FONOLOJIA ZALISHI



FONOLOJIA ZALISHI
Nadharia ya fonolojia zalishi (FZ) iliasisiwa na Noam Chomsky na Morris Halle mnmo mwaka (1968). Nadharia hii inachanganua Fonolojia Vitamkwa na Fonolojia Arudhi katka lugha za binadamu. Nadharia hii ilieta mapinduzi makubwa katika taaluma ya fonolojia miaka ya 1960.
Nadharia ya FZ inadai kuwa uchanganuzi wa sauti za lugha asilia hubainishwa kwa kanuni na sheria za kimajumui zinazohusisha umbo la ndani na umbo la nje la mfumo wa sauti. Hii ina maana kwamba sauti za lugha katika mfumo wa lugha asilia za binadamu huhusisha kanuni maalumu zinazohusu ukokotoaji kutoka umbo la ndani kwenda umbo la nje.
Nadharia ya FZ ina misingi mikuu mitatu ambayo ndiyo huongoza uchambuzi na uchanganuzi wa vipengele vya kifonolojia.
Misingi ya nadharia ya FZ
1. Maumbo na miundo yote ya lugha asilia ya binadamu inatokana na kuwepo kwa umbo la ndani ambalo hujengeka taratibu akilini mwa msemaji mzawa tangu anapoanza kujifunza lugha utotoni hadi anapopata umilisi kamili wa lugha yake. Umbo hili ndilo linalomwongoza kupata mfumo kamili wa lugha kadri anavyoitumia lugha hiyo. Kwa mfano: mu+ana, ki+akula nk.
2. Maumbo ya nje yanashabihiana na maumbo ya ndani, hivyo huakisi maumbo halisi ya ndani ya lugha wakati wa usemaji lakini yanaweza kufanyiwa marekebisho kidogo tu. Hii ina maana kwamba umbo la ndani linapokumbana na kanuni za lugha huweza kufanyiwa marekebisho kidogo tu au kutofanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya lugha kimawasiliano na umilisi wa kisarufi kwa mtumia lugha.
Umbo la ndani umbo la nje
Mfano: Mu+alimu mwalimu Kanuni ya uyeyushaji
Mu+toto mtoto kanuni ya udondoshaji
Wa+izi wezi kanuni ya mvutano wa irabu
3. Sauti zote zitumikazo katika lugha asilia za binadamu hutokana na mifumo ya mkondohewa ambayo inaenda ndani au nje ya mapafu. Mkondohewa unadhibitiwa na alasauti zilizomo katika chemba ya pua, kinywa na koo la binadamu. Udhibiti huo unakuwa katika jinsi na mahali pa kutolea/ kuingia kwa hewa mapafuni.
Nadharia ya FZ ina mihimili minne ambayo kwayo nadharia hii hufanya kazi ya kuchanganua, kuchambua na kuwakilisha vipengele vya kifonolojia
Mihimili ya FZ
1. Matumizi ya sifa uwilikinzani katika ubainishi wa sifa pambanuzi za fonimu. Nadharia ya FZ inatumia sifa uwilikinzani katika ubainishaji wa sifa pambanuzi za fonimu za lugha.
Kwa mfano sifa ya usilabi [±], irabu zote za lugha zina sifa ya [+sila] kwa sababu zinaweza kufanya kazi katika mfumo wa lugha kama silabi, mfano kwenye neno “ua” kuna silabi mbili ambazo zote ni irabu. Kutokana na sifa pambanuzi hii fonimu zote ambazo ni kosonanti na viyeyusho havina sifa ya usilabi hivyo tutabainisha kama [-sila].
2. Matumizi ya sheria na kanuni rasmi zinazotumika kulikokotoa umbo la ndani kwenda umbo la nje.
Kwa mfano sheria ya udondoshaji /u/........./Ø/ /K-K
3. Kuwepo kwa utaratibu rasmi, madhubuti, usiobadilifu katika matumizi ya sheria katika kulikokotoa umbo la ndani kwenda umbo la nje.
Kwa mfano neno lenye sifa kanuni ya uyeyushaji. Kanuni zitakuwa kama ifuataavyo:
a. Kanuni ya uyeyushaji: Irabu /u/ hubadilika kuwa kiyeyusho /w/ katika mazingira ya kufuatiwa na irabu isiyofanana nayo mara tu baada ya mpaka wa mofimu.
b. Kanuni ya ufidiaji wakaa: Wakaa uliopungua kwenye irabu /u/ kwa sababu ya kanuni ya uyeshushaji hufidiwa katika irabu inayofuata, kwa hivyo irabu hiyo huwa na wakaa mrefu kupita kawaida.
4. Kuwepo na sababu mujarabu zinazoonesha kwa nini maelezo au uchanganuzi fulani ni bora zaidi kuliko mwingine au maelezo mengine. Ufafanuzi wenye kujitosheleza juu ya uchanganuzi utolewe.
5. Matumizi ya uwakilishi moza katika uchanganuzi wa viarudhi: FZ inadai kuwa sifa ya kiarudhi inamilikiwa na kitamkwa chenye kubebe sifa hiyo. Kwa mfano mkazo katika neno hili: /mto̍to/, mkazo unamilikiwa na unachukuliwa kuwa ni sifa pambanuzi ya irabu o ya silabi ya pili kutoka mwi
Powered by Blogger.