuliwaza jamii baada ya kazi.

Sanaa hii ilirithishwa toka kizazi hadi kizazi kwa njia ya masimulizi na binadamu alivyozidi kujiendeleza kisayansi na kiteknolojia akahifadhi taaluma hii katika maandishi.Ndiyo sababu tunasema chanzo cha fasihi ni sawa na chanzo cha binadamu mwenyewe na jinsi binadamu alivyozidi na atakavyozidi ndiyo taaluma hii ilivyokuwa na kuendelea.

3       Fasihi inatokana na sihiri,Istilahi Sihiri’ ina maana ya Uwezo au nguvu ya kimiujiza inayotumiwa na watu kusababisha matokeo fulani.Watalaam  hawa wanadai kuwa  chimbuko la fasihi ni haja ya mwanadamu kukabiliana na  kujaribu kuyathibiti mazingira yake. Haja hiyo haikutimilika ipasavyo katika hatua zake za mwanzo  za maendeleo ya mwanadamu kwani uwezo wa kisayansi na kiteknolojia wa mwanadamu wa wakati huo bado ulikuwa kiwango cha chini sana.Hivyo Imani au miujiza ilichukua nafasi ya sayansi na ugunduzi.Fasihi ilichimbuka kama chombo cha sihiri  hivyo katika kujaribu kuyashinda mazingira,Mfano Wawindaji walichora picha ya mnyama waliyetaka kumuwinda kabla ya kwenda kuwinda,kisha walichoma mkuki au mshale kwa kuamini kuwa kitendo hicho kitatokea kuwa kweli watakapo kwenda kuwinda.Nyimbo walizoimba wakati wa kufanya sihiri hiyo ndiyo fasihi ya mwanzo.

 

Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inachangnya dhima na chimbuko kwani kutumika kwa nyimbo au ushairi katika sihiri hakuthibitishi kuwa sihiri ndiyo chimbuko lake.Sihiri ni amali moja tu kati ya amali nyingi za wanadamu wa mwanzo zilizotumia ushairi.

4       Nadharia ya Mwigo,Wataalam wa nadharia wanadai kuwa Fasihi imetokana na mwigo(Uigaji),Katika nadharia hii inaeleza kuwa mwanadamu alianza kuwa mbunifu kwa kuiga maumbile yaliyomzunguka.Hivyo sanaa za mwanzo mara nyingi zilijaribu kusawiri vitu vilivyomo katika mazingira ,mfano wanyama,ndege,miti,watu.

Nadharia hii ni kale,ilianzisha na wataalamu wa kiyunani  na walioieneza zaidi ni Plato (Republic) na Aristotle (Poetics)  Plato anahusisha mwigo na dhana ya uungu.Anaeleza kuwa Maumbile na vilivyomo ni mwigo tu wa sanaa ya kiungu.Sanaa ya Mwanadamu (Hususani ushairi) ambayo huiga tu mambo hayo yaliyomo  katika maumbile haiwezi kuwa na ukweli  au uhalisi wa kuwa inaiga maumbile ambayo na yenyewe  yanaiga kazi ya Mungu.Hivyo alishauri aina fulani za ushairi zipigwe marufuku kwa sababu zinapotosha ukweli.

Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba inasisitiza mno uigaji na kusahau suala la ubunifu katika sanaa na fasihi.Kama wasanii wangeig maisha na mazingira tu,sanaa yao ingepwaya sana na haingekuwa tofauti na picha ya fotografia au maelezo ya matendo ya mazingira na matendo ya kila siku ya mwanadamu.

 

KAZI ZA FASIHI KATIKA MIFUMO MBALIMBALI

Kwa kuwa mwanadamu ni alfa na Omega wa Fasihi ni dhahiri kuwa maendeleo yake yanahusiana na maendeleo ya fasihi.Hata hivyo sio kila maendeleo huwa na mafanikio mazuri na hivyo si kila fasihi inatoa mawazo mema.Fasihi kama zao la jamii huenda sambamba na maendeleo  ya jamii yanayotokana na kazi  na fasihi hujitokeza katika Nyanja zote za kimaendeleo ziwe za kisiasa,kiuchumi,na kiutamaduni.Safari ndefu ya kimaendeleo imo katika mifumo mitano (5) ya uzalishaji mali.Mifumo hiyo ni kama ifuatayo:

( a ) Fasihi katika mfumo wa Ujima

 Huu ni mfumo wa mwanzo kabisa wa maisha ya binadamu.Fasihi ya kipindi hiki ilikuwa fasihi ya uzalishaji mali.Mfumo wa ujima haukuwa na matabaka ya watu hivyo fasihi ya wakati huo ilijishughulisha na manufaa na maslahi ya watu wote Katika jamii.Katika mfumo huu fasihi na sanaa ni vitu vilivyokuwa vimefungamana na mahitaji ya kukidhi haja ya lazima ya watu. Fasihi katika kipindi hiki ililea amali za jamii ambazo zilikuwa  ni KAZI na USAWA yaani Fasihi ililinganishwa na kazi.Hata hivyo kutokana na uduni wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia,Fasihi ya wakati huo iliilea jamii katika jamii katika kutawaliwa na nguvu za jamii na mazingira.Katika kipindi hiki fasihi haikuwa kitu cha anasa.Mazingira ya wakati huo yalikuwa ya kiuhasama sana,hayakuruhusu kuwepo na anasa ya aina yeyote ile.Kutokana na mazingira hayo Fasihi ilizuka kuwa silaha mojawapo ya mapambano hayo.

 

( b ) Fasihi katika mfumo wa Utumwa,

Mfumo huu ulitawaliwa na utabaka ambapo kulikuwa na mabwana na watumwa wao.Mfumo huu uliruhusu baadhi ya watu kuishi kwa jasho la wengine.Watu hao waliishi maisha ya anasa kutokana na ziada ya mali iliyozalishwa na watumwa wao.Katika mfumo huu uzalishaji mali umewekwa migongoni mwa watu wa tabaka la chini la watwana.Katika shughuli za kisanaa,mfano upande wa ushairi ,watu wa matabaka ya mabwana waliwekewa  watwana na kuwaburudisha  kwa kuwaimbia nyimbo na mashairi.Fasihi nyingi zilikuwa zaile za kuwatukuza mabwana;zinazotukuza utumwa.Fasihi nyingi za wakati huu zilitumiwa ili kuendeleza itikadi za kibwana.

 Pia kulikuwa na fasihi inayopinga mfumo huu wa kinyonyaji.Watumwa wanaotumiwa kuwa vyombo vya kuzalisha mali,wanatunga visa,hadithi,mashairi na nyimbo za kupinga mfumo wa kitumwa.Mara nyingi  mabwana wenye watumwa iliwabidi wawasake na kuwatenganisha watumwa wenye historian a lugha moja iliyowaruhusu kutunga fasihi ya pamoja iliyelea hoja na hisi zao za kupinga unyonywaji huo.

Kugunduliwa kwa maandishi kulileta sura mpya kwa upande wa fasihi ya wakati huo. Uandishi ulikuwa kwa watu wa tabaka la mabwana tu;nao ulielekezwa katika kutoa kazi za fasihi zinazotetea maslahi ya tabaka hilo.Kutokana na ugunduzi wa maandishi watunzi walianza mfano kukaa na kupanga juu ya vina na mizani katika ushairi.Kalam na karatasi zilitumika keneza mitazamo na itikadi za kibwana.Falsafa na mitazamo ya kiulimwengu wakati huo ilielekezwa huko katika kuulinda na kuuhalalisha mfumo wa kitumwa.Kwa mfano,mwanafalsafa Aristotle,katika falsafa zake,alisisitiza na kuhalalisha utumwa kwa kueleza kuwa kuwa ilikuwa amri ya MUNGU kwamba watu wengine wawe watumwa na wengine wawe mabwana.

Hatimaye mfumo huu wa kitumwa ulianza kutetereka kwa mikinzano mbalimbali.Biashara ambayo hustawi sana katika hatua za mwanzo za mfumo huu zilianza kufilisika .Wakati huo huo watumwa hujizatiti na kupinga vikali sana utumwa wao.Watu ambao hapo awali walikuwa na mali zao chache kama vile mashamba na ambazo walinyang’anywa na mabwana wenye watumwa,nao waliungana pamoja na watumwa katika harakati za kuupinga utumwa.

Katika hatua hii ya kukata roho kwa mfumo huu wa kitumwa ,ulitumika kama chombo kimojawapo cha kiitikadi cha kupinga mfumo huo.Tanzu mbali mbali za fasihi kama vile hadithi,ushairi,nyimbo n.k zilielekezwa katika harakati hizo.

( c ) Fasihi katika mfumo wa kikabaila (Kimwinyi)

Ni mfumo ambao uhusiano wa kitabaka  unakuwa kiwango cha juu kabisa.Tabaka tawala la makabaila linamiliki njia zote za uzalishaji mali yaani kiuchumi na kiutamaduni.Njia za kiuchumi hutawaliwa  kwa mbinu mbalimbali  za kukodisha mashamba.Mfano aliyekodishwa anapangiwa kutoa fungu kuba sana kwa mwenye shamba wakati wa mavuno.Mtwana wa wakati huu hutofautiani sana na mtumwa wa kipindi cha mfumo utumwa.Fasihi ya wakati huu anatawaliwa na falsafa zinazojaribu kuhalalisha uhusiano huo wa wenye mashamba na njia nyingine za uzalishaji mali na wale wasio na chochote isipokuwa jasho lao.Fasihi ya kipindi cha ukabaila iliweka msisitizo kuusu mapambo yasiyo na maana;msisitizo ambao unaathiri kazi ya fasihi pia.Mfano katika utenzi wa Al-Inkishafi(1810) mwandishi anasema;

37. Nyumba zao mbake zikinawiri,

   Kwa taa za kowa na za sufuri,

  Masiku yakele kama nahari,

 Haiba na jaha iwazingiye.

 

        38. Wapambiye sini ya kuteuwa,

               Na kula kikombe kinakishiwa,

              Kati watiziye kuzi za kowa,

               Katika mapambo yanawirije.

 Katika utenzi huu,Sayyid Abdallah A.Nassir anatuusia kuhusu maisha na ametumia lugha ya picha ya maisha ya uozo wa wafalme wa Pate kama kielelezo cha uzuri usio na kifani wa maisha ya hapa duniani.Halafu anaonyesha jinsi ambavyo maisha haya anayoyaona kuwa uzuri mwingi yanamalizikia katika kaburi ambako miili ya hao wafalme inakuwa chakula kikubwa cha funza.Uozo wa maisha ya mamwinyi wa pate  umeibua Fani na Maudhui ya Al-inkishafi (1810)

  Pia katika Utendi wa mwanakupona (1962) mwandishi anamuusia binti yake kuwa ajikubali kuwa pambo mbele ya mume wake.Anasema;

                  38.  Na kowa na kuisinga,

                          Na nyee zako kufunga,

                          Na asmini kutunga,

                          Na firashini kutia

 

              39     Nawe ipambe libasi

                       Ukae kama arusi,

                       Maguu tia kugesi,

                      N mikononi makoa.

 

 

            41. Pete sikose za ndani,

                   Hina sikome nyaani,

                   Wanda sitoe matoni,

                   Na inshini kuitia

Katika utendi huu mwandishi anamuasa mwanamke aweke na kuelekeza akili yote kwenye kujipamba ambapo kwa kufanya hivi kumemfanya mwanamke abaki katik nafasi duni sana katika jamii;nafasi ya chini ya kuonekana,kujiona na kujikubali kuwa pambo la kuufurahisha moyo na jicho pamoja na uchu wa mwanamume.

 Pia mfumo huu unamdanganya akubali kumtumikia na kumtii mume wake bila kumbishia wala kumjibu kwa lolote lile atakalosema.Mwanamke anaaswa kwamba amtii na amuogope mume wake;

                  28. Keti naye kwa adabu,

Usimtie ghadhabu,

 Akinena simjibu,

 Itahidi kunyamaa,

 

36. Mpumbaze apumbae,

Amriye sikatae,

 Maovu kieta yeye,

 Mungu atakulipa.

 Katika ubeti wa 36 wa utenzi huu inaonyesha wazi kuwa dini ilitumika kama taasisi kubwa ya kudumisha na kuhalalisha unyonyaji na mgawanyiko wa jamii katika matabaka ya watu.Katika utenzi huu,binti anausiwa kuwa afuate yote anayoambiwa na anayoamriwa  na mume wake kwani yote ni amri ya MUNGU.Hapa tunagundua athari za kitabaka zilizojikita katika dini na mafundisho yake.Athari hizo zinazidi kumdidimiza  na kumkandamiza zaidi na kumfanya mtu duni sana.

Katika mfumo huu maisha huwa ya kibiashara na yaliyozingwa na imani kubwa juu ya pesa.Pesa  zinaanza kuabudiwa katika mfumo huu,nazo hujitokeza  katika nyuso mbalimbali za rundo la utajiri wa makabaila.Katika utenzi wa sundiata jambo hili linajitokeza waziwazi mwandishi anaelezea kuhusu utajiri wa wafalme kama vile Mansa Mussa.Mfumo huu wa kikabaila haukuendelea kuwapo muda wote. Mikinzano ambayo daima huwapo baina ya wanyonyaji na wanyonywaji ,pamoja na nguvu za vibwanyenye uchwara ambao walikwishaumbika katika harakati za kitabaka.Upande mmoja wa harakati  hizo walikuwepa wakulima wanyonywaji  pamoja na vibwanyenye ambao daima wamekuwa wakijitahidi kuangusha mfumo huu wa kikabaila ili badala yake wakite mizizi ya kibepari.Nguvu zote hizi za kiuchumi na kisiasa  hatimaye kuuangusha mfumo wa kikabaila.

 Katika kipindi hiki pia fasihi ilikuwa chombo kilichosaidia kuendeleza harakati za kuuangusha mfumo wa kikabaila wakati makabaila waliitumia fasihi kueneza na kuendeleza itikati zao za kikabaila,papohapo wanyonywaji nao pia walitunga fasihi yao inayoeleza hisia zao,taabu zao na umuhimu wa kujikomboa.Kwa wakulima fasihi yao ilikuwa ndiyo silaha ya kifasihi na kwa vibepari uchwara piawalikuwa na fasihi yao ya kupinga ukabaila na kutetea umuhimu wa kuwa na mfumo mpya wa maisha yaani mfumo wa kibepari.Mfano wa fasihi ya Kiswahili ya wakati huo ni kama vile; Utenzi wa fumo liyongo (1913) ambap awali utenzi huu ulielezwa kwa njia yam domo tu.Kwa watu wa tabaka la chini waliosimulia kisa hiki cha liyongo kilionekana kuwa cha kusifu ushujaa wa mtu huyo lakini papo hapo liyongo alikuwa mtetezi na mpenda watu wanyonge.

 

( d ) Fasihi katika mfumo wa kibepari

Fasihi ni zao la jamii na hufungamana na mfumo wa maisha ya jamii na pia ulifungamana n mapambano ya kudumu dhidi ya mazingira ,yaani kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni.Katika mapambano hayo dhidi ya mazingira kulikuwa na mitazamo tofauti ya fasihi.Pia fasihi ilionekana kuwa ni silaha mojawapo kati ya silaha nyingi zilizotumiwa na tabaka moja kutetea maslahi yake kwenye mapambano ya kudumu ya kitabaka katika jamii

Katika ubepari kuna matabaka mawili ya watu yaani wenye mali wanaoshikilia rasilimali zote na wanyonge wasio na kitu.Fasihi ya kibepari ilielezea uzuri wa fedha kwa sababu pesa iliabudiwa sana katika mfumo huu.Waanii wa kipindi hiki ni wale walionuia kupata pesa,wasanii hawa walivaa uso wa udanganyifu huku tegemeo lao kubwa ni gunia la fedha,unyang’anyi na umalaya.Mfumo hu umefanikiwa kuwatenga waandishi na jamii zao.Wengi wametunga kazi zao za fasihi ambazo maudhui yake,dhamira na lengo lake pamoja na fani  kama vile Mzimu wa watu wa kale (1958),Kisima cha giningi (1958),Siri ya sufuri (1974),Duniani kuna watu (1973),Mwana wa Yungi hulewa (1976), na Kosa la Bwana Msa (1984) zaidi wasanii hawa walishighulikia suala la kusisimua msomaji na kumpumbaza kwa visa vya upelelezi.Fasihi ya kibepari iliifumba macho jamii isiione machungu  yanayoisakama jamii.Fasihi hii huwafumba macho watu (jamii) ili wasione udanganyifu ulioshamiri katika jamii hiyo.Huwaficha wagandamizaji na kuwapa nguvu za kumiliki jamii kisiasa ,kiuchumi,na kiutamaduni ili kuendeleza matabaka yanayo wanufaisha wachache.

 Fasihi ya kibepari haikomboi watu kimawazo ili waweze kuchambua na kutambua jamii yao kwa jicho pevu.Haiwachochei wanaogandamizwa kukataa machungu yanayosababisha na wagandamizaji wachache.Katika mfumo huu fani huwa kubwa kuliko maudhui yaliyopatikana humo.Kazi a fasihi iliyo nzuri ni ile ambayo fani na maudhui huwa katika uwiano ulio sawa.Fani isaidie kuyaweka maudhui katika hali nzuri ya kueleweka kwa jamii.

 

( e )Fasihi katika mfumo wa kijamaa

Mfumo huu huu ulibuniwa na Marx na Angels ambao walidai kuwa mfumo huu utatetea na kuleta kheri kwa umma.Fasihi ya mfumo huu itakuwa ya kunufaisha umma na kulinda amali na hali ya jamii.Matunda ya kazi huwa kwa faida ya wote.Usawa,utu na kuheshimiwa ndiyo msingi wa fasihi ya kijamaa.Fasihi ya kijamaa ni ya jamii nzima ambapo huiangalia jamii kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni.Huyamulika matatizo ya jamii.Ni chombo cha kuunganisha,kuadibu,kuhimiza,kuongoza na kushauri jamii katika lake la kufuta unyonge na uchafu unaoikabili jamii.

 Fani na maudhui katika fasihi ya kijamaa ni vitu ambavyo hufungamana kwa mtazamo wa jumla.Fasihi lazima iwe wazi ili watu wa ngazi zote waweze kuelewa na kuzichukua fikra nzuri zilizomo.Uhuru wa kuikosoa na kuichambua jamii ni wazi kwa fasihi hii,tofauti na fasihi ya kibwenyenye ambayo uhuru huu haupo.Hivyo basi, fasihi iliyo ya kweli ni ile inayoelewesha umma katika mapambano yake dhidi ya mazingira,kuikosoa jamii,na kuielekeza jamii katika ukombozi wa kweli.Fasihi ya dhati ni sharti iendeleze shabaha zilizofikiwa na umma yaani wakulima na wafanyakazi.

 

MADA NDOGO- 3 : UHURU WA MWANDISHI/MTUNZI WA KAZI ZA KIFASIHI

 

UHURU WA MWANDISHI/MTUNZI

Ni ile hali ya mwandishi wa fasihi kuwa huru na wazi katika kutoa mawazo au hisia zake kwa jamii.Ni uhuru wa kuandika na kulikosoa tabaka lolote katika jamii bila kupata matatizo yoyote.

Mwandisihi ni nani?

Ni mtu yoyote atumiaye muda wake mwingi  kuandika na kuzungumzia jamii yake kwa njia ya maandishi.

 

Dhana ya uhuru wa mwandishi ni pana sana na inatazamwa kwa kuangalia vipengele kadhaa kama ifuatavyo:

    Mosi,uhuru wa mwandishi uko katika utashi,Bila utashi mwandishi atakuwa mwoga na mwepesi wa kukata tamaa.Atayumbishwa haraka kutoka kwenye msingi wa falsafa yake na Imani aliyo nayo juu ya mabadiliko yatokeayo katika jamii.Makombora ya wahakiki na wanasiasa huweza kumyumbisha, lakini kwa mwandishi mwenye utashi makombora hayo humkomaza.

Baadhi ya waandishi walioonyesha utashi wao katika Afrika ni ‘Ole Soyinka na Ngugi wa Thiongowaandishi hawa wameshambuliwa sana na wahakiki, lakini misimamo yao ni ile ile, pia wamewahi kufungwa na walipotoka kifungoni hawakubadili misimamo yao na wamekuwa hivyo kwa sababu ya utashi wa falsafa zao katika fasihi ya kiswahili, waandishi wenye utashi wapo na msingi wa kuwepo kwao ni kutoyumbishwa na matamshi ya jukwaani na wahakiki ambao hawajapevuka.

Pili,uhuru wa mwandishi umo katika kuwa na falsafa moja inayoeleweka, Falsafa ifanyayo maandishi ya mwandishi moja yawe na kitu kijulikanacho kama lengo.Waandishi waliotajwa hapo juu yaani Ole Sanyika na Ngugi wa Thiongo ndio wanaongoza kuwa na falsafa zao zinazojulikana. Katika fasihi ya Kiswahili tunaona waandishi wachache wenye falsafa zao inayojulikana wengi tulio nao wanaandika kufuatana na jambo fulani au tukio la wakati huo bila kulinganisha leo ataandika juu ya mapenzi, kesho juu ya upelelezi na kesho kutwa mapinduzi mwishowe anakuwa na orodha ndefu ya vitabu visivyokuwa na lengo.Waandishi wachache tulio nao ambao wameelekea kuwa na falsafa inayoongoza maandishi yao ni kama Shaban Robert, G.Kezilahabi na Mohamedi Suleiman.Bila kuwa na falsafa maalumu ni rahisi  sana mwandishi kuyumbishwa.

Tatu,Mwandishi kuitawala vema Sanaa yake,kama unaandika riwaya na hujui misingi ya Sanaa ya aina hiyo atajikuta katika kikwazo,utajikuta uhuru wa kisanaa unaweza kujaribu, lakini kazi utakayoitoa itakuwa hafifu.Kazi nzuri ya kisanaa ni ile inayounganisha vema ubunifu na uhalisia.Mwandishi akielemea sana katika ubunifu anazua matatizo mengine kazi ngumu aliyonayo mwandishi ni katika kupata barabara msitari huo.Mwandishi mwenye vitabu vingi anaweza kuwa na kitabu kimoja tu kilichoupatia vema mstari huo. Katika fasihi ya Kiswahili waandishi walioupatia msitari huo tunao ni kama vile Ebraim Hussein,Penina Mhando,Mohamed Suleiman, C.G Mng’ong’o na J.A.Safari.Msanii anayeweza kuitawala  vema Sanaa yake anaunganisha vizuri Sanaa na maudhui yake.

Mwisho, uhuru wa mwandishi umo katika lugha anayotumia,ili msanii atawale vema Sanaa yake nilazima ajue lugha anayotumia.Lugha ndicho kiungo maalumukati ya Sanaa na kazi ya kifasihimwandishi kama hajui vema lugha anayotumia atajikuta hana uhuru wa kukisema anachotaka kwa hiyo lugha ndiyo nguzo ya nne katika uhuru wa mwandishi, waandishi wa Kiswahili  waliokwisha kutajwa wanakitawala Kiswahili sanifu,Kiswahili sanifu ndiyo msingi wa fasihi ya Kiswahili.

 

SIFA ZA MTUNZI WA KAZI YA FASIHI

ü Awe mbunifu ili aweze kutoa kazi ya fasihi yenye mvuto

ü Ajue vizuri utamaduni wa jamii anayoitungia kazi ya fasihi.Pia ajue mabadiliko yanayotokea katika mifumo mbalimbali ikiwamo ya kisiasa na kiuchumi.

ü Awe na ujuzi wa lugha anayotumia kutunga kazi yake ili aweze kuteua msamiati,nahau,misemo na methali ambazo zinaendana na kile anachokitunga.

ü Awe na ujuzi wa utanzu husika.Mathalani kama anatunga shairi,ni lazima ajue kanuni na mbinu za utunzi wa mashairi.Hivyo ni muhimu mtunzi asome kazi mbalimbali zinazohusu utanzu husika ili kuongeza ujuzi na kubaini mambo ambayo hayajaandikiwa.Kama ni mtunzi simulizi ajue kanuni za utunzi simulizi wa fani husika.

ü Awe na uwezo wa kupanga matukio kwa sababu mpangilio mzuri wa matukio hufanya kazi ya fasihi ivutie.

 

Je kuna uhuru wa mwandishi?

Kwa ujumla uhuru wa mwandishi ni uhuru ikiwa hakufaulu kudhuru tabaka tawala hii ni kwa sababu suala la uhuru wa mwandishi ni la kitabaka na lilianza pale jamii ilipogawanyika katika matabaka kwa maana hii uhuru wa mwandishi unaamuliwa na tabaka tawala

Kuanzia enzi za utumwa, maandishi ya liyovumbuliwa katika  fasihi andishi ya mwanzo ilikuwa ya wateule wachache tu na wenye vyeo vyao.Hao mabwana, wamwinyi na mabepari walihakikisha kila mbinu inatumika ikiwemo ya udhibiti wa maandishi ili kuendeleza na kulinda utawala wao.

Kwaujumla  mwandishi hana uhuru kwa vyovyote vile kwa sababu yeye ni tokeo la jamii Fulani, kila jamii ina mipaka yake ambayo mtu hatakiwi kukiuka kwa vyovyote vile mwandishi huyu amebanwa na mipaka hiyo asivuke.Pindi avukapo mipaka hiyo atapambana na jamii hiyo (tabaka tawala) vitabu vya mwandishi huyo vitapigwa marufuku au vitabu vikitolewa havitanunuliwa au serikali itavikusanya na kuvifanyia mipango mwingine. Katika Afrika  kuna mifano mingi ya udhibiti wa waandishi mfano mzuri ni mwandishi maarufu wa Kenya Ngugi wa Thiongo ambaye kazi zake hasa ya “Ngaahika Ndeenda”(I will marry when I want)- Nitaolewa Nitakapotaka, ilimgombanisha na vyombo vya dola hadi akawekwa kizuizini, Ngugi ni mwandishi wa kwanza kufichua siri za mfumo wa kibepari kwa watu wanyonge aliliuzi tabaka tawala la jamii yake ambalo halikusita kutumia udhibiti na vyombo vyake vya Mabavu.

Baada ya uhuru vitabu vingi sana viliandikwa kwa kudhibitisha maandishi mbalimbali uliojitokeza waziwazi E.Kazilahabi aliandika riwaya “Rosa mistika”(1971),kitabu hiki kilipigwa marufuku kisitumike mashuleni na wala kisiuzwe waziwazi madukani.Ilidaiwa na waliokipiga marufuku kuwa kilikiuka maadili ya jamii kwa kueleza mambo ya aibu kwa wazi.Sura ya kumi ndiyo hasa ilitolewa mfano wa uchafu wa kitabu hiki.Udhibiti huo ulifanywa na Wizara ya Elimu na ulizusha maswali mengi kwa wasomaji.Wasomaji walianza kujiuliza, Je si kweli uchafu uelezwao katika “Rosa mistika” umo ndani ya jamii ya Tanzania? Je upotofu na uongozi mbaya ulifuchuliwa na riwaya hiyo hii si upo kati yetu? Kwa baadhi ya wasomaji ilielekea kuwa suala la uchafu wa maelezo yatokeayo kitandani baina ya wakuu wa chuo na wanafunzi wao lilitumika kama kisingizio tu cha kudhibiti ukweli wa masuala mengine nyeti yaliyowagusa viongozi yaliyowakilishwa na watu kama vileBwana Maendeleo Deogratius anayeshiriki katika kuwaharibu vijana.

Vitabu vingine ambavyo havieleweki vinasema nini, maudhui, falsafa na ujumbe wa mwandishi ni mashetani(E.Hussein)“Aliyeonja Pepo”(F.Topan) na “Ayubu” Paukwa theatre Association.Na hivi viko kwa kukwepa mkono mrefu wa tabaka tawala.

 

TATHMINI YA UHURU WA MTUNZI WA KAZI YA FASIHI

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

DHANA YA SANAA

Sanaa ni uzuri unajitokeza katika umbo lililosanifiwa umbo ambalo mtu hulitumia kuelezea hisia zinazomgusa kwa kutoa kielelezo au vielelezo vyenye dhana maalumu.Sanaa ni matokeo ya kazi ya mikono na akili ya mtu,ambayo huwa na umbo dhahiri lenye maana au dhana maalum.Sanaa huweza kujitokeza katika maumbo au sura tofautitofauti kama ilivyo katika kielelezo kifuatacho;

 

MCHORO WA SANAA

 

 

 

 

 

 

AINA ZA SANAA

i)Sanaa za Uonyeshi,ni sanaa ambazo uzuri wake hujitokeza katika umbo la kudumu, umbo ambalo linaweza kuhifadhiwa na uzuri wake kuonyeshwa wakati wowote. mfano uchoraji, uchongaji, kutarizi, ufinyanzi, n.k. Sanaa ambazo hututolea vitu kama vile picha, vinyago, nguo zilizotarizwa, vyungu n.k.

ii)Sanaa za Ghibu,ni sanaa ambazo uzuri wake haujitokezi kwenye umbo linaloonekana kwa macho au kushikika bali  katika umbo linalogusa hisia mfano ushairi, uimbaji, upgaji muziki, n.k. Uzuri wa sanaa hizi umo katika kuzisikia.

iii)Sanaa za Vitendo,ni sanaa ambazo uzuri wake umo katika umbo la vitendo. Uzuri wa sanaa  hizi umo katika umbo la vitendo, na ili kuupata uzuri huu yampasa mtu kutazama vitendo vikifanyika. Umbo hili linalazimisha kuwepo kwa mwanasanaa (mtendaji) na mtazamaji(Hadhira) wa sanaa mahali pamoja kwa wakati mmoja, ama sivyo sanaa haikamiliki. Hali hii ndiyo inayosababisha sanaa hizi za vitendo kuitwa sanaa zamaonyesho kwa sababu lazima wakati zinapototendeka awepomtu wa kuonyeshwa, maana uzuri wake umo katika vitendo vyenyewe.

 

SIFA ZA SANAA ZA MAONESHO

*    Dhana ya kutendeka (mchezo unaooneshwa)

*    Mtendaji (fanani)

*    Uwanja wa kutendea/jukwaa maalumu

*    Watazamaji (hadhira).

*    Utendaji (matendo yanayofanywa na wahusika)

Hivyo sanaa za maonyesho ni dhana zilizo kwenye umbo linalotendeka na  ili dhana hii itendeke inahitaji mtu wa kuitenda (mtendaji). Mtendaji huhitaji uwanja wa kutendea hiyo dhana, na wakati akiitenda hiyo dhana wanakuwepo watazamaji.

 

Tanzu za Sanaa za Maonyesho

i)       Tambiko

Ni sadaka inayotolewa kwa miungu au mahoka, mizimu, pepo, n.k.  wakati wa kusalia miungu.

Matambiko yalikuwa na umuhimu mkubwa katika jamii za babu zetu kuliko siku hizi. Jamii ya asili ilipokabiliwa na matatizo yaliyowashinda kama vile magonjwa, ukame, au kukosa mtoto, n.k. walifanya tambiko na kusali ili miungu yao iwasaidie. Wakati fulani walifanya matambiko kwa ajili ya kuomba radhi au kutoa heshima na shukrani.

Mara nyingi matambiko haya huandamana na kafara kama sadaka inayotolewa na jamii kwa wahenga wao. Kafara inaweza kuwa ya kuku, kondoo,ng’ombe, mbuzi au chakula. Katika jamii nyingi za Kiafrika kabla ya ukoloni walitoa kafara ya binadamu.

Fani katika Tambiko

Ø Sanaa

Katika tambiko sanaa inayotendeka ni ule ufundi wa kutenda vitendo kwa ukamilifu kwa kutambika kwa kutumia ufundi wa aina fulani.

Ø Wahusika

Wahusika watambiko ni wale wazee maarufu walioteuliwa na jamii kuendesha shughuli hizi za matambiko. Si watu wote katika jamii huhusika.

Ø Mazingira (Mahali)

Tambiko linaweza kufanyika porini, makaburini, njia panda, kwenye mti mkubwa au mahali popote kutegemeana na aina ya tambiko lenyewe.

 

 

 

 

UMUHIMU WA TAMBIKO

·        Hujenga imani kama chombo cha kutatulia matatizo ya jamii. Jamii ya asili ilipokabiliwa na matatizo ilifanya tambiko na kusali ili miungu iwasaidie kuondokana na tatizo hilo.

·        Tambiko husaidia kuendeleza mila na desturi za jamii.

·        Tambiko hujenga na kuimarisha mahusiano miongoni mwa wanajamii.

·        Matambiko huiongoza jamii katika mapambano dhidi ya matatizo mbalimbali yanayowakabili.

 

HASARA ZA TAMBIKO

·        Hujenga dhana potofu katika jamii kwani watu huamini nguvu fulani bila kuwa na uhakika au uthibitisho wa kisayansi.

·        Huleta hasara kubwa kwa jamii kwani kafara ya tambiko inahitaji mnyama au chakula, ambapo watu hutumia hela nyingi kuvipata vitu hivyo.

ii)    Mivigha

Ni sherehe zinazofanywa na jamii katika kipindi maalumu cha mwaka. Mivigha hufanywa  kwa lengo la kufundisha jambo fulani maalumu kwa maisha ya jamii. Sanaa za maonyesho katika kundi hili zinahusu kuingizwa kwa mwanajamii kwenye kundi la watu wa aina fulani kutoka kundi la watu wa aina nyingine. Mfano jando na unyago, harusi, kutawazwa chifu, n.k.Katika jando na unyago mtu hutoka kundi la watoto kuingia kundi la watu wazima, mtu aliyeoa anatoka kundi la makapera kwenda kundi la waliooa au kutawazwa chifu, mtu anatoka kundi la raia na kuingia kundi la watawala n.k.

Kutoka kundi moja kuingia kundi jingine ni hatua iliyopewa umuhimu mkubwa katika jamii ya asili. Umuhimu huu uliambatana na madaraka mapya yaliyo mkabili mwanajamii kuingia katika kundi jipya. Kila kundi la watu lilikuwa na madaraka fulani mbayo kutekelezwa kwake ndiko kulikoleta maendeleo ya jamii .

Fani katika  Mivigha

Ø Sanaa

Sanaa katika mivigha ni ule ufundi wa kutenda kikamlifu na kiufundi katika kudhihirisha yale yanayotendeka.

Ø Wahusika

Katika mivigha wahusika ni wa aina tatu:

a)    Mtendaji/watendaji,ni wale wote wanaoshiriki kutenda ile dhana ya kuwatoa watu kutoka kundi moja na kuwaingiza katika kundi lingine. Vitendo hivyo huambatana na nyimbo, michezo mbalimbali n.k.

b)    Watazamaji ,ni wale wanaoingia kutoka kundi moja na kwenda kundi lingine. Hawa ndio watazamaji, kwa sababu maneno, nyimbo, vitendo, ngoma, n.k. vyote vinafanyika ili wao wavione na wajifunze na baadae watekeleze yale waliyojifunza.

c)     Waangaliaji, ni wale wanaoangalia mambo yanayotendeka bila wao kushiriki katika kucheza au kuimba au kutoa mafunzo, wanaangalia tu. Hawa kwa upande wa sanaa za maonyesho sio watazamaji kwa sababu yale yafanywayo hayawasilishwi kwao. Wakiwepo au wasiwepo bado vitendo vinatendeka tu bila maana yake kupotea. Hawa wanaitwa “waangaliaji”

(d) Mahali /Mandhari,kwa upande wa mivigha uwanja wa kutendea ni mahali sherehe zinapofanyika. Inaweza ikawa ndani ya nyumba, au porini, kwenye uwanja wanje ya nyumba,milimani au mapanngoni, n.k.

 

UMUHIMU WA MIVIGHA

·        Mivigha hufundisha umuhimu wa kazi kama vile kilimo, uwindaji, uhunzi, ufinyanzi, ushonaji, n.k.

·        Mivigha huhimiza umuhimu wa ujasiri katika maisha.

·        Mivigha  hufundisha suala zima la unyumba na malezi kwa ujumla mfano  umuhimu wa uzazi na malezi bora.

·        Mivigha husisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano katika jamii.

 

HASARA ZA MIVIGHA

·        Hugharimu pesa nyingi sana ambapo huwaacha wenye sherehe kwenye madeni makubwa.

·        Sherehe huweza kusababisha ugomvi, chuki, dharau, tamaa, n.k.

·        Huleta ushindani na matokeo yake husababisha baadhi ya watu wasio na uwezo hujiingiza katika wizi, utapeli, ujambazi, n.k.

  3. Majigambo

Ni masimulizi ya kujigamba kwa mtu kuhusu mambo ya kishujaa aliyopata kuyatenda maishani mwake. Majigambo hayo husimuliwa katika lugha ya kishairi na masimulizi yake huambatanishwa na vitendo vya mjigambaji mwenyewe.

Mtambaji anapotamba katika sanaa hii, kwa kawaida huwa na tabia ya kujivuna au kujitapa kuwa yeye ni bora kuliko wengine wote.

Wakati wa utambaji mazingira humtawala fanani. Pengine fanani alikuwa akitamba kuonyesha utukufu wake kwa mfalme wao. Au alikuwa akitamba wakati wa kujiandaa kwenda vitani.

Fani katika Majigambo

Ø Sanaa

Sanaa katika majigambo ni ule ufundi anaoutenda mjigambaji, kwa kujigamba kwa ufundi huku akionyesha vitendo waziwazi alivyopata kuvitenda maishani mwake.

Ø Wahusika

Hapa kuna mtendaji na watazamaji

·        Mtendaji ,ni yule anayejigamba mbele ya wenzake, yaani Yule anayejigamba kuhusu mambo yake ya kishujaa aliyoyatenda maishani mwake.

·        Watazamaji,ni wale wanaotazama vitendo vinavyotendwa na mtendaji.

Ø Mahali/Jukwaa maalum

Uwanja wa kutendea ni mahali popote ambapo majigambo yanaweza kufanyikia. Hapa inaweza kuwa kwenye uwanja mkubwa ambapo sherehe hizo zinafanyikia au kwenye ukumbi.

Ø Matumizi ya Ngoma katika Majigambo

Majigambo vile vile yaliambatana na ngoma, wakati mwingine ngoma zilichezwa na katikati ya ngoma mjigambaji mmoja alijitokeza na kuanza kujigamba, alipomaliza alirudi kucheza ngoma na mwingine alijitokeza tena.

 

UMUHIMU WA MAJIGAMBO

·        Hudumisha utu wa mwanaume katika jamii.

·        Hudumisha ari ya kuwa wakakamavu, shujaa na jasiri katika jamii.

·        Huburudisha jamii yaani mtendaji na wasikilizaji.

 

HASARA ZA MAJIGAMBO

·        Hukuza na kuendeleza ubinafsi kwani fanani huonekana ni bora zaidi kuliko watu wengine.

·        Mkusanyiko wa hadhira hutumia pesa au vyakula kwa wingi, hivyo husababisha umasikini .

·        Majigambo husababisha unafiki kwa sababu fanani huonyesha mafanikio yake tu na sehemu alizoshindwa hagusii kabisa, kitu ambacho si cha kweli katika maisha ya mwanadamu.

 

4       .Michezo ya Watoto

Ni mchezo mbalimbali inayochezwa na watoto, na michezo hiyo hufungamana na hali ya utamaduni, uchumi na siasa ya jamii inayohusika. Mchezo hii husaidia watoto waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii yao. Kwa njia hii watoto hujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji kama vile kilimo, kupika chakula, kuwinda, n.k. Vile vile hucheza mchezo wa baba na mama. Hapa mtoto mmoja anakuwa mama, mwingine baba na wengine watoto. Mchezo huu huakisi mambo halisi ya nyumbani.

 

Fani katika Michezo ya Watoto

Ø Sanaa

Sanaa katika michezo ya watoto wadogo ni ule ufundi wa kutenda vitendo kikamilifu na kuonyesha ujuzi mkubwa katika utendaji huo

Ø Wahusika

Kuna watendaji na watazamaji. Watendaji ni watoto wenyewe wanaocheza michezo hiyo, yaani wavulana na wasichana. Idadi ya watendaji inategemea aina ya mchezo wenyewe.Watazamaji ni wale wanaotazama mchezo huo. Hapa  wanaweza wakawa watoto wenyewe ambao hawachezi au jamii inayowazunguka watoto hao.

Ø Mahali/Jukwaa maalum  la kutendea

Uwanja wa kutendea michezo ya watoto ni sehemu yoyote itakayochaguliwa na watoto wenyewe kulingana na michezo unaohusika. Kwa mfano, wanaweza kucheza uwanjani, chini ya mti, barabarani, chumbani, sebuleni, kando ya nyumba, n.k.

 

UMUHIMU WA MICHEZO YA WATOTO

·        Huwasaidia watoto wadogo kujifunza mambo mbalimbali yanayotokea katika jamii yao. Kwa njia hii watoto hujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji mali, utamaduni na siasa ya jamii yao.

·        Huwasaidia watoto kujifunza kuwa na ujasiri, ushujaa, udadisi wa mbinu mbalimbali za kupambana na matatizo yanayojitokeza katika jamii.

·         Hurithisha amali za jamii toka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Michezo hii hurithisha mila na desturi za jamii fulani kwa kucheza michezo hiyo.

·        Michezo hiyo huburudisha watoto. Katika kucheza michezo hiyo, watoto huburudika na kustarehe.

·        Huwasaidia watoto huimarisha viungo vya mwili kwa watoto wanaocheza michezo hiyo.

 

HASARA ZA MICHEZO YA WATOTO WADOGO

Ø Watoto huweza kuumizana kutokana na michezo hii.

Ø Ikiwa wazazi wa watoto hawa wana tabia chafu kama ile ya kugombana, kutukanana ovyo, vivyo hivyo watoto hawa watarithi tabia chafu kutoka kwa wazazi wao na wanaweza kuwaambukiza wenzao.

5       Utani,

Ni hali ya kufanyiana mizaha pasipo kuogopa na kushtakiana au utani ni uhusiano wa kutaniana au kufanyiana masihara ambao ni tofauti na desturi za kutokuheshimiana. Madhumuni yake makubwa ni kupunguza na kuondoa kabisa uhasama na chuki iliyokuwepo baina ya makundi fulani ya watu.

Fani katika Utani

Ø Sanaa

Sanaa katika utani ni ule ufundi na uwezo wa kutaniana baina ya wahusika wanaohusika na utani huo.

Ø Wahusika

Katika utani, washiriki wanaweza kuwa mtu na mtu, familia na familia, kabila na kabila, ukoo na ukoo au nchi na nchi.

Ø Mahali

Uwanja wa kutendea inaweza kuwa mahali popote ambapo utani unaweza kufanyika. Inaweza ikawa kwenye harusi, msibani, kwenye pombe wakati watu wanakunywa, n.k.

 

UMUHIMU WA UTANI

·        Kutoa maadili na mafunzo fulani kwa jamii.

·        Kuimarisha umoja na ushirikiano miongoni mwa wanajamii (kujenga undugu)

·        Kuhimiza ujasiri na juhudi katika maisha.

·        Kuhimiza upendo katika maisha.

·        Hukuza na kuimarisha mila na desturi za jamii.

 

HASARA ZA UTANI

·        Husababisha ugomvi katika jamii.

·        Huleta hasara za kuchukuliana vitu bila malipo.

·        Huvunja au kuvunjiana heshima miongoni mwa wahusika.

 

Kazi za fasihi zipo katika nyanja zifuatazo uchoraji, ususi, fasihi, ufinyanzi, muziki, ufumaji, utarizi na maonesho.Nyanja hizi za Sanaa zinaweza kuonyeshwa kwenye kielelezo hiki:-

Muziki

Utarizi

 SANAA

        Fasihi

Uchoraji

Ufumaji

 

 

 

 

 


Ufinyanzi

FASIHI                                 

        Uchongaji

Sanaa  za Maonyesho

Ususi

 

 


Kila kipengele cha Sanaa kinatofautiana   na kingine kwa umbo na matumizi. Fasihi ni kipengele cha Sanaa kinachotumia maneno kuumba huo uzuri wa kisanaa.

TOFAUTI KATI YA FASIHI NA TANZU NYINGINE ZA SANAA

1.     Lugha , kazi zote za kifasihi zinaundwa kisanaa kwa kutumia lugha inayotumika au kuandikika. Lugha hiyo hubeba maana Fulani (ujumbe) kwa jamii Fulani.Hivyo lugha ndiyo inayotufautisha fasihi na Sanaa nyingine. Kwa mfano, uchoraji kipengele chake muhimu kalamu, rangi na kipande cha nguo au karatasi. Ufinyanzi lugha yake ni udongo , uchongaji wa vinyago lugha yake ni gogo la mti n.k. Fasihi si maelezo ya kawaida kawaidakama vile matangazo, taarifa ya habari au barua, fasihi ni maelezo yenye mguso kisanaa. Kazi za kifasihi, huumbwa kimafumbo hutumia nahau au misemo , methali, tamathali za semi, taswira na ishara mbali mbali. Kazi za fasihihufikirisha mtu huweza kutumia akili ili aweze kugundua kazi ya kifasihi aliyosoma au kuisikia kuwa ina maana gani.

2.     Wahusika,kazi yeyote ya fasihi inakuwa na wahusika wake ambao matukio mbali mbali yanayohusu jamii huwazungukia wahusika ni watu ama viumbe, waliokusudiwa wawakilishe tabia za watu katika kazi za fasihi. Kwa upande mwingine wahusika ni muhimu sana katikakutoa na kufikisha dhamira kwa hadira iliyokusudiwa na mwandishi lakini kazi nyingine za sanaa si lazima ziwe na wahusika mfano uchongaji,uchoraji hazina wahusika ambao wanatenda.

3.     Mandhari, kazi ya fasihi inakuwa na mandhri ambayo huonesha tukio linaponyika. Mandharihiyo inaweza kuwa ya kubuni au ya kweli.Mandhari husaidia kujenga hisia inayokusudiwa na mwandishi Lakini kazi nyingine za sanaa hazina mandhari inayoonesha mahali tendo lilipofanyika mfano Udarizi hauwezi kuonesha wapi tendo limefanyika

4       . Utendaji, katika fasihi simulizi utendaji  hushirikisha fanani na hadhira kwa wakati mmoja. Vile vile utendaji humfanya fanani aweze kuonyesha baadhi yamatendo katika usimulizi wake Lakini kazi nyingine za sanaa  utendaji wake haushirikishi fanani na hadhira katika utendaji mfano  uchongaji,baada ya mchongaji kuchonga kinyago anaweza kukiweka mahali popote na hadhira ikakiona lakini haitapata nafasi ya kuuliza maswali n.k

5       Fani na maudhui,kazi za fasihi zina sehemu mbili yaani fani na maudhui na sehemu hizi zinategemeana. Maudhui ni kile kinachosemwa na fani ni namna kinavyosemwa. Kazi nyingine za Sanaa vile vile zinafanikisha ujumbe kwa hadhira lakini mbinu na vifaa vinavyotumika ni sehemu ya fasihi. Kwa ujumla kazi za kifasihi, fani na maudhui yake ni ya hali ya juu sana ukilinganisha  na Sanaa nyinginezo.

 

KWA VIPI FASIHI NI SANAA?

Usanaa wa fasihi hujitokeza katikavipengele mbali mbali kama ifuatavyo:-

1.     Mtindo, Sanaa katika fasihi hujidhihirisha katika namna kueleza jamii (mtindo) katika kueleza jambo kunakuwa na aina fulani ya kiufundi ambao mwanafasihi huutumia katika kufikisha ujumbe kwa jamii yake.Kwa mfano ‘’Mla ni leoleo ,mla jana kala nini?/alileni?’’,Alileni maana yake alikula nini?,,Methali hii imefupisha taarifa ambayo ingeweza kutolewa hivi,mtu anayekula leo ndiye mlaji wa kweli,aliyekula jana hajulikani.Methali hii hutumiwa kutukumbusha kwamba mtu mwenye uwezo au mali leo ndiye atakayeheshimiwa wala si Yule aliyekuwa na uwezo au mali jana.

2.     Muundo,Kazi ya fasihi hupangiliwa katika muundo maalumu ili iweze kuwasilishwa vyema kwa jamii husika.Kila utanzu wa fasihi una muundo wake.Mfano,shairi la kimapokeo huundwa na vipande,mishororo,beti,urari wa vina na mizani.Aidha ,utanzu kama vile methali huundwa na pande mbili;upande wa kwanza huanzisha kauli na upande wa pili hukamilisha kauli hiyo.Pande hizi hutegemeana na kukamilishana.Muundo ndio unaotoa umbo au sura ya kazi husika.

3.     Matumizi ya lugha,Kazi za fasihi huwasilishwa kwa lugha ya kisanaa.Lugha ya kisanaa ni ile iliyojaa nahau, misemo, methali, tamathali za semi,taswira na ishara mbalimbali. Lugha itumikayo katika fasihi ni ya kisanaa. Ni lugha iliyopambwana inayokusudiwa kuibua hisia za namna Fulani kwa hadhira yake. Lugha hiyo inaweza kuchekesha, kukejeli, kubeza, kuchokoza, kutia hamasa au kushawishi. Matumizi ya lugha yako ya aina tofauti, kuna tamathali za semi, misemo, nahau, methali. Lugha ya wahusika hasa lahaja zao, uchaguzi wa msamiati,ufundi wa kutoa maelezo hasa ya wahusika, mandhari na matukio, uteuzi wa lugha yenyewe itumiwayo.

4.     Wahusika,Katika fasihi,wahusika ni vitu,watu au viumbe wengine waliokusudiwa kuwasilisha dhana,mawazo au tabia za watu.wahusika huwa na tabia zinazotofautiana kati yao. Wanaundwa kiufundi sana na msanii anaweza kuamua anataka wahusika wanaowakilisha tabia na matendo fulani tu katika jamii na kwa hiyo atawaumba wahusika hao ili kukamilisha nia na lengo lake.Katika kutofautisha tabia na hali za wahusika,mwandishi analazimika kutumia mbinu ya kuwapa majina wahusika wake. Wahusika wanaweza kuumbwa kinafsi au kiakili na kimwili. Kutokana na ujenzi wa aina hii mhusika huonyesha wasifu wake wa ndani na nje au anaweza kuonyesha mabadiliko yake kila anapokutana na mazingira tofauti.

5.     Mandhari,mandhari ni dhana inayorejelea mahali na wakati kazi ya fasihi inapotendeka.Hiki ni kipengele cha kisanaa kwasababu kinadokeza muktadha wa utokeaji au utendekaji wa tukio la kifasihi.Uteuzi na uumbaji wa mandhari hufanywa kwa ufundi; hivyo,kutoa mchango mkubwa katika kujenga mvuto wa kazi.Kazi za fasihi hutumia mandhari halisi au za kubuni.Fasihi hujengwa katika mazingira maalum. Mandhari husaidia sana kujenga hisia inayokusudiwa na mwandishi.

6.     Uwasilishaji,Uwasilishaji wa kazi yafasihi hufanywa kwa njia yam domo,vitendo au maandishi.Uwasilishaji huo hufanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali  kama vile mpangilio wa matukio,ucheshi na taharuki ili kuleta mvuto katika kazi husika.Mbinu nyingine katika fasihi simulizi huhusisha namna ya utamkaji maneno na sentensi,uchezaji,matumizi ya viungo vya mwili,matumizi ya ala mbalimbali,matumizi ya maleba,uigizaji,kubadili muundo wa simulizi,pamoja na uhusishaji  wa kazi husika na miktadha iliyokaribu na ufahamu wa hadhira.Katika kazi za fasihi andishi,ufundi wa uwasilishaji hufanywa kwa kutumia mbinu kama vile uumbaji wa wahusika,matumizi ya lugha na uumbaji wa mandhari.

 

FASIHI KAMA CHOMBO CHA UKOMBOZI

Ukombozi ni harakati za jamii yoyote zenye lengo la kuitoa jamii hiyo kwa nguvu (kwa silaha) au kwa mazungumzo kutoka katika makucha ya watumwa kisiasa,kiuchumi,kimawazo na kiutamaduni.Jamii inaweza kuwa ni ya kitumwa kisiasa ikiwa haitakuwa na fursa ya kushika hatamu ya uongozi wao na badala yake ikategemea uongozi kutoka kwa jamii nyingine jamii itaitwa ya kitumwa ,kiuchumi,ikiwa haitakuwa na haki ya kuendesha njia mbalimbali za uzalishaji mali.Pia jamii isiyoweza kufikiri na kuamua wala kutokuthamini mawazo yake yenyewe na badala yake ikawa katika mgawanyiko wa ibada na itikadi za kigeni ni jamii isiyo huru kimawazo vile vile jamii haitakuwa huru kiutamaduni ikiwa itakosa kuthamini uaminifu,uumbaji na ugunduzi wake yenyewe badala yake ikasujudu amali zilizo na chimbuko kutoka nje.Nyanja za ukombozi wa jinsi fasihi ya Kiswahili ilivyozitazama mpaka leo

(a)Kisiasa

Ukombozi wa kisiasa unapatikanaje?

Unapatikana tu baada ya kupigania uhuru wa bendera kuwa ndio wa kwanza kupatikana kwa nchi ambayo iko katika harakati za kujikomboa.Katika maandishi ya mengi fasihi ukweli huu unajitokeza kwa mfano katika utenzi wa uhuru wakenya msanii anatuonyesha  juu ya vita vya kumng’oa mkoloni kutoka katika kiti cha uongozi kwanza baada ya mwafrika kupandisha bendera yake mambo mengine yafuatevilevile katika utenzi wa uhuru wa Tanganyika na utenzi wa jamhuriya Tanzania “mwandishi anasisitiza  uhuru wa bendera ukielezwa kuwa kabla ya ukombozi wa aina nyingine kufuata.

Kwa hiyo ukombozi huu wa mwanzo (uhuru wa bendera) husababisha uhuru wa kisiasa wanchi kisha uhuru wa kisiasa huwa ni jukwaa la ukombozi wa uchumi na mambo mengine,vitabu vingine vinavyozungumzia ukombozi wa kisiasa ni mzalendo,F.E.MK Senkoro) Ubeberu Utashindwa(J.K Kiimbila),Tone la Mwisho(E.Mbogo),Kinjikitile na Mashetani(E.Hussein),Nuru mpya(R.Rutashobya)

 

 

 

 

(b)Kiuchumi

Uhuru wa bendera ni sehemu ya mwanzo tu wa ukombozi wa jamii nchi zinaweza kujidai ni huru kumbe uchumi wake bado ungali mikononi mwa nchi nyingine.Nchi nyingi zinazoendelea bado ziko katika harakati hii ya kutaka kujikomboa kiuchumi.Waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili  wamezungumzia sana suala la uchumi katika  mfano ‘’Mashairi ya Azimiola Arusha’’mwandishi anaonyesha na kushambulia unyonyaji ambao ni adui wa uhuru wetu.

Vilevile waandishi wanasisitiza kufanya kazi kama njia ya kuimarisha uchumi.Pia wameeleza kuwa unyonyaji unaweza kukomeshwa kwa kutaifisha njia zote za uzalishaji mali na kuwa mikononi mwa umma. Pia Katika tamthiliya ya “Bwana mkubwa” (J.P Mbonde)mwandishi ameonesha kuwa kwa sasa shabaha yetu sisi ni kupigana na ukoloni mambo leo ili kupata uhuru kamili.Ukoloni mambo leo ni kikwazo cha ukombozi wa kiuchumi. Kwa sababu ya ulegevu wa uhuru wa kisiasa nchi inaweza kuwa na mali  lakini ikizembea kufanya kweli ipasavyo yaweza kufanyiwa njama na ukoloni ndio maana upo umuhimu wa bidii katika kazi na uzalishaji wa mali kisha linafuata swala la ulinzi wa mali hiyo.

Kuzikomboa njia za uzalishaji mali hakutoshi kwani kila hila zao zisizoisha wakoloni wanaweza wakatupora mali hiyo tunapaswa kuwa macho.Katika utenzi wa “Zinduko la ujamaa” mwandishianaeleza utaifishaji wa njia kuu za uchumi na uhalali wa utaifishaji huo. Mwandishi anaonyesha kuwa utaifishaji huo ulifanywa si kwa kuwaona wakoloni kuwa wanadhuluma bali kama njia moja wapo ambayo itaongeza kwenye ukombozi wa kiuchumi katika jamii. Lengo moja ni kufuta ubinafsi ambao unapelekea tofauti za kitabaka na badala yake manufaa ya umma kwa ujumla.

Ukombozi wa kiuchumi si utaifishaji wa njia za uzalishaji mali tu na wala si kukomesha ukabaila na ubepari bali ni kuongeza juhudi katika kazi mbali mbali ili kuongeza kiasi cha pato la kitaifa. Waandishi wengine wanazungumzia ukombozi wa kiuchumi ni kama vile, “Nuru mpya” (G. R. Rutashobya) “Mashetani” (E. Hussein) “Sauti ya dhiki” (A. Abdallah) “Kasri ya mwinyi fuad” (Shafi Adam Shafi) Zetu bora mkulima na wasifu wa siti binti saad(S. Robert).

 

 

 

C) Kimawazo

Ukombozi wa kimawazo ni uhuru wa mtu katika upeo wa fikra pasipo kutegemea mtu mwingine. Hapa mtu aliye huru awe anajiamini mwenyewe na awe mtu kama watu wengine. Awe mwenye uwezo wa kuwaza, kuamua na kutenda, kuchanganua na kupanga kama watu wengine. Mtu aliye mtumwa wa kimawazo anaweza kufananishwa na mnyama wa kufugwa.Mnyama wa kufugwa daima ni mtumwa na bwana wake wakati wote huongojea amri kutoka kwa bwana wake.

Maandishi ya fasihi yanazungumziakwa upana swala hili la uhuru wa mawazo . Katika riwaya ya “Njozi za usiku” dhana hii ya utumwa wa kimawazoipo ndani ya watu wengi ambao wanashikilia hasa baada ya maajilio ya elimu iliyokuja pamoja na ukoloni na ikatumika kwa upotofu. Katika riwaya hii msanii anaonyesha kuwa wale waliosoma walidharau kazi zote za mikono, walifikiri kuwa kazi za mikono zinafaa kwa wale ambao hawakusoma. Wao wanafikiri kuwa kazi ya mtu aliyesoma ni kushika kalamu na kuandika tu au kuwasimamia ambao hawakusoma.Tangu uhuru wa Tanzania kumekuwa na harakati za kufutilia mbal ukanganyifu wa namna hii katika mawazo ya watu. Mawazo ya namna hii ndio yamekuwa yakiwafanya watu wengi wa hali ya chini waamini kuwa uchumi walionao wamepewa na Mungu.

Vile vile kimawazo watu waliamini kwamba kila jambo lilitokana na watawala wa kizungu lilikuwa ni bora kabisa. Kwa mfano hata majina yliletwa toka Ulaya  naya kwetu ya asili kuachwa. Haya yanajadiliwa wazi katika tamthiliya ya “Bwana mkubwa” (J. P. Mbonde)

Katika ukombozi wa kimawazo kuna swala la ukombozi wa mwanamke na swala la dini.Katika suala la ukombozi wa mwanamke watu wengi wanalitazama kirahisi jambo hili. Wengi wanadhani kuwa mwanamke hana haki ya kujibagua kutoka kwa wanaume na kujipigania haki yake. Watu hawa hawaelewi ni mapinduzi gani ambayo hawa wanapigania.Katika fasihi ya Kiswahili Shaban Robert amewatetea wanawake katika kazi zake mbali mbali ikiemo Diwani ya”Wasifu wa siti binti saad” na siku ya watenzi wote. Shaaban Robert amemtazama mwanamke kama mtu anayestahili  utu kama watu wengine wowote wale.

Katika kitabu cha “Wasifu wa Siti binti Saad” msanii au mwandishi anaeleza wazi jinsi jamii ilivyomfanya mwanamke kama chombo cha kutunzwa utawani ili kiwe kizuri kipate kuwavutia wanaokitafuta na baada ya kutoka utawani kikawa mikononi mwa mwanaume kikamtegemea kwa hiyo mwanamke alikuwa ni mtu aliyechukuliwa kama hana wajibu wowote wa maana Zaidi ya kuwa mtegemeaji. Lakini Shabn Robert aliona kuwa ( uk 23) “Ukimdunisha mtu leo utamuona juu ya kilele cha utukufu kesho.

Mawazo ya mwandishi ni kwamba wanawake ni vyema watazamwe katika hali zao za maisha katika ubaya na uzuri kama wanaume. Kuhusu suala la dini linajitokeza katika riwaya ya “Kichwa maji” ambapo mwandishi anaona dini imeanzishwa na waoga ambao hutawaliwa na milango yao ya fahamu badalaya kutawaliwa na akili au bongo zao.

Jambo muhimu katika kumkomboa mtu kimawazo ni kwamba ikiwa dini itaendelea kuwepo isiwe na mtazamo duni na finyu na athari zake ambazo alikuja nazo mkoloni akidai kuwa tamaduni zetu ni za kishenzi. Sharti elimundiyo iwe ya kutafakari na kugeuza mfumo wa maisha ya jamii.

Katika dini pia kuna madhehebu mbali mbali ambayo kati yao kuna uhasama mkubwa, muislamu anadai kuwa yeye ni bora Zaidi kuliko mkristo na mkristo anajiona yeye ni bora kuliko muislamu. Madhehebu yote haya yamechimbuka huko mashariki ya kati…….katika kitabu cha “Bwana mkubwa” (uk 18-19”)……kwanini basi mlitutenganisha katika vikundi vidogo vya madhehebu tofauti kati ya wakristo na waislamu iwapo Mungu ni yule yule mmoja leo mnatueleza tuombe kuungana, utengano alianzisha nani? na kwa faida ya nani?........mbona babu zetu walimwabudu Mungu wao toka zamani kabla ya ujio wa wazungu.

Kwa ujumla dini imechangia kwa kiasi kikubwa sana katika kudumisha mtu kimawazo na kumfanya atumie fahamu tu kwa hiyo katika kumkomboa mtu kimawazo sharti suala la dini litupiwe jicho kali fasihi inazidi kuona jicho lake.

 

(d)Kiutamaduni.

Kwa ujumla utamaduni wanchi zilizotawaliwa na ukoloni umeathiriwa sana na ukoloni huo watu wa nchi hizo wanazipoteza kidogo kidogo thamani za utamaduni zao.Katika fasihi ya Kiswahili ukweli huu wa mambo yameoneshwa  katika kitabu cha “Njozi za Usiku” mwandishi wa riwaya hii ameelezea namna vijana wote hasa waliosoma hawataki kabisa kusikia kuhusu mila na desturi zao (uk 51).Hadi leo vijana wengi wakiwa kwao (vijijini) na ikatokea kwamba kuna ngoma za kienyeji zinachezwa wao husimama mbali au kando wakitazama kwa dharau mambo yanayotendeka mbele yao.Wanaamini kabisa kuwa ngoma hizo ni za kishenzi ngoma ambazo zinafaa kuchezwa na watu wasiosoma watu wasio staarabika.

Katika riwaya ya “Kichwa maji” mwandishi ameonesha jinsi isivyo  kawaida kwa msomi au watu wenye cheo serikalini kucheza ngoma za kienyeji lakini vijana hao hao mwanzoni wasomi wenye mwazo ya kisiasa wakisikia sehemu fulani kuna mziki au disko watajitahidi sana ili wasikose kufika huko.Kwa sasa kuna mtindo mwingine wa kupaka madawa ya kujichubua ngozi waonekane weupe na wengine huvaa nywele za bandia au maiti ili kuficha nywele zao za kipilipili.Huu wote ni utumwa wa kimawazo kwa upande fulani watu hawa wanaamini kuwa uzungu ndilo shina la maarifa, watu hawa hawajui kwamba kuna wazungu wengine ni maskini zaidi hata kuliko sisi wenyewe.

Hivyo ili tujikomboe katika nyanja hizi ni lazima tuondoe ubinafsi, uroho wa madaraka na ulevi wa madaraka hapa nchini.

 

MADA NDOGO; UHURU WA MWANDISHI/MTUNZI WA KAZI ZA KIFASIHI

Dhana ya uhuru wa mwandishi ni pana sana na inatazamwa kwa kuangalia vipengele kadhaa kama ifuatavyo:

Mosi,uhuru wa mwandishi uko katika utashi wa mwandishi mwenyewe.

Utashi ni hiari ya mtu ya kutenda jambo; hali ya kuwa na hamu ya kutaka kutenda jambo. Bila utashi mwandishi atakuwa mwoga na mwepesi wa kukata tamaa.Atayumbishwa haraka kutoka kwenye msingi wa falsafa yake na Imani aliyo nayo juu ya mabadiliko yatokeayo katika jamii.Makombora ya wahakiki na wanasiasa huweza kumyumbisha, lakini kwa mwandishi mwenye utashi makombora hayo humkomaza.

Kwa Afrika kuna waandishi walioonesha utashi wao ni ‘Ole Soyinka na Ngugi wa Thiongowaandishi hawa wameshambuliwa sana na wahakiki, lakini misimamo yao ni ile ile, pia wamewahi kufungwa na walipotoka kifungoni hawakubadili misimamo yao na wamekuwa hivyo kwa sababu ya utashi wa falsafa zao katika fasihi ya kiswahili, waandishi wenye utashi wapo na msingi wa kuwepo kwao ni kutoyumbishwa na matamshi ya jukwaani na wahakiki ambao hawajapevuka.

Pili,uhuru wa mwandishi umo katika kuwa na falsafa moja inayoeleweka,

Falsafa ni mwelekeo wa imani ya msanii au mtunzi kuhusu maisha ya jamii.Falsafa inayofanya maandishi ya mwandishi moja yawe na kitu kijulikanacho kama lengo.Waandishi waliotajwa hapo juu yaani Ole Soyinka na Ngugi wa Thiongo ndio wanaongoza kuwa na falsafa zao zinazojulikana. Katika fasihi ya Kiswahili tunaona waandishi wachache wenye falsafa zao inayojulikana wengi tulio nao wanaandika kufuatana na jambo fulani au tukio la wakati huo bila kulinganisha leo ataandika juu ya mapenzi, kesho juu ya upelelezi na kesho kutwa mapinduzi mwishowe anakuwa na orodha ndefu ya vitabu visivyokuwa na lengo.Waandishi wachache tulio nao ambao wameelekea kuwa na falsafa inayoongoza maandishi yao ni kama Shaban Robert, G.Kezilahabi na Mohamedi Suleiman.Bila kuwa na falsafa maalumu ni rahisi  sana mwandishi kuyumbishwa.

 

Tatu,Mwandishi kuitawala vema Sanaa yake,kama unaandika riwaya na hujui misingi ya Sanaa ya aina hiyo atajikuta katika kikwazo,utajikuta uhuru wa kisanaa unaweza kujaribu, lakini kazi utakayoitoa itakuwa hafifu.Kazi nzuri ya kisanaa ni ile inayounganisha vema ubunifu na uhalisia.Mwandishi akielemea sana katika ubunifu anazua matatizo mengine kazi ngumu aliyonayo mwandishi ni katika kupata barabara msitari huo.Mwandishi mwenye vitabu vingi anaweza kuwa na kitabu kimoja tu kilichoupatia vema mstari huo. Katika fasihi ya Kiswahili waandishi walioupatia msitari huo tunao ni kama vile Ebraim Hussein,Penina Mhando,Mohamed Suleiman,C.G Mng’ong’o na J.A.Safari.Msanii anayeweza kuitawala  vema Sanaa yake anaunganisha vizuri Sanaa na maudhui yake.

 

Mwisho, uhuru wa mwandishi umo katika lugha anayotumia,ili msanii atawale vema Sanaa yake nilazima ajue lugha anayotumia.Lugha ndicho kiungo maalumukati ya Sanaa na kazi ya kifasihimwandishi kama hajui vema lugha anayotumia atajikuta hana uhuru wa kukisema anachotaka kwa hiyo lugha ndiyo nguzo ya nne katika uhuru wa mwandishi, waandishi wa Kiswahili  waliokwisha kutajwa wanakitawala Kiswahili sanifu,Kiswahili sanifu ndiyo msingi wa fasihi ya Kiswahili.

 

 

Ni kweli kuna uhuru wa mwandishi?

Uhuru wa mwandishi ni nini?

Ni ile hali ya mwandishi wa fasihi kuwa huru na wazi katika kutoa mawazo au hisia zake kwa jamii.Ni uhuru wa kuandika na kulikosoa tabaka lolote katika jamii bila kupata matatizo yoyote.

 

Mwandisihi ni nani?

Ni mtu yoyote atumiaye muda wake mwingi  kuandika na kuzungumzia jamii yake kwa njia ya maandishi.

 

Je kuna uhuru wa mwandishi?

Kwa ujumla uhuru wa mwandishi ni uhuru ikiwa hakufaulu kudhuru tabaka tawala hii ni kwa sababu suala la uhuru wa mwandishi ni la kitabaka na lilianza pale jamii ilipogawanyika katika matabaka kwa maana hii uhuru wa mwandishi unaamuliwa na tabaka tawala

Kuanzia enzi za utumwa, maandishi ya liyovumbuliwa katika  fasihi andishi ya mwanzo ilikuwa ya wateule wachache tu na wenye vyeo vyao.Hao mabwana, wamwinyi na mabepari walihakikisha kila mbinu inatumika ikiwemo ya udhibiti wa maandishi ili kuendeleza na kulinda utawala wao.

Goya B. (1974-78) anasema kuwa mwandishi hana uhuru kwa vyovyote vile kwa sababu yeye ni tokeo la jamii Fulani, kila jamii ina mipaka yake ambayo mtu hatakiwi kukiuka kwa vyovyote vile mwandishi huyu amebanwa na mipaka hiyo asivuke.Pindi avukapo mipaka hiyo atapambana na jamii hiyo (tabaka tawala) vitabu vya mwandishi huyo vitapigwa marufuku au vitabu vikitolewa havitanunuliwa au serikali itavikusanya na kuvifanyia mipango mwingine. Katika Afrika  kuna mifano mingi ya udhibiti wa waandishi mfano mzuri ni mwandishi maarufu wa Kenya Ngugi wa Thiongo ambaye kazi zake hasa ya “Ngaahika Ngeenda”(I will marry when I want)- Nitaolewa Nitakapotaka, ilimgombanisha na vyombo vya dola hadi akawekwa kizuizini, Ngugi ni mwandishi wa kwanza kufichua siri za mfumo wa kibepari kwa watu wanyonge aliliuzi tabaka tawala la jamii yake ambalo halikusita kutumia udhibiti na vyombo vyake vya Mabavu.

Baada ya uhuru vitabu vingi sana viliandikwa kwa kudhibitisha mambo mbalimbali yaliyojitokeza waziwazi E.Kazilahabi aliandika riwaya“Rosa mistika”(1971),kitabu hiki kilipigwa marufuku kisitumike mashuleni na wala kisiuzwe waziwazi madukani.Ilidaiwa na waliokipiga marufuku kuwa kilikiuka maadili ya jamii kwa kueleza mambo ya aibu kwa wazi.Sura ya kumi ndiyo hasa ilitolewa mfano wa uchafu wa kitabu hiki.Udhibiti huo ulifanywa na Wizara ya Elimu na ulizusha maswali mengi kwa wasomaji.Wasomaji walianza kujiuliza, Je si kweli uchafu uelezwao katika “Rosa mistika” umo ndani ya jamii ya Tanzania? Je upotofu na uongozi mbaya ulifuchuliwa na riwaya hiyo hii si upo kati yetu? Kwa baadhi ya wasomaji ilielekea kuwa suala la uchafu wa maelezo yatokeayo kitandani baina ya wakuu wa chuo na wanafunzi wao lilitumika kama kisingizio tu cha kudhibiti ukweli wa masuala mengine nyeti yaliyowagusa viongozi yaliyowakilishwa na watu kama vile Bwana Maendeleo Deogratius anayeshiriki katika kuwaharibu vijana.

Vitabu vingine ambavyo havieleweki vinasema nini, maudhui, falsafa na ujumbe wa mwandishi ni mashetani(E.Hussein)“Aliyeonja Pepo”(F.Topan) na “Ayubu” Paukwa theatre Association.Na hivi viko kwa kukwepa mkono mrefu wa tabaka tawala.

 

DHIMA YA UHURU WA MWANDISHI.

·        Mwandishi atakuwa huru kuikosoa jamii au tabaka lolote litakaloenda kinyume na utaratibu wa jamii bila matatizo.Mwandishi atakuwa huru kuonyesha dhuluma, ukatili na ujangili unaofanywa katika jamii na tabaka lolote bila matatizo yoyote.

·        Kukiwa na uhuru wa mwandishi, msanii atakuwa na falsafa inayoeleweka pamoja na utashi wake.Hii itamfanya mwandishi awe na msimamo unaoeleweka.Msimamo  wake utamsaidia kuifundisha na kuielimisha jamii bila uoga.Ataijiulisha jamii hali yake na ataonesha jamii njia za kufikia haja na kutatua matatizo ya jamii bila uoga

·        Mwandishi atakuwa huru kutoa mwongozo katika jamii kwa kuikomboa jamii kutoka katika fikra mbovu za kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa na tabaka tawala ili jamii ipate haki na heshima bila woga wa kuliondoa tabaka ambalo ndilo lenye mamlaka yote katika jamii.

·        Uandishi wa kikasuku utapungua, waandishi au wasanii huacha tabia ya kuwa vipaza sauti vya tabaka fulani katika jamii, wasanii makasuku huandika mambo bila kufikiri na kurudiarudia  mawazo yaliyokwisha semwa na wanasiasa majukwaani bila fikra mpya kwa hali hii hupotosha jamii.Hivyo kunapokuwa na uhuru wa mwandishi wa kutosha hali hii haiwezi kutokea kwa sababu mwandishi ataandika mambo mbalimbali yanayojitokeza katika jamii na hataweza kujikomba au kujipendekeza kwa tabaka tawala lenye mamlaka yote katika jamii.

·        Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi fasihi inakuwa chombo cha kuikomboa jamii kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kifikra (kimawazo). katika jamii ya kitabaka fasihi ni mali ya tabaka tawala na hutumia fasihi kutetea na kulinda maslahi yao.Hivyo inapokuwa mali ya jamii nzima inatumiwa na jamii hiyo katika kuwakomboa wanajamii wote.

·        Kunapokuwa na uhuru wa mwandishi, mwandishi anakuwa huru kuichokoza na kuisukasuka (kuichochea)jamii bila matatizo yeyote. Mwandishi atachokoza jamii ya wakulima na wafanyakazi kufikiri ili waweze kulichunguza tabaka tawala kwa jicho pevu na kutoa hadharani uozo uliopo katika kunyonywa, kupuuzwa,kuonewa, kugandamizwa na kunyanyaswa na tabaka tawala

·        Mwandishi atakuwa huru kuelimisha na kuishauri jamii katika mambo muhimu yanayojitokeza katika jamii bila woga.Mwandishi ataishauri jamii kuhusiana na mambo kama vile afya, elimu na ichague mambo gani yanafaa kuhifadhiwa na yapi hayafai vile vile msanii anakuwa huru kuirekebisha jamii bila woga kwa kuangalia yapi ni mazuri na yapi ni mabovu yanayotendeka katika jamii.

 

SABABU ZA UDHIBITI WA KAZI ZA FASIHI

Kazi nyingi za fasihi hudhibitiwa kutokana na sababu zifuatazo;

Ø Msanii kushindwa kuitawala vema lugha yake yaani kutumia lugha vibaya kama vile lugha ya matusi,lugha isiyosanifu n.k

Ø Kulinda maadili ya jamii hasa kwa waandishi wanaoandika baadhi ya mambo ambayo hayapaswi kuelezwa wazi mfano mambo yanayohusiana na mila na desturi za jamii kama vile Jando na  Unyago.

Ø Kulinda maslahi ya taasisi Fulani kama vile Serikali au wizara ,bunge,kanisa n.k mfano baadhi ya kazi za Ngugi Wathiongo zilidhibitiwa kwasababu ya kuikosoa serikali  iliyokuwa madarakani nchini Kenya.

Ø Kuzuia uvunjifu wa amani hasa kama kazi hiyo imelielezea vibaya tabaka tawala.

 

ATHARI HASI ZA UDHIBITI WA KAZI ZA FASIHI

Ø Hupunguza  uhuru wa mwandishi wa kazi ya fasihi

Ø Huondoa demokrasia ya wanajamii kuandika lolote bila woga.

Ø Hufinya taaluma ya uandishi na sanaa yake

Ø Hupelekea kuibuka wa kazi za fasihi ya kikasuku

Ø Hupelekea watunzi wa kazi ya fasihi kukosa falsafa inayoeleweka

Ø Wasanii watakuwa na hofu hivyo watashindwa hivyo watashindwa kuielimisha jamii katika mambo muhimu.

 

MBINU AU NJIA ZA KUEPUKA UDHIBITI WA KAZI ZA FASIHI

Baadhi ya mbinu au njia za kuepuka udhibiti wa kazi za fasihi ni hizi zifuatazo;

Ø Kutumia mafumbo mengi na lugha ya picha katika utunzi wa kazi za fasihi.

Ø Kutumia ucheshi kwa kiasi kikubwa yaani mbinu  ya igizo ndani ya igizo.

Ø Kutumia wahusika wa kubuni katika kazi za fasihi.

Ø Kutumia mandhari  ya kubuni katika uandishi wa kazi za fasihi

 

MADA NDOGO; DHANA YA UDHAMINI KATIKA KAZI ZA FASIHI

UDHAMINI

Ni hali ya watu au shirika fulani kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia kitu fulani . Mdhamini au wadhamini ni kundi la watu wenye shabaha zinazofanana wenye kusimama kama ufadhili wa mradi fulani. Katika fasihi hawa ni wale wanaosimamia makundi maalumu kipropaganda na kiitikadi.

 

AINA ZA UDHAMINI

Kuna udhamini wa nne mbili:-

i)                   Udhamini wa Jamii

ii)                Udhamini wa ushawishi

iii)              Udamini wa nguvu

iv)              Udhamini wa mtunzi mwenyewe

 

Ø Udhamini wa jamii

Ni udhamini ambao walengwa wa kazi ya sanaa ni wanajamii wenyewe.Wao ndio wasomaji wa mashairi,riwaya au tamthiliya na ndio wanunuzi wa kazi za sanaa.Mwandishi na msanii hujitahidi kuwaridhisha wanajamii ili waipende na kuinunua kazi yake.

Ø Udhamini wa mtunzi mwenyewe

Katika aina hii ya udhamini mtunzi wa kazi ya fasihi anaweza kujidhamini yeye mwenyewe wakati wa uchapishaji wa kazi zake.Wakati mwingine hutumia fedha zake katika kuhakikisha kuwa kazi yake inazalishwa kupitia usimamizi wake.Wakati mwingine anaweza kusambaza kazi zake yeye mwenyewe au kupitia kwa wasambazaji mbalimbali ambao wanakuwa kama mawakala wake.Katika udhamini huu mtunzi huandika au kutunga kazi za fasihi zenye ujumbe anaoutaka yeye mwenyewe kwasababu hafuati matakwa ya mtu mwingine.Msanii anayeweza kujidhamini anauwezo wa kutetea tabaka lolote analolitaka.

 

Ø Udhamini wa ushawishi

Ni aina ya udhamini ambao mdhamini huwashawishi na kuwanunuawaandishi au wasanii. Matokeo yake ni kwamba msanii anafungwa na matakwa ya mdhamini.

Ø Udhamini wa nguvu

Huu ni udhamini unaotumia vyombo vya dola kama vile jeshi, polisi, magereza kumdhamini mtunzi au mwandishi n.k.Hakuna hiari katika udhamini wa nguvu, kila kitu kinaendeshwa kama vile mashine tu. Kwa ujumla mwandishi akidhaminiwa kwa nguvu za serikali huwa kama kasuku aimbaye na kuutukuza mfumo wa maisha uliopo katika jamii hata kama roho na moyo wake viko mbali sana na mfumo huo. Lakini msanii anapodhaminiwa kutetea umma, lazima kutakuwa na madhara yake katika jamii yake inayohusika.

Mwandishi wa fasihi katika kila nchi atakuwa na udhamini unaolingana na mazingira yake kwa mfano katika nchi ya Tanzania, mwandishi anaweza kuandika kwa udhamini wa jamii yake inayohusika.Mdhamini anaweza kuwamtu binafsi mwenye fedha, shirika, chombo cha serikali, chama fulani au kundi la mataifa kwa ushirikiano. Pia mdhamini ni mwakilishi wa wenye mamlaka juu yake, kwa mfano katika serikali yaTanzania chuo kikuu ni mwakilishi wa serikali na serikali ni mwakilishi wa tabaka tawala. Hivyo msanii anayedhaminiwa na chuo kikuu ambacho ni chombo cha serikali hatimaye anajikuta anafanya kazi ili kuendeleza maslahi ya tabaka tawala.

 

SABABU ZA UDHAMINI KATIKA KAZI ZA FASIHI

Ø Kutojiamini,Baadhi ya wasanii ni waoga na hawajajiamini katika kufanya kazi zao.Wanafikiri kuwa bila mtu Fulani hawawezi kufaninikiwa kisanaa.Kwa hiyo huwalazimu kutafuta mdhamini ili wafanikiwe.

Ø Kulazimishwa,Hii inatokea pale ambapo tabaka moja katika jamii lina nguvu za kisiasa na kiuchumi kiasi cha kuwa na nguvu juu ya matabaka mengine.Hivyo msanii apende asipende atadhaminiwa na tabaka lenye nguvu.Iwapo msanii atakataa kudhaminiwa na tabaka hilo,kazi zake zinaweza kupigwa marufuku au kuthibitiwa.

Ø Uhaba wa fedha kwa waandishi za kuendeshea shughuli zao za uandishi katika uandishi wa kazi za fasihi. Pesa zinahitajika kwa ajili ya kununulia karatasi, kalamu, uchapaji n.k.

Ø Kulinda na kutetea maslahi yawadhamini wao. Hii inatokea zaidi kama mdhamini ni wa tabaka tawala. Kama tabaka linalo tawala ni la mabepari kazi za fasihi zitatetea tabaka hilo.

Ø Kutaka kujulikana au kuipendekeza.Baadhi ya waandishi hudhaminiwa kwasababu ya kutakakujulikaa na kwa upande mwingine mdhamini anawadhamini waandishi kwa lengo hilo.

Ø Tamaa ya kupata fedha za haraka.Hawa huandika vitabu vyenye kujaa wahusika wakuu, mafundi wa kufanya mahaba, kutumia madawa ya kulevya na kufanya mapenzi kwa kutumia mipira ya kiume na kike bila kujali staha utamaduni wa jamii yake. Mwandishi anachojali hapa ni pesa na sio matakwa ya jamii yake.

Ø Kulazimishwa na tabaka tawala.Waandishi hawawanakubali udhamini huo kwakuogopa udhabiti wa kazi zao na tabaka tawala. Waandishi hawa wakikataa udhamini huo kazi zao zitadhibitiwana kupigwa marufuku zisisomwe au kuchapishwakabisa.

 

ATHARI ZA UDHAMINI

Udhamini unafaida na hasara katika kazi za kifasihi.Zifuatazo ni faida na hasara hizo.

 

   Faida za udhamini

Ø Husaidia baadhi ya waandishi/wasanii kufanya tafiti za masuala mbalimbali yanayohusu jamii.Baada ya tafiti hizo,wasanii huwasilisha masuala hayo kwa njia ya sanaa.

Ø Husaidia kuibua na kuendeleza vipaji vya wasanii chipukizi ambao hawana fedha za kutosha ili kukamilisha kazi zao na kuonesha vipaji vyao kwa jamii.Kwa mfano,mashindano ya uandishi wa kazi za fasihi kwa shule za sekondari yaliyodhaminiwa na Umoja wa Waandishi wa Vitabu Tanzania (UWAVITA) miaka ya 1970 yalisaidia kuibua na kuendeleza vipaji vya waandishi chipukizi ikiwa ni pamoja na kuchapisha kazi zao.Pia mashindano ya ushairi ya ‘Tuzo ya Ebrahimu Hussein’’ yamesaidia kuibua vipaji vya washairi chipukizi,pia Bongo star search ya TBC1 na Tanzania House of Talents ( THT) ambayo ipo chini ya Clouds Media group hudhamini wanamziki wachanga.Wadhamini hawa huweza kuibua na kuendeleza vipaji vya washiriki.

Ø Husaidia kuleta ushindani na ubora wa kazi katika soko la kazi za fasihi.Uwepo wa wadhamini wengi husababisha kuwapo kwa wasanii wengi na hivyo kuwa na kazi za kutosha.Matokeo yake huleta ushindani wa bei katika soko.Hili husaidia kuinua kiwango cha ubora wa kazi husika kwani kazi duni hukosa wanunuzi hata kama zitauzwa kwa bei ya chini.

Ø Baadhi ya wasanii hujipatia fedha kutokana na kudhaminiwa.Hii inatokana na mgao ( mrabaha) wanaoupata baada ya kazi zao kuuzwa.Vilevile ,wasanii huwatajirisha wadhamini kutokana na mauzo ya kazi zao.

Ø Husaidia jamii kupata kazi mbalimbali za fasihi,hasa fasihi  andishi ambayo inahitaji fedha nyingi ili ikamilike.Kupitia msaada wa wadhamini,mwandishi hapati shida kuzalisha na kusambaza kazi yake kwa umma.Kazi hizi zote hufanywa na wadhamini na hivyo huwafikia  walengwa kiurahisi.

 

HASARA ZA UDHAMINI

Ø Mwandishi anayedhaminiwa anatakiwa kuandika yale tu ambayo mdhamini wake anayataka. Msanii hatakuwa na uhuru wa kuandika kitu chochote na kwa njia anayotaka.

Ø Mapana ya uandishi wake kidata, kigiografia na kimaudhui huamuliwa na mdhamini na kutegemea mahitaji yake na kiwango cha fedha alichonacho mdhamini.

Ø Ufafanuzi wa data na maudhui ya kazi ya fasihi lazima ulingane na mtazamo wa itikadi ya mdhamini.Hii ina maana kuwa mwandishi wa kazi ya fasihi hawezi kufanya ufafanuzi wa data na maudhui mwenyewe bila kumshirikisha mdhamini.

Ø Matokeo ya uandishi wa kazi za fasihi mara nyingi ni mali ya mdhamini na hutumia kuendeleza maslahi yake mabayo sio lazima yalingane na malengo ya mwandishi.

Ø Wasanii au waandishi wengi kutokana na kudhaminiwa huanza kuandika kazi zao kwa kupenda pesa hii huwafanya waandishi kuwa makasuku kwasababu ya kuandika yale tu yasemwayo na mdhamini wake bila kuyafanyia uchambuzi wa kina.

Ø Udhamini hukuza utabaka katika jamii, hapa tunakuwa na tabaka la wenye nacho (mdhamini) na tabaka la wasionacho (msanii) mdhamini humnyonya msanii.

Ø Kuzuka kwa fasihi pendwa (riwaya ya pendwa).Hapa waandishi huandika kazi zao kwa lengo la kupata pesa za haraka, huandika riwaya pendwa ambazo zina soko kubwa hapa nchini hasa kwa vijana na wakati huo huo riwaya hizo hazifunzi lolote jamii Zaidi ya kuburudisha.

Ø Huchochea rushwa, hii ni kwa sababu waandishi wengi wanataka udhamini huo na matokeo yake wale wanapata udhamini huo lazima watoe chochote (rushwa) kwa mdhamini.

 

 

 

UMUHIMU WA UDHAMINI

·        Husaidia waandishi chipukizi katika kuchapisha kazi zao.

·        Husaidia waandishi katika kufanya utafiti wa mambo mbalimbali yatakiwayo katika Sanaa hiyo ya fasihi.

·        Husaidia jamii kupata kazi mbali mbali za kifasihi.

·        Husaidia kuleta ushindani wa ubora wa kazi katika soko la kazi za fasihi.

·        Husaidia kuinua vipaji hasa vya waandishi chipukizi.

 

 

 

 

MADA  2 : MAENDELEO YA FASIHI SIMULIZI

UWASILISHAJI NA UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

Fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji wake.

AU

Ni fasihi inayotungwa kichwani kabla ya uwasilishaji,au papo kwa papo,na kuwasilishwa kwa njia yam domo,vitendo au ishara.

Mazungumzo hayo huwa katika mfumo wa masimulizi kwa kuumbwa, kutambwa, kuganwa au kutongolewa.Fasihi simulizi hueleza jamii kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa. Fasihi huzungumzia juu ya yale mambo ambayo huzunguka jamii husika na  huathiriwa sambamba na mabadiliko ya jamii na kwa hiyo nayo hubadilika kimaudhui na kifani kufuatia mabadiliko ya mifumo ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii.Fasihi simulizi ni utanzu wa Sanaa ambao hukua na kubadilika kutokana na mabadiliko ya wakati na mifumo ya jamii.

 

VIPENGELE MUHIMU VYA FASIHI SIMULIZI

(a) Msimulizi (fanani),Huyu huwa ni mtu ambaye anaitamba hadithi, kuimba wimbo, kusimulia au kutoa vitendawili au methali.

(b) Wasikilizaji au watazamaji (Hadhira),Hawa ni washiriki katika kutazama au kusikiliza fani ya fasihi simulizi na mara nyingine huwa wanatumiwa na fanani kama wahusika katika kazi yake

(c)  Mandhari, Hili ni jukwaa au mahali ambapo tukio la kifasihi (fasihi simulizi) litatendeka.Pahali au mahali hapo yaweza kuwa nyumbani, uwanjani, kuzunguka moto, baharini n.k.

(d) Tukio/Dhana inayotendeka,Hili huwa ni tendo linalotendeka katika jukwaa la fasihi simulizi. Tendo hili laweza kuwa ni usimulizi wa hadithi, kutega vitendawili, kuimba nyimbo au wimbo au kutoa methali.

 

SIFA ZA FASIHI SIMULIZI.

Ø Huwasilishwa kwa njia ya mdomo ,vitendo na ishara.

Ø Ufanisi wake kisanaa hutegemea uwezo wa fanani au wahusika.

Ø Masimulizi yake huweza kuathiriwa na mazingira ,hisia na hali.

Ø Huweza kubadilika kutoka kizazi kimoja hadi kingine katika mazingira mbalimbali kutegemea ufundi na kumbukumbu ya fanani.

Ø Fasihi simulizihushirikisha fanani na hadhira katika utendaji kwa wakati mmoja.Hii humfanya fanani aweze uonyesha baadhi ya matendo katika usimulizi wake kama vile kutumia viungo vya mwili kwa kuchezesha midomo, kukunja uso, kubinya macho, kuchezesha mabega n.k.

Ø Fasihi simulizi ina sifa ya kuwepo kwa fanani ambaye huweza kusimulia kwa kuimba, kusoma kwa sauti au kubadilisha mtindo wa usimuliaji wake,fanani huweza kufanya yote hayo kama akiona hadhira yake imechoka kusikiliza.Pia ana uwezo wa kuona kama ujumbe wake umeeleweka au la!

Ø Fasihi simulizi zina sifa ya kwenda na wakati na mazingira, tabia hii inatokana na jinsi fasihi simulizi inavyoenea wasikilizaji huwa wengi na hata kama baadhi tanzu za fasihi simulizi zilipitwa na wakati zinaweza kubadilishwa na fanani ili zisadifu mazingira maalumu ya wakati huo.

Ø Fasihi simulizi huzaliwa, hukua, huishi hata kufa hii inasababishwa na mabadiliko ya mazingira ambayo hufuata mfumo wa kihistoria wa jamii, mfano kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya kuhifadhi fasihi simulizi katika maandishi ya fasihi simulizi huonekana chapwa kwa sababu ya mambo kama vile miondoko au ngoa, vinakuwa havimo.

Ø Fasihi simulizi inauwanja maalumu wa kutendea, Fasihi simulizi huwa na sehemu inayochaguliwa kwa ajili ya aina fulani ya fasihi simulizi itakayofanywa na wahusika. mfano tambiko huwa na sehemu maalumu ya kutambikia kama vile sehemu yenye pango,kwenye mti mkubwa kama vile mbuyu, njia panda, makaburini n.k.Hivyo ni wazi kwamba fasihi simulizi inahitaji uwanja wa kutendea yenye kuhusisha vitendo.

Ø Fasihi simulizi ni mali ya jamii nzima.Tanzu zake zote zikishatendwa humilikiwa na jamii kwa pamoja na hii ndiyo inayopatiwa uwezo wa kurithishwa kizazi kimoja hadi kingine.Hivyo huwafikia watu wengi hata wale wasiojua kusoma na kuandika.

 

TANZU ZA FASIHI SIMULIZI

Fasihi simulizi imegawanyika katika tanzu mbalimbali kufuatana na wataalamu walivyoainisha.Baadhi ya tanzu hizo ni Hadithi,Ushairi,Semi na Sanaa za maonesho na kila utanzu umegawanyika katika vipera mbalimbali kama inavyoonesha katika kielelezo kifuatacho;

FASIHI YA KISWAHILI

 

 

 

 


            Hadithi             Ushairi                     Semi        Sanaa za maonesho

Ngano Vigano

Visasili Soga

Hekaya Tarihi

Visakale

Mashairi  Nyimbo

Tenzi Ngonjera

Majigambo Maghani

Methali Nahau Misemo Mafumbo Vitendawili Mizungu Lakabu Misimu

Ngonjera Majigambo Maigizo Tambiko Vchekesho Ngoma Sarakasi Mazingaombwe Utani Mivigha Michezo ya watoto

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa msingi huo, fasihi simulizi ni aina ya fasihi ambayo hutumia lugha ya

kisanaa ya mazungumzo katika kuwasilisha fikra za binadamu kwa hadhira

iliyokusudiwa.  Fasihi simulizi ni masimulizi yanayotumia lugha ya sanaa na

matendo katika uwasilishaji wake unaofanyika kwa kushirikisha fanani

(msimuliaji au mzungumzaji) na hadhira (msikilizaji au wasikilizaji).  Mifano ya

kazi za fasihi simulizi ni hadithi, ngonjera, maigizo na nyimbo. Fasihi simulizi ni

fasihi inayohusisha tukio au fani inayotendeka, fanani, hadhira na mandhari

(mazingira na wakati).  Fasihi simulizi ina tanzu kuu nne (4), ambazo ni hadithi,

semi, ushairi na sanaa za maonesho.

 

Dhima ya fasihi simulizi.

Fasihi simulizi ina dhima, majukumu, kazi au umuhimu mkubwa kwa jamii kama ifuatavyo:-

(a)    Fasihi simulizi huburudisha jamii.

Fasihi simulizi hufunza maadili mema katika jamii.  Huonya, hukataza na hukosoa maovu yaliyomo k atika jamii.  Kwa mfano kupitia hadithi, hususani ngano na vigano, jamii hujifunza maadili mema na hukatazwa kutenda maovu.

 

(b)    Fasihi simulizi huburudisha jami.

Fasihi simulizi hutumia ubunifu au ufundi katika fani ili kumburudisha msikilizaji na mtazamaji.  Fasihi simulizi humburudisha mtu kimwili na kiakili kwa kupitia nyimbo, matendo ya wahusika, ala za muziki, hadithi, n.k.

 

(c)    Fasihi simulizi huhifadhi na hurithisha utamaduni au amali za jamii. 

Fasihi simulizi hutunza utamaduni au amali (mila na desturi) za jamii na huwea kueneza au kurithisha utamaduni au amali hizo kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kupitia nyimbo, methali, vitendawili, maonesho, hadithi na ushairi.

 

(d)    Fasihi simulizi hukomboa jamii.

Fasihi simulizi huzungumzia mambo muhimu yanayoleta mabadiliko katika jamii, ikiwemo kuwasihi watu waache mila potofu kama mauaji ya albino, ukeketaji na unyanyasaji wa kijinsia kwa kupitia nyimbo mballllilmbali, mfano nyimbo za bendi na za dini.  Kwa msingi huo, jamii inakomboka kutoka kwenye fikra potofu na uovu mwingine.

 

(e)    Fasihi simulizi hikuza na huendeleza lugha.

Fasihi simulizi huibua maneno au msamiati mbalimbali kiasi cha kuikuza lugha kutokana na mawasiliano ya wanajamii ya kila siku kupitia misemo, nyimbo,        tamathali za semi, methali na vitendawili.  Mambo hayo ndiyo yanayoivutia jamii kujifunza lugha.  Msamiati unaoibuliwa hufanya lugha ikue na kuendelezwa kwa watu wengine.

 

(f)     Fasihi simlizi huhifadhi historia muhimu ya jamii.

Fasihi simulizi hutumika kutunza kumbukumbu ya mambo muhimu ya kihistoria ya jamii ambayo vizazi vijavyo havina budi kujifunza.  Historia ya jamii huhifadhiwa kupita hadithi anuai kama vile visakale, tarihi, ngano na visasili.

 

(g)    Fasihi simulizi huhimiza na huhamasisha utendaji wa shughuli mbalimbali katika jamii.

Kwa mfano, katika jamii ya wakulima, nyimbo zinzao imbwa wakati wa kulima na mavuno huhamasisha utendaji kazi.  Aitha, katika jamii ya waavuvi, nyimbo wanazoimba huchochea bidii ya kazi n.k.

 

(h)    Fasihi simulizi hutoa mchango mkubwa katika fasihi andishi.

Kimsingi, maudhui ya fasihi andishi hutokana na m change wa fasihi simulizi.  Fasihi andishi hutumia vipoengele mbalimbali vya fasihi simulizi ili kuipa ubora kazi hiyo.  Vipengele vinavyotumiwa ni pamoja na wahusika wasio binadamu (mfano wanyama), semi mbalimbali, mbinu ya masimulizi ya hadithi na ushairi wa fasihi simulizi (mfano nyimbo).

 

(i)     Fasihi simulizi huhimiza amani, upendo na ushirikiano katika jamii.

(j)     Fasihi simulizi hufariji na huliwaza jamii.  Kwa mfano kupitia nyimbo za msiba.

(k)    Fasihi simulizi huchochea au huhimiza ujasiri na ushujaa katika maisha. Kwa mfano kupitia nyimbo za vita.

 

Sifa bainifu zinazoipa uhai fasihi simulizi.

Fasihi simulizi ni hai kw asababu ya sifa zifuatazo:-

a)     Hubadilika kulingana na  mazingira, wakati na mifumo ya jamii.

b)     Huhusisha utendaji (matendo) kwa kutumia viungo vya mwili.

c)     Hadhira hushiriki moja kwa moja wakati wa uwasilishaji wa kazi ya kifasihi.  Hadhira huweza kuuliza maswali, kushiriki utendaji na kushagilia.

d)     Huwa na uwanja maalulmu wa kutendea.  Kwa mfano katika jukwa ambalo huleta uhalisia wa kazi husika.

e)     Hukutanisha fanani na hadhira, hivyo hupelekea kukuza uhusiano kati ya fanani na hadhira,

f)      Hupokea marekebisho ya papo hapo.

 

Umuhimu wa viungo vya mwili katika fasihi simulizi.

Viungo vya mwili (mdomo, kikono, pua, miguu, ulimi, macho na kichwa)vina umuhimu mkubwa sana katika kukamilisha fasihi simulizi kama ifuatavyo:-

(a)    Mdomo: humsaidia fanani kuwasilisha ujumbe kwa hadhira.  Pia

huwasaidia hadhira kuonesha ushiriki wao kwa kuitikia, kuuliza maswali, kujibu, n.k.

 

(b)    Mikono: humsaidia fanani kusisitiza mazungumzo, kuita, kuzuia na kuingiza matendo.  Aidha, mikono huwasaidia hadhira kupiga makofi.

 

(c)    Pua: husaidia katika kuigiza kunusa na kuashira harufu mbaya na nzuri.

 

(d)    Ulimi: husaidia katika kutamka maneno kwa usahihi.  Pia, ulimi husaidia kupiga yowe au vigelegele na kuigiza sauti mbalimbali.

 

(e)    Macho: humsaidia fanani kuonesha  ishara mbalimbali wakatiwa uwasilishaji ili kuonesha au kusisistiza jambo Fulani.  Kwa mfano kukataza, kuruhusu, kushangaa, n.k.

 

(f)     Kichwa: humwezesha mtu kuhifadhi kazi fulanil ya fasihi kwa ajili ya kumbukumbu na kuiwasilisha mahali inapohitajika.

 

Wahusika wa fasihi simulizi

Wahusika ni watendaji katika kazi ya fasihi.   Fasihi simulizi ina wahusika wa aina tano (5) kama ifuatavyo:-

1.     Fanani (msimuliaji / mzungumzaji)

2.     Hadhhira (msikililzaji / wasikilizaji)

3.     Binadamu (watu)

4.     Wanyama na viumbe wengine, kama vile fisi, samba, samaki (pono) sungura kobe, n.n

5.     Mahali na vitu visivyo na uhai, kama vile jingo, pango, vichaka, bwawa, mto, mlima, kiti, mawe, n.k.

 

Sababu za fasihi simulizi kutumia wahusika walio binadamu.

Fasihi simulizi hutumia wahusika wasio binadamu kwa sababu zifuatazo:-

(a)    Kuepuka migogoro katika jamii.  Fasihi simulizi huepika kutumia majina halisi ya wahusika (binadamu) ili kukwepa uchukuaji wa hatua wa wahusika wanaotajwa.

(b)   Kuvuta umakini wa hadhira au wasikilizaji.  Hadhira kuu ya fasihi simulizi katika utanzu wa hadithi ni watoto.  Watoto huvutiwa na wanya.  Hivyo utumiaji wa wahusika wanyama katika hadithi huvuta umakini wa watoto kuisikiliza hadithi hiyo.

(c)   Kuburudisha na kufurahisha hadhira.  Matendo ya baadhi ya wahusika wanyama, kama vile fisi, sungura na kobe, hufurahisha sana.  Hivyo wanapotumiwa katika masimulizi ya hadithi hadhira hufurahi na huburudika.

(d)    Kudhihirisha uhalisia wa tabia za binadamu.  Baadhi ya wanyama wanahulka au tabia zinazofanana na binadamu.  Kwa mfano, tabia ya ulafi na uchoyo (fisi), tabia ya ukaatili (samba) na tabia ya ujanja (sungura).

(e)    Kuwajengea hadhira uwezo mkubwa wa kufikiri na kupata mafunzo au maadili ya kazi husika

(f)     Kuonesha ubunifu wa fanani.

(g)    Kutia hofu au woga kwa hdhira kwa lengo la kuifanyahadhira hiyo iache mambo mabaya.

 

Fasihi simulizi ya zamani (ya kimapokeo) na Fasihi simulizi ya teknolojia mpya (ya kisasa) Fasihi simulizi ya zamani au ya kimapokeo ni fasihi simulizi iliyokuwepo k abla ya ugunduzi wa teiknolojia mpya ya kisasa ya kuhifadhia na kuwsilisha kazi za maisha yake ya kila siku na kuanza kuwasiliana kwa lugha.

 

 

Sifa bainifu za fasihi simulizi ya zamani au ya kiapokeo.

Fasihi simulizi ya zamani au ya kimapokeo ina sifa muhimu zifuatazo:-

(a)    Ililenga zaidi katika kurithisha utamaduni (mila na desturi) kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo.  Hii ina maana kuwa ilirithisha utamaduni wa jamii kutoka kizazi cha babu na bibi hadi kizazi cha watoto na wajukuu wao.  Urithishwaji huu ulifanywa kwa njia ya nyimbo, majigambo, ngoma, hadithi na mashiri ya zamani.

(b)    Usambazaji wake ulifanyika kupitia sauti iliyotoka mdomoni mwa msanii.  Usambazaji huu uliruhusu kazi ya kifasihi kubadilika kadri msanii alivyosimulia.

(c)    Uwasilishaji wake ulikuwa unafanyika katika wakati maalumu.  Mathalani uwasilishaji ulifanyika jioni na usiku pale nuru ya mbalamlwezi ilipojitokeza.

(d)    Uwasilishaji ulikuwa ukifanyika katika eneo maalumu, kama vile jukwaani, chini ya amti, nyumbani, n.k.

(e)    Fanani na hadhira walionana ana kwa ana wakati wa uwailishaji.  Hii ina maana kuwa anayerithisha yaani fanani (msimuliaji) na anayerithishwa yaani hadhira (msikilizaji au wasikilizaji) walikuwa pamoja eneo moja na kwa wakati mmoja.  Fanani alitumia viungo vyake vya mwili katika kukamilisha yale aliyoyasema.  Hadhira aliweza kushiriki kwa kuchezesha viungo, kupiga makofi, kupiga vigelegele, kuitikia, n.k.

(f)     Hadhira alikuwa yupo hai zaidi na fanani alikuwa yupoo huru wakati wa uwasilishaji.  Hadhira alikuwa hai zaidi kufanya lolote wakati wa uwasilishaji wa kazi ya kifasihi, vilevile, fanani alikuwa huru zaidi katika kutumia viungo vya mwili wake wakati wa uwasilishaji na aliweza kubadilisha kazi yake kadri alivyoona inafaa.

(g)    Ilikuwa ni mli ya jamii nzima.  Fasihi simulizi ya zamani au ya kimapokeo ilikuwa inamilikiwa na kila mwanajamii; hakukuwa na haki miliki ya kazi za kifasihi.

(h)    Ilikuwa inahifadhiwa kichwani mwa mwanadamu.

 

Fasihi simulizi ya teknolojia mpya au ya k isasa

Technolojia ni maarifa mapya na maendeleo ya kisayansi yaliyowekwa katika

matumizi na ugunduzi wa vitu mbalimbali kama vile zana au mitambo ya

mawasiliano

 

Fasihi simulizi ya teknolojia mpya  au ya kisasa ni fasihi simulizi inayotumia teknolojia (maarifa mapya ya kisayansi) katika kuhifadhi na kuwasilisha kazi za kifasihi.  Huhusisha matumizi ya televisheni (runinga), komopyuta (tarakilishi), kanda za video, tepurekoda (vinasa sauti), santuri (CD), satelaiti, simu za mikononi, barua pepe, n.k.

 

Sifa bainifu za fasihi simulizi ya teknolojia mpya au ya kisasa.

Fasihi simulizi ya teknolojia mpya au ya kisasa ina sif amuhimu fifuatazo:-

(a)    Huhifadhiwa kwa kutumia vyombo mbalimbali vya kisasa vya kiteknolojia kama vile kanda za video, santuri (CD), DVD, kompyuta (tarakilishi), tepurekoda (vinasa sauti), simu za mkononi, mtandaoni, n.k.

(b)    Husambazwa au huenezwa kwa kutumia vyombo vya kisasa vya kiteknolojia, kama vile satelaiti, redio,  mtandao, barua pepe, televisheni (runinga), simu za mkononi, n.k.

(c)    Huwasilishwa kwa watu wengi walio mbali kwa muda  mfupi kwa sababu ya kutumia vyombo mbalimbali vya kisasa vya vya kiteknolojia.

(d)    Mara nyingi fanai na hadhira hawaonani ana kwa ana wakati wa uwasilishaji.

(e)    Mara nyingi huburudisha jamii kupitia maigizo, nyimbo na filamu.

(f)     Msanii hana uhuru wa kutosha wa kufanya marekebisho kwani  ikisharekodiwa hubaki hivyo hivyo mpaka wakati mwingine.

(g)    Uwasilishaji na usambazaji huweza kufanyika eneo au mahali popote

(h)    Uwasilishiaji unafanyika wakati wowote.

(i)     Mara nyingi fasihi simulizi hii si mali ya jamii nzima kwa sababu huhusisha haki miliki ya kazi za kifasihi.

 

Tofauti kati kati ya utenzi,ushairi wa kimapokeo na masivina

Hoja

Utenzi

Ushairi wa Kimapokeo

Masivina

Idadi ya mishororo

Huwa na mishororo mine (4) tu kwa kila ubeti.

Huwa na mshororo mmoja, miwili, mitatu, mine, mitano, sita nau mtunzi

Hakuna idadi kamili ya mistari au mshororo kwa kila ubeti

Mizani

Mshororo au mstari mmoja huwa na mizani nane (8)

Mstari au mshororo mmoja huwa na mizani kumi na site (16)

Mizani hutofautiana toka mshororo mmoja hadi mwingine.

Vina

Huwa na kina cha mwisho tu katika kila mshororo.  Kina cha mwisho katika kituo bahari huwa ni hichohicho.

Huwa na kina cha kati na cha m wisho katika kila mshororo.

Sio lazima kutumia vina kwa kila mstari.

Dua au maombi

Mara nyingi utenzi huanza kwa dua au maombi na humaliza kwa dua au maombi

Dua au maombi sio jambo linalojitokeza sana, ingawa kuna washairi wanatumia hivi

Dua au maombi hayajitokezi kabisa.

Kujitosheleza kimaana

Ubeti mmoja haujitoshelezi kimaana, hivyo mawazo yake huendelez katika ubeti unaofuata.

Ubeti mmoja hujitosheleza kimaana. Shairi  linaweza kuundwa na ubeti mmoja tu

Mara nyingi maana inapatikana baada yak soma shairi zima

Muundo

Hutumia muundo wa tarbia tu.

Huweza kutumia muundo tamolitha, tathnia, tathlitha, tarbia, takhamisa au sabilia

Hayana muundo unaoeleweka

Urefu

Utenzi ni utungo mrefu sana.  Mara nyingi huanzia beti 100.

Shairi la kimapokeo ni utungo mfupi, huwa na beti chache, na wakati mwingine huweza kuwa na ubeti mmoja tu.

Masivina huwa na urefu wa kawaida (si marefu sana wala si mfupi sana).

 

 

 

Tofauti kati ya fasihi simulizi na Fasihi Andishi

 

FASIHI SIMULIZI

FASIHI ANDISHI

1.

Huwasilishwa kwa mdomo au maasimulizi.

Huwasilishwa kwa njia ya kuandika (maandishi).

2.

Hufanyiwa marekebisho papo hapo endapo itakosewa.

Haiwezi kufanyiwa marekebisho ya papo hapo.

3.

Hubadilika kulingana na mazingira au eneo na wakati.

Haibadiliki kulingana na mazingira na wakati

4.

Huwasilishwa pasipo na gharama yoyote.

Huwasilishwa kw akuhusisha gharama mbalimbali.  Kwa mfano kalamu, rangi, rula, uchapishaji, karatasi, n.k.

5.

Inahusisha watu wengi (wanaojua na wasiojua kusoma na kuandika).

Inahusisha wanaojua kusoma na kuandika tu.

6

Hukutanisha ana kwa ana fanani na hadhira

Haikutanishi ana kwa ana fanani  (mwandishi) na hadhira (msomaji).

7.

Haifanyiwi maandalizi au matayarisho ya kina kabla ya kuwasilishwa.

Fanani (mwandishi) hufikiri na hujiandaa kwa muda mrefu kabla ya kuwasilisha ujumbe kwa hadhira kimaandishi

8.

Inahusisha utendaji.  Vitendo vya fanani huonekana kwa macho

Haihusishi utendaji unaoonekana dhahiri.

9.

Humilikiwa na jamii nzima.

Humilikiwa na mtu binafsi (mtunzi / mwandishi)

10

Ilianza pale tu mwanadamu alipoanza kutumia lugha.

Ilianza baada ya kugunduliwa kwa maandishi

11.

Ina wahusika wengi; huhusisha watu, wanyama, ndege, miungu, wadudu, mizimu na vitu.

Ina wahusika wachache, hutumia mhusika binadamu tu.

12.

Ina tanzu nne, ambazo ni hadith, semi, ushairi na sanaa za maonesho.

Ina tanzu tatu, ambazo nihadithi tamthiliya na ushairi.

13.

Hutumia lugha ya hadhira husika yaani lugha inayoeleweka na hadhira

Hutumia zaidi lugha anayoimudu mwandishi au ile ya wasomaji waliokusudiwa.

14.

Hutumia muundo rahisi wa moja kwa  moja

Mara nyingi hutumia muundo changamano na rejea au rejeshi.

15.

Mazingira ya uwasilishaji huambatana na tukio maalumu la kijamii katika wakati maalumu.

Mazingira ya uwasilishaji hayaambatani na tukio na wakati maalumu kwani hadhira huweza kujisomea kusomewa kazi ya kifasihi wakati wowote bila tukio lolote.  Kwa mfano, tamthiliya huweza kusomwa au kuonishwa hadharani wakati wowote pasi na tukio lolote.

 

 

FASIHI YA KISWAHILI  NA  FASIHI KWA KISWAHILI

Fasihi ya Kiswahilini fasihi iliyoandikwa na mswahili kwa lugha ya Kiswahili inayohusu mila na desturi au utamaduni  wa waswahili  ( watu wa Afrika Mashariki na kati )Fasihi ya Kiswahili imetokana na kujitambulisha kuwa inashughulikia utamaduni wa waswahili ambao ndio watumiaji wakubwa wa lugha ya Kiswahili.Kuenea kw alugha ya Kiswahili sehemu mbalimbali za Afrika mashariki na kati imepelekea lugha ya Kiswahili iwe chombo cha fasihi ya waswahili.

Maendeleo ya Fasihi ya Kiswahili.

Maendeleo ya fasihi ya Kiswahili yanaweza kugawanywa katika Vipindi vine (4) vya kihistoria kama ifuatavyo:-

(a)    Fasihi ya Kiswahili kabla ya  ujio wa wageni.

Kabla ya kuingiliana na wageni (Waarabu, Wajerumani, Waingereza na wengine), fasihi ya Kiswahili ilikuwa ikisimuliwa kwa njia yam domo bila kuandikwa.  Fasihi ya Kiswahhili ilikuwa na tanzu mbalimbali, kama vile ngano, methali, vitendawili, nyimbo, mashairi, n.k.  Wahusika wa tanzu hizo walikuwa wanyama, mizimu, mashetani, n.k. lakini walipewa tabia na matendo ya kibinadamu.  Nyimbo na mashairi ya wakati huo hayakufuata arudhi, kaida au kanuni ambazo hivi leo zinachukuliwa kama mizani ya kupima ushairi wa Kiswahili.  Fasihi simulizi ya Kiswahili imeendelea kudidimia au kufifia kutokana na maendeleo na kuibuka kwa hati au maandishi.

 

(b)    Fasihi ya Kiswahili baada ya ujio wa Waarabu.

Waarabu walipowasili katika upwa au pwani ya Afrika Mashariki waliathiri fasihi simulizi ya Kiswahili kwa sababu ya kuleta hati za Kiarabu ambazo matokeo yake ni kuibuka kwa fasihi andishi.  Fasihi ya Kiswahili ambayo hapo awali ilikuwa ikisimuliwa au ikiwasilishwa kwa mdomo ikianza kuandikwa kwa hati za Kiarabu.  Fasihi iliyoandikwa kwa hati za Kiarabu ilikuwa ni hadithi na mashairi, hasa mashairi marefu (mashairi yenye beti nyingi) ambayo haikuwa rahisi kukumbukwa na watu.  Kadhalika, hadithi za Kiarabu na Kiajemi zilianza kutafisiriwa na kuingizwa katika fasihiya Kiswahili.  Miongoni mwa hadithi zilizotafisiliwa ni Masimulizi ya Alfa Lela Ulela na Hekaya za Abunuwasi. Katika pindi hiki, watunzi wa mashairi walianza kutunga mashairi yenye kuzingatia arudhi, kaida au kanuni za vina, mizani na vituo.

 (c)   Fasihi ya Kiswahili wakati wa ukoloni.

Wazungu (Wajerumani, Waingereza na wengine) walileta hati za Kilatini, hivyo uandishi wa kazi za kifasihi ulizidi kupanuka.  Fasihi mbalimbali za wazunguzilitafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.  Kwa mfano, Mashimo ya Mfalme Suleimani.  Hadithi za Esopo na Kisima Chenye Hazina. Katika kipindi hiki,waswahili na wasio waswahili walianza kuandika kazi mbalimbali zakifasihi kwa lugha ya Kiswahili.  Mfano wa kazi ya kifasihi ni Hadithi za desturi za Waswahili iliyoandikwa na W. Velten.  Licha ya hayo, wazungu waliwashawishi waafrika kupitia Halmashauri ya Kusanifisha Lugha (iliyoundwa mwaka 1930) kuanza kuandika riwaya (hadithi) zao.  Halmashauri au kamati hiyo iliandaa mashindano ya waandishi wa kiafrika kwa kutumia lugha ya Kiswahili.  Mashindano haya yaliibua waandishi mbalimbali kama vile Shabani Robert, Abdallah.  Farsy na M. S. Jemedaar.  Shabani Robert aliandika kitabu cha Adili na Nduguze, Farsy aliandika kitabu cha Kurwa na Doto na Abdallah aliandika kitabu cha Mzimu wa Watu wa Kale (1958).

 

Pamoja na riwaya, kulizuka utunzi wa tamthiliya au michezo ya kuigiza.  Watuzi wa thamthiliiyia waliojitokeza ni pamoja na Henry Kuriya, Gerishon Ngugi, HyslopGharam, Ibrahim Hussein, Mazrui, Kitsao na wengine.  Pia, baadhi ya tamthiliyaza wazungu zilitafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo ya Mabepari wa Venisi, iliyotafsiriwa na J. K. Nyerere.

 

(d)    Fasihi ya Kiswahili baada ya uhuru.

Kuanzia miaka ya 1960, fasihi simulizi ya Kiswahili ilianza kufufuliwa baada ya kuathiriwa na wakoloni na kupoteza umaana au umuhimu wakae katika jamii.  Vikundi mballimbali vya sanaa, ikiwemo muziki, vilianlzilshwa kwa lengo la kuendeleza tanzu mbalimbali za fasihi simulizi na kulinda amali za jamii.  Kwa mfano nchini Tanzania vilianzishwa vikundi vya muziki wa taarabu.

 

Maendeleo mengine ni kuzuka kwa utunzi wa kazi za ushairi.  Watunzi wa mashairi huru au ya kisasa (mashairi yasiyofuata arudhi, kaida au kanuni za vina, mizani na kituo) waliibuka katika kipindi hiki kiasi cha kuzua mgogoro wa ushairi. Kulijitokeza watu (wataalalmu) waliopinga vikali utunzi wa mashairi ya mtindo huu.  Mgogoro wa ushairi ulihusisha wataalamu wanaotetea utunzi wa mashairi bila kuzingatia vina, mizani na vituo (wanausasa, wanamamboleo au wanamapinduzi), ambao ni M. Mlokozi, E. Kezilahabi, Kahigi, Mazrui, n.k. dhidi ya wataalamu waliopinga mtindo huu wa mashairi (wanamapokeo au washairi wa jadi), ambao ni Mathias Mnyampala, Chiraghdin, Kandoro, n.k. Mgogoro huu ulidumu zaidi ya miaka kumi (10).  Wanausasa, wanamamboleo au wanamapinduzi walidharauliwa na kuitwavijana chipukizi katika tasnia ya utunzi wa jashairi.  Madai haya hayana mashiko kwani kile kiitwacho arudhi, kaida au kanuni ni athari ya wageni wa Kiarabu katika fasihi ya Kiswahili.

 

Fasihi kwa Kiswahili  ni fasihi inayotafsiriwa katika Kiswahili kutoka lugha nyingine.Mifano ya fasihi kwa Kiswahili ni Mabepari wa Venisi  kilichotafsiriwa na J.K Nyerere toka katika kitabu cha kiingereza kilichoandikwa na William Shakespeare

 

MAPUNGUFU/MATATIZO YANAYOIKABILI FASIHI YA KISWAHILI

Ø Uchache wa wataalamu wa fasihi ya Kiswahili. Katika jamii ya wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili kuna uchache wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ambapo tatizo hili linapelekea kuwa na wataalamu wachache wa fasihi ya Kiswahili.

Ø Uchache wa kazi za fasihi zinazolenga kuikomboa jamii kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni.Waandishi wengi wanaandika kazi zao kwa lengo la kuburudisha wasomaji badala ya kuyamulika kwa kina matatizo ya jamii ya waswahili.

Ø Mwamko mdogo  wa wanajamii  wa kusoma kazi za fasihi ya Kiswahili.Jamii  ya waswahili hawana tabia ya kusoma vitabu na maandiko mbalimbali ya Kiswahili.Wanafunzi pekee wakiwa shuleni husoma fasihi ya Kiswahili kama vile riwaya na Tamthiliya.

Ø Uchache wa kazi za fasihi ya Kiswahili zilizosambazwa. Kazi nyingi za fasihi ya Kiswahili hazijasambazwa vyakutosha maeneo yote ya mjini na kijijini.Kazi nyingi za kifasihi zinasambazwa maeneo ya mjini japokuwa sio katika miji yote lakini watu wengi wa kijijini wanakosa kusoma kazi hizo kwasababu hazijawafikia.

Ø Kuongezeka kwa kasi  kwa  riwaya pendwa.Waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili wamejikita zaidi katika kujipatia  fedha za haraka kwa kuandika fasihi pendwa ilikupata pesa za haraka sokoni.Mfano Wowowo la kajala  na Shemeji Pita kwa Huku viliandikwa na Irene Ndauka na  Raisi anampenda mke wangu na Kifo ni haki yangu  viliandikwa na Erick Shigongo

Ø Wasanii kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu utamaduni wa mswahili.Waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili hawana uelewa wa kutosha juu ya utamaduni wa mswahili  hali inayopelekea wao kushindwa kuandika fasihi ya Kiswahili.

 

TOFAUTI  KATI  YA FASIHI YA KISWAHILI NA FASIHI KWA KISWAHILI

Fasihi ya Kiswahili na fasihi kwa Kiswahili hutofautiana  katika mambo yafuatayo;

Ø Asili ya mtunzi,Fasihi ya Kiswahili  hutungwa na mswahili aliyezaliwa uswahilini na ambaye anafahamu kwa undani maisha yaliyomlea na kumkuza msanii lakini mtunzi  wa fasihi kwa Kiswahili  huandikwa na mtu yeyote asiyemswahili

Ø Utamaduni unaoshughulikiwa,Fasihi ya Kiswahili hushughulikia au husawiri utamaduni wa waswahili yaani watu  wa Afrika Mashariki na kati lakini fasihi kwa Kiswahili haishughuliki na utamaduni wa waswahili pamoja na utamaduni wa kigeni

Ø Majina ya wahusika,Katika fasihi ya Kiswahili majina ya wahusika huwa ni yale yanayopatika katika mazingira halisi ya mswahili mfano Mwajuma,Abdalla n. lakini katika Fasihi kwa Kiswahili majina ya wahusika sio yale yanayopatikana katika mazingira  halisi ya mswahili.

Ø Mandhari,Fasihi ya Kiswahili husawiri mandhari halisi ya mswahili au mahali ambapo waswahili wanaishi lakini fasihi kwa Kiswahili haiandikiwi mandhari ya mswahili.

Ø Mavazi ya wahusika (maleba), Fasihi ya Kiswahili huhusisha mavazi ya wahusika yanayovaliwa katika mazingira halisi ya mswahili mfano,kanzu,balaghashia,baibui,Dera,n.k  lakini fasihi kwa Kiswahili mavazi ya wahusika si yale yanayopatikana katika mazingira ya mswahili.

Ø Lugha,Fasihi ya Kiswahili hubuniwa na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili kuanzia  mwanzo bila kutafsiriwa kutoka kwenye lugha nyingine Lakini fasihi kwa Kiswahili hubuniwa na kuandikwa kwa lugha nyingine kasha kutafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

Ø Umri,Fasihi ya Kiswahili ilianza mapema katika pwani ya Afrika Mashariki kabla ya kuwasili kwa wageni.Fasihi ya Kiswahili kabla ya ujio wa wageni ilikuwa haijaandikwa; ilikuwa kama fasihi simulizi ya Kiswahili kama vile nyimbo,mashairi,ngano,methali,nahau,vitendawili,n.k Lakini fasihi kwa Kiswahili ililetwa na wageni,hivyo ilitumiwa baada ya fasihi ya Kiswahili.Waarabu walipowasili pwani ya Afrika mashariki walikuta waswahili wanatumia fasihi simulizi ya Kiswahili,ndipo walipoanzisha fasihi kwa Kiswahili yaani walianza kutafsiri hadithi za kiarabu na kiajemi katika lugha ya Kiswahili.

 

 

MCHANGO WA FASIHI SIMULIZI KATIKA FASIHI ANDISHI

Fasihi simulizi ina mchango mkubwa sana katika fasihi Andishi kifani n kimaudhui

A.Kimaudhui,Dhamira nyingi ambazo ndicho kiini cha maandishi mengi katika  Fasihi Andishi zilikwishajadiliwa  katika fasihi simulizi.Dhamira hizo ni kama vile Mapenzi,Siasa,Matabaka,Uhuru,Ukombozi,Usawa,Unyonge wa mwanamke,Uchawi na Ushirikina n.k Fasihi simulizi haijavumbua dhamira mpya kabisa bali maudhui/dhamira zote za kale.

B. Kifani,Vipengele mbalimbali vya fani ya fasihi simulizi katika kufikisha ujumbe kwa jamii zao.Vipengele hivyo ni;

1.    Muundo,Fasihi simulizi muundo wake ni wa moja kwa moja pia kuna baadhi ya waandishi wa Fasihi Andishi ambao wametumia muundo wa moja kwa moja.Mfano Riwaya ya Kuli (1979) ya Shafi A. ShafiAmetumia muundo wa moja kwa moja.

2. Mtindo,Fasihi simulizi hutumia mtindo wa masimulizi pia kuna baadhi ya waandishi wa Fasihi Andishi hutumia mtindo wa masimulizi.Mfano Riwaya ya Shida (1975)ya Balisdya

3. Wahusika,Waandishi wa Fasihi andishi hutumia wahusika wasio binadamu katika kazi zao ambao kwa kawaida hupatikana katika fasihi simulizi tu.Mfano Mashetani (1971),Pambo (1975),Adili na Nduguze (1952) Kusadikika (1951) na Kufikirika (1967)  wametumia wahusika mashetaniambao hupatikana katika fasihi simulizi tu. Wahusika kama wanyama,majini,mazimwi hupatikana katika fasihi simulizi tu.

 4. Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi,hapa wahusika husimulia hadithi mbali mbali katika fasihi andishi .Hawa husimuliana hadithi za kimapokeo ambapo hadithi ni kipera cha fasihi simulizi.Mfano Njozi iliyopotea (1980),Lina Ubani (1984), Mashetani (1971)

5 .Matumizi ya mtambaji hasa katika tamthiliya,Waandishi wengi wa tamthiliya wametumia mbinu ya utambaji ambapo wanakuwa na mtambaji anayetamba hadithi fulani.Mfano,  Lina Ubani (1984),Nguzo mama (1980),Pambo (1975)

6.Matumizi ya mianzo ya hadithi za Fasihi simulizi,Mfano tamthiliya ya Jogoo kijijini na ngao ya jadi(1970) Kilio Chetu (1995) ,Kivuli kinaishi (1990),Riwaya hizi zimetumia mianzo maalum ya fasihi simulizi mfano paukwa……,pakawa.

7. Matumizi ya Semi mbali mbali,Fasihi  andishi hutumia semi mbalimbali ambazo ni ni tanzu za fasihi simulizi.Semi ambazo hutumiwa sana ni misemo,nahau,methali,tamathali ,vitendawili na tanzu nyingine

8. Matumizi ya Ushairi na nyimbo,Waandishi wengi hutumia sana nyimbo katika kazi zao ili kuzipa mvuto,mfano Riwaya ya Njozi iliyopotea (1980),tamthiliya ya Kilio chetu wametumia sana nyimbo katika kufikisha ujumbe kwa jamii husika.

 

MADA NDOGO-1;  UWASILISHAJI NA UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

(a) UWASILISHAJI WA FASIHI SIMULIZI

Uwasilishaji hutumiwa kuelezea njia au mtindo unaotumiwa kufanya kazi ya kifasihi iwafikie walengwa .Mfano uwasilishaji wa maigizo ni kutendwa kwake jukwaani mbali ya hadhira ya watazamaji.Tangu zamani, uzalishaji wa tanzu za mbalimbali za fasihi simulizi huwasilishwa kwa masimulizi ya mdomo na matendo.

Fasihi simulizi hubuni hadithi, nyimbo, methali n.k. zinazobaini hisia zao mbalimbali kuhusu maisha na mazingira yao.Fasihi simulizi pia inaweza kuzungumzia historia ya watu wa jumuiya Fulani itikadi zao na mambo mengine mengi wanayoyathamini katika kuishi kwa pamoja.

Kwa kuwa fasihi simulizi haiandikwi kuhifadhiwa kwake kunategemea kurithishana kwa mdomo kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia hii kizazi kimoja kinaweza kurithisha kizazi kingine yale mambo muhimu ambayo kinataka yaendelee katika jamii hiyo mambo ambayo yamefungamana na mazingira yao maisha yao utamaduni wao na itikadi zao.

 

(b)UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

UENEZAJI:

 Hutumiwa kueleza uhusianokati ya hadithi na jamii mbali mbali.Nadharia hii  huonyesha kuwa inawezekana kuwa jamii zinazohusika ziliingiliana kihistoria au kutokana na ukaribu wao wa kijiografia n zilihusiana kihistoria. kuingiliana huku kunaweza kuwa msingi wa kuwako kwa hadithi zinazosimuliwa ambazo zinafanana katika jamii mbalimbali.

Mfano;utenzi wa Fumo Liyongo unapatikana katika jamii kadhaa za pwani ya Kenya kama waswahili, wapokomo, wabajuni n.k. Inawezekana kuwa kupatikana huku ni tokeo la ueneaji hasa kwa kuwa hizi ni jamii zinazokaribiana kijiografia za zilizohusiana kihistoria.

 

SABABU ZA KUENEA KWA FASIHI SIMULIZI.

a)     Kuanzishwa kwa vikundi vya Sanaa na muziki,Vikundi mbalimbali vya Sanaa na muziki vilianzishwa ambavyo kazi yake ni kuendeleza tanzu mbalimbali za fasihi simulizi hapa nchini.Vikundi vya Sanaa za maonyesho, Vikundi vya taarabu na muziki mfano, Ottu Jazz Band,Kilimanjro orchestra,Kilwa Band n.k vinafanya kazi kubwa ya kueneza na kuendeleza fasihi simulizi hapa nchini.

b)    Muingiliano na fasihi andishi,Kuenea kwa kazi ya fasihi simulizi kwa asili ni kwa mdomo na masikio yaani usimulizi, hata hivyo maendeleo ya watu yamefanya baadhi ya kazi za fasihi simulizi zienee kwa maandishi.Maandishi ni jitihada za kuhifadhi kazi ya fasihi simulizi na kuifikisha mahali ili ikatambuliwe au isimuliwe.Hadithi mbalimbali kama vile Hekaya za Abunuasi (1915),Hadithi za Esopo (1890),Fasihi simulizi ya mtanzania.Hadithi (1977) .Hizi zote zimehifadhiwa na kuenezwa kwa maandishi.

Fasihi andishi inatumia vipengele mbalimbali vya fasihi simulizi katika uandishi wake na hivyo kuviendeleza. vipengele hivyo kama vile ,Matumizi ya semi mbalimbali,Matumizi ya nyimbo,Matumizi ya hadithi ndani ya hadithi,Matumizi ya mianzo na mishilizo ya hadithi za fasihi simulizi,Matumizi ya majigambo, utani n.k.

Kwa sasa methali, vitendawili, nahau, vimewekwa katika maandishi kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye na hivyo vinaenezwa kwa njia ya maandishi.

c)     Ufundishaji shuleni na vyuoni,mfumo wa Elimu nchini nao umesaidia kueneza fasihi simulizi kwa kiasi kikubwa hapa nchini kwa sasa fasihi simulizi ni somo linalofundishwa toka darasa la kwanza hadi ngazi za juu (chuo kikuu)

Vile vile kuna vyuo hapa nchini vinavyofundisha baadhi ya tanzu mbalimbali za fasihi simulizi kama vile Sanaa za maonyesho na muziki. Mfano chuo cha Bagamoyo, Butimba, Nyegezi na chuo kikuu cha Dar-es-salaam.

d)    Mabadiliko ya kiteknolojia.

Kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa sasa fasihi simulizi inaenezwa kwa vyombo vya habari kama vile kaseti, redio, video, luninga, mitandao ya kijamii n.k.Mfano Redio Tanzania (TBC) kupitia kipindi chake cha “Mama na Mwana” “Watoto Wetu” vimesaidia sana kueneza fasihi simulizi hapa nchini Tanzania. Luninga nazo zimesaidia sana kueneza fasihi simulizi nchini kupitia vipindi mbalimbali vya michezo ya kuigiza.Hivyo mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia hayawezi kuwa fasihi simulizi

E)Mwingiliano wa mataifa mengine.Katika mwingiliano muziki umesaidia sana kukuza fasihi simulizi.Hali hii imesaidia kuleta muziki wa kizazi kipya (muziki wa kufoka foka) pamoja na Rege  vijana wa kizazi kipya wamechota miundo na mitindo ya muziki kutoka nje na kuendeleza muziki wao ingawa madhui bado wanajadili yale yale yaliyojadiliwa na wanamuziki wa zamani.Matumizi ya fasihi simulizi katika Sayansi na Teknolojia yamesaidia sana kuenea kwa fasihi simulizi kwani fasihi simulizi inapata hadhira kubwa kwa wakati mmoja lakini hadhira hiyo haionani ana kwa ana na fanani wao kwa kutumia vyombo hivyo vya Sayansi na Teknolojia.

 

ATHARI ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA KATIKA UWASILISHAJI NA UENEZAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

Mwanzo fasihi simulizi iliwasilishwa na kuenezwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo hivyo fanani na hadhira walionana ana kwa ana wakati wa uwasilishaji lakini zama hizi za Sayansi na Teknolojia, uwasilishaji na uenezaji unatumia vyombo vya habari kama vile redio, video, televisheni, kanda kunasia sauti, mtandao na hata kompyuta, mara nyingi hasa hadhira haiwi ana kwa ana na fanani hutokea hadhira ikawa inaangalia luninga au sinema au tamthiliya jukwaani kwenye mazingira kama hayo si rahisi hadhira kushiriki kikamilifu katika utendaji.Kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia fasihi inaathiriwa katika vipengele vifuatavyo:-

1.     Uwasilishaji. Mwanzoni fasihi simulizi iliwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo hivyo fanani na hadhira walikuwa wanaonana ana kwa ana wakati wa uwasilishaji lakini katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia, uwasilishaji wa fasihi  simulizi unatumia vyombo kama, vile redio, luninga, video, kanda, mtandao na hata kompyuta na sio lazima msanii awepo.

2.     Uhifadhi, kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia sasa fasihi simulizi inaweza kuhifadhiwa vizuri Zaidi kuliko inavyofikiriwa na wanamapokeo  kwani leo hii fasihi simulizi inaweza kuwekwa katika mkanda wa kompyuta (flash disc) CD, DVD, Maandishi n.k na ikaendelea kuwepo kwa miaka mingi sawa sawa na fasihi andishi hata zaidi.Kwa upande wa video na DVD, uhifadhi wake huendelea kuonyesha vitendo na sauti huweza kudumu hata zaidi ya maandishi.

3.     Wakati na mahali, zamani fasihi simulizi ilifanyika sana saa za jioni, kando ya moto au barazani. Aidha kwa vile fasihi simulizi hutolewa redioni inaweza kusimuliwa wakati wowote na mahali popote ambapo kipindi kinasikika na kwa saa na wakati huo. Majumbani, mijini watoto hawazunguki moto tena, bali husubiri wakati kipindi kinaporushwa kwa siku maalumu na wanaizunguka luninga au redio.

4.     Hadhira au ushirikishwaji wa hadhira, zamani hadhira ya fasihi simulizi ilikuwa inaonana ana kwa ana na fanani wake wakati wa uwasilishaji wake. Hadhira iliweza kuchangia kazi ya fasihi hiyo na hata kuathiri uumbwaji wake, ikaitwa hadhira tende. Lakini katika muktadha wa maendeleo ya  sayansi si lazima fanani na hadhira waonane ana kwa ana .

MADA NDOGO-2 ;UHIFADHI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

Kwa sasa fasihi simulizi inaweza kukusanywa na kuhifadhiwa kwa njia zifuatazo:-

a)     Kichwa,uhifadhi wa fasihi simulizi ni katika vichwa vya watu kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Jambo hili limekuwa likifanyika kwa muda mrefu sana.Hivyo kutokana na kuhifadhiwa katika vichwa ndio maana fasihi simulizi imekuwa ikirithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

b)    Maandishi, Tangu maandishi yagunduliwe baadhi ya kazi za fasihi simulizi zimekuwa zikihifadhiwa kwenye maandishi kwa ajili ya kumbukumbu ya baadaye. Kazi za fasihi simulizi zikihifadhiwa katika maandishi inaweza kufanya watu wasijue ni simulizi au andishi. Hata hivyo vidokezo kadhaa husaidiakujua  kazi za fasihi simulizi kama vile kuwana mianzo maalum,mfano  “Paukwaa!  Pakawa! Au hadithi…….hadithi njoo” n.k. Aghalabu fasihi simulizi huwa na mtiririko(muundo) wa moja kwa moja usio na urejeshi.

c)     Kanda za kunasia sauti (tepu rekoda),Hii ni njia moja wapo inayotumika kuhifadhi tanzu mbali mbali za fasihi simulizi. Kanda hizo hushika sauti pamoja na vidokezo vyake, kwa hiyo wasikilizaji ili wapate wanachokitaka lazima wanunue kanda hizo.

d)    Kanda za video, luninga na filamu z sinema CD, DVD na Kompyuta/Tanakilishi.Mtandao, pichaza video hurekodi sura na sauti,Picha hizo hutembeana kuonyeshwa kwenye skirini ya video na lunnga. Picha za sinema hupigwa kwa aina maalumu za kamera ambazo hupiga picha za mfululizo katika utepe maalumu. Picha hizo huonyeshwa kwa mashine na huonekana  zinatembea, kamera nyingi za sinema za siku hizi zina mitambo ya kurekodi sauti pia. Hivyo kwa kutumia filamu za sinema na video tunaweza kuhifadhi na kuonyesha kazi za fasihi simulizi.

 

 

 

ATHARI ZA MBINU MBALI MBALI ZA UHIFADHI WA FASIHI SIMULIZI

Ø KICHWANI

Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi kichwani una matatizo yafuatayo:-

·        Kumbukumbu za akili zinaweza kupungua au kufifia au fanani kufa kabisa. Hali hii ikitokea fasihi simulizi hupotea.

·        Mtu anayehifadhi kichwani anaweza kubadilisha mambo muhimu katika simulizi na hivyo kugeuza kiini cha masimulizi hayo.

·        Kutokana na mazingira pamoja na mabadiliko kuna tatizo la kupata watu wanaoweza kuhifadhi kazi hiyo.

 

Ø MAANDISHI

              Uhifadhi kwa kutumia maandishi una matatizo yafuatayo:-

·        Baadhi ya  mambo  hayawezi kuhifadhiwa katika maandishi. Mambo hayo ni yale yanayohusiana na utendaji, sauti, vitendo, toni, kuimba, muziki n.k. Matokeo ya kukosekana kwa vitu hivi ni kwamba ladha au athari ya kazi inayowasilishwa hupungua.

·        Kukosa  sauti kwa hiyo msomaji anapaswa atie sauti na mahadhi yake mwenyewe.Shughuli hii inaweza kuharibu au kufanya kazi ya fasihi ipungue ubora wake.

·        Hakuna ushirikishwaji kati ya fanani na hadhira, kwa hiyo hadhira inashiriki kwa kuona maandishi.

·        Haibadiliki kulingana na wakati na mazingira. Hivyo huweza kudumu katika hali ile ile kwa muda mrefu kama ilivyo fasihi andishi.

·        Inakuwa ya ubaguzi au watu wachache yaani wale wanaojua kusoma na kuandika. Wale wasiojua kusoma na kuandika itawawia vigumu kuelewa fasihi hiyo iliyoko katika maandishi.

·        Ni gharama kubwa,kuhifadhi masimulizi katika maandishi, hii ni kwasababu uandishi hutumia kalamu na karatasi. Hivyo hapa zinahitajika pesa za kununulia kalamu na karatasi na gharama za uchapaji.

 

Ø KANDA ZA KUNASIA SAUTI

 Uhifadhi kwa kutumia maandishi una matatizo yafuatayo:-

·        Kanda za kunasia sauti husikika sauti tu,Matendo hayawezi kushikwa na hii kuathiri tena uhifadhi na utoaji wa kazi za fasihi simulizi.

·        Hakuna ushirikishwaji wa hadhira kwani fanani na hadhira hawaonani ana kwa ana kwa hiyo hadhira inashiriki kwa kusikiliza kanda tu, sikio huathirika lakini jicho halioni.

·        Ni gharama, kuhifadhi fasihi simulizi kwa njia hii kwani kununua tepurekoda pamoja na kanda zenyewe, betri, spea hupatikana kwa shida na kwa bei ghali licha ya hiyo si wote wenye uwezo wa kununua tepurekoda hivyo ni watu wachache sana wenye uwezo wa kuhifadhi fasih simulizi kwa kutumia chombo hiki.

·        Haitabadilika kulingana na wakati au mahitaji ya hadhira, Huweza kudumu katika hali ile ile kwa muda mrefu kama ilivyo fasihi andishi.

 

Ø KANDA ZA VIDEO, LUNINGA, FILAMU ZA SINEMA, CD, DVD, VCD NA KOMPYUTA

Njia hii ina matatizo yafuatayo:-

v Upungufu wa ushirikishwaji wa hadhira,Hadhira haiwezi kushiriki ila inasaidia kufanya fasihi simulizi kupata hadhira kubwa ingawa hadhira hiyo haionani ana kwa ana na fanani wao.Kanda hizo huwa zinatazamwa nawatu wengi hivyo kupata hadhira wengi kwa wakati mmoja ambao hawawasiliani na fanani wao.

v Ni gharama,kwani vitu hivyo vinahitaji pesa nyingi za kununulia vifaa hivyo ambapo ni  watu wachache wenye uwezo wa kununua vifaa hivyo.

v Haibadiliki kulingana na mahitaji ya jamii au hadhira au wakati,Huweza kudumu katika hali ile ile kwa muda mrefu kama ilivyo fasihi andishi

v Vifaa hivyo vinahitaji mahali pazuri ambapo panaweza kutunza vyombo hivyo kwa muda mrefu, endapo havitahifadhiwa  hivyo kuna hatari ya kupoteza kilichohifadhiwa katika vyombo hivi.

 

MADA NDOGO-3; KUHAKIKI KAZI ZA FASIHI SIMULIZI.

Kazi za fasihi simulizi zinaweza kupimwa na kuonekana kama zinafaa au hazifai. Kazi hizi hupimwa kwa kuzingatia uhusiano wake na hali halisi ya jamii.Katika upimaji  vipengele vya fasihi simulizi huangaliwa  jinsi vilivyotumika.Upimaji wa ubora wa kazi ya fasihi simulizi hujumuisha umuhimu wa mambo yaliyosemwa katika jamii inayohusika au namna mambo hayo yanayosemwa Hivyo mhakiki atajiuliza maswali kama:-

Ø Ujumbe utolewao hapa ni wa kweli na una manufaa au la!

Ø Je maadili yatolewayo hapa yanalingana na wakati tulionao?

Ø Je nahau, misemo, methali na tamathali za semi zinalingana na jambo linalosemwa au la!

Ø Je mtiririko wa matukio unasaidia msikilizaji kuelewa kisa au unamchanganya?

Maswali ya namna hiyo yanamsaidia mhakiki kuelewa ubora wa kazi ya fasihi simulizi.Pia yaweza kutumiwa na mtunzi wa kazi ya fasihi simulizi ili kurekebisha kazi yake na kuifanya iwe bora Zaidi.

 

FANI KATIKA FASIHI SIMULIZI

FANI

Ni  ule ufundi wa kisanaa anaotumia msanii katika kazi yake

AU Fani ni ustadi au ubingwa au mbinu ambazo msanii wa kazi ya fasihi hutumia katika kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira yake. 

AU Fani ni Sanaa na jumla ya vipengele vya lugha vilivyowekwa katika mpangilio mahususi ili kutoa  maana fulani kwa hadhira.

AU Fani ni umbo lililosanifiwa ili kueleza hisia za fanani.

 

VIPENGELE VYA FANI

1.Tukio,Katika tanzu za fasihi simulizi mara nyingi ni lazima pawe na jambo au tukio ambalo huchukuliwa kama kiini au chanzo cha utanzu utakaohusishwa fani au utanzu unaotumiwa na msanii hauibuki tu hivi hivi.Tukio huwa ndio kishawishi cha fanani wa fasihi simulizi .Mfano: Nyimbo za unyago huibuka katika mazingira yake, methali za kutuliza zaweza kutumiwa pale ambapo pana majonzi ya aina fulani, kwa hiyo ni lazima pawe na tukio ambalo litachukua chemichemi ya utanzu utakaotumiwa na fanani kuwasilisha ujumbe wake kwa hadhira.

2.Mazingira/mandhari, Mazingira ni pale ambapo matukio ya fasihi simulizi yaliibuka ama yalitokea.Ufundi wa kuchora mazingira unatoa picha halisi, picha inayoonekana waziwazi juu ya mazingira yaliyohusika.Fasihi simulizi hutegemea sana muktadha au mazingira maalumu hivyo tungo za fasihi simulizi huwa zimejikita katika utamaduni wa jamii zinamoibukia vifaa ambavyo vinatumika katika fasihi simulizi vinategemea mazingira yanayohusika, mfano msanii anapodhaminia kutoa picha ya kuogofya anatumia mazingira ambayo yanaogofya kama vile mazingira ya misituni na wahusika kama majitu ili kuleta dhana ya hofu katika mazingira yake.

3.Muundo,Katika fasihi simulizi muundo ni mpangilio na mtiririko wa kazi ya fasihi simulizi kwa upande wa visa na matukio.Katika muundo kinachozingatiwa ni  jinsi fanani alivyofuma na kuunda hata alivyounganisha tukio moja na lingine kimoja na kingine, wazo na wazo, ubeti na ubeti na mstari wa beti na mwingine.Kuna miundo mbalimali katika tanzu mbalimbali za fasihi simulizi, kama vile muundo wa moja kwa moja na kuna muundo changamano.

Katika mashairi kuna miundo mbalimbali ambayo hutumiwa kuainisha mashairi kwa kufuata idadi ya mistari katika kila ubeti, miundo hii ndiyo hutupa mashairi ya tarbia, tathilitha, takhmisa na n.k.Katika hadithi na hata katika tamthiliya waweza kuwa na muundo ambao fanani ameanza kutokamwanzo akaenda katikati na baadae kumalizia kisa chake aina hii ya muundo unaitwa mtiririkoshanga.Mtirirko wa namna hii hujengwa kwa kutumia visa au vitukio mbalimbali na vinaweza kuongezwa na kupunguzwa bila kupoteza maana ya hadithi au tamthiliya.

4.     Mtindo,Katika kazi ya fasihi mtindo ni ile namna ambayo msanii hutunga kazi yake na kuipa sura ambayo kifani na kimaudhui huainisha kanuni au kaida zilizofuatwa kama zilizopo  ni za kipekee. Mtindo ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi kwa njia ambayo hatimaye huonyesha nafsi na labda upekee wa mtunzi wa kazi hiyo.

Katika  tamthiliya na riwaya  katika mtindo kinachotazamwa ni matumizi ya nafsi,matumizi ya monolojia,masimulizi na dayalojia,matumizi ya hadithi ndani ya hadithi,matumizi ya barua n.k

 Upande wa mashairi kuna mitindo mbalimbali kama vile Mtindo wa Pindu,mtindo wa kuhoji,mtindo wa beti kubadilishana vina,mtindo wa kidato n.k na shairi linaweza kuwa la vina na mizani au la kisasa ambalo halifuati kanuni za urari wa vina na mizani.

5.     Matumizi ya lugha.

Ni kipengele muhimu cha fani ya fasihi, lugha ndiyo malighafi ya fasihi.Lugha inayotumika katika kazi ya fasihi ni lugha ya kisanaa inayopambwa na inayokusudiwa kuibua hisia fulani kwa hadhira yake.Inaweza kuathiri moyo ya hadhira na kulingana na jinsi inavyotumiwa kwa lengo la kuchekesha, kukejeli, kubeza, kuchokoza, kutia hamasa au kushawishi

     ’ Fani lazima iwe na utanashati na ulimbwende wa kipekee wenye mvuto na mnato wa kuteka na kusisimua hisi za wasikilizaji wasomaji au watazamaji’’(khatibu 1981:16)

Matumizi ya lugha fasaha, uteuzi wa misamiati na matumizi ya misemo na methali zinazosadifu mazingira ya jaini inayohusika kufanya kazi hiyo ya fasihi simulizi kuwa sumaku ya kuvutia msomaji, msikilizaji au mtazamaji.Tamathali za semi za aina mbalimbali hutumika kujenga picha mfano ya tamathali za semi ni kama vile sitiari, tashihisi, kejeli, kijembe, tabaini, tuniaba, tashibihan.k.Taswira ni lugha ambayo huchora pichaza watu, vitu au mahali kwa kutumia ishara katika taswira unaweza kubainisha maelezo ambayo jinsi yanavypangwa na msanii huweza kufanya hadhira zipate aina mbalimbali za hisi za kunusa, kusikia, kuona na kugusa.Mara nyingi hutumiwa na wasanii ili kunasa hisia zao kwa hadhira.

Hivyo wasanii hutumia maneno ambayo huumba picha kamili ya kitu, hali, wazo, dhana au uzoefu fulani wa jamii inayohusika.Mara nyingi matumizi ya picha huenda sambamba na ishara mbalimbali ili kuwakilisha vitu, dhana au mawazo mengine.

6.     Upeo

Katika fasihi simulizi upeo ni kama kilele cha kazi yenyewe, kuna upeo wa aina mbili;

Upeo wa juu ,ni zile sehemu za kazi hiyo ambazo hutosheleza haja za wasikilizaji au watazamaji. Katika sehemu hii hadhira hupata majibu muhimu ambayo kazi hiyo imechelewesha kwa kutumia taharuki mbinu rejeshi, mtindo wa kiutelezi n.k.Mara nyingi watunzi wa kazi za fasihi huweka kipeo cha juu mwishoni mwa kazi zao  ingawa si lazima kuwa na kipeo kimoja tu wakati mwingine waweza kupata kazi ya fasihi simulizi ambayo haina kipeo kabisa

Katika kazi mbalimbali za fasihi wasanii hujenga mgogoro ambao hujtokeza na kukua, jinsi kazi hizo zinavyokua, kipeo cha juu hutokea pale ambapo msanii hujaribu kutoa suluhisho kwa mgogoro uliojengwa katika kazi yake.

Upeo wa chini ,ni sehemu ambayo matatizo yaliyounda kazi ya fasihi yanatatuliwa.Upeo wa chini ni pale ambapo haja na mataajio ya hadhira hayakukidhiwa, katika baadhi ya kazi za fasihi vipeo vya chini hudhihirisha udhaifu wa kazi hiyo lakini katika kazi nyingine upeo wa chini huwa umekusudiwa hivyo na mtunzi.Hali hii ya pili hujitokeza hasa katika kazi ya fasihi ambayo upeo wa chini hutumiwa kwa lengo la kushangaza hadhira.

7.     UCHESHI KATIKA KAZI ZA FASIHI

Ucheshi ni kipengele muhimu cha kifani katika kazi ya fasihi hasa fasihi simulizi.Ucheshi ni mbinu ya kifani ambayo watunzi hutumia katika kazi zao za fasihi kwa lengo la kuchekesha na kuburudisha hadhira na kuondolea uchovu.

Wasanii mbalimbali hutumia mbinu tofautitofauti kuleta vichekesho katika kazi zao.Baadhi yao hutumia vitendawili ili kujenga, kejeli, dhihaka, n.k. vichekesho pia huweza kutumiwa ili kujenga maudhui.

8.     WAHUSIKA.

Ni viumbe ambavyo hutumiwa na wasanii katika mtiririko wa matukio kuelezea visa vyake.Wahusika wanaweza kuwa watu, miti, wadudu, mizimu, misitu na wanyama.Wahusika huwa ni viumbe ambavyo vinatenda na kutendewa wanatumwa na msanii kusimamia hali mbalimbali za binadamu katika jamii wanamoishi.

Hawa ndio uti wa mgongo wa fani ya fasihi simulizi, Bilawahusika mtiririko wa matukio au visa hukosa pahali pa kujishikiilia.Wahusika si viumbe maalumu wa mtunzi kwa vile ndiyo wanaotumia kutoa picha au kuwasilisha mawazo na fikra zake kwa jamii inayowakilishwa na wahusika hao.Katika Fasihi simulizi  wahusika wanaweza kuwa binadamu ,wanyama,au vitu fulani vilivyopewa fursa ya mandhari na kauli kama binadamu.

 

VIPENGELE VYA MAUDHUI KATIKA FASIHI SIMULIZI

Ø MAUDHUI

Ni jumla ya mambo yote yanayosemwa na msimuliaji au mwandishi katika kazi yake.Vipengele vya maudhui au umbo la ndani la kazi ya fasihi ni kama vile

Ø Dhamira, Ni kusudio la mtunzi wa kazi ya fasihi.Kazi ya fasihi inaweza kuwa na dhamira kuu pamoja na dhamira ndogondogo.Ubainishaji wa dhamira hufanywa na hadhira,hivyo dhamira hufahamika kutokana na fasili za wasikilizaji au wsomi wa kazi ya fasihi.

Ø Ujumbe: Ili dhamira ya mtunzi itimie, msanii hutoa taarifa fulani fulani kwa hadhira yake.Taarifa hizo huitwa ujumbe. Ujumbe unaweza kutamkwa wazi au kwa uficho. Kwa mfano methali ya “Asiyesikia la mkuu huvunjika guu”ina ujumbe huu ukidharau maonyo ya wakubwa utapatamatatizo,Siku za mwizi ni arobaini ujumbe wa methali hii chenye mwanzo kina mwisho kwa kawaida kazi moja ya fasihi inaweza kuwa na  taarifa Zaidi ya moja.

Ø Mafunzo: Ni mafundisho au nasaha za mtunzi katika kazi ya fasihi.Mafunzo pia huwa na maana kulingana na fasiliya hadhira.Mafunzo humfikirisha msikilizaji au msomaji kwa njia ya ujumbe.Mfano katika ujumbe huu  akaibaakafungwa hapa funzo ni tusiibe wakati mwingine kazi za fasihi inaweza kutoa mafunzo mabaya (maadili) mtunzi anaweza kukusudia hivyo au kutokusudia hivyo.

Ø Migogoro: Hii huelekeza kisa lakini hujizatiti juu ya migogoro ya maisha anayosimulia fanani.Baadhi ya kazi za fasihi huonyesha ukinzano uliopo baina ya makundi ya watu au hali ya aina moja dhidi ya hali nyingine kuna aina nyingi za migogoro lakini Zaidi ni ile ya kisiasa, kiuchumi na kitamaduni au ile ya kibinafsi mfano: matatizo yanayosababishwa na uzembe dhidi ya watetezi wa kazi (viongozi) dhidi ya usasa katika mila na desturi husababisha mgongano wa kiutamaduni.

Ø Falsafa: Ni mafunzo makuu ya msanii (mtunzi) kuhusu maisha. Mawazo haya hutokana na uchanganuzi wa kimantiki na huwa ndio hekima na busara za msanii (mtunzi) huyo.Ni Imani ya mwandishi au fanani katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo katika jamii.

 

 

UMUHIMU NA UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI SIMULIZI.

Fani ni jumla ya mambo mengi yanayoijenga kazi ya fasihi.Mambo haya ni kama vile muundo, mtindo, mandhari,wahusika na matumizi ya lugha na maudhui ni jumla ya mawazo au dhamira, msimamo, mtazamo, falsafa na ujumbe katika  kazi ya fasihi.

Kwa ujumla fani na maudhui ni vitu vya muhimu sana katika fasihi simulizi kwa sababu mtunzi hutumia vipengele hivi katika kujenga kazi yake anayotaka kuwasilisha kwa jamii husika.Maudhui ni kila kina kinachosemwa na fani ni namna kinavyosemwa.

Fani na maudhui ni vitu  vinavyohusiana, vinaathiriana,vinategemeana na kukamilishana katika kujenga kazi ya fasihi simulizi na kila kipengele kimo ndani ya kingine

Mudhui hujumuisha viungo mbalimbali vya kazi ya fasihi simulizi na fani ni mbinu za kisanaa zinazotumiwa na msanii ili kuvifanya viungo hivyo viyasawili maisha kwa njia ivutiayo hadhira.kila kigezo (fani na maudhui) kimo ndani ya kingine huku vikishirikiana na kuathiriana katika kujenga au kubomoa kazi ya fasihi simulizi.

 

 

MADA NDOGO-4 ; KUTUNGA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI

Utungaji ni uundaji wa mawazo na kuyapanga maneno yakuwasilisha ama kwa njia ya mdomo au kwa njia ya maandishi.Utungaji unweza kutolewa kawa njia mdomo aqu kwa njia ya maandishi.

Mambo ya kuzingatia katika kutunga kazi ya fasihi simulizi.

i)       Kuwa na jambo lakuelezea (tukio).Mtunzi anapaswa kuwa na jambo ambalo anaona kuwa linasababisha mivutano katika jamii.Jambohilo lazima litoke katika jamii inayohusika na isiwe nje ya jamii hiyo.

ii)    Kuteua utanzu atakaotumia.Mtunzi  ni vyema kujua ni utanzu upi atakaotumia katika kuwasilisha jambo hilo kwa jamii.Kwa kawaida fasihi simulizi ina tanzu nne ambazo ni hadithi, ushauri, semi na Sanaa za maonyesho (maigizo).

iii)  Kuteua vipengele vya maudhui, mtunzi anapaswa aangalie nini dhamira yake, kuna ujumbe gani kwa hadhira, hadhira itapata maadili gani na je migogoro ipi na iwasilishwe vipi ili isipotoshe lengo zima la kazi yake.

iv)  Kuteua kipera kitakachotumika katika uwasilishaji wa kazi yake kwa hadhira, mfano kama mtunzi ameamua kutumia utanzu wa hadithi; hanabudi kuchagua kipera kimoja wapo kati ya ngano, soga, vigano, visasili au tarihi (visakale)

v)    Uteuzi wa vipengele vya fani.Baada ya kubaini vipengele vya maudhui, msanii anapaswa aangalie namna atakavyowasilisha maudhui hayo kwa jamii.Hapa atatumia au atashughulika na vipengele vya fani ambavyo atavitumia katika kuwasilisha ujumbe wake.Vipengele hivyo ni muundo, mtindo, wahusika, matumizi ya lugha na mandhari.Sehemu hii ndiyo ambayo mtunzi anatakiwa kutumia ufundi na ubunifu wa hali ya juu ili kazi yake ieleweke, ielimishe na kusisimua hadhira.

 

 

 

 

 

 

MADA YA 3: KUHAKIKI KAZI YA FASIHI ANDISHI

MADA NDOGO-1: MAENDELEO YA FASIHI ANDISHI.

Fasihi Andishi ni kazi ya sanaa inayotumia lugha na kuwasilishwa kwa njia ya maandishi.Msingi wa utunzi na uwasilishaji wa sanaa hii ipo katika maandishi.Fasihi andishi ni changa ikilinganishwa na fasihi simulizi kwa sababu fasihi simulizi imekuwepo kabla ya uvumbuzi wa teknolojia ya uandishi,uchapaji na uchapishaji.

 

SIFA ZA FASIHI ANDISHI

Fasihi andishi inasifa zifuatazo;

Ø Ni changa kuliko fasihi simulizi

Ø Huwasilishwa kwa njia ya maandishi

Ø Ni mali ya mtu binafsi

Ø Haiwezi kubadilishwa kirahisi ikishaandikwa

Ø Baadhi ya tanzu zake kama riwaya hutungwa kwa muda mrefu.

 

 

A.Mwelekeo wa kazi za fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar wakati wa ukoloni.

Kimaudhui Kazi nyingi za fasihi andishi nchini Tanganyika na Zanzibar zilishughulikia masuala mbalimbali ya kimaisha lakini kazi nyingi zilikuwa na mambo ya mila na tabia kama njia ya kufundisha maadili .vile vile zilishughulikia utamaduni, mawaidha, dini, maadili mema na maonyo na kazi zilizoopinga ukoloni .Wakati  wa ukoloni  nchini Tanganyika na Zanzibar  kazi za fasihi zilishughulikia mambo kadhaa kama ifuatavyo:

Mosi,Suala la Utumwa,katika riwaya ya “Uhuru wa watumwa‘(1934) chaJames Mbotela kinashughulikia uhusiano baina ya mataifa ya magharibi na ya Afrika.Katika riwaya  hii mwarabu na muislamu wanalaumiwa kwa utumwa uliokuwepo Afrika Mashariki wakati mkoloni anasifiwa kwa kuleta uhuru japokuwa utumwa ulitiliwa nguvu na ukoloni.

       Kwa ujumla hadithi ya uhuru wa watumwa inaonyesha ubaya wa biashara ya utumwa iliyoendeshwa na waarabu na papo hapo inaonyesha matukio yaliyowapata watumwa mambo yaliyowaumiza na uchungu ulowapata watumwa hao.

    Mwandishi anaeleza mateso ya watumwa  kwa uchungu na mchomo mkali.Pia hadithi hii inawatukuza wakoloni wa Kiingereza,ikijaribu kumfanya mwafrika akubali kutawaliwa.Hadithi hii inausuta utumwa wa kimwili uku ukiusifu ule wa akili na mawazo ambao ni utumwa ulio mbaya zaidi.

Mwaka 1949-1960  kazi nyingi za fasihi za Kiswahili hasa riwaya zilifuata mkondo wa ngano na fasihi simulizi kama za Paukwa   pakawa…hapo zamani za kale palitokea…..,Kimaudhui fasihi simulizi zilijadili maadili ya kufuatwa katika kujenga jamii  inayofaa katika maisha.Mfano mzuri wa vitabu hivi ni Adili na Nduguzi (1952) utenzi wa mwanakupona (1858) na Al-inkishafi (1890).

Katika Adili na Nduguze  mwandishi alitumia visasili vya jadi ya kiarabu kama vile matumizi ya majini anaonya dhidi ya uchoyo na kuhimiza moyo wa wema, usamehevu na kutosheka.

Pili Suala la nafasi ya Mwanamke,Katika utenzi wa mwanakupona,mama anatoa mafunzo kwa binti yake.Humo ndani ya utenzi mwanamke anapaswa kujitazama kwa nyenzo tatu.ambazo ni;

Ø Yeye ni nyenzo ya starehe ya mume wake hivyo inampasa ajitahidi mno kumfurahisha ili apate rehema zake, kwani Mungu hata acha kumtia hatiani kwa kutomtimizia haja mume wake na atakapomkana mbele ya Mungu.

Ø Inampasa mwanamke awanyenyekee wanaume wote isipokuwa watumwa tu na aonyeshe kilicho na heshima kubwa kwao.

Ø Mwanamke ajione kuwa yu mmoja wa matajiri au maskini (watumwa).

Binti anayeandikiwa shairi hili ni tajiri naye anaaswa asichanganyike na watumwa, watu duni waliodharauliwa duniani

Tatu,suala la  ukombozi/uhuru , miaka ya 1950-1960 Shughuli za kisiasa zilipamba moto na kusababisha kuibuka kwa fasihi ya kisiasa ambayo wasanii wake walizitumia kumpinga mkoloni.Shaaban Robert alionyesha upinzani wake hasa katika riwaya zake za Kusadikika (1951) na Kufikirika (1967) ambamo zaidi ya kuwatetea wajumbe mbalimbali walikuwa  wakiutetea uhuru wa Tanganyika na Zanzibar. Pia mwandishi anaitetea serikali ya kikoloni kwa kejeli kubwa kwani ilikuwa inainyonya Tanganyika na Zanzibar kwa ajili tu ya kukidhi “Ugumba na Utasa” wa mfalme na malkia.Ugumba na Utasa ambao Shaaban Robert  kautumia kwa  ishara tu ya mahitaji ya wakoloni.

Nne,suala la  Uongozi,Katika “Kusadikika”mwandishi anajadili suala la haki ya watu dhidi ya uongozi kandamizi wa kiimla, utawala usio na kiasi wala mpaka ni utawala ambao  hukwamisha maendeleo ya nchi na watu wake.Kwa sababu huwanyima  watu uhuru wa kufikiri na kuchangia katika maendeleo ya nchi yao. Kwa kutumia mbinu ya kejeli, tashtiti,misemo, nahau. mwandishi amejitahidi kufikisha lengo lake la kuonyesha hasara ya kuyakwamisha maendeleo ya nchi.

Tano suala la Ukoloni,ukoloni  wa kiutamaduni ni mwanzo tu wa ukoloni wa siasa na uchumi. Hata katika riwaya ya Tafsiri ya hadithi ya ”Chinua Achebe”ShujaaOkonkwo (1932) ambapo wamisionari walitangulia kuja ili baadae watawala waje na kuiteka nchi yote.Hivyo wamisionari walishirikiana na watawala katika kuwanyanyasa na kuwanyonya watu.

TOFAUTI  KATI YA MHUSIKA  MKUU WA  ZAMANI NA WASASA

Mhusika wa zamani alikuwa na  sifa zifutazo;

Ø Alikuwani halisi mwenye sifa zisizo za kawaida ambaye alisanifiwa na msanii kwa makusudi mazima ya kuumba.

Ø Alikuwa mfano bora wa kuigwa na kumfanya awe kielelezo cha ukweli na ukamilifu wa maisha na mwenye kupigania na kuleta mambo hayo bila kuwa na dosari.

Ø  Alitafakari maisha ya jamii kwa njia ya matendo makubwa na lugha teule.

Ø Alijitokeza  kuwa mtendaji mkuu wa  wakati wote

Ø  Hakuwa na saikolojia wala hisia

Ø  Mhusika mkuu wa zamani kama vile wa kwenye hadithi ya kifasihi alijitokeza kama mhusika mkuu wa wa wakati wote. Kwa msanii wa namna hiyo ya wahusika, dhana za wakati na ukweli uliokamilika zilikuwa katika hali ya kutobadilika wakati na ukweli vilikuwa na vitu vilivyotitia pamoja.

Kwa jinsi hiyo maandishi ya kisanii yaliyopewa jukumu la kuzibeba sifa hizo yalilengwa kuwa ni ya wakati wote, yasizeeke.

 Mhusika mkuu wa kisasa anayaona maswala yasiyotulia  bali ni maswala ambayo yana badilika pamoja na jamii.Na baadhi ya wasanii wa kisasa wanaona kuwa,suala la ukweli uliokamilika kwa kiasi kikubwa ni ndoto iliyomo katika vichwa  vya watu tu na wala si maisha halisi.

     Mhusika mkuu wa kisasa  yuko katika wakati  maalumu wa kihistoria ambapo anayazamia maisha kwa undani na kuyatafakari. Kadri  Shaban  Robert alivyozidi kuandika kama Maisha yangu na baada ya miaka Hamsini(1966),Wasifu wa Siti binti Saad (1967) Siku ya utenzi wote(1968) ndivyo alivyozidi kuwapa wahusika wake sifa zinazokaribia au zinazoelekeana katika hali halisi ya maisha.Hii ina maana kwamba mkabala wake  ulizidi kuelekea katika hali ya kueleza ukweli kwa kutumia mbinu za kisanii ambazo hazikutenga kazi ya Sanaa kwa kiasi kikubwa na uyakinifu wa maisha.Kwa ujumla fasihi Andishi ya awali ilihusu zaidi maadili na masuala ya kidini kama katika”Adili na nduguze”.

Pia uwepo wa  mvutano  baina ya wakoloni na waafrika, Ulikuwa unadhihirishwa katika baadhi ya kazi za fasihi Andishi za awali.Pia maandishi mengine ya fasihi yalihusu matarajio ya jamii itakiwayo baada ya ukoloni, kama katika kufikirika na kusadikika, katika kipindi hiki tanzu za fasihi andishi zilizokuwapo ni riwaya na ushairi. Baada ya uhuru, tamthiliya zote za Kiswahili zilizochapishwa zilikuwa zimeandikwa na wakenya, watanzania hawakujitokeza katika uwanja huu hadi baada ya uhuru.

 

B: Mwelekeo wa kazi za fasihi Andishi nchini Tanzania baada ya uhuru

 Baada ya uhuru kulikuwa na fasihi mchangamano ambayo ni vigumu kuainisha hadi tukio kuu la kutangazwa kwa Azimio la Arusha, kabla ya hapo fasihi kwa kiasi kikubwa, ilikuwa ya kushangilia uhuru uliopatikana hasa katika magazeti ambako mashairi na hadithi nyingi zilionyesha hoi hoi ya lelemama za uhuru.

Kwa upande wa mashairi, vitabu kama vile Utenzi wa uhuru wa Tanganyika(1967) na utenzi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania(1968) viliandikwa wakati huo. Ni kipindi hicho cha uhuru utanzu wa tamthiliya ulijitokeza kwa mara ya kwanza kwa upande wa Tanganyika na Zanzibar.

Mwandishi maarufu wa tamthiliya aliyejitokeza kipindi hicho Ebrahim Hussein ambaye tamthiliya yake ya kwanza “wakati ukuta”(1969) ilichapishwa ikifuatiwa na tamthiliya ya “Kinjekitile”(1969)

Fasihi ya Kiswahili imepevuka zaidi kwenye miaka ya 1970. Mulokozi(1996) anasema karibu tanzu zote za fasihi Andishi ya Kiswahili zimepata wawakilishi. Hali hii imejitokeza fasihi za mokondo mbali mbali.

Kimaudhui, fasihi andishi nchini Tanzania baada ya uhuru imejadili dhamira mbali mbali ambazo zinatokana na matukio  mbali mbali ya kihistoria yaliyojitokeza katika jamii yetu ya Tanzania.

Kipindi maalumu cha maisha kina matukio yake maalumu ambayo huigusa jamii kwa uzuri au ubaya na kuwa dundo la moyo la kipindi hicho ndichi kinachojenga kilele. Aidha tukio linapokuwa dundo la moyo la kipindi fulani cha maisha huwa pia mada kuu(muhimu) ya wakati huo kwa jamii inayohusika.Mada hiyo uweza kujitokeza kinagaubaga katika taaluma mbali mbali za jamii na fasihi ikachukua nafasi muhimu.

Kipindi cha uhuru ( miaka   ya 1960) fasihi ya kipindi hiki ilitawaliwa na ukombozi wa bara la Afrika na ujenzi wa jamii mpya baada ya uhuru. Masuala haya  yaliyojitokeza  katika fasihi andishi ya Tanzania wakati huo. Hivyo palitokea fasihi andishi za kisiasa na kifalsafa zilizojadili kuhusiana na  maisha, utawala na ujenzi wa jamii mpya.Kazi nyingi za fasihi zilipingana  na ukandamizaji, ubinafsi na pamoja na unyama mwingine uliokuwa unafanywa.

Pia  fasihi za kipindi hiki zilijadili suala  la ubinadamu,Usawa na Ustawi. Baadhi ya kazi hizo ni za Shaaban Robert,ambazo ni  Utu bora mkulima (1987) na siku ya watenzi wote(1968)

Pia zinajadili suala la ukombozi, mfano riwaya ya kiimbila “Lila na Fila” (1966) iligusa dhamira hiyo kiishara na  Tamthiliya ya E. Hussein”Kinjekitile” (1969). Katika kipindi cha miaka ya sitini ilitokea fasihi ya aliyojadili  maadili mema na maonyo.

Fasihi hii ya  maadili inawakilishwa na J.M Somba “kuishi kwingi kuona mengi”(1968) “Alipanda upepo akavunatufani” (1968) Mathias Mnyapala “Diwani ya mnyapala(1965) S.A Kandoro “Mashairi ya Saadan”(1972), Akili mali “Diwani ya Akili Mali”(1967)

Kazi nyingine ya fasihi iliyojitokeza katika kipande hiki ni  riwaya na hadithi fupi za upelelezi na za mapenzi.Fasihi ya aina hii ilizuka kutokana na nguvu mbali mbali za jamii.

     Kwa Tanzania, aina hii ya fasihi ililetwa kwa mara ya kwanza na M.S Abdulla alipoandika riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale”(1959) na miaka ya 1960 aliandika riwaya ya “kisima cha giningi”(1968) akafuatiwa na katalambula  aliyeandika kitabu cha “Simu ya Kifo”(1965)

Mwisho, kazi za fasihi zilijitokeza miaka ya sitini ni fasihi ya mila na utamaduni inayowakilishwa na M.S Farsy “Kurwa na Dotto”(1960) F.Nkwera “Mzishi wa baba ana radhi zake” (1968)

Kipindi cha Azimio la Arusha mwaka 1967, Azimio la Arusha ,Baada ya azimio la Arusha kutangazwa  Azimio  lilionekana kwa wanasiasa na wananchi wengi kuwa ndio dira ya kuitetea jamii ya Tanzania katika maisha bora ya ufanisi na maendeleo, kwa hiyo kipindi cha miaka mitano  hivi baada ya Azimio la Arusha kulikuwa na fasihi ambayo ilitukuza maadili ya awali yaliyotokana na tamko la Azimio la  Arusha.

Maudhui yaliyotawala fasihi ya kipindi hiki ni ujenzi wa jamii mpya kwa kupitia nguzo ya siasa ya ujamaa na kujitegemea. Kazi hizi zilizosisita mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni, zilizopigania jamii mpya Ijapokuwa bila kuonyesha kimantiki (kiyakinifu) vipi jambo hilo lingewezekana. Mfano wa kazi hizi ni:-Mashairi ya miaka kumi ya Azimio la Arusha (1977),Mashairi ya Azimio la Arusha  (1970),Utenzi wa zinduko la ujamaa (1972),Utenzi wa kumbukumbu ya Azimio la Arusha (1970),Matunda ya Azimio la Arusha (1980),Liwazo la ujamaa (1978),Mtu ni utu (1971),Ndoto ya Ndaria (1976),Njozi za usiku (1970),Kijiji chetu (1971) n.k

Vile vile  Azimio la Arusha pamoja na  siasa yake iliyosisitiza kuhusu umuhimu wa vijiji na umuhimu wa kilimo, zilitokea kazi za fasihi ambazo zilihubiri kuhusu maisha bora wa vijiji yaliyo linganishwa na yale ya mjini.

  Baadhi ya watalaam waliolitazama  suala la siasa ya ujamaa ni pamoja na  Shaaban Robert katika riwaya yake ya “Utubora Mkulima”(1968) ,Penina Muhando,”Hatia” (1971) Balisidya Shida (1975) Mnyampala, Ngonjera za ukuta  (1968) Mbogo “Giza limeingia”(1980)  mashairi mbali mbali katika magazeti n.k katika kazi hizi mvutano baina ya mji na kijiji ambao ulileta matatizo ya wizi, ujambazi, umalaya na mengine ya aina hiyo yalitolewa dawa moja tu  ambayo ni kurudi vijijini. Jibu hili halikuwa sahihi kwani linakwepa kiini hasa cha tatizo  na  lilipotosha maana halisi ya kijiji na kilichotakiwa kuundwa katika jamii ya Tanzani.Kijiji kilionekana kuwa mahali pa kuwa lundika wahuni walioshindwa maisha ya mjini.

Katika kipindi hiki cha 1970-1980,zilijitokeza kazi ambazo zilitazama suala lakujenga jamii mpya kwa kutafakari na kujiuliza na hata kwa mashaka na wasi wasi pia. Hususani baada ya kubaini utata, migongano ya kitabaka na ukuaji wa haraka wa ubepari wa kimji. Mfano,Kiu (1972) Kichwa maji (1974),Gamba la nyoka (1979),Nyota ya Rehema (1978) Dunia uwanja wa fujo (1979)

Kwa ujumla miaka ya 1980 riwaya ya Kiswahili imeshuhudia jaribio la muundo wa riwaya ya kifalsafa. Lakini kama ilivyogusiwa kwa kiasi kikubwa mikondo ya riwaya imeendelea kuwa ile ile ya miaka ya sabini. Riwaya ya ukasuku katika upande wa riwaya dhati imepotea. Badala yake kuwa riwaya inayopevuka nakutumia ukweli wa mambo. Inayojaribu kubainisha migongano ya kijamii katika vipengele mbali mbali vya maisha hususani vya kiuchumiu ijapokuwa waandishi wanafanya hivyo katika mkabala au mitazamo ya maisha inayotufautiana,mikabala hiyo ni kama vile;Mfumo wa vyama vingi,Utandawazi

Kipindi  cha   mfumo wa vyama vingi, Mfumo wa vyama vingi ulianza miaka ya 1990 hapa nchini ambapo uliambatana na kuanzishwa kwa utitiri wa vyama vingi.Fasihi andishi iliyojitokeza kipindi hiki ilizungumzia mfumo wa vyama vingi na athari zake kwa jamii yake. Mfano  wa kazi hizo ni riwaya ya “Nyuma ya pazia” (1996), na mashairi mbali mbali yaliyokuwa yanaandikwa kwenye magazeti.

Kipindi cha utandawazi,mfumo huu  ulienda sambamba na ubinafsishaji wa soko huria umewaathiri sana waandishi wa fasihi ya Kiswahili.Katika fasihi ya Kiswahili  utandawazi umesababisha kuzuka kwa fasihi mpya ya Kiswahili ambayo imezaliwa mwanzoni mwa miaka ya 1990,muda mfupi baada ya neno utandawazi kuingia masikioni na kuzama akilini mwetu kuanzia 1980.

Utandwazi  ni  mfumo wa uhusiano wa kimataifa katika nyanja mbalimbali kama vile biashara,uchumi au siasa uliowezeshwa na maendeleo ya teknolojia ya habari yanayofanya mataifa na jamii kuwasiliana kwa urahisi.Pia katika  utamaduni, miongoni mwa jamii tofauti za dunia zimekuwa na mfungamano na uhusiano uliojitokeza katika miaka mingi iliyopita hasa katika biashara na uchumi,na kiutamaduni.Mfungamano na uhusiano huu unaotofautishwa  na uhusiano mwingine wa aina hii uliojitokeza kabla,kwasababu utandawazi umepata kazi kubwa ya kuwekeza mitaji na kuvuna faida kubwa  kiuchumi  kiutamaduni, ikisaidiwa na maendeleo makubwa ya kiteknolojia yaliyopatikana karibuni hasa ya vyombo vya habari vya masafa marefu.Utandawazi unahusishwa na kuenea kwa tamaduni za kimataifa (Marekani na Ulaya) kwa njia ya biashara (kama vile vinywaji vya Cocacola, Bia na pombe kali ambazo zamani zilikuwa hazijulikani). Mtiririko wa muziki na taswira kupitia video,luninga,mitandao ya kompyuta/Tanakilishi na simu,CD, DVD na VCD.Mfano wa fasihi ya Kiswahili ni kama vile Nagona(1990), Mzingile(1990),Babu alipofufuka(2001). Makuadi wa soko huria(2002),Dunia yao(2005), Mkama duma(2005) zimeathiriwa sana na utandawazi wa kimagharibi, sifa moja kubwa ya kimaudhui miongoni mwa kazi hizi ni ile ya kushughulikia kwa kina matatizo ambayo yana kabili ulimwengu wetu leo.Ingawa bado riwaya hii inajishughulisha kwa kiwango fulani na matatizo ya ndani ya nchi na jamii husika kwa kiasi kikubwa imekiuka mipaka ya kitaifa na kuenea kwa kiasi kikubwa inachunguza si jamii ya Tanzania tu bali dunia yote huku ikionyesha athari za utandawazi kwa jamii hizo.

  Katika riwaya ya  Babu alipofufuka (2001), Dunia yao(2003) na   Bina- Adamu (2002), Suala zima linaloshughulikiwa kifalsafa ni siasa. Nini maana ya kuishi? Nini maana ya uhuru? Nini maana ya maendeleo? Nini maana ya uraia wa mtu? Nini maana ya uzalendo? Kwanini kikundi kidogo cha watu wapange maisha ya watu wengi katika  jamii Fulani  na  nje ya jamii hiyo? Kuna dunia ngapi katika dunia moja ya jamii fulani?  Mipaka ya dunia hizo ni miembamba au mipana kwa kiasi gani? Nini maana ya kifo? Nini maana ya kuishi? Inawezekana mtu anayeishi akawa amekufa? Nguvu zipi zinaongoza ulimwengu wetu?  Zinaongoza kwa mslahi ya nani?  Athari hizi za utandawazi katika jamii na maisha  halisi zimehitimishwa na  Chachage, ambaye riwaya yake ya “Makuadi wa soko huria”(2002) inavua nguo na kusambaratisha utandawazi na utetezi wake wa ndani.

Kwa jumla maendeleo ya fasihi Andishi nchini Tanzania  baada ya uhuru ni makubwa sana ukilinganisha na wakati wa ukoloni. Tanzu zote za fasihi  Andishi, riwaya, hadithi fupi ushairi na tamthiliya zimepanuka sana. Vile vile kama waandishi wengi sana wa tanzu hizo na uandishi wao umekuwa ukibadilika kulingana na mabadiliko mbali mbali yanayoitokeza katika jamii. Kila tukio la kihistoria lililotokea katika jamii limezaa kazi zake za fasihi.

 

MADA NDOGO 2; KUHAKIKI USHAIRI

USHAIRI

 Ushairi ni Sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalumu wa maneno fasaha na yenye muwala,kwa lugha ya mkato, picha au sitiari au ishara katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kueleza tukio, wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi fulani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.Kutokana na maana hiyo kuna mambo muhimu yanayojitokeza katika ushairi:

Ø Ushairi ni Sanaa yaani kazi iliyobuniwa na mtunzi mahususi.

Ø Ushairi una ufungamano na hisia.

Ø Ushairi una mpangilio wa aina fulani kuanzia kiwango cha sauti, neno, sentesi hadi ubeti.

Ø Ushairi huchota hisia na tafakari zake kutoka katika ulimwengu halisi wa maisha ya jamii na mara nyingi hufungamana na falsafa ya jamii fulani.

Ø Ushairi hutumia lugha ya mkato yenye kueleza mambo mengine kwa maneno machache kwa kutumia mbinu za taswira na tamathali za semi.

Ø Ushairi huzingatia sana dhana ya urari (ulinganifu wa vitu) kimuundo.

Ø Ushairi una uhusiano na muziki (nidhimu) ngoma na uchoraji (mchoraji) hutumia rangi na brashi mshairi hutumia taswira na maneno.

AINA   ZA MASHAIRI YA KISWAHILI

Kuna aina tatu za ushairi waKiswahili.Aina hizo ni:-

 

1)    USHAIRI WA KIMAPOKEO

Ni mashairi na tenzi za kijadi zenye kufuata kanuni za urari wa mzani na mpangilio wa vina vya mwisho au kati.Katika ushairi wa kimapokeo kuna mambo ya msingi ambayo   ni uti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili.Shairi la Kiswahili lazima liwe na vina na mizani,mistari ubeti na kituo.

Katika utenzi (aina pia ya ushairi wa kimapokeo) kuna kuwa na bahari katika mstari wake wa mwisho.Ushairi wa kimapokeo unaweza kugawanyika katika sehemu kuu mbili yani Tenzi  na Mashairi

a)    TENZI

Ni utungo ambao kimaudhui huelezea tukio fulani linalotokea katika jamii au liliwahi kutokea.Pengine huweza kuwa maelezo juu ya wasifu wa mtu fulani, jambo fulani la kihistoria au jambo lolote zito linaloelezwa kwa maelezo marefu.Utenzi ni masimulizi marefu juu ya jambo fulani maalumu.

Katika upande wa fani utenzi una sifa za pekee kabisa

v Beti,Utenzi una beti nyingi kuliko yalivyo mashairi au aina nyingine yoyote ya ushairi.Beti hizi zaweza kuwa 100,200,300 au zaidi kutegemeana na ufundi wa mshairi mwenyewe.

v Mizani,Utenzi huwa hauna mizani ndefu,tenzi zilizoshamiri sana katika jamii hii ni zile zenye mzani nane nane katika kila mistari zaweza pia kwenda zaidi ya nane kufikia kumi na moja lakini hazuii zaidi ya hapo

v Vina,Katika utenzi kila ubeti huwa na mistari minne, mistari mitatu ya kwanza ikiwa ina vina vyenye urari sawa na ule wa mwisho ikiwa na kina tofauti ingawa vina vya mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari sawa lakini vina hivyo hubadilika badilika toka ubeti mmoja hadi mwingine.

v Uunganifu, utenzi ni utungo wenye visa/hadithi vilivyounganika kimantiki ( kimawazo) katika mtiririko na msuko wake kimatukio huwiana.

v Kina cha mwisho,Katika utenzi kina cha mwisho katika msitari wa mwisho wa kila ubeti huwa hakibadiliki badiliki,kina cha mwisho wataalamu wengi wa ushairi hukiita bahari  kwa sababu huwa kimetenda na kuongelewa katika utenzi mzima  Mfano wa tenzi: S.Robert, Mapenzi bora,A.Abdilatif, Utenzi wa maisha ya Adam na Hawa (1971)   J.K.Nyerere, Utenzi wa Injili kadiri ya utungo wa Luka (1996).Mfano Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK)

 

 

          Ubeti 6: Liyongo Kitamkali

                        Akabalighi vijali

                       Akawa mtu wa kweli

                       Na hiba huongeya

        Ubeti 7: Kilimo kama utukufu

                       Mpana sana mrefu

                       Majimboni yu maarufu

                      Watu hujakumwangalia

   Ubeti 10:Sultani pate Bwana,

          Papo nae akanena,

          Wagala mumemwona,

           Liyongo kiwatokeya

b)    MASHAIRI

Shairi kama sehemu ya ushairi, ni utungo ambao huelezea kwa ufupi mambo fulani kuhusu binadamu na mazingira yake.Aghalabu mashairi huelezea mambo yanayomhusu binadamu na maisha yake ya kila siku.Mashairi ya kimapokeo yanapoandikwa hufuata kanuni za vina, mizani, mistari, ubeti na kituo mfano:-

KUNTU SAUTI YA KIZA (FUNGATE YA UHURU-UK 38)

Nyuki ni mtanashati, umbo na zake tabia,

Yeye yu kila wakati, vichafu huvikimbia,

Mchana na kulati, hatui kwa kukosea,

Kuntu sauti za kiza, Nyuki hapendi vichafu.

 

Ni inzi na sio nyuki, Nadhafa hajazoea,

Kwa uchafu ni ashiki, hawezi kuuachia,

Vianzavyo humiliki, fahari hujonea,

Kuntu Sauti za kiza, Nyuki hanyoni vichafu.

 

U WAPI UZURI WAKO

U wapi uzuri wako, haupo umepotea,

Ya wapi maringo yako, na hashuo za dunia,

Leo upo peke yako, sote tumekukimbia.

 

Sasa ni chano cha maji, watu wajichanyatia,

Umekwisha ujuwaji, haya zimekupatia,

Yale usoyatarajia kwako yamekuhamia.

 

DAFINA

Paa ni kuruka angani, kama ndege wa tiara

Paa ni mnyama porini, ni mwenye nyingi, Papara

Paa ni kuteka mengine, moto uwako imara

Paa ni toa migombani, Samaki atie sura

Paa Pia ni la nyumba, makuti au kurara

Mgodi wa Kiswahili ni dafina isiyokwisha

 

2.     USHAIRI WA MLEGEZO / KISASA / MASIVINA

Ni mashairi yasiofuata urari wa vina na mizani.Vina vinaweza kutoka lakini si lazima katika mistari.Pia mapigo yanaweza kuwa sawa kwa idadi katika mfululizo wa vipande kadhaa lakini si katika tungo nzima.Mfano:

CHAI YA JIONI

Wakati tunywapo chai hapa upenuni

Na kuwatazama watotowetu

Wakicheza bembea kwa furaha

Tujue kamba ya bembea yetu

Imeshalika na imeanza kuoza

Na bado kidogo tutaporomoka

 

Kulikuwa na wakati uinisukuma juu

Nikaenda zaidi ya nusu duara

Kulikua na wakati nilidaka

Ulipokimbia na kuanguka

 

 

Sasa tukisubiri ndoto tusizoweza kutekeleza tena

Tumalize machicha ya chai yetu ya jioni

Bila kutema tena na kuwa tabasamu

Baada ya hapo tujilambe lambe utamu utamu

Uliobakia kwenye midomo yetu

Tukikumbuka siku ilee ya kwanza

Tulipoutana jioni chini ya mwembe

Tukifunga bembea yetu

Naye umbwa samba akikusubiri

Lakini kabla hatujaondoka kimya kimya

Kukamilisha nusu duara iliyobakia

Tuhakikishe vikombe vyetu visafi

(Kazilahabi 1988)

 

 

 

VIJENZI VYA USHAIRI WA KISWAHILI

Ushairi wa Kiswahili unajengwa na vipengele vifuatavyo:-

1.     Mpangilio wa maneno

Maneno ya ushairi hupangwa ili  kuleta maana fulani,sauti za aina fulani  au urari fulani wa mizani.Katika shairi la Kazilahabi “Kisu mdomoni” ,(kiuchumi) uk 10 kuna mstari ufuatao.

“Ya nyuma sana nisijali ya mbele sana niyakabili. Hapa neno “sana” limewekwa makusudi kati ya “nyuma” na “nisijali” ili kupata maana mbili. Mambo ya zamani sana (ya nyuma sana) na kutojali jambo neno (sana nisijali) kama neno sana kinga kuja baada ya nisijali maana hizo mbili zisingalitokeza.Vivyo hivyo uwili huu wa maana tunaupata katika kipande cha pili cha mstari huo “ya mbele sana niyakabili” kutokana na mpangilio wa maneno.

2.     Takriri na Ridhimu au wizani

Takriri ni mbinu ya kurudia rudia jambo kwa kusudi maalumu, vina na urari wa mizani ni aina ya takriri. Mtunzi anaweza pia kurudia rudia maneno fulani au silabi fulani kwa shabaha malumu. Kwa mfano katika shairi la “ Kufa moyo” Shaaban Robert  anatumia mbinu ya takriri kwa kurudi rudia kifungu cha maneno “ siku ya ………. Kwa msisitizo:-

Siku ya panga kufuta, mashujaa kwenda kona

Siku ya kuja matata, kwa damu kwenda mdundo

Siku ya watu kuteta, kufa moyo mfundo

Siku ya kung’ara nyota za watenzi wa mtindo

      (Shaaban Robert 1991 : 48-49)

Takriri hutumika sana katika nyimbo na mashairi ili kutia msisitizo.

Ridhimu ni mapigo asili ya lugha ,kila lugha ina mapigo yake.Mawimbi ya sauti yenye kupanda na kushuka na yanayofunga maana na mfuatano wa sauti usio na maana yoyote.

Ridhimu ya ushairi wa muziki hutokana na mlingano wa vipande vya mapigo ya lugha au sauti . Katika muziki vipande hivyo vya mapigoni lazima vilingane kabisa katika ushairi.Vinaweza kupitana kidogo ili kupunguza maudhi masikioni.

3.     Taswira au Picha

Taswira ni mbinu ya kuumba picha ya jambo katika mawazo ya msomaji au msikilizaji wa tungo hilo kwa kutumia maneno. Picha ya maneno ikichorwa vizuri mtu huweza kuhisi, kuona, na hata kunusa kile kinachozungumzwa.

Mfano:

Amina umejenga, umekufa umetangulia

Kama ua umefunga, baada ya kuchanua

Nakuombea mwanga, peponi kukubaliwa

Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua

(S. Robert Amina 1966: 3)

Katika ubeti huu, mshairi analinganisha maisha ya mauti ya Amina kwa njia ya picha na ua mbalo limekuwa likichanua na kisha likafunga au kunyauka.

4.     Tamathali za Semi

Tamathari ni umithilishaji yaani uwakilishaji wa jambo kwa kulinganisha au kulifananisha na jingine.Kwa mfano badala ya kusema “Juma alikuja mbio sana” Mshairi atasema “Juma alikuja kama umeme” Tamathari nzuri hupanua, huyadumisha na huipa uhai na uhalisia zaidi dhana inayoelezwa, huburudisha na kuzindua akili ya msomaji au msikilizaji wa shairi na athari ya kudumu katika hisia na mawazo yake.

Tamathari zinazotumika zaidi katika ushairi ni Tashbiha, tafsida, tashhisi, mbalagha, kejeli, sitiari n.k.

5.     Hisia za kishairi

Hisia hizi hutokana na msukumo wa ndani wa moyoni alionao mshairi wakati anapotunga shairi lake na hujidhihirisha katika uteuzi na mpangilio mzuri wa maneno yenye kuwakilisha maudhui husika kwa mfano, maudhui ya huzuni hudhihirika katika maneno yanayotumika ambayo aghalabu yanadokeza hali ya huzuni, vina vyenye sauti ya kilio.Mfano ee, lel, lel, lel, ea, aa, ya n.k.

Mfano mzuri ni shairi la Shaaban Robert la AMINA ambazo linaomboleza kifo cha mkewe.Hisia za furaha pia huweza kuwasilishwa kwa njia hizo hizo

   Mfano:-Shairi la Cheka kwa furaha

          Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?

            Haya cheka ha! ha!, ndio ada duniani,

            Basu cheka kwa! kwa!, usifike moyo wako.

            (Robert, kielelezo cha fasihi 1968:16)

6.     Lugha ya mkato.

Shairi huzungumza mambo wa ufupi kuliko ulivyo katika maongezi ya kawaida. Hivyo ni muhimu kwa mtunzi kujua namna ya kueleza jambo kwa Lugha ya mkato.Hii inawezekana kwa kutumia taswira na tamathali badala ya maelezo marefu.

7.     Mchezo wa maneno

Mbinu ya kuchezea maneno hutumiwa na washairi ili kutoa maana ya kile kisemwako na kuongeza utamu wa usemaji mara nyingi maneno yenye umbile moja lakini maana tofauti hutumiwa kwa ajili hii mfano katika Shairi la M.Mulokozi la “wale, wale” maana tatu za neno wake (yaani kundi la watu na hao watafune na kumeza chakula “na” “wale”wale” kwa maana ya “hao hao” si wengine zinachezewa ili kuleta ujumbe fulani.Mshairi anaona kuwa hakuna mabadiliko ya msingi yaliyotokea .Kundi lile la walaji limerejea katika madaraka kadharika maneno “kura” na “kula” yamewekwa sambamba ili kuonyesha uhusiano uliopo kati ya uchaguzi (kupiga kura) ulaji.

            Wale wale

            Wale wale ndiyo wao

            Bado wapo palepale

            Wao wale wenye vyao

            Na vya kwao vile vile

            Wala kale wala leo

            Kura huko kule kule

            Mwendo huu ndiyo huo

            Bado tupo pale pale

            (Mulokozi 1990)

 

FANI NA MAUDHUI

Ushairi kama Sanaa hujengwa na mambo mawili ambayo ni fani na maudhui.Maudhui ni mambo yaliyomo (yanayozungumzwa) ndani ya shairi na fani ni njia anazozitumia mtunzi kuyasawirisha maudhui yake kwa hadhira yake.Fani na maudhui huingiliana hutegemeana na kukamilishana.Ni mambo ambayo hayatunganiki, fani hubeba maudhui, na maudhui huathiriwa na fani.Uwiano wa fani na maudhui ndiyo kigezo bora cha ndani cha ubora wa shairi.

Katika fani kuna mambo yafuatayo:- Muundo, mtindo, matumizi ya lugha na jina la kitabu katika kipengele cha lugha kuna mpangilio wa maneno, tamathali za semi, methali, misemo, picha n.k.

Maudhui ni mawazo yanayosemwa ndani kazi ya Sanaa.Mada kuu inayayozungumziwa katika shairi huitwa dhamira.Dhamira inapounganishwa na mtazamo wa mtunzi, Shabaha na ujumbe hupatikana yanaweza kuhusu jambo lolote linalohusika.Maudhui yanaweza kuhusu jambo lolote linalomkera mwanadamu kwa mfano maana ya maisha, mapenzi, mauti, ndoa, elimu, kazi, dini, ukombozi, usaliti n.k.

 

UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI

a)    Mtindo wa mashairi

Masharti ya Kiswahili yana mtindo mingi sana katika utungaji wake kwa hakika si rahisi kutambua ama au idadi ya aina za utungaji wa ushairi,kwani hii hususani kutegemeana sana na ufundi wa mtungaji mwenyewe.Baadhi ya mtindo ya utungaji wa ushairi ni kama ifuatavyo

a)    Mtindo wa pindu

Katika utungaji wa aina hii silabi mbil za mwisho wa mstari hurudiwa rudiwa kwa mfano: kama mstari wa kwanza uliishia na neno “fahamu” basi mstari wa pili utaanza na silabi mbili za mwisho, yaani “hamu” wakati mwingine huitwa “Mkufu”

 

 

 

Mfano:   Zipokeeni Salamu, lamu kilwa na mvita,

            Vita kwa wanadamu, damu zinawezachonyota,

             Nyota njema ni agumu, gumu jema kulipata,

             Pata kwa kuyafuata, fuata mambo mazuri.

       

             Zuri katika dunia, nia mama yanaleta,

             Leta kila la sheria, ria huleta matata,

        Tata watu hujifia, fia ipo kwa kupita,

             Pita usije kupita, pita katika mazuri.

(wamitila, kichocheo cha fasihi simulizi na andishi Uk 224)

b)    Mtindo wa msisitizo

Kuna msisitizo wa aina mbili, kuna msisitizo wa wima na msisitizo wa ulalo

Msisitizo wa wima ni kule kuwa na neno moja likawa linatokea mwanzoni na linarudiwa katika kila mistari wa shairi zima

Mfano:   Ua langu la moyo, nitunzo nipowe

            Ua langu usinitunze, ua nitunze nitowe

          Ua nikae shingoni, ua usinichambue

          Ua la moyo ua, Ua lichanue kwangu

                 (Diwani ya Akilimani 1973:63)

Msisitizo wa ulalo ni ule wa kutumia kibwagizo kama kiini cha habari yote inayozungumziwa katika shairi lote na ikawa hicho kibwagizo cha rudiwa rudiwa katika kila ubeti wa shairi

Mfano:    Kokoni kucha kuchile, risala enenda hima,

             Kufika similatile, ulitimavu si mwema,

             Kumbe nao watambule, haya ninayoyasema,

             Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.

 

             Sipendelei kusudi, na manji mno kusema,

             Nendapo hijitahidi, kimya change hatuzamu,

             Kanama sio mwadi, watu wengine si wema,

             Iwapo kimya si chema, na maneno hayafai.

(fani na taratibu za ushairi wa Kiswahili 1939:18)

 

 

c)     Mtindo wa beti kubadilisha vina.

Iwapo katika ubeti wa kwanza kina cha kati kilikuwa “na” na ile ile cha mwisho kilikuwa “ma” basi katika ubeti unaofuata kina cha kati kitakuwa “ma” na kile cha mwisho kitakuwa “na”.

Mfano:    Kila shairi nalia, chozi latoka machoni,

             Na ninyi mwangalia, wala hamniponzeni,

             Mpenzi kankimbia, naudhika simwoni

             Nirudie we mwandani, roho ipate tulia.

 

             Nakuomba samahani, magoti nakupigia,

             Nisamehe nuksani, zote nilo kutendea,

             Naapa kwa yangu dini, kamwe sitayarudia,

             Narudia we mwandani, roho ipate tulia.

d)    Mtindo wa kubadilisha vina vya kati toka ubeti ili hali vile vina vya mwisho katika ubeti vikibaki vile vile

Katika ubeti wa kina kina cha mwisho kilikuwa “za” basi kina hicho kitaendelea kujitokeza ubeti mmoja hadi ubeti mwingine wakati vile vya kati vitaendelea kubadilikabadilika.Mfano:    

Jalali wangu mchunga, nikidhi yako rehema

 Niweke natangatanga, nitabaruku kwa wema,

Niweke kwenye kiunga,cha malisho ya uzima,

Na majani ya rehema, na vijito vyenye raha.

 

Tabaruku moyo wangu, nisifikwe na zahama,

  Pasinifike machungu, kwani u mwenye hunena,  

 Nakutegemea tangu, wala sinayo tahuma,

 Uniongoze kwa wema, nami nitakutukuza.

 (fani na taratibu za ushairi wa Kiswahili 1986:38-39)

e)     Mtindo wa kidato

Katika muundo huu baadhi ya mistari na maneno yake au silabi zake zina maneno machache au zimefupishwa tofauti na mistari mingine ambayo huwa na silabi au maneno mengi.Ufupishaji huu wa maneno au silabi katika baadhi ya mistari hufanywa kwa lengo maalumu.

Mfano:Tohara, kwa wanawake ni hatari

              Madhara, kwa wake uke, hushamiri

              Hasara, ya peke yake, hudhurika

              Zinduka

            (Wasakatonge 2004:02)

f)      Mtindo wa kuhoji

Huu ni mtindo unaotumiwa na mwandishi wa kuuliza maswali ambayo aidha majibu yake yako wazi au hayako wazi hivyo mtindo huu unaweza kutumika kama tashtiti.

Mfano:     Si wewe?

              Ukinijia mapema kama ukidayatema,

              Nikawa kama wako baba na mama,

              Kakulea kwa ugonjwa na uzima,

              Ni wewe uso hisani.

 

              Si wewe?

              Niliyekunyima chungu kukutafutia tamu,

              Kila kichota hakisishi hamu,

              Ukazoa bila kufahamu,

              Kuhujua kuichota,

              Ni wewe ujilaumu.

         (Fungate la uhuru 1996:42-43)

g)    Mtindo Nafsi

Huu ni mtindo ambao mwandishi anaweza kutumia nafsi ya umoja au wingi au nafsi kundi kila nafsi ina maana yake kimaudhui.Nafsi moja huzungumzia mambo fulani yanayomkabili mtu mmoja tu.Mara nyingi huwa ni maonyo, mawaidha au sifa.

Mfano:     Umeshapwelea nchi kavu,

              Wako werevu umekwisha,

              Sasa tunatweta,

              Utaabani,

              Ni wewe ulo mrafi,

              Si wewe?

         (Wasakatonge 2004:21-22)

o   Nafsi nyingi hutokea pale mashairi anapozungumzia na kundi fulani la watu huku na yeye akiwa mmojawapo.

 

Mfano:     Hatukubali tena,

              Kwetu kurudisha ubwana,

              Kwetu kuurejesha utwana,

              Kwetu kuurejesha utumwa.

              Hatukubali katu,

              Ndani ya nchi yetu.

              Hiyo huru.

        (Wasakaonge 2004:30-31)

o   Lakini nafsi kundi hutoka pale ambapo mwandishi au msanii anapozungumza na kundi la watu huku yeye akiwa ama msimulizi.Hutoa masimulizi kama hadithi au hotuba fulani.

Mfano:     Jua kali ni wasakatonge.

              Wao ni wengi ulimwenguni

              Tabaka lisilo ahueni

              Siku zote wako matesoni

                  Ziada ya pato hawaoni

             Lakini watakomboka lini?

              (Wasakatonge 2004:5)

h)    Mtindo ambao unaruhusu kipande kizima cha mstari wa mwisho wa ubeti kuweza kurudiwa, kikiwa ni chanzo cha huo ubeti unaofuata:-

Iwapo mstari wa mwisho wa ubeti wa kwanza ulikuwa kama “Uwanjani nayanena, leo wote wataona” Basi ule mstari wa kwanza na ubeti wa pili utaanza na “leo wote wataona”

Mfano:    Chochote ulichonacho, kilikuwa kwa mwenzako,

             Leo yeye hako nacho, kimesha hamia kwako,

             Huenda utokwe nacho, kiende kwa mwingine huko,

             Kiumbe wacha vituko, sione ulichonacho.

 

             Sione ulichonacho, ukaendesha vituko,

        Na upambwe chokochoko, mwishowe ni pukutiko,

            Malao akupambacho, kilipambiwa mwenzako

             Kiumbe wacha vituko,sione ulichonacho.

         (Sheria za kutungo mashairi na Diwani ya Amri 1967:30)

Kimsingi mitindo katika ushairi ni mingi sana na hutegemea ufundi wa mshairi katika kuunda mashairi yake na ushair unaweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa.

 

ii)  Miundo ya Mashairi

Muundo ni neno pana ambalo hujumlisha mjengo wa shairi yaani jinsi ulionekana.Mashairi yana mundo mbalimbali kutegemea ufundi wa mshairi mwenyewe kimsingi Shairi linaweza kuwa la kimapokeo au likawa Shairi kisasa. Shairi la kimapokeo huwa na mpangilio maalumu wa vina na mizani, silabi, vituo, beti n.k.Idadi ya mistari huzaa aina mbalimbali za mashairi.

a)    Muundo wa Tarbia 

Kila ubeti wa shairi huwa na mistari mine na kila mstari huwa na mizani kumi na sita (16) vile vile katika muundo huu kila mstari unakua umegawanika katika viande viwili vilivyo na mizani sawa kila kipande kukiwa na mizani nane.

Mfano:     Amkeni kumekucha, wakubwa hata wadogo,

                Wadoho siku waacha, kwa kuogopa kinyongo,

                Kinyongo sikuficha, kukificha ni uongo,

                Mnapowacha madogo, na makubwa mtawaacha.

 

                Na wakubwa mtawaacha, mnapoacha madogo,

                Mfano kama kuchacha, chakula japo kidogo,

                Kidogo kinapochacha, kikubwa hakina kingo,

                Mnapowacha madogo, na wakubwa mtawaacha.

                   (Masahiri ya Saadani 1972:25)

 

 

 

b)    Muundo wa Tathnia

Kila ubeti wa shairi huwa na mistari miwili muundo huu unatiwa zaidi katika nyimbo si muundo ambao hutumika sana katika mashairi ya kawaida ya kusomwa kam mashairi au ya kuimbiwa.

Mfano:    Mjamzito, umelazwa “Thieta”

                 Lazima kupasuliwa

                Chake kitoto tumbo kinatweta

              Hawezi kujifungua

 

                Mwili u moto, tumbo linamkeketa

              Kwa kite anaunguwa

                Jasho na Joto, kiungo cha mpwita

              Na mauti yanamwita

                Ni jambo zito, daktari kufata

              Wauguzi waameitwa

(Fungate la uhuru 1988:08)

c)     Muundo wa Tathilitha

Kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari mitatu

Mfano:    Kujitawala si kwema, kuliko kutawaliwa,

               Kujitawala ni umma, kila yao kuamua,

               Kujitawala si kama, wanguzi na rushwa.

 

 

               Kujitawala khatamu, na umma kushikiliwa,

               Kujitawala hukumu, makosa kushitakiwa,

               Kujitawala si sumu, mara kwa mara kuuwa.

 

    

                 Kujitawala kisomo, kupiga kubwa hatua,

               Kujitawala kilimo, njaa na kuondoa,

               Kujitawala si somo, njiani kusimuliwa.

d)    Muundo wa Takhimisa

Kila ubeti wa shairi unakuwa na mistari, mitano

Mfano:     Hao nyani wanaruka, mara hapa mara kule,

                Hao nyani wanabweka, hawaoni soga mbele,

                Hao nyani wanaanguka, waingiwa na ndwele, 

                Nyani wanababaika,misitu una upele

                Msitu haukaliki, nyani wanahangaika.

 

 

                Msitu wawaka moto, kufukuzwa hao nyani,

                Umeligundua pato, la nyani lenye utani,

                Moto waziona kwato, zilizoko mapangoni,

                Nyani watupa watoto, hawakubaliki mwituni

                Msitu haukaliki, Nyani wanahangaika.

e)     Muundo wa Sabilia

Katika muundo huu mtunzi au mshairi anakuwa na uhuru wa kuweka zaidi ya mistari mitano katika kila ubeti, ubeti unakuwa na mistari sita na kuendelea

Mfano:     Mmea unapokuwa, huifurahisha mvua.

                Lakini siposogea, hulisingizia jua

                Uliamini ni mola, hata maji kukupatia

                Ulikubali kabila, haliishi bila mila

                  Mwanadamu kadhalika, kukua kufurahika

                Huupenda uhakika, wa nyota yake kufika

                Umri wa kuridhisha, huhitaji kujitwisha

                Hapa, ukiufikisha, huona, kufanikiwa

                Maisha ya hupenda, ni, mazuri ya kwenda

         Na siyo yenye kupinda, haya daima hupenda

     (Diwani ya Mloka 2002:18)

iii)   Matumizi ya Lugha.

Hiki ni kipengele muhimu sana katika kazi yeyote ile ya Sanaa ya kifasihi. Matumizi ya Lugha ndiyo yanayofanya kazi fulani ionekane tofauti na nyingine au itofautishe kazi ya Sanaa ya kifasihi na ile isiyo ya kifasihi.Luha ndiyo mzizi wa kazi ya fasihi kwani fasihi ni kazi ya Sanaa inayotoa maudhui ya kutumia Lugha ya maneno.Matumizi ya Lugha katika kazi ya fasihi yako ya aina mbalimbali

a)    Methali, misemo na nahau

Mhakiki anapaswa avifahamu na ajue kuvichambua katika ushairi.Vipengele hivyo vina kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi

*    METHALI

Ni kazi ya Sanaa ya kifasihi inayotumia mafumbo kwa kwaida semi zote zina hakima ndani yake.Ubora wa hekima hiyo hutegemea muktadha hali ambapo methali hutumika.Methali pia ina kazi ya kufurahisha, kutisha, kuonya nakadhalika, waandishi hutumia methali katika kazi zao nani jukumu la mhakiki kuzitambua hizo

*    MISEMO NA NAHAU

Matumizi ya misemo na nahau hushabihana na yale ya methali.Misemo, misimu na nahau huzaliwa, hukua nap engine hufa

     -Sekela amenipaka mafuta kwa mgongo wa chupa (sekela amenipa sifa zilizostahili)

     -Juma katutangulia (Juma amekufa)

b)    Tamathali za Semi

Mulokozi & Kahigi wanasema kuwa tamathali za semi ni maneno, nahau au semi ambazo hutumiwa [H1] na waandishi wa fasihi ili kutia nguvu na msisitizo katika maana, mtindo, na pengine sauti katika maandishi hayo.Tamathali za semi zinatumiwa pia [H2] kuipamba kazi ya Sanaa ya kifasihi kwa kuongeza utamu wa Lugha.

Baadhi ya tamathali za semi ni:-

Ø Tashbiha

Hii ni tamathali ya ufananisha au mlinganisha wa vitu viwili au zaidi katika tashbiha kama ilivyo katika sitiari huwa kuna vitu vitatu vinavyofananishwa ambavyo wataalamu wameviita kuzungumzwa, kufananisha na kiungo.Katika tashbiha hakuna maana dhahania bali kuna ulinganishaji wa vitu viwili vilivyobayana.

Mfano:     Kweli ni sawa na radi, inapotoa kauli…

                Kweli kinywnani ikiwa sawa na moto wa nili

               Kweli kama msumeno hukoreza sawa kweli

Ø Tashhisi (uhaishaji)

Washairi mara nyingine huweza kukipa kitu kisichokuwa na uhai sifa za kitu chenye uhai, hasa sifa za binadamu, kisanaa maelezo ya kitashhisi huwa na upekee unaomwingia msomaji akilini haraka, kwani si jambo a kawaida, mathalani kuona mti “Ukimpungia mtu mkono” au “nyumba ikimkodolea macho mgeni”

Mfano: kimya hakineni jambo si kimya chawatazama…

            Kimya chajazua mambo, pasiwe mwenye kusema.

            Kimya kipimeni sana, msione kutosema.

            Kimya hakichi kunena, kitakapo kusimama.

            Kimya chaja watukana, na kizuwe yalozama.

Katika ubeti huu “kimya” (ambayo ni nomino dhahania) kimepewa sifa za binadamu kinaweza kunena, kutazama, kuzua mambo, kusimama na kutukana.

Ø Metonumia

Hii ni tamathali inayotumia neno (au semi) kuwakilisha neno, kitu, mtu au dhana nyingine yenye kuhusiana nalo neno hilo huweza kutumiwa kwa kuwa dhana inayozungumziwa au kwa kuwa linataja ktu ambacho ni sehemu na kuwakilisha cha kitu kingine kikubwa zaidi.

Mfano neno “kitambi” huweza kutumiwa kuwakilisha tajiri au kabila “meno” huweza kuwakilisha kicheko

Ø Mubalagha

Ni matumizi ya lugha yaliyotiwa chumvi ili kuongeza utamu na kuleta athari fulani katika ushairi wa majigambo, tamathili hii hutumika sana maana huo ni ushairi wa kujitapa na mtu mwenye kujitapa aghalabu hujilimbikizia sifa. Mara nyingi mubalagha hutumika katika tenzi zenye kusimulia habari za mashujaa.

Mfano: katika utenzi wa fumo Lyongo kuna mfano unaokusudiwa kuonyesha ukubwa wa (kimo na umbo) na nguvu za Lyongo.

        “Ruhu zikienda kishindo

              Zima zao hukoma ondo

              Huyo ni bwana wa kondo

              Ashindaye jeshi miya

Ingawa wagala wanajulikana kuwa ni watu warefu akini vimo vyao vilifika magotini tu (ondo) pia Lyongo

Ø Kejeli

Ni usemi ambao maana ya ndani ni kinyume cha maanayake halisi. Ni usemi wa kebehi ambamo kisemwacho na msemaji. Pia kejeli ni tukio ambalo ni kinyume cha lile linatazamiwa au lililotakiwa na ambalo kutokea kwake huwa ni namna ya dhihaka

Katika shairi la “Ibada na Haki” Shabaan Robert anatumia usemi wa kejeli kukebehi watu wanothamini fedha kuliko dini.

Anasema hivi:       Huifanya fedha mungu wao

                    Itazame adha na Imani yao!

                    Na mwenye akili kama hana fedha

                    Hatajwi mahali ila kwa rakadha

                    Na kuadhiriwa kuwa mtu chini,

                    Tazama dunia ilivyo na dini  

Katika mstari wa pili “Itazame adha na Imani yako!” kuna kejeli, mshairi anachotaka kutuambia ni kwamba watu hao hawana adha wala Imani katika mstariwa mwisho “Tazama dunia ilivyo na dini” Anakusudia kutuambia

“Tazama dunia ilivyo na dini kwa hiyo semi hizo ni kejeli kinachosemwa ni kinyume na maana yake halisi kadha toka alama za mshangao!) zimetumika kusisitiza hali ya kejeli.

         

          MBINU ZA KISANAA

Kuna mbinu mbalimbali za kisanaa ambazo hutumika katika kazi za kifasihi ya ushairi na ambazo mhakiki atatakiwa azitambue na kuzifafanua mbinu hizo ni kama vile

Ø Takriri

Ni kurudia rudia neno, sauti, herufi au wazo katika kazi ya Sanaa ya kifasihi.

Mfano:  kweli kitu mahabubu, mwenyezi nijaze kweli

            Kweli siri ya ajabu, huwapa watu fadhili

              Kweli chimbo la johari, linahimili la kweli

              Kweli inatafakari, husema na kujadili

Katika ubeti huu neno “kweli” limerudiwa rudiwa. Neno hili linasisitiza wazo kuu la mwandishi

Ø Onomatopea

Ni mwigo wa sauti. Hutumiwa na washairi kutoa picha au dhana ya kile kinachowakilishwa au kupambanuliwa na sauti hizo. Mfano tukisema “maji yalimwagika mwaaa!” neno mwaaa! Ni onomatopea linawakilisha sauti au kishindo cha maji yanayomwagika. Baadhi ya onomatopea ambazo zimekwisha kuwa sehemu za msamiati wa kawaida. Mfano: pikipiki, bomboni, kata n.k.

Katika shairi la “Cheke kwa furaha” Shabaan Robert ametumia onomatopea ili kuleta dhana ya kucheka

             “Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?

               Haya cheka ha! ha! ha! Ndiyo ada duniani

               Basi cheka kwa! kwa! kwa! Usafike moyo wote

               Pamoja na malaika, wema mbinguni waliko

Maneno ha! ha! ha! na kwa! kwa! kwa!  Ni onomatopea yanayotoa sauti ya kusikika ya sauti ya mtu anayecheka. Huu ni mpangilio maalumu wa sauti ili kutoa picha ya kusikika ya dhana inayozungumzwa

Ø Mjalizo

Ni kuunganisha maneno yanayofwatana bila kutumia viunganishi mfano: bila kutumia “na, kwa” n.k. Mfano:  Nilikaa, nikashangaa, nikachoka

                  Niliimba, nikanuna, nikacheka

Ø Mdokezo

Hii ni mbinu ya kisanaa ambapo mwandishi anaukatiza usemi fulani na kumuacha msomaji. Aghalabu pana vielekezi vinavyoweza kumsaidia msomaji katika kukamilisha.

Mfano:     wimbo la mauaji limezidi

              Mashaka…ah! Shida tupu

              Maneno…tena anyway…

              Labda tusubiri.

Ø Tashtiti 

Ni matumizi ya maswali ambayo majibu yake kwa kawaida yanakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa yameeleweka. Swali hili linakuwa kwa ajili ya msisitizo tu au mshangao.

Mfano:  Mtu anayemfahamu amekufa anauliza

               -Adela ameachana nami?

          Au mtu anayemfahamu amekutembelea

           - Jamani hata Luiza naye kaja?

           -Aisee ni wewe?

Ø Usambamba

Ni takriri ya sentensi au kifungu vya maneno vyenye kufanana kimaana au kimuundo. Usambamba huonekena sana katika ushairi simulizi

Shabaan Robert amekitumia kipengele hiki mara kwa mara atika mashairi yake katika shairi lake “kinyume” anasema

          Tulifululiza mwendo lakini sana twasita

          Tulikwenda kwa mshindo lakini sana twanyata

Katika mistari yote miwili wazo linalosisitiza ni moja maneno tu ndiyo yanabadilika uwezo wao wa zamani katika utendaji mambo unalinganishwa na udhaifu “wao” wa sasa.

c)     Taswira au Picha

Dhana hii hutumiwa kueleza neno, kirai au maelezo ambayo yanaunda picha fulani katika akili ya msomaji. Taswira zinaweza kuwa za kimaelezo (yaani maelezo fulani yanaunda picha) au za ki-ishara (zinazounda picha ambayo inaashiria jambo fulani au imeficha ujumbe mwingine). Taswira huweza kuundwakwa matumizi ya tamathali za semi hasa tashbiha na sitiari.

Kimsingi taswira nyingi ni taswira za uoni (yaani zinamchochea msomaji kuona picha fulani)

Mfano:     Neno lenye mzunguko, halipatikani mwisho,

          Wa huku hafiki huko,wala halina matisha.

              Halishibishi huchosha, wala hapati utuvu,

              Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka.

 

              Na milima akapanda, apendako akafika,

              Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,

              Na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dinani

              Hupati kupenda bara, na hushuki baharini

              Tazama mashaka gani, njia ya dira si njia

Katika shairi hili tunapewa picha tatu mahususi picha ya kwanza ni neno linalozunguka mshairi anatuambia kuwa neno ambalo halifuati njia iliyonyooka neno lenye mzunguko halifiki mwisho wake na halileti mradi uliokusudiwa “Halina malisho”

Hapa neno limefanya kuwa kitu chenye uwezo wa kutembea na kuzunguka

 

Picha ya pili ni ya mtu aendaye safari ngumu kwa ujasiri na moyo wa dhati akipanda milima na kushuka na mabonde akipenya misitu na kuvuka mito hadi kufika kule anapokwenda. Huyu ni mtu asiyeogopa matatizo anayeshikilia njia ngumu lakini nyoofu, alimradi anajua kuwa itamfikisha kwenye lengo lake. Ni mtu anayepamana na matatizo badala ya kuyakimbia mtu wa kwenda njia iliyonyooka

 

Picha ya tatu ni dira, dira ni chombo kitumiwacho na mabaharia na wasafiri wengine kusahihisha majira yao, wasipotee njia. Dira ni chombo cha mviringo na mshale wake aghalabu huzungukia palepale ulipo, katu hautoki nje ya dira. Picha hii inasisitiza wazo la mwandishi kuwa njia yenye kuzunguka haiwezi kumfikisha mtu kwenye lengolake. Mshale wa dira huzunguka daima lakini haufiki kokote.

Picha hizi tatu kwa pamoja zimefaulu kufikisha ujumbe wa mwandishi kuhusu maisha na namna ya kuyakabili tuyakabili kwa juhudi na ujasiri na nia.

JINA LA KITABU

Jina la kitabu ni vyema liwiane na yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Mfano: “Fungate la uhuru” (1988) jina hili linawiana vipi na yale yaliyomo ndani ya kitabu hicho?

PICHA YA JALADA KATIKA UCHAMBUZI

Kazi ya kifasihi kuwa na picha au michoro fulani kwenye majalada yao. Inawezekana majalada hayo yakawa na uhusiano fulani na dhamira na maudhui ya kazi zinazohusika. Picha hizi huweza kuwa kielelezo muhimu cha fani kwenye uchambuzi wa kazi ya kifasihi. Hata hivyo si kazi zote za kifasihi ambazo zinaonyesha uwiano kati ya majalada yake na yaliyomo.

 

UHAKIKI WA VIPENGELE VYA MAUDHUI

Maudhui katika mashairi hupatikana baada ya mhakiki kupitia beti zote za shairi lile ili kupata ujumbe wa shairi lazima itambidi mhakiki ajumlishe yaliyo katika beti mbalimbali za shairi lile.

Kwa ufupi katika ushairi uchambuzi wa maudhui mhakiki anapaswa kuangalia:

Ø DHAMIRA

Ni wazo kuu katika kazi ya fasihi.

Ø UJUMBE

Ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazifulani ya fasihi.

Ø FALSAFA YA MWANDISHI

Ni wazo ambalo mtu anaamini lina ukweli fulani unaitawala maisha yake.

Ø MSIMAMO WA MWANDISHI

Ni hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili linaweza kuwa halikubaliki na wengi, lakini yeye atalishikilia tu.

Ø MTAZAMO WA MWANDISHI

Ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe

 

 

 

 

 

HATUA ZA UCHAMBUZI WA USHAIRI

Katika uchambuzi huu wa vitendo, kielelezo tutatumia shairi la “Wauwaji wa Albino wapigwe vita” Shairi hilo linasema hivi:

Kwa kweli inashangaza, ni mambo hufikirika,

Ukijaribu kuwaza, wenzetu wanatutukana

Albino wanaweza, kifo kimeshawafikia

Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

 

Ni unyama wa kuzidi, albino kuwashika

Huu wote ni ukaidi, utajiri kuusaka

Tena ni kwa makusudi, maovu umeyashika

Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

 

Mikononi wanawakata, kwa mashoka na mapanga

Kuwasema sita sita, huu wote ni ujinga

Kwa vitisho wajikita, kusikiliza waganga

Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

 

Albino tuwalinde, wamekuwa almasi

Wasakwa kila upande, sababu ya ibilisi

Yatupasa tuwalinde, binadamu kama sisi

Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

 

Majumba kuyabomoa, pande zote kuzunguka

Damu isiyo hatia, kwa wingi inamwagika

Mola inamlilia, hukumu ipo hakika

Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

 

Albino ni wenzetu, uzao wao ni halisi

Acha tofauti zetu, tena tuwape nafasi

Tujenge taifa letu, tuuache ukakasi

Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

 

 

Ujinga na upumbavu, kuwaua albino

Wajawa maumivu, mikono na visigino

Sahitaji utulivu, upole mshikamano

Ni wauwaji wabaya, vikali walaaniwe.

 

Zamu yako inakuja, mwisho wao utafika

Wenyewe watajitaja, tena bila ya mashaka

Sote tuwe na umoja, kufungua mashtaka

Kuwasaka wauwaji, kusudi wahukumiwe.

 

HATUA ZA KUCHAMBUA SHAIRI

1.     Lisome shairi zima toka manzo hadi mwisho ili upate picha ya jumla, kimaana na kiumbo ya shairi hilo. Katika hatua hii kama shairi ni gumu linaweza lisieleweke, kwa bahati shairi la “wauwaji wa albino wapigwe vita” linaeleweka bila tatizo

2.     Rudia kulisoma tena shairi hilo polepole, andika maana ya jumla unayoipata. Unaweza kupata maana zaidi ya moja katika “Wauwaji wa albino wapigwe vita” maana ya jumla inayojitokeza ni maombolezo ya mauwaji ya Albino

3.     Huku ukiwa na kalamu yako ya risasi, rudia kulisoma tena shairi hilo mstari baada ya mstari. Pigia kila neno usemi, sentensi au kipengele kinachoelekea kuwa na umuhimu au dhima maalumu ya kifani au kimaudhui.

Katika shairi ili pengine utayapigie mstari mafungu ya maneno yafuatayo:

          -Albino wanaweza kifo kimeshawafikia

          -Ni wauwaji wabaya vikali walaaniwe

          -wasakwa kila upande sababu ya ibilisi

          -damu isiyo hatia kwa wingi inamwagika

          -Albino ni wenzetu uzao wao ni halisi

4.     Jaribu kufanya kisisisi maneno hayo yalyopigiwa mstari au kuorodheshwa katika hatua ya tatu bila shaka yapo mambo ambayo undani wake hutauelewa katika hatua hii, hivyo aghalabu itabidi

a)     Urejee mambo hayo yalivyotumika

b)    Urejee katika muktadha wa shairi hilo kama una ufahamu kwa upande wa wauwaji wa Albino wapigwe vita, muktadha huo ni mauaji ya Albino

Jiulize semi, sentesi hizi zinasema/zinaonyesha au zinadokeza nini? Kwa nini mtunzi kaamua kutumia maneno hayo na si mengine? Je yanahusiana vipi na maana ya jumla uliyopata katika hatua ya pili.

5.     Chunguza vipengele vingine vya kisanaa na kimuundo alivyovitumia mtunzi. Jiulize kama vinaoana na madokezo ya maana uliyoyapata katika hatua ya nne. Vipengele unavyoweza kuchunguza katika hatua hii ni muundo wa shairi, vina, mizani, wizani, takriri, milio ya maneno, tamathali n.k. kwa mfano hadhihirika kuwa muundo wa shairi ni kijadi ambao hautuambii lolote kuhusu maana ya shairi hili vifanye uchambuzi vipengele vya kisanaa ulivyovipambanua

6.     Husisha ufafanuzi wake hadi hatua hiina maana ya shairi iliyokwisha kujitokeza kuona kama mambo hayo yanaoana barabara au bado kuna pengo au mkinzano.

Baada ya hatua hii utakuwa umepata maana kamili ya shairi ambayo unaweza kuitetea kifasihi kwa kurejea katika shairi lenyewe si lazima maana unayopata/unazopata ioane/zioane na maana watakazopata wengine jambo muhimu ni kuwa na ushahidi wa kutosha kuweza kutetea hoja zako.

Maana ambayo umepata hadi sasa yaweza kuelezwa iwe:

Mshairi anaomboleza mauaji ya Albino ambayo yanafanywa na  watu mbalimbali kwa Imani za kishirikina anaonyesha kuwa kuua binadamu wenzetu ni unyama na ni ukatili. Anamwomba Mungu awaepushie Albino na mates ohayo.

7.     Hadi hatua hii umepata maana ya shairi lakini bado hujapata maudhui yake. Ili kupata maudhui unatakiwa upambanue dhamir kuu ya/za shairi hili na uonyeshe mtazamo wa mshairi kuhusu dhamira hizo. Katika shairi hili ni dhahiri dhamira kuu ni “Mauaji ya Albino” mtunzi anasawiri tukio la mauaji ya Albino mwandishi anaonyesha kuwa mauaji ya albino ni tukio lenye kuleta majonzi na kilio. Mtazamo wake kuhusu mauaji ya Albino ni kwamba wanaofanya hivyo hawana utu hivyo ni sawa na wanyama wa porini na anaonyesha kuwa kuwaua albino ni kinyume cha utu

Mtunzi anazungumzia pia dhamira ya ujinga. Mwandishi anaonyesha kuwa ujinga ni kikwazo cha maendeleo ya jamii kwani wote wanaojihusisha na mauaji ya albino ni wajinga na wanataka kupata utajiri kwa njia za mkato.

8.     Katika hatua hii mchambuzi ana uhuru wa kuithamini kusifu au kwaani. Baada ya kulichambua na kulielewa vizuri shairi hilo katika hatua saba zilizotangulia sasa unaweza kulitolea tathmini ya kifani na kimaudhui katika kufanya tathmini ni muhimu kuzingatia muktadha wa wakati lilipotungwa na wakati wa leo.

Tathmini yako itazingatia muktadha yote miwili unaweza kusema kuwa, shairi hilo lilipotungwa ulikuwa na umuhimu wake leo labda umepungua kwa kuwa muktadha huo wa vifo vya Albino umepita. Hata hivyo labda shairi limebaki na umuhimu wa kihisia na kifalsafa kuhusu tatizo la maisha na mauti na ufumbuzi wake.

 

HISTORIA NA MAENDELEO YA KISHAIRI WA KISWAHILI

Wataalamu wengi wanakubali kuwa ushairi wa Kiswahili ni tungo simulizi hasa ngoma na nyimbo. Kabla ya karne ya 10 BK ushairi wa Kiswahili ulikuwa ukitungwa na kugharura kwa ghibu bila kuandikwa.

Kuanzia mwaka 1000 B, mambo mawili yaliletwa na kuathiri ushairi, mambo hayo ni Dini ya kiislamu na Uandishi wa hati ya kiarabu waswahili wengi walijifunza kusoma na kuandika hati za kiarabu, hali hiyo ilienda sambamba na ustawi wa miji ya Pwani katika biashara na majengo ya mawe mashujaa mashuhuri wa miji ya Pwani wanokumbukwa katika tendi na masimulizihuenda waliishi katika hicho ni Fumo Lyongo wa Shangapate kaskazini mwa upwa wa Kenya kati ya karne ya 8 na 9

Katika kipindi hiko washairi wengi walitunga mashairi mengi kwa ghiba kwa sababu hayakukusudiwa kuhifadhiwa kwa maandishi kwa kipindi kirefu ni tarihi na baadhi ya mswada hiyo imepotea. Tungo zilizosalia ni Fumo Lyongo ambayo ilandikwa 1500 BK kutoka katika mapokeo ya mdomo.

-“kumswifu” yanga au suifa ya mwana ning utingo wa mwanzo kuhifadhiwa kwa maandishi.

Mwaka 1500-1700 BK kulikuwa ni kipindi cha uvamizi wa maneno katika kipindi hicho tungo chache zilihifadhiwa zikiwasifia maneno mashairi yaliyo wasifia wareno> mfano

·        mzungu mgeli} 1630 nukuu ya baadhi ya vipande vyake;

Mzungu mgeli u mwongo,

Mato yako yana chongo,

Kwani kuwata  mpango,

Kwenda kibanga uwani?

Lakini tungo mashuhuri za wakati huo ni:

·        Utendi wa Hamziyya (Seyyid Aidamis bin Athumani 1652)

·        Siri lasirari (Binti Lamba 1668)

·        Utendi wa Tambika (Taboka) {Mwango bin Athumani 1728}

·        Hamziya ni tafsiri ya utendi wa kiarabu kuhusu maisha ya Mtume Muhamadi

 

1750-1900 kipindi cha waarabu

Sehemu kubwa za tendi mashuhuri za wakati ambazo mpaka leo zipo ni:

·        Tendi za dini na vitu

-         Utenzi wa Shufaka

-         Utenzi wa masahibu

-         Utenzi wa kijamaa

-         Utenzi wa mayasa na mikidadi

-         Utenzi wa Ras L Ghuli (unahusu vita vya waarabu kati ya waislam na makafiri-{1855})

·        Tungo za kitamaduni, mawaidha na Tumbuiza

Tungo hizi zilikuwa nyingi na zilikuwa katika maandishi na zilihusu (maudhui yake) kueleza mandhari ya Afrika Mashariki mfano tungo hizi ni:

-         Utenzi wa Inkishafi (1810)

Mtunzi: Seyyid Abdallah bin Nasri.

Utenzi huu unazungumzia matokeo ya uvamizi wa waarabu na wareno ambapo matokeo yake ni kuporomoka kwa mji wa Pate.

Ø Utenzi wa Mwana kupona (1858)

Unahusu utamaduni na misingi ya Dini. Utenzi huu uliandikwa kama wosia kwa binti yake na kwa kiasi kikubwa unahusu unyumba pia ndani yake kuna mafundisho ya unyago kwa watu wa Pwani.

Kundi jingine kubwa ni mashairi ya siasa kundi hili liliwakilisha/lilisimamiwa na akina Muyaka bin Haji wa Mombasa. Huyo alitunga mashairi ya kupinga waarabu wa Oman mfano;Suid bin Said (1810-1876),Kibabina (1776-1834) na wengine.

Wote hawa walitunga mashairi yaliyohusu harakati za kisiasa na kijamii za wakati huo, wa baadhi yao walifungwa au kuuwawa gerezani kwa sababu ya kupinga kutawaliwa. Mchango mkubwa wa hawa ni kuendeleza mashairi ya unne (tarbia)

Kwa ujumla katika kipindi hiki mambo yaliyojitokeza katika maendelezo ya ushairi ni manne:

Ø Umbo la tarbia (unne) ulifika kilele

Ø Utendi

Ø Kanuni ya utunzi ziliwekwa wakati huo

Ø Hati ya maandishi (Kiswahili n kiarabu) ilisanifiwa kuzingatia sauti za lugha ya Kiswahili.

1885-1918 USHAIRI WAKATI WA UKOLONI WA KIJERUMANI

Ushairi wa wakati huo unaweza kugawanyika katika makundi matatu.

*    Ushairi wa kawaida-mashairi haya yalihusu mawaidha, mapenzi na dini.

*    Ushairi wakusifu wakoloni- huu uliandikwa kwenye magazeti na vitabu mfano kitabu maarufu cha Dr. C,kinachoitwa Velter (1907) Prose and Poesie der Sua heli .Kitabu hiki kilisifu utawala wa kidachi

Ø Ushairi wa upinzani.

Ushairi huu ulipinga utawala wa kikoloni.

Mfano: utenzi wa vita vya wadachi (H.Abdallah)

Ø Utenzi wa vita vya majimaji

Katika kipindi hiki mambo matatu yalitokea katika ushairi kwa upande wa Tanzania.

*    Kuandika kwa kutumia hati ya kirumi hati hii ulienea kwa kupitia Elimu kanisa na ilianza kutumiwa na watunzi baada ya hati ya kirabu

*    Utafiti kuhusu ushairi ulianza wakati huo na wachambuzi maarufu walikuwa C.Velter Buttner na K.Mein holf n.k

*    Hawa walisaidiwa na waafrika kama vile Mohamed Kajunwa, utenzi wa Fumo Lyongo Rev.Taylor ndiye aliyekusanya mashairi ya Fumo Lyongo.

1918-1961 UKOLONI WA KIINGEREZA

Kipindi hiki kiliambatana na mambo matatu mapya:-

a)    Elimu .Hii ilieneza lugha ya Kiswahili na ushairi katika maeneo ya bara kupitia shuleni maarifa ya kusoma na kuandika. Hati ya maandishi ya kirumi ilienea kupitia elimu

b)    Kuanzishwa kwa mashirika ya uchapishwaji.Katika kipindi hiki magazeti mengi yalichapwa kwa lugha ya Kiswahili na kusambazwa. Baadhi ya magazeti yalikuwa na kurasa maalumu ya ushairi ambapo ulisaidia kuwakutanisha watunzi kutoka Afrika Mashariki.

Mfano: Gazeti la “Mambo leo” 1923 kupitia gazeti hilo watunzi maarufu kama S.Robert, Mdanzi Hamasa, Mzee Waziri (kijana) walipata umaarufu kupitia mambo leo

Pia kuanzishwa kwa shirika la wachapishaji vitabu Afrika Mashariki (E.A.L.B) kulisaidia sana kukuza na kueneza Sanaa ya ushairi.

c)     Shughuli za siasa za kudai Uhuru ziliibua ushairi wa kisiasa mnamo mwaka 1950-1960.

Mfano: S.Kandoro alitunga mashairi mengi pia kipindi hicho ushairi ulikuwa wa aina.

1.     Mashairi yaliyosawili mfumo wa uchumi wa kikoloni. Mfano Matatizo ya kazi, umanamba, mshahara mdogo n.k haya yote yalitolewa na gazeti la mamba leo.

2.     Mashairi yaliyohusu utaifa yalianza miaka 1930. Haya yalijiuliza mwafrika ni nani? kwa nini mzungu yupo hapa?

Mfano:  S.Robert- mashairi ya kutetea weusi mfano Shairi la Rangi zetu,S.A.Kandoro kwetu ni kwao kwa nini?

 Pia kulikuwa na mashairi ya kutetea Lugha mfano S.Robert (Titi la mama li Tamu)  S.Kandoro (Kitumie Kiswahili)

3.     Mashairi ya kisiasa ambayo yalihimiza watu waungane ili waweze kujitawala wenyewe mfano,S.Kandoro shairi la siafu wamekazana

4.     Pia kipindi hiki walitokea wachunguzi wengi sana wa ushairi wa Kiswahili.

Mfano:     Withchens (1930), A.Wine, B.E.Damman (1930-50) Lumbart, H.Cory W.Whitely n.k. “wazungu”. Waafrika Sr. Mbarak Hisway, Hamis Kitumbe

 

USHAIRI BAADA YA UHURU

Baada ya uhuru ushairi ulisambaa zaidi kutokana na msukumo wa kisiasa fani mpya mfano Ngonjera na mtiririko au tungo huru zilizanziashwa ili kuzingatia mahitaji mapya ya kisiasa na kisanaa. Ushairi wa Kiswahili baada ya uhuru ulikuwa wa aina kuu mbili

v Mashairi ya kawaida: Haya yalitungwa sana magazetini na vitabu vya mashairi mbalimbali vilichapishwa ambapo Dhamira za malezi, mapenzi , dini, mawaidha n.k.

o   Akilimali snow- white

o   Mwinyi khatibu- Mohamed

o   Andanenga

o   S.Kandoro

o   S.Robert

1.     Mashairi ya kisiasa: Hapa kuna makundi mbalimbali ya mashairi ya kushangilia Uhuru.Mfano: Utenzi wa uhuru wa Tanganyika,Utenzi wa jamhuri wa Tanzania, Utenzi wa uhuru wa Kenya.

a)     Mashairi yanayojadili dhamira ya ujenzi wa jamii mpya. Katika mashairi yao walisisitiza watu wafanye kazi ili kuinua pato.

Mfano: S.Kandoro katika shairi la kujitawala,J.K.Nyerere-chombo cha taifa letu

b)    Mashairi ya Ujamaa

Hayo yalitokea baada ya Azimio la Arusha ambalo yalisisitiza siasa ya ujamaa na kujitegemea, ambapo walipinga unyonyaji, ukupe, ukabila na ubepari. Walitukuza kilimo na kuwashawishi watu kurudi shamba (kijijini)

Mfano: Mashairi ya Azimio la Arusha (kamaji), Ngonjera za Matias Mnyapara, Mashairi ya miaka 10 ya Azimio la Arusha (    Abdulah)

Tatizo kubwa lilijitokeza katika hiki ni ukasuku ambapo waandishi wengi walikariri hotuba za viongozi bila kuzifanyia uchambuzi na kuziandikia mashairi.

c)     Mashairi yaliyohakiki siasa iliyokuwepo na hawa walikuwa na mitazamo mbalimbali.

·        Wanauhalisia

Walihakiki dhana ya ujamaa na ukombozi na kuchambua mafanikio ya matatizo yake hasa katika utekelezaji wa malengo ya Azimio la Arusha. Waandishi hao ni E.Kezilahabi, E.Husein, Z.Mochiwa na T.A.Mvungi.

·        Washairi wa Mlengo wa kushoto

Hawa walikuwa na mambo yafuatayo walichukua msimamo wa kufanya kazi na mkabala wa kitabaka katika kutolea tungo zao

·        Waliona usoshalisti  kama suluhisho la matatizo yao.

             Ili usoshalist upatikane waliona ni lazima kumwaga damu (kutumia nguvu). Kundi hili lilikuwa  na K.Kahigi, na M.Mulokozi, Ally Salehe, M.S.Khatibu, A.Abdullah na S.A.Mohamed.

Hivyo Sanaa hii ambayo ilianza upwa wa Kenya na Tanzania katika karne ya 10-15 sasa imeenea Afrika Mashariki nzima hadi Rwanda, Burundi na Kongo

 

 

 

MGOGORO KUHUSU USHAIRI WA KISWAHILI

Mgogogro huu ulianza mwisho mwa miaka ya sitini (1968) na mwanzoni mwa miaka ya sabini. Mgogoro ulihusisha pande mbili yaani washairi wa kimapokeo (wasiokubali mabadiliko hawa walisisitiza kuwa vina na mizani ni uti wa mgongo wa shairi la Kiswahili)  lakini wanamabadiliko waliona kuwa si lazima shairi liwe na vina na mizani.

Sababu kuu zilizozua utata ni mbili

v Maana ushairi kwa ujumla

v Maana ya shairi la Kiswahili

Mvutano huu unahusisha na mabadiliko ya kidunia yaliyotokea miaka ya Sitini na Sabini katika Nyanja mbalimbali za maisha hata kupelekea washairi nao kuhitaji mabadiliko katika tasnia ya ushairi kwa upande wa fani.

Msukumo huu wa kuleta mabadiliko katika tasnia ya ushairi uliletwa na wanazuoni akina E.Kezilabahi, Jared Angira na E.Husein wasomi hawa walijishughulisha na utunzi wa mashairi hivyo baada ya kusoma fasihi za nchi mbalimbali waligundua kuwa vina na mizani ni wazo lilizofuatwa na washauri wote duniani hivyo waliamua kuasi sharia hizo ili kuleta mabadiliko ya kuondoa minyororo iliyowafunga kuhusu utungaji wa shairi la Kiswahili kwa pamoja waandishi hawa waliweza kutunga mashairi mengi au tungo zisizofuata ruwaza ya vina na mizani na pia waliungwa mkono na watunzi wengi kama vile M.M.Mulokozi, K.K.Kahigi miaka ya themanini washairi wengi waliibuka kuungana na kundi hilo. Mfano: Henry Mhanika  na T.Mvungi.Madai ya wana mabadiliko kutunga tungo zao yalikuwa kama ifuatavyo:

v Mbinu na njia za kutunga mashairi ya Kiswahili zilikuwa chache mno.

v Kutunga kwa kufuata taratibu za muundo wa tungo za Kiswahili (mapokeo) kuliwanyimia uhuru walidai kuwa hakuna sharia za utunzi wa mashairi katika (diwani ya Amri) (sharia za kutunga mashairi).

v Muundo wa tungo zao zisizofuata kaida ni wa kiasilia. Hii ina maana kuwa ushairi wa mwanzo haukuwa na mizani wala vina.

Kwa  maana  nyingine  kuwa mgogoro huo ulijitokeza baina ya wazee akina Kuluta Amri,Saadam Kandoro, Ustadhi, Andanenga, n.k na vijana akina E.Kezilahabi.

 

 

 

 

 

MADA NDOGO ;KUHAKIKI  RIWAYA

Riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni yenye mawaidha, lugha ya nathari, mchanganyiko wa visa, wahusika kadhaa na matukio yaliyosukwa kimantiki yenye kufungamana na wakati na kushabihiana na maisha halisi.

 

SIFA ZA RIWAYA

1.     Urefu, Riwaya kwa kawaida huwa ndefu ikilinganishwa na tanzu nyingine za kinathari kama vile hadithi fupi. Mfano wa Riwaya ya Bwana Mnyombokera na Bibi Bagomoka (198 ) iliyoandikwa na Kiterezi, Hii ina mamia ya kurasa

2.     Matukio,Riwaya humulika hali halisi ya maisha ya binadamu ingawa matukio ya riwaya si lazima yawe ya kweli yametokea, yanaweza kupatikana katika ulimwengu halisi wa binadamu matukio kama vile rushwa, wizi wa mali ya umma, matabaka, uongozi mbaya, athari za pesa katika ndoa na mapenzi na tatizo la usafiri Dar-es-salaam katika “Pepo ya mabwegwe” (1981) iliyoandikwa na Mwakyembe, mambo yaliyoandikwa yamo katika jamii yetu kwa sasa.

3.     Muundo,Riwaya huwa na miundo changamano ukilinganisha na kazi nyingine za kinathari. Riwaya inaweza kua na muundo wa msago, rejea au rukia, wakati mwingine inaweza kuwa na muundo changamano yaani inakuwa na muundo miwili katika kazi moja.

4.     Mandhari yake ni pana

Mandhari ya riwaya ni mapana na kikamilifu kwani riwaya hushughurikia mawazo mengi, hujishughulisha na vipengele vingi vya maisha ambavyo hupatikana katika nyakati na mahali tofauti kama vile shuleni, mijini, vijijini, nyumbani, barabarani n.k. ili kushughulikia mazingira mapana mwandishi hutumia kipindi kirefu cha wakati ikilinganishwa kazi nyingine kama vile hadithi fupi ambayo huweza kuchukua kipindi kimoja tu kukuamilika.

5.     Wahusika ,Wahusika wa riwaya ni wengi na waliokuwa zaidi. Riwaya hushughulikia masuala mengi huwa na wahusika wengi wanaomwezesha mwandishi kukidhi haja hiyo kuna wahusika wanaobadilika kwa lengo la kuonyesha hali halisi ya maisha kuna wale wasiobadilika ili kutumiwa kukashifu au kuhimiza hali fulani n.k. Riwaya ya Ziraili na Ua la faraja na Mkufya na Makuadi wa Soko Huira iliyoandikwa na Chacha Gezina wahusika wengi.

6.     Mtindo,Riwaya hutumia mtindo wa wasimulizi, monolojia au dayolojia na nafsi zote tatu. Mwandishi anaweza kuwa ndiye msimulizi au mhusika fulani akawa ndiye anayesimulia au wahusika wakawa wanajibizana wao kwa wao.

Mfano: Njama (1981), Uchu (2000), Kikosi cha Kisasi(1979) vya musiba ametumia zaidi mtindo wa monolojia na dayolojia kidogo.

 

AINA  ZA RIWAYA

Kuna michepuo miwili ya riwaya  ambayo ni;

A.   RIWAYA YA DHATI

Riwaya dhati ni riwaya yenye kuchambua masuala mazito ya kijamii, kutafuta sababu zake athari zake na ikiwezekana ufumbuzi wake. Ni riwaya inayokusudiwa kumkera na kumfikirisha msomaji, sio kumstarehesha mtu.

 

MATAWI YA RIWAYA YA DHATI

1.     Riwaya ya kijamii

Ni riwaaya inayosawiri maisha na matatizo ya kawaida ya jamii. Matatizo haya huweza kuwa ya kifamilia, kiuhusiano wa kitabaka ya kisasa ya kiutamaduni n.k. Utanzu huu ndiyo wenye idadi kubwa zaidi ya riwaya.Mfano:

*    Shabaan Robert “Siku ya watenzi wote” (1968)

*    M.S.Moamed “Nyota ya Rehema” (1978)

*    S.A..Mohamed “Dunia mti mkavu” (1980)

*    E.Kezilahabi “Rosa mistika” (1971)

*    J.N.Somba “Alipanda upepo Akavuna Tufan” (1969)

*    Alex Banzi “Titi la mkwe” (1972)

2.     Riwaya ya kisaikolojia

Ni riwaya inayododosa nafsi ya mhusika, fikra, hisia, mawazo, Imani, hofu, mashaka na matumaini na matamanio yake binafsi na athari za mambo hayo kwake binafsi na labda jamii yake. Baadhi ya watunzi waliojipambua katika utanzu huu ni

*    E.Kezilahabi “Kichwa maji” (1974)

*    M.S.Mohamed “Kiu” (1972)

*    S.A.Mohamed “Tata za Asumini” (1990)

*    K.G.Mkangi “Ukiwa” (1973)

3.     Riwaya ya kitawasifu

Ni riwaya ambayo husimulia habari za maandishi tangu kuzaliwa kwakwe hadi pale inapokomea au hadi kufa.Mfano:

*    Shabaan Robert “Maisha Baada ya miaka Hamsini” (1966)

*    Maisha ya Hemed Bin Muhamed “Tipu Tipu” (1950)

4.     Istiara

Ni riwaya ya mafumbo ambayo umbo lake la nje ni ishara au kuwakilisha tu cha jambo jingine.Mfano:

*    Riwaya ya Nathanuel Swift (1926)

*    Safari za Gulliver (Mfasiri F.Johnson) (1945)

*    Shamba la wanyama (Msafiri F.Mkwegere)

Ni ishara ya mfumo wa utawala wa dikteta wa kisovieti wa enzi za Staliri. Yaelekea pia riwaya Shabaan Robert (1951) kusadikika ni ishara kuhusu utawala na mabavu wa kikolono.

5.     Riwaya ya kigano

Ni riwaya yenye umbo la mtindo wa ngano mathalani huweza kuwa na wahusika wanyama, visa vya ajabu ajabu, mandhari ya kubuni na visa vyenye kutendeka nje ya wakati wa kihistoria.

Mfano:    -Shabaan Robert (1952) “Adui na nduguze”

             -J.K.Kimbila (1966) “Lila na fila”

6.     Riwaya teti

Ni riwaya inayosimulia vituko na masahibu ya watu, wapuuzi, walaghai, wajanja na kwa njia inayosisimua na kuchekesha. Aghalabu hao huwa ni watu wanaovutia wa tabaka la chini na bapa. Matukio ya Riwaya hii hayana msukumo ulioshikamana vizuri shabaha yake mojawapo ni kuziteta na kuzikejeli tabia za matabaka na watu mbalimbali katika jamii.

Mfano:    Hadithi za “Hekaya za Abunuasi na Hadithi nyingine (1915) imefanana na vituko vya riwaya teti.

7.     Riwaya ya wasifu

Ni riwaya inayoandikwa na mtu mwingine kuhusu maisha ya mtu mwingine tangu kuzaliwa hadi kufa kwake.Mfano:

*    J.Makabarah “Maisha ya Salum Abdallah” (1975)

*    S.Robert “Wasifu wa Siti bint Saad” (1967)

8.     Riwaya chuku

Ni riwaya ya vituko na masaibu yasiyokuwa ya kawaida ni riwaya isiyozingatia uhalisia mara nyingi masaibu ya Riwaya chuku huambatana na mapenzi, mfano; baadhi ya hadithi za Alfu-lela-Ulela (1929) ni chuku katika fasihi ya Kiswahili. Riwaya za Shabaan Robert za “Adili na Nduguze” (1952) na “Kusadikika” (1951) zinaingia katika kundi hili.

9.     Riwaya ya kihistoria

Hii huchanganya historia halisi na Sanaa kwa makusudi ili kutoa maudhui fulani. Mara nyingi riwaya hii hujikita kwenye matukio makuu ya kihistoria yalioathiri mwenendo na mwelekeo wa jamii au taifa linalohusika na historia ya kubuni, matukio ya kweli na ya kubuni. Hata hivyo riwaya hiyo inazingatia zaidi namna matukio makuu ya kihistoria yalivyomwathiri na yalivyoathiriwa na matendo ya mtu binafsi aliyeyashiriki baadhi watunzi mashuhuri wa riwaya za kihistoria niMfano: 

*    Olef Msewa “Kifo cha ugenini” (1977)

*    M.Karuthi “Kaburi bila msalaba” (1971)

*    S.A.Shafi “Kuli” (1979)

*    A.Lihamba “Wimbo wa Sokomoko” (1990)

*    B.Mapalala “kwa heri iselemaguzi” (1992)

*    G.Ruhumbika “Miradi Bubu ya wazalendo” (1992)

10.                      Riwaya ya kimaadili.

Ni riwaya inayowapa watu maadili mema na wengine maadili hayo ni ya kidini wausika wanakuwa na sifa za kudumu kama vile upendo wa ukarimu.Mfano:   

*    Shabaan Robert “Adili na Nduguze” (1952)

*    M.Mnyapala “Mrina Sali na wenzake wawili” (1961)

*    G.Mhina “Mtu ni Utu” (1971)

11.                      Riwaya ya kimapinduzi

Ni riwaya inayojadili matatizo ya kisiasa katika jamii. Riwaya hii ni mwelekeo fulani wa kuleta mabadiliko ya kisiasa katika jamii.

Mfano: wa riwaya hizi ni “kuli” (1978), Kabwela (1978), Mzalendo (1977) Ubeberu Utawashinda (1971) n.k.

12.                      Riwaya ya kifalsafa

Ni riwaya zinazojadili migogoro ya kimaisha kifalsafa. Riwaya hizi hujuliza maswali kama vile

·        Ukweli ni nini?

·        Maisha ni nini?

·        Kifo ni nini?

·        Kuwepo na kutokuwepo ni nini? n.k

Muundo wa riwaya hizi ni wa kimchangamano au a mviringo na wahusika huvunjwa vunjwa hivyo mhusika wa riwaya hizi ni wazo tu au hawapo kabisaMfano:    

·         E.Kezilahabi- “Nagona” (1987) Mzingile (1991)

·        S.Mohamed- “Kiza katika nune” (1988)

·        K.G.Mkangi- “Mafuta” (1984) n.k

13.                      Riwaya Barua

Ni riwaya ambayo sehemu yake kubwa husimuliwa kwa njia ya barua wanazoandikiana baadhi ya wahusika.Mfano:   

*    Mariam Ba “Barua ndefu kama hii “(1980) Msafiri Maganda

*    Walter Tribisch “Nampenda mvulana. Barua ya siri” (1964)

14.                      Riwaya ya vitisho

Ni riwaya yenye visa vya kutisha na kusisimua damu mara nyingi visa hivyo huambatana na mambo ya ajabu au miujizaMfano: 

*    C.Mung’ong’o “Mirathi ya Hatari” (1977)

*    N.J.Kuboja mbojo Simba-mtu (1971)

 B ) RIWAYA PENDWA

Ni riwaya iliyokusudiwa kuwastarehesha na kuburudisha msomaji tu lengo hili kulihimiza kwa kusawiri visa na vituko vya kusisimuwa damu

Mfano: Vituko vya majambazi na uhalifu, ususi na mahaba ya waziwazi.

Riwaya pendwa huwa na mafunzo kidogo kama lengo la ziada katika Tanzania aina hii ya riwaya ililetwa kwa mara ya kwanza na Abdull alipoandika riwaya ya “Mzimu wa watu wa kale“ (1957/8) na miaka ya 1960

-          Katalambula (1965) simu ya kifo

 

SIFA ZA RIWAYA PENDWA

1.      Matumizi makubwa ya taharuki na utendaji

Taharuki hutumika kuelezea hamu kubwa anayokuwa nayo msomaji katika kujua yatakayotokea katika hadithi fulani. Taharuki hutokea pale ambapo msomaji ana hamu kubwa au anajua yanayoweza kutokea laikini hajui jinsi yatakavyotokea.

Riwaya pendwa ni riwaya ya taharuki kwa sababu ya kimsingi ya fani yake hujiweka katika mbinu ya kisanaa ya taharuki. Taharuki imepewa nafasi kubwa katika aina hii ya riwaya kwa njia ya vituko vya kusisimua vinavyojibainisha kwa njia ya mkingano iliyosukwa kwa namna ya ufundi usiokuwa wa kawaida.

Kwa upande wa utendaji wahusika wake n hodari sana katika kutenda, katika kuwindana, kupigana kwa silaha na mikono mitupu na kufanya matukio yake utendaji unaojitokeza humu unaziteka nafsi za wasomaji wake.

2.      Hutumia wahusika walewale.

Riwaya pendwa inasifa ya kutumia wahusika walewale hivyo ikawa na uwezo wa kujiendeza katika vijitabu kadhaa. Karibu kila mwandishi maarufu wa aina hii ya riwaya ameandika vitabu zaidi ya kimoja. Sifa hiyo ya kuwatumia wahusika walewale imefanya kijitabu kimoja katika mfuatano wa vitabu kadhaa vya mwandishi mmoja kionekane kama tukio linalojitegemea katika mfululizo wa matukio. Ili kuustawisha na kuwisisitiza mfuatano huo, baadhi ya waandishi wameweza hata kudondoa kazi za nyuma katika kazi zao za baadae mfano Abdallah “Kosa la bwana Musa”,Hofu (1988) musiba,Salamu Toka Kuzimu (1993) Mtobwa,Tutarudi na roho zetu?? (1987)

3.      Mhusika mkuu hupewa sifa zisizo za kawaida

Mhusika mkuu ameumbwa juu ya wahusika wengine anatawaliwa, hivyo ana sifa ya ubabe sifa ya kuwa kielelezo chenye ukamilifu, yaani kutokana na dosari.

Mfano:       Abdallah “ Kosa la Bwana Musa”

Mhusika mkuu ndiye mshindi hata apitapo katika taabu na mashaka ya aina gani tunajua hatimaye ni mshindi katika mambo yake. Wahusika hawa wakuu hutenda na kuendesha mambo yao kama miungu wadogo pasi na kukosea hata wakawa wasioaminika.

 

4.      Mandhari yake huundwa kwa namna ya pekee

Wasanii wa riwaya pendwa wanatumia mandhari ya kitanzania au kiafrika, lakini sehemu kubwa ya matukio ama imo ndani ya vichwa vya wasanii au filamu za upelelezi, uhalifu na mapenzi za kigeni.

5.      Upangaji holela wa matukio

Katika riwaya pendwa kuna upangaji wa haraka wa mtiririko wa matukio kiasi kwamba sehemu zingine zinakosa upatanifu na mantiki.

6.      Kuenzi jinsia ya kike kama chombo cha anasa na uhalifu.

Riwaya pendwa hua zina mapenzi ndani yake kana kwamba upelelezi au shughuli inayofanyika haiwezi kusisimua bila mapenzi, yaani hazina dawa, dawa ya kazi ni mapenzi.

7.      Hutumia lugha ya kila siku

Mara nyingi riwaya pendwa hutumia mitindo wa masimulizi na monolojia na kwa kiasi kidogo dayolojia. Lugha yake ni rahisi ya mazungumzo ya kila siku.

 

ATHARI ZA RIWAYA PENDWA

1.      Hudumaza vipaji vya waandishi wetu kwani huiga kila kitu.

Kazi hizi zinadhihirisha jinsi gani fasihi pendwa za kigeni pamoja na filamu zinaathiri waandishi wetu. Riwaya pendwa ni matokeo ya mwigo ambayo yameathiri uasili wa waandishi wetu katika ubunifu kimaudhui na kifani kazi hizi zinashindwa kabisa kudhihirisha umahiri wa waandishi wetu katika kubuni kazi na sanaa zenye mawazo yao wenyewe.

2.      Hufundisha majangili na wahalifu mbinu mpya katika shughuli zao za kufanya uhalifu.

Riwaya pendwa husababisha uhalifu katika jamii.Mfano: Athari mbaya za tamaduni za kigeni zinazokuja kwa njia ya filamu na riwaya pendwa ni kama vile kuzuka kwa makundi ya kiharamia hapa nchini ambayo yanavamia benki, baa, maduka na kuwaibia watu kwa kutumia silaha mbalimbali.

3.      Hazichambui kwa undani misingi ya matatizo ya jamii.

Riwaya hizi haziingi kwa undani katika misingi ya matatizo ya jamii kama kuna tatizo linalosababisha upelelezi je kiini chake ni nini? Riwaya hizi zinataja juu ya wivu, tamaa, uovu wa aina hiyo bila kuyahusisha vilivyo mazingira ya jamii (mfano filamu zinaitwa 24)

 

AINA ZA RIWAYA PENDWA

1.      Riwaya ya Mahaba

Ni riwaya yenye kusawiri uhusiano wa kimapenzi kati ya mvulana na msichana au mwanaume na mwanamke. Siku hizi zipo zenye kusawiri mapenzi haramu pia.Kwa mfano: Mapenzi baina ya watu wa jinsia moja (mashoga)

Mfano:        J.Simbamwene “Mwisho wa mapenzi” (1972),J.D.Kiango “Jeraha la moyo” (1974),S.M.Komba “Pete” (1978),J.Simbamwene “Kweli unanipenda” (1978)

2.      Riwaya ya Uhalifu/Ujambazi

Ni riwaya zinazosimulia vituko vya uhalifu. Mfano: wizi, ujambazi, uuaji, magendo, utapeli, n.k. Aghalabu polisi huhusishwa katika kuwasaka na kuwadhibiti wahalifu hao.

Mfano:J.Simbamwene (1972) “Kwa sababu ya pesa”,H.Katalambula (1975) “Buriani”,L.O.Omolo (1970) “Mtu mwenye miwani meusi”,S.J.Chadhoro (1972) “Kifo changu  ni fedheha”,Hammie Rajab (1979) “Ufunguo wa Bandia”

3.      Riwaya ya Upelelezi

Riwaya hii huelezea mambo mawili kosa au uhalifu na upelelezi wa uhalifu huo hadi mwalifu anapopatikana.

Hivyo wahusika wake ni wahalifu, wadhulumiwa (waliotendewa kosa) na upelelezi wakiwemo polisi. Mtunzi wa kwanza wa riwaya ya upelelezi nchini Tanzania ni mfano;M.S.Abdallah na riwaya zake ni:-Mzimu wa watu wa kale (1958),Kisima cha giningi(1968),Duniani kuna watu (1973),Siri ya sifuri (1974),Mwana wa yungi Hulewa (1976),Kosa la Bwana Musa (1984),Watunzi  wengine wa riwaya ya upelelezi ni:-H.Katalambwa na E.Ganzile,Simbamwene (1984) “Dimbwi la Damu”,E.Ganzele (1980) “Kijasho chembamba”

4.      Riwaya ya Ujasusi

Ni riwaya ya upelelezi wa kimataifa majasusi ni wapelelezi wanaotumwa na nchi, serikali au waajiri wao kwenda katika nchi nyingine kuchunguza siri zao hasa siri za kijeshi (silaha walizonazo) siri za kisayansi na kiuchumi n.k ili taarifa hizo ziwanufaishe waliowatuma wakati Fulani hutumwa kwenda kuharibu silaha zao au nyenzo za uchumi na maadui

Mfano wa riwaya za ujasusi ni:-E.Musiba (1979) “Kikosi cha kisasi”,E.Musiba (1981) “Njama”,K.M.Kassani (1982) “Mpango”,Mtobwa (1987) “Je tutarudi na roho zetu?”,Hammie Rajab (1984) “Roho mkononi”

 

UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI

Vipengele vya fani ni kama vile:-

a)     Muundo

Muundo hutumika kueleza mpangilio wa kazi ya kifasihi. Mpangilo huu hujionyesha kwenye maumbo ya kazi za kifasihi kama hadithi fupi au riwaya. Muundo ni namna au jinsi kazi za fasihi inavyoonekana yaani umbo lake, ilivyogawanyika. Mfano sura, mfuatano wa matukio yake (mtiririko wa matukio), msuko n.k. matukio yanaweza kufuatana kwa njia sahihi nay a moja kwa moja (msuko sahahi) au yakawa na uchangamano ambao unahusisha kwenda mbele na kurudi nyuma (msuko changamano)

b)    Mtindo

Ni jumla ya mbinu au sifa zinazomwezesha mandishi kuwasilisha ujumbe wake.Mtindo huelezea jinsi mwandishi anavyoiunda kazi yake.Dhana hii inarejesha sifa maalumu za mwandishi au mazoea ya mwandishi fulani ambayo hujionyesha kwenye fani yake. Mazoea hayo ya mwandishi yanapambanua msanii huyu na wenzake kiasi kwamba msomaji anaweza kusema hii ni kazi inayoandikwa na fulani kwa kusoma tu katika mtindo wa riwaya kuna vipengele vifuatavyo;

·        Matumizi ya Lugha

·        Usimulizi wa nafsi (Msanii anaweza kusimulia matukio kwa kutumia nafsi ya 1,2 na ya 3)

·        Matumizi ya masimulizi (msanii hutoa masimulizi yake juu ya mfululizo wa matukio kama yalivyotokea katika kipindi fulani cha maisha ya wahusika. Msanii husema nini kilitokea jinsi gani kilitokea na mahali ambapo hayo yalitokea

·        Matumizi ya monolojia ni masimulizi yanayofanywa na mhusika mmoja katika hadithi au kazi nyingine za kisanaa katika mbinu hii, hadithi inayojitokeza kama inasimuliwa na mhusika aliye hadithini. Mwandishi anaonekana kuwa hayupo. Pia hadithi inaweza kujitokeza ikisimuliwa katikaa nyakati mbalimbali.

·        Matumizi ya dayolojia, ni mazungumzo baina ya wahusika wawili au zaidi katika riwaya.

·        Matumizi ya tanzu nyingine za kifasihi simulizi kama vile nyimbo, mashairi, majigambo, hadithi matumizi ya barua n.k.

·        Uteuzi wa wahusika na ujengaji wa mandhari.

c)     Wahusika

Ni viumbe wa sanaa wanabuniwa kutokana na mazingira ya msanii. Hatua ya kwanza katika utungaji wa kazi ya sanaa ni wazo, wazo kutokana na hali halisi anayoiona msanii ili kueleza fikra rai au falsafa yake kuhusu kile akionacho anaichukua Lugha na kuifinyanga.

Wahusika wake pia huwaweka katika mandhari yatakayomsaidia kuwakilisha hoja zake kutokana na vitendo, maingiliano na fikra zao kuna wasanii wanaotumia wanyama au wadudu kama wahusika kwa lengo la kufikisha maudhui fulani kwa jamii au dhamira, mitazamo yao, kwa jamii.

d)    Mandhari

Ni mahali au makazi maalumu yaliyojengwa na mtunzi na yanamatokeo, matukio mbalimbali ya fasihi. Mandhari ni mazingira ya wahusika na matukio na inahusu mahali wanamokaa wahusika na kuingiliana, mazingira ya kijamii na kiuchumi ya wahusika hao na nafasi zao za kitabaka kufahamu mandhari kunatusaidia kuelewa hisia, imani, tabia, na maumbile ya wahusika. Mandhari hutupatia mwelekeo kuhusu maudhui.

e)     Matumizi ya Lugha

Lugha ina nafasi kubwa sana katika fasihi kwa kuwa fasihi yenyewe ni sanaa ya lugha. Lugha hiyo ndiyo nyenzo inayotofautisha fasihi na sanaa nyingine kama uchoraji, ufinyanzi, udarizi n.k

Lugha ni nguzo kuu ya kazi za kifasihi na uchunguzi wowote wa kazi hizo hauna budi kuangalia suala la lugha kazi ya kifasihi  huyawasilisha  maudhui yake, dhamira yake kwa kutegemea lugha. Baadhi ya wahakiki wa fasihi wa kwanza kuwa  fasihi hutumia lugha kwa namna maalumu, inayozoea lugha ambayo inajulukana kama lugha ya kifasihi. Katika matumizi ya lugha kuna vipengele kama:-

Tamadhali za semi, kama vile tashibiha, sitiari, tafsida, tashihisi, kejeli, mubalagha, dhihaka n.k

·        Mbinu nyingine za kisanaa ni kama vile takriri, tanakali sauti, mdokezo, tashititi, mjalizo n.k

·        Matumizi ya majali maana ya watu aghalabu huwa na maana. Wasomaji wa riwaya ni vyema tuyachunguze majina na kuyahusisha na matukio, dhamira, maudhui na ujumbe wa riwaya husika. Mfano wa riwaya ni “Adili na Nduguze” (1952) mhusika Adili ni mwadilifu

·        Matumizi ya jazanda au Taswira ni mafumbo ambamo ndani maana ya kitu imejificha na mfano katika riwaya ya “Dunia mti mkavu” (1980) mvua inatumiwa kama jazanda na matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi.

·        Uteuzi na mpangilio wa maneno. Lugha ni nyenzo ya kimsingi ya msanii na jinsi anavyotumia huathiri jinsi msomaji atakavyoisoma, kuielewa na kuathiriwa na riwaya fulani mfano wa matumizi ya miundo fulani huweza kuathiriwa na maswala yanayozungumzwa.

·        Matumizi ya semi, kama vile methali, misemo, nahau, misimu mafumbo n.k vipengele hivi vina kazi ya kufafanua maudhui ya kazi ya fasihi

·        Matumizi ya taharuki. Hii ni mbinu inayotumiwa na watunzi wa kazi za kubuni ili kutetea hisia na hamu ya msomaji ili kujenga taharuki. Mtunzi husuka matukio yenye mshikamano na kutiririka kwa muwala ambao unamfanya msomaji asiitue kazi hiyo hadi kikomo chake kazi yenye taharuki haichoki kuisoma bali inaburudani ndani yake.

JINA LA KITABU

Jina la kitabu ni vyema lisadifu yale yaliyomo ndani ya kitabu. Mfano Je Shetani msalabani (1982) linasadifu vipi yale yaliyomo ndani ya riwaya hiyo?

 

UHAKIKI WA MAUDHUI

Maudhui ya riwaya kama kazi yoyote nyingine ya fasihi yaweza kuwa kitu, mtu, tukio au jambo lolote katika maisha yetu. Maudhui hudhihirika baada ya kuangalia mambo mengi, mathalani tukio mbalimbali

Kwa ujumla, maudhui ni muhimu katika riwaya hasa ndiyo msingi wa riwaya kwa hivyo ni lazima tutegemee mambo yaliyojitokeza katika ile riwaya yaani maudhui lazima itoke ndani ya riwaya na sio nje.

Katika bahari hii ya maudhui, hatuna budi  kuichunguza jumuiya iliyozungumzwa. Matokeo yote katika utunzi ule yatapimwa kwa mujibu wa hali ya jumuiya. Mhakiki astahili kuichunguza jumuiya ili kuweza kuhukumu kama mtunzi amezingatia kutoa hali halisi ya jumuiya yake.

Maudhui huwa ni ya aina mbalimbali kwa ujumla huwa yanalenga migogoro na mikinzano katika jamii. Baadhi ya maudhui ya kazi zote za riwaya na sanaa kwa jumla ni kama vile:-

*    Mgongano wa tabaka kati ya watawala na watawaliwa

*    Migongano kati ya wenye elimu na wasiopata elimu

*    Migongano kati ya walio na mali na wasionayo

*    Migongano kati ya mwenye kupigania usawa kati ya mume ne mke na wenye kupinga usawa huu n.k

Kwa ujumla maudhui hutupa mafunzo, ujumbe na kutufahamisha falsafa

MADA NDOGO ;UHAKIKI WA TAMTHILIYA

Tamthiliya ni utungo wa kidrama ambao ni aina mojawapo ya maandishi ya sanaa za maonyesho. Ni sanaa inayoonyeshwa kwa vitendo katika sanaa hii ili mtu apate maadili au utamu uliomo katika sanaa mpaka asome vitendo vya wahusika waliotumiwa na msanii na kuvitafakari kwa makini.

Tamthiliya huonyesha matendo ya wanajamii kwa njia ya kuigiza, maigizo ambayo hatimaye huweza kuonyeshwa kwenye majukwaa katika sanaa za maonyesho wahusika wake huonyesha matendo waziwazi kwa njia ya kuigiza. Wausika hawa huzungumzia nafsi zao wakati zamu zao za kuongea zinapowafikia ili mradi kila mmoja hujaribu kuonyesha waziwazi kuridhika au kutoridhika kwake kufutana na nafasi anayoiwakilisha katika jamii inayohusika.

SIFA ZA TAMTHILIYA

Tamthiliya huwa na sifa za kawaida za sanaa za maonyesho, sifa hizo ni:

ü Dhana inayotendeka

Dhana inayotendeka ni kile kinachoongelewa katika tamthiliya na kinaweza kuwa cha kubuni au cha kweli. Dhana inayotendeka kwa kawaida huhusu mzozo fulani unaohusisha pande mbili. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kilio chetu” (1995), dhana inayotendeka ni “Vita dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI”

ü Kuwepo kwa mtendaji

Hapa ni wale wanaotenda ile dhana, yaani wahusika. Ili tamthiliya ikamilike lazima wawepo wale wanaotenda lile tendo ambao wanaitwa wahusika. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Mashetani” (Hussein) watendaji wakuu ni: Juma na Kitaru na watendaji wadogo ni: Mama Kitaru, Baba Kitaru, Daktari, Bibi, Mama Juma, n.k

ü Kuwa na uwanja maalumu wa kutendea

Tamthiliya huigizwa sehemu fulani. Hapa kuna jukwaa ambako wahusika wanaingiliana katika uigizaji wao. Ukubwa au upana wa eneo hilo ni muhimu sio tu kwa athari, bali pia kwa kuupitisha ujumbe fulani.

ü Kuwepo kwa watazamaji

Hawa hutazama dhana inayotendeka. Kwa tamthiliya iliyoandikwa, watazamaji hapa ni wasomaji, yaani wale wanaosoma kazi hiyo ya sanaa. Kwa hiyo, tamthiliya inaingizwa mbele ya watazamaji (hadhira).

ü Kusudio la kisanaa.

Hili hutupa uhakika kuwa kinachotendeka hapo kimedhamiriwa kuwa sanaa na si kitu kingine kwa mujibu wa kanuni za jamii inayohusika.

ü Muktadha wa kisanaa

Ni sifa nyingine ya tamthiliya. Muktadha  wa kisanaa unafafanua mazingira ya tukio hilo. Kwa mfano, ugomvi wa walevi kilabuni au baa si sanaa za maonyesho kwa sababu muktadha wa tukio hilo haulipokei kama sanaa.

ü Tamthiliya ni kazi ya kubuni kama kazi nyingine za kifasihi.

Hii ni muhimu ili kutofautisha kati ya tendo la dhati katika maisha na tendo la sanaa.

ü Matukio ya tamthiliya huigizwa kwa hadhira hai.

Hapa basi pana mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wahusika, ambao ni vipaza sauti vya mtunzi na hadhira.

ü Tamthiliya, hadithi yake imegawika kimuundo katika matendo na maonyesho

Matendo na maonyesho huonyesha matukio mbalimbali. Kila tendo huzingatia tendo moja kuu ndani ya mchezo; na hugawanyika katika sehemu ndogo ziitwazo maonyesho. Onyesho moja kwa kawaida huwasilisha tuko moja linalotendeka mahali pamoja.

ü Mgogoro wa tamthiliya huwa mwanzoni

Mwandishi hana wakati wa kutoa maelezo mengi. Kwa mfano, katika tamthiliya ya “Kifo Kisimani “ ya Kathaka wa Mberia, mgogoro kati ya Mtukufu Bokona na wanyonge unajitokeza mwanzoni

ü Hutawaliwa na dayalojia au majibizano

 

AINA ZA TAMTHILIYA

1.     Tanzia

Tanzia ni ile inayohusika na mambo yenye uzito, kifikirika na kihisia katika maisha ya binadamu. Mhusika mkuu ambaye hupewa sifa nyingi zinazovutia, hukabiliwa na shida au tatizo;tatizo ambalo linaweza kumkabili mtu yeyote. Lakini namna anavyojitahidi kulitanua tatizo hili, namna anavyopigana vita kushinda shida inayomkabili, hali ya ulimwenguni na tabia za binadamu, zinamfanya asiweze kufaulu na mwishowe anashindwa katika vita hii. Kwa mfano, tamthiliya ya “Mzalendo Kimathi” (1978) “Kinjekitile” (1969), “Pungwa” (1988), “Kilio cha haki” (1981) ni mfano wa tanzia. Katika tamthiliya zote hizi mhusika mkuu anashindwa na hata anakufa au anauawa, lakini kifo chake si kile cha ajali barabarani, bali ni kifo kinachokuja baada ya mapambano marefu, mapambano yanayochepuza hisia za ushujaa wa binadamu

2.     Ramsa (komedia)

Ramsa ni ile inayokusudiwa kufurahisha au inayochekeshachekesha na yenye mwisho mwema. Aina hii ya tamthiliya ni kwamba hutuchorea picha yakini ya maisha yetu, huwa haijaribu kuisawiri picha hiyo kwa undani na uzito kama uleunaojitokeza katika tanzia. Mfano wa ramsa ni tamthiliya ya Aliyeonja Pepo (1973)

3.     Melodrama na vichekesho

Melodrama inafanana sana na tanzia, ingawa mara nyingi mhusika mkuu wa meleodrama humaliza kwa ushindi, matokeo yake huwa yanasisimua sana, na mwendo wa msuko wake huwa ni wa harakaharaka zaidi.

Vichekesho, kwa upande mwingine; huwa  vinakusudia kutuonyesha vituko vitakavyotuchekesha tu. Ujenzi wa wahusika huwa ni muhimu, matukio huwa hayawekewi sababu zozote au sababu za kuturidhisha na msuko wake huwa hauna uchangamano mzuri. Tamthiliya nyingi zinazoonyeshwa katika televisheni ni vichekesho.

4.     Tamthiliya ya kihistoria

Hii ni aina ya tamthiliya inayoelezea tukio fulani la kihistoria katika jamii fulani. Msomaji wa tamthiliya hii huweza kukutana na sifa za tanzia pamoja na tamthiliya chekeshi. Mhusika mkuu wa tamthiliya hii mara nyingi huwa ni shujaa aliyejitoa mhanga kuipigania na kuitetea jamii yake ili iweze kuondokana na matatizo yanayoiandama, hususani ya kisiasa na kiuchumi.

Tukio la kihistoria linaloelezewa kwenye tamthiliya hii huwa limeiathiri jamii husika kwa kiasi kikubwa na hivyo huwa si rahisi kusahaulika. Vitabu vya tamthiliya vinavyoelezea matukio ya kihistoria ni kama vile Kinjekitile, Mzalendo Kimathi, Mkwawa wa Uhehe (1979) pamoja na Tone la Mwisho.

 

Tamthilia husimulia hadithi au kisa Fulani. Hadithi au kisa hicho huweza kuwa ni ya kubuni au ni tukio la kweli la historia au ni mchanganyiko wa yote mawili.Hadithi au kisa  hicho kwa kawaida huhusu mzozo Fulani unaohusisha pande mbili:Upande wa mpinzani wa jagina/nguli.Hadithi hiyo husukwa kwa namna inayoujenga mgogoro wa pande hizo mbili hadi kufikia mwisho wake.

Katika jadi ya utunzi wa tamthiliya mtiririko wa matukio kwa kawaida huwa na umbo la piramidi lenye hatua zifuatazo;

 

 

      C

 


 B         

                                                 D

 

 

 


     A                                                                                  E

 

Hatua A:  Mwanzo

Hatua hii ndiyo mwanzo au “utangulizi” wa mchezo.Katika hatua hii:

Ø Hali ya tamthilia (ya majonzi, ya miujiza, ya nderemo)hudhihirishwa.

Ø Mandhari (yaani wakati na mahali panapotokea vitendo vya hadithi) huelezwa;

Ø Baadhiya wahusika hutambulishwa;

Ø Taarifa nyingine muhimu (kwa mfano matukio yaliyotangulia kisa hiki) hudokezwa.

 

Hatua B: Tatizo / Kukua kwa mgogoro

Mvutano kati ya pande mbili au zaidi zinazozozana hujitokeza.Tatizo linalosababisha mgogoro huo hudhihirishwa.Majaribio ya kutanzua mgogoro hufanywa na kushindwa.  Kila hatua muhimu katika ukuaji wa mgogoro huo huitwa kipeo (turning point).Vipeo kadhaa vidogo huweza kufikiwa na kukiukwa bila usuluhishi

 

Hatua C:  Kilelecha Mgogoro

Mantiki ya mivutanona matukio hatimaye huifikisha hadithi kileleni kwenye kilele cha hadithi (climax).  Katika hatua hii mzozo hufikia kiwango cha juu kabisa pasina uwezekano wa kurudi nyuma.

 

Hatua D:  Mshuko

Katika hatua hii mvutano huanza kulegea na hutokea mshuko wa taharuki. Mgogoro huwaelekeza wahusika kwenye pambano la mwisho.

 

Hatua E:  Mkasa / Suluhisho

Kama tamthiliya ni ya kitanzia, katika hatua hii jagina hushindwa (amahupatwa na mauti ama maanguko ya aina nyingine), na mgogoro hufikia hatima yake.Kama tamthiliya ni komedia, mvutano baina ya pande zinazozozana husuluhishwa na hali ya utangamano hurejeshwa.

 

v VITENDO

Kitendo

Tamthilia nyingi  hugawanyika katika sehemu kuu ziitwazo vitendo. Kila Kitendo (act) huzingatia tendo moja kuu ndani ya mchezo.  Kwa mfano, katika  mpangilio wa matukio ulioelezwa hapo juu, kila kipengele kingeweza kuwa kitendo kimoja.Hivyo tamthiliya yenyempangilio huo kijadi ilitakiwa kuwa na vitendo vitano.Katika tamthiliya za Kiyunani, kumalizika kwa kitendo kuliashiriwa na kuingia kwa wazumi (chorus) jukwaani.  Siku hizi zipo tamthilia zenye kitendo kimoja, vitendo viwili, vitatu, vitano na hata zaidi.

 

v ONYESHO

Kila kitendo hugawanyika katika sehemu ndogo ndogo ziitwazo maonesho.Onyesho (scene) moja kwa kawaida huwasilisha tukio moja linalotendeka mahali pamoja.Kwa kawaida onesho moja huunganishwa na jingine kwa kuzingatia mantiki ya kile kinachosimuliwa; tukio moja likimalizika.Wakati wa maigizo jukwaani mabadiliko ya maonesho huashiriwa kwa kufunga pazia au kuzima taa  au kwa wahusika kuondoka jukwaani.

 

v WAHUSIKA NA WAIGIZAJI

Usawiri wa wahusika wa tamthiliya hufanywa kwa njia ya matendo, kwani fursa ya kutoa maelezo marefu haipo.Wahusika wa tamthiliya hawana tofauti kubwa na wahusika wa hadithi:huweza kuwa mviringo, bapa, watu wa tabaka la juu wanyonge, n.k.Tamthiliya huwa na wahusika wakuu na wahusika wadogo.

 

·        WAHUSIKA WAKUU

          Jagina:   Shujaa wa tamthiliya ambaye matendo mengi yanahusu maisha na majaliwa yake, kwa mfano Kinjeketile katika mchezo wa Kinjeketile(E. Hussein, OUP 1969), ndiye Jagina au nguli yaani mhusika-kiini, au mtenzi mkuu.Katika baadhi ya tamthiliya,jagina na nguli ni mhusika yule yule, lakini si lazima iwe hivyo.Yawezekana nguli asiwe jagina wa tamthilia inayohusiika.Katika tanzia ya Kiyunani, jagina aghalabu alikuwa ni mtu wa tabaka la juu ambaye aliangamia kutokana na ama ila (dosari) fulani katika tabia au maamuzi yake kwa ama kwa sababu ya kusakamwa na mazingira yanayomzidi uwezo, ama yote mawili.

o   Mkizani:  mhusika mkuu anayepambana na ngullli au jagina.

o   Muwi :  Mhusika muovu, kwa mfano Shylock katika Shakespeare Mabepari wa Venisi (mf. J.K. Nyerer, OUP 1969).

 

Wahusika Wadogo

Hawa aghalabu huwa ni wengi, na baadhi yao huwa na jukumu dogo tu katika tamthiliya.  Wahusika wadogo watokeao mara kwa mara ni:katika tamthiliya.Wahusika wadogo watokeao mara kwa mara ni:

o   Mfoili:Mhusika anayewekwa sambamba na jagina na aliye na sifa totauti na za jagina kwa lengola kumpamba na kumpambanua jagina vizuri zaidi.

 

o   Msimulizi :Huyu ni mhusika anayetumiwa na mtunzi kutoa maelezo na ufafanuzi kuhusu matendo, wahusika na matukio katika mchezo. Katika baadhi ya michezo mhusika huyu hupewa jina jingine; kwa mfano Brecht katika The Caucasian Chalk Circle (1948) anamwita “Mwimbaji.”

 

o   Chizi: Mhusika mcheshi ambaye hufanya vituko vya kipumbavu na kusema maneno ya kijingajinga ili kuiburudisha hadhira, na wakati mwingine kutoa ujumbe fulani.

 

Waigizaji, Waigizaji pengine huitwa wamithilishaji.Hawa ni watu wanaotokea jukwaani mahali pa wahusika wa mchezo na kuiga vitendo na tabia za hao wahusikawanao wawakilisha.Waigizaji hawana budi kuteuliwa vizuri ili wawakilishe na kuwasilisha sawasawa umbo, hali, hisia, tabia, mawazo na matendo ya wahusika  wanaowami thilisha.

 

o   Dayalojia (Mazungumzo ya Wahusika)

Hadithi ya tamthilia husonga mbele kwa njia ya vitendo na mazungumzoya wahusika.Mazungumzo hayo ya wahusika ndiyo huitwa dialojia.  Mafanikio ya michezo mingi hutegemea namna mtunzi anavyofaulu kuweka diolojia inayovutia na kuaminika.  Dialojia lazima iwe na maneno machache yaliyoteuliwa vizuri ili kuisogeza mbele hadithi au kudhihirisha jambo Fulani alilolikusudia mtunzi. 

*    Baadhi ya tamthiliya hutumia monolojia pia,Katika monolojia, mhusika huzungumza mwenyewe kudhihirisha mawazo aliyonayo moyoni.

*    Pia kuna tamthiliya zinazotumia masimulizi,ambapo hutokea msimulizi na kueleza au kusimulia mambo yaliyotokea mithili ya mtambaji wa hadithi au utendi. Mbinu hii inatumika katika drama-tendi.  Baadhi ya tamthilia za Kiswahili, kwa mfano M. Mlokozi Mkwava wa Uhehe (EAPH 1979) zimetumia mbinu hii.

 

UHAKIKI WA VIPENGELE VYA FANI

Uhakiki wa tamthliya kimsingi huzingatia kanuni na misingi ileile ya uhakiki wa Riwaya. Kuna mambo ya msingi yz hizo tanzu mbili kufanana na kutofautiana. Mambo muhimu yanayochunguzwa wakati wa kuhakiki fani ya tamthiliya ni:

a)     Utendaji/tukio/tendo.

Kitu muhimu sana katika ujenzi wa tamthiliya ni tukio. Kutokana na tukio moja, msanii anao uwezo wa kuibua dhamira mbalimbali. Wataalamu wa taaluma hii husisitiza umuhimu wa tendo au tukio katika tamthiliya kwa kusema “drama ni tendon a wahusika ni tendo”

Tendo huanza pale mhusika anapoulza, “Ninataka nini? Je, lengo langu ni nini?” Kwa kawaida, aina ya tendo/tukio litaathiri matokeo ya tamthiliya itakayoandikwa.

Mwandishi mwenyewe anapaswa kuamua juu ya aina ya tamthiliya anayotaka kuandika, lugha, mtindo, wahusika au mandhari anayotumia. Kwa hali hiyo, uteuzi wa tendo/tukio la kuandikia tamthiliya lazima uende pamoja na uteuzi mzuri wa vipengele vingine vya kisanaa kama vile lugha, wahusika, mandhari, n.k.

b)    Lugha

Lugha ndiyo nyenzo kuu ya kazi ya fasihi. Dhamira na maudhui ya kazi ya kifasihi haziwezi kuwasilishwa na kuwafikia wasomaji bila ya kuwako kwa lugha. Uchunguzi wa matumizi ya lugha ni muhimu katika uhakiki wa tamthiliya. Je, mambo gani ya kuchunguza hapa? Hapa tunachunguza:

·        Matumizi ya nahau na misemo.

·        Uteuzi na mpangilio wa maneno/msamiati.

·        Tamathali za semi. Kwa mfano, sitiari, tashibiha, tafsida, tashihisi, n.k.

·        Mbinu nyingine za matumizi ya lugha. Kwa mfano, takriri, tanakali sauti, majazi, mdokezo, mjalizo n.k.

·        Matumizi ya taswira na ishara mbalimbali.

·        Matumizi ya mkopo na kutohoa.

c)     Wahusika

Katika tamthiliya, wahusika ni nguzo muhimu sana. Wahusika si watu halisi bali ni watu wa kubuniwa, wenye sifa muhimu za binadamu. Wahusika huwa na athari kubwa kwa hadhira kutokana na sababu mbalimbali:-

*    Wahusika wanabebeshwa sifa nyingi tofauti ambazo zinawakilisha maisha halisi ya watu hai.

*    Mwandishi wa tamthiliya hulazimika kumjenga mhusika mmoja kwa kuvutia na kumpa mbinu za ki-drama, mambo ya kushangaza au mbinu yoyote ile anayoichagua mwandishi. Kama tamthiliya inaigizwa jukwaani, wale waongozaji wa tamthiliya hiyo wanaweza kuathiri mchezo huo pia. Kama ilivyo katika riwaya, tamthiliya huwa na wahusika wakuu na wahusika wadogo.

d)    Muundo wa tamthiliya

Muundo katika tamthiliya humaanisha msuko wa vitendo na mgogoro kuanzia mwanzo wa mchezo, kuingia kwenye kilele (upeo) na kuhitimisha kwenye ufumbuzi/masuluhisho ya mchezo huo (mwisho). Kwa upande mwingine, muundo huonyesha mpangilio wa maonesho kutoka mwanzo hadi mwisho wa tamthiliya.

Kwa ujumla, tamthiliya inakuwa na mwanzo unaomwelekeza msomaji kwenye wahusika na migogoro au mkinzano unaokuwa na kufikia upeo kasha msuko wa aina fulani kabla ya kufikia ufumbuzi. Muundo unaweza kuwa wa moja kwa moja au muundo wa rejea.

e)     Maelekezo ya jukwaani

Haya ni yale maelezo ambayo huandikwa kwa mabano katika tamthiliya na huandikwa kwa hati ya mlazo. Je, maelezo hayo hufanya kazi gani?

*    Hueleza mienendo na miondoko ya wahusika.

*    Hutoa maelezo kuhusu wasifu wa wahusika, mavazi, lugha ya ishara za uso, n.k.

*    Hutoa maelezo kuhusu mandhari au mahali pa mchezo.

*    Hufafanua matendo mbalimbali yanayotokea jukwaani.

*    Hueleza wasifu wa mazingira na hata malebaya wahusika.

*    Hutoa vielekezi vy jinsi ya kuandaa jukwaa kwa ajili ya uigizaji

*    Hutoa tathmini ya matendo ya wahusika au lugha; kwa kuonyesha wapi pana kinaya, n.k

f)      Mandhari

Madhari hutumiwa kuelezea sehemu ambako tendo fulani hutendeka. Neon hili huweza kutumiwa kwa mapana kuelezea pia mazingira ya kisaikolojia ya tendo fulani. Mandhari huweza kurejelea yale mazingira ya jukwaani na hata wakati wenyewe katika tamthiliya. Mandhari yanaweza kuwa ya kubuni au ya kweli (halisi)

g)     Upeo/kilele

Upeo ni sehemu ya tamthiliya ambamo taharuki  na matamanio ya hadhira hufikia kilele.sehemu ambapo hadhira huanza kupata suluhisho la mgogoro uliomo katika tamthiliya. Peo katika tamthiliya ni za aina mbili upeo wa juu na wa chini

·        Upeo wa juu ni ule ambao unakidhi haja za hadhira au jamii inayoipokea. Katika sehemu hii, jamii hupata majawabu muhimu ambayo tamthiliya huwa imeyachelewesha kwa kutumia mbinu kama vile za taharuki, mbinu rejeshi, mtindo telezi, n.k. Sehemu hizi mara nyingi husisimua hadhira kwa hali ya juu sana.

·        Upeo wa chini ni ule ambao haukidhi haja ya wasomaji wa tamthiliya inayohusika. Katika baadhi ya kazi za tamthiliya upeo wa chini huonyesha udhaifu wa kazi ya sanaa ya msanii anayehusika. Wakati mwingine upeo wa chini umekusudiwa na msanii na huutumia sana katika hadithi fupi na lengo kubwa huwa ni kuipa hadhira mshangao.

h)    Jina la kitabu na jalada lake

Kama ilivyo kwenye uhakiki wa riwaya, katika tamthiliya vilevile tunaangalia uhusiano wa jian la kitabu na yaliyomo katika kitabu, hali kadhalika jalada na uhusiano wake na maudhui ya kazi inayohusika.

i)       Mtindo katika tamthiliya.

Tamthiliya yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni mazungumzo au dayolojia. Mazungumzo/dayolojia hutumiwa kuelezea majibizano baina ya wahusika wawili au zaidi waliopo kwenye jukwaa au katika tamthiliya maongezi au majibizano si kwa ajili ya kujibizana tu. Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa, mazungumzo hayo si mazungumzo tu, lazima yaendeleze tendo kuu katika tamthiliya. Mazungumzo ndiyo nguzo ya kukuza dhamira na maudhui.

*    Mazungumzo mazuri yana uhalisia na uthabiti.

*    Mazungumzo sio maelezo tu bali yanaonyesha matendo ya ndani.

*    Mazungumzo mazuri hukuza na kuendeleza tendo kuu na msuko

*    Mazungumzo sio maongezi yanayovutia tu, lazima yawe na lengo.

*    Ikiwa mazungumzo yanakuza na kuendeleza tendo kuu, basi yanatekeleza jukumu la kidrama.

*    Mazungumzo yanaweza kutokea sambamba; kwa kuwako kwa wahusika kadhaa jukwaani.

*    Mazungumzo na uzungumzi nafsi wa wahusika huchukuliwa kama sehemu ya mazungumzo ya tamthiliya kwa sababu ya kuliendeleza tendo kuu.

*    Mazungumzo huweza kuonyesha sifa zisizokuwa za kawaida katika maongezi ya kila siku ikiwa mwandishi anataka kulimulika jambo fulani.

*    Mazungumzo ya mhusika yanaweza kuyavunja mtarajio fulani wa wasomaji au hadhira katika hali fulani kwa ajili ya kupitisha ujumbe fulani.

*    Mazungumzo ndiyo njia kuu ya kuindeleza hadithi iliyopo katika tamthiliya kwa kuwa mwandishi hana uhuru wa kutumia mbinu za usimilizi, isipokuwa katika maelezo ya jukwaani. Tamthiliya yoyote hupambanuliwa kwa mtindo wake ambao ni dayolojia.Dayolojia ndiyo mtindo mkuu wa tamthiliya nyingi.

*    Dayolojia ni majibizano baina ya wahusika wawili au zaidi, ambao hujadili jambo fulani.

UHAKIKI WA MAUDHUI

Maudhui hutujulisha lile lililomgusa mwandishi mpaka kuunda ile kazi yake. Hili linaweza kuwa ni wazo tu au aliloshuhudia au hata likawa ni jumuisho la mambo mengi.

Maudhui pia hutuangazia jinsi jumuiya ya mwandishi ilivyo kwa kuwa fasihi ni kioo cha jamii. Kupitia maudhui, tunaweza kugundua mazingira ya mwandishi yalivyo.

Mwandishi hutumia maudhui yake kutudhihirishia mivutano, misuguano na pia maendeleo ya jamii yake. Maudhui ndiyo lengo la mwandishi. Ndicho chombo chake  cha kutuonyesha furaha na matatizo ya jumuiya iliyomzingira na kuwathiri kimawazo. Kuathirika huku kwa mwandishi hasa hujitokeza zaidi baada ya kusoma kazi zake nyingi.

Kwa hivyo, basi maudhui ya kazi yoyote ile ya fasihi yatahusu mambo ambayo yalimsukuma mwandishi hadi akaiunda kazi ile. Pia yatahusu mafunzo ambayo mwandishi aliliengea hadhira yake. Zaidi ya haya, kwa kuwa maudhui hayatenganishwi na mazingira na jamii, itambidi mwenye kuyachambua ayalinganishe na hali ya jamii ya mwandishi katika vipengele mbalimbali vya maisha. Mathalani, itambidi achunguze siasa, uchumi, utamaduni, n.k.

Mwanafasihi mmoja, Senkoro (1981), amefafanua maudhui kama yanayojumlisha mawazo nap engine mafunzo mbalimbali yaliyomsukuma mtunzinama msanii hadi akatunga kazi fulani ya sanaa. Huwa msanii huyo amekusudia hadhira yake ya wasomaji, wasikilizaji ama watazamaji wayapate mawazo au mafunzo hayo. Kwa hiyo, haya twaweza kuyaita kuwa ni lengo la msanii kwa hadhira. Mawazo na mafunzo haya hayazuki hivi hivi tu. Kwa hiyo, kuna umuhimu wakati wa kuyachambua na kujadili yahusishwe na hali halisi ya jamii.

Mhakiki anachunguza maudhui ya kazi ya fasihi anaweza kuongozwa na maswali yafuatayo:-

*    Je, wazo kuu la msanii n nini?

*    Je, msanii ametazamia hadhira ya aina gani?

*    Je, kuna kundi lolote analoliunga mkono?

*    Je, kuna kundi analolibeza?

*    Je, msanii ameipa hadhira yake mbinu zipi za kuitatua migogoro aliyoichunguza?

Katika tamthiliya ya Kiswahili, kuna dhamira mbalimbali ambazo waandishi wamezishughulikia kwa mujibu wa Mulokozi (1996). Dhamira hizo ni:-

1.     Migongano ya kiutamaduni

Hizi zinonyesha mvutano kati ya utamaduni wa jadi wa Kiafrika na utamaduni wa Kizungu au kati ya mji na shamba. Suala hili limejadiliwa kwa dhati zaidi katika

§  E.Hussein “Wakati Ukuta” (1969)

§  E.Hussein “Kwenye Ukingo wa Thim” (1989)

§  P.Mhando “Hatia”

§  J.Ngugi “Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi” (1961)

§  H.M.Liyoka “Dunia Imeharibika” (1978)

§  C.Riwa na M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo! Paulo!”  (1976) n.k

2.     Matatizo ya kijamii

Kwa mfano, mapenzi, ndoa, ufukara na urithi. Karibu  tamthiliya zote za mawazo zilihusu kipengele hiki. Kwa mfano, Nakupenda Lakini…(1957) na Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (1961), zilizungumzia matatizo ya mapenzi yanayokumbana na vikwazo vya kiuchumi na vinginevyo. Tamthiliya za Hyslope zilihusu matatizo ya urithi, rushwa, fitina na tama. Tatizo la mimba limejitokeza katika Hatia, katika Mke Mwenza (1982), tunakutana na tatizo la wivu katika ndoa za mitala.

3.     Dini

Hizi ziko katika makundi mawili:

·        Tamthiliya za kanisani zenye kufundisha dini. Kwa mfano, zile tamthiliya zinazoingizwa kanisani kukiwa na shughuli au sherehe fulani.

·        Tamthiliya zinazochambua na kuhakiki asasi na maundisho ya dini kifasihi. Hizi ni kama vile

·        F.Topan “Aliyeonja Pepo” (1973)

·        Muba-“Maalimu” (1980)

·        Mulokozi “Mkwawa wa Uhehe” (1979).

 Hawa wanaonyesha mikinzano iliyomo ndani ya mafundisho ya kidini, hasa pale mafundisho hayo yanapogongana na maisha halisi, sayansi au mantiki. Tamthiliya nyingine zinazoonyesha mgongano huo ni Kinjekitile (1969) na Njia Panda (1981).

4.     Ukombozi

Hizi zinazungumzia juu ya harakati za kumwondoa mkoloni hapa Afrika. Mfano wa tamthiliya hizo ni Nkwera “Mkwawa Mahinya” katika “Johari Ndogo” (1968), E.Hussein “Kinjekitile” (1969) na “Mashetani” (1971), M.Mulokozi “Mkwawa wa Uhehe” (1979), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), P.Muhando, N.Balisidya na A.Lihamba “Harakati za Ukombozi” (1972) na M.S.Masanja “Damu Imemwagika na Paulo! Paulo!” (1976), n.k. Tamthiliya hizi licha ya kujadili ukombozi wa kisiasa, vile vile zinajadili ukombozi wa kiuchumi na kiutamaduni.

5.     Ujenzi wa jamii mpya

Baadhi ya tamthiliya zinazojadiliwa zinazojadili suala hili ni za Ngahyoma “Kijiji Chetu” na M.Rutashobya “Nuru Mpya” (1980). Hawa walipendekeza marekebisho katika mfumo uliopo. Baadhi wameonyesha tu kuwa mambo siyo sawa. Mfano: Mbogo- Giza Limeingia (1980) na Hussein- “Mashetani” (1971) na wengineo wanalitazama suala hili kitabaka na kuhimiza mapambano ya wafanyakazi dhidi ya mabepari na ubepari- Kahigi na Ngemera- “Mwanzo wa Tufani” (1976) na Mazrui “Kilio cha Haki” (1981).

6.     Uke na matatizo ya kijinsia

Hawa wanaonyesha hali duni ya mwanamke katika jamii ya sasa, kutafuta sababu za hali hiyo na kupendekeza ufumbuzi. Baadhi ya tamthiliya hizo ni P.Muhando-“Nguzo Mama” (1982), Ngozi-“Machozi ya Mwanamke” (1977), Mulokozi-“Mkwawa wa Uhehe” (1979), Mazrui “Kilio cha Haki” (1981), E.Mbogo “Tone la Mwisho” (1981), E.Hussein “Kwenye Ukingo wa Thim” (1989).

7.     Uchawi, uganga na itikadi za jadi

Suala hili limejitokeza katika tamthiliya kadhaa. Kwa mfano, Mhanika-“Njia Panda” (1981), Mbogo “Ngoma ya Ng’wanamalundi” (1988), Hussein “Kinjekitile” (1969) na Kitsao “Mfarakano” (1975). Kwa ujumla, uganga na itikadi za jadi katika tamthiliya hizi husawiriwankama amali muhimu za jamii zifaazo kutatua baadhi ya matatizo ya kimaisha.

8.     Tatizo la ugonjwa wa UKIMWI

Hawa wanaonyesha madhara yanayotokana na ugonjwa wa UKIMWI kwa jamii. Tamthiliya hizo ni Ushuhuda wa Mifupa (1990), Mwalimu Rose (2007), Orodha (2006) na Kilio Chetu (1995).

 

TOFAUTI KATI YA TENZI NA MASHAIRI

Tenzi na mashairi hutofautiana, hasa katika vipengele muhimu vifuatavyo:

1.     Muundo,tenzi hutumia muundo wa tarbia tu katika beti zake ambapo mashairi yana uhuru wa kutumia miundo mingine tofauti kama vile tathlitha, takhmisa n.k

2.     Urefu,tenzi kwa kawaida huwa ni  ndefu kwa vile hutokea zikiwa katika mtindo wa usimulizi, na hivyo kuwa na beti nyingi sana ili kkamilisha usimulizi wa kisa ambapo mashairi kwa kawaida hutumia beti chache

3.     Vina,tenzi zina vina vya mwisho tu; hazina vina vya kati ambapo mashairi yana vina vya kati na vya mwisho.

4.     Urefu na mistari ,tenzi mistari yake ni mifupi; haigawanyiki katika nusu ya kwanza nay a pili, mashairi yake ni mirefu; na hugawanyika mara mbili, nusu ya kwanza na nusu ya pili (huitwa vipande).

5.     Idadi ya mizani, tenzi  katika mistari yake huwa na mizani nane tu, mashairi huwa na mizani 16 katika mistari yake.

6.     Kituo,kituo cha tenzi hubadilikabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine. Kituo cha shairi kinaweza kubadilika au kutokubadilika

 

KANUNI ZA UTUNZI WA NGONJERA

Ngonjera ni tungo za kishairi zinazowasilishwa kwa kutumia mazungumzo ya majibizano baina ya watu wawili au zaidi. Mazungumzo hayo huwa na mjadala wa malumbano yenye lengo la kutoa ujumbe maalumu kwa wasikilizaji

Katika majibizano hayo, mhusika mmoja hueleza jambo fulani kwa ubeti mmoja, mhusika wa pili naye hujibu kwa kupinga au kuunga mkono hoja za mhusika aliyetangulia. Mwishoni mwa ngonjera wahusika hao huwa wanaondoa tofauti zao na kuwa na msimamo mmoja. Hali hiyo hutokea pale mhusika mmoja anakubali kulegeza msimamo wake na kukubaliana na mtazamo wa mwenzake.

Kanuni za utungaji wa ngonjera hazitofautiani na kanuni za utungaji wa mashairi ya kimapokezi. Ngonjera sharti iwe na kichwa, beti, vina, mizani, muwala, utoshelezi, kituo na urari wa mistari ya beti. Ngonjera pia, hutakiwa kutumia lugha ya kisanaa kama ilivyo kwa mashairi.

Mfano wa ngonjera: Mwenye nyumba na mhitaji  

MWENYE NYUMBA:  Nakwambieni jamaa, vya nyumbani mwangu visa,

                        Mpangaji amekaa, huu mwezi wa tisa,

                      Mpangaki ana baa, atoapo zangu pesa,

                   Hivi sasa nimenusa, nataka kumfukuza.

MHITAJI: Taibu maneno yako, yananipata kabisa,

                              Mimi mhitaji kwako, chumba sina nimekosa,

                              Sema kodi iliyoko, unayopokea sasa,

                              Nami nitakupa pesa, upate kumfukza.

MWENYE NYUMBA:  Kwa hesabu iliyoko, mimi sipati halasa,

                   Thelethini ndizo ziko, alipazo Bwana Musa,

                   Kinipa sitini zako, atatoka hivi sasa,

                   Himiza unipe pesa, nipate kumfukuza.

 

MHITAJI: Sitini ni hizi hapa, pokea ni kama posa,

                             Na kodi hasa talipa, daima bila kukosa,

                             Tena Wallahi naapa, kulipa sitakutesa,

                             Nenda kafanye mkasa, upate kumfukuza.

(Kutoka: Ngonjera za UKUTA, uk 86-87)

 

TOFAUTI KATI YA NGONJERA NA MASHAIRI

Ngonjera hutofutiana na mashairi katika vipengele vine, navyo ni wahusika, namna ya uwasilishaji, kituo, na matumizi ya lugha.

1.     Wahusika,ngonjera hutumia wahusika wanaojibizana. Wahusika hao wanaweza  kuwa wawili au zaidi, ambapo shairi hutumia mhusika mmoja tu anayezungumza au anayetoa mawazo yake pasipo kujibizana na mtu.

2.     Uwasilishaji, ngonjera huwasilishwa kwa njia ya uzungumzaji wa kujibizana, mashairi huwasilishwa kwa njia ya uimbaji.

3.     Kituo,ngonjera huwa na vituo tofauti kwa vile kila mzungumzaji huwa na ktuo chake, lakini shairi huwa na kituo kimoja tu na hata kama kitabadilikabadilika huwa hakilengi kuonyesha mtazamo wa ukinzani wa mada inayojadiliwa kama ilivyo kwa vituo vya ngonjera.

4.     Matumizi ya lugha, ngonjera hutumia sana lugha rahisi lakini mashairi hutumia sana lugha ya kuzama

 

 

       MASWALI MBALI YA FASIHI KWA UJUMLA

 

1.       Linganisha fasihi simulizi na ile fasihi andishi ukionesha

uhusiano uliopo pamoja na kutofautiana kwake.

 

Jibu

Fasihi simulizi ni fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na wazungumzaji wake na hutegemea nyenzo mbalimbali za kuonekana na kusikika zitumiwazo na binadamu katika kujielezea.  Fasihi hii hushirikisha na kuwafikia watu wengi na kujielezea.  Fasihi hii hushirikisha na kuwafikia watu wengi na hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine.  Tanzu za fasihi simulizi ni pamoja na hadithi, ushairi, semi, pamoja na sanaa za maonyesho.

Fasihi andishi ni fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi.  Fasihi hii hutegemea mwandishi ambaye huwasiliana na hadhira yake (jamii) kwa njia ya maandishi.  Tanzu za fasihi andishi ni pamoja na: ushairi, hadithi, na tamthiliya.

 

Uhusiano uliopo baina ya Fasihi Simulizi na FAsihii Andishi

(i)      Zote hutumia ufundi wa lugha ili kuwasilisha ujumbe wake.

(ii)     Zote hujadili dhamira zinazotokana na  migogoro na matatizo ya wanadamu katika mazingira yake kama vile maana ya maisha, mapenzi, mauti, upweke, ubinafsi, choyo, tama, uoga, ushujaa wivu, migongano ya kitabaka, migongano ya kijinsia, ndoa, mila, malezi, dini, sayasi na teknolojia.  Kwa ufupi zote zinamhusu mwanadamu.

(iii)    Zote zinadhima inayofanana ambayo ni kusawiri maisha na matatizo ya mwanadamu katika mazingira yake, kuliwaza, kuburudisha, kufundisha, kufurahisha, kueleza maisha, kuadibu, kuhifadhi mila, maarifa na lugha ya jamii, kutoa ujumbe na kuhifadhi na kueneza itikadi fulani.

(iv)    Zote huzaliwa, hustawi (hukua na kufa kufuatana na wakati.

 ( V )   Zote zina vipengele viwili maalumu-fani na maudhui.

 

 

TOFAUTI KATI YA FASIHI ANDISHI NA FASIHI SIMULIZI:

FASIHI SIMULIZI

FASIHI ANDISHI

1.      Uwasilishaji: Huwasilishwa na fanani ana kwa ana kwa hadhira yake. Huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo, hutegemea sauti.

1.  Huwasilishwa kwa maandishi. 

     Mwandishi hana uwezo wa kuwasiliana

     moja kwa moja na hadhira yake.

2.       Maandalizi: Kwa kawaidahutungwa papo kwa papo wakati wa utendaji.

2.   Hutungwa kwa utulivu kwa kipindi

      kirefu kabla ya kuwasilishwa kwa

      hadhira.

3.       Mazingira ya uwasilishaji

  Huambatana na tukio maalum la  

  kijamii, kwa wakati maalumu.

3.   Kujisomea au kusomewa: Tamthiliya

      huweza kusomwa tu au kuonyeshwa

      hadharani wakati wowote bila tukio

      lolote

4.       Hadhira: Ni watu wote wa jamii au

kundi linalohusika hushiriki katika

  utendaji.

4.   Zaidi ni wale tu wajuao kusoma na

      kuandika

5.       Umri: Ina umri mkubwakuliko fasihi andishi, pengine ndiyo maana

  huitwa fasihi  kongwe.

5.   Ina umri mdogo kuliko fasihi simulizi.  Hii inatokana na ukweli kuwa

      maandishi yamegunduliwa hivi

      karibuni

 

6.       Umilikaji: Kwa kawaidaikishatendwa

hugeuka kuwa mali ya jamii nzima.

6.   Kwa kawaida ni mali ya mtunzi /

      mwandishi

7.   Tanzu: Ina tanzu mbalimbali lakini ni

      nyingi kuliko zile za fasihi andishi. 

      Tanzu hizo ni:- ushairi, semi, hadithi

      na sanaa za maonesho.

7.   Ina tanzu tatu tu:- ushairi,tamthiliya

      na riwaya.

8.   Lugha:  Hutumia lugha ya hadhira

      inayohusika.

8.   Hutumia lugha anayoimudu  zaidi

      mtunzi au ile ya wasomaji

      waliokusudiwa.

9.   Uhifadhi: Uhifadhiwa kwa kichwa na

      kusambazwa kwa njia ya masimulizi. 

      Vilevile huweza kuhifadhiwa kwa

      maandishi, kanda za kunasia sauti,

      kanda za video, televisheni, filamu za

      sinema, tanakilishi, CD, DVD, VCD,n.k.

9.   Huhifadhiwa kwa njia ya maandishi

      katika maktaba, hifadhi za nyaraka

      n.k.  Na kusambazwa kwa

      maandishi

10.  Mabadiliko:  Hubadilika haraka

       kutokana na mahitaji ya hadhira na

       wakati.  Ni nadra sana kudumu katika

       hali ileile baada ya mtunzi kufariki.

10.  Haibadiliki kutegemea mahitaji ya

       hadhira na wakati. Huweza kudumu

       katika hali ileile kwa muda mrefu

       baada ya mwandishi kufariki

11.  Marekebisho / masahihisho:   Mtunzi

       huweza kusahihisha au kurekebisha

       kazi yake wakati wa kuwasilisha au

       baadae kidogo kutegemea maono na

       hisia za hadhira yake

11.  Huweza kurekebishwa wakati wa

       kutunga au wakati wa kuto toleo

       jipya. Lakini mara nyingi mtunzi

       hana fursa ya kuwasiliana na

wasomaji wake.  Kitabukikishatoka

        mitamboni ni vigumu kukifanyia 

       marekebisho.

12.  Wahusika:  Hutumia sana wahusika

       wasiokuwa binadamu kama vile

       wanyama, mimea, vitu visivyo na

       uhai, n.k.  Wahusika hawa wana

       uwezo wa kuchukua majukumu mawili

       kwa wakati mmoja.  Mfano: 

       Wahusika wafuatao

       hutambulika:-

       -  Msimuliaji (fanani)

       -  Msikilizaji (hadhira)

       -  Wanyama

       -  Binadamu

       -  Vitu na  mahali

12.  Zaidi hutumia wahusika binadamu. 

       Mara chache huweza kutumia 

       wahusika wasiokuwa binadamu. 

       Kwakawaida wahusika hushika

       jukumu moja kwa wakati mmoja. 

       Wahusika wanaweza kuwa watu au

       wanyama.  Wahusika wanawweza

       kuwa watu au wanyama.  Wahusika

       wanaotambulika ni:

       -  Wahusika wakuu

       -  Wahusika wadogo

          (wasaidizi)

       -  Wahusika wajenzi

13.  Utendaji:  Huambatana na

       utendaji kama vile

       matumizi ya viimbo, shida,

       makofi, kuimba, n.k.

13.  Hakuna utendaji.

 

2.     Eleza matatizo ya usambazaji wa sanaa za maonyesho nchini Tanzania.

 

Jibu

Sanaa za maonyesho ni nzuri wa kisanaa ulioweka katika umbo la kutendeka na kuonekana kwa macho. Uzuri huo unajitokeza katika umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisia zinazomgusa kwa kutoa kielekezo au vielelezo vyenye dhana maalumu. Kutokana na utamaduni wa Kiafrika, sanaa za maonyesho ni dhana inayotendeka. Na ili dhana hii itendeke anahitaji uwanja wa kutendea hiyo dhana. Wakati akiitenda hiyo dhana wanakuwapo watazamaji (hadhira). Kwa hiyo basi, sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni dhana inayotendeka, mtendaji, uwanja wa kutendeka na watazamaji. Katika utanzu huu wa fasihi simulizi huingia vijitanzu kama vile ngoma, jando na unyago, michezo ya watoto, majigambo, tambiko, sherehe, miviga na utani.

     Baada ya uhuru Tanzania imejaribu kufanyabidii kubwa katika kuzifufua tena amali mbalimbali za utamaduni wake. Baada ya fasihi simulizi kujeruhiwa vibaya kutokana na muono potofu wa wakoloni juu ya umaana wake, watanzania waliona kuwa upo umuhimu mkubwa wa kufufua tena fasihi simulizi ya Mtanzania. Hii inatokana na ukweli kuwa umuhimu wa fasihi unapatikana kutokana na jinsi jamii yenyewe invyothamini fasihi na utamaduni wake.

 

Ø Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

Ø Watu kutokuelewa maana ya Sanaa za maonesho.Watu wengi wana fikra potofu kwani hudhani Sanaa za maonesho ni vichekesho hivyo hazina maana yeyote.

Ø Kukosa hamasa au uungwaji mkono na taasisi za serikali na zisizo za kiserikali.Walimu wengi wanaofundisha somo la fasihi ya Kiswahili hawatilii maanani Sanaa za maonesho shuleni. Kwa sasa shuleni na mtaani  hakuna tena vikundi vya Sanaa za maonesho.

Ø Kutokuwepo kwa mipango madhubuti  kuhusu Sanaa za maonesho.Kwa  sasa vikundi vya Sanaa za maonesho shuleni na maeneo ya kazi vimekosa/vimenyimwa muda wa kutosha wa kufanya matayarisho na hivyo kufifisha ari ya watu ya kupenda Sanaa za maonesho.

Ø Uhaba wa maandishi yanayofaa kuhusu Sanaa za maonesho.Watu hawaoni kuwa ni jambo la muhimu kuandika mambo ya ngoma za utamaduni,michezo ya watoto au jando na unyago.Hivyo hakuna maandishi ya kutosha kuhusu Sanaa za maonesho.

 

3.     Eleza ni kwa nini wakati mwingine fasihi simulizi hutumia wahusika wasiokuwa binadamu?

 

Jibu

Wahusika katika kazi yoyote ta ya sanaa itumiayo lugha ni watu, wanyama, vitu, mahali, n.k. Wahusika hao kimsingi hujengwa kisanaa na mwandishi ama fanani ili waweze kukidhi na kuwakilisha dhima mbalimbali za maisha katiika jamii.

     Fasihi humhusu binadamu. Mhusika mkuu wa fasihi ni mwanadamu. Mwanadamu ndiye kwa haki ni shamirisho kipozi, na kitondo cha fasihi. Hata hivyo tofauti na fasihi andishi, fasihi simulizi huwatumia wahusika kama wanyama na vitu kujenga dhima yake. sababu za kuwatumia wahusika ambao sio binadamu ni kama hizi zifuatazo:-

 

Mosi, binadamu wana hulka mbalimbali.Wakati mwingine hulka za binadamu asimuliwaye hadithi inalingana na ile ya kiumbe Fulani kisichokuwa binadamu kama vile wanyama, mawe, miti, n.k.

     Pili, fasihi simulizi imejaa lugha ya mafumbo, aghalabu hutumia sitiari ifaayo ili kueleza kisa cha binadamu, bila ya kusabibisha kufadhaika kwa baadhi ya wanahadhira wanaohusika na tabia hiyo.

Tatu, kupunguza makali ya mguso aupatao mwanadamu anayelingana na kiumbe kinachotajwa kama mhusika.Aidha, lugha hii ya kutaja kitu/mnyama pahala pa jina la binadamu ni sanaa inayoakisi vizuri zaidi wazo la msanii. Ni ada ya fasihi ya Mbantu kujengesha utu na uungwana. Mathalani, anapotumika mbweha au fisi kuwasema watu wenye uchoyo na ulafi, ujumbe huwafika watu bila kubomoa haiba yao. Kutaja majina ya watu kungewaumba watu.

Nne, Kuepuka udhibiti wa kazi za fasihi.

Tano, kuepuka migogoro

 

4.     Fafanua sifa muhimu na vipendele mluhimu ambavyo hupambanua hadithi fupi ya Kiswahili.

 

Au

Hadithi fupi ya Kiswahili inajipambanua vipi na riwaya ya Kiswahili?

 

Au

Eleza tofauti za msingi kati ya riwaya na hadithi fupi.

 

Zingatia

Ni muhimu kutambua kuwa baadhi ya sifa hizi zinaweza pia kupatikana katika tanzu nyingine za kisanaa kama vile riwaya na tamthiliya

 

Tofauti za misingi kati ya riwaya na hadith fupi.

 

RIWAYA

HADITHI FUPI

(i)   Upana wa 

      Mawanda

Hutumia mawanda mapana.  Hii ina maana kuwa kila jambo linapewa uzito wake na kuelezwa kwa mapana vya kutosha.

Hutumia mawanda yasiyo mapana kila jambo huelezwa kwa kifupi na kimkato tu.

(ii)   Wahusika

Hutumia wahusika wengi.  Wahusika wanaweza kuwa wahusika wa aina nyingi  kama vile wahusika wakuu, wasaidizi au wajenzi: na wote wanaelezwa na kujengwa kirefu.

Hutumia wahusika wachache zaidi ukilinganisha riwaya.  Mara nyingi wahusika huwa wawili, na wakizidi sana hawafiki 10, na wahusika hawa hugawanywa katika mafungu makuu mawili: wema na ubaya

 

(iii)  Mandari 

      (mazingira)

Riwaya hutumia mangira yenye kuwa na uhalisia.  Aidha, inawezekana kutumia mazingira dhahania ingawa si jambo la kawaida.

Riwaya huwa na mazingira yenye kuwa na uhalisia. Aidha inawezekana kutumia mazingira dhahama ingawa ni jambo la kawaida

(iv)  Urefu

Riwaya ni kazi ya kubuni ambayo kimsingi ni ndefu, urefu huu unatokana na uchangamano wa visa pamoja na kuwa na wahusika wengi.

Ni kazi ya kubuni ambayo kimsingi ni fupi ukilinganisha na riwaya.

(v)   Utenzi wa

Tukio

Ina uwezo wa kutumia matukio mengi yanayoweza kujengana.  Kwa hiyio tunaweza kuwa na hadith ndani ya hadithi kulingana na matukio yake.

Hutumia tukio moja au mawili yapate kuelezwa vizuri na kwa ufupi kabisa.

(vi)  Muundo

Muundo wa riwaya ni wa kichangamano zaidi ya ule wa hadithi fupi, uchanganano huu basi umelazimisha kuwepo kwa miundo mbalimbali ya riwaya kama vile:

1.   muundo kioo

2.   muundo wa rukia

3.   muundo wa msago

Inaweza kutumia miundo yote, la msingi msanii aangalie mawanda yasiwe mapana.  Muundo kama vile mpomoko mwanzo kilele mwisho  huweka

(vii)   Uhalisia

Riwaya huonesha maisha ya mtu kwa nyenzo ya wakati

Hadithi fupi huyachora maisha ya mtu kwa kutumia kigezo cha amali

(viii)  Mtindo

Riwaya hutumia mitindo ya aina mbalimbali.  Hapa kuna matumizi ya masimulizi, monolojia na dayolojia

Hadithi  fupi mara nyingi hutumia masimulizi

(ix)   Dhamira

Huwa na dhamira kuu na dhamira ndogo ndogo nyingi.

Huwa na dhamira chache, aghalabu dhamira kuu moja.

(x)   Mwendo

Ina mwendo wa taratibu.  Vituko huelezwa taratibu / polepole

Mwendo ni wa haraka haraka.  Hueleza mambo kwa ufupi na mwisho hutoa funzo fulani.

 

5.     Fafanua dhana na dhima ya dayolojia katika kazi ya sanaa.

 

Jibu

Dayolojia ni mazungumzo ya watu wawili au zaidi yanayowakilishwa kimaandishi katika

kazi ya sanaa zitumiazo lugha, hususani hadithi fupi, riwaya au tamthiliya.  Kwa kawaida,

dayolojia haitumiki katika kazi za kitaaluma kama vile Fizikia, Hisabati, Jiografia, Historia.

 

Dayolojia katika kazi ya fasihi ina dhima mbalimbali kama ifuatavyo:

(a)      Kusaidia kuyasukumia matukio (dhahania) upande ule ambao mwandishi

ameukusudia.  Mbinu hii hutumika pia kama pambo la kazi ya sanaa.

(b)     Dayolojia inapotumika huzingatia sana tabia, hali halisi, uhusika na ujumla wa wahusika wake.  Kwa hiyo:  msomaji wa kazi ya sanaa anaweza kutambua ujenzi wa mhusika fulani kutokana na jinsi alivyotumia dayolojia katika kazi yake.  Wahusika hao watahusiana na pia kuonesha tofauti kati yao, wataonesha tofauti kitabia, kitaifa, kitabaka.  Kila mhusika ataionesha rejesta au lahaja yake, kazi yake na uwezo alionao.

(c)      Dayolojia pia hujaribu kuiga hali halisi ya maisha ya jamii wakati inapotumika.

(d)     Hujaribu kuonesha uhusiano wa kimawazo ulioopo kati ya watu wanaozungumza au kujibizana katika kazi ya sanaa ya tamthiliya au hadithi huku wakitoa damira na maudhui muhimu yaliyokusudiwa kuifikia jamii.

(e)      Dayolojia kati ya watu wawili au zaidi hujengwa na mwandishi ili kuleta tofauti za maumbile na mazungumzo.  Mwandishi huwaonesha wahusika hao kwa kuzingatia utabaka wao.  Mambo kama vile maneno, ridhimu na mwendo wa sentensi na matamshi nayo pia yanayotofautiana.

(f)      Kwa msomaji, mbinu hii ya kidayolojia husaidia kuhamasisha na kupunguza uchovu wakati wa kusoma kazi za sanaa.

(g)     Vilevile baadhi ya waandishi hutumia mbinu hii ili kuepuka mahubiri katika kazi yao (hususani riwaya).

 

6.     Eleza tofauti ya hadhira ya fasihi simulizi na hadhira ya fasihi andishi.

 

Au

Ni kwa vipi hadhira ya fasihi simulizi hutofautiana na hadhira ya fasihi andishi?

 

 

 

 

Tofauti ya Hadhira ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi

FASIHI SIMULIZI

FASIHI ANDISHI

1.   Hadhira ya fasihi simulizi

      huonana ana kwa ana na fanani

      wake.

1.   Hadhira ya fasihi andishi haionani

      ana kwa ana na mwandishi wake

2.   Hadhira ya fasihi simulizi

      hushiriki katika utendaji kwa

      kuuliza maswali, kupiga makofi,

      kuimba Wimbo n.k.

2.   Hadhira ya fasihi andishi haishiriki

      katika utendaji kwani mwandishi  

      hujitungia kazi yake akiwa peke

      yake.

 

 

3.   Hadhira ya fasihi simulizi ni

      kubwa sana kwani hujumuisha

     watu wote katika jamii yaani

     wanaojua kusoma na kuandika

     na wasiojua kusoma na

     kuandika.

3.   Hadhira ya fasihi andishi ni ya

      wachache yaani wale tu wanaojua  

      kusoma na kuandika.

4.  Hadhira ya fasihi simulizi ni hai,

     kwani hujulikana na msanii

     mwenyewe na hivyo kujua umri

     wao, uwezo wao matakwa yao,

     n.k.

4.   Hadhira ya fasihi andishi si hai

      kwani mwandishi hawezi kuwa na

      uhakika wakati akiandaa kazi

      yake kama itatosheleza matakwa

      ya hadhira yake.

5.   Hadhira ya fasihi simulizi

      humiliki baadhi ya tanzu kwa

      kufuata rika Fulani mfano

      vitendawili – watoto, methali –

      watu wazima na watoto, misimu

      – vijana wa mitaani, tambiko –

      watu wazima, n.k.

5.   Hadhira ya fasihi andishi

      haitabiriki, haichagui au kuteua

      watu wa rika Fulani, mfano kitabu

      cha riwaya au tamthiliya huweza

      kusomwa na watoto, vijana, 

      wazee, n.k.

6.   Hadhira ya fasihi simulizi

      humiliki kazi ya fanani bila

      matatizo, hivyo hii kazi huwa ni

      mali ya jamii nzima.

6.   Hadhira ya fasihi andishi haina

      uwezo wa kumiliki hiyo kazi,

      hivyo hii kazi hubaki kuwa mali ya 

      mtunzi peke yake.

7.   Hadhira ya fasihi simulizi mara

      nyingi huwa hainunui kazi ya

      fasihi simulizi.

7.   Hadhira ya fasihi andishi sharti

      inunue fasihi hiyo ingawa ni mali

      ya jamii na ndio hadhira waliompa

      msanii cha kuandika.

 

7.     Linganisha fasihi simulizi na ile fasihi andishi ukionesha

uhusiano uliopo pamoja na kutofautiana kwake.

 

Jibu

Fasihi simulizi ni fasihi ambayo hutumia mdomo katika kuumbwa, kuwasilishwa na kusambazwa kwa wasikilizaji na wazungumzaji wake na hutegemea nyenzo mbalimbali za kuonekana na kusikika zitumiwazo na binadamu katika kujielezea.  Fasihi hii hushirikisha na kuwafikia watu wengi na kujielezea.  Fasihi hii hushirikisha na kuwafikia watu wengi na hurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine.  Tanzu za fasihi simulizi ni pamoja na hadithi, ushairi, semi, pamoja na sanaa za maonyesho.

          Fasihi andishi ni fasihi inayowasilishwa kwa njia ya maandishi.  Fasihi hii hutegemea mwandishi ambaye huwasiliana na hadhira yake (jamii) kwa njia ya maandishi.  Tanzu za fasihi andishi ni pamoja na: ushairi, hadithi, na tamthiliya.

 

Uhusiano uliopo baina ya Fasihi Simulizi na FAsihii Andishi

(i)      Zote hutumia ufundi wa lugha ili kuwasilisha ujumbe wake.

(ii)     Zote hujadili dhamira zinazotokana na  migogoro na matatizo ya wanadamu katika mazingira yake kama vile maana ya maisha, mapenzi, mauti, upweke, ubinafsi, choyo, tama, uoga, ushujaa wivu, migongano ya kitabaka, migongano ya kijinsia, ndoa, mila, malezi, dini, sayasi na teknolojia.  Kwa ufupi zote zinamhusu mwanadamu.

(iii)    Zote zinadhima inayofanana ambayo ni kusawiri maisha na matatizo ya mwanadamu katika mazingira yake, kuliwaza, kuburudisha, kufundisha, kufurahisha, kueleza maisha, kuadibu, kuhifadhi mila, maarifa na lugha ya jamii, kutoa ujumbe na kuhifadhi na kueneza itikadi fulani.

(iv)    Zote huzaliwa, hustawi (hukua na kufa kufuatana na wakati.

(v)     Zote zina vipengele viwili maalumu-fani na maudhui.

 

Tofauti kati ya Fasihi Andishi na Fasihi Simulizi:

FASIHI SIMULIZI

FASIHI ANDISHI

7.      Uwasilishaji: Huwasilishwa na fanani ana kwa ana kwa hadhira yake. Huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo, hutegemea sauti.

1.  Huwasilishwa kwa maandishi. 

     Mwandishi hana uwezo wa kuwasiliana

     moja kwa moja na hadhira yake.

8.       Maandalizi: Kwa kawaidahutungwa

papo kwa papo wakati wa utendaji.

2.   Hutungwa kwa utulivu kwa kipindi

      kirefu kabla ya kuwasilishwa kwa

      hadhira.

9.       Mazingira ya uwasilishaji

  Huambatana na tukio maalum la  

  kijamii, kwa wakati maalumu.

3.   Kujisomea au kusomewa: Tamthiliya

      huweza kusomwa tu au kuonyeshwa

      hadharani wakati wowote bila tukio

      lolote

10.              Hadhira: Ni watu wote wa jamii au

kundi linalohusika hushiriki katika

  utendaji.

4.   Zaidi ni wale tu wajuao kusoma na

      kuandika

11.              Umri: Ina umri mkubwakuliko fasihi

andishi, pengine ndiyo maana

  huitwa fasihi  kongwe.

5.   Ina umri mdogo kuliko fasihi simulizi. 

      Hii inatokana na ukweli kuwa

      maandishi yamegunduliwa hivi

      karibuni

 

12.              Umilikaji: Kwa kawaidaikishatendwa

hugeuka kuwa mali ya jamii nzima.

6.   Kwa kawaida ni mali ya mtunzi /

      mwandishi

7.   Tanzu: Ina tanzu mbalimbali lakini ni

      nyingi kuliko zile za fasihi andishi. 

      Tanzu hizo ni:- ushairi, semi, hadithi

      na sanaa za maonesho.

7.   Ina tanzu tatu tu:- ushairi,tamthiliya

      na riwaya.

8.   Lugha:  Hutumia lugha ya hadhira

      inayohusika.

8.   Hutumia lugha anayoimudu  zaidi

      mtunzi au ile ya wasomaji

      waliokusudiwa.

9.   Uhifadhi: Uhifadhiwa kwa kichwa na

      kusambazwa kwa njia ya masimulizi. 

      Vilevile huweza kuhifadhiwa kwa

      maandishi, kanda za kunasia sauti,

      kanda za video, televisheni, filamu za

      sinema, tanakilishi, CD, DVD, VCD,n.k.

9.   Huhifadhiwa kwa njia ya maandishi

      katika maktaba, hifadhi za nyaraka

      n.k.  Na kusambazwa kwa

      maandishi

10.  Mabadiliko:  Hubadilika haraka

       kutokana na mahitaji ya hadhira na

       wakati.  Ni nadra sana kudumu katika

       hali ileile baada ya mtunzi kufariki.

10.  Haibadiliki kutegemea mahitaji ya

       hadhira na wakati. Huweza kudumu

       katika hali ileile kwa muda mrefu

       baada ya mwandishi kufariki

11.  Marekebisho / masahihisho:   Mtunzi

       huweza kusahihisha au kurekebisha

       kazi yake wakati wa kuwasilisha au

       baadae kidogo kutegemea maono na

       hisia za hadhira yake

11. Huweza kurekebishwa wakati wa

       kutunga au wakati wa kuto toleo

       jipya. Lakini mara nyingi mtunzi

       hana fursa ya kuwasiliana na

       wasomaji wake.  Kitabu kikishatoka

        mitamboni ni vigumu kukifanyia 

       marekebisho.

12.  Wahusika:  Hutumia sana wahusika

       wasiokuwa binadamu kama vile

       wanyama, mimea, vitu visivyo na

       uhai, n.k.  Wahusika hawa wana

       uwezo wa kuchukua majukumu mawili

       kwa wakati mmoja.  Mfano: 

       Wahusika wafuatao

       hutambulika:-

       -  Msimuliaji (fanani)

       -  Msikilizaji (hadhira)

       -  Wanyama

       -  Binadamu

       -  Vitu na  mahali

12.  Zaidi hutumia wahusika binadamu. 

       Mara chache huweza kutumia 

       wahusika wasiokuwa binadamu. 

       Kwakawaida wahusika hushika

       jukumu moja kwa wakati mmoja. 

       Wahusika wanaweza kuwa watu au

       wanyama.  Wahusika wanawweza

       kuwa watu au wanyama.  Wahusika

       wanaotambulika ni:

       -  Wahusika wakuu

       -  Wahusika wadogo

          (wasaidizi)

       -  Wahusika wajenzi

13.  Utendaji:  Huambatana na

       utendaji kama vile

       matumizi ya viimbo, shida,

       makofi, kuimba, n.k.

13.  Hakuna utendaji.

 

8.     Eleza matatizo ya usambazaji wa sanaa za maonyesho nchini Tanzania.

 

Jibu

Sanaa za maonyesho ni nzuri wa kisanaa ulioweka katika umbo la kutendeka na kuonekana kwa macho. Uzuri huo unajitokeza katika umbo ambalo mtu hulitumia kueleza hisia zinazomgusa kwa kutoa kielekezo au vielelezo vyenye dhana maalumu. Kutokana na utamaduni wa Kiafrika, sanaa za maonyesho ni dhana inayotendeka. Na ili dhana hii itendeke anahitaji uwanja wa kutendea hiyo dhana. Wakati akiitenda hiyo dhana wanakuwapo watazamaji (hadhira).

     Kwa hiyo basi, sanaa za maonyesho ni kitendo chochote chenye sifa nne ambazo ni dhana inayotendeka, mtendaji, uwanja wa kutendeka na watazamaji. Katika utanzu huu wa fasihi simulizi huingia vijitanzu kama vile ngoma, jando na unyago, michezo ya watoto, majigambo, tambiko, sherehe, miviga na utani.

     Baada ya uhuru Tanzania imejaribu kufanyabidii kubwa katika kuzifufua tena amali mbalimbali za utamaduni wake. Baada ya fasihi simulizi kujeruhiwa vibaya kutokana na muono potofu wa wakoloni juu ya umaana wake, watanzania waliona kuwa upo umuhimu mkubwa wa kufufua tena fasihi simulizi ya Mtanzania. Hii inatokana na ukweli kuwa umuhimu wa fasihi unapatikana kutokana na jinsi jamii yenyewe invyothamini fasihi na utamaduni wake.

 

Ø Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

Ø Watu kutokuelewa maana ya Sanaa za maonesho.Watu wengi wana fikra potofu kwani hudhani Sanaa za maonesho ni vichekesho hivyo hazina maana yeyote.

Ø Kukosa hamasa au uungwaji mkono na taasisi za serikali na zisizo za kiserikali.Walimu wengi wanaofundisha somo la fasihi ya Kiswahili hawatilii maanani Sanaa za maonesho shuleni. Kwa sasa shuleni na mtaani  hakuna tena vikundi vya Sanaa za maonesho.

Ø Kutokuwepo kwa mipango madhubuti  kuhusu Sanaa za maonesho.Kwa  sasa vikundi vya Sanaa za maonesho shuleni na maeneo ya kazi vimekosa/vimenyimwa muda wa kutosha wa kufanya matayarisho na hivyo kufifisha ari ya watu ya kupenda Sanaa za maonesho.

Ø Uhaba wa maandishi yanayofaa kuhusu Sanaa za maonesho.Watu hawaoni kuwa ni jambo la muhimu kuandika mambo ya ngoma za utamaduni,michezo ya watoto au jando na unyago.Hivyo hakuna maandishi ya kutosha kuhusu Sanaa za maonesho.

 

9.     Fafanua dhana na dhima ya dayolojia katika kazi ya sanaa.

 

Jibu

Dayolojia ni mazungumzo ya watu wawili au zaidi yanayowakilishwa kimaandishi katika

kazi ya sanaa zitumiazo lugha, hususani hadithi fupi, riwaya au tamthiliya.  Kwa kawaida,

dayolojia haitumiki katika kazi za kitaaluma kama vile Fizikia, Hisabati, Jiografia, Historia.

Dayolojia katika kazi ya fasihi ina dhima mbalimbali kama ifuatavyo:

(a)      Kusaidia kuyasukumia matukio (dhahania) upande ule ambao mwandishi

ameukusudia.  Mbinu hii hutumika pia kama pambo la kazi ya sanaa.

(b)     Dayolojia inapotumika huzingatia sana tabia, hali halisi, uhusika na ujumla wa wahusika wake.  Kwa hiyo:  msomaji wa kazi ya sanaa anaweza kutambua ujenzi wa mhusika fulani kutokana na jinsi alivyotumia dayolojia katika kazi yake.  Wahusika hao watahusiana na pia kuonesha tofauti kati yao, wataonesha tofauti kitabia, kitaifa, kitabaka.  Kila mhusika ataionesha rejesta au lahaja yake, kazi yake na uwezo alionao.

(c)      Dayolojia  hujaribu kuiga hali halisi ya maisha ya jamii wakati inapotumika.

(d)     Hujaribu kuonesha uhusiano wa kimawazo ulioopo kati ya watu wanaozungumza au kujibizana katika kazi ya sanaa ya tamthiliya au hadithi huku wakitoa damira na maudhui muhimu yaliyokusudiwa kuifikia jamii.

(e)      Dayolojia kati ya watu wawili au zaidi hujengwa na mwandishi ili kuleta tofauti za maumbile na mazungumzo.  Mwandishi huwaonesha wahusika hao kwa kuzingatia

utabaka wao. Mambo kama vile maneno, ridhimu na mwendo wa sentensi na matamshi nayo pia yanayotofautiana.

(e)  Husaidia kuhamasisha na kupunguza uchovu wakati wa kusoma kazi za sanaa.

 

 

 

 

 

 

9       Fasihi  ya Kiswahili inakabiliwa na changamoto nyingi’.Kwa hoja tano ( 5 ) na mifano  kuntu jadili dai hili.

Fasihi ya Kiswahili ni fasihi iliyoandikwa na mswahili  kwa lugha ya Kiswahili inayohusu mila,desturi na utamaduni wa mswahili ( watu wa Afrika mashariki na kati).

 

Changamoto

Ø Uhaba wa wataalamu wa fasihi ya Kiswahili.Tatizo la uchache wa wataalamu wa lugha ya Kiswahili linapelekea uchache wa kazi za fasihi ya Kiswahili zinazoandikwa na kuwasilishwa kwa jamii.

Ø Uchache wa kazi za fasihi zilizosambazwa. Kazi nyingi za fasihi ya Kiswahili hazijasambazwa vya kutosha maeneo yote ya mjini na vijijini.Kazi nyingi za fasihi ya Kiswahili zinasambazwa maeneo ya mjini ingawa sio yote lakini watu wengi wa vijijini bado hazijawafikia.

Ø Uhaba wa fedha kwa waandishi

Ø Uchache wa hadhira kwani waswahili wengi hupenda fasihi ya kigeni

Ø Baadhi ya tanzu haziwezi kuhifadhiwa katika njia za kisasa.Mfano Tambiko,Jando na unyago

Ø Uchache wa kazi za fasihi ya Kiswahili zinazoikomboa jamii kisiasa,kiuchumi,kifikra na kiutamaduni.Waandishi wengi huandika kazi zao kwa lengo la kuburudisha wasomaji na sio kujadili kwa kina matatizo ya jamii ili kuisaidia jamii iondokane nayo.

Ø Kuongezeka kwa kazi za fasihi pendwa.Waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili wamejikita katika uandishi wa fasihi pendwa ili kupata fedha za haraka hivyo huandika kazi ambazo zitanunuliwa kwa haraka sokoni.Mfano  Wowowo la kajala  na ‘shemeji pita kwa huku’zilizoandikwa na Irene Ndauka.

 

 

 

 Mwandishi Mwl Godlove Gwivaha -0758 006447

 


 [H

 [H2]

Powered by Blogger.