HISTORIA YA WAKWERE



HISTORIA YA WAKWERE.
Wakwere ni miongoni mwa makabila yenye watu wachache hapa Tanzania.Asili ya kabila hili ni ukoo wa PAZI KALAMA LUKILA ambapo ndani yake walikuwepo wakutu,wadoe,waluguru na wakwere,hii ilitokana na mfumo wa maisha ya watu wa zamani ya kuhamahama na ndipo wakwere wakawa kama kabila linalojitegemea na kuunda mifumo yake ya kimaisha kwa ufupi hii ndio historia ya wakwere kwenye asili yake.
NANI CHIFU WA WAKWERE??
Chifu wa wakwere kumbukumbu zinasema kuwa mzee MRISHO KIKWETE ndiye aliyekuwa chifu wa wakwere wa zamani na kama tunavyofaham cheo hicho huwa kinarithishwa ama kwa mtoto au kwa mjukuu.
Ukweli ni kwamba wakati wa ukoloni,watoto wa machifu ndio waliopewa kipao mbele kwenye elimu,mtoto wa kwanza wa chifu alikuwa ni msomi na alipata bahati ya kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali zikiwemo Tanga, Same na Pangani, mtoto huyo alikuwa anaitwa HALFANI MRISHO KIKWETE.
Kwakuwa Halfani alikuwa ni mtoto wa kiume wa wa chifu na pia ni mtumishi wa uma chifu aliwaza nani atakuwa mrithi wangu???? Wakati chifu anawaza hayo yote ndipo aliposikia mke wa mtoto wake ni mjamzito,licha ya kuwa haikuwa ni mimba ya kwanza kwa mkwe wake huyo suala la kushangaza kwenye historia chifu alicheza kamali kwenye ujauzito huo,chifu alitamka maneno kazaa juu ya kiumbe atakayezaliwa, nanukuu "kama atazaliwa mtoto wa kiume,basi yeye ndiye atakayekuwa mrithi wa cheo changu"
Kwa bahati mtoto aliyezaliwa alikuwa wa kiume basi chifu alifurahi sana,chifu kwa furaha aliyokuwa nayo aliamua kumpa mtoto huyo jina lake hivyo mtoto huyo aliitwa MRISHO HALFANI MRISHO KIKWETE
Nitafafanua kidogo lakini yeye ndiye............................
kwa maana hiyo wakwere wote ni ndugu kwakuwa wote wametoka kwenye ukoo wa PAZI KALAMA LUKALI
Taarifa hii ni kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari zikiwemo kumbukumbu za kihistoria,viongozi wa kimila wa kabila la wakwere N.K
Powered by Blogger.