HADITHI




SEHEMU YA 76 Muda ule tulipanga kwenda kumalizana na Masanja kabisa na tulikuwa tunaomba Mungu Klinita awe bado hajamfungua baba yake. Muda ule ningekuwa na simu ningempigia klinita kumjulisha asimfungue masanja ila hatukuwa na Simu. Kusimama na kutafuta simu ndio tungejichelewesha zaidi. "Nashangaa mlikuwa mnataka kunipeleka Hospitalini kwanza mngeambiwa mtafute kibari kutoka polisi cha mimi kutibiwa sijui mgenikitoa wapi. Matonya ongeza Mwenda bhana kabla sijafa nile nyama ya masanja maana nahisi kifua changu kinawaka moto sijui nakaribiakufa"Aliongea Mzee Juma huku akiwa anatabasamu hali iliyonifanya kubaini kuwa mzee Juma alikuwa anapenda sana kumuona Masanja akifa. Matonya alicheza na usukani vilivyo hata dakika tano hazikwisha tayari tulishafika kwa Masanja Gheti lilifunguliwa na tuliingiza Gari hadi ndani. Yulipofika pale tulishuka na kumuacha mzee Juma kwenye Gari. Mlinzi mmoja ambaye alikuwepo pale alitukaribisha ndani sijui yeye alikuwa bado hajausoma mchezo. Kupitia Bastora moja ambaye Matonya alikuwa nayo ambaye alipewa kituoni alijiweka vizuri na kuanza kuusogelea mlango wa chumba cha Klinita. Tulipofika Mlangoni nilishitulia na Mlio wa Risasi kutoka kwenye kile chumba ingawa mlio haukusikika sana Kutokana na kile chumba kuwa gymsang bord. Ule mlio wa Risasi kwa kweli ulinilegeza na Muhusika pale Nilijua lazima alikuwa ni Klinita huenda alimfungua baba yake. Mlio wa Risasi ulitufanya kujiandaa vizuri na kusimama pembeni ya mlango ili akitoka tu analo. Ni kweli baada ya dakika moja tangu mlio usikike mlango wa chumba ulifunguliwa na Masanja alitoka. Alipotoka tu matonya alimuweka chini ya ulinzi. "Tumebadilisha Ratiba bana tumeona bora tuje kuchukua roho yako mapema maana tumeona utamaliza watu wengi. Pia Mzee juma anahamu na Nyama yako ale kabla ya kufa ili akawasimulie wazazi wake"Yalikuwa maneno machache sana aliyongea Matonya. Alipoongea vile matonya masanja alitaka kutoa bastora kiunoni kwa ajili ya kujitetea lakini Mzungu alikuwa mwepesi alimtwanga mtama ambao ulimpeleka hadi chini. Matonya hakutaka kufyatua risasi maana angewashitua walinzi ambao wengi wanakuwa ndani ya vyumba ya ile nyumba. Nilipoona Matonya amemuweza masanja mimi nilikimbia hadi ndani ya kile chumba kwenda kuangalia nani yule alikuwa amepigwa risasi. Nilipoingia kwenye kile chumba nilibaki nikiwa nimedua kwa kile ambacho nilikiona. Kwa kweli sikuamini macho yangu kama Masanja alikuwa amemuua Klinita. "Nenda salama mpenzi wangu Klinita hakika hatujafikia kile ambacho tulikuwa tunakipanga. Pia Asante kwa Kuhatarisha maisha yako ili kunitetea mimi nakupenda kuliko maelezo na Pumzika mahali pema na mimi nakuja"Niliongea Maneno machache sana kwa klinita na kutoka chumbani. Sikutaka kufikilia sana maana kwa jinsi ambavyo nilikuwa nampenda klinita ningeshindwa kufanya kazi. Nilipotoka chumbani nilimwambia Matonya kuwa klinita kafa. Tulimchukua Masanja huku akiwa chini ya ulinzi. Mlinzi naye ilibidi tumuweke chini ya ulinzi ili kuchelewesha taarifa kufika polisi. Tulienda tukawapakia hadi kwenye Gari na safari ya kuelekea Porini ambako tungeenda kula nyama ya Masanja ilianza. Tulikimbiza Gari kama muda wa Nusu saa tayari tulishaingia porini. Tulipolianza tu pori tulisimamisha gari tukamshusha yule Mlinzi na kumueleza kuwa masanja ndio amemuua mwanae na kumwambia kuwa atoe taarifa polisi kuwa wafungwa wale ndio wanaenda kumla nyama masanja kutokana unyama wa kuwauwa watu mbalimbali na kesi wakatupiwa wale wafungwa ambao sisi. Baada ya kumpa yale maelezo tuliendelea na safari. Tulitembea tena kama dakika tano ndani ya pori gari tulienda kusimamisha tukamshusha masanja na mzee juma na kuingia naye porini. Huko porini tulimfikisha masanja tukamfunga Kamba kisha tulikata Paja lake na kumchomea Haraka Mzee Juma ili ale kwani Hali yake ilikuwa mbaya. Tulikuwa tunapeleka vitu haraka ili kuwahi Mzee Juma aone wakati tunamuua masanja kama yeye alivyosema. Nyama ya masanja tuliichoma kisha tukakata vipande vidogo vidogo tukampa mzee juma na kuanza kula kwa shida maana hali yake ilikuwa mbaya sana. Wakati mzee Juma akiwa anakula nyama Huku Masanja alikuwa analia kwa uchungu kuomba msamaha kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana. Mzee juma alikula kama finyango tano ya nyama ya masanja huku akitabasamu kisha tulimpa maji akanywa. Alipokunywa maji tulimfungua masanja kamba na kumsogeza karibu na Mzee Juma kisha tulimpa mzee juma kisu ili alipe kisasi. Ingawa mzee Juma alikuwa amepigwa Risasi kwenye mbavu lakini alijikaza kwa nguvu zote huku machozi yakimtoka na kukipeleka kisu kwenye kifua cha Masanja. Alipopeleka kile kisu mzee juma alicheka sana hali ilimyomfanya hadi kuanguka chini na kutulia kimya. Nilipoenda kumgeuza nilikuta tayari kafa huku akiwa anacheka. Ile hali ilinisikitisha sana ila sikuwa na jinsi . Sisi kisasi kwa masanja tulikifanya haraka kwa kumuwekea miti akiwa vile vile bado anahema na kisu kikiwa kifuani na kuchoma moto. Baada ya kuchoma moto tulimuacha na mzee Juma pale huku tukiwa tumeandika ujumbe wa maelezo yote ya Unyama aliyofanya masanja hadi kufikia kumpa adhabu ile na kuondoka. Tulitembea Mguuu kwa mguu tena Hadi kwenye kijiji kimoja ambacho hata jina sikijui. Tulipofika kwenye kile kijiji tulinunua ijabu za kike na kuvaa lengo tusafiri kama wanawake hadi namanga Arusha huko tungevuka Mpaka wa Tanzania na kuingia kenya na kwenda kutafuta Usafiri wa kwenda brazil maana Tanzania tulikuwa tunatafutwa. Mungu siyo Athumani tulisafiri salama hadi sasa hivi Tupo Brazil naendelea na Maisha mazuri ninawatoto wawili na nimeoa binti wa kibrazil. Watoto wangu wote wakike wakwanza nimemuita klinita na wapili Magreth. One day nitarudi Tanzania tayari mmenisahau. MWISHOOOOO WA HADITHI HII. TUKUTANE KWENYE KIGONGO KINGINE. PIA NAFURAHI MASHABIKI ZANGU MNANIKUBALI POPOTE KWENYE HADITHI ZA WATU NAONA JINA LANGU. MFANO KWENYE HADITHI NA POST ZA SHIGONGO WATU MNANITAJA SANA NAFARILIJIKA.
Powered by Blogger.