Simulizi; NABII WA UONGO


Simulizi; NABII WA UONGO

*SEHEMU YA 6**

Jua lilichomoza mapema sana kama kawaida! ,ilikuwa ni moja ya siku za ajabu sana. Kwani Joka lile ambalo nilipewa kuweza kunilinda na kunitumikia lilianza kupiga kelele na fujo nyingi sana nyumbani kwangu, na kunifanya nizidi kuwa na hofu isiyo kuwa ya kawaida.

"Zikipita siku tano akiwa hajapata chakula,nyoka huyu atapiga kelele za ajabu ,kelele za hasira, jitahidi sana bila hivyo utaharibu kila kitu ",niliikumbuka sauti iliyokuwa ikinisisitiza kuhakikisha nyoka wangu niliyepewa anapata chakula chake ndani ya siku tano. Japokuwa ilikuwa asubuhi, lakini mwili wangu uliweza kulowa kwa jasho ambalo lilitokana na hofu iliyokuwa ikinikosesha amani.

"Nimekwisha!, leo naumbuka !",niliongea kwa sauti ya chini sana huku nikitoka ndani ya nyumba yangu kuelekea kanisani kwangu, kanisa ambalo lilikuwa karibu tu na nyumba yangu. Japo nilifunga madirisha ya nyumba yangu, lakini kelele za nyoka yule niliweza kuzisikia mpaka kanisani kwangu.

Sauti zile waumini wengi wa kanisa langu hawakuweza kuzisikia, hasa watu ambao walikuwa watenda dhambi na walioingia kanisani kwangu kufuata maajabu yangu niliokuwa nikiyatenda. Lakini watu wachache waliomjua mungu kweli kweli, waliweza kuzisikia sauti za kutisha kutoka nyumbani kwangu, sauti ambazo zilikuwa za Nyoka niliyemfungia katika chumba cha siri kwa siku tano mfululizo bila kumpatia chakula chochote kile.

"Kulikoni mchungaji!, naskia sauti za kutisha kutoka nyumbani kwako!

"Mbona mimi sisikii? "

"Hata mimi pia sisikii, "

"Jamani! baba Juliet yuko sahihi! Hata mimi nasikia sauti hizo, tena sauti zenyewe sio za kimungu kabisaa!

"Msiwe na hofu! Tuendelee na ibada, kama sauti hizo mnazosema mnazisikia zikiendelea tena, itabidi tuzikemee kwa maombi! bila shaka shetani atakua ananinyemelea kuniangusha nisiweze kumtumikia Mungu ",

Yalikuwa ni majibizano yaliyokuwa yakiendelea kati yangu, na viongozi wenzangu wa kanisa. Ni baada ya kusubiliwa kwa muda mrefu niweze kuanza ibada, bila kutambua kuwa kiumbe ambacho waliweza kusikia kelele zake ndicho kilicho nichelewesha kuingia kanisani. Lakini nilijikuta nakutana na ujumbe ambao ulinishtua sana kutoka kwa baba yake Juliet, kwani ndiye aliyeanzisha mazungumzo kutokana na sauti za ajabu alizozisikia ,na kuzidi kutoniamini kwani siku zote alikuwa na mashaka juu ya uchungaji wangu. Mashaka yaliyoanza siku moja alipokuja kunitembelea nyumbani kwangu na kukuta chupa ya konyagi ikiwa mezani kwangu, na alipojaribu kuniuliza kuhusu chupa ile nilimzungusha zungusha tu bila kumpatia jibu lolote la kuridhisha.


****-***

Juliet alionekana kuwa na haraka sana, japo alikuwa mzimu, lakini alifanya kila kitu kama binadamu wengine ili tu wageni wake, baba pamoja na mama yangu mzazi wasiweze kumtilia mashaka.

"Twendeni haraka kanisani, kuna hatari! ",Juliet aliongea huku akiwa ameshika funguo yake ya gari, lakini pia katika mkono wake wa kulia alikuwa ameshika biblia.

"Hatariiiii !!"wazazi wangu walishtuka, na kujikuta wakijibu kauli ya Juliet kwa wakati mmoja tena kwa mshangao.

"Hapana! Ulimi umetereza tu, twendeni kanisani ibada imesha anza! Tunachelewa! ",Juliet alitengua kauli yake ,alijikuta akitamka ukweli ambao alikuwa amepanga kuuficha mpaka watakapofika kanisani. Lakini wazazi wangu hawakuendelea kushangaa, walifikiri kweli Juliet alikuwa amepitiwa tu kutamka maneno yale, la hasha!

Hatari ya nyoka kuvunja chumba cha siri nyumbani kwangu, na kisha kulishambulia kanisa kwa ajili ya kujipatia chakula, ndio hatari ambayo Juliet alikuwa akiizungumzia. Alikuwa ameshaona kila kitu ambacho kilikuwa kinaelekea kutokea.

"Mtoto wetu anakuja lini, nani anahubiri leo?  Wewe au! " ,baba aliuliza swali, huku akimshika mkono mama yangu mzazi na kumwongoza kupanda gari la Juliet. Siku zote baba hakupenda kuaibishwa, ndio maana alitembea na mama bega kwa bega ili tu mama asije kuharibu katika jambo lolote lile.

"Mimi ndio nitahubiri! ",Juliet aliongea huku akiliondoa gari lake na kujisogeza katika mitaa ya kijichi, mahali ambapo kanisa langu lilikuwa likipatikana. Siku huyo Juliet alipanga kusema kila kitu kuhusu mimi, na kuweza kuokoa watu ambao wangezidi kuuawa kwa ajili ya kutolewa kama sadaka.

*******

Bagamoyo;
     Mzee Jabir alifika Bagamoyo haraka sana asubuhi na mapema siku ya jumapili, taarifa ya kutisha kutoka kwa mganga ndiyo iliyomfanya afunge safari kutoka Dar es salam, na kufika katika ofisi ya chama chao cha kishetani, ofisi ambayo ilipatikana katika makazi ya mganga wa kienyeji aliyekuwa akiishi Bagamoyo.

Taarifa kuhusu Juliet kumtokea na kumtisha mganga, ndiyo iliyomfanya mganga kufika Bagamoyo huku akiwa na hofu isiyo ya kawaida.

"Bora umefika! Juliet yuko njiani anaelekea kanisani kwa Hakika!  Anaenda kuharibu kila kitu, inatakiwa tumzuie!  Harafu pia, nyoka aliyetoka katika mwili wa Nyoka wetu mkubwa na kumpatia Hakika aweze kuishi naye! Ana hasira sana! Siku tano zimepita bila kula chakula chochote! Waliokuwa wanatakiwa kuliwa ni wazazi wa Hakika, lakini Juliet kawaokoa ",mzee Jabir baada ya kufika kwa mganga, alikutana na taarifa nyingi zilizoendelea kumshitua na kumuongezea maswali. Aliamini kuwa mzimu wa Juliet, haukuwa wa kawaida na ulionekana kuwa na nguvu nyingi na ndio maana uliweza kugundua kila kitu ambacho walikuwa wakipanga.

"Mganga tunafanya nini sasa kumzuia Juliet! " ,

"Mimi mwenyewe nakusikiliza wewe tushauriane ",

"Haina jinsi inabidi mtukufu nyoka umwamushe atusaidie "

"Kuamka sio shida! Lakini hana nguvu za kutosha kupambana! na yeye tangu amtafune Juliet, hajapata chakula chochote kile ……

Yalikuwa ni majibizano yaliyokuwa yakiendelea, maongezi kati ya wanachama wawili wa chama cha kishetani cha kumpinga Mungu. Mzee Jabir, pamoja na mganga wa kienyeji maarufu nchini Tanzania na nchi jirani. Mganga ambaye alipatikana Bagamoyo mkoa wa Pwani.

*ITAENDELEA **

Mzimu wa Juliet unawapeleka wazazi wa Hakika kanisani! Nini kitatokea kanisani kwani Juliet ameshakufa, na wazazi wake hawatambui hilo.

Je Mzee Jabir na mganga watafanya nini ?

Vipi kuhusu Nyoka aliye nyumbani kwa nabii Hakika!
Powered by Blogger.