METHALI, NAHAU, NI VIPERA VYA SEMI
METHALI, NAHAU, NI VIPERA VYA SEMI
Kamusi ni hazina la lugha |
Fasihi simulizi ina tanzu zake na Semi ni moja ya tanzu zake. Utanzu huu nao una VIPERA vyake ambayo ni methali, nahau, misemo, simo, vitanza ndimi, vichezea meno na mgafumbo ambayo hujumuisha vitendawili, chemsha bongo, malumbo na mizungu.
Katika somo hili nitaelezea kwa kifupi maana na kutoa mifano ya Methali na Nahau na kuonesha ukaribu wa nahau, misemo na methali.
Methali na nahau zote ni
semi zitumiazo lugha fupi fupi na ya mkato.
Methali
Maana.
Methali ni usemi wa kimapokeo, japo zipo methali zinazozaliwa kila wakati na nyingine kufa. ambao unaotumiwa kwa kufumbia jambo kwa maneno ya kawaida bali kwa njia ya mkato huku ukibainisha ukweli au kutolea ushauri kwa kulenga kwa usahihi kile kinachozungumziwa.
Kwa ufupi methali ni kauli inayobeba busara au falsafa za jamii husika.
Mifano ya methali za kimapokeo ni:
i. Pema usijapo pema ukipema si pema tena.
ii. Kozi mwana mandanda kulala njaa kupenda.
iii. Mwenda omo na tezi marejeo ni ngamani.
iv. Mwapiza la nje hupata la ndani.
v. Macho hayana pazia.
vi. Ukilima pakubwa ukivuna pamekwisha.
Mifano ya methali zilizozaliwa hivi karibuni kwa uchache ni:
i. Usiteme 'big G' yako kwa karanga za kuonjeshwa.
ii.Ukilima shamba njiani ujue kulinda ndege.
iii.Ukitaka kujua mwenendo wa mjinga mvishe kilemba.
iv. Kiyoo cha gari hakifungwi katika tairi ya gari
v. Ama kweli kama hujui unakokwenda huwezi kupotea.
vi. Akimbiaye peke yake siku zote yeye ni mshindi.
vii. Usiku rafikiye ni giza.l
Misemo
Maana
Msemo ni fungu la maneno lenye maana mahsusi lenye kutoa fundisho ama kuelezea dhana fulani kwa j amii lisilo na kitenzi ndani yake.
Wengi huchanganya misemo na nahau. Tofauti kubwa kati ya tungo hizi ni kitenzi. Nahau huwa na kitenzi lakini msemo hauna kitenzi ndani yake
Ifuatayo ni mifano michache ya misemo ya Kiswahili na maana zake:
i. Mkono wa birika=mchoyo
ii. Sindano na uzi. =ushirikiano au umoja
iii. Kiti moto=nyama ya nguruwe au misukosuko ya madaraka.
iv. Hamadi kibindoni=akiba uliyo nayo mkononi.
v. Mwana haramu= mtoto wa nje ya ndoa.
vi. Kiwi cha macho= tamaa ya mapenzi.
viii. Mkono mrefu = mwizi
viii. Akali ya watu= watu wachache.
ix. Umti wa watu = watu wengi.
Katika mkutadha wa maongezi aghalabu misemo huongezewa kitenzi na kutenda kazi ya nahau lakini maana hubakia kuwa ile ile ya awali.
Nahau
Maana
Usemi mfupi ulio na kitenzi unaotumia maneno ya kikawaida, lakini yakiwa na maana iliyojificha na iliyotofauti na maana ya maneno hayo.
mfano:
i). Kujikaza kisabuni = kutia bidii,
ii).kuvaa miwani = kulewa,
iii).Kuoga mwaka= kusherehekea kumaliza mwaka kwa salama.
Zifuatazo ni nahau maarufu za lugha ya Kiswahili. Kila lugha ina nahau zake na kusudio kuu la matumizi ya nahau ni kuifanya lugha kuwa safi.Neno hili lina asili ya Kiarabu na maana yake ya asili ikiwa ni usafi wa lugha ikimaanisha matumizi sahihi ya lugha.
1 Amekula chumvi nyingi=ameishi miaka.
mingi
2, Ana mkono wa birika= mtu mchoyo
3.Ametutupa mkono= amefariki, amekufa
4.Ameaga dunia=amekufa, amefariki
5.Amevaa miwani=amelewa
6.Amepiga kite=amependeza
7.Amepara jiko=kaoa
8.Amefumga pingu za maisha=ameolewa
9.Anawalanda wazazi wake =
kawafanana wazazi wake kwa sura
10. Kawachukua wazazi wake=anafanana
na wazazi wake kwa sura na tabia.
11.Kawabeba wazazi wake = anawajali na
kuwatunza wazazi wake.
12. Chemsha bongo = fikiri kwa makini na
haraka.
13.Amekuwa toinyo=hana pua.
14. Amekuwa popo =amekuwa kigeugeu
15. Ahadi ni deni = timiza ahadi yako
16.Amewachukua wazee wake =
anawatunza vizuri wazazi
17.Amekuwa mwalimu= yu msemaji sana
18.Amemwaga unga = amefukuzwa kazi
19..Ana ulimu wa upanga=ana maneno
makali
20.Ameongeza unga = mepanda cheo
21.Agizia risasi = piga risasi
22.Kuchungulia kaburi= kunusurika kifo
23..Fyata mkia= nyamaza kimya
24.Fimbo zimemwota mgongoni=ana
alama za mapigo ya fmbo mgongoni
25.Hamadi kibindoni= akiba iliyopo
mkononi]
26.Hawapikiki chungu
kimoja=hawapatani kamwe
27.Kupika majungu = kumteta mtu kwa
siri
28.Kumvika mtu kilemba cha ukoka =
umsifu mtu kwa unafiki
29Kula mlungula /kula rushwa = kupokea
rushwa
30.Kupelekwa miyomboni = kutiwa au
kupelekwa jandoni
31.Kujipalia mkaa = ujitia matatani
32.Kumeza au kumezzea mate = utamani
33.Kumuuma mtu sikio = kumnong'oneza
mtu jambo la siri
34.Kumpa nyama ya ulimi =
kumdanganya mtu kwa maneno
matamu
35.Kumchimba mtu = kumpeleleza mtu
siri yake
36.Kutia chumvi katika mazungumzo =
uongea habari za uwongo
37.Vunjika moyo = kata tamaa
38.Kata maini = kutia uchungu
39. Kujikosoa = kujisahihisha
40.Kutia utambi = kuchochea ugomvi
41.Kumeza maneno = kutunza siri
moyoni
42.Kula njama kufanya mkutano wa siri.
43.Kumkalia mtu kitako = kumsema
au kumsengenya mtu
44.Kupiga mtu vijembe = kumsema mtu
kwa fumbo
45.Kiinua mgong = malipo ya pongezi ya
uzeeni bada ya kustaafu kazi
46.Kazi ya majungu = kazi ya kumpatia
mtu posho
47.Kaza kamba au kaza roho =usikate tamaa
48..Kumwonyesha mgongo = kujificha
49.Kuona cha mtema kuni = kupata
mateso au kuuliwa kwa kukatwa
kichwa
50.Maneno ya uwani = maneno yasiyo na
maana au porojo
51.Mate ya fisi = tamaa kupita kiasi
52.Kata tamaa = vunjika moyo kutokuwa
na hamu ya jambo fulani.
53. Mbiu ya mgambo = tangazo
54.Mungu amemnyooshea kidole = mungu amemuadhibu
55.Mkubwa jalala = kila lawama hutupwa kwa mkubwa
56.Mkaa jikoni= mvivu wa kutembea
57.Mungu si Athumani= mungu hapendelei
58.Paka mafuta kwa mgongo wa chupa = danganya
59.Usiwe kabaila = usichume tokana na jasho la mwingine
60.Usiwe kupe = fanya kazi
61.Usiwe bwanyenye = usichume kwa vitega uchumi vyake.
62. Usiwe na mirija = usinyonye wenzako
63.Utawala msonga= utawala wa wachache
64.Usiwe nyang'au = nchi moja kuifanyia nyingine ubaya na udhulumati.
65.Usiwe kikaragosi = nchi kuwa kibaraka wa nchi kubwa.
66.Usiwe chui katika ngozi ya kondoo=kujifanya rafiki kumbe ni adui
67.Kutoa ya mwaka =kufanya jambo zuri na la pekee
68.Kumpa mtu ukweli wake = kumwambia mtu wazi ubaya wake.
69.Pua kukaribiana kushikana na uso =kukunja uso kwa hasira
70.Kusema kutoka moyono=kunena kilicho kweli
71.Sina hali= sijiwezi kiuchumi
72.Kupiga uvuvi = kukaa tu bila kazi
73.Kupiga kubwa = kwenda moja kwa moja, kusepa
74.Kumwekea mtu deko = kulipiza kisasi
Mtu mwenye ndimi mbili = kigeugeu
75.Miamba ya mitishamba =wanga hodari wa kienyeji
76.Kupiga supu = kutegea kazi wengine wafanye
77.Kupiga mali shoka = kugawana mali au urithi
78. Kula vumbi kuhangaika maisha, pata tabu kutafuta riziki
79.Mafungulia ng'ombe =muda wa kati ya saa mbili na saa tatu asubuhi.
80.Kutia kiraka =fichia siri
81.Kumlainisha mtu= kumzungumzia mtu maneno matamu mpaka akubali matakwa yako.
82. Kupiga pamba=kuvaa vizuri
83.Kufulia = kuishiwa
84.Umangimeza=uongozi wa kuamrisha watu, udikiteta au uongozi wa imla