Simulizi; "THE BLACK KILLER " (Muuaji mweusi)



Simulizi ;"THE BLACK KILLER "         (muuaji mweusi)


Mtunzi; HAKIKA JONATHAN
*SEHEMU YA 08**

Bwana Sarehe Athuman aliyewahi kuwa waziri wa ulinzi kabla ya kuvuliwa cheo hicho kutokana na tuhuma nzito ya kuhusika na mauaji kumtafuna na kuwekwa rumande, anakutwa akiwa amekufa ndani ya gereza la Segerea jijini Dar es salaam huku povu zito likitoka mdomoni mwake. Kulingana na ripoti za madaktari, walingundua kifo cha bwana Sarehe kilisababishwa na sumu kali iliyokuwa imewekwa katika chakula chake, maisha yake yalishindwa kuokolewa kwani sumu hiyo kali huua muda mfupi tu baada ya kuingia katika mfumo wa damu. "Sumu hii inaonekana imeathiri tumbo lake, kwani utumbo wake unaonekana kukatika katika kutokana na kemikali hiyo baada ya kuila ikiwa imechanganyikana na chakula alichokula ",dokta alisikika akitoa ripoti ya uchunguzi, kuhusu chanzo cha kifo cha mr Sarehe, kilichotokea katika mazingira ya kutatanisha.

"Hapa sasa, nitaishi kwa uhuru hapa Tanzania …pesa ndo kila kitu bwana …ningezubaa yule mshenzi angenitaja tu baadae ",mfanyabiashara tajiri sana Tanzania anayejihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya pamoja na madini  ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee, bwana Benedict Mathayo, anazungumza maneno ya kujisifu baada ya kutoa rushwa kwa walinzi wa magereza na kukubali kumuwekea sumu Mr Sarehe kwenye chakula chake, na kisha kumsababishia mauti. Bwana Sarehe alishirikina na Benedict pamoja na Paul Agustino kutega bomu katika sherehe ya uhuru wa Tanzania ili kumuua raisi, na kisha waweze kuipindua nchi. Benedict aliamua kumuua kwa sumu mr Sarehe, ili asiweze kumtaja kuwa na yeye alikuwa ni muhusika wa mauaji yale ya maelfu ya watu na viongozi wakubwa yaliyoyokea baada ya mlipuko wa bomu katika uwanja wa taifa, huku raisi akibaki mlemavu wa miguu.
…………………………………
Paul baada ya kupiga makasia kwa muda mrefu katika mto Amazon, anajikuta akitokea nchi nyingine kabisa tofauti na Marekani. "Mmmmh ni nchi gani nzuri kiasi hiki ",Paul alizungumza mwenyewe huku akishangaa ufukwe mzuri wa nchi ngeni aliyoifikia baada ya kupiga makasia kwa wiki nzima ndani ya maji katika mto Amazon. "Welcome Mexico"(karibu Mexico) msichana mrembo aliyekuwa akivua samaki ufukweni mwa mto Amazon alimkaribisha ugenini bwana Paul baada ya kumuona akishangaa sana mazingira ya nchi ya Mexico, msichana yule alionekana kulindwa na walinzi wengi wenye siraha nzito kama bunduki pamoja na siraha za jadi, ishara iliyomfanya Paul kuwa makini na msichana yule kwani aliamini atakuwa ni malkia wa eneo lile. "Thank you my sister, "(asante sana dada yangu) Paul alimjibu msichana yule, na ghafla alidondoka chini na kupoteza fahamu kutokana na njaa kali aliyokuwa nayo kwa muda wa wiki nzima. Baada ya Paul kuzimia, msichana yule mrembo aliwaamrisha walinzi wake kumpatia msaada Paul na kisha kumpeleka katika kambi yao waliyokuwa wakiishi.
Jacline na wenzake wakiwa katika hali ya uchovu sana, wanajikuta wakitokea katika ufukwe wa mto Amazon na kuona nyayo za miguu za Paul Agustino. "Bila shaka mtu huyu kaelekea nchi  ya Mexico, siunaona nyayo zake za miguu alizopita ……na mto huu bila kukosea unapita nchi hiyo",Godfrey aliongea huku akitazama nyayo za miguu zilizoachwa na Paul. "Tupumzikeni hapa, kisha tutaendelea na safari kesho …mimi nimechoka ",Jacline alitoa wazo lililoungwa mkono na kila mmoja  kutokana na uchovu mkubwa waliokuwa nao.


…………………………………


"Who are you ??",(wewe ni nani), Paul alimuulza msichana mrembo baada ya kuzinduka na kisha kupewa chakula na kukibugia kama kichaa, "Aim the queen of this land ",(mimi ni malikia wa eneo hili)  mrembo yule aliyekuwa amevalia mavazi ya asili huku akizungukwa na walinzi, alimjibu Paul na kisha kuketi vizuri kwa ajili ya mazungumzo. "Who are you ??( wewe ni nani?) ,malikia yule alimuulza Paul swali, na kwa kujiamini sana Paul aliweza kumdanganya malikia yule bila uongo wake kugundulika. "Aim from Tanzania, our plane got an accident when I was flying back home from Dubai …all passengers died but only my self who is still alive……please can you help me to go back home",(ninatokea Tanzania, ndege yetu ilipata ajari wakati natoka Dubai kurudi nyumbani Tanzania ……abiria wote walikufa lakini mimi peke yangu ndio bado ninaishi ……tafadhali unaweza kunisaidia nirudi nyumbani)  Paul alimweleza malikia yule kwa hisia na uchungu mkubwa, hali iliyomfanya malikia yule kuwa na huruma na kutaka kumsaidia Paul kurudi Tanzania.


"I will help you by giving you gords, you will sell them and get transport fee …",(nitakusaidia kwa kukupatia dhahabu, utaziuza na utapata nauli) Malikia yule alimweleza Paul namna atakavyomsaidia, huku Paul mawazo yake yakihama kabisa na kufikiria namna ya kuua jeshi la malikia yule na kisha kutokomea na dhahabu zote zilizomilikiwa na jamii ile.


**ITAENDELEA **

Powered by Blogger.